TANESCO yatangaza mgawo wa umeme

Dawa ni kuondoa monopoly ya TANESCO na kubadilisha policy za sasa za umeme,ruhusu private investors wawekeze kwenye umeme kuanzia kwenye uzalishaji mpaka usambazaji then wape incentive kubwa kuanzia tax cut mpaka mikopo,bila kusahau very strong regulatory body!
 
Nakubaliana na wewe asilimia 100. Upo sahihi kabisa na ndivyo hali ilivyo. Ndiyo hali ninayopigana nayo. Soma ripoti yangu ya mwaka niliyotoa Aprili 2009 Bungeni.
Nimekuwa nikipigana wabunge wasiwe wajumbe wa Bodi za Mashirika haya ili kupunguza 'kugawana' misosi.
Nimepigania sana kuanzishwa kwa Office of State Entreprises ili kudhibiti mashirika na bodi zao. Au kuimarisha ofisi ya Treasury registrar.
Nimepigania Bodi kupewa mikataba ili kuwadhibiti.
Hawa wnasiasa wote wa CCM hawa mnaowasikia wanapiga kelele wamo kwenye mabodi au marafiki zao wamo kwa mabodi na wananipiga vita kwa kuwapinga. Lakini sitaacha maana ninaamini ni njia sahihi.

Nakubali mawaziri wanatumia vibaya mashirika yao, mawaziri wote kabisa na ninagombana nao sana. The other day i invoked act no. 3 to detain Mary Nagu and she ran from Dodoma and by the time parliamentary officer found her in Dar she had rectified what she did for NDC. I was to do the same to Ngeleja for not appointing TPDC Board for two years!

Nakubaliana na wewe kabisa na ndio maana nasema sisi wanasiasa tufanye oversight (our constitutional role). Wataalamu wafanye kazi zao. Lakini sisi tunawapowaingilia katika kazi zao ndio tunaharibu. Thats my stand kaka!
Tunashukuru sana kwa michango yenu wote
 
Kweli hili Taifa letu sielewi linaelekea wapi jamani.. Sasa tufuate ushauri wa nani wadau??
 
Poleni sana Watanzania wenzangu. Mpaka leo mna discuss kuhusu mgao wa umeme.
 
Duh kama kweli Watanzania tunaanza hivi sijui itakuaje maana kila siku matatizo lukuki
 
Kwanza sio ajabu kuanza mgawo wa umeme, alishausemea tangu alipokataliwa kununua mitambo mibovu. Ilikuwa suala la muda tu. Mambo uote hayo ya kupambana si waliyajua katika uwezo wao?
 
Hivi ni kwanini tunapoteza hela nyingi kujaribu kuwaita watu waje kuwekeza ikiwa kama tunashindwa hata kuviendeleza vyanzo vyetu vya umeme ambavyo vipo tele. Tuna gas, maji, coal na upepo wa kutosha. Vyote hivi vinatushinda kuvitumia kutengenezea umeme? Au ndo emergency imetengenezwa makusudi ili Richmond izaliwe tena?
 
kuna kigezo gani mgao ni kwa watu wachache tuu?mimi jirani zangu sice mgao uanze hawajakatiwa sasa sijajua kigezo ni nini, ila nahisi pia TANESCO hakuna vichwa, ni vishoka na usanii usanii mwingi zaidi, sasa nini maana ya company au organisation performance? wao wanajipimaje? na kwanini waendelee kuwepo? hii nchi na viongozi wote laana tupu!!
 
Watanganyika! Hebu tusemeni sasa kwa sauti moja kwamba imetosha! naomba kuuliza, hivi ni kitu gani Tanzania kwa sasa kipo shwari? nini kinaendeshwa na kuzaa matunda au kuhudumia wananchi ipasavyo? naomba nikumbushwe labda namwonea bwana mkubwa JK. Kama hakuna, basi naomba niseme kwa sauti kuu, kunajambo la kufanya la sivyo tunakoelekea ni kubaya zaidi, hebu niwakubushe kuwa ni miezi michache iliyopita tulihakikishiwa serikali inanunua mitambo kwa ajili ya kuepusha mgao wa umeme, pia ikasemekana mvua zilinyesha vizuri nmaji yalijaa, sawa najua pia yanapungua, lakini leo kunamgao, madai yao mashine zimeharibika tena zote, ya kihansi na SONGAS zote mara moja! hili linaleta wasiwasi,ukiacha hilo TANESCO wenyewe wanasema mgao ni mdogo lakini umeme unakatwa hata sehemu nyeti za uzalishaji mali, hospitali na balozini, tena kwa saa zaidi ya kumi mchana wakati umeme unahitajika zaidi kuzalisha. Kwangu mimi hii ni hujuma tena ya hali ya juu ilikudhibitisha maneno yaliyokwishasemwa au/na kutoa malipizi kwa mapambano ya ufisasdi yanayoendelea kwani tufahamu kwamba baadhi ya walengwa wapo TANESCO, mimi naamini kwa asilimia kubwa kwamba Huu NI UMAFIA wa baadhi ya watu wachache ambao kwa muda mrefu sasa wamekua wakiuhujumu uchumi wa watanganyika bila huruma ya maisha ya watoto, wajawazito na wazee wanakufa kwa njaa, magonjwa na huduma mbovu wakati nchi yetu ni TAJIRI, nasema haya kwa hasira kwasababu sasa hujuma inafanywa waziwazi bila kujali macho ya watanganyika milioni 40 yanayoshudia. Nasema hukumu ya hawa ni KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI HADHARANI.
 
Tatizo la kuchanganya siasa na taaluma. Dr rashid alitumia taaluma toka kwa wataalamu wake na wana siasa wanalieleza kisiasa.

Sasa ndio ukweli unathihiri
 
Mpaka sasa Dr.Rashid anafanya nini TANESCO wakati ameshindwa kazi,waliomteua wanamuogopa?
 
Kwa kuongezea, kwa nini serikali imeingia kwenye mikataba na IPTL, RICHMOND etc. kwa mfano pesa za richmond za mkataba $172million ( three years contract) zingeweza kununua mitambo mipya 3 ya 100MW toka GE/ROLL ROYCE/ DRESSALAND/SIEMENS etc. bahati nzuri nafanya kazi kati ya hizo kampuni hapa Ohio, gharama ya mtambo (equipment only ya 100 MW ni 30-35million) ukiongeza installation cost , shipping etc ambayo ni 25-75% ya cost ya equipment. utaona kwamba mtambo mmoja ni kati ya 50-60 million mpaka kuwashwa. juzi juzi tu Tanesco wametangaza tender ya 100MW kwa gharama ya $120million, hizi pesa zingetosha kununua mitambo 2 ya 100MW. miezi kama miwili niliongea na classmate wangu tuliyekuwa naye Colombia university ambaye anafanya kazi roll-royce internation kaniambia kuna jamaa wanaitwa noor oil ya waharabu na wahindi wamepeleka bid ya hiyo tender kwa kutumia jina la roll royce kwa haraka haraka nikamwambia huyo classmate wangu kwamba mbona hawa jamaa ni wale wa richmond wanakuja kwa sura nyingine, kwa hiyo tunasubiri tender itoke kwa kweli safari hii tutatumia international lawyer kuwafikisha hawa noor na tanesco kwenye international court ya corruption. haiwezekani mtambo wa 100mw ambao gharama yake ni 50-60million wanunue kwa 120million.
Hii NOOR OIL ilikuwa imekuja kwa gear ya kujenga pipeline kuanzia Dar mpaka mwanza na kujenga refinery in Dar. Hii ndiyo ilikuwa gear yao. Lakini ofisi zao zilikuwa Water Front (Former Nasaco Building) na MD wake ni dada mmoja, I think wa kiarabu au kihindi halafu inasadikika ni dadake/nduguye RA na ni mke wa mheshimiwa sana. Sasa kama ndivyo ilivyo then......wale wenye data tuanikieni kila kitu ili tujue mapema na tupige mbiu mapema kabisaaa!!!!
 
Unachotakiwa kutambua ni kuwa TANESCO, kwa kufuata sheria, walikuwa na muda wa kutosha kuanza mchakato wa kunua mitambo mipya mapema. Hukukuwa na haja ya kuchapia au kuvizia mitambo chakavu katika hilo.
Maamuzi ya kununua mitambo hayapaswi kushabihiana na maamuzi ya kunua maandazi au kanga; kwamba ukiwa na pesa mfukoni basi unakwenda kununua utakacho mara moja.
Katika hili la kupendekeza TANESCO inunue mitambo chakavu ya Dowans, Zito Kabwe ama hakuwa na vision au kulikuwa na msukumo kutoka nje ya 'uwezo' wake. Hakuwa Zito tunayemjua.

..well said Mkuu Sophist.........Itachukua muda sana wengi wetu kuelewa hilo hapo juu..........halafu mijitu isiyoelewa maneno kama hayo juu ndio inapewa mashirika yetu ya umma........damn...........anyway "NDIVYO TULIVYO"
 
Richmond ndugu yangu hawamo. Huyu mwandishi alichanganya tu. Wao ndio walipewa mwaka 2004 wakashindwa.NOIT sasa ni Qatarians, Russians and CCM!

Thanks alot for very prompt responses and your sources backing your arguments. Impressed!
Kama Richmond ina uhusiano na RA then impliedly NOIT nayo ina uhusiano. Kumbuka MD wake hapa TZ ni dada yake ambaye pia inasadikika anauhusiano wa kimapenzi au wa mke na mume mheshimiwa mkubwa saana. Hii pia ni prompt nyingine ya kuiangalia.
 
Shukran kwa maelezo mazuri sana. Tender ya TANESCO ilitangazwa katika magazeti ya kimataifa kwa kampuni zinazojenga mitambo na sio middlemen. Hivyo hao NOIT hata wafanyeje hawawezi kupata. Sasa na wewe nawe kwa nini hukushauri kampuni unayofanyia kazi ibid?

TANESCO hawakutangaza bei ya kununua. Wao walisema wanataka mtambo mmoja wa 100MW na mwingine 60MW. Bei itatokana na wazabuni waliomba, atakaetoa bei nzuri na mtambo imara ndie anapaswa kupata. Bei bado na sio taratibu za tenda kusema ninanunua kwa bei hii, sasa zabuni haitakuwa na maana.

Hebu niambie, katika hiyo kampuni yako inachukua muda gani kuanzia order mpaka commissioning?

Mwisho - umezungumzia fedha za Richmond zingeweza kununua mitambo kadhaa. Lakini hatukulipa hizi fedha kwa Richmond. Tuliwapa advance ya 30m usd halafu tukakatana katika charges. Mpaka mkataba wa Dowans unavunjwa tulikuwa tunawadai 8m usd zilizobaki.

Kama katika vitambulisho - serikali haikai na 172m usd na kusema mkataba huu pesa hizi, hapana. Serikali haina pesa zilizokaa kwa kuchotwa. Huwa zinalipwa kidogokidogo kutokana na makusanyo ya kodi, Hivyo mkataba wa Richmond ulikuwa umesambazwa over 2 years na zile 172m usd zilikuwa zilipwe over 2 years kutokana na kiwango cha umeme tulichokuwa tunanunua. Nadhani umenielewa!
Then I think the general public was mislead through the media and even the Mwakyembe report as it was portraying as the whole was actually spent. Most of us has had that notion in our minds which was wrong.
 
Sasa hivi kila kitu ni vurugu tupu Tanzania hivyo kuna nini katika taifa langu mbona mimi sielewi tunakwenda wapi??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom