Tanzania: Vyeti bandia, elimu za kununua na watumishi vihiyo

Kumbe Mheshimiwa waziri wa elimu pia naona alikasoma haka ka ujumbe. Ila mi huu uzi ninaupenda sana. Hapa hili likifanikiwa tutakuwa na strong institutions huko makazini
 
Baba Jessica kilaza mwendo kasi binti yake Jessica kilaza mwendo kasi. Ni hatari tupu!
 
Hili jipu mbona haliivi?? Waandishi wa Habari andikeni pia kuhusu hili. Ina maana huu uzi waziri wa elimu hauoni??? Ngoja niupandishe tena.

Tanzania tusingesonga mbele kama haya mambo ya short cut yasingeanza kuonekana.
It begins with you!
 
Dah!ningejua ningebaki Czech Rep!rafik YANGU alinishaur nibadil uraia nikakataa,watu wenye elimu feki ndio wako kwenye system wanakula bata,huku sisi watoto wa mama ntilie na elimu yetu tunapigwa vumbi kwenye ajira isio Rasmi huku ndo tunawalipia kodi vihiyo
 
Haka ka uzi huwa nakapenda sana. Ngoja nikasogeze ili Mheshimiwa awe anakaona ona kidogo.
 
Mheshimiwa Rais, nina sana na haka kauzi. Ni ka toka mwaka 2006, miaka kumi imeisha. Si kafanyiwe kazi kidogo.
 
Matokeo yake wameharibu elimu mara utasikia div 5, mara GPA, mara twisheni, mara msululu wa vitabu, wabunge kila kitu ni Ndiyooo.. Raisi asifanye utani aulize hspa jf kuna majibu yote.
 
Jamani wanajumuiya ya Wa-Tanzania tuishio British Virgin Islands tumeshutushwa na habari kuwa kuna baadhi ya viongozi wetu serikalini wana shahada za PhD kutoka kisiwani hapa. Ukweli hapa hakuna chuo kama hicho. Hiki kisiwa ni kidogo mno kuna wakazi wapatao 23,000. Kisiwa hiki kina secondary 2 na community collage moja.

Uchumi wa kisiwa hiki unategemea sana Utalihi na Financial services which includes offshore banking and registration of companies. Baada ya kutembelea web site ya Commonwealth Open University, Ni kweli nimegundua kuwa imekuwa registered hapa. Cha ajabu address yao ni ya hapa(box no.) lakini, Palm Chambers ambalo ni jengo halipo hapa. Kuonyesha kuwa ni fake, hawakutoa simu yao, ila wametoa fax number. Kutokana na fax number hizi number ni za USA (Florida).

Baadae nilikwenda kwa msajiri wa makampuni nilielezwa kuwa Commonwealth Open University imekuwa registered kama kampuni lakini haina Learning Institution yoyote. Baada ya kuuliza zaidi information hizo, niliambiwa nijaze form harafu nitapewa details baada ya kulipia $ 25.

Registry Of Corporate Affairs,
P.O . Box 418,
Road Town, Tortola, British Virgin Islands.
Fax 1 284 494 6331:
Simu 1 284 494 5491:
E-mail corporateregistry@bvifsc.vg Website www.bvifsc.vg

Sikuweza kulipia ili nipate maelezo hayo. Baada ya kujadiliana na wenzangu hapa tumejua kuna watu wajanja wachache wanatumia mwanya huu kuwaibia fedha watu na kuwapa degree baada ya kuwalipa pesa. Hicho chuo hakipo, hao jamaa ni matapeli.

Naomba serikali, Wizara ya Elimu, UTUMISHI mjue kuwa hakuna chuo kama hicho hapa. Kama kingekuwa ni chuo basi tungeweza kuona hizo ofisi zao hapa. Kuna Mtanzania mwenzetu ambaye amekaa hapa zaidi ya miaka kumi. Hajawahi kuona ofisi hiyo (Palm Chambers).

Tuko tayari kushirikiana na mtu yoyote ili kukomesha ununuaji wa yeti fake hasa kwa viongozi wetu.

Shukrani.

===========
Nov 10, 2014:

Watumishi 1,360 wakutwa na vyeti feki

UDANGANYIFU katika vyeti wakati wa kuomba ajira umeendelea kukithiri nchini, ambapo ndani ya mwaka mmoja tu, kuanzia Julai mwaka jana mpaka Juni mwaka huu, watumishi 1,360 wamekutwa na vyeti visivyo halali. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, alisema hayo jana mbele ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya baraza hilo.

Katika uhakiki huo, baadhi ya watumishi wakiwemo wa Serikali walikutwa wakitumia vyeti vya kughushi ambavyo imebadilishwa matokeo, wengine walikutwa na vyeti vya bandia huku wengine wakitumia vyeti vya watu wengine.

Hii si mara ya kwanza kwa Serikali kuelezea uozo huo katika elimu, ambapo Julai mwaka jana Msemaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Riziki Abraham, alitoa taarifa ikieleza kuwa Sekretarieti hiyo ilibaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti 677, kwa watumishi serikalini.

Aidha, Oktoba mwaka jana Ofisa Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Sekretarieti hiyo, Kasim Nyaki, alieleza kuwa vyeti vya Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi (Veta) ni miongoni vyeti vinavyoongoza kutumiwa katika udanganyifu kwa watu wanaoomba kazi kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Nyaki alisema kuwa kati ya watu 517 waliotumia vyeti vya Veta kuomba ajira kupitia sekretarieti hiyo, watu 304 walitoa vyeti halali, lakini watu 213 walighushi.

Mbali na hao, alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa kati ya watu 13,554 walioomba ajira katika miaka mitatu yaani 2010, 2011 na 2012, watu 816 walibainika kudanganya kwa kutumia vyeti vya taasisi mbalimbali za elimu, vyeti vya kuzaliwa na vinginevyo.
Kutokana na hali hiyo, Dk Msonde alisema Baraza hilo limeamua kushirikiana kwa karibu na mamlaka za ajira na udahili, ili kuhakikisha uhakiki wa vyeti vinavyotolewa na baraza hilo, unafanyika kabla ya mtahiniwa kuajiriwa au kudahiliwa.

Mbali na ushirikiano huo, Baraza hilo limeazimia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya kutumia udanganyifu katika vyeti.

Aidha, Baraza hilo pia limeanza kutoa vyeti vyenye picha ya mmiliki kuanzia 2008, ili kupunguza kasi ya udanganyifu huo.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeanza utaratibu wa kutoa vyeti mbadala kwa watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa waliohitimu kuanzia mwaka 2008 ambao vyeti vyao vilikuwa na picha.

Dk Msonde alisema hatua hiyo ya kutoa vyeti kwa waliopoteza, inatarajiwa kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa sababu mbalimbali kwa kupata vyeti mbadala, huku likiweka utaratibu madhubuti kuhakikisha fursa hiyo haitumiwi vibaya.

Akizungumzia kudhibiti wizi na udanganyifu katika mitihani, alisema Baraza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na kwa kiasi kikubwa na kudhibiti udanganyifu wakati wa ufanyaji mitihani.

Alisema Baraza hilo linakabiliwa na upungufu wa fedha za kuendesha mitihani ya taifa, ambao usipofanyiwa kazi, utaathiri uendeshaji wa mitihani ya kidato cha sita na ualimu.

Ukata huo alisema pia utaathiri uongezaji wa viwango vya posho za wasahihishaji kwa mitihani ya kidato cha nne, sita na mitihani ya ualimu kama ilivyokuwa imepangwa.

Alisema katika mwaka wa fedha 2014/15, kulikuwa na umuhimu wa kuongeza posho ya wasahihishaji kwa kuwa posho hiyo imekuwa ikilalamikiwa na washiriki kwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na posho zinazolipwa na mamlaka nyingine, ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa shughuli za mitihani.

Akizindua bodi hiyo, Waziri Kawambwa alisema wakati matokeo ya kidato cha nne mwaka huu yakianza kutolewa kwa mfumo mpya wa Wastani wa Pointi (GPA) ni vema kutoa elimu wakati huu kabla na baada ya mtihani, ili kuzuia mtafaruku.

Alisema utoaji wa elimu kwa wadau wote wa elimu, wanafunzi na wazazi utasaidia kudhibiti upotoshaji mara utekelezaji utakapoanza.

“Hili lifanywe kwa juhudi na umakini ili kuepusha upotoshaji unaoweza kufanywa na baadhi ya watu, elimu kuhusu mfumo mpya wa kutunuku matokeo itolewe kwa kutumia aina zote za mawasiliano na umma kabla, wakati na baada ya mitihani.

Bodi hiyo mpya inaongozwa na Mwenyekiti wake, Rwekaza Mukandala na wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Makenya Mabhoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Misani na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi, Mahmoud Mringo.

Wengine ni Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani la Zanzibar, Ameir Selemani Haji, Mkuu wa Skuli ya Ualimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Dk Maryam Jaffar Ismail, Mkurugenzi wa Idara ya Sekondari, Asia Iddi Issa, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Shaban Kamchacho, Mkuu wa Sekondari ya Kisimiri Meru, Emmanuel Kasongo na Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kimara Baruti, Rehema Ramole.


CHANZO: Habari Leo


Shukrani mkuu, wakati umefika kwa Tanzania kusafishwa. Wewe jiulize mtu hajasoma eti anapewa wizara nyeti serikalini aiongoze. Mtu kama huyu ataleta ufanisi gani katika wizara husika?
 
Mwanzilishi wa Kuuza vyeti na mitihani yuko hapa Dar ana Kijiji cha Maghorofa.
 
Mkandara ninakubaliana na wewe kuwa watalaam wengine pia wafuatiliwe!

Ila kusema wabunge ni kupoteza muda NA HELA ! hapo sikubaliani na wewe.

Hawa wabunge ndiyo wanaotunga sheria za nchi?

ndiyo wana kamati mbali mbali mfano mipango ya uchumi.

Na WAMO KATIKA kamati nyingi tu muhimu kwa nchi yetu tembelea website yao!!

wanatakiwa kuangalia mikataba ya nchi yetu nk!

wanapitisha bajeti ya kuendesha nchi!!!

Baada ya wao kufanya hayo maamuzi makubwa na mazito ya nchi NDIPO WATALAAM WENGINE WANAKUJA KUTEKELEZA!

KWA MTIZAMO WANGU MDOGO NINAKUPINGA! ILA INAONEKANA UMEINDIKA KWA UCHUNGU KIFALSAFA!
HAWA WANAOSOMEA PHD ZA KUNUNUA KWA MWAKA MOJA KWELI WATAMBULIKE DR? AU NI DEGREE ZA HESHIMA? PHD NI AT LEAST TWO YEARS FULL TIME NA MWENYE EXPERIENCE!
 
wageni wanaofanya kazi nchini ni vyema wakakaguliwa vyeti vyao na welesi wao katika kazi. Naona udhaifu mkubwa wa serikali yetu kufanya work permit kama chanzoncha mapato nchini Matokeo yake wanaingiza vihiyo wanaosababisha RAIA kukosa ajira. Naomba suala la vyeti liende had I kwenye taasisi binafsi na NGOs maana huko ndiko wamejaa makanjanja wa elimu duniani.
 
Watanzania wenzangu,hivi mpaka sasa hamuoni kuwa kuna umuhimu wa PhD za watu kuhakikiwa?

Naomba mawazo yenu katika hili.
 
Back
Top Bottom