Mbunge Cherehani akutana na Walimu Shule za Msingi Ushetu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Cherehani Akutana na Walimu Shule za Msingi Ushetu

Walimu wa shule za Msingi katika Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga wametakiwa kuongeza ubunifu na jitihada katika ufundishaji ili kuongeza hali ya ufaulu wa wanafunzi kutoka daraja C hadi kufikia daraja A.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani katika kikao cha walimu wa shule 119 zote za msingi Ushetu kilichofanyika Kata ya Nyamilangano ambapo amesema, licha ya changamotono zilizopo kwa walimu lakini ni wajibu wao kuongeza ubunifu wa kufundisha wanafunzi.

Cherehani amesema, anatambua jitihada zilizofanywa na walimu hao japo kuwa zipo changamoto zinazosababisha walimu kushindwa kutimiza majukumu yao ikiwemo ubovu wa Miundombinu huku akieleza kuwa kuanzia mwaka 2021 wakati anaingia madarakani, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha zaidi ya Bilioni 1.5 kila mwaka kwaajili ya Elimu hali ambayo imepunguza kero ya ubovu wa Miundombinu Shuleni.

Aidha, amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hadija Kabojela kufuatilia na kuwachukulia hatua watendaji wa kata na vijiji wanaoshirikiana na wazazi wa wanafunzi watoro ambao baadhi yao wanashawishiwa ili watoto waache shule kwaajili ya kilimo au kuolewa.

Pia Cherehani amemuomba Mkurugenzi huyo kuwapandisha Madaraja waalimu wenye sifa ambao kwa muda mrefu wameshindwa kupanda vyeo licha ya kukidhi vigezo vya elimu na uzoefu kazini.

Mkurugenzi Kabojela amesema, suala la walimu kupanda madaraja ameanza kulifanyia kazi mara moja, ambapo Sambamba na hilo amewataka maafisa elimu na kamati ya shule husika kutembelea mara kwa mara shule zao ili kuona utendaji kazi wa Walimu na mwenendo wa wanafunzi wao kwakuwa hali hiyo itaongeza umakini na nidhamu kwa walimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji Doa Limbu ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyankende Limbu amepongeza jitihada za Walimu hao na kuwasihi wanapoingia katika kamati ya ujenzi wa shule waendelee na moyo wa Uaminifu katika usimamizi miradi mbalimbali inayoletwa shuleni kwao.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.01.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.01.jpeg
    45.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.01(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.01(1).jpeg
    52.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.02.jpeg
    56.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.02(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-08 at 15.58.02(1).jpeg
    43.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom