Tanzania: Vyeti bandia, elimu za kununua na watumishi vihiyo

Jina moja
Ubin mmoja
Mwaka aliomaliza shule na shule ni moja. Utashangaaa cheti kimoja wafanyakaz wawil
Huyu afisa kilimo yule mwanasheria. Hili ni jipu WATUMBUAJI NJOOO INBOX NIWASONTESHEEEE
Mkuu ikitokea Magufuli ajitoe Mhanga awalete F.B.I waje wachunguze vyeti na Digrii za wale wanaojiita Wasomi Tanzania hakika Dunia utashuhudia vioja vya karne maana 90%! Hawana Taaluma vichwani ni Wasomi feki wanafanya kazi Kwa mazoea kijanja janja.
 
Mh Rais,Magufuli,hii hoja ni nzito.

Hili ni jipu baab kubwa.

Hapa ndipo taasisi nyingi za uma zinapoathirika utendaji kazi kutokana na kujaa watu ambao kiuhalisia hawako competent kwa nafasi walizo nazo.
Nchi inakosa nguvu kazi sahihi kutokana na wataalam magumashi kuenea kila pahala,matokeo yake ni ubabaishaji everywhere wabunge,lawyers,mainjinia,madaktari,mafundi,eeeverywhere ni rushwa na ubabaishaji tuu!
Kabla hujawasha gari yako kwa safari,hakikisha tairi zako ni bora.
Mheshimiwa,tumbua hili jipu.
Ni baba wa majipu.
Mkuu haya Majipu ni makubwa yanahitaji madaktari Bingwa tena Hosptal za rufaa , Magufuli akitaka apate Ukweli na Haki lazima awaazime wachunguzi wa uhalifu wa kimataifa toka huzo Ulaya, Marekani nk , lakini akiwapa kazi wachunguzi wa ndani watakula Rushwa na kuchakachua kila kitu .
 
Hii hatari kubwa sana kwa ustawi wa taifa la watu ambao elimu ndo nyenzo kuu na kipimo cha maendeleo ktk nchi zinazoendelea. Elimu, elimu, elimu.
 
Swala hili ni nyeti na lilishazungumziwa sana huko nyuma hapa JF, lakini mamlaka husika hazikuchukua hatua zozote stahiki kwa kuwa inawezekana kwa njia moja au nyingine wanahusika na uozo huu.

Tatizo hili ni kubwa,na inawezekana kukawa na uhusiano mkubwa na utendaji mbovu uliopo katika vyombo vingi vya uma.Itakuwa busara kama vyeti vyote vitahakikiwa upya ili kujiridhisha kwamba tuna watu mahiri na wanaostahili katika sehemu zote za utendaji wa uma.
kila shetwan na mbuyu wake
 
Hili Jipu ni hatari, ila kama tunataka refrom Tanzania then hamna namna, hili la Vyeti feki + kuwa na vyeti halali lakini kichwani hamna kitu yapasa litumbuliwe ASAP
 
Kama wanaokwiba ni wale wenye vyeti FEKI una maana waliovuta EPA, waliopiga ESCROW, waliotakatisha MABEHEWA feki, waliotoa bandarini MAKONTENA 349 wote wana vyeti FEKI ?? Aliyehitimu chuo kikuu kwa kununua mitihani, kwa ku-copy na ku-paste research papers cheti chake siyo FEKI? Ndiyo maana wawekezaji wanapo ajili wanaangalia uelewa (IQ) wa mtu, hii ni ushahidi kwamba majority ya madegree ya bongo ni FEKI. Hata scholarship ni lazima kwanza wasome, wafanye mtihani wakifaulu ndiyo waendelee na masomo. Sometimes hapa bongo hakuna tofauti kati ya vyeti FEKI na vyeti HALISI
Well said
 
Kwa serikali ya awamu ya 4 hili lilikuwa ni kama 'UGALI wa ZEGE'...unaulaje na kwa mboga gani. Kama naibu waziri tu wa wakati huo alikuwa FEKI na VYETI FEKI....angewezaje kujikamua jipu lake mwenyewe?? Hata sasa, tumeambiwa 'TUHACHANE NA MAKABURI YA ZAMANI'! Ukigusa hili, kwa mfano sehemu kubwa ya watumishi wa idara zinazohusiana na usalama watatumbuliwa...JPM analiweza hili??
 
Miye naogopa kumwelekeza walipojaa wenye vyeti fake. Labda akianza hii kazi nitamtajia mmojammoja na mahali walipo. Ila kwa sasa naitunza hii siri.
 
Muda ukifika watajulikana tu mkuu. Tuvute subira. Ila mi huyu waziri wa elimu naona labda analivutia kasi.
 
Kumbe hata akina mahanga, Mary nagu, chegeni doctorate zao hazitambuliki kulingana na uzi huu.
 
Nakumbuka kuna mawaziri walituhumiwa kuwa na vyeti feki mfano anaejiita dr. Mary nagu tena bungeni na vyama vya upinzani jambo la kushangaza hawakuwai kukanusha popote, wapo akina sumaye, yusuph makamba, lyatonga mrema nk
 
Vyeti bandia ni kila mahali. Juzi tu kulikuwa na Katibu mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) alikuwa na PhD feki. Huko chuo cha Ufundi arusha inadaiwa Mkuu wa Chuo Bwana Richard Masika ana cheti feki cha PhD. Masika bado hajashitukiwa kwa hiyo anaendelea na shughuli zake kama kawaida. Inasemekana Daktari Masika alipata PhD yake huko Hungary miaka ya 1993, lakini mpaka leo hajawahi kuandika chochote kama njia ya kufanya elimu yake iwe hai.

Ilitisha zaidi pale Dakitari Masika aliposema hadharani, kuwa hajui Research inafanywaje na hafahamu Thesis ni nini.

Wafanyakazi wa chuo hicho wanasema chuo chao ni nyumbani kwa vyeti feki. Wakataja watu wenye vyeti feki akiwemo na Mkuu wa chuo. Hii ni hali ya hatari sana!
 
Hili jipu mbona haliivi?? Waandishi wa Habari andikeni pia kuhusu hili. Ina maana huu uzi waziri wa elimu hauoni??? Ngoja niupandishe tena.
 
Huu uzi upo toka 2006, mbona hufanyiwi kazi??? Au walengwa ni wengi ndo maana hushughulikiwi.
 
Back
Top Bottom