Lingamie mara ngapi.. wewe umeshtuka leo!Ndugu zangu nyote mnaotoa maoni katika Jukwaa la Siasa, mimi nina ombi kwenu. TULIOKOE TAIFA LETU. Tunaandika na kutoa maoni, lakini kusema kweli Taifa letu linaelekea pabaya.
Bajeti imenichanganya! Bilioni 19 kutengwa kwa chai na bilioni 35 kwa safari ni jambo la kusahgaza sana wakati tunaambiwa kwamba kuna mtikisiko wa uchumi.
Fedha zilizotengwa kuzilipa kampuni zilizonunua mazao, nazo ni tatizo. Kampuni hizi ni ngapi na zinadai kiasi gani? Je, zikiundwa Kagoda, ili fedha ipatikane kiulaini kuiingia kwenye kampeni za CCM mwaka ujao? Maana CCM imejijgengea utamaduni wa kushinda kwa kutumia fedha.
Ni lazima kitu kifanyike. Tuache maneno na kuanza kufanya kazi ya kuwaelimisha watu. Tuna kazi ya kuwlatoa usingizini. Watanzania wachache wanaweza kusoma habari ndani ya mtandao. Watanzania wachache wanaweza kusoma magazeti, watanzania wachache wana redio na runinga. Hivyo ni lazima tubuni mbinu za kuwaelimisha watu wetu ili tuliokoe taifa letu. Vinginevyo tunaangamia na kuliangamiza taifa letu la Tanzania.