Je, ni walimu pekee ndio watumishi wenye kero ya kuhitaji madaraja mserereko?

Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
418
630
Salam wana JF!

Kuna sintofahamu kubwa imeibuka miongoni mwa watumishi wa umma hasa wale wa kada zingine tofauti na walimu. Hii ni kutokana na namna serikali inavyoonyesha ubaguzi katika kushughulikia kero za walimu dhidi ya kero za watumishi wengine, Mfano kwa miaka miwili mfululizo sererikali imeendesha zoezi la kuwapandisha walimu madaraja kwa mserereko kufuatia mkwamo wa madaraja ya watumishi uliotokea mwaka 2016 hadi 2018, kufuatia lile zoezi gumzo la uhakiki wa watumishi chini ya serikali ya awamu ya tano.

Katika zoezi lile serikali ilisitisha masuala yote yaliyohusu maslahi ya watumishi ili kupisha zoezi hilo, na hivyo kuathiri utaratibu mzima wa kupandisha watumishi madaraja hasa wale ambao walikuwa wameshakidhi vigezo vya kupandishwa madaraja kwa miaka hiyo.

Hivyo serikali ya awamu ya sita ilikuja na mkakati wa kutibu majeraha ya watumishi walioathirika na zoezi hilo. Hata hivyo nia hii njema ya serikali imeingia doa kutokana na kuegemea katika kutatua kero za watumishi wa kundi moja la walimu tu, huku watumishi wa kada nyingine wakiachwa bila utaratibu wowote wa kupatiwa ufumbuzi wa kero zao.

Hili limejionyesha kwa zaidi ya mara moja sasa, mathalani katika mwongozo wa bajeti kwa mwaka 2022/2023, serikali iliziagiza taasisi zake na hasa mamlaka za serikali za mitaa kutenga bajeti itakayowezesha kufidia madaraja mserereko kwa watumishi ambao waliathiriwa na zoezi la uhakiki mwaka 2016 na kucheleweshwa kupanda madaja yao hadi mwaka 2018, ambapo iliagiza wapandishwe tena madaraja yao hata kama walipandishwa mwaka uliopita!

Taarifa hizi ziliwapa faraja na matumaini watumishi wengi lakini cha kushangaza agizo hilo lilitekelezwa kwa walimu tu lakini watumishi wengine wakaambiwa wasubili utaratibu mwingine! Hata hivyo wakati watumishi wa kada nyingine wakiendelea kusubili huo utaratibu mwingine, huku wakiamini kuwa labda mwaka huu itakuwa zamu ya watumishi wa kada nyingine lakini mambo yamekuwa tofauti kwani hata mwaka huu mwanzoni mwa mwezi wa Februari serikali iliunda timu iliyoweka kambi ya siku 14 mkoani Dodoma kwa ajili ya kushughulikia kero ya madaraja ya walimu ili kuwapa mserereko wale ambao madaraja yao yamekwama kwa muda mrefu, zoezi hili lilikuwa ni kwaajili ya walimu tu na si watumishi wa kada nyingine.

Jambo hili linazua sintofahamu na maswali mengi kuliko majibu, mfano watumishi wengine wanajiuliza;

  • Je ni walimu peke yao ndio watumishi wenye kero za madaraja zinahitaji kushughulikiwa na kupewa mserereko?
  • Je ni walimu peke yao ndio watumishi walioathirika na lile zoezi la uhakiki wa watumishi?
  • Je serikali ikishughulikia kero za walimu peke yao ndio itakuwa imemaliza kero kwa watumishi wote?
  • Je serikali ikishughulikia kero za walimu peke yao ndipo tutapata maendeleo tunayokusudia kuyapata kupitia nguvu kazi ya watumishi wa umma?
  • Je huu utaratibu wa kushughulikia kero za watumishi wa serikali kwa mfumo wa ubaguzi ni maagizo ya nani na kwa maslahi ya nani?
  • Je utaratibu huu una nia gani? Ni msukumo wa kisiasa au ni utaratibu wa kawaida?
  • Je vyombo vyote vinavyohusu watumishi vimeshirikishwa na vikatoa Baraka hizi kwa kuzingatia sheria zetu?
Hapana shaka sote tulikuwa mashuhuda wa namna zoezi la uhakiki wa watumishi lilivoendeshwa mawaka 2016 hadi 2018, Zoezi hili liliwagusa watumishi wa kada zote. Kuna watumishi wengi tu wa kada nyingine tangu ule mwaka 2016 hadi leo hii hawakuwahi kupandishwa madaraja yao wala kufidiwa athari hizo kwa namna yoyote ile. Lakini serikali bado imewaweka kushoto inashughulikia kero za walimu tu kanakwamba walimu pekee ndio wenye kero za madaraja ilihali kuna watumishi wa kada nyingine wana kero kubwa kuliko hata za walimu!

Ieleweke kuwa ukimya wa hawa watumishi haimaanishi kuwa hawana kero, bali ni ustaarabu na uvumilivu wao , sasa uvumilivu wa binadamu una ukomo , hivyo serikali isingoje mpaka uvumilivu wao ufikie ukomo. Ifahamike pia kuwa kwasasa serikali ilishasawazisha ule utofauti uliokuwepo miaka ya nyuma katika viwango vya mishahara kwa ngazi moja ya daraja la mshahara kati ya kada ya ualimu na kada nyingine. Hivi sasa mwalimu anayepokea mshahara wa ngazi ya daraja D kiasi cha mshahara wake ni sawa ni kada nyingine, hivyo kushughulikia kero za watumishi kwa mtindo wa kutanguliza kundi flani na kubagua watumishi wa kada nyingine ni kuzalisha chuki na matabaka miongoni mwa watumishi wake.

Na kama serikali inafanya hayo kwa msukumo wa kisiasa kutokana ukweli kuwa tunaelekea kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu na huu wa serikali za mitaa, kwa kukumbuka kuwa walimu ndio wasimamizi wa chaguzi hizo, Basi itakuwa inakosea kubagua watumishi wa kada nyingine kwani katika zoezi zima la uchaguzi mkuu sio walimu pekee yao wanaohusika kufanikisha chaguzi hizo.

Mathalani watumishi wa kada ya IT (Maofisa TEHAMA) walio wengi wamebadilishiwa miundo ya utumishi kutoka kada nyingine hivyo wengi wao wana mkwamo wa madaraja kwa muda mrefu lakini serikali haiwajali katika kutatua kero hizo , ikumbukwe kuwa maofisa TEHAMA, ndio wanaingiza na kutuma kura za uchaguzi zilizopigwa toka kwenye vituo mbalimbali vya uchaguzi na kuzituma Tume ya uchaguzi , hivyo kubagua au kupuuzia kero za watumishi wa kundi hili ni hatari mno.

Wito wangu kwa serikali , ifanyike opesheresheni kwa watumishi wote, zipitishwe formu za kujaza kwa watumishi wote wenye kero za madaraja na zichambuliwe na kushughulikiwa kwa haki, kila mtumishi anayestahili kupewa mserereko wa madaraja na apewe kwa haki bila ubaguzi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mbona hakuna mwl ata mmoja aliyepata huo mserereko na labda uanze mwaka huu

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Mwaka jana serikali ilitoa hilo agizo mwezi march na baadaye mwezi July zikapitishwa form kwa walimu waliostahili mserereko kujaza kisha zikapandishwa kushughulikiwa, kama hukufikiwa basi ni bahati mbaya na fursa imetolewa tena mwaka huu
 
Mwaka jana serikali ilitoa hilo agizo mwezi march na baadaye mwezi July zikapitishwa form kwa walimu waliostahili mserereko kujaza kisha zikapandishwa kushughulikiwa, kama hukufikiwa basi ni bahati mbaya na fursa imetolewa tena mwaka huu
Mkuu hizo fomu zilitolewa na mwaka jana mwishoni zilitoka pia ila hakuna mpka sasa aliyepandishwa mserereko

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Katika zoezi lile serikali ilisitisha masuala yote yaliyohusu maslahi ya watumishi ili kupisha zoezi hilo, na hivyo kuathiri utaratibu mzima wa kupandisha watumishi madaraja hasa wale ambao walikuwa wameshakidhi vigezo vya kupandishwa madaraja kwa miaka hiyo.
Ndiyo maajabu ya viongozi wa nchi hii wameshindwa kupandisha masaraja watumishi, wameshindwa kulipa malimbikizo yao ila chapchap wanawalipa wake wa viongozi
 
Hakuna mwalimu aliyepata daraja la mserereko mpaka leo hii labda hao walimu waendelee kusubiri kwani mwaka wa fedha haujaisha ahadi ya mh Raisi inaweza ikatekelezwa labda kabla ya mei mosi 2024
 
Hakuna mwalimu aliyepata daraja la mserereko mpaka leo hii labda hao walimu waendelee kusubiri kwani mwaka wa fedha haujaisha ahadi ya mh Raisi inaweza ikatekelezwa labda kabla ya mei mosi 2024
Ndiyo nilikua namuambia kuwa hakuna mwl aliyepata huo mserereko ila jamaa anabisha tu. Hivi ile kazi walikua wanaifanya maafisa utumishi dodom kwa siku 14 ilikua ni kazi gani mkuu?

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom