The Tanzania Political Chaseboard: Tafsiri ya Mambo Mazito Kisiasa Tukielekea 2015

BURIANI KAMANDA KARIM: KIFO CHA HUYU KIJANA SASA HUENDA UKALETA MAANA MPYA KABISA NA LISILOTARAJIWA KATIKA SWALA ZIMA LA SAKATA YA GESI KUFULIWA KUSINI AU BAGAMOYO:yell:

SAWA NA KIJANA BUAZIZI WA TUNISIA ALIYEWATIA MACHUNGU TAIFA ZIMA NA UMMA NCHI HIYO KUONA HERI KUTIMUA SERIKALI FISADI NCHINI HUMO NAYE HAYATI KARIM ANAINGIA KATIKA HISTORIA KUWA NI SHUJAA WA KUTETEA GESI YA KUSINI IWAONDOLEE MDHALILIKO WA 'KUITWA MACHINGA WASOTAJI WA KUDUMU KAMA WANAVYOJULIKANA JAMII YA KUSINI MWA NCHI HII.

KALALE SALAMA KIJANA MWENZETU NA YULE MAMA MJAMZITO MLIOONDOLEWA ROHO KWA KUTOA TU MAONI YENU KWAMBA GESI IPATE KUFULIWA HUKO HUKO KUSINI KABLA YA KUSAFIRISHWA ILI MIKOA HII ILIOSAHAULIKA NAYO IPATE KUENDELEA.

KAMANDA KARIM INGAWAJE UMEANGUSHWA LEO HII KUTOKANA NA UBINAFSI NA MASLAHI YA BAADHI YA VIONGOZI WETU WACHACHE KULAZIMISHWA KUFUNIKA MASLAHI YA WALIO WENGI, HATA HIVYO KILE KILICHOKUFANYA UKAANGUSHWA KWA RISASI KAMWE HAITOANGUSHWA NA MTU AWAYE YEYOTE YULE.

NASEMA KALALE SALAMA KAMANDA KARIMU:

:shock:


:yell:
Pumzika kwa Amani ya Bwana, kijana na mpiganaji wa ukweli umeshindana na wadhalimu wa nchi hii umeshinda tena ushindi wako ni wa kipekee na siku yaja kuudhiilika kuwa tanzania ni yenye neema kwa wote na mwisho wa mafisadi utakua umekwisha..

Amani na mwanga wa nuru ya bwana ikuangazie siku ya ushindi wa mauti na uzima wa milele, Mungu Baba na mwanaye Yesu kristo wakuepushe na adhabu ya kaburi umeshinda karimu lala salama kamanda.
 
Back
Top Bottom