Tayari nimepanga kutembelea vyombo zaidi vya habari

Status
Not open for further replies.
Kama kawaida yake Tambwe v2.0,
Anaanzisha thread kisha anatimka bila kuzingatia kuwa kuna watu wamemuuliza maswali na yanahitaji majibu. Hata hivyo sishangai maana ndiyo jadi yake.
 
Kidumu..Kaka umewashika pabaya,,Ukiona mtu anapiga kelele lazima ujue gemu ngumu,,.CCM ipo na itazidi kuwepo..Sababu hakuna viongozi makini na imara Nje ya CCM..Mwendo huohuo watakimbia tuu,tubaki wenye nia ya KWELI na DHATI.
 
Nape,

Ningependa kujua kuhusu suala la kuvuana Magamba maana siku tisini zinakaribia kuisha, natanguliza shukrani.
 
Nimesoma thread ya vita dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na lile la ziara yangu kwenye vyombo vya habari. Nimejaribu kujibu lakini naona mara tu baada ya kuingia threda zile zinahamishwa mara hii huku ukirudi unakuta imeshapelekwa kwingine hivyo mtirirko wa hoja unakuwa tabu.... Hizi ni hoja mbili tofauti na ndo maana nimeamua kuanzisha nyingine maana mkanganyo unaozungushwa kule sijajua ni nini?

Mods ni ya kweli hayo asemayo....? au ndio majungu, uongo, kupakana matope na kuharibiana Jamvi letu
 
tatizo la wanasiasa ni kuwa wakizusha wao wanataka uzushi wao uonekane ni ukweli mtakatifu, wakizushiwa wao wanataka ionekane ni dhambi isiyosameheka. Nape ukikubali kuwa bondia usiogope ngumi za uso na ukiwa mfungwa uchagui gereza.

Usianze kufundisha watu ustaharabu wakati chama chako ndio mabingwa wa siasa za maji taka na uzushi, nyinyi wenyewe ktk vikao vyenu mmeweka mkakati wa kuingiza vijana wenu humu JF kujibu mashambulizi na kushambulia yaani kukitetea CHAMA CHA KUJIVUA GAMBA kwa lolote, halafu unakuja humu unasema wanaoleta uzushi humu wanaua hii FORUM sasa unataka uonekane mstaarabu na mwenye busara sana au?

KIMSINGI tunawakaribisha sana hao vijana mlio waandaa akiwemona January na bila kuwatenga mzee MUKAMA na MSEKWA. Mkumbuke kuwa jukwaa hili ni huru na ustaarabu ni jadi yetu, tujadili kwa hoja na si kutuwekea vitisho kama ilivyo ada yenu, humu jukwaani hatutishiani POLISI wala USALAMA WA TAIFA. Hoja na uzalendo ndio msingi mkuu wa jukwaa, waambieni mlio watuma wawe na uvumilivu wakishindwa kwa hoja wasilete matusi na vitisho wakipigwa BAN waanze kupiga yowe ktk magazeti halafu wanarudi humu wakiwa wamebadili ID zao.
 
Kidumu..Kaka umewashika pabaya,,Ukiona mtu anapiga kelele lazima ujue gemu ngumu,,.CCM ipo na itazidi kuwepo..Sababu hakuna viongozi makini na imara Nje ya CCM..Mwendo huohuo watakimbia tuu,tubaki wenye nia ya KWELI na DHATI.[/Q

Eti "hakuna viongozi makini na imara Nje ya CCM" kama usemayo ni kweli basi maneno IMARA na MAKINI yamepoteza maana yake ya asili. Tusipende kuongea maneno ya kisiasa katika JUKWAA makini kama hili, ni vyema maneno hayo muyatamke mnapokuwa kwenye vikao vyenu vya SHINA na CCM family. Hivi kama usemacho unakipima mbona mnavuana GAMBA? Halafu GAMBA halivuliki? Hivi ukizungumza VIONGOZI wenu ni MAKINI na IMARA unamjumuisha na JK?
 
Sasa unatembele hizo media hausi kujifunza au kuwaelekeza nini cha kuandika? Mbona ziara yako malengo yake hayaelweki?
 
Mnape Jr unaongela uzushi ??? are you serious ??? hivi kuna mzushi na muongo zaidi ya boss wako wa propaganda ? Tambwe hiza. Nape tangu umepata hicho cheo umeanza kupotea njia Leo wewe ni mtu wa kudhihaki gari la wagonjwa kisa gari hilo katoa mbunge wa chadema? halafu sasa hivi unakurupuka sana unaongea ongea hovyo, huwa najiuliza huyu ndiyo nape niliyekuwa namsikia na kumsoma.

Juzi mbowe karejesha Shangingi kuokoa fedha za serikali umenukuriwa ukimpongeza kisha ukasema anatafuta umaarufu wa 2015, ulinishangaza sana nikajua kweli siku hizi haunazo. kwa kizazi hiki mtu akiipenda ccm hana budi kuwa na moyo wa mwenda wazimu
 
Wakati mwingine nasikitika sana kwa mambo yanayoendelea kuipa sura hii jf, inanisikitisha. Pamoja na yote yanayoendelea na kusemwa kote JF bado ni mahali ambapo ukipita utapata kitu, hutatoka bila kitu ndivyo nilivyozoea au tulivyozoea wengi wetu, lakini hali inayoendelea kwasasa inatutia uvivu wengi kuja hapa na si ajabu wako wengi ambao wameshakata tamaa ya kuja hapa kwasababu ndio forum inayoongoza kwasasa kwa habari za kutunga na kuzusha, hatuitendei haki jamii na wadau wakubwa wa forum hii.

Kila kukicha watu hapa wana tunga uongo na kuzusha kama vile ni kweli na wana hakika na wanayoyasema, si ndo maana kuna sehemu ya tetesi basi walau kama huna hakika?

Nimesoma thread ya vita dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na lile la ziara yangu kwenye vyombo vya habari. Nimejaribu kujibu lakini naona mara tu baada ya kuingia threda zile zinahamishwa mara hii huku ukirudi unakuta imeshapelekwa kwingine hivyo mtirirko wa hoja unakuwa tabu.... Hizi ni hoja mbili tofauti na ndo maana nimeamua kuanzisha nyingine maana mkanganyo unaozungushwa kule sijajua ni nini?

Lakini kwa kifupi, tumeandika barua kwenye vyombo vyote vya habari(news rooms) kuzitembelea wakiwemo mwananchi, na ratiba ilishapangwa kuwatembelea, na hata hao tanzania daima nitakwenda na ratiba ipo muda mrefu, sasa huu uzushi mara ooh nape kapeleka sijui taarifa gani kwenye kikao unatoka wapi? Swala hili hata kwenye kikao halijafika ni mpango wa kazi wa ndani ya idara, hichi si chama cha mfukoni hii taasisi kila idara ina mipango yake, sasa hicho kikao cha wapi?

But naamini watu wako kazini zaidi, lakini hata kama ni kazi ya propaganda huwa haifanywi hivyo, uongo wa wazi kabisa na kujaribu kupandikiza chuki'''''' hii imepitiliza.......

Tusiharibu hadhi ya forum hii kwa kuzusha maneno ya siyo na ukweli hata chembe..... Kweli ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huviwezi.......

wewe fanya juhudi adui yako lowassa muda si mrefu anakutia hatiani sijui akichukua chama chake wewe utakimbilia wapi?
 
Nilikusikia wakati ukisema uongo na kuunganisha maneno ya ovyo juu ya Mbowe kurudisha shangingi, umezalisha tabia ya uongo, fitina na umbeya katika siasa sasa vimeanza kukuuma unalia kutaka huruma na bado watakushughulikia mpaka utasikia kichefuchefu mi yangu macha na ubongo. Walikushauri ustupe mawe wakati umejificha kwenye ya vioo
 
Mh.Nape ninamashaka na ukweli na nia yako na ushauri kuhusu hali ya hewa hapa jamvini kwaa sababu zifuatazo ni CCM hiyo hiyo iliyotamka ya kua JF inakichafu na kua JF ni ya CHADEMA au inatumiwa na CHADEMA,ni CCM hiyo hiyo iliyoapa kupambana na JF,Ni wewe mmoja ya kiongozi wa CCM unaeisifia JF kua ni sehemu unapoweza kupata kitu kwa mtiliriko wa hoja yako tunashindwa kuelewa umesimama wapi.Je CCM inatumia mbinu gani kupambana na JF kama ilivyoahidi kufanya,ebu tujuze labda zitatuondolea kushuku kua kupandikizwaa mamruki wa kutuma habari za uzushi sio moja ya mbinu ya CCM kuichafuria jina JF ili ionekane ni mahala pa uzushi na madudu yote yanayofanywa na chama tawala yanayoanikwa hapa yaonekane ni ya uongo!Mh.Nape kwa mambo yanayoendelea ndani ya CCM na serikali mchawi wenu mtafuteni huko huko.Nani asiyefahamu kwamba uzushi majungu ni moja ya nguzo ya chama tawala,nani asiefahamu ya kua kwa serikali na CCM kwa yeyote anaeikoso ni mtovu wa nidhamu na adui hata kama unaosemwa ni ukweli?Mh.Nape mambo mengi mazito yamekua yakijadiliwa hapa jamvini ambapo kama yangepata ushiriki wako labda tungekua tunapata picha kamili katika baadhi ya mambo mazito lakini hujitokezi tunajua unakazi nyingi lakini kama umepata muda kutoa maoni yako kwa jambo hili jepesi la ziara zako vyombo vya habari tunaimani unaweza kupata muda walau mara moja kuzungumzia mambo mazito.Kama kuna habari muhimu vyombo vya habari vitakufuata vyenyewe.Mwisho mkanganyiko na kauli zinazokinzani katika serikali na chama tawala CCM ni moja ya sababu ya hali inayojitokeza.Unaweza kua na nia nzuri lakini kua na nia nzuri chini ya chama cha chako na nidhamu ya chama chako inatutia MASHAKA!
 
Oh dear,nape kwa ujengaji hoja huu chama gamba kitatoka madarakani kabla ya 2015 as slaa predicted
 
Wakati mwingine nasikitika sana kwa mambo yanayoendelea kuipa sura hii jf, inanisikitisha. Pamoja na yote yanayoendelea na kusemwa kote JF bado ni mahali ambapo ukipita utapata kitu, hutatoka bila kitu ndivyo nilivyozoea au tulivyozoea wengi wetu, lakini hali inayoendelea kwasasa inatutia uvivu wengi kuja hapa na si ajabu wako wengi ambao wameshakata tamaa ya kuja hapa kwasababu ndio forum inayoongoza kwasasa kwa habari za kutunga na kuzusha, hatuitendei haki jamii na wadau wakubwa wa forum hii. ........


Nape
  • unakumbuka wakati unapinga juu ya ule mradi wa Jengo la UVCMM. Unajua kuna waktu mpaka leo kuna kundi la watu wanasikitika juu ya hoja zako kuwa zilikuwa ni zakupotosha ?
  • Unajua maana ya demokrasio sio lazima watu wawe na mtazamo mmoja lakini kinachotakiwa ni hoja zenye mshiko?

Nape ukweli Kwa sasa unapata uvivu wa kuja hapa sababu umeshasogezwa karibu na "jikoni" au uko jikoni. Huwezi kuanza kuwatazama wapishi kwa jicho lile lile ulilokuwa unawatazama nalo mika saba au nane iliyopita.

Elewe sio waote wanaokukosoa wako sahihi na wewe sio mara zote hoja zako ni sahihi. Ukikiri na kubali hilo utakuwa na amani. tatizo lenu nyine wanaisasa mnadhani ndio mnajua kila kitu. Sikilizeni watu na kubalini na badilisheni njia mnapokosea

Mh.Nape ninamashaka na ukweli na nia yako na ushauri kuhusu hali ya hewa hapa jamvini kwaa sababu zifuatazo ni CCM hiyo hiyo iliyotamka ya kua JF inakichafu na kua JF ni ya CHADEMA au inatumiwa

Nje ya tpic lakini next time usichague colur na font ya ain hii, Unaumiza watu macho.
 
Kidumu..Kaka umewashika pabaya,,Ukiona mtu anapiga kelele lazima ujue gemu ngumu,,.CCM ipo na itazidi kuwepo..Sababu hakuna viongozi makini na imara Nje ya CCM..Mwendo huohuo watakimbia tuu,tubaki wenye nia ya KWELI na DHATI.
IMARA ktk ufisadi,na MAKINI ktk kuiba kura na kudai POSHO,
 
Mh.Nape ninamashaka na ukweli na nia yako na ushauri kuhusu hali ya hewa hapa jamvini kwaa sababu zifuatazo ni CCM hiyo hiyo iliyotamka ya kua JF inakichafu na kua JF ni ya CHADEMA au inatumiwa na CHADEMA,ni CCM hiyo hiyo iliyoapa kupambana na JF,Ni wewe mmoja ya kiongozi wa CCM unaeisifia JF kua ni sehemu unapoweza kupata kitu kwa mtiliriko wa hoja yako tunashindwa kuelewa umesimama wapi.Je CCM inatumia mbinu gani kupambana na JF kama ilivyoahidi kufanya,ebu tujuze labda zitatuondolea kushuku kua kupandikizwaa mamruki wa kutuma habari za uzushi sio moja ya mbinu ya CCM kuichafuria jina JF ili ionekane ni mahala pa uzushi na madudu yote yanayofanywa na chama tawala yanayoanikwa hapa yaonekane ni ya uongo!Mh.Nape kwa mambo yanayoendelea ndani ya CCM na serikali mchawi wenu mtafuteni huko huko.Nani asiyefahamu kwamba uzushi majungu ni moja ya nguzo ya chama tawala,nani asiefahamu ya kua kwa serikali na CCM kwa yeyote anaeikoso ni mtovu wa nidhamu na adui hata kama unaosemwa ni ukweli?Mh.Nape mambo mengi mazito yamekua yakijadiliwa hapa jamvini ambapo kama yangepata ushiriki wako labda tungekua tunapata picha kamili katika baadhi ya mambo mazito lakini hujitokezi tunajua unakazi nyingi lakini kama umepata muda kutoa maoni yako kwa jambo hili jepesi la ziara zako vyombo vya habari tunaimani unaweza kupata muda walau mara moja kuzungumzia mambo mazito.Kama kuna habari muhimu vyombo vya habari vitakufuata vyenyewe.Mwisho mkanganyiko na kauli zinazokinzani katika serikali na chama tawala CCM ni moja ya sababu ya hali inayojitokeza.Unaweza kua na nia nzuri lakini kua na nia nzuri chini ya chama cha chako na nidhamu ya chama chako inatutia MASHAKA1

Urembo wa rangi kwenye maandishi nadhani hauna tija, mbwembwe hizi fanya kwenye barua za mapenzi, mimi siwezi kusoma comment yako unaniumiza macho bila sababu, lingine macho yangu hayana lens ya kuyakuza hayo maandishi yako.
 
I totally agree with you Nape. Kuna uzushi, majungu na hoja nyingine za uwongo humu jamvini, hasa kwenye "jukwaa la siasa". However, there are credible people in this forum who almost always produce useful information. Also, other topics in this forums are quite useful to many of us. Try the Education topic, jobs, software and downloads, etc etcIn the present format of the forum where everybody sends in what they think it is worth sending out, and comes out "as it is", you can not avoid hayo majungu na uwongo. Najua MOD wanajitahidi sana ku-check the balance but it is almost an impossible task to filter all information coming in.Remember, there is no editorial board that review the contents of threads before they come out, so to blame the forum is basically an indication that one do not understand the notion of free speech. You pick what is useful and leave what is useless to you, period.
Thus, making it even more important to include the JF headquarter in Nape's program of visiting house media, so he can exchange views with Maxence and Mods & other staff at JF. Go Nape go...... I salute JF and all its members!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom