Tanzania: Vyeti bandia, elimu za kununua na watumishi vihiyo

IMG_20161109_165102_080.jpg
IMG_20161109_114328_627.JPG
 
Watanzania wenzangu,hivi mpaka sasa hamuoni kuwa kuna umuhimu wa PhD za watu kuhakikiwa?

Naomba mawazo yenu katika hili.
PhD hutolewa na mamlaka inayotambulika. Ni TCU tu wenye mamlaka ya kuhakiki degrees. Kama mtu umesoma nje ya nchi ( mfano mi nimesoma masters, na PhD nje ya nchi) napaswa kusubmit vyeti vyangu vihakikiwe TCU ili kuona kama vyuo vilivyo nipa hizo elimu zinatambulika ili kujenga uhalali wa degree zangu
 
PhD hutolewa na mamlaka inayotambulika. Ni TCU tu wenye mamlaka ya kuhakiki degrees. Kama mtu umesoma nje ya nchi ( mfano mi nimesoma masters, na PhD nje ya nchi) napaswa kusubmit vyeti vyangu vihakikiwe TCU ili kuona kama vyuo vilivyo nipa hizo elimu zinatambulika ili kujenga uhalali wa degree zangu
Hujanisaidia chochote hapa maana hujajibu hoja.
 
Watanzania wenzangu,hivi mpaka sasa hamuoni kuwa kuna umuhimu wa PhD za watu kuhakikiwa?

Naomba mawazo yenu katika hili.
Tuoneshe kwanza cheti chako na cha mbowe vya form four
Ni Tanzania tu,utapata mtu hakufika hata kidato cha nne,anahoji uhalali wa elimu ya Phd holder-Harrison Mwakyembe.
 
Ama kweli nchi maskini maskini tu....

Tunapoteza muda na fedha za walipa kodi ati kutafuta WABUNGE wanaogushi vyeti?..Hivi Mbunge anatakiwa kuwa na cheti gani?... badala ya kuweka nguvu hiyo ktk kuwaangalia wataalam wetu ktk taasisi mbalimbali (hasa walimu) tumeweka kwa wabunge ambao huchaguliwa kwa kura za wananchi na sio vyeti vyao..... what a crap!

Ikiwa kuna mtu kati yenu ataweza kunipa list ya vyuo vyote vinavyotambulika Tanzania na sio list ya Mareakani ama Uingereza naweza kusikiliza. Hata hivyo kisheria list hiyo haimkatazi mtu kutundika cheti chake ukutani ama kutangulia jina lake. Hakuna kati yenu anayeweza kusema EN hakusoma kabisa kupitia internet na kupata shahada hiyo wala hakuna mtu anayeweza kusema NI lazima usome miaka mitano kupata shahada fulani.
KUGUSHI cheti ni kununua cheti bila mhusika kupata elimu ya cheti husika. Mengine yote hayahusiani na mtu yeyote isipokuwa mwajiri wa mtu huyo.....Mbunge hakuajiriwa na Sitta.

Dhumuni kubwa la kutambulika ama kutotambulika kwa cheti ni ktk kuweka utaratibu wa elimu unaokubalika nchini humo ktk kufungua biashara, ajira na wakati mwingine kuendelea kimasomo. Kila shule, tajiri na hadi nchi zina mapendekezo yake na hayafanani kabisa.

Prof. Sarungi pamoja na vyeti vyake hawezi kufanya kazi Marekani ama Canada kama daktari, kwa sababu vyeti vyake havitambuliki. Hii haina maana Prof. Sarungi kagushi vyeti, pia Hukohuko marekani ama canada hawana sheria ya kumtakataza Sarungi kutotanguliza Prof. mbele ya jina lake ktk hati ama sahihi anazoweka nchini Marekani. na magazeti yote yatampa cheo chake cha U professor ingawa haruhusiwi kufanya kazi kama Daktari nchini humo.

Huyu huyu Dr. sarungi anaweza kabisa kukubalika nchi nyingine na vyeti hivyo hivyo kwa kupata kazi ama kufungua biashara.

Ikiwa swala ni muda wa kuhitimu masomo, hili ni tatizo letu sisi, halihusiani kabisa na nafasi ya ubunge.

Tumeletewa wataalam kibao toka nje ambao ni feki, kazi zote kubwa zinafaywa na vijana wetu wanaolipwa robo ya misharaha ya wataalam hawa - hatusemi kitu. Wakenya na waganda kibao wana vyeti feki sehemu za uzalishaji hatusemi kitu, madawa toka india yote feki hatusemi kitu, chakula kinachoagizwa toka nje feki hatusemi kitu - ila tumekisia Mbunge fulani ana cheti feki (pale panapotukuna) basi nchi nzima imekuwa deal hali watu ndio wanazidi kufa kwa njaa umaskini na kila adha.
JPM alifanyia kazi mjadala huu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom