TAMISEMI itusaidie Walimu tuliopandishwa Madaraja Halmashauri ya Moshi tupewe Barua za Uthibitisho

Aug 31, 2022
54
99
Naomba kufikisha kero yangu ambayo inanigusa binafsi pamoja na Watumishi wa Kada ya Ualimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi huku Mkoa wa Kilimanjaro.

Sisi Walimu ambao tulipandishwa madaraja tangu Mwaka 2021 hadi kufikia leo ninavyoweka malalamiko haya hatujapewa Barua za Uthibitishi wa kupanda Madara licha ya kuwa tumekuwa tukifuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote.

Wahusika wa suala hili ni Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) lakini hawatoi msaada wowote zaidi ya kutuzungusha tu.

Barua hizo ni muhimu sana kwetu kwasababu zinatumika katika kuwasilisha madai mbalimbali Serikalini na ni haki yetu kuwa nayo.

Tunaomba TAMISEMI itusaidie kupata barua hizi kwasababu tunaanza kupata mashaka juu ya kupata stahiki zetu.

Kawaida unapokuwa na barua hiyo ya kupandishwa ajira inakurahisishia akati unapotaka kupandishwa cheo katika ngazi inayofuata, kwa kuwa huku Serikalini Walimu huwa tunatakiwa kupandishwa cheo kila baada ya miaka mitatu, hivyo basi itakapofika mwakani inamaanisha sisi tuliopandishwa vyeo Mwaka 2021 lazima tutaingia kwenye changamoto ya kuanza kusumbuana na mamlaka.

Nakumbuka kabla ya Mwaka 2021 utaratibu uliokuwepo ilikuwa ni unapandishwa cheo kwa barua kisha mshahara unachelewa kupandishwa, baada ya malalamiko kuwa mengi ikaonekana Serikali inachelewa kupandisha mshahara licha ya barua kuwa zimefika mapema, utaratibu ukabadilika kuanzia Aprili 2021.

Kilichokuwa kinafanyika ni Walimu kupandishiwa mshahara kisha barua inakuja baadaye, hata mimi mshahara umepanda kulingana na cheo changu lakini changamoto ni hiyo barua ambayo naweza kuitumia kwenye matumizi yangu mbalimbali ya kiofisi.
 
Kwanza tsd/tsc huwa wanapitia humu ili wasome madai yenu? Kdc sio mbali na mnakofanyia kazi mnaweza kupeleka madai yenu kwenye sanduku la maoni. Naona kama mnapiga kelele, hamuogopi kupelekwa kule chini chemchem na mawala mkatumikie adhabu huko?
 
Moshi nilikuwa najua wote wafanyabiashara kumbe na walimu walioajiriwa wapo
 
Back
Top Bottom