Tamko la TCRA kuhusu ujumbe wa simu unaomchafua Dr. Slaa

Mkulima

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
1,034
1,022
Tamko la TCRA kuhusu ujumbe wa simu unaowachafua baadhi ya wagombea wa Uraisi 2010

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA, imekiri kupata taarifa za kuwepo kwa ujumbe unaosambazwa kupitia simu za kiganjani ambao umekuwa ukiwahamasisha wananchi kutokuwachagua baadhi ya wagombea wa nafasi ya Uraisi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 Oktoba 2010.

Akihojiwa na TBC, Naibu Mkurugenzi wa TCRA, Richard Kayombo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha namba hizo huku akitoa rai kwa Wananchi kutokuzijibu au kusambaza ujumbe huo.

"Tumepokea malalamiko mengi tu, na ujumbe unakuja kwenye namba ambazo 03588108226 na mwingine kwenye namba 03588976578. Kwa mwelekeo wa haraka haraka, hizi namba zinaonekana ni namba za nje ya nchi. Lakini kwenye teknolojia, chochote kinaweza kikatokea. Inawezekana ni kweli ni namba ya nje ya nchi, lakini laini inayotumika na mtu aliyeko kwenye nchi nyingine. Lakini vile vile, inawezekana ni ujanja wa simu kutoka kwenye mtandao" alisema Kayombo.

Hata hivyo, Kayombo alisema TCRA itazuia matumizi ya namba hizo kwa sasa mpaka uchaguzi utakapokamilika hapo Oktoba 31, 2010.

Aidha, wananchi wameaswa kutojibu wala kusambaza ujumbe wanaotumiwa katika simu zao ili kuepuka uwezekano wa kukumbwa na uchunguzi unaoendelea wa kubaini chanzo cha mtandao huo.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya saa mbili ya TBC, tarehe 11 Oktoba 2010.
 
mbona message center inaonyesha namba ni ya hapa nchini? ukiingia kwenye msy center ni +255......?TCRA wamechakachuliwa
 
HAWA WAOngo MSG Center inaanza +255................................. kwanini wasiweze kutrack hii number??
 
Unategemea a public entity ambayo mkuu wake ameteuliwa na Rasi wa chama kilicho madarakani halafu utegemee atanena kinyume nao. Ingekuwa ni CCM wamechafuliwa ungekuta wanahaha usiku na mchana kumtafuta mchawi.
 
Uchunguzi wa TCRA uanzie pale Upanga mtaa wa Mindu, kwenye ofisi kuu ya kampeni za JK inayoendeshwa na Miraji Jakaya Kikwete na timu yake ya wana IT aliosoma nao Bangalore India!
 
TCRA hapo ndo mnaponichefua mimi...si mlisema miongoni mwa sababu za kusajili number ni kujua na kubaini wanaotumia simu vibaya ikiwamo hili.?sasa mnanichanganya natamani nipasue hata simu..nyoosehni maelezo sio mnaleta majibu ya kwenye kitchen party hapa..fanyeni uchunguzi toeni ripoti kamili inayoeleweka
 
Tamko la TCRA kuhusu ujumbe wa simu unaowachafua baadhi ya wagombea wa Uraisi 2010

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA, imekiri kupata taarifa za kuwepo kwa ujumbe unaosambazwa kupitia simu za kiganjani ambao umekuwa ukiwahamasisha wananchi kutokuwachagua baadhi ya wagombea wa nafasi ya Uraisi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 Oktoba 2010.

Akihojiwa na TBC, Naibu Mkurugenzi wa TCRA, Richard Kayombo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha namba hizo huku akitoa rai kwa Wananchi kutokuzijibu au kusambaza ujumbe huo.

"Tumepokea malalamiko mengi tu, na ujumbe unakuja kwenye namba ambazo 03588108226 na mwingine kwenye namba 03588976578. Kwa mwelekeo wa haraka haraka, hizi namba zinaonekana ni namba za nje ya nchi. Lakini kwenye teknolojia, chochote kinaweza kikatokea. Inawezekana ni kweli ni namba ya nje ya nchi, lakini laini inayotumika na mtu aliyeko kwenye nchi nyingine. Lakini vile vile, inawezekana ni ujanja wa simu kutoka kwenye mtandao" alisema Kayombo.

Hata hivyo, Kayombo alisema TCRA itazuia matumizi ya namba hizo kwa sasa mpaka uchaguzi utakapokamilika hapo Oktoba 31, 2010.

Aidha, wananchi wameaswa kutojibu wala kusambaza ujumbe wanaotumiwa katika simu zao ili kuepuka uwezekano wa kukumbwa na uchunguzi unaoendelea wa kubaini chanzo cha mtandao huo.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya saa mbili ya TBC, tarehe 11 Oktoba 2010.

Hizo namba ni za hapa hapa Tanzania.

Zimefanyiwa 'ciphering' na wahuni wa Kihindi
 
TCRA wanao uwezo wa kumjua anayetuma huo ujumbe kwa sababu anatuma kutokea hapahapa nchini kutokana na msg center inavyojionyesha inaanza na +255.
 
jibu la kisiasa kutoka kwa watalaam wa technology!!!!! yaani tunaelekea kubaya sana kama tutaruhusu siasa iingilie professional zetu. Itafika sehemu hata madaktari, engineers, accountants watatoa opinion za ki-professional kwa influence ya wanasiasa. Hivi amekosekana mtu anayeweza kusimamia ukweli kulingana na taaluma yake. Kuwagundua hawa jamaa wanaotuma hii sms ni kazi ndogo sana lakini jamaa anadai eti @#$@$@$%#@
 
Tamko la TCRA kuhusu ujumbe wa simu unaowachafua baadhi ya wagombea wa Uraisi 2010

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA, imekiri kupata taarifa za kuwepo kwa ujumbe unaosambazwa kupitia simu za kiganjani ambao umekuwa ukiwahamasisha wananchi kutokuwachagua baadhi ya wagombea wa nafasi ya Uraisi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 Oktoba 2010.

Akihojiwa na TBC, Naibu Mkurugenzi wa TCRA, Richard Kayombo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha namba hizo huku akitoa rai kwa Wananchi kutokuzijibu au kusambaza ujumbe huo.

"Tumepokea malalamiko mengi tu, na ujumbe unakuja kwenye namba ambazo 03588108226 na mwingine kwenye namba 03588976578. Kwa mwelekeo wa haraka haraka, hizi namba zinaonekana ni namba za nje ya nchi. Lakini kwenye teknolojia, chochote kinaweza kikatokea. Inawezekana ni kweli ni namba ya nje ya nchi, lakini laini inayotumika na mtu aliyeko kwenye nchi nyingine. Lakini vile vile, inawezekana ni ujanja wa simu kutoka kwenye mtandao" alisema Kayombo.

Hata hivyo, Kayombo alisema TCRA itazuia matumizi ya namba hizo kwa sasa mpaka uchaguzi utakapokamilika hapo Oktoba 31, 2010.

Aidha, wananchi wameaswa kutojibu wala kusambaza ujumbe wanaotumiwa katika simu zao ili kuepuka uwezekano wa kukumbwa na uchunguzi unaoendelea wa kubaini chanzo cha mtandao huo.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya saa mbili ya TBC, tarehe 11 Oktoba 2010.

Ukweli ni kwamba TCRA wanauwezo wa kuchambua kitecknologia na kutujulisha hii issue ilivyo. mimi nilipata hizo sms mara mbili.
1. +3588108226
2. +3588976578
nilijaribu usiku huo huo kuzipiga bila mafanikio, nikaomba mtandao wangu wa zain wanisaidie kunielewesha, lakini hawajanijibu.

laniki Jani nikapokea ujumbe mwingine toka namba ya hapa hapa nchini ya Tigo nilipojaribu kuipiga haikwenda wala haipo. ujumbe huu ulitoka CHADEMA namba waliyotumia ni:
1. +255719780033

TCRA tusaidieni acheni mzaha.
 
Uchunguzi wa TCRA uanzie pale Upanga mtaa wa Mindu, kwenye ofisi kuu ya kampeni za JK inayoendeshwa na Miraji Jakaya Kikwete na timu yake ya wana IT aliosoma nao Bangalore India!

Ni Mtaa wa Undali Nyumba Na 197. Yupo sec officer mmoja aitwaye Majid Kikula pale, mtaalamu wa IT na kazi yake kubwa ni kuchakachua daftari la kura wakisaidiana na NEC. Yuko pia Maharage Chande, Edgar Masatu na mwingine aitwaye Sinyau. Wana kazi moja tu waliyopewa -- kumpa ushindi JK kwa asilimia 80%.

It angers, it enrages. BYE BYE T Tanzania peace!!!!!
 
Kwa wataalamu wa IT, si muwarushie tu mdudu hapo kwa hawa jamaa?

Wana bahati sikusoma mambo ya IT. Ningeliwalima nikiwa hapahapa Sikonge.....

Ni Mtaa wa Undali Nyumba Na 197. Yupo sec officer mmoja aitwaye Majid Kikula pale, mtaalamu wa IT na kazi yake kubwa ni kuchakachua daftari la kura wakisaidiana na NEC. Yuko pia Maharage Chande, Edgar Masatu na mwingine aitwaye Sinyau. Wana kazi moja tu waliyopewa -- kumpa ushindi JK kwa asilimia 80%.

It angers, it enrages. BYE BYE T Tanzania peace!!!!!
 
+35 doesnt exist.

However countries use the following:
+350 – Gibraltar
+351 – Portugal
+352 – Luxembourg
+353 – Ireland
+354 – Iceland
+355 – Albania
+356 – Malta
+357 – Cyprus
+358 – Finland
+359 – Bulgaria
 
Why the hell did they have us run around like monkeys to register our mobile lines?
and now they can't trace a sh**t out of it?.
With my super slow internet God knows how! I came up with Finland having area code +358.
+3 and +35 have no country, but still most Finland numbers goes +358 (area code2 or 3digits)
(phone number mostly 7digits)well i might be wrong but im far better than TCRA boss.
SO i think if TCRA take their job seriously, they can nab these stupid monkeys, just like they worked
their a** off to catch up with the great guy from zeutamu blog.
 
Ni weekendi iliyopita, watanzania wengi sana walitumiwa jumbe za simu kuwa mgombea mmoja wa chama cha siasa atamwaga damu.
Mimi binafsi nilikuwa suijasikia kauli ya mwanasiasa huyo na hata kama tungesikia sisi siyo mambumbumbu kutochagua nani anatufaa.

Lakini cah kushangaza ni pale mamlaka husika zilipojifanya kutojua kabisa na hata kutofanya uchunguzi kidogo to eti code no +3.... ni yawapi wakati ni Finland. lakini pia walisema kuwa watawauliza makampuni ya simu wakati wakijua kabisa kuwa makampuni hayo hayana code hizo, na kwa ujumbe ule hakuna ambaye angekubali.

Lakiini sasa jana jioni CCM wametuma jumbe zenye kushabihiana na zile japo tofauti ni wamesema tusicahgue wapinzani.

Kwanza wana JF kuna watu wamepata hizi?
Na hatuna sababu ya kuamini kuwa waliotuma ni hao hao CCM kwa kutumia mtandao?? maana mbaya wa CHADEMA kwa sasa ni CCM peke yake na hakuna mwingine!!

Sasa kama umegombana na mtu, halafu ukadhurika, Je mtuhumiwa wa kwanza si mbaya wako!?

1. Kwanza CCM tunawashauri, kama wapiga kura wamechoka basi wasubirini tu maana kama ni amani walinzi ni wananchi na siyo chama ,
2. Chama hiki kinafahamika na mazuri yaliyofanyika yanajulikana, lakini na uchovu wake unaonekana!
3.Chama kiache kabisa kuwapotosha watu kwa hoja zisizokuwa na maana na za uwongo mkubwa.
4. Chama kiombe tu kura kwa watu kistaarabu bila ya kumhofia mtu na kumtafutia hoja ambazo hata yeye mwenyewe hajawahi kuziota.
5. CCM waachie wapiga kura waamue nani wa kuwatumikia siyo lazima wao tu.
 
Back
Top Bottom