Tanzania: Nini tatizo letu kama Taifa? Tunajikwamuaje?

Mkuu,
Napinga hoja yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Una point nzuri Ila ulipoiharibu ni hapo kwenye Hiyo kauli ya kichochezi ya umwagaji Damu. Kwanza Watanzania tumezoea kuishi kwa umoja na kushirikiana katika jamii zinazotuzunguka. WanaSiasa ndio wameleta haya matatizo yote ya chuki za Kidini, Kiukanda, Kikabila, Kiitikadi, Kijinsia n.k.

Naomba nikukumbushe tu kwamba Tanzannia ni Nchi ambayo Ina SHERIA na KANUNI. Watanzania tulio wengi tulizoea kuishi na kufanya shughuli zetu kiujanja ujanja bila kufuata taratibu za nchi.
Umekuja utawala wa awamu ya 5 ambao unarudisha mfumo wa kufuata Sheria na taratibu za nchi, matokeo yake tunaona watu wasio waadilifu na weledi kutwa kukicha wanaiponda na kuikebehi SERIKALI kwa manufaa Yao binafsi na sio kwa manufaa ya TAIFA.

Wewe Kama ni Mtanzania MZALENDO nafikiri utatafakari upya hiyo kauli yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Kila la heri.
Mbn huelezi unapinga kwa point ipi sheria tulizo nazo zinaruhusu kunyima haki vyama vingine au una maanisha serikali niya chama kimoja tu.

Serikali wameiponda kwa vipi na wewe unae sifia tu hata cuf kunyimwa haki ni sawa. Wewe kwa taarifa yako HAKI HUINUA TAIFA kwa mawazo yako watu wote ni wanachama wa ccm. Kwa hiyo ni sawa wengine kunyinwa haki zao.

Nini maana ya kuwa na vyama vingine kama haki ni ccm kutawala pekee yake. Watu wakiamua kudai haki za kisiasa kw kuingia barabarani sheria hizo unazozisema zitazuia. Nani mchochezi kati ya wewe na anaye tahadharisha ushabiki mwingine hauna maana hautapona usifikirie eti kwa kuwa mnaoshabikia ccm mtakuwa salama, wote yakiingia machafuko wote tunakuwa matatizoni saidia kuwaambia ccm wanachochea na kukaribisha uvunjifu wa amani.

Kuzuia kitu kama hicho kisitokee sikuzuia kwa kuwanyamazisha watu kwa mabunduki ni kutenda haki kwa vitendo. Kufanyia kwa vitendo usawa unao usema.
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni
1- Elimu mbovu na wasomi wasiojiweza
2- Siasa mbovu na viongozi wasiojiweza
3- Katiba ,, ,, na watendaji wasiojiweza
4- Sera mbovu na mipango tusiyoiweza
 
Kwa kifupi kabisa, TATIZO LETU KUBWA NI KUKOSA MKAKATI SAHIHI WA KISIASA.

Hatujawahi kupata uongozi makini uliodhamiria kujenga utaifa wa dhati (nation building) wa Tanzania. Kama Mwalimu JKN alivyosema pale Mbeya Stadium kabla ya ukoloni halikuwepo taifa la Tanganyika (wala Tanzania). Uhuru ulipowasili ulikabidhiwa kwa kundi la watu waliokuwa na dhana za kila aina (kuanzia utaifa kwa JKN, ukabila, udini, ubinafsi n.k. kwa wengine). Kama kawaida ya Waafrika "waliopigania uhuru", wengi walitaka kujipatia "utambulisho na manufaa maalum" kwao na kwa makundi yao. Mwalimu alitaka kujenga taifa la Tanzania lakini alishughulika zaidi kibinafsi na kidikteta kiasi kwamba hakujenga timu kubwa na imara inayojitegemea yenye maono (visheni) ya ujenzi wa taifa imara la Tanzania. Aidha, alikazania zaidi kurundika kila kitu kwenye mfumo wa chama kimoja ambacho alikuwa na udhibiti binafsi wa asilimia 100.

Athari yake kubwa ni kujenga kada kubwa ya wanafiki wenye kujikomba badala ya kufanya kazi makini ya uimarishaji wa utaifa na uzalendo. Hata mifumo ya kuhakikisha umakini katika kusimamia rasilimali, maadili na tunu za taifa haikuwekwa. Kila kitu kiliachwa kutegemea rehema ya rais aliyepo madarakani.

Tanzania imekuwa na wasomi wengi na bora tu. Wengi tuliopata bahati ya kusoma angalau hadi sekondari enzi za mwalimu, tulipitia mfumo bora sana wa elimu. Tanzania ina neema kubwa sana ya rasilimali na utajiri mwingi tu wa asili. Tanzania ina watu wengi wasio wakorofi, wasioshikilia misimamo mikali ya kikabila wala kidini; ni wavumilivu sana na, hivyo, tumeepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tumekuwa nchi imara (stable) kwa upande huo. LAKINI uongozi wetu umegubikwa na ubinafsi uliopitiliza kiasi kwamba umediriki kusaini mikataba ya kifisadi na wageni inayohujumu "taifa" isivyoelezeka. Nchi nyingi zina "red lines" ambazo ukitaka kuiba huzivuki, lakini sio Tanzania. Hii ni kwa sababu kitu kinachoitwa taifa hakithaminiwi kabisa bali maslahi binafsi.

Halafu tumejenga mwenendo wa ulaghai mkubwa sana tukitumia kauli za "amani', "utulivu", "upendo", "uzalendo" na "mshikamano" wa kipekee wa watanzania huku wananchi wakinyanyaswa vilivyo na kutakiwa kuwa kimya muda wote ili "wasiharibu sifa nzuri" ya Tanzania. Hatua anazochukua rais wa sasa, JPM, na jinsi zinavyoshangiliwa (pamoja na mishkeli yake) zinadhihirisha kiwango cha unafiki ambao hili "taifa" limeulea na kuuvumilia tangu uhuru.

KINACHOHITAJIKA SASA NI "JIBU SAHIHI LA KISIASA". RAIS MAGUFULI AMEANZA VIZURI KWA KUUTIKISA (SHOCK) MFUMO WA UNAFIKI NA UFISADI TULIOISHI NAO TANGU UHURU. NA MATOKEO YAKE YAMEDHIHIRISHA UOZO TULIOKUWA NAO MIAKA YOTE HIYO. HAKUNA UBISHI.

HATARI INAYOELEKEA KUJITOKEZA SASA NI KWA HUYU RAIS KUFANYA MAKOSA YALIYOFANYWA NA MWALIMU JKN YALIYOTUACHIA TAIFA LISILO ENDELEVU; LILILOBAKIA KUWA PEPO YA WANAFIKI NA MAFISADI WASIO NA HAYA WALA MIPAKA: WAKITUMIA MWAMVULI WA SIASA KUFANYA HUJUMA ZA KILA AINA KUJINUFAISHA BILA KUJALI WANALIWEKA TAIFA KWENYE MUSTAKABALI UPI.

TUKO KATIKA KIPINDI NYETI (CRITICAL). WALE WALIO KARIBU NA KWENYE NAFASI ZA USHAURI, WAJITAHIDI KUMSAIDIA RAIS AHAKIKISHE ANAPOENDELEA KUI-SHOCK SYSTEM BASI KAZI YA KUIMARISHA MIFUMO SAHIHI NA ENDELEVU YA UTENDAJI NA USIMAMIZI IWEKWE.

NA RAIS NAYE
ATILIE MAANANI SANA UMUHIMU WA KAZI YA KUJENGA MIFUMO IMARA, ENDELEVU YA KITAIFA. KWA KADIRI WANANCHI WATAKAPOONA MISINGI YA KUJENGA TAIFA IKIIMARISHWA, HAKI KUTENDEKA, WAOVU KUADHIBIWA NA WEMA KUZAWADIWA BILA UPENDELEO, BILA SHAKA WENGI WENYE NIA WATAIMARISHA UZALENDO NA KUREJESHA HAMU YA KUJENGA TAIFA WAKIJUA KUWA TAIFA LITAKUWA AMINIFU KWA AJILI YAO NA VIZAZI VYAO. SIO SASA HATA WAKITAKA KULIPA KODI WANAKUWA NA SHAKA KUWA ITAENDA KUWANUFAISHA WAJANJA WACHACHE.

HALAFU KAULI ZA UZALENDO ZINATOLEWA KINAFIKI TU.
 
Kila kiongozi/ utawala unakuja na style yake hatuna specific national standards za kufuata
Lililokua jema kisheria uongozi uliopita sio jema kwa sasa
Kama taifa tuwe na plan flan amazing ambayo regardless utawala itaendelea kutekelezwa
 
Mfano
Ishu ya Dodoma ni nzuri japo yataka maandalizi ya muda mrefu mana sio emergency ile ni jambo la kitaifa instead tunaona matamko ya kukurupuka kwa viongozi bila kujali wanaathiri maisha ya watumishi weng

Mfano 2
posho mbalimbali za watumishi ziko kisheria jamaa saiv amekata, who knows atakaekuja atarudisha yani tunakosa mwelekeo tunaenda kwa hisia za kiongozi jambo ambalo lina madhara yake
 
Kwa kifupi kabisa, TATIZO LETU KUBWA NI KUKOSA MKAKATI SAHIHI WA KISIASA. Hatujawahi kupata uongozi makini uliodhamiria kujenga utaifa wa dhati (nation building) wa Tanzania. Kama Mwalimu JKN alivyosema pale Mbeya Stadium kabla ya ukoloni halikuwepo taifa la Tanganyika (wala Tanzania). Uhuru ulipowasili ulikabidhiwa kwa kundi la watu waliokuwa na dhana za kila aina (kuanzia utaifa kwa JKN, ukabila, udini, ubinafsi n.k. kwa wengine). Kama kawaida ya Waafrika "waliopigania uhuru", wengi walitaka kujipatia "utambulisho na manufaa maalum" kwao na kwa makundi yao. Mwalimu alitaka kujenga taifa la Tanzania lakini alishughulika zaidi kibinafsi na kidikteta kiasi kwamba hakujenga timu kubwa na imara inayojitegemea yenye maono (visheni) ya ujenzi wa taifa imara la Tanzania. Aidha, alikazania zaidi kurundika kila kitu kwenye mfumo wa chama kimoja ambacho alikuwa na udhibiti binafsi wa asilimia 100.

Athari yake kubwa ni kujenga kada kubwa ya wanafiki wenye kujikomba badala ya kufanya kazi makini ya uimarishaji wa utaifa na uzalendo. Hata mifumo ya kuhakikisha umakini katika kusimamia rasilimali, maadili na tunu za taifa haikuwekwa. Kila kitu kiliachwa kutegemea rehema ya rais aliyepo madarakani.

Tanzania imekuwa na wasomi wengi na bora tu. Wengi tuliopata bahati ya kusoma angalau hadi sekondari enzi za mwalimu, tulipitia mfumo bora sana wa elimu. Tanzania ina neema kubwa sana ya rasilimali na utajiri mwingi tu wa asili. Tanzania ina watu wengi wasio wakorofi, wasioshikilia misimamo mikali ya kikabila wala kidini; ni wavumilivu sana na, hivyo, tumeepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tumekuwa nchi imara (stable) kwa upande huo. LAKINI uongozi wetu umegubikwa na ubinafsi uliopitiliza kiasi kwamba umediriki kusaini mikataba ya kifisadi na wageni inayohujumu "taifa" isivyoelezeka. Nchi nyingi zina "red lines" ambazo ukitaka kuiba huzivuki, lakini sio Tanzania. Hii ni kwa sababu kitu kinachoitwa taifa hakithaminiwi kabisa bali maslahi binafsi.

Halafu tumejenga mwenendo wa ulaghai mkubwa sana tukitumia kauli za "amani', "utulivu", "upendo", "uzalendo" na "mshikamano" wa kipekee wa watanzania huku wananchi wakinyanyaswa vilivyo na kutakiwa kuwa kimya muda wote ili "wasiharibu sifa nzuri" ya Tanzania. Hatua anazochukua rais wa sasa, JPM, na jinsi zinavyoshangiliwa (pamoja na mishkeli yake) zinadhihirisha kiwango cha unafiki ambao hili "taifa" limeulea na kuuvumilia tangu uhuru.

KINACHOHITAJIKA SASA NI "JIBU SAHIHI LA KISIASA". RAIS MAGUFULI AMEANZA VIZURI KWA KUUTIKISA (SHOCK) MFUMO WA UNAFIKI NA UFISADI TULIOISHI NAO TANGU UHURU. NA MATOKEO YAKE YAMEDHIHIRISHA UOZO TULIOKUWA NAO MIAKA YOTE HIYO. HAKUNA UBISHI. HATARI INAYOELEKEA KUJITOKEZA SASA NI KWA HUYU RAIS KUFANYA MAKOSA YALIYOFANYWA NA MWALIMU JKN YALIYOTUACHIA TAIFA LISILO ENDELEVU; LILILOBAKIA KUWA PEPO YA WANAFIKI NA MAFISADI WASIO NA HAYA WALA MIPAKA: WAKITUMIA MWAMVULI WA SIASA KUFANYA HUJUMA ZA KILA AINA KUJINUFAISHA BILA KUJALI WANALIWEKA TAIFA KWENYE MUSTAKABALI UPI.

TUKO KATIKA KIPINDI NYETI (CRITICAL). WALE WALIO KARIBU NA KWENYE NAFASI ZA USHAURI, WAJITAHIDI KUMSAIDIA RAIS AHAKIKISHE ANAPOENDELEA KUI-SHOCK SYSTEM BASI KAZI YA KUIMARISHA MIFUMO SAHIHI NA ENDELEVU YA UTENDAJI NA USIMAMIZI IWEKWE. NA RAISI NAYE ATILIE MAANANI SANA UMUHIMU WA KAZI YA KUJENGA MIFUMO IMARA, ENDELEVU YA KITAIFA. KWA KADIRI WANANCHI WATAKAPOONA MISINGI YA KUJENGA TAIFA IKIIMARISHWA, HAKI KUTENDEKA, WAOVU KUADHIBIWA NA WEMA KUZAWADIWA BILA UPENDELEO, BILA SHAKA WENGI WENYE NIA WATAIMARISHA UZALENDO NA KUREJESHA HAMU YA KUJENGA TAIFA WAKIJUA KUWA TAIFA LITAKUWA AMINIFU KWA AJILI YAO NA VIZAZI VYAO. SIO SASA HATA WAKITAKA KULIPA KODI WANAKUWA NA SHAKA KUWA ITAENDA KUWANUFAISHA WAJANJA WACHACHE. HALAFU KAULI ZA UZALENDO ZINATOLEWA KINAFIKI TU.
Ni wapi uliona wanasiasa wakileta mapinduzi ya maendeleo?
 
Mkuu usiumize kichwa na nchi hii, wewe pambana na maisha yako na familia yako. Kuna watu wengi tu ambao hawana muda wa siasa wanazidi kutajirika, ikiwemo wahindi, siasa za nchi hii achia wenyewe
 
Tatizo siyo la kisiasa, wala uvivu, au kukosa elimu, na siyo hata uwivu. Tatizo ni kukosekana kwa uhuru wa kuchagua au kama milton freedman alivyouita "Freedom to choose". Wengi hamta elewa hii concept kwahiyo someni kwa umakini.

Ukiangalia historia na nchi, jamii na idadi za watu walioendelea wote walipoanza walianza kwa kufeli mara chungumzima.
Marekani ilipoanza ilikosea mambo chungu mzima. Lakini kupitia kuwapa watu uhuru na kuondokana na sheria zinazozuia uhuru wa kujitegemea na wa soko, watu wakaanza kuwa wabunifu.

Fikra za watanzania ni kwamba "kukiwa na tatizo lazima serikali iingilie na iamuwe jinsi watu watakavyo tatua hilo tatizo na iamue jinsi watu watakavyoishi ili kuepuka hilo tatizo" wakati hao hao watu ukiwauliza "je ukiwaga na tatizo kwenye mahusiano yako kimaisha na serikali iingilie hayo mahusiano na ichague jinsi utakavyo ishi?" Atakwambia hapana.

Watu hawaelewi kwamba maendeleo ya kifikira, kinchi, kiuchumi, kiafya, kielimu na kadhalika ni kama maendeleo ya mahusiano uliyonayo na watu maishani. Hayo maendeleo hayahitaji serikali bali uhuru wa kufeli. Fikira mbaya, uchumi mbaya, huduma za afya mbaya, elimu mbaya zote zitaachwa watu wakizichoka kama vile wanavyo wachoka marafiki wabaya na kuwaacha. Ambacho hatufikirii ni kwamba hatuhitaji kuwalazimisha marafiki zetu wawe watu wazuri kwasababu wanajua wakiwa watu wabaya wataachika haraka sana. Ni hivyo hivyo na sekta zinazo hitaji maendeleo. Watu kwenye hizo sekta watakaofeli hawahitaji kulazimishwa na serikali ili watoe huduma bora kwa bei nafuu, wao wenyewe watalazimika kubadilika wakiona watu wanawakimbia au kuwaacha.

Cha muhimu kuelewa kutokana na huo ufafanuzi ni kwamba ni serikali pekee ambayo inajua kwamba haiwezi kuachika kwasababu watu hawana uhuru huo. Hii ndiyo maana viongozi wa serikali hawaogopi kufanya makosa kwasababu wanajua wakifeli bado wataendelea kuwa madarakani au kulipwa. Kitu kinachowezesha serikali kuendelea bila kujali wateja au wananchi ni mikopo na hela ambazo serikali yenyewe haina.

Kwenye soko, biashara zote zinajua kwamba zitapoteza hela na kuishia kufunga zisipo wafurahisha wateja lakini kwasababu serikali ni ukiritimba kwenye sekta yake yani watu hawana uhuru wa kuchagua uongozi mwingine mbali na serikali, basi kila siku itaendelea kufanya inachofanya bila kujali na itaendelea kukopa hela bila kujua uwezo wa kuzilipa na watu hawataweza kuiacha huduma yake.

Huu ndiyo uhuru nianaouongelea na ni uhuru huu unaoleta maendeleo kwenye soko lakini ni uhuru huu ambao unakosekana ikija kwenye sekta ya uongozi.
 
Mkuu,
Napinga hoja yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Una point nzuri Ila ulipoiharibu ni hapo kwenye Hiyo kauli ya kichochezi ya umwagaji Damu. Kwanza Watanzania tumezoea kuishi kwa umoja na kushirikiana katika jamii zinazotuzunguka. WanaSiasa ndio wameleta haya matatizo yote ya chuki za Kidini, Kiukanda, Kikabila, Kiitikadi, Kijinsia n.k.

Naomba nikukumbushe tu kwamba Tanzannia ni Nchi ambayo Ina SHERIA na KANUNI. Watanzania tulio wengi tulizoea kuishi na kufanya shughuli zetu kiujanja ujanja bila kufuata taratibu za nchi.
Umekuja utawala wa awamu ya 5 ambao unarudisha mfumo wa kufuata Sheria na taratibu za nchi, matokeo yake tunaona watu wasio waadilifu na weledi kutwa kukicha wanaiponda na kuikebehi SERIKALI kwa manufaa Yao binafsi na sio kwa manufaa ya TAIFA.

Wewe Kama ni Mtanzania MZALENDO nafikiri utatafakari upya hiyo kauli yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Kila la heri.
Mkuu kwa ukweli wako kutoka moyoni wewe unadhani sheria inafatwa?naomba nipe mifano michache na nini kipya tangu sheria iyo sheria ifwate kimetokea kimenufaisha wananchi ?
 
Kwanza kabisa Hatuna dira kama taifa. Kila awamu inakuja na lake.

Pili tumeshindwa kutofautisha siasa na serekali....utendaji na siasa, siasa na weledi.

Tatu Kwa kiasi kikukwa uzalendo umepunguwa.

Mwisho wananch wengi hawana uwezo wa kutambuwa, kuhoji na kupambanuwa mambo.

Hivyo shida kubwa ni Elimu
 
Nakuhakikishia pasipo na Shaka HAKUNA litakalotokea. Serikali na vyombo vyake vya ULINZI NA USALAMA wako makini kuliko unavyofikiria wewe na baadhi ya watu wenye fikra Kama zako. Kama huamini Jaribu kuibeep serikali uone Kama hawatakupigia.
So umakini wa Vyombo vya usalama ni kuwapiga na kuwalemaza critics wa serikali!? Qwi Qwi Qwi, hii itakua tafsiri mpya kabisa ya umakini wa vyombo vya usalama.
 
Kwa fikira zangu binafsi naona ni UNAFIKI na UOGA.

UNAFIKI
Kama watanzania tutaacha unafiki wa kufumbia vile tunavyoona havifai katika jamii yetu ni wazi kwamba hakuna siku wala sehemu tutasonga mbele. Unafiki mkubwa unachangiwa na ubinafsi wa watu kujijali wao ama na kakikundi kadogo kanako wazunguka kufikia hatua kwamba wanatanguliza mbele kila kinacho wapa fursa wao ya kunufaika. Ka unafiki haka kanapelekea watu kufumbia macho mambo ya msingi ya kulisaidia taifa hata pale anaeyatenda kakosea hawatothubutu kumsahihisha kwa wakati muafaka zaidi ya kusubiri adondoke kwanza wamnyooshee vidole.

WOGA
Uoga ni zao la unafiki. palipo na unafiki uoga uzengea zengea siku zote. na hili linahusisha uoga wa kushindwa kumsahihisha mkubwa japo kakosea na uoga wa mkubwa kutosikiliza maono ya mdogo akiogopa kuzalilika kuwa karekebishwa na mdogo. Uoga wa kinafiki ni ule wa kukubali kila kinacholetwa mbele yako ukihofia aliyekuletea ni nani labda pengine anashikiria dhamana yako. Ni wazi hili linaturudisha nyuma sana.

MATOKEO
Uoga upelekea watu kukumbatia maarifa waliyonayo kulisaidia taifa kusonga mbele. Hujenga jamii ya ndio mzee na hivyo kuendeshwa na fikra binafsi za mtu mmoja mmoja. Unafiki ni kiwango cha juu kabisa cha kukosa uzalendo kinachopelekea watu kutenda kwa masilahi binafsi. Unafiki uzalisha rushwa miongoni mwa wanafiki wanao ficha maovu yao ndani ya msuli mithili ya busha. Muhimu turejee nyanja ambazo mwalimu Nyerere alisistiza miaka ya sitini huko kuhusu kujisahihisha sisi na jamii kwa ujumla.
 
The problems of the world(Tanzania) cannot possibly be solved by skeptics or cynics whose horizons are limited by the obvious realities. We need men who can dream of things that never were.”
– JFK
Hakuna solution nzur kma hyo
 
Back
Top Bottom