Tabia hii haifai

Nkanaga

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
653
619
Unaingia bar ukiwa mpole, mstaarabu na adabu zako zote. Tena kumbuka umetoka kwako kwa heshima kuwa baba kaenda matembezini, ofisini kwako mchana uliondoka kwa adabu zote kama boss. Hapo bar sasa, chupa ya kwanza.......ya pili.....ya tatu.....kinywaji kimekolea. Tabia ya kuanza kufanya mazoezi ya kutomasa chuchu na makalio ya huyo dada aliyekuhudumia inatoka wapi tena baba/boss? Huo ni udhalilishaji....kumbuka hiyo ni ajira kama ajira yoyote ile.
 
Bila kufanya hayo usiyoyapenda, ulevi utakua hauna maana weee vp? Raha ya pombe ni kujiachilia utakavyo.
 
Bila kufanya hayo usiyoyapenda, ulevi utakua hauna maana weee vp? Raha ya pombe ni kujiachilia utakavyo.[/QU ...hatukatai kujiachilia km usemavyo....cheza kiasi, imba, jishike kichwa, kifua...poa. Sio umtomase mhudum bila ridhaa yake...kumbuka yu dada/mchumba/mke wa mtu, hapo yupo kazini.
 
Haya huwa ni makusudi tu na ulimbuken,mbona wakiongozana na wake zao huwa hawayafanyi haya na wanakua wamelewa haswaa,hebu mccngizie pombe![/QU ....kweli mkuu wakiongozana na wake zao huwa wapole na wenye adabu km sio wale wa siku zote.
 
Huku anaimba kwa sauti kuuubwa 'wanaume tumeumbwa matesoo....matesoo kuhangaika' au taarab ya Mzee Yusuf...

mambo ya mtoto huyu mashaalah(mzee Yusuph)....ameumbwa,akaumbika...ovyoooooo!! na wao wanajidhalilisha pia!
 
Kuna mzee jirani yangu yeye akilewa lazima apige mikelele akiigiza mlio wa Mbwa abwekavyo na mziki ukicheza hukata mauno kuzidi Funza wa chooni !
 
mambo ya mtoto huyu mashaalah(mzee Yusuph)....ameumbwa,akaumbika...ovyoooooo!! na wao wanajidhalilisha pia!

Mwisho wa siku na kuibiwa vitu vyake kama wallet na simu anaibiwa ila hakomi kesho anarudia tena...kanakuwa ni ka-routine. Wala hashtuki na nyumbani anaitwa baba mwenye heshima zake..kila akirudi mke yupo kwenye kochi anapiga mbu....khaaaaa!!!
 
Mwisho wa siku na kuibiwa vitu vyake kama wallet na simu anaibiwa ila hakomi kesho anarudia tena...kanakuwa ni ka-routine. Wala hashtuki na nyumbani anaitwa baba mwenye heshima zake..kila akirudi mke yupo kwenye kochi anapiga mbu....khaaaaa!!!

Dah,ndoa zataka moyo jamani...ukikuta tena ndo hakuna mlinzi wa kumfungulia na wewe ukilala ndo gogo husikii,inabidi tu ung'ae tu macho umsubiri mfalme arudi kwake....kazi kweli kweli....hapo midharau na kejeli juu!!
 
mwenye tabia hiyo siku ajisahau aende kwenye bar za jeshi aone balaa lake,atachezea vitasa mpaka pombe zimuishe.....kule unalewa ukiwa mguu sawa otherwise utatoka hapo unatambaa ka nyoka
 
Hiyo ni tabia ya baadhi ya watu kutoka utotoni, waweza kuta kati wawili au mmoja kati ya wateja wote walioko bar muda huo, nadhani sio wote ambao wakipata kilaji wanakuwa na tabia kama hizo, vinginevyo bar zingekuwa na fujo sana.
 
Back
Top Bottom