Polisi wanasa katibu wa CUF na mtumishi wa halmashauri Kibiti wakitengeneza vyeti feki

Jun 4, 2022
68
184
Jeshi la Polisi wilaya ya Kibiti limemkamata Rashid Mkinga (36) kwa tuhuma za kutengeneza Vyeti feki vya kuzaliwa. Tukio hilo lililotokea Januari 15, 2024 majira ya saa 1 usiku katika Kitongoji cha Kibiti B, Kata na Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Katika mahojiano ya awali yaliyofanywa na Jeshi la Polisi, Mkinga amekiri kuhusika na vitendo hivyo kwa kushirikiana na Dkt. Abdul Salim Msemo (53) mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Idara ya Afya ambaye pia amekamatwa na Vyombo vya Dola.

Watuhumiwa hao wamekutwa na Kompyuta tatu (03) zilizokuwa na nakala za Vyeti vya Kuzaliwa na Taaluma za watu mbalimbali, Bima za Afya 15 zenye taarifa zinazotofautiana, Vyeti vya Ndoa na Vyeti vya Kuzaliwa.

Mkinga anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Ikwiriri kilichopo Rufiji na muda wowote yeye na mwenzake watafikishwa Mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
Picsart_24-01-17_14-29-50-218.jpg
 
• Siyo hayo tu, yapo mengi tu,

• Hapo inaonekana wamechomana wenyewe kwa wenyewe.
 
Jeshi la Polisi wilaya ya Kibiti limemkamata Rashid Mkinga (36) kwa tuhuma za kutengeneza Vyeti feki vya kuzaliwa. Tukio hilo lililotokea Januari 15, 2024 majira ya saa 1 usiku katika Kitongoji cha Kibiti B, Kata na Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Katika mahojiano ya awali yaliyofanywa na Jeshi la Polisi, Mkinga amekiri kuhusika na vitendo hivyo kwa kushirikiana na Dkt. Abdul Salim Msemo (53) mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Idara ya Afya ambaye pia amekamatwa na Vyombo vya Dola.

Watuhumiwa hao wamekutwa na Kompyuta tatu (03) zilizokuwa na nakala za Vyeti vya Kuzaliwa na Taaluma za watu mbalimbali, Bima za Afya 15 zenye taarifa zinazotofautiana, Vyeti vya Ndoa na Vyeti vya Kuzaliwa.

Mkinga anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Ikwiriri kilichopo Rufiji na muda wowote yeye na mwenzake watafikishwa Mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
View attachment 2874455
Why CUF, huyo mtumishi wa halamshauri mbona hamsemi ni CCM?

Mwanachama wa CCM anayefanya kazi Kibiti na Mwana CUF anayefanya kazi ya stationary wakutwa wakirudufu vyeti bandia.
 
Dah! Mimi namuonea tu huruma huyo Daktari! Kwa umri wake huo wa miaka 53, maana yake amebakiza miaka 2 tu ili astaafu kwa hiyari, na miaka 7 pekee ili astafu kwa mujibu wa sheria!!

Ila mwisho wa siku ndiyo hivyo tena! Hela imekuwa kwake haitoshi kwa chochote!! Dili za dawa zimejaa kibao! Achilia mbali viposho na visemina vya hapa na pale.
 
Watu tunawashauri kila siku waibe mali za umma wawe salama, angalia akina Bashe, Aweso, Mwigulu, JK, Rostam, Makamba n.k wapo salama kabisa hakuna usumbufu na polisi wala paka yoyote
 
Dah! Mimi namuonea tu huruma huyo Daktari! Kwa umri wake huo wa miaka 53, maana yake amebakiza miaka 2 tu ili astaafu kwa hiyari, na miaka 7 pekee ili astafu kwa mujibu wa sheria!!

Ila mwisho wa siku ndiyo hivyo tena! Hela imekuwa kwake haitoshi kwa chochote!! Dili za dawa zimejaa kibao! Achilia mbali viposho na visemina vya hapa na pale.
Ngoma ipo kwenye kuprove kuwa ameshiriki hizi ni tuhuma peke ake atachomoa vizuri sn.
 
Kukikuwa na haja ya chama kutajwa
Ndo walivyo, bado hawajaamini Kama chama hicho kimekufa,wanakiogopa Sana,mwaka 2000 jamaa mmoja alimchoma na pasi kijana kuwadi aliyekua akitumwa na wakware kwa mkewe,mwenye mke alikua katibu wa cuf wilaya, gazeti la majira likaruka na habari ya 'katibu wa cuf...'
 
Back
Top Bottom