Ushauri kwa viongozi wangu wa chama na Serikali kuhusu ahadi za umeme

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Sasa ni dhahiri kuwa suala la umeme linakitweza na kukiaibisha chama tawala-CCM. Pia, umeme unaitweza na kuiaibisha Serikali iliyopo madarakani. Umeme unakatikakatika. Umeme haueleweki. Umeme hauaminiki. Umeme hauzoeleki. Umeme unagawiwa. Unaleta athari kubwa kwa wananchi na kwa nchi.

Mimi najua kwa hakika kuwa ukali wa mgawo wa sasa wa umeme umechagizwa na 'kuungua' kwa mtambo mmojawapo muhimu katika uzalishaji wa umeme pale kwenye kituo chetu cha kuzalisha umeme cha Kidatu. Ila kulitumika nguvu za kimamlaka dhidi ya nguvu za kitaalamu.

Najua kwa hakika kuwa baada ya maji kuwa mengi na mtambo huo kuzidiwa na wingi wa maji, wataalamu wa TANESCO walishauri bila kiburi kuwa maji yafunguliwe kidogo ili ujazo wa maji ubaki unaotakiwa. Wakakataliwa kwa ukali wa hatari na shari. Mashine ikaungua, umeme ukapungua.

Kwasasa, badala ya viongozi wa chama na Serikali kila mmoja kusema lake juu ya mgawo wa umeme na lini hasa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere litaanza kutupa umeme wa kusaza, viongozi wangu mkae kimya. Kauli zenu zinatofautiana na kujishanganya. Mnapelekapeleka mbele kama alivyokuwa Pele bila kelele. Mbaki kimya.

Umeme, tupeni muda tujipange!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Magufuli City, Dodoma)
 
Back
Top Bottom