Tanzania: Vyeti bandia, elimu za kununua na watumishi vihiyo

DrWHO

Naona swali lako la vyuo vikuu feki hapa UK limepata jibu. kutoka ile thread nyingine.
 
Jamani someni vichwa/utangulizi wa habari kabla ya kuuliza maswali.

Hii list imetolewa na Council on Higher Education Accreditation.

Kwa kuongezea tu, ukienda pale MSTHE utakuta copy, ukienda Utumishi Serikalini utakuta pia, na hata Tume ya Uchaguzi.

IFM ndiyo tu wameamua kuiweka Online ili kila mtu ajionee na macho yake. Wengine wote wameamua kufungia makabatini.
 
kudos to Aljazeera,

thanks, nadhani akina Nungwi, "umeme ulikuwa umewakatikia list hiyo ilipotolewa" kama ile story ya mchaga anadaiwa pesa ktk simu akajibu "sikusikii mvua kubwa inanyesha........... lakini helloo aliisikia!!"

Sasa, ukijumuisha ushahidi wa Bob Mkandara aliyepiga simu sehemu husika na kuambiwa hawatoi PhD na hii list aliyotuwekea Mzee Aljazeera,

Please wafuatao hebu, ondoeni hizo "Dr" mbele ya majina yenu (acheni ubishi wa kitoto), si vibaya kukiri kuwa umekosa,

1.Nchimbi
2.Nagu
3.Kamala
4.Warioba
5.Masaburi na kuendelea

Tunaomba pia Bunge litoe tamko rasmi kuondoa heshima wanayopewa hawa watu ya u "Dr" ........please hii inashusha SANA HADHI YA BUNGE
 
Jamani someni vichwa/utangulizi wa habari kabla ya kuuliza maswali.

Hii list imetolewa na Council on Higher Education Accreditation.

Kwa kuongezea tu, ukienda pale MSTHE utakuta copy, ukienda Utumishi Serikalini utakuta pia, na hata Tume ya Uchaguzi.

IFM ndiyo tu wameamua kuiweka Online ili kila mtu ajionee na macho yake. Wengine wote wameamua kufungia makabatini.

Sasa basi wabunge na viongozi wengine wa serikali waanze kuonyesha mfano mzuri kwa kuonyesha kuwa digrii zao zote ni za halali kwa kupeleka vyeti vyao vikahakikiwe na taasisi husika. Wale wenye digrii uchwala vile vile wawaombe wananchi misamaha kwa kuwa waliwarubuni kupata kura kwa kutumia digrii hizo za bandia.
 
kudos to Aljazeera,

thanks, nadhani akina Nungwi, "umeme ulikuwa umewakatikia list hiyo ilipotolewa" kama ile story ya mchaga anadaiwa pesa ktk simu akajibu "sikusikii mvua kubwa inanyesha........... lakini helloo aliisikia!!"

Sasa, ukijumuisha ushahidi wa Bob Mkandara aliyepiga simu sehemu husika na kuambiwa hawatoi PhD na hii list aliyotuwekea Mzee Aljazeera,

Please wafuatao hebu, ondoeni hizo "Dr" mbele ya majina yenu (acheni ubishi wa kitoto), si vibaya kukiri,

1.Nchimbi
2.Nagu
3.Kamala
4.Warioba
5.Masaburi na kuendelea

Tunaomba pia Bunge litoe tamko rasmi kuondoa heshima wanayopewa hawa watu ya u "Dr" ........please hii inashusha SANA HADHI YA BUNGE


Wewe unawafahamu wenye "PihechiDi" tu, wapo wenye masters na bachelors kibao ikiwa ni pamoja na akina Anthony Dialo, Augustine Mrema, Makongoro Mahanga (DR), George Nangale (DR), David Mathayo David (DR) na waalimu kadhaa wa Mzumbe.
 
Mzee MKJJ na wewe umesoma vyuo vya uchochoroni mbona umestuka sana

elimu yangu miye ya kidato cha sita tu... baada ya kugundua kuwa Chuo hakimfanyi mtu kuwa muadilifu na anayelipenda taifa lake I gave up!! I decided to join the rank of Bill Gates and the likes ambao kwao Chuo is the greatest BS ever invented!
 
elimu yangu miye ya kidato cha sita tu... baada ya kugundua kuwa Chuo hakimfanyi mtu kuwa muadilifu na anayelipenda taifa lake I gave up!! I decided to join the rank of Bill Gates and the likes ambao kwao Chuo is the greatest BS ever invented!
Aisee wewe umetukana matusi ya nguoni wote waliokwenda chuoni. Inawezekana kabisa hukuwa na maana hiyo ila kwa kuandika hivyo umevuka mpaka kabisa. Umefanya kama vile wote waliokwenda chuoni siyo waadilifu na hawalipendi taifa, ikiwa ni pamoja na Mwalimu Nyerere (rip). Vile vile unaainisha kuwa wale wote wanaofanya chuoni ni BS!!. Labda nimekuelewa tofauti.

Ninavyoelewa ni kuwa Bill Gates hasemi chuo ni BS na ndiyo maana anatoa hela nyingi kusaidia elimu; kazi zote za maana pale Microsoft anazitoa kwa waliokwenda chuo tu. Vile vile Bill Gates huyo huyo ameshasema mara nyingi tu kuwa kuacha kwake chuo kulitokana na yeye kupenda sana computer programming ambayo wakati huo ilikuwa haifundishwi. Anaamini kuwa angeendelea na shule huenda angeweza kufanya mambo makubwa zaidi ingawa sasa hivi hawezi kurudisha time nyuma.
 
Vyeti vya mawaziri 13 vyachunguzwa

Shahada za udaktari wa falsafa za mawaziri 13 na wabunge kadhaa sasa zimeingia kwenye utata baada ya kugundulika kuwa walitunukiwa bila kuwa na sifa za kitaaluma.

Habari ambazo RAI imezipata zinasema kuwa shahada hizo zimebainika kuwa na utata baada ya uchunguzi wa kitaalam uliofanywa kwa kuwasiliana na vyuo kadhaa duniani, ambavyo ndivyo vilivyotunuku shahada hizo.

Kwa mujibu wa habari hizo, wahusika bado hawajaelezwa kutokana na umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi kwa watu wengine wakiwamo wabunge.

Uchunguzi wa awali unazihusu zaidi shahada za udaktari wa falsafa na baadaye zitafuata shahada nyingine zilizopatikana katika mazingira ya kutatanisha.

Habari ambazo RAI imezipata zinasema kuwa kazi hiyo inafanywa na watu maalum chini ya maelekezo ya wizara ya sayansi teknolojia na elimu ya juu.

Kwa mujibu wa habari hizo, mawasiliano yanafanywa baina ya maofisa wa hapa nchini na vyuo ambavyo viliwatunukia wahusika shahada hizo za udaktari wa falsafa, na tayari taarifa muhimu zimekusanywa ili kubaini kama ni halali au batili.

RAI ilidokezwa hivi karibuni kwamba mawasiliano ya awali yaliyopatikana hadi mwishoni mwa Novemba mwaka jana tayari yamebaini kuna mawaziri na wabunge kadhaa wenye shahada ambazo zina utata au za kununua.

Hata hivyo, bado wahusika ambao shahada zao hizo zimegunduliwa kuwa na utata hawajataarifiwa kwa kuwa zoezi hilo bado liko katika hatua za mwanzo tu.

RAI imedokezwa kwamba baadhi ya wahusika wamekuwa wakijipatia shahada hizo kwa muda mfupi sana tofauti na muda unaotakiwa kufuzu shahada,wengi wao wakituhumiwa kununua shahada hizo kutoka nje ya nchi.

Taarifa zinasema kwamba hatua ya kuzichunguza shahada hizo imeanza na shahada za udaktari wa falsafa na baadaye zitafuata shahada za uzamili.

Mpango wa kufuatilia shahada za watu mbali mbali hapa nchini ulitangazwa na waziri wa sayansi,teknolojia na elimu ya juu,Professor Peter Msolla, kufuatia malalamiko yaliyoanza kutolewa na watu mbali mbali hapa nchini.

Wapo walionung'unika kwamba kuna watu ambao wamejipatia shahada mbali mbali,kwa njia ya kuzinunua lakini hawana uwezo wa kitaaluma kulingana na shahada walizonazo.

Chanzo: GAZETI LA RAI
 
Nungwi,

Naona na hawa RAI wanaleta za UDSM hawa, Upo wapi? zama zile ilikuwa shida ni umeme, sasa hivi je, come out to defend "Dr" Warioba et al........as the storm is just around the corner!!
 
Professor Msolla na bodi yako tafadhali fanya kweli.Isiwe nguvu ya soda au mazingaombwe ya kwenye media portals. Anza na mawaziri na wabunge, then njoo kwenye academia,then kwenye hospital na research centres,makampuni and finally the general public.Ni zoezi gumu na lazima litakujengea maadui but you can't get a better opportunity to serve your country and you shall be remembered for that. The public is behind you!
 
Mimi sina matumaini na outcome ya jambo hili na sina imani na Msolwa kama anaweza kufanya kweli na hasa kwa Mawaziri ambao ni wana mtandao na wako karibu Muungana. Hizi ni danganya toto na sitegemei chochote kabisa
 
Hapa mimi namuunga mkono Prof. Msola kwani ni hatua nzuri tu aliyofikia, maana mwanzo aliahidi kufuatilia hilo, tukaona kimyaa tukaanza kulalamika, lakini ameonesha kuwa kile kimya kilikuwa na maana yake. Hivyo siyo kila mara tuwe watu wa kutoa critism tu, pamoja na mabaya wanayofanya lakini wakifanya mazuri tuwapongezeni jamani. Na kwa nini tukose matumaini ya outcome yake wakati ndiyo kwanza swala linaanza. Tuweke imani na tusubiri. Ikifika wakati hatusikii result then tunaweza kuhoji imekuwaje. Lakini kwa sasa mawazo yangu tumsaidie huyo Msola na watu wake kumtajia Mawaziri wote na Wabunge wote wanaohusika na vyeti , degree bandia. Tukiwapa orodha itasaidia Taifa kwa ujumla.
 
Hakuna kitu....wanajaribu ku divert attention toka kwenye issue ya radar!!!!!!!!You watch.
 
Mama Lu
Nakubaliana nawe kabisa . Unaona kwenye Richmond nako walileta shake up ya mawaziri watu kimya na sasa radar wameona hili lakini we are vigilant
 
Hata mimi naona hapa hakutakuwa na la maana. Nimesikia huko Mzumbe na kwenye vyuo vingine wahusika wameanza kuitwa na kuambiwa wahalalishe vyeti vyao. Suala litafichwa na kushughulikiwa kimya kimya wakati ili kutoa fundisho ilitakiwa hitimisho la hili jambo liwe wazi.
 
Ogah.

Hajatajwa DR.Warioba kwenye hii makala ya rai.
na inawezekana mwandishi ni Fikiraduni au DR.assad wameona hakuna anayewasiliza.

walitajwa ni mawaziri si staff wa Mzumbe university.
msolla hawezi kuguza Mzumbe hata kidogo.
 
Back
Top Bottom