Tanzania: Nini tatizo letu kama Taifa? Tunajikwamuaje?

Mziwanda,
Chief mkandara. Kiongozi anatoka ndani ya jamii husika, na uzalendo si lazima uanzie na uongozi, bali kwa mtu mmoja mmoja. Suala la uhuru lina upana wake. Uhuru wa bendera kwa mtazamo wangu ulikuwa na nguvu miaka ya mwanzo ya uhuru. Miaka ya 90 hadi leo mambo mengi ni ya kujitakia. Mikataba mibovu na uwekezaji holela na soko huria ndio vimetufikisha hapa. Uzalendo tangu ngazi ya mwanajamii hadi mtawala ungetumika, hayo mambo hapo juu yangetujenga. Uhuru tulio nao unatosha sana kujiletea maendeleo
Mkuu nitakuuliza wewe UZALENDO ni kitu gani?..devotion to what?..Ni nini haswa context inayojenga neno hili ktk jamii yetu? Unaweza vipi kuomba uzalendo toka kwa wananchi ikiwa hatuna Utamaduni hata huo wa kujenga Nationalism. Hatuna itikadi inayounda sheria na ethics kiasi kwamba kipimo halali cha Uzalendo wa Mtanzania kitatokana na mila na desturi za watu hawa..Nambie mkuu wangu pengine mimi natzama upande usokuwa na tija kabisa lakini ukweli ni kwamba Taifa bila mwongozo ni sawa na Merikebu inayokwenda pasipo dira..

Kila naposoma maandishi yetu ktk vyombo mbali mbali, Uzalendo umechukuliwa kama kitambulisho cha Uraia (Uhuru wa Bendera) kwani taifa lote bado linatawaliwa kifikra. Mtu akihamia Ulaya na kuchukua Uraia basi huyo sii Mzalendo! Mtu akikipinga chama CCM huyo sii Mzalendo hata kama uongozi ni mbaya. Mikataba mibovu sii matokeo ya wananchi kukosa Uzalendo isipokuwa ni matokeo ya kutokuwa na itikadi ambayo sote tunahitajika kuwa devoted to (Uzalendo)

Na ndio maana Mkandara akipiga kelele hapa kulaani Ufisadi wa Mkapa wapo wengine wataniona mchawi kwa sababu Ufisadi wake kulingana na Katiba (msahafu wa kuiga) sii HARAMU..ingawa consciousness yetu ya Uzalendo inatuambia kabisa kuwa kitendo hicho ni Haramu na mtu kama huyu anahitaji kufia Jela..Tumeshindwa kutenganisha Patrotism na Natinalism ktk matetezi yetu ya Uhuru wa Mtanzania kama vile watu wasiokuwa na dini.

Na hakuna mafundisho yoyote ya Kijamii yanayolaani Ufisadi. Kwa hiyo hata Ukimchagua kiongozi ambaye haamini Ufisadi ni haramu utaweza vipi kumpima Uzalendo wake ili hali wewe mwenyewe huamini kama Ufisadi ni haramu.
 
Tatizo letu kitaifa ni WANANCHI WENYEWE.

Hayo mengine mnayaleta kujaza nafasi tu, ilala tatizo kubwa ni la wananchi kukosa self awareness na somo la uraia. Hawajui haki zao za msingi na ni rahisi kudanganyika.
Na hao wananchi ndio wanaochagua viongozi wasio na uzalendo na walafi.

Kwahiyo tatizo ni WANANCHI na si VIONGOZI
 
Mziwanda,
Mkuu wangu Uongozi bora pamoja na hayo ulowaweka..Kiongozi anayeweza kusimamisha sheria hutokana na kujibainisha huko na ndiye tutakayeweza kumwita Kiongozi Bora..
Kwa mtazamo wangu kuna mambo muhimu sana ambayo yamesababisha hali hii tulokuwa nayo leo.

UHURU.
Uhuru wetu umepewa tafsiri ya Uhuru wa bendera, uhuru ambao unatangaza nchi yetu kwa rangi za bendera yake/zake na sii WATU wake. Tumesahau kabisa sababu zilitufanya tugombee Uhuru kama Taifa la WATU wa aina fulani na wenye tamaduni na mila amabazo zilikuwa msingi na ndizo zimetupa ID ya Utanzania..Pasipo wananchi kuwa na Utamaduni wao bila shaka hupoteza hata thamani ya Uhuru wao. Hivyo tulipopoteza ID yetu tumepoteza Uhuru na mwongozo wetu Kitaifa.

Na ndio maana hatuna culture ya kuifuata zaidi ya kuiga toka nje. Hatuna malengo kama jamii moja isipokuwa tunajipima kwa matamanio ya Kibinadamu..Haki za Umoja wa Mataifa zinatumika zaidi ya kufikiria KHaki zetu wenyewe kwanza kama Taifa huru. Hivyo, WATU hawawezi kulijenga Taifa ambalo hawawezi Kujibainisha nalo Kifikra (kiroho) isipokuwa kwa kutazama nje.

Ndio maana tunapokuja ktk swala la Viongozi bora tunapata Utata mkubwa kutambua Ubora upi unaotakiwa toka kwa viongozi wetu ikiwa sisi wenyewe hatuna malengo isipokuwa mahitaji yetu yanapangwa kutokana na matatizo tunayokutana nayo njiani kama vile msafiri Jangwani.
Nimesoma habari nyingi sana humu kuhusiana na Uongozi uliopo lakini maajabu ya Mussa ni kwamba hata sisi wananchi wenyewe hatufahamu tunataka nini toka kwa kiongozi zaidi ya kuwa responsible na maandishi ya culture za kigeni.
Hata huyo Mussa aliwaokoa Wayahudi kwa imani ya Mungu wake, dini yake na waliomfuata wakitanguliwa na Imani ya Mungu wa Mussa (Jews) kuwaoondoa ktk utumwa. Na Mussa mwenyewe alikuwa na imani na uwezo wa Mungu wake ndipo uongozi wake unapokuja kuwa muhimu..Na ni kutokana na Imani hiyo ya wayahudi (Jews) ndio iliwafikisha na kuunda taifa la Israel pasipo kujali kuna watu wa kabiola moja ama nasaba wasioamini Mungu wa Mussa kuwa ni maadui zao.. (vita Ya Jericho).


Kwa mtazamo wangu, MATATIZO yetu ni mengi sana kabla hatujafikia kujiuliza nini MAHITAJI YETU..Na Tatizo kubwa kuliko yote ni kupoteza Uhuru wetu, jambo ambalo limezaa viongozi wabovu ambao pia wamezaa Ufisadi. Hivyo sielewi kama suluhisho la Matatizo ya Tanzania inatakiwa tuanze juu kwenye UHuru tukishuka chini hadi Ufisadi au Tuanze toka kwa Ufisadi na kupanda juu kufikia kuutambua Uhuru wetu.


Bob;

Utaandika sana mkuu, na baadaye leo nitarudi kujadiliana na wewe ila mi nasema tatizo kubwa ni WANANCHI wenyewe.

Fikiria kwa undani, nitarudi baadaye.
 
Mkandara:
Kuna tofauti kati ya utaifa (nationalism) na uzalendo (patriotism). utaifa ni hali ya kujumuika pamoja na kuwa na kauli moja kama jamii dhidi ya mtu au watu wasio wa jamii husika. wamarekani wana utaifa. mashariki ya kati wana utaifa. utaifa hujengwa juu ya misingi ya utamaduni imara. utamaduni humtambulisha mtu au watu fulani dhidi ya wengine. bahati mbaya Africa utamaduni wetu ni duni na ndio maana utaifa wetu nao ni duni.

uzalendo kwa upande wa pili ni hali ya mtu mmoja mmoja kuwa na huruma na uchungu juu ya jamii yake dhidi ya hila za mwanajamii mwenza au mvamizi wa mali au identity ya jamii husika. ukiegemea sana siasa kuna upotofu wa maana za misamiati inayotumika. rushwa kwa mfano imepewa jina takrima. mtoto anayezaliwa leo akakulia katika hiyo takrima hawezi kujua tofauti yake. ndio maana uzalendo wa kisiasa na ule ulio katika maandishi ni vitu viwili tofauti.

naamini kuwa ufisadi ni haramu tena sana. ndio umetufikisha hapa kama taifa, na mafisadi wanajulikana sema tu wanalindana na wana nguvu na wana ngozi ya kambale. anayesema kuipinga ccm si uzalendo nae ni fanatic au anajua anachofanya-indoctrination. na neno uzalendo limetumika kwa wajinga (ujinga si tusi) kama ganzi ya akili (opium of the mind) kuwapumbaza na kuwafanya wajione wana dhambi pale wanapotaka kukosoa ukweli uliofichwa. bahati nzuri tuna watu wenye upeo wa kung'amua hayo na wanayafanyia kazi japo katika mazingira magumu. tukitaka kuyaondoa haya masahibu yote dawa ni kuwa wazalendo kwa maana halisi ya uzalendo. shida ipo katika kuupandikiza tena huo uzalendo ndani ya wana jamii. pale sisi kama taifa tutakaposena hapana kwa mikataba mibovu, ufisadi, uvivu, uharibifu wa rasilimali, n.k. hapa tuzungumzie kuhusu mkakati wa kujenga utaifa na uzalendo.
 
Tatizo kubwa tulilonalo kama jamii ni elimu ya uraia. wananchi hawajui haki zao na jinsi ya kufuatilia haki zao zinapochukuliwa na viongozi au watu maarufu. Hiyo ndo inapelekea viongozi wetu wanafanya wanavyotaka kwa sababu hakuna anayewawajibisha. Kama tungekuwa tunafahamu haki zetu watu wa richmond ni wengineo wangeishakuwa wamewajibishwa kama siyo na serikali basi jamii yenyewe. Hakuna anayeweza kushinda nguvu ya umma.
 
FairPlayer & mziwanda,

Shukran sana wakuu zangu kwa kufungua mjadala mpya ambao ni muhimu sana ktk kutafuta haswa wapi tulipoharibikiwa.

Kwa maana nikiwasoma nyote napata picha mbili tofauti kwani FairPlayer anazungumzia zaidi wananchi kukosa elimu ya Uraia (Utaifa) ambayo ndiyo imetuunganisha sisi sote kama Taifa moja chini ya bendera ya Tanzania..Na huko ndipo tunakuta hiyo Katiba yenye madudu ya ajabu ajabu..Lakini at the same notion Ufisadi unaweza laaniwa na kuhukumiwa ktk misingi ya Nationalism na sii Patriotism..

Ni mtazamo wangu na ndicho haswa kilichonisukuma kumuuliza Mziwanda maana haswa ya Uzalendo kwani mara nyingi sana Uzalendo hautazami mali ya seriikali (Utaifa) kama ni haramu kwa sababu haipo ktk misingi ya sheria na hata ethics za wahusika haswa pale Taifa (national status) inapojengwa na multicultural ama makabila mengi. Na ndipo tunapopoteza mila na desturi kiasi kwamba leo hii kama Watanzania hatuna culture.

Hakika mmefungua mjadala mpya unaoweza pingana kwa kiasi kikubwa na hizi hisia za wananchi kukosa /Utaifa/Uzalendo ama malengo ya kutoa hoja au changamoto kwa wanasiasa, wahubiri na hata Vyombo na taasisi ambazo zimefikia maamuzi ya kutaka kuwafundisha wananchi Elimu ya Uraia (Utaifa) ili hali Katiba yenyewe ina hitlafu kibao zikiwemo hizi za kuhalalisha Ufisadi kutokana na kutokuwa na miiko na maadili.

Pia nakubaliana kabisa Na Mziwanda anaposema wananchi wamekosa Uzalendo na sababu haswa ya kukosa Uzalendo ni kwamba hakuna hakuna ethics wala sheria zinazoambatana na Uzalendo inapofikia kutazama Ufisadi wa mali za Taifa na ndio maana leo tunashindwa kukemea Ufisadi kwa sababu sii haramu kuchukua/kuiba - Mali ya Serikali.

Naomba kuwakilisha mtazamo wangu ktk hizo sura mbili...
 
Mambo makubwa yanayosababisha viongozi wetu washindwe kutimiza wajibu wao kama upaswavyo, ni kama yafuatayo:

1. Kutokujiamini (lack of self confidence)
2. Ubinafsi (selfishness)
3. Kutoelewa mipango iliyoko mbele yao kwa utekelezaji
4. Kulindana kwa kuzingatia usaidizi katika mambo yasiyo na tija kwa Taifa
5. Kuweka kipaumbele ajenda za kisiasa na kuacha kutekeleza ajenda muhimu za kiuchumi, kijamii na kimaendeleo halisia
6. Kutoaminiana
7. Kutofahamu maana halisi ya uongozi na kuwa kiongozi hutakiwa kuongoza kwa mifano
8. Uteuzi mbovu wa viongozi wa ngazi mbalimbali
9. Kutokujali matokeo ya maamuzi yanayofanywa na viongozi.
 
Recta,
Mkuu kidogo mimi nashindwa kukubaliana na hoja yako hasa pale unaposema HAWAELEWI..ni kitu ambacho kinatokana na kutoeleimka kama sikoei... MKuu jamaa hawa wanaelewa sana!

Mimi naamini kabisa kwamba viongozi wetu wote wanachokosa ni Uzalendo, na sisi Wananchi tumekosa sii tu elimu ya Uraia bali wamepoteza hata Uraia wetu..Sisi ni wakimbizi ndani ya nchi yetu wenyewe..And all these are the core sins of SELFISHNESS ambayo imetokana na Umaskini wa hali na Mali kwa muda mrefu sana, 40yrs ni maisha ya mtu mweusi!.
Viongozi wetu kwa Ubianfsi wao:-
1. Wanajiamini sana na ndio maana wanafanya madudu haya kinyume cha sheria.
2. Ubinafsi (selfishness) mara nyingi hutokana na Umaskini kuliko Utajiri.
3. Wanaelewa vizuri mipango yao binafsi mbele, na hawana sababu ya kufikiria taifa zima ikiwa wanajua mbele ya safari Meli hii itazama tu. Hivyo wanachukua lifejackets zao mapema.
4. Wanalindana kwa makusudi kabisa kwani wanajua kwamba wanayoyafanya sii mema. Utawala wetu ni Mafia, wana a cetain code of conduct for procurement, hivyo kulindana ni lazima kabisa.. it's part of mutual expectations among them.
5. Toka lini Criminals wakaaminiana! ndio hapo utashangaa kwamba pamoja na kuwa wanazo Principals zao bado kila mmoja humwogopa mwenziwe hasa inapokuja swwla la vyeo.
6 Mkuu wanafahamu kabisa maana ya Uongozi isipokuwa hawa watu wanaongoza a crime gang ambayo inafanya kazi Kitaifa. Nina imani kwamba hata Mafia Don Vito Andolini Corleonne (The Godfather) alikuwa kiongozi mzuri sana kwa kazi yake na hakuwa kiongozi wa Taifa..
7. Kuhusu Uteuzi mbaya ni kwa mtazamo wetu sisi kwani hawa watu hawana tena Uzalendo ni Mafia mkuu wangu, Tunategema wamteuwe nani nje ya kundi lao.
8. Mkuu wanajua sana matokeo ya kila linalofanyika, na mara nyingi hupanga wakajua wananchi wata reacxt vipi na wai watajibu vipi.. Soma ile marda ya Mwanakijiji - Tukinunua basi tumerogwa.

Hivyo, mkuu wangu sisi sote tunaitazama picha kama mfungwa magereza ambaye hafahamu kinachopita nje, lakini amini maneno yangu kwamba hawa viongozi wetu sii wajinga na wala sii kwamba hawana elimu au hawafai Uongozi isipokuwa wameamua kuliibia Taifa. Ni ndito waliyoipoitisha toka Azimio la Arusha lilipofutwa Zanzibar.. Haya yote tunayoyaona ni matokeo ya mipango ilopangwa miaka kibao illiyopita..
Trust me, I thought Kikweite hakuwa kati yao lakini ndio hivyo tena, I was very wrong!
 
Tatizo la Tanzania ni kukosa kiongozi mwenye mtizamo wa kimapinduzi na maendeleo ya taifa letu, mengine yote ni ya ziada tu! Wala hatuhitaji viongzi wengi tunahitaji mmoja tu mwenye vision basi, kama alivyo Kagame kwa Rwanda au Museveni (japokuwa naye sasa keshanogewa)
 
Ndugu zangu wana JF mwanzoni mwa miaka ya sitini, sabini na nusu ya themanini nchi yetu ilikuwa na hatua nzuri sana ya maendeleo!

Kipindi kile kila mtanzania aliguswa na maendeleo ya nchi kiasi cha kushiriki hata shughuli za umma kama shamba la kijiji n.k. nilidhani hadi sasa tungekuwa mbali mno katika Afrika na pengine hata kidunia. Lakini tulipo hapamithiliki na utajiri wetu wa maliasili na rasilimali watu tulizonazo. Tumebadilisha viongozi kadhaa wa kadhaa hadi kufikia hatua wengine tukawaita chaguo la Mungu!

Hebu tujadili ndugu zangu tatizo liko wapi, Viongozi?! Viongozwa?! Ukubwa wa nchi?! Ujinga wetu ama watu wa nje wanatupumbaza? Hebu tuiangalie Kenya kwa sasa. Hatuwakuti tena katika uchumi. Wanayo mipango mikubwa kwa midogo. Sisi je tufanye nini?

Wana JF mabingwa wangu wa uchambuzi leteni utatuzi labda tutasikiwa na watanzania na sisi tujivunie Tanzania yetu kisiwa cha amani jamani!
 
Unajua ndo tunatoka kwenye mawazo ya kijamaa na kuingia kwenye mawazo ya kibeberu "capitalistic economy". Ukweli ndio ujamaa ulikuwa na mazuri yake na mabaya yake hasa kiuchumi. Ukisema turudi kwenye ujamaa tuliokuwa nao basi uchumi wetu utaporomoka sawa na kuporomosha jiwe kutoka kileleni mwa kilima hadi chini.

Ukweli ni kwamba kwa sasa nchi yetu imeanza kupiga hatua kubwa kimaendeleo na baada ya miaka si mingi tutakuwa mbali.

Fursa ni nyingi sana Tanzania, ila ni wachache sana wenye upeo wa kuona hilo na kulifanyia kazi
 
ndungu wana JF katika utafiti wangu nimegundua kwamba, tatizo letu kubwa watanzania na linaloweza kusababisha umwagaji damu ni kutokuwepo haki ya kisiasa kati ya vyama vya siasa ingawa kuna matatizo mengine kama kutokuwepo na haki kati ya viongozi wa mashirika na wafanyakazi wa kawaida na kati ya haki ya wafanyabiashara wadogo na wafanya biashara wakubwa na kati ya haki ya matajiri na masikini.
watu makini kama sisi kina gogo la shamba tunaona hili suala la kwanza lakutokuwepo haki kati ya vyama vya siasa litapelekea umwagaji wa damu katika nchi yetu na ishara hii itajitokeza kwenye kikao cha bunge kitakachoanza tarehe 26, kwa bahati mbaya viongozi wetu wakuu hili hawalioni na kama wanaliona wanadhani umwagaji wa damu ukitokea wataomwagika damu watakuwa sio ndugu zao au marafiki zao na baya zaidi wanatuchukia sisi tunaotaadharisha kwa kubainisha yatakayotokea. ila kwa wale wote watakaosoma haya niliyoandika waweke kumbukumbu ili yatakapotokea ajue kwamba akina gogo la shamba walitaadharisha haya mapema ingawaje kuna baadhi ya watu watapuuza nilichoandika
 
Mkuu,
Napinga hoja yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Una point nzuri Ila ulipoiharibu ni hapo kwenye Hiyo kauli ya kichochezi ya umwagaji Damu. Kwanza Watanzania tumezoea kuishi kwa umoja na kushirikiana katika jamii zinazotuzunguka. WanaSiasa ndio wameleta haya matatizo yote ya chuki za Kidini, Kiukanda, Kikabila, Kiitikadi, Kijinsia n.k.

Naomba nikukumbushe tu kwamba Tanzannia ni Nchi ambayo Ina SHERIA na KANUNI. Watanzania tulio wengi tulizoea kuishi na kufanya shughuli zetu kiujanja ujanja bila kufuata taratibu za nchi.
Umekuja utawala wa awamu ya 5 ambao unarudisha mfumo wa kufuata Sheria na taratibu za nchi, matokeo yake tunaona watu wasio waadilifu na weledi kutwa kukicha wanaiponda na kuikebehi SERIKALI kwa manufaa Yao binafsi na sio kwa manufaa ya TAIFA.

Wewe Kama ni Mtanzania MZALENDO nafikiri utatafakari upya hiyo kauli yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Kila la heri.
 
Mkuu,
Napinga hoja yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Una point nzuri Ila ulipoiharibu ni hapo kwenye Hiyo kauli ya kichochezi ya umwagaji Damu. Kwanza Watanzania tumezoea kuishi kwa umoja na kushirikiana katika jamii zinazotuzunguka. WanaSiasa ndio wameleta haya matatizo yote ya chuki za Kidini, Kiukanda, Kikabila, Kiitikadi, Kijinsia n.k.

Naomba nikukumbushe tu kwamba Tanzannia ni Nchi ambayo Ina SHERIA na KANUNI. Watanzania tulio wengi tulizoea kuishi na kufanya shughuli zetu kiujanja ujanja bila kufuata taratibu za nchi.
Umekuja utawala wa awamu ya 5 ambao unarudisha mfumo wa kufuata Sheria na taratibu za nchi, matokeo yake tunaona watu wasio waadilifu na weledi kutwa kukicha wanaiponda na kuikebehi SERIKALI kwa manufaa Yao binafsi na sio kwa manufaa ya TAIFA.

Wewe Kama ni Mtanzania MZALENDO nafikiri utatafakari upya hiyo kauli yako ya UMWAGAJI WA DAMU. Kila la heri.
nakuomba uweke kumbukumbu ili litakapotokea ukumbuke kama hilo nililitolea taadhari hiyo ndio hojs ysngu tu,
 
nakuomba uweke kumbukumbu ili litakapotokea ukumbuke kama hilo nililitolea taadhari hiyo ndio hojs ysngu tu,
Nakuhakikishia pasipo na Shaka HAKUNA litakalotokea. Serikali na vyombo vyake vya ULINZI NA USALAMA wako makini kuliko unavyofikiria wewe na baadhi ya watu wenye fikra Kama zako. Kama huamini Jaribu kuibeep serikali uone Kama hawatakupigia.
 
Nakuhakikishia pasipo na Shaka HAKUNA litakalotokea. Serikali na vyombo vyake vya ULINZI NA USALAMA wako makini kuliko unavyofikiria wewe na baadhi ya watu wenye fikra Kama zako. Kama huamini Jaribu kuibeep serikali uone Kama hawatakupigia.
Usirahisishe hivyo. Hata hiyo serikali ni watu kama wewe. Kikubwa ni kutoa hamasa wajaribu kutoa haki pande zote. Sio kisa vyombo vya usalama vipo macho. Basi wengine wanyimwe haki. Sikubaliani na wewe
 
Back
Top Bottom