Tayari nimepanga kutembelea vyombo zaidi vya habari

Status
Not open for further replies.
Nape sijui vipi huyu jamaaa...........

Mambo yake yamekaa kama F-16. Anakuja na kuachia kombora na huyooo anatimka zake kurudi kwenye Base.

Si ajabu hurudi tena kama MGENI ili asionekane na hapo huwa anaangalia watu wanamjibu vipi......

Mods, habari kama hizi, ni kweli muwe mnazifuta. Kama hawezi kuandika na abaki kutetea kile alichokiandika, hamna haja ya kuendelea kuziacha hizo habari hapa JF. Mbona FB huwa anaandika na baadaye kubaki kutetea? Au kwa sababu watoto wa Magamba huwa wanamsifia siyo?

Mwanzo nilipomsikia jamaa, nilikuwa naona ni mzinga wa BUSARA. Ila leo, nimegundua jamaa ni ...................

Nape hebu waige vijana wenzio kama Mnyika, Zitto, Lema nk nk. Kijana bado mdogo kabisa na tayari KOTI lako lina Chawa kibao?
 
Nape:
Kaushauri kadogo tu.
Punguza wingi wa Thread Humu. Sijui ni kwanini umeanzisha Thread kama hii?
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Nape Jr. Iwapo utakomaa ki-Bill@, utawatandika wengi sana kwa hoja na kuwafukuzilia mbali, Ila inabidi uwe na muda wa Mzee wa Kijiji wa kukaa mtandaoni kwa muda mrefu sana, kitu ambacho kwa majukumu makubwa uliyobebeshwa na chama sidhani kama utaweza. Hata hivyo ujumbe wako umefika
 
Nape ni mpuuzi sana .Mtumwa wa mawazo hata kwenye jina utaona eti Mnauye Jr upuuzi wako umeanzia hapo . KUharibu forum hii inaharibiwa na wajinga toka huko kwenu kila kukija wanakuja na uvumi , tetesi nk . Ndiyo maana wanajibiwa kwa kadiri wanavyo kuja .Nawe unapata majibu yako kwa kadiri unavyo andika .Chama gani ni kama NGO ambacho kinakunyima usingizi ?Unapayuka sana .
 
Tusiharibu hadhi ya forum hii kwa kuzusha maneno ya siyo na ukweli hata chembe..... Kweli ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huviwezi.......

Ni sahihi na kweli, hadhi ya jamii forum ni kubwa japo watu wa idara za propaganda ya vyama vya siasa inajaribu kupenyeza siasa chafu ndani ya JF lakini ukweli unabaki pale pale JF ni kwa ajili ya waelevu [Intellectuals]. Hizo zingine thread zenye mlengo wa kudumaza uelewe na mfumo wa kujuzuna ni vitu vyepesi visivyo na mashiko.

Itamuuma sana mwelevu akitukanwa au kubezwa na mwelevu mwenzie lakini itakuwa haina maana yoyote kwa mwelevu kutukanwa au kubezwa na mtu asiye mwelevu kwake.Mwalimu alipata kusema mwelevu akikushauli jambo la kipambavu na anajua kuwa anakushauli upumbavu nawe ukaukubali upumbavu ule atakuzarau sana sana.Na mimi naongezea hapo kuwa nitamdharau kuliko nitakavyomzarau mjinga.

Jamii Forum inamchango mkubwa kwa jamii ya waelevu [Intellectuals] ambao kwa namna nyingineyo yoyote wanachangia kwa kiwango kikubwa sana katika ustawi wa TAIFA MAMA TANZANIA.

Bila kujali itikadi yoyote ya kisiasa wala dini humu ndani JF wanajamii wanapeana taarifa,maaarifa,burudani nk.Hivyo hao wengine ambao dhahili wewe kama mtu wa kitengo cha habari na propaganda ndani ya chama chako, unajua dhahili wanachangia kupoteza maana ya JF, ni wa kudharauliwa kama Mwalimu alivyotamka.Hivyo hata uchangiaji wa wa thread unaangaliwa na upeo wa mtoa thread katika ufahamu wa hayo anayoyazungumzia.

Itakuwa kicheko kwa mwelevu kwenda kuchangia thread kwa Mtu ambae dhahili inaonekana aelewi nini anachokizungumzia au kwa makusudi ameamua kupotosha ukweli,kwangu mimi naita ni uchizi.

JF ni jukwaa huru hivyo kila mmoja wetu ana uhuru kulitumia ila tu asivunje sheria halali zinazotawala jukwaa hili.

Ushauri kwa wale wote wanaoeneza hayo wanayofikiri waelevu wanayameza ndani ya jukwaa hili, thubutu nina hakika waelevu [Intellectuals] wote humu ndani ya JF, pumba na makapi uacha humu humu na wana JF makini uondoka na vitu muhimu [Content].

Wengi wetu humu ni kizazi cha Intellectuals wa DOTCOM GENERATION [DG],ukiwemo wewe nape,lakini mbinu ya kufikisha ujumbe wa kuyakataa haya yanayopatikana humu [taarifa, maarifa] ndani ya Jukwaa la JF ndio sio sahihi.Mbinu zianazotumika humu dhahili niza kizamani sana,zile za kupandikiza shetani [devil],wazee wetu enzi hizo za vita baridi, zama za kizazi cha TYPWRITER GENERATION [TG].

Hata wewe nape kamwe kamwe bro usikubali kamwe kutumia mbinu ya kupambana na adui kwa kumfuta kwa stahili hiyo ya kizamani ya kila anayekupinga wewe ni adui yako. No msogelee huyo anayekupinga na kuishi naye ujifunze hicho huyo anayekupinga anachojivunia na mbele ya safari wewe na yeye mtasafiri boti mmoja.

Kukubali kuwa binadamu wote tunatofauti na kila mtu mungu amempa karama zake,ukikazania kukijenga chama chako kwa mbinu za wazazi wetu wa miaka hiyo ya TG bro itakula kwako.Jenga hoja karibisha midahalo hata kama yatakayosemwa ni machungiu kwa chama chako. Uchungu huo ndio utakuwa TIBA kwa chama chako.Manake hata ugonjwa mkali kwa binadamu wakati mwingine utolewa kwa dawa chungu.Kungoa jina au kukamua JIPU kwaitaji maumivu ndivyo hiyo vivyo kwa chama chako kuludi kukubalika kwa kundi la DG yaitajika mbinu za kisasa na zenye kukubalika na ambazo ziko wazi sana na nyepesi sana kutumika.

Mbinu hizo zitatumika tu kma sitasimamiwa na kuratibiwa na kizazi chako cha DOTCOM GENERATION,haswa Intellectuals wa kizazi hiki na sio wazee wanaosinzia kwenye mikutano na mabunge yetu.

Naomba nikuuulize siunajua kuwa IPOD ikitoka leo USA baada ya siku chache vijana wa kitanzania watakuwa nayo mkononi,ukiforecast life style miaka ishirini kwa umri wako wa sasa ndio unatakuwa japo umefika makamo ya utu uzima, mbele unaona nini? kwa wadogo zako wa sasa wanaochezea simu za mikononi, majumbani.Ni maisha mengine kabisa na sio maisha ya wazee wetu waliosoma kwa kwenda kilometer tatu kwa miguu, lakini wanalazimisha kutuamulia maisha ya kizazi kijacho ambacho wao hawatakuwapo.Na mpenda mzee Mwinyi na usemi wake wa kila kizazi na vitabu vyake.

Mwisho JF kamwe iko pale pale, kama kuna mtu anafikili itapoteza maana thubutu, This is evolution, ni kwa faida yako wewe na wale wote kizazi hiki kinahusika kuitumia.Cha msingi Wana JF, mimi na wewe tunaitaji Tanzania yenye faida kwa watanzania wote na hata hayo maisha bora ambayo ndio kauri mbiu ya chama chako yanawezekana ndani ya Taifa hili.Ila ni vision yako, mimi na wana JF ambao ni DOTCOM GENERATION tunaifikisha huko pasi kuangalia nani ni mfuasi wa chama gani.Mara nyingi ikitokea nikaongea na wazee wetu wa miaka yao uwa awaamini kuwa ndani ya miaka Kumi na Tano, Taifa hili la Watanzania linaweza kuwa sawa na Malasia au nchi yoyote kutoka Tiger Countries.Wao kazi yao kutumia vipimo kama demokrasia ya Marekani imechukua miaka mia mbili hivyo sisi bado tu wachanga,miaka Hamsini [50] unadhubutu kuita Taifa hili changa. [Shame on You, wale wote mnaosema Taifa hili bado changa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!].

Mnanitukana mimi,baadhi ya Wana JF, Nape na hata Ndugu Mbowe nafikiri ni kizazi baada ya uhuru vijana wote waliozaliwa baada ya uhuru. Ukubwa wa TAIFA uzingatie pia kizazi kinachofuata baada ya uhuru kina vision gani,kuhusu hatima ya TAIFA hili.Chama chako kungangania maamuizi yenye fikra za miaka ya TG believe me Itakula kwenu,japo kwa msingi ambao Mwalimu aliujenga kwa chama hicho ilipaswa kiongoze kwa muda kwani kina mfumo imara [Stable] ukilinganisha na vyama vingine,ili litaonekana kwa waelevu [Intellectuals] tu kuliko raia wa kawaida au mtanzania wa kawaida kuweza kutambua.Lakini kubebana huku na madhambi mbalimbali yenye kukela umma wa Watanzania hakika itakua dhambi kwa chama chako daima.Jibuni majibu ya UMMA na kutumia watu wasafi na vijana wa kizazi kipya kama wewe, kuludisha imani ya chama chenu kwa Wananchi, na si kulusha mawe kwa adui huku wewe uko kwenye Nyumba ya vioo.
 
Wakati mwingine nasikitika sana kwa mambo yanayoendelea kuipa sura hii jf, inanisikitisha. Pamoja na yote yanayoendelea na kusemwa kote JF bado ni mahali ambapo ukipita utapata kitu, hutatoka bila kitu ndivyo nilivyozoea au tulivyozoea wengi wetu, lakini hali inayoendelea kwasasa inatutia uvivu wengi kuja hapa na si ajabu wako wengi ambao wameshakata tamaa ya kuja hapa kwasababu ndio forum inayoongoza kwasasa kwa habari za kutunga na kuzusha, hatuitendei haki jamii na wadau wakubwa wa forum hii.

Kila kukicha watu hapa wana tunga uongo na kuzusha kama vile ni kweli na wana hakika na wanayoyasema, si ndo maana kuna sehemu ya tetesi basi walau kama huna hakika?

Nimesoma thread ya vita dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na lile la ziara yangu kwenye vyombo vya habari. Nimejaribu kujibu lakini naona mara tu baada ya kuingia threda zile zinahamishwa mara hii huku ukirudi unakuta imeshapelekwa kwingine hivyo mtirirko wa hoja unakuwa tabu.... Hizi ni hoja mbili tofauti na ndo maana nimeamua kuanzisha nyingine maana mkanganyo unaozungushwa kule sijajua ni nini?

Lakini kwa kifupi, tumeandika barua kwenye vyombo vyote vya habari(news rooms) kuzitembelea wakiwemo mwananchi, na ratiba ilishapangwa kuwatembelea, na hata hao tanzania daima nitakwenda na ratiba ipo muda mrefu, sasa huu uzushi mara ooh nape kapeleka sijui taarifa gani kwenye kikao unatoka wapi? Swala hili hata kwenye kikao halijafika ni mpango wa kazi wa ndani ya idara, hichi si chama cha mfukoni hii taasisi kila idara ina mipango yake, sasa hicho kikao cha wapi?

But naamini watu wako kazini zaidi, lakini hata kama ni kazi ya propaganda huwa haifanywi hivyo, uongo wa wazi kabisa na kujaribu kupandikiza chuki'''''' hii imepitiliza.......

Tusiharibu hadhi ya forum hii kwa kuzusha maneno ya siyo na ukweli hata chembe..... Kweli ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huviwezi.......

Nape, ni lini umeanza tena kubehave kama Sophia Simba? - please resque the credibilities you had while in UVCCM. ndizo zilikufanya ukafika hapo... halafu, siku si karibu zimekwisha za wanamagamba kutoka CCM?- any action? reaction? any progress?
 
Bwana mdogo Nape Nnauye, Mimi nadhani hujui unachokifanya.

Kama kweli ungekuwa uko serious, kwa kuzingatia cheo chako, ungekuja hapa JF kwa kujenga hoja zenye mashiko, na hili ungeanza kutoka huko huko nje na katika mikutano yako. Unaheshimika kwa jinsi unavyoji-project kwa jamii. Kuna njia nzuri tu za kujenga hoja ukiwa CCM, lakini wengi hamzitumii hizo.

Mnakuja na maelezo fulani mepesi mepesi tu. Kwa cheo chako, ulitakiwa kuwa na washauri ambao ni wataalamu katika mambo kadhaa ikiwembo ujengaji wa hoja, syllogisms, speech, nk. Cheo chako ni kikubwa sana na ukiongea wengi wanakusikiliza na kuchambua unachosema. kwa hiyo kila sentensi inatakiwa kuwa imebeba tani kadhaa za ujumbe.

Inatakiwa unachosema hata mtu akikisoma miaka 50 baadaye, akiri kwamba kweli kuna kitu kilizungumzwa. sasa kwa jinsi unavyosema, unavyoandika (nilivyoona humu), kwa kweli nasikitika kukuarifu kwamba bado kazi unayo, na kama wewe ndio kweli katibu mwenezi wa CCM, basi kazi tunayo.

Kaa chini bwana mdogo na utafakari na ufanyie kazi ushauri huu. Wala hutakuwa na haja ya kuandika malalamiko kama hayo ulioandika
 
LAT-I always salute you,we are proud of you kamanda..You are the one made Chadema to be as it is to people.Keep it up for what you are doing in the parliament!!!

ha haaaaaa haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

mkuu naona umeamua kusoma kirefu cha id from right to left

some sort of bravery
 
Nape,

Wewe na Viongozi wenzako wa ccm msichopenda kusikia ni ukweli kwamba ccm imekwisha na itaendelea kwisha, yaani haina mvuto kwa wanachi wameichoka, huo ndio ukweli lazima mkubali sio enzi zile watu sasa wamefumbuka na hawawezi kuendelea kuishi katika lindi la umasikini huku nyinyi mkila nchi na kuwaimbisha ccm yajenga nchi, hiyo haipo kaka na uende ukapeleke ujumbe huko kwa wenzio, sisi ndio tupo kitaa na tunajua kinachoendelea uraiani ndugu.
 
Nape misukule yako uliyotuma kuja kuchafua hadhi ya JF imeshindwa kazi, sana sana imezidi kudhihirisha ukilaza wako.Hivi barua za kuwatimua magambani kina Lowasa,Rostam na Chenge zimeshaandaliwa? Siku zinazidi kukariabia.
 
nape ni nini hasa unataka kuwaambia wanaJF ni kwamba wanazusha au kulubuniwa au unataka huruma ya wana JF??
 
Mkeshaji-Dont you know who is LAT?
I replied to LAT as Iam interested with how replied to Nauye Jr

mkuu acha tujirushe na kupiga story humu kwenye hii thread hamna kitu humu

hewa imejaa kwenye hii mada
 
I totally agree with you Nape. Kuna uzushi, majungu na hoja nyingine za uwongo humu jamvini, hasa kwenye "jukwaa la siasa". However, there are credible people in this forum who almost always produce useful information. Also, other topics in this forums are quite useful to many of us. Try the Education topic, jobs, software and downloads, etc etc

In the present format of the forum where everybody sends in what they think it is worth sending out, and comes out "as it is", you can not avoid hayo majungu na uwongo. Najua MOD wanajitahidi sana ku-check the balance but it is almost an impossible task to filter all information coming in.

Remember, there is no editorial board that review the contents of threads before they come out, so to blame the forum is basically an indication that one do not understand the notion of free speech. You pick what is useful and leave what is useless to you, period.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom