Wanaume acheni kuwaogopa mabinti zenu waliovunja ungo, mama zao wamewashindwa. Hii dhambi mtaibeba

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,850
Ndugu zangu salaam sana.

Nagusia wababa na watoto wenu wa kike mliowaachia jukumu la malezi mama zao. moderator naombeni huu uzi utembee wenyewe msiuunganishe

TAHADHARI
HAYA MAANDIKO MATAKATIFU NA SHERIA YA NCHI JUU YA MTOTO HAZIBAGUI UPANDE WOWOTE WA JINSIA YA MTOTO NA WALA KUTOA UHALALI WOWOTE WA MZAZI KWENDA KINYUME, HIVYO KWA BINAFSI YANGU MWENYEWE NITAJIKITA KWEYE KUONGELEA WAZAZI WA KIUME NA MABINTI ZAO

1: KATIKA UKRISTO
Mithali 22:6

[6]Mlee mtoto katika njia impasayo,
Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Mithali 23:13
[13]Usimnyime mtoto wako mapigo;
Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

2: KATIKA UISLAM
Surah Luquman Ayat 17 (31:17 Quran)

“Ewe mwanangu mpendwa! Simamisha Sala, na himiza yaliyo mema na kataza maovu, na subiri kwa yale yanayokusibu. Hakika! Hizi ni baadhi ya amri muhimu zilizoamrishwa na Mwenyezi Mungu zisizo na msamaha.

Surat Al-baqarah 2: 195
Na toeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema; Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

Amesema Mtume (s.a.w.): “Yatosha kwa mtu kupata dhambi kwa kumtupa yule anayemtegemea.”

3: KISHERIA
Sheria ya Mtoto Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Na. 21 ya 2009.
Rejea. : Toleo la 2014 la tafsiri ya sheria ya mtoto sura ya 13 sehemu ya kwanza kifungu cha kwanza

Sehemu ya pili haki na ustawi wa mtoto, Wajibu na majukumu ya mzazi

a) Haki ya mtoto

9.-(1) Mtoto atakuwa na haki ya kuishi, utu, heshima, mapumziko, uhuru, huduma za afya, elimu na malazi toka kwa wazazi wake.

9: 3(b) kutoa mwongozo malezi, msaada na matunzo kwa mtoto na
kuhakikisha uhakika wa mtoto kuishi na maendeleo
“kuendelezwa”; na

(c) kuhakikisha kuwa kwa muda ambao mzazi hatakuwepo,
mtoto atapata malezi toka kwa mtu anayefaa,
isipokuwa tu pale ambapo mzazi amekabidhi haki na wajibu huo kwa
mtu mwingine kulingana na sheria au kwa taratibu za kimila.

Kwa kuzingatia utangulizi hapo juu
kumekua na mazoea kama wanavyodai baazi ya wazee wetu kwamba ni nature mara nyingi mtoto wa kike utakuta anakua sana upande wa baba yake na mtoto wa kiume anakua sana upande wa mama yake. Japo mtoto wakiume akifika umri flani katika malezi na makatazo mazito mazito utakuta baba akibase sana kwa mtoto wa kiume kwa lengo zuri la kumkaza kitabia, kumnyoosha kama rula na kumuwajibisha kimajukumu ipasavyo asije kuwa mwanaume laini laini na mwenye kuiga tabia za dada zake pamoja na hulka za kike kike huku akiwasahau watoto wake wa kike na kujisemea ni jukumu la mama yake kuongea nao

Ndugu zangu haya yote yanatokana wanaume kwa uoga wa wivu, fitina na makelele ya wake zao hasa pale binti wanapo vunja ungo na kuendelea kuwaganda baba zao. Wake / mama zao wamekua wakihisi baba anataka kula kuku na mayai yake hasa pale anapo muona binti yake kaanza kuwa na mashepu mazuri mazuri pamoja na chuchu saa sita na bado yupo karibu sana na baba yake. Wanaume wengi ili kuepuka kadhia na taswira mbaya ya mama zao wamekua wakijitoa polepole na kuanza kukaa mbali na watoto wao wa kike huku wakiwaachia wa mama watoto wa kike na kujisahau kwamba kama wazazi wakiume anapaswa kuwanyoosha binti zake kwa ukaribu zaidi ili waje kuwa wake wema, mama bora na uwa zuri la baadae huko waendako, kwenye familia na hata katika jamii.

Bali wazazi wakiume wengi wamewaachia wa mama jukumu la kuonge na watoto wao wa kike, kuwafundisha adabu na kuwakanda mabinti pale wanapo vunja ungo jambo ambalo wa mama limewashinda maana binti anapo balehe nakuvunja uongo mara nyingi sana anajiona sasa na yeye yupo sawa na mama yake na muda mwingine utaona anakua anamtunishia mama yake matritri huku akimtingishia materco, kiburi pamoja nakutomsikiliza mama yake kile kizuri anacho fundishwa. Utakuta binti anakatazwa na mama yake asifanye hichi ni kibaya au asivae hivi, asiwe na marafiki hawa, asiende kweye nyumba za wanaume ila binti hasikii kabisa na wala hamsikilizi mama yake kwa chochote kwasababu baba amekaa kimnya tuu huongei chochote hivyo wa/mtoto wake wa kike wanaona kutokuongea kwako na kumkanya wewe kama baba yake labda yupo sahihi ni mama tu anamwonea.

Wanaume hii tabia ya kuwanyamazia na kuwaogopa hawa mabinti zenu wanapovunja ungo kisa tuu kuepuka kadhia na makelele ya mama zao ndiyo iliyopelekea sana mabinti wengi kuharibikiwa. Mama zao wameshindwa kuwakanda na sasa wameona tu acha liwalo na liwe na wanaume wakibakia kuwarushia lawama wake/ mama wa mabinti zao kwa kushindwa kuongea na watoto wao wa kike badala ya kuchukua hatua za haraka kuwanusuru hawa watoto wakike katika upotevu huu wanaouendea kwa kasi sana huku wakisukumwa na utandawazi na mabadiliko ya ukuaji

Hii dhambi ya upotevu wa mabinti wazazi wakiume jiandaeni kuibeba maana siku zote mtoto hawezi kumshinda baba yake atamshinda mama na siyo baba maana mama ni mwanamke na yeye ni chombo dhaifu kisicho na nguvu. Baba ndiye kiongozi mwenye mamlaka na utawala hawezi kumshindwa mwanae, ukiona baba umewashindwa wanao kuwanyoosha, kuwaongoza na kuwatawala jua hakika umelaaniwa

Wazazi wa kiume badilikeni ingilieni kati kuokoa hawa mabinti na siyo kuwaachia tuu mama zao
 
Wanawake wanavimba wakiona baba anatembeza bakora. Ukimwogopa mke wako akaanza kuwa msemaji mkuu wa familia ujue watoto wataharibika.

La pili ni hizi English medium sijui international. Zimeharibu watoto na kiukweli wife material na husband materials tutakuwa tunaagiza mikoani.
 
Back
Top Bottom