The Tanzania Political Chaseboard: Tafsiri ya Mambo Mazito Kisiasa Tukielekea 2015

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,190
URAIS WA KI-UDALALI, MBELEKO MBELEKO, UANAMTANDAO NA VIGEZO VINGINE UCHWARA VINAVYOZUIA DEMOKRASIA KUFANYA KAZI KATIKA UHALISIA WAKE NA KWA KUZINGATIA TAMADUNI ZA TAIFA LETU JUU YA HILO KAMWE HAYANA NAFASI 2015

Mara nyingi mtatizo ya ki-utawala kwa Rais Kikwete ama ndani ya chama chake au ndani ya serikali yake yanatokea mra nyingi kuwa ni ya kujitakia mwenyewe hasa kwa kuokota mawazo ya barabarani na kuyarasmisha kinyume na matarajio ya watu na vyombo sahihi vyenye dhamana, mamlaka na madaraka kamili kuyafikia maamuzi ya kisera kama hayo.

Ndio, nasema hiviii, hili la 'Urais kwa Majaribio kwa Umri wa Vijitoto' ni mfano hai wa matatizo ya kujitakia mwenyewe Rais wetu maana jambo hili wala si kitu rahisi kukublika kama anavyodhani ndani ya taifa lililofifishiwa matumaini kama hili la kwetu kwa mambo mengi kwenda kombo ki-uongozi. Hakika haya yote ni matatizo ya kujitakia kuzua mtafaruku baada ya mtafaruku na kuendeleza mipasuko ya ajabu ndani ya chama chake CCM.

Baya zaidi, kitendo cha mwana-CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe kugeuka Chief Decision-Maker on all unpopular policy issues within Chama Cha Mapinduzi fraternity na makada wa chama hicho wakiwemo wabunge kujikuta hawajui hili wala lile bali tu hulazimika kufuata maamuzi yake hayo kwa Rais Kikwete, hili nalo huenda likawafanya Wana-CCM wenye dhamana ya kufanya maamuzi kama hayo ya kisera (Policy Decisions) sio tu kumchukia zaidi kada huyo wa CHADEMA bali zaidi huenda wakamgomea ki-aina Mwenyekiti wao CCM taifa pamoja na DHANA POTOFU WA 'KUFANYIA MAJARIBIO YA WATANZANIA ZAIDI YA MILIONI 48 KWA KUWEKA 'URAIS WA TAIFA HILI MIKONONI MWAO VIJITOTO'. Na kwamba hayo yote yafanyike kwa hisani na maelekeze ya akina Zitto Kabwe na Januari Makamba.

Kiukweli maisha ya WaTanzania kufanyiwa nayo majaribio zaidi tena baada ya lile jaribio la dhana ya USPIKA KWA MISINGI YA JINSIA YA MTU kutuangukia vibaya mno kule bungeni, Umma wa Tanzania tunasema kwa kauli moja kwamba HAKIPITI KITU HAPA mpaka kupigiwa kura ya maoni kitaifa tena chini ya Tume Huru ya Uchaguzi ili sisi wenyewe wananchi wenye nchi hii tukayatolee maamuzi ya mwisho Contencious Constitutional issue kama hiyo na wala si vinginevyo.

Hakuna kuburuzwa mtu tena kwa mawazo ya kutoka kwenye ndoto ya mtu mmoja usingizini kwake kutwishwa kwenye mabega ya WTanzania karibia milioni 50 kulifuata tu kama kondoo bila kuhoji juu ya malengo yake na faida na hasara zitakazotokana na mambo kama hayo.

Binafsi naamini kwamba nchi yetu imekua ya amani wa kuigwa si ki-ajali tu bali ni kufuatia ukweli kwamba kuna baadhi ya mambo TULIJIZUIA KUJIINGIZA KAMA TAIFA, kama vile kuendekeza Urais KWA MISINGI WA UMRI WA 'VIJITOTO, Urais kwa misingi ya Dini ya mtu, Urais Kwa kufunuana nguo kuangalia kwanza JINSIA WALIZOUMBWA NAZO WATU, na vile vile hivi sasa tunaongeza kwenye orodha hiyo kujikatalia Urais wa Mbeleko kule kubebew tu mtu ndani ya gunia na watu kujistukia tu tumebwagiwa hata yule tusiemdhania kabisa ikulu Magogoni.

Rais wa JMT wa vipindi vijavyo watapatikana kwa kura ya wananchi moja kwa moja bila udalali wa ki-mbeleko mbeleko cha 'mwenzetu mara mwanamtandao' na kupitishwa kwa zengwe na ghiliba nyingi, urais wa aina hiyo haina nafasi tena katika Tanzania tunayoitaka mara baada ya Rais Kikwete; rais ajaye safari hii atapatikana kwa misingi yaUADILIFU, USHINDANI WA KUFA MTU, MHUSIKA MWENYEWE KUJINADI ANACHOKIFUATA IKULU na wla si mtu kutuletea tu vijivigezo mara usikie ooh safari hii KIGEZO ni mpaka mtu atoke mkoa wa Mwanza au Zanzibar ndio agombee urais.

Nasema hiviiiii, tuache kabisa mizaha katika taasisi hii kubwa aajabu na yenye kubeba matumaini ya mamilioni ya watu katika nchi na sasa kuanza kuliangalia sawa tu na cheo cha U-Katibu Kata vile.
 
wazo zuri alakini utekelezaji wake utakua mgumu sana kwani katiba mpya tunayoipigania itakua bado haijaanza kutumika kwani magamba na hila zao hawatakubali kuipitisha haraka.katiba ndio msingi imara katika kuleta usawa kwenye kila jambo,hasa masuala ya siasa,kwani siasa ndio inayoonekana kushika mhimili wote katika kuongoza taifa.elimu inahitajika sana katika hili suala la katiba mpya sio vijijini tu hata mijini kwani muamko unaoonekana vijijini ni mkuawa sana kuliko mijini ,hata jiji la daresalama linaonekana ndio liko nyuma kuliko hata wale wa vijijini.
 
Uwezo Tunao, tumekusikia, sisi ndio Watanzania na huo uliokuwepo ndio utaratibu wetu wa kumpata rais wetu na utaendelea hivi hivi kwa kufuata kanuni za Newtons Law of Motion " A body in Motion...". Tanzanian politics is a body in motion!.
 
Hao wenye umri mkubwa unaowataka wewe wameifanyia nini la maana TZ? Acha wivu wa kike! Kabila Jr, amekuwa rais na umri wa miaka 30.
 
KUFIKIA TAMATI KWA ULE UZI WA 'UFISADI BILA MAJIBU WATU FULANI WAJIUZULU NDANI YA SIKU 90' NDIO MWANZO WA UZI MPYA UNAOTAFSIRI MCHEZO WA BAO KISIASA NCHINI KATIKA MBIO HIZI KUNAKOELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015

Ile thread ndefu sana iliochukua miezi mitatu; 'UFISADI BILA MAJIBU: RAIS KIKWETE NA LOWASSA WAJIUZULU NDANI YA SIKU 90', iloendeshwa kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu hadi hivi sasa leo hii imefikia tamati yake.

Itakumbukwa kwamba katika uzi huo mwendeshaji wake, UWEZO TUNAO, aliweka bayana kwamba si kazi yake kwenda kuwafukuza watu fulani ofisini isipokua jukumu lake mle ni kule kuweka rekodi sawa kwenye kumbukumbu zetu katika historia kwamba kamwe hakunyamazia UFISADI wakati unapodaiwa kutendeka katika taifa letu.

Sasa kama watu waliotajwa saaaana ndani ya uzi ule bado watakua wameendelea KUGANGAMALA ki-kichwa ngumu tu kubakia katika ofisi husika bila ya kuchukua hatua stahiki kukaa pembeni ili uchunguzi huru ufanyike kubainisha kama madai dhidi yao yalikua ni ya kweli au laa, hiyo wala si jukumu la mwanaharakati UWEZO TUNAO kuwasemea kwanini wameamua kula jiwe katika nyadhifa hizo na ofisi za umma wakati kuna SINTOFAHAMU juu yao.

Na pale ambapo thread ile tajwa hapo juu inapotiaa tamati ndipo sasa kunapozaliwa THREAD nyingine murua itakayokua na malengo ya kuyaona mapema mazito ya kimkakati kisiasa ndani na nje ya vyama mbali mbali vya ushindani katika nchi yetu, viongozi wetu, na mchezo mzima wa siasa jinsi wanavyoicheza na wanavyoonekana kutokuichrza na kuyatolea maoni na tafsiri stahiki kwa faida ya Umma wa Tanzania ambayo JF imejitolea kuielimisha kiundani zaidi kupitia kwa wanachama wake akiwemo UWEZO TUNAO.

Ni vema pia ieleweke kwamba wakati THREAD hii mpya itakayoendelea mpaka wiki mbili mara baada ya Rais Mpya wa JMT kuapishwa huko 2015 itakua ikiongozwa hapa na pale na UWEZO TUNAO, uchangiaji wa kutofautiana kwa hoja ama kuunga mkono kwa misingi hiyo hiyo siku zote itabaki wazi kwa mwana JF yeyote atakayetembelea mahali hapa.

Karibuni katika hii safari nyingine ndefu mpaka pale ambapo Rais wa Walalahoi wa nchi hii atakapoapishwa bila udalali, ghiliba wala zengwe la aina yoyote ile.
 
Mkuu Pasco, heshima mbeele kwanza kama tai!!

E bwana e, tuaachwe watu tuamue wenyewe kuliko kuwafungia wengine milango nje shauri ya kigezo tu cha umri.

Hadi hapo ni muhimu kujiuliza kwamba tukitazama nyuma tunakotoka kama taifa, Tamaduni zetu za Kitaifa zinatuelekeza nini juu ya umri wa kupatikana mtu wa kugombea kiti cha urais katika nchi hii.

Na vile vile tukajihoji zaidi kwamba hizo hizo tamaduni zetu za kitaifa kupatikana kwa rais wa JMT zimetufaa kwa kiasi gani au zimepitwa na wakati kwa kiasi gani kiasi cha kutufanya leo hii tuondokane nazo? Je mizania ya faida na hasara juu ya uamuzi mzito kama huo wa ki-katiba unatuambia nini hadi hivi sasa?

Watu tujadili jambo hili with open minds bila kubeba SHUJAA WAKO KISIASA akilini mwako pindi unapoendelea kumwaga nguvu za hoja humu.

Uwezo Tunao, tumekusikia, sisi ndio Watanzania na huo uliokuwepo ndio utaratibu wetu wa kumpata rais wetu na utaendelea hivi hivi kwa kufuata kanuni za Newtons Law of Motion " A body in Motion...". Tanzanian politics is a body in motion!.
 
On the account of numerous leadership mis-sharps, mismanagement of public coffers, outright state-machinery backed vote rigging and the worse-off escalating instances of unabeted corruption in the country, does President Kikwete still have any MORAL AUTHORITY AND LEGITIMACY left of him to become a sole pace-setter for the public criteria to be followed to get Tanzania's net president?
 
Mkuu hoja yako imetulia kuliko kawaida.

Civil war or the military coup to overthrow the Goverment, no matter how the leader of the group of persons be, if is seventiny years old or twenty years old, he can be the President.

Lakini kwa tawala zetu za kiraia za Kiafrika bado hatujafikia kiwango cha kuanzia miaka 35 mtu
anaweza kuchaguliwa kuwa Rais, tusijidanganye bado wakati. ukomavu ndio muhimi ya muhimili
huo, kwa kuanzia miaka arobaini na kuendelea hicho ni kiwango kizuri.

Ukiangalia marais wote
walioanza na umri wa chini ya miaka arobaini, walianza vibaya kiutawala na walimalizia vibaya sana.
Kwa sababu walikuwa wanayumbishwa na washauri kutokana na wao kutoelewa wapi waelekee,
na mpaka wanaposhtuka muda unakuwa umeshapita bila ya kuwa na mema wala mafanikio.

Tuchulie mfano Hayati Nyerere, personal secretary wake alikuwa mwanamke mama wa kiingereza,
na ambaye alikuwa mshauri wake mkuu, sasa angalia iliwezekana vipi amshauri afuate siasa ya
ujamaa na kujitegemea, yaani Marxist wakati Uingereza hawapo katika mfumo huo, labda inawezekana
ulikuwa ni mfumo wa waingereza kuiangamiza nchi yetu bila kujijua.

Na yeye wakati huo hakuwa na
ukomavu na hakuelewa nini kinchoendelea. Ndio hivyo Mobutu alivyozungushwa akili na wabeligiji,
na ndio hivyo Gaddafi alivozungushwa akili na Warusi. kwa sababu ya kiungia katika madaraka bado
wadogo, na bila ukomavu na kushindwa kujiongoza wenyewe.

Huo ndio muono wangu. tupiganishe
akili na mawazo kuchambua uzuri na athari zake, kuhusu kigezo cha umri. ingawaje JK. alizungumzia
kuhusu ndani ya chama chake, lakini inafaa kujadiliwa pia na wanabodi.
 
Mie nilikuwa nafikiri Raisi huwa tunamchaguwa wenyewe kwa uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Labda tukubali tu kuwa chaguo letu haku zaa matarajio yetu.

Bora tuwe waangalifu tunapo mchaguwa. Sio kwa baby face wala jinsia bali kwa uwezo alionao. Na tuwe tayari kumtimuwa anapo vuruga mambo. Hili nadhani hata sasa laweza kufanyika. Lakini waTZ waoga na wana nidhamu sana na ndiyo maan akuna amani hadi leo.
 
Ni kweli 2015 tuongozwe na mambo makuu matatu kumpata rais kwa kura za wananchi;

(1) REKODI ZURU YA UADILIFU USIOACHA MASWALI KUHUSU KITU UFISADI

(2) RAIS MWENYE REKODI YA UWEZO KIUTENDAJI WENYE FAIDA KWA UMMA WA TANZANIA.

(3) MCHA MUNGU ANAYEMTEGEMEA MUNGU NA MUNGU TU KWA ULINZI WAKE NA MAAMUZI YAKE

Mie nilikuwa nafikiri Raisi huwa tunamchaguwa wenyewe kwa uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Labda tukubali tu kuwa chaguo letu haku zaa matarajio yetu.

Bora tuwe waangalifu tunapo mchaguwa. Sio kwa baby face wala jinsia bali kwa uwezo alionao. Na tuwe tayari kumtimuwa anapo vuruga mambo. Hili nadhani hata sasa laweza kufanyika. Lakini waTZ waoga na wana nidhamu sana na ndiyo maan akuna amani hadi leo.
 
KUFIKIA TAMATI KWA ULE UZI WA 'UFISADI BILA MAJIBU WATU FULANI WAJIUZULU NDANI YA SIKU 90' NDIO MWANZO WA UZI MPYA UNAOTAFSIRI MCHEZO WA BAO KISIASA NCHINI KATIKA MBIO HIZI KUNAKOELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015

Ile thread ndefu sana iliochukua miezi mitatu; 'UFISADI BILA MAJIBU: RAIS KIKWETE NA LOWASSA WAJIUZULU NDANI YA SIKU 90', iloendeshwa kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu hadi hivi sasa leo hii imefikia tamati yake.

Itakumbukwa kwamba katika uzi huo mwendeshaji wake, UWEZO TUNAO, aliweka bayana kwamba si kazi yake kwenda kuwafukuza watu fulani ofisini isipokua jukumu lake mle ni kule kuweka rekodi sawa kwenye kumbukumbu zetu katika historia kwamba kamwe hakunyamazia UFISADI wakati unapodaiwa kutendeka katika taifa letu.

Sasa kama watu waliotajwa saaaana ndani ya uzi ule bado watakua wameendelea KUGANGAMALA ki-kichwa ngumu tu kubakia katika ofisi husika bila ya kuchukua hatua stahiki kukaa pembeni ili uchunguzi huru ufanyike kubainisha kama madai dhidi yao yalikua ni ya kweli au laa, hiyo wala si jukumu la mwanaharakati UWEZO TUNAO kuwasemea kwanini wameamua kula jiwe katika nyadhifa hizo na ofisi za umma wakati kuna SINTOFAHAMU juu yao.

Na pale ambapo thread ile tajwa hapo juu inapotiaa tamati ndipo sasa kunapozaliwa THREAD nyingine murua itakayokua na malengo ya kuyaona mapema mazito ya kimkakati kisiasa ndani na nje ya vyama mbali mbali vya ushindani katika nchi yetu, viongozi wetu, na mchezo mzima wa siasa jinsi wanavyoicheza na wanavyoonekana kutokuichrza na kuyatolea maoni na tafsiri stahiki kwa faida ya Umma wa Tanzania ambayo JF imejitolea kuielimisha kiundani zaidi kupitia kwa wanachama wake akiwemo UWEZO TUNAO.

Ni vema pia ieleweke kwamba wakati THREAD hii mpya itakayoendelea mpaka wiki mbili mara baada ya Rais Mpya wa JMT kuapishwa huko 2015 itakua ikiongozwa hapa na pale na UWEZO TUNAO, uchangiaji wa kutofautiana kwa hoja ama kuunga mkono kwa misingi hiyo hiyo siku zote itabaki wazi kwa mwana JF yeyote atakayetembelea mahali hapa.

Karibuni katika hii safari nyingine ndefu mpaka pale ambapo Rais wa Walalahoi wa nchi hii atakapoapishwa bila udalali, ghiliba wala zengwe la aina yoyote ile.
Asante UT, uu miongoni mwa great thinkers wachache tulionao humu jukwaani!. Keep it up!.
 
tatizo ni mpango mkakati mbovu tunaouona hapa. jukumu la kuamua next presidential material sio la mtu au kikundi kidogo cha watu. ni mchakato unaohusu vyama husika kutuleta kwa watanzania wagombea wanaowakilisha vyama vyao na sisi kuchagua kati yao anetufaa. umri, kanda, kabila umbile sio kigezo
 
RAIS KIKWETE ANAPOMPIGA VITA MWALIMU JULIUS NYERERE KABURINI LEO HII KWA KUHIMIZA 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ALILOTUKATAZA WATANZANIA LICHA YA MADHARA MAKUBWA TUNAYOYAVUNA HIVI SASA KWAKE MWENYEWE HIVI SASA, YOTE NI KWA FAIDA YA NANI?

Rais Kikwete kamwe hawezi kurusiwa kwa mara ya tatu kufanyia majaribio ya kimaabara maisha ya WaTanzania kwa misingi ya kukamatishwa mawazo ya kiayawani barabarani kila kukicha huku taifaa likiendelea kuangamia kwa kiasi kikubwa kwa kila Jaribio la Kisiasa analolifnya ama ndani au nje ya chama chake.

By Candid Scope
ccccm.JPG


ccccm1.JPG

JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012


Mpaka hivi sasa, ni jambo lililo dhahiri kwa Watanzania waliowengi taifa limefikia hapa tulipofika kutokana na mambo matatu mazito ya kimajriobio hayo hayo.

Kwanza, madhara mazito yalioifikia taifa hili ilianza na jaribio la kwanza la kutumika dhna ya 'URAIS WA VIJITOTO' na matokeo yake tukampata Mhe Kikwete kuwa ndiye rais wa JMT licha ya Mwalimu Nyerere kuktalia jambo hili na kuonya kwa nguvu nyingi zaidi watu tusidhubuti kukumbatia jambo hili.

Kiukweli katika nchi hii hakuna hata mtu mmoja atakayeweza kusahau mambo gani ambayo yametupata na yanyoendelea kutupata kutokana na mtaji wa dhambi ya kwenda kinyume na ushauri wa Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere, kwa kukumbatia 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ambayo hivi sasa tena imempata dalali mpya kwa jina la Rais Jakaya M. Kikwete.

Sote hatuna shaka kwamba uongozi wa nchi si sawa na uongozi wa jimbo wala kata hivyo mtu gani akachaguliwe kuongoza WaTanzania zaidi ya milioni 48 si swala la kuchezea chezea.

Inasikitisha mno jinsi ambavyo urais wa nchi hii unavyoendelea kukosa thamani na hata kuanza kurahisishwa kiasi hiki kwa namna mbavyo hata Rais Kikwete anafika mahala anakwenda kujibana mahali kujadilian jambo linalogusa mustakabali wa nchi na vijitoto kwenye mazungumzo binafsi na akina Zitto Kabwe na Januari Makamba kwenye mgahawa na kisha kesho yake kuonelea kuwa sasa hizo ndoto binafsi sasa ziwe ni Mambo ya Ki-Katiba ambayo kila Mtanzania ataswa kuyafuata. Katu hatudanganyiki na mawazo ya barabarani ya aina hiyo.

Hapa chini ni kijisehemu tu cha baadhi ya hatua za kimajaribio ya kimaabara ya Rais Kikwete kudiriki kucheza kamari na mchezo wa potea pata na maisha ya mamilioni y WaTanzania kwa namna isivyofaa hata tone:

1. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijitokeza naa kamari ya kwanza kabisa ya kutuletea kitu walichokiita DAMU CHANGA (kwa maana ya Ndg Jakaya Mrisho Kikwete) kugombea kiti cha urais wa taifa letu.

Sote hivi sasa ni mashahidi jinsi gani kila kitu ndani ya nchi kimepuputika na tumebakiwa tu na janga la taifa kwa kukubaliana na uamuzi huo huo kufanya uchaguzi chini ya DHANA HIYO HIYO POTOFU LA 'URAIS WA NCHI KUKABIDHIWA VIJITOTO' ambao hata kusimamia tu mambo yao ya kimapenzi tu na visichana vyao yenyewe bado ni mtihani.

Kwa nini watu turudie kosa eti kwa jina tu la kuchagua UDOGO WA UMRI kama kigezo ki-kuu mtu kuongoza nchi??

2. Kwa mara nyingine Rais Kikwete mwenyewe, kwa mtiririko ule ule uliojaa MAWAZO YA KUKOMOA MAADUI WAKE, akaja na DHANA POTOFU nyingine kwamba bunge letu ambalo ni mhimili muhimu mno kikatiba kwa kazi ya kutunga sheria za nchi sasa kiongozi wake kwa maana ya spika ili apatikane ni sharti KILA MMOJA WAO AMA AVUE SURUALI AU SKETI KUMTAMBUA JINSIA ALIVYOUMBWA halafu eti kwa kigezo hicho tu ikawa ni leseni kwa baadhi ya washindani kuwashinda wengine kwenye kinyang'anyiro na kuibuka kuwa MA-SPIKA UBWETE AMBAO KILA SIKU UFANYAJI WAKE KAZI NI MADUDU MATUPU NA KAZI NYINGINE NI KUDAI TU POSHO.

Sasa hivi nako chaguo letu kwa kuzingatia DHANA POTOFU LA JINSI nalo linatutokea puani mpaka kinamma wanaharakati kulazimika kuingia barabarani kupinga jinsi gani Spika Anne Makinda anavyowadhalilisha kwa maamuzi yake ya ki-shabiki hata kwa masuala mazito kwa mustakabali mzima wa nchi.

Kweli Rais Kikwete bado tu huoni jinsi gani ulivyotuuza hadi hapo na bunge kuonekana kupwaya ajabu kutokana na mojawapo misururu ya mi-dhana yako yanayopingana na katiba ulioapa kulinda?

3. Kwa jinsi ambavyo Rais Kikwete amedhihirisha wazi kwa umma wa Tanzania kwamba yeye na MAFISADI nchini ni damdam, leo hii anapata wapi uhalali mbele ya uso wa jami na ujasiri uliomshinda kuwavua gamba mafisadi, eti kuja kuliambia taifa na wala si CCM yake kwamba Rais wa Tanzania ajaye atakua ni mtu wa aina hivi mara vile??

Mwenzetu huyu kwa jinsi alivyoongoza kwa KUKUMBATIA MAFISADI Tanzania na kutumia dola kuua wananchi kila kona ya taifa hili, moja kwa moja inamfanya awe ni mtu ambaye hana MORAL AUTHORITY kutuambia wananchi kwamba Rais ajaye atakua ni wa namna gani vile.

4. Isitoshe, masuala ya raia yupi mwenye umri gani ataweza KUWA NA HAKI YA KUZALIWA KUJITOKEZA KUCHAGUA AU KUCHAGULIWA kwa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya mipaka hii ni SUALA NYETI NA LA MSINGI KI-KATIBA ya JMT hivyo hakuna mtu yeyote au taasisi itakayojifurahisha na njozi zake mwenyewe kulivibadilishia vichochoroni huko Magogoni kwa malengo yasio na faida kwa Umma wa Tanzania.

Hivyo, mabadiliko makubwa kama haya eti kwa ajili tu ya HIVI VIJITOTO FISADI ni sharti kwanza tuletewe wananchi kwenye REFERENDUM ILI TUKAIPITISHE KWENYE TNURI LA KIDEMOKRASIA halisi.

5. CCM ikitaka a political showdown wa aina yoyote eti kwa ghiliba hizo hizo wanazozitumia hivi sasa kuzuia baadhi ya watu wenye hamu kubwa ya kugombea urais ndani ya chama chao, na sasa waanze kuvusha ghiliba hizo hizo kwenda kwa vyama vingine kwa kutaka URAIS WA HIVO VITOTO VIWILI VIWAKILISHI NA VINARA WA MAFISADI NCHINI, CHADEMA kipo katika nafasi zuri mara 50 zaidi ya hapo kugeuza ghilib hii mpya kurojeka zaidi ya uji na tena nda ya kipindi kifupi haijawahi kuonekana.


URAIS wa taifa hili kwa msururu wa dhana potofu kama vile JINSIA na au UMRI hauna nafasi hata kidogo kwa nchi hii mpaka mawazo ambayo ni HIGHLY CONTENCIOUS kama hayo yawe yamepitishwa kwenye KURA YA MAONI KITAIFA ikisimamiwa na Tume Huru ya uchaguzi ambalo si hili tume la huyu Jaji wa Mondo, Kondoa.

NOTE:
Na kama huu ndio mkondo mpya wa kutekeleza ile azma ya Rais Kikwete kwamba 'ninapoondoka madarakani uongozi wa nchi simuachii Mtanzania Mkristo ng'o' basi wenye mawazo haya mhesabu kula ya chuya kwa kuwa hamjafaulu bado katika hili la urais wa Januari Maakamba na na Zitto Kabwe!!!

Source: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015 « Zitto na Demokrasia

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015



KABWE ZUBERI ZITTO, MPKIGOMA KASKAZINI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015

Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais'.

Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais.


Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama changu, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.


Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais.

Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu.

Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu.

Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.


Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.


Dar es Salaam29 Februari 2012
 
MASIKIO YA KUTOBOLEWA KUSHOTO NA KULIA KWA HUYU KIJANA 'HAOI SUMARI' SASA KUKIGHARIMU CCM UBUNGE ARUMERU MASHARIKI BAADA YA WASHILI KUKANA TABIA HIYO KWENDA KINYUME NA MILA NA DESTURI YA WAMERU

Kwa nchi za Magharibi mwanamme hata akiamua kutoboa masikio na kuvaa hereni au hata kutoboa ulimi na kuipamba kama ya ndugu yetu Ben Kinyaia wala hakuna ajabu yoyote katika hilo.

Ila mwanamme mtu mzima mwenye kustahili kuwa na mji wake anapofanya mambo kama haya kiukweli jamii yetu hatujafika mahala kubariki kitendo kama hicho Tanzania hii.

Sasa pale inapotokea kwamba mtu kama huyo anayesadikiwa na mambo ya kwenda kinyume kabisa na mila na desturi ya jamii yetu hii pindi anapoamua kupanda jukwaani kuomba nafasi ya uongozi katika ngazi yoyote ile ni wazi kwamba hiyo ni sababu tosha ya kufanya jamii imkatae kabisa na kumtupilia mbali kabisa kwa kuwekwa katika kundi moja na wanaume ambao hupendelea kujikabidhi miili yao kwa kutumika na wanaume wenzake.

Mpaka hapo naona tatizo kubwa kuliko hata ukubwa wa mlima Meru ikiwa imesimama mbele yake huyu mgombea wa CCM kule Arumeru Mashariki kuwa na deni kubwa ya kujitenga kule na haya madai mazito ya kujumuishwa katika fungu moja na Mashoga nchini.
 
Je zile siku 100 za KJ 2458 zinaisha lini?

Pia kuna watu wanasema serikali hii haitafika April.
 
Naona kama vile mwenzetu aidha utakua umekosea THREAD unayoizungumzia au kidogo tatizo liko tu kwenye kuchanganya madesa hadi hapo. Wala hakuna lingine hapo.

Ukiangalia hapo kwenye RED; hilo la siku 100 ni kama vile umeleta habari mpya kabisaaa ambayo chanzo chake ni wewe mwenyewe hivyo zitaisha lini mwenzetu msaada tunausubiri kwako.

Nalo hilo la 'Aprili' na kwamba 'watu' wasiofahamika wanasema na wapi wanasemea, kivipi na lini yote hayo umetunyima fursa ya kujifunza nazo toka kwako.

Labda tu niseme ni vema ukajipanga upya kwani kuna kila dalili kwamba unalo jambo zuri tu unalotamani kulifahamisha JF pamoja na sisi wasomaji wako ila tu mahesabu ndio yanakwenda yanakugomea vile.

Kwa wakati huo utakapokua ukijiandaa upya bila kua na dalili zozote za kuchanganya desa kule, vile vile naona kuna umuhimu nikushauri ukaipitie posti namba 6 ya kwenye uzi huu ile mwenzetu ukapate kujiridhisha zaidi mwelekeo wa kile ulichotamani kutuambia.

Karibu Jukwaani.


Je zile siku 100 za KJ 2458 zinaisha lini?

Pia kuna watu wanasema serikali hii haitafika April.
 
Jamani pale ahadi zinapozidi uwezo na ukosefu wa mikakati ya wazi, kila utakachosema baada ya hapo hata kama ina maana sana tu watu huchukulia kuwa ni yale yale na kuona kila kitu ni usanii ule ule tu.

Masikini ahadi za CCM zisizotekelezeka sasa kugeuka kaburi la chama hiki kisiasa kila kona ya taifa hili na wapiga kura kugubikwa na chuki moyoni usiolezeka kirahisi!!!


Mbona JK hawajampiga mayai viza! Wanafiki. tazama chini hapo:

AHADI ZA CCM UCHAGUZI MKUU 2010

Ninyi watoto wa nyoka acheni kumwaga sumu humu. Mmezewea majungu kama wazazi wenu. Kila kukicha huyu hivi yule vipi. fitna na majungu hamna issue?

Haya pelekeni list hii hapa chini kwa hao waliowatuma maana wamejisahau ni nini waliahidi na wajibu wao ni upi.

1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora

2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini

3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga

4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga

5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma

6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini

7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma

8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera

9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera

10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini

11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini

12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera

13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera

14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera

15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya

16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera

17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali

18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza

19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza

20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita

21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba

22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro

23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini

24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa

25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea

26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya

27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga

28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa

29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro

30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini

31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora

32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu

33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini

34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara

35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma

36.Kulinda haki za walemavu - Makete

37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini

38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha

39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini

40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora

41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini

42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma

43.Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido

44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga

45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini

46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma

47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido

48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro

49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara

50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini

51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini

52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa

53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa

54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa

55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda

56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara

57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa

58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar

59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar

60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti

61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma

62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma

63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma

64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma

65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam

66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara

67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha

68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha

69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
70 ...
 
Watu tunasubiri kwa hamu kubwa kuona jinsi gani CCM kama taasisi inavyoenda Arumeru Mashariki kumpigia kampeni Mbunge binafsi wa Kambi ya Ndg Lowassa mara baada ya kuiumbua taasisi hiyo ya kichama kwenye marudio ya kura ya maoni jimboni hapo.

CCM kulamba matapishi yake baada ya mgombea wa kambi ya Rais Kikwete kutupwa nje? Watu wanasubiri kwa hamu kuona unafiki na uzandiki unavyojitokeza hadharani majukwaani hivi karibuni tena bila kuwa na uso wa aibu kwa wanamagamba hawa.
 
Back
Top Bottom