A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Tanga, hapa kwetu kuna kero moja kubwa ambao binafsi naona inaweza kuwa inawagusa watu wengi kwa maana ambao wanaumia au wanakwazwa na kinachofanyika.
Ni kuhusu Hospitali ya Rufaa Bombo hasa Kitengo cha Emergency, kwani kuna uzembe mkubwa sana unaofanywa na wahusika wa kitengo hicho wanaotoa huduma.
Watoa huduma ni wengi lakini utendaji kazi wao hauridhishi, majibu ya watoa hudumu hao ni ya dharau na kutojali watu, ukifika hapo ni kama vile umeenda kuomba msaada wakati wao wapo kwenye majukumu yao.
Simaanishi lazima wasikilize kwa kunyenyekea mahitaji ya wanaofika hapo lakini aina ya majibu yao ni ya dharau na kutojali hali wanazopitia watu wanaofika eneo hilo iwe ni wagonjwa au waliosindikiza wenzao waliopata majanga.