Nawasalimu wanachama wa jukwaa hili. Niombe kwenu ushauri kuhusu walimu waliojiendeleza wa shule za msingi na sekondari.
Kuna ndugu yangu amenisimulia kuhusu kutopandishwa cheo/daraja kwa walimu waliopanda cheo kwa mara ya mwisho mwaka 2019 na walipaswa kupanda tena mwaka huu 2023 Kwa mujibu wa Sheria na taratibu za wizara husika. Sasa wamepatwa na mshangao baada ya kuona hawajapandishwa vyeo Kwa mwaka 2023 kwasababu wamejiendeleza kielimu.
Hivyo kutakiwa kutumikia muundo waliobadilishiwa. Wakati katika sekta zingine mtumishi akisoma anabadilishiwa muundo na kupandisha cheo Kwa haraka pasipo kucheleshewa.
Swali lao ni kwamba:
1. Je, ni dhambi walimu kujiendeleza kielimu? Kama sio dhambi, kwanini wanapatiwa adhabu ya muundo unaowafanya waliojiendeleza kuwa nyuma kicheo na walimu waliokuwa na cheo kimoja ambao hawakujiendeleza?
2. Kama sio dhambi, basi kwanini walimu waliojiendeleza waachwe kupandishwa vyeo Sawa na ambao hawakujiendeleza?
Pia kama ni dhambi na ili kuepuka walimu kupoteza muda na gharama za kujisomesha, itangazwe rasmi kwamba walimu hakuna kujiendeleza. Wabaki kama walivyo na kuendelea kupanda daraja lisiloathiriwa na muundo.
Pia kuna kundi la walimu waliokumbwa na kadhia hii ambao walitumia muda wao wa jioni kujisomea. Kundi lingine ni la walimu waliopata ruhusa ya kusoma lakini mwajiri hakuwalipia gharama za masomo na kusainishwa barua ya kujilipia gharama hizo.
Pia Kuna kundi la walimu ambao baada ya kuhitimu elimu ya stashahada na shahada waliandika barua ya kuomba kubadilishiwa muundo lakini hawakujibiwa Kwa wakati hivyo wote kupewa barua za muundo 2021 baada ya miaka 5 hadi 6 tangu walipopeleka barua hizo na kutopandishwa vyeo vyao Kwa mwaka 2023.
Kundi lingine ni la wale ambao hawakupeleka kabisa lkn wakakutana na adhabu ya kubadilishiwa muundo pasipokupandishwa cheo. Na asilimia kubwa haya yamefanyika Kwa Manispaa ya Kinondoni.
Niombe wataalamu wa haya mambo kuwasaidia hawa walimu kupaza sauti ili wapate stahiki zao Sawa na sekta zingine wanaowabadilishia watumishi wao mara tu baada ya kurejea toka masomoni, maana asilimia kubwa hili swala limewaathiri kisaikolojia na kushindwa kufanya KAZI Kwa weledi kutekeleza majukumu yao ya Kila siku. Huku wakirundikiwa majumu mengi kama KPI.
Nawasilisha.