TANESCO yatangaza mgawo wa umeme

Mkubwa wangu
Niko hapa Dar. Mgao wa umeme eneo ninaloishi unaanza saa moja hivi. Juzi, ijumaa tulikatiwa kwa masaa kama 13. Ni balaa tupu. Kwa sisi ambao shughuli zetu nyingi tunazifanya kwa kutumia computer, you can imagine! Uzalishaji viwandani, mahospitalini, vyuoni, yaani karaha tupu. Bado watu wanathubutu kuongelea vipaumbele vya taifa!

Duh, poleni sana masaa 13 bila umeme! unajua mkuu wangu kusema kweli Bongo tuna ustaarabu wa kitumwa yaani ile ewallah bwana huku ukicharazwa bakora!..Nashindwa hata kufikiria tu hali hiyo ingetokea nchi hizi kwanza maduka yote yangevunjwa vunjwa, ujambazi ungeongezeka mara 10, billions na mabillioni ya hasara zingetokea acha mbali hasara za viwanda na biashara za watu...Nina hakika rais au waziri mkuu angetakiwa kujiuzuru mara moja!... Sii nchi ya Wadanganyika ambayo kila kitu ni Mungu hakutujalia!

Hata hivyo tumsubiri Zitto atuletee habari kamili nini Tanesco wamejibu..inashangaza sana kuona generators za Songos na mashirika mengine zilizowekwa majuzi tu (less than 4 years) tayari imekwisha haribika beyond repair!. kisha tunaambiwa mitambo hiyo ilikuwa mipya!
 
Hili tatizo la umeme linachukua miongo mingapi kulitatua? Maana tokea niko shule ya vidudu mpaka sasa na approach miaka 40 bado lipo tu....why?

Shida ni pale mpangaji anapolalama na tatizo la umeme ... ebo kwani mie Tanesco kama vipi weka generata ukihama hama nalo.
 
Poleni sana lakini mkome kuchagua CCM kwa madai wapinzani hawako tayari,nimekaa states zaidi ya miak kumi sijawahi kuona umeme ukikatika kwa hiyo hata home inawezekana,tatizo ni CCM tuu!
 
Tutaishi maisha haya ya kubahatisha mpaka lini? Tz imekua haina kitu ambacho kitaendeshwa bila ya kuleta maendeleo, sasa wametangaza mgao, haya matatizo yatakwisha lini. yaani nilivyokasirika nashindwa hatakuendelea kuandika, wacha niishie hapa, maana hii ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
 
Kuna kazi kubwa sana katika siasa za Tanzania maana kila mtu ni msemaji wa mambo muhimu katika Taifa letu. Inasikitisha sana
 
Kaka i would do the same with TPDC and STAMICO. These Parastatals have to be guided like nothing. They are potential champions of our economy - TANESCO; TPDC and STAMICO!
Kama mashirika haya yanahitaji guidance ya kiwango hicho ujue tatizo hasa ni Menejimenti unayoisifia hapa kwamba wanakaribia kutengeneza faida! Usidanganywe na uandikaji wa vitabu vya mahesabu ya mashirika haya au ukaguzi unaofanywa na CAG. Vyote ni vya kubumba na usanii mtupu. Kiini cha matatizo ya mashirika ya UMMA ni ulafi wa ninyi wanasiasa wetu ambao umezipa mianya menejimenti za mashirika haya kuyatafuna kwelikweli.
Hebu fikiria waziri anapojengewa nyumba ya milioni 500 na shirika lililo chini ya wizara yake au anapopewa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kampeni mwakani. Rushwa hi imekomaa sana kwenye wizara nyingi na mashirika yake na ushahidi wake ni mgumu mno. Waziri wa kazi anaishi hivo na NSSF yake; waziri wa maji anaishi hivo na DAWASA na mamlaka nyingine za maji mijini; Waziri wa miundombinu anaishi hivo na mameneja wa TANROADS wa mikoa;.......Kamati zenu za Bunge nazo mkipita huko mnalambishwa bahasha nzitonzito; mambo ni magumu mno hadi pale wanasiasa wala rushwa watakapodhibitiwa kwa sheria kama zile za CHINA.
 
Bado mimi napata shida katika kujua kwa kiasi gani watu kama hawa mawazo yao yanavyoweza kuwa sio ya maana na kuona ni kitu cha kawaida sana. hivyo hata kama iwe vipi bado watu watasema tu maana mpaka lile tatizo la msingi liishe kabisa
 
ukosefu wa viongozi walio na mwanga wa mawazo ndio uliotufikisha katika tatizo hili lisilo la lazima la upungufu wa umeme.

akina mwakyembe, shelukindo na wenzao wanajijenga kisiasa kupitia hoja rahisi kama hii ya DOWANS..

Tunakosaa visionary leaders wenye kuweka masilahi ya taifa mbele zaidi kuliko masilahi yao ya kupita ya kisiasa.

pia poor decision making process ya serikali,bunge vimetufikishaa hapa tulipoooo.
waziri wa nishati anapata kazi rahisi kutokuwajibika kutokana na kuzungukwaa na viongozii wababaishaji kama bunge.

leo tuna mgawoo wa umeme kwa tahadhariii amabayoo ilitolewaa mapemaaaaa..
je hiyoo mitambooo mipyaa mbonaa haijanunuliwaa mpaka sasa?

tusonge mbele kwa kuwa na upeo wa mbelee zaidiii kulikooo siasaaa za kichovuuu
 
tanzania tunachokosa ni kitu kimoja kikubwa,kuchanganya SIASA na TAALUMA( Politics with Technical issues), yapo mambo ambayo siasa inatakiwa iyaongelee baada ya Technical part kuapprove 100%, tena bila kuingiliwa! kwa mtindo huu wa kutojali taaluma za watu ndo inatufikisha huku tulipo,tupo almost 80yrs back,still tunajisifia tunao viongozi bila vission,mission na objectives, tutafika wapi,kama karne hii nchi inashondwa kuzalisha umeme wa just few Mw's? mito,maziwa,natural gas, vyote hivi ni natural, tumepewa na Mungu mwenyezi bureee, ni kutumia tuu. Mimi kama ningekuwa president na mawaziri, makatibu wakuu wote kwanza hata suti singevaa,safari za nje kwa wenzetu ningeona aibu kwenda sababu ninaonekana kama chizi, daily safari zoote huwezi hata kucopy and paste? wananchi tupo duni and ni rahisi sana kuwaongoza but still tumelala! inatia hasira na karaha! namini tumelaaniwa na shetani kwani hata yeye hawezi kuishi tz!!
 
Zitto alikuwa sahihi kwenye hili na kama kawaida yetu tuliacha kufuata ushauri wa kitaalam tukavamia ushabiki wa maneno ya "wapiganaji" leo taifa linaingia kwenye kiza anaeumia ni mwananchi wa kawaida.

Akina Mwakyembe na genge lake nyuso zimewashuka wanaona hata haya kusema kitu.
 
Jamani hivi hiyo mitambo ya Dowans ingenunuliwa ndio tusingekuwa na mgao sasa hivi??

Oh my God!!
 
Mimi si mshabiki wa Chadema kama chama lakini kuna viongozi na wa admire ambao ni slaa na Zitto. lakini wengine wote ni pasua kichwa yaani wale wale!!! wakipewa nafasi tutarudi miaka mingi nyuma... nawashauri watafute chama kingine huko waliko wamepotea tena sanaaaaaa! hatuhitaji conservative na mabepari Tanzania tutakwisha kuibiwa.
 
Kama mashirika haya yanahitaji guidance ya kiwango hicho ujue tatizo hasa ni Menejimenti unayoisifia hapa kwamba wanakaribia kutengeneza faida! Usidanganywe na uandikaji wa vitabu vya mahesabu ya mashirika haya au ukaguzi unaofanywa na CAG. Vyote ni vya kubumba na usanii mtupu. Kiini cha matatizo ya mashirika ya UMMA ni ulafi wa ninyi wanasiasa wetu ambao umezipa mianya menejimenti za mashirika haya kuyatafuna kwelikweli.
Hebu fikiria waziri anapojengewa nyumba ya milioni 500 na shirika lililo chini ya wizara yake au anapopewa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kampeni mwakani. Rushwa hi imekomaa sana kwenye wizara nyingi na mashirika yake na ushahidi wake ni mgumu mno. Waziri wa kazi anaishi hivo na NSSF yake; waziri wa maji anaishi hivo na DAWASA na mamlaka nyingine za maji mijini; Waziri wa miundombinu anaishi hivo na mameneja wa TANROADS wa mikoa;.......Kamati zenu za Bunge nazo mkipita huko mnalambishwa bahasha nzitonzito; mambo ni magumu mno hadi pale wanasiasa wala rushwa watakapodhibitiwa kwa sheria kama zile za CHINA.

Nakubaliana na wewe asilimia 100. Upo sahihi kabisa na ndivyo hali ilivyo. Ndiyo hali ninayopigana nayo. Soma ripoti yangu ya mwaka niliyotoa Aprili 2009 Bungeni.
Nimekuwa nikipigana wabunge wasiwe wajumbe wa Bodi za Mashirika haya ili kupunguza 'kugawana' misosi.
Nimepigania sana kuanzishwa kwa Office of State Entreprises ili kudhibiti mashirika na bodi zao. Au kuimarisha ofisi ya Treasury registrar.
Nimepigania Bodi kupewa mikataba ili kuwadhibiti.
Hawa wnasiasa wote wa CCM hawa mnaowasikia wanapiga kelele wamo kwenye mabodi au marafiki zao wamo kwa mabodi na wananipiga vita kwa kuwapinga. Lakini sitaacha maana ninaamini ni njia sahihi.

Nakubali mawaziri wanatumia vibaya mashirika yao, mawaziri wote kabisa na ninagombana nao sana. The other day i invoked act no. 3 to detain Mary Nagu and she ran from Dodoma and by the time parliamentary officer found her in Dar she had rectified what she did for NDC. I was to do the same to Ngeleja for not appointing TPDC Board for two years!

Nakubaliana na wewe kabisa na ndio maana nasema sisi wanasiasa tufanye oversight (our constitutional role). Wataalamu wafanye kazi zao. Lakini sisi tunawapowaingilia katika kazi zao ndio tunaharibu. Thats my stand kaka!
 
Mimi naamini Zitto Kabwe ni mwanasiasa wa mfano kwa vijana wengi huko tuendako. Na ninaamini alikuwa na bado yuko sahihi katika hili la umeme kwasababu zifuatazo;
1. Zitto ameonesha kwamba yupo tayari kufanya maamuzi kitaalamu zaidi kuliko kisiasa hata kama maamuzi hayo ni unpupolar...kitu ambacho JK ana CCM wanakikosa mno.
2. Zitto anaweza kusimamia maamuzi unpopular bila kuyumba mpaka anapoamini vinginevyo. Nakumbuka Mzee Ndesambulo alikaririwa na TanzaniaDaima la Jumapili wakati huo akionya hatari ya nchi kuingia giza kama taifa litaendekeza cheap politics...badae akachimba baada ya kuona ngoma ya siasa za bei nafuu inakuwa nzito kufunika taalama yake ya biashara.
3.Engineer Stella Manyanya, mwanamke wa kilokole, ambae ni mmoja wa wajumbe wa ilikuwa kamati ya kuchunguza Richmond, alikaririwa na gazeti la majira akionesha kutokuwa na wasiwasi kwa hoja kuwa kinachotakiwa sio mkataba, ni mitambo ya kunusuru taifa dhidi ya mgawo.
4.Profesa Lipumba, akizungumza kama mtaalamu wa masuala ya uchumi mbele ya wahariri wa Tanzania alionesha hilo, na kushauri ununuzi wa mitambo kwa misingi ya ubora wake na unafuu wa gharama bila kujali inauzwa na nani, cha msingi taratibu za manunuzi zifuatwe.
5.Dr Lwaitama pia alisisitiza msimamo wa kununua mitambo kwa hoja za kitaalamu zaidi kuliko siasa, hasa katika mazingira ya kwetu ambapo siasa zinaendeshwa kienyeji mno, hakuna professionalism...ndo sababu akamsifu zitto katika hili.
6.Mmoja wa washauri waandamizi katika masuala ya nishati pale benki ya dunia, Engineer Ralph Karhammar alisema suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans limebebwa na siasa kiasi cha kuvuka mijadala ya kitaalamu..
7. Mimi narudia kusisitiza, kwamba uahaba wa umeme kwa sasa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza bado hayafikii 100MG...kama tungefanya mamuzi sahihi kitaalamu tusingetaabika na mgawo unao tukabilli sasa...tatizo la umeme tanzania kwa sehemu kubwa msingi wake sio uongozi wa tanesco, ni uongozi wa nchi....mimi nimepata kuona mipango mikubwa sana ya tanesco ya namna ya kukabiliana na tatizo la umeme kwa miaka mingi ijayo. lakini serikali haitekelezi, inabaki inaendesha sekta ya umeme ki misheni town, matokeo yake inaonekana tanesco kila kukicha wakija na mipango ya dharula, sio tanesco unayotaka haya, ni serikali ya JK.......mimi naamini tunahitaji kubadili mwelekeo wa siasa zetu, tukiacha taifa liendeshwe kwa misingi ya nani ana influence ya media, nani hana, tumekwisha!.....
 
sphist unapaswa kujua kuwa tanesco ni shirika kubwa sana, na mafanikio yake kwa sehemu kubwa yanategemea ufanisi wa serikali...tanesco imekwishawasilisha mikakati ya umeme tanzania kwa miongo kadhaa ijayo, serikali haitekelezi, tanesco wafanyaje?
 
Nakubaliana na wewe asilimia 100. Upo sahihi kabisa na ndivyo hali ilivyo. Ndiyo hali ninayopigana nayo. Soma ripoti yangu ya mwaka niliyotoa Aprili 2009 Bungeni.
Nimekuwa nikipigana wabunge wasiwe wajumbe wa Bodi za Mashirika haya ili kupunguza 'kugawana' misosi.
Nimepigania sana kuanzishwa kwa Office of State Entreprises ili kudhibiti mashirika na bodi zao. Au kuimarisha ofisi ya Treasury registrar.
Nimepigania Bodi kupewa mikataba ili kuwadhibiti.
Hawa wnasiasa wote wa CCM hawa mnaowasikia wanapiga kelele wamo kwenye mabodi au marafiki zao wamo kwa mabodi na wananipiga vita kwa kuwapinga. Lakini sitaacha maana ninaamini ni njia sahihi.

Nakubali mawaziri wanatumia vibaya mashirika yao, mawaziri wote kabisa na ninagombana nao sana. The other day i invoked act no. 3 to detain Mary Nagu and she ran from Dodoma and by the time parliamentary officer found her in Dar she had rectified what she did for NDC. I was to do the same to Ngeleja for not appointing TPDC Board for two years!

Nakubaliana na wewe kabisa na ndio maana nasema sisi wanasiasa tufanye oversight (our constitutional role). Wataalamu wafanye kazi zao. Lakini sisi tunawapowaingilia katika kazi zao ndio tunaharibu. Thats my stand kaka!

Hapa umenena. Kwa kuongezea tuu. Wakuu wa haya mashirika wasiteuliwe na Rais. Kazi hiyo iachiwe bodi. Kwa kuteuliwa na Rais kunawapa kinga dhidi ya bodi na kuifanya ishindwe kufanya kazi yake ambayo ni kudhibiti menejimenti!

Amandla......
 
Unachotakiwa kutambua ni kuwa TANESCO, kwa kufuata sheria, walikuwa na muda wa kutosha kuanza mchakato wa kunua mitambo mipya mapema. Hukukuwa na haja ya kuchapia au kuvizia mitambo chakavu katika hilo.
Maamuzi ya kununua mitambo hayapaswi kushabihiana na maamuzi ya kunua maandazi au kanga; kwamba ukiwa na pesa mfukoni basi unakwenda kununua utakacho mara moja.
Katika hili la kupendekeza TANESCO inunue mitambo chakavu ya Dowans, Zito Kabwe ama hakuwa na vision au kulikuwa na msukumo kutoka nje ya 'uwezo' wake. Hakuwa Zito tunayemjua.

Hivi wewe mwenzangu umesoma hicho kilichoandikwa na Mbala-mwezi na kukielewa au umejibu tu bila kusoma? Maana naona ulichojibu hakiendani kabisa na hoja za msingi za makala husika.
 
Si vibaya tukajikumbusha wizi uliofanywa na Richmond/Dowans hasa kwa wale wanaolaumu Watanzania walio wengi kupinga kununuliwa kwa mtambo wao kama tulivyoshinikizwa na MD wa TANESCO, Idrissa Rashid

Siri ya wizi mkubwa Richmond

Mwandishi Wetu Januari 28, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Watimka na mabilioni ya walipa kodi

Walichotewa kabla hata ya kazi

WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisubiriwa na wabunge kuwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuhusu kampuni ya Richmond Development, kampuni hiyo iliyorithiwa na kampuni ya Dowans, ilitokomea na zaidi ya Sh. bilioni 23, Raia Mwema imebaini.

Kinyume cha maelezo yaliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wakuu serikalini katika Bunge, kwamba Richmond haikuwahi kupewa fedha za Serikali, ukweli ni kwamba kampuni hiyo ilichotewa zaidi ya Sh. bilioni 30 (Dola 30,696,598 za Marekani).

Kiasi hicho ni sawa na asilimia 35 ya gharama ya kodi ambayo msingi wake ulikuwa kufanikisha mchakato wa ufunguaji wa hati ya muamana (letter of credit) kati ya kampuni hiyo na Benki ya Biashara.

Malipo hayo ya asilimia 35 ni utekelezaji wa makubalino yaliyofikiwa awali, kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa baada ya kupewa kitita hicho cha zaidi ya Sh bilioni 30, Richmond ilipewa masharti ya kurejesha fedha hizo serikalini katika malipo ambayo yangefanyika kwa awamu tatu.

Hesabu zilizofanywa ni kwamba Richmond ilitakiwa kurejesha serikalini dola 1,279,044 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 1.3), kila mwezi, lakini katika mikupuo (awamu) mitatu.

Hesabu hizo zinabainisha kuwa kama makubaliano hayo yangefanyika bila ukorofi au kasoro yoyote, Richmond ingefanikiwa kurejesha serikalini fedha ilizopewa katika miaka miwili. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba, Richmond ingelipa deni hilo serikalini ndani ya muda wa uhai wa mkataba wake na Serikali, ambao ni miaka miwili.

Lakini uchunguzi zaidi wa Raia Mwema umebaini kuwa malipo ya awali yalipaswa kuanza kufanyika Novemba, mwaka 2007. Hata hivyo, kutokana na utata wa kampuni ya Richmond hasa kwa upande wa uwezo wake kiteknolojia na utendaji, kampuni hiyo iliuza shughuli zake kwa kampuni nyingine binafsi ya Dowans.

Imebainika kuwa wakati mchakato wa uuzaji wa shughuli za kampuni hiyo kwa Dowans unafanyika, Richmond ilikuwa haijarejesha fedha ilizopewa na Serikali na kwa kuwa Dowans ndiyo iliyobeba mikoba, ilipaswa kuendeleza urejeshaji huo wa fedha.

Kutokana na hali hiyo ya fedha za Serikali kubaki kwa 'wawekezaji' hao waliopasiana mpira wa uwajibikaji, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia timu ya watalaamu wa sheria, ilichunguza mkataba kati yake na Richmond ambao ulirithiwa na Dowans.

Taarifa ya timu ya wanasheria wa TANESCO ilibaini kuwa mkataba huo hauna nguvu za kisheria na kuamuru uvunjwe. Mkataba ukavunjwa rasmi Agosti mosi, mwaka 2008.

Hata hivyo, wakati mkataba huo unavunjwa uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizopaswa kurejeshwa Serikali hazikuwa zimerejeshwa zote.

Imebainika kuwa fedha zilizorejeshwa hadi mkataba unavunjwa ni jumla ya dola 7,674,186 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 7.7), huku dola za Marekani 23,022,412 (zaidi ya Sh. bilioni 23) zikibakia kwa Richmond na mrithi wake Dowans.

Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinaeleza kuwa kutokana na hali hiyo Bodi ya TANESCO pamoja na uongozi wa shirika hilo umekwisha kuchukua hatua.

Hizo ni pamoja na maagizo ya Bodi ya TANESCO kwa uongozi wa shirika hilo kuchukua hatua zinazostahili kuhusu deni hilo na kutokana na maagizo hayo, uongozi wa TANESCO ulilazimika kutoa taarifa rasmi serikalini ili hatimaye ijulikane namna fedha hizo zitakavyorejeshwa.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imechunguza mchakato huo na kubaini kuwa Serikali ilitoa fedha hizo kwa Richmond.

Ofisi hiyo ya CAG, katika taarifa yake ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka ulioishia Desemba 31, mwaka 2007, imeweka bayana kuwa fedha hizo bado hazijarejeshwa serikalini.

"Tunafahamu kutokana na taarifa za uongozi kwamba mkataba kati ya TANESCO na Dowans ulivunjwa Agosti mosi, 2008. Matokeo yake ni kwamba kiasi cha fedha kilichotolewa na kutakiwa kurejeshwa kinaweza kuwa hasara kwa TANESCO au Serikali," inaeleza sehemu ya waraka rasmi wa ofisi ya CAG kwa serikali ambao Raia Mwema imeuona.

Kampuni ya Richmond Development ilipewa zabuni tata na Serikali kuagiza mitambo ili kuzalisha umeme wa dharura nchini.


Kutokana na utata wa zabuni hiyo, Bunge lililazimika kuunda Kamati Teule kuchunguza na kubaini upungufu ambao hatimaye ulimgharimu aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibharim Msabaha waliojiuzulu Februari 2008.

Mbali na viongozi hao kujiuzulu, Kamati ya Bunge iliwasilisha mapendekezo 23 yanayohitaji kufanyiwa kazi na Serikali. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali na baadhi ya vyombo nyeti, akiwamo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Katika mkutano wa Bunge ulioanza wiki hii, Serikali inatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo. Taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 
Ilinibidi niumize kichwa sana kufikiri mawazo ya walimu wangu hawa pamoja na ule waraka wa Mh Zitto Kabwe mwenyewe alioutuma kwetu watanzania kutueleza misingi ya yeye kuamini anachokiamini, kwa upande mmoja, huku kambi nyingine ya wajuzi wa mambo, akina Dk Harrison Mwakyembe, Spika Sitta na Mzee Shellukindo ambao kwa matukio kadhaa ikiwa ni pamoja na kusaidia mchakato wa kumwondoa Waziri Mkuu wa kwanza wa seriikali ya Jakaya Kikwete kwa tuhuma za ufisadi wamefanikiwa kujijengea uhalali wa kuitwa wazalendo kirahisi.

Lakini wakati hayo yakiendelea. Na mjadala ulitaka kuhama kwenye hoja na kuchukua sura ile ile ya awali. Kwamba akina Mwakyembe wanapinga ufisadi na hivyo kila anayetofautiana nao katika lolote, kwa nguvu ya vyombo vya habari vilivyopo kambi yao mtu huyo anaweza kufanywa aonekane anapingana na vita dhidi ya ufisadi.

Nimesema kwa kutumia vyombo vya kambi yao kwasababu kwa jinsi siasa za Tanzania zinavyokwenda, vyombo vya habari vinaelekea kupoteza mantiki ya uhuru wake kama wamiliki wataendelea kuwa waamuzi wakuu wa vyombo vyao viandike nini, visiandike nini! Wakati haya yakiendelea, unajitokeza mkanganyiko mwingine wa aina yake, ambao mpaka sasa sijapata majibu yake. Mana kwa upande mmoja, Waziri wa Nishati na Madini, Bwana William Ngereje kwa kutumia kitambu cha kumbukumbu za mijadala ya bunge- hansard, ametuthibitishia mkanganyiko mkubwa wa mawazo ya watu walewale lakini wanaothibitisha kufikiria tofauti katika kadhia yenye muktadha uleule.

Mpaka sasa Waziri Ngereja amefanikiwa kutuonesha kwamba, kwanza mazingira ya mkataba wa IPTL hayana tofauti na ule wa Dowans, isipokuwa anashangaa kuona wabunge walewale(akina Shellukindo na Mwakyembe) walioisukuma na wanaoendelea kusukuma serikali inunue mitambo iliyoingia nchini kifisadi ya IPTL wanakataa serikali isinunue mitambo ya DOWANS iliyoingia nchini katika mazingira hayo hayo ya kifisadi.Tuhuma hizi ni kipimo cha uadilifu, na zaidi ni kipimo cha kama mawazo wanayoyatoa akina Mwakyembe, Spika Sitta na Shellukindo hayaendi sambamba ama maslahi binfasi ya kibiashara au kambi za kisiasa ndani ya chama cha Mapinduzi.

Binafsi naamini ni muhimu akina Dk Mwakyembe na Mzee Shellukindo wafafanue suala hili kwa heshima yao kama wanasiasa. Maana ni ukweli usiopingika kwamba hata maelezo ya awali yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Mzee Shellukindo kukosoa msimamo wa Waziri Ngereja bado maelezo hayo yanapwaya kuweza kuitwa majibu. Swali linalohitaji majibu ni hili, “ kwanini Dk Mwakyembe na Mzee Shellukindo walipokuwa Kamati ya Viwanda na Biashara walisisitiza na bado wameendelea kusisitiza serikali inunue mitambo/kampuni ya IPTL ilhali kampuni hiyo imekwishathibitika mahakamani kuwa mchakato wake unahusika na ufisadi mkubwa unaoligharimu taifa hili hasara ya zaidi ya bilioni3 kila mwezi?”.

Sisemi kwamba ni muhimu wala ni lazimaTANESCO wanunue DOWANS, ila napata mashaka makubwa kama wananchi tunaweza kufanya maamuzi kwa kuzingatia aina hii ya wabunge, na kama tunaweza kuwa na wabunge wa aina hii. Napata mashaka kwamba inawezekana kumbe tatizo sio TANESCO au serikali, na kwamba huenda tatizo ni aina ya wabunge tulionao. Mana inapofika mahala Mzee Shellukindo na wenzake wanataka kutuaminisha kuwa mazingira ya mikataba hii(DOWANS na IPTL) ni tofauti lakini wameshindwa kutueleza tofauti hiyo ni ipi?”Inatisha. Ninachojua na kuamini ni kwamba; Yote ni mitakaba ya kifisadi, Yote ni mitumba. IPTL ni mitumba ya tangu mwaka 1990, wakati DOWANS ni mitumba ya tangu mwaka 2006.

Hapa hawa jamaa hawawezi kutoa jibu la maana kwa kuwa hansard inawasuta na pia ununuzi wa mitambo chakavu upo sehemu nyingi tu. Hata ATCL alinunua ndege iliyotumika. Sasa ni ajabu gani kwa Tanesco kufanya hivyo?



Tumeambiwa kuwa sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 anakataza kununua mitambo ambayo ni mitumba. Lakini katika maelezo ya Mh Zitto Kabwe, TanzaniaDaima ya Jumatano,Machi11,2009, Mh Zitto Kabwe anasema hakuna sheria inayokataza kununua mitambo ambayo ni mitumba, na kwamba kinachokataza ni kanuni(regulations), sio sheria(laws).

Hapa napo ninapata shida. Kwani machi4, 2009 Bwana Mwakyembe ambaye ni daktari wa sheria alisisitiza katika kipindi maalumu kuhusu suala hili, kilichorushwa ITV akijenga hoja kuwa “Zitto kabwe anataka sheria ya manunuzi iliyotungwa na bunge ivunjwe ili mitambo ya Dowans inunuliwe” haya ni maneno yanayotia hasira, mana bunge ni chombo na mamlaka kubwa sana. Na sheria ya nchi ni kitu kikubwa sana . Sasa swali ambalo Daktari wa sheria, Bwana Mwakyembe hajajibu ni kama kweli aliupotosha Umma kwa makusudi au bahati mbaya kwamba sheria ya manunuzi(ambayo kimsingi inatungwa na bunge) haizungumzii kutonnunua mitumba bali kanuni (ambazo kimsingi zinatungwa na waziri) ndio zinazungumzia kutonunua mitumba.Sisemi kwamba watanzania wapo tayari kuingia gizani ili kulinda sheria ya manunuzi kama ingekuwepo kama kikwazo, bali ninachosema ni usahihi wa kipi kinakataza kununua mitumba; sheria ya nchi au kanuni ya wizara?



Dr. Mwakyembe nadhani wakati akizungumza TBC hakujua kuwa ni Kanuni na wala si sheria. Lakini kwa tabia yake ya majivuno, hawezi kuomba radhi.


Ni muhimu sana mjadala huu ukaachwa uchukue sura ya kitaalamu zaidi kuliko hivi tunavyokwenda kisiasa mno ihali siasa zetu bado changa na hajiwa za kitaaluma vya kutosha. Maana kama tutaenda hivi hasara yake ni kuacha umma upoteze mwelekeo katika mambo ya msingi. Ndio maana nakubaliana kabisa na hoja iliyotolewa na gazeti maarufu Afrika Mashariki-The east Africa la machi 09-15, 2009 ambapo mtaalamu aliyebobea katika masuala ya nishati pale benki ya dunia, Bwana Ralph Karhammar alisema “ mjadala unaendelea kati ya makao makuu ya benki Washington na mwakilishi wa benki hiyo wa Dar es Salaam kupima athari za mgawanyiko kati ya kambi hizo mbili” na kuongeza kwamba “ Suala la ununuzi wa mitambo ya DOWANS limebebwa na siasa kiasi cha kuvuka mijadala ya kitaalamu” na Kwa mujibu wa gazeti hilo, linasema kuwa “ Vyanzo vya karibu na Benki ya dunia vinaonesha kwamba benki ya dunia inakubaliana na hoja za kambi inayounga mkono ununuzi wa mitambo ya DOWANS ili kupunguza uhaba wa umeme ambao kwa sasa unafikia mapungufu ya kiasi cha 192 MW”


Endapo watajibu, hapa watakimbilia hoja yao ya kawaida kuwa na wataalamu wa Benki ya Dunia nao ni Mafisadi na wamekula rushwa.

Kauli ya Mtaalamu huyu wa Benki ya dunia inanikumbusha umuhimu wa azimio la Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma chini ya Mh Zitto Kabwe waliopendekeza Kamati mbili, ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma na ile ya Nishati na Madini zikutane ili kupata mwafaka kwa kupambambanua tatizo hili kwa kina. Na huu ndio msimamo ulioungwa mkono hata na Dk Willibrod Slaa alipohojiwa na ITV “ kwamba kwakuwa Kamati hizi mbili ndizo zenye taarifa za TANESCO ni vema zingekutanishwa ili kubadilishana mawazo na uzoefu kabla ya kuishauri serikali juu ya uamuzi wa kufanya kwa sasa”.

Najua wengine wanaweza kusema kwamba Spika Sitta ameshasema kanuni haziruhusu Kamati mbili kukutana. Sawa. Lakini ni muhimu tukumbuke tu kwamba Spika Sitta alichosema ni kwamba hakuna mahala kwenye kanuni panaporuhusu Kamati mbili kukutana. Kwahiyo kanuni ipo kimya. Ndio maana mi nahoji, Hivi kanuni zikiwa kimya inakuwa zimekataza au zimeruhusu?

Maana akili ya kawaida inaniaminisha kwamba kanuni za bunge sio msahafu wala biblia, vitabu ambavyo tunaamini vimekamilika. Ndio sababu katika mazingira mengine kinachotumika ni ama busara ya Spika wa bunge au uzoefu wa maamuzi yaliyokwishafanywa au yanayofanywa katika mabunge ya Jumuiya ya madola

Kimsingi kama hakuna kinachofichwa wala kutafutwa hapakuwa na sababu za kwanini Spika asiruhusu Kamati hizi mbili kukutana tena kwa suala nyeti na linalottikisa siasa za nchi yetu kiasi hiki. Nasema hivyo kwasababu kuna wengi waliposikia Spika amesema kanuni haziruhusu walifikiri kabisa kwamba kuna sehemu ya kitabu cha kanuni za bunge inakaza kamati mbili kukutana au kutokutana . Kumbe hoja ni kwamba hakuna kipengele kinachozungumzia uhalali au uhalamu wa Kamati mbili za bunge kukutana.

Ni katika misingi hiyo, busara ya kawaida zinazonesha kwamba uamuzi sahihi ilikuwa ni kwa Kamati mbili hizo kukutana badala ya kamati hizo mbili pamoja na Spika wao wa bunge kulumbana kwenye magazeti kiasi cha kutilia mashaka kama kweli bunge letu lina viwango na speed tuliyoahidiwa na Spika Sitta!..Tatizo limejitokeza, Kamati inayohusika na sera imeshafanya maamuzi, lakini inaelezwa bila kuhusisha TANESCO. Kamati ya hesabu za Mashirika ya Umma ikiwa ni pamoja na TANESCO, limepitia hali ya TANESCO kifedha inaona kuna tatizo(kwasababu TANESCO inatumia asilimia 84 ya mapato yake kulipia asilimia42 ya umeme inaopata toka makampuni), TANESCO wanaeleza msingi wa tatizo lakini Kamati ya Mahesabu inaona msingi wake upo kisera, inaogopa kufanya maamuzi ili isigongane na Kamati nyingine ya Nishati na Madini.Uamuzi ambao ni wa busara! Lakini cha kushangaza alianza Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Bwana Shellukindo kukataa mwitto huo akifuatiwa na Makamu wake, Dk Harrison Mwakyembe na kuhitimishwa na Spika Samweli Sitta, wote wakikataa!

Katika mazingira hayo, ndipo watu walio huru kifikra wanaona kwamba pengine kuna tatizo la ziada. Mana kama kweli umeme ni tatizo, na Kama Kamati moja inaomba kukutana kujadili, Tatizo liko wapi?.... hata kama kila moja itakuwa na msimamo wake, si ndio utapatikana ufumbuzi kwa kuchanga mawazo ya pande mbili? Spika aliogopa nini kukubali Kamati mbili zikutane?.

Kama kanuni hazisemi kuruhusu , je ni kweli maamuzi yote ya bunge yanafanywa kwa mujibu wa kanuni kusema? Kama Kamati ya akina Dk Harrison Mwakyembe na Shellukindo inazo hoja za msingi, si ndio ingezitumia kuishawishi Kamati ya akina Zitto Kabwe?..Mana kitendo cha Spika Sitta kuzuia Kamati hizi mbili kukutana ndio kumesababisha dunia nzima kujua kwamba Kamati mbili za bunge zinavutana kufuatia sakata la DOWANS.kitu ambacho hakikuwa na ulazima wowote..na sasa kimezidi kuzusha maswali mengine ya ziada kuhusu misingi ya mvutano huo.


Hapa tatizo si Kanuni za Bunge bali kambi ya akina Shellukindo inajuwa kuwa kamati hizi mbili zikikutana ana kwa ana Kamati ya Nishati na Madini itazidiwa hoja. Kwa hiyo ikabidi watumie nguvu za ziada za Spika kuepuka hilo.

Kumbuka pia kuwa wakati Bunge lilipokuja juu kuhusu kutoridhika kwake na hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu maamuzi ya Bunge kuhusu Richmond, Mh. Zitto alipendekeza kuwa kwa kuwa mihimili miwili ya Bunge na Utawala vimekingana, basi wapeleke suala hilo kwa muhimili wa tatu yaani muhimili wa Sheria ili waliangalie upya na kwa undani suala hilo. Spika alikataa kata kata kwani walijua kuwa suala hilo kwa kuwa liliendeshwa kisiasa zaidi kuliko kisheria, basi lingegonga mwamba na hata pengine kumrudishia Lowassa heshima yake.


Nimesema maswali mengi yameanza kuibuka kwasababu, ni hivi karibuni tu, gazeti la Mtanzania Jumapili, liliandika habari kwamba Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Bwana Harrison Mwakyembe ni mmoja wa wamiliki wa mradi wa umeme wa POWER POOL EAST AFRICA LTD, yenye usajili wa BRELA Na 49624 na kwamba kwa thamini ya hisa alizo nazo kufikia mwaka 2007 ni karibu bilioni1.5. Sasa swali linalojitokeza hapa ni ile hoja ya mgongano wa maslahi.

Kwamba mtu anayelilia TANESCO impe biashara ya kuiuzia umeme ndo anapewa kazi ya kusimamia sera ikiwa ni pamoja na kuangalia mwenendo wa miradi ya Umeme..Sipindi kwamba Dk Mwakyembe asifanye biashara ya miradi ya Umeme kwasababu yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ambayo inatazama mwenendo wa miradi ya Umeme nchini na mwelekeo wa Shirika la Umeme kwa ujumla wake. Ninachosema, na ambacho kanuni za bunge; ile ya 61(1) na ile ya 114(19) ni umuhimu wa mbunge mwenye maslahi katika jambo husika kutangaza kuwa ana maslahi na kiasi cha maslahi hayo. Kitu ambacho Mwalimu wetu Dk Mwakyembe hajafanya tangu awe mbunge.Kwanini hajasema? Anajua yeye!

Ndio maana ni rahisi kuhusisha msimamo wa Dk Harrison Mwakyembe pengine na kushindwa kwa kampuni yake kupewa mradi wa kuzalisha umeme na TANESCO hata kama inawezekana tuhuma anazotoa dhidi ya shirika hilo ni za kweli. Na endapo atapewa mradi na kubadili msimamo ni rahisi kuhusianisha masimamo huo kwa mabadiliko hayo, kitu ambacho sio afya kwa mwanasiasa. Siandiki hivi kwa kupuuza kazi ya Dk Mwakyembe kwa Taifa hili, la hasha! Natambua mchango wake, nathamini mchango wake. Ninachokifanya hapa ni kujaribu kuwekana sawa tunapojadili mijadala mikubwa kama hii ili siku moja tufikie viwango vya kujadiliana maswala na maswali makubwa ya kitaifa bila harufu ya maslahi binafsi ambayo sasa harufu yake imeanza kudhihiri.

Ukweli ni kuwa mapaka Bunge litakwisha Spika hawezi kuruhusu hoja hiyo ya mgongano wa maslahi iletwe Bungeni. Hivi hiyo kampuni ya Power Pool (EA) imeishia wapi?



Ni muhimu tujue kwamba watu sio mawe. Leo anaweza kuwa hivi, kesho akawa vile. Ni Dk Mwakyembe huyuhuyu aliyetukana waandishi wa habari mwaka 2006 kwasababu za kulinda alichotaka kulinda, na Ni Dk Mwakyembe huyuhuyu aliyeponda harakati za wanazuoni kudai haki zao mwaka 2007, kiasi cha Dk Willibrod Slaa kwa uchungu, alipokuwa akihutubia wanazuoni wa mkoa wa Morogoro kwenye Kongamano kuhusu Elimu ya juu nchini, akioneshwa kusikitishwa kwake na mchango wa Dk Mwakyembe bungeni kuhusu elimu ya juu alisema “ Elimu zingine bora wangepewa mbwa”. Ndio maana nakubaliana na Falsafa ya Profesa Shivji! Kwamba “ Tilia mashaka kila kitu”.





Kweli kabisa. Hongera sana kwa uchambuzi wako wa kina na nuunga mkono 100%
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom