Kama Taifa tunaitaji kujua sababu ya Mgao wa Umeme hata kipindi hiki cha mvua

ruukada

Member
Feb 24, 2014
67
117
Kama Mtanzania nayeguswa na jinsi wananchi wanavyoteseka kwa mgao wa umeme ususani kwenye sekta ya wajasiliamali wadogo ( Welding/wanausika na aluminiam, viwanda vidogo vya kushona, saluni za kike/kiume, wachuuzi wa samaki, na wengine kibao) inatia huzuni kwa kweli.

Unajiuliza kweli hii shida ya umeme inasababishwa na binadamu? Miundo mbinu? upungufu wa maji? ama ongezeko la matumizi ukilinganisha na kinachozalishwa?

Hakuna kiongozi aliyewai kuongea ukweli kwenye ili na kuja na suluhisho kwa miaka zaidi ya 20 sasa. Nakumbuka kipindi cha Rais Kikwete kulitokea mgao mmoja Takatifu ambao mpaka ulitajirisha baadhi ya watu kwa uwizi wa mafuta ya generator za majumbani kwa watu. Zikaja kampuni kama IPTL kutatuta tatizo na zenyewe zikawa tatizo. Ikaibuliwa miradi ya "Umeme wa Gesi" kama suluhisho la kudumu na tukaaminishwa tutauza umeme mpaka kwa jirani lakini nayo ikawa sehemu ya tatizo.

Akaja Mwamba (Mungu haiweke Roho yake mahali pema peponi), akaishukia TANESCO kwa nguvu zote na kukiri mbele ya TAIFA ili kwamba kuna watu wanafanya hujuma ili wauze mafuta na generator na kwamba bwawa la Mtera limejaa tope kwa makusudi ya watu. Mkurugenzi wa TANESCO akatumbuliwa.

Swali la kujiuliza watu awo waliokuwa wanafanya hujuma ni wakina nani na wana nguvu gani na je walikamatwa? jibu ni Hapana! japokuwa Kelele za Mwenda zake zisaidia kwa kiasi kikuwa kutokuwepo kwa kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Akaja Mama (Rais wetu Mpendwa), Tatizo likaaanza taratibu (Mkurugenzi aliyetumbuliwa akarudishwa) , akatokea Januari Makamba akajaribu kulizuia lisiwe janga la taifa kwa kiasi alichoweza mara Paa! wakamtoa bila ya sababu zenye mashiko.

Kilichofuata baada ya siku chache sana ni kwamba taarifa tofauti zinazo kinzana kuhusiana na TANESCO zikaanza kila kukicha.

Mara msemaji wa TANESCO aseme kutokana na ukame kina cha maji kimepungua kwa hiyo kutakuwa na mgao mdogo, mara Kiongozi mwingi akaja kusema kuna itilifu ya mtambo , mara Kiongozi mwingine akaja kusema kiasi kinachozalishwa hakitoshelezi maitaji (demand and Supply).

Itimisho likafanywa na Mama mwenye TAIFA LAKE (RAIS wa NCHI) na kusema tutakuwa na mgao wa umeme kwa miezi 6 mpaka March, 2023 na baada ya apo TANZANIA kutakuwa hakuna mgao wa UMEME TENA. hakueleza shida ni nini? na mda wote uwo watakuwa wanafanya nini ? na iyo timeframe wameipataje ?

Mie na wewe tunaelewa tatizo sio kina cha maji ( sasa mvua imenyesha ya kutosha mpaka inaleta mahafa kila kona). Tatizo sio miundo mbinu (hakuna utengenezaji wa miundo mbinu unaofanyika kwa mara moja kwa taifa zima na kwa mda mrefu hivyo. inatakiwa ifanyike kwa phases na kwa haraka kwa kuwa fedha tunazo).

ITIMISHO
tatizo la TANESCO linasababishwa na Mtu ama kikundi cha watu ambao wana nguvu na hawagusiki na wanafanya ama kwa manufaa yao binafsi au kwa niaba ya uwongozi uliopo. Nasema ili kwakuwa baada ya March 2023 mgao utakuwepo tuu, lini? Wazungu wanasema "time will tell"

Swali je! ukiweka kwenye mzani , hayo maslai yanayopatikana yanaendana na impact ya kiuchumi inayosabishwa na ukosefu wa umeme ama gharama zinazotumika kutumia generator ili kuendesha biashara zisife na kupoteza wateja?

Tunaomba Wabunge/ Vyama vya Upinzani kulipigia kelele ili bila kuchoka kwa kuwa linatugusa wote kama sio nyumbani basi kwenye biashara zetu na ni Aibu kwa TAIFA linalozungukwa za vyanzo vya maji kila kona na gesi kila kona kuishi kama tuko karne ya 19.
 
Hili swali la msingi sana, huu mgao wa umeme umeshageuzwa kama mtaji wa wanasiasa, kila siku mgao wa umeme wakati tunaona mvua zinanyesha mpaka mafuriko yanaua watanzania wenzetu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Sasa mbona mlikuwa mnasema shida makamba?
Kipindi Makamba anaungia kulikuwa hakuna mgao alipoingia yeye ofisini tu na mgao ukaanza ndio Hadi Leo

Kipindi Cha Magufuli tuliwahi kukaa miezi 4 bila ya umeme kukatika
 
Back
Top Bottom