Heri kuishi kwenye Dari au jangwani pekee Yako kuliko kuishi na mwanamke mgomvi

bongo dili

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
12,371
24,601

MWANAMKE HAPASWI KUWA MGOMVI​

Mithali 21:9, 19;
"Ni afadhali kukaa ktk pembe ya darini, kuliko ktk nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi."

"Ni afadhali kukaa ktk nchi ya nyika, kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi."

Leo nataka tuanze mfululizo wa somo hili, lengo likiwa ni kuboresha mahusiano yetu ya uchumba hadi ndoa lkn pia mahusiano ya familia kwa maana ya mama, baba na watoto.

Ktk mahusiano ktk ngazi hizi tatu, yaani Uchumba, Ndoa (mume na mke) na Familia (baba, mama na watoto), mwanamke ana sehemu kubwa ktk kujenga mahusiano bora, kwa maana ya kuhakikisha amani, utulivu na furaha ya mahusiano yao ktk uchumba, ndoa au familia yanadumishwa.

Mara nyingi, nyumba huwa na amani, furaha na utulivu kutokana na mwanamke alivyo. Hapa sina maana kwamba kila kunapokosekana amani ni mwanamke kasababisha, hapana, wakati mwingine siyo yeye ila ni mwanaume, lkn kuendelea au kukoma kwa hali hiyo inategemeana sana tabia ya mwanamke husika.

Hata hivyo, ktk somo letu hili tutajifunza juu ya tabia mbili ambazo mwanamke akiwa nazo ni hatari zaidi kuliko mwanaume akiwa nazo; Ugomvi, na Uchokozi. Hizi ni tabia ambazo mara zote huwa haziachani, palipo na ugomvi pana uchokozi. Mgomvi siku zote ni mchokozi, na mchokozi siku zote ni mgomvi. Mgomvi anatumia uchokozi kusababisha ugomvi, yeye hajisikii raha watu wanapokuwa na amani. Lazima tu, atasababisha ugomvi.

Ugomvi ni nini? Ni hali ya kuwa na mzozo au fujo, hali ya kugombana; kuwa na ghasia, vita, migogoro, chokochoko, shari n.k.

Mgomvi ni mtu gani? Ni mtu mwenye tabia ya kugombana na watu, mshari, mchokochoko, mghasia; Kwa kifupi ni mtu mwenye tabia ya ugomvi.

Kwa hiyo basi, ugomvi ni tabia, na kama ni tabia basi huzaliwa, hukua pia hufa.

Uchokozi ni nini? Ni tabia ya kumtafuta mtu shari, au ugomvi, ugobo au ushari.

Mchokozi ni nani? Ni mtu atafutaye shari au ugomvi; ni mtu mwenye kuchochea ugomvi, mkorofi.

Uchokozi nayo ni tabia, na tabia huzaliwa, hukua pia hufa.

Kabla hatujaanza kuangalia tabia hizi mbili huzaliwaje, hukuaje, na iwapo tutataka zife, basi hufaje, na nini dalili zake, tuangalie kwa nini Biblia imesema ni bora kukaa peke yako kuliko kukaa na mwanamke mgomvi, mchokozi.

Darini:
Ni mahali pasipo na watu, ni pa upweke, hapana kitu chochote cha faida, pana joto kali, pana giza, hapana hewa ya kutosha. Huwezi kuweka kitanda ukalala, mara nyingi huwa ni pachafu na kwa sababu
hiyo pana wadudu ambao ni hatari.

Nyika:
Mahali pasipo na watu, hapana maji, hapana miti ya kivuli, jua ni kali, pana sifa za jangwa. Ni vigumu mtu kuishi Nyikani.

Nyumba pana:
Nyumba hii ina mwanga wa kutosha, hewa ya kutosha, samani za kutosha, chakula, viyoyozi, maji ya kutosha. Kwa kifupi ina kila kitu anachohitaji mwanadamu kuishi, lkn inapokuwa na mwanamke mgomvi, mchokozi pamoja na vitu vyote hivyo haifai kuishi au kukaa.

Kwa hiyo ni bora kukaa nyikani na darini pasipo na watu wala vitu unavyovihitaji bila mwanamke mgomvi, mchokozi kuliko kwenye nyumba pana yenye kila unachokihitaji na mwanamke mgomvi, mchokozi.

Hii ina maana gani? Kuliko kuoa mwanamke mgomvi, mchokozi ni bora usioe maisha yako yote. Kwa nini, kwa sababu, mtu (mwanaume) anaweza kufanikiwa ktk maisha yake iwapo ana Amani na Pili, anamwanamke nyuma yake anayemtia moyo na kumfariji. Hawezi kufanikiwa ktk ya magomvi na uchokozi na hasa kutoka kwa mtu anayempenda zaidi na ambaye ni msaada wake wa karibu ktk mambo yote yahusuyo ndoa yao na familia yao. Kwa mantiki hii, ni rahisi mwanaume kufanikiwa akiwa peke yake maadamu ana Amani kuliko akiwa ameoa mwanamke mgomvi, mchokozi.

Ni wazi kabisa kwamba, mwanamke ameumbwa kwa ajili ya mwanaume ili awe msaada kwa mwanaume huyo. Hii inamaanisha kuwa kuna mambo ambayo mwanaume hawezi kufanya akiwa peke yake, anamuhitaji mwanamke. Na moja ya jambo kubwa ambalo mwanaume anahitaji sana kwa mwanamke ni faraja na kutiwa moyo ktk mambo yote mazuri anayofanya mwanaume. Ushauri pia ni hitaji la mwanaume toka kwa mke wake.
Japokuwa ni kweli kabisa wakati mwingine mwanaume huonyesha kutohitaji ushauri wa mkewe lkn ni wazi anauhitaji sana. Na mara nyingi huufanyia kazi kwa siri anapokuja gundua alikataa wakati alikuwa anauhitaji.

Wanawake wamepewa hali fulani ktk mfumo wa fahamu zao unaowasaidia kuhisi hatari au uheri wa jambo mbeleni, na ushauri anaoutoa mara nyingi hutaweza kipawa hiki walichopewa na Mungu, japokuwa si mara zote hisia zao huwa sawasawa, na ndio maana ktk ushauri wao weka na akili zako ktk kupima mambo.

Sasa ktk mazingira haya, mwanamke mgomvi, mchokozi hawezi kuwa namna anavyotakiwa kwa mumewe, kwanza hawezi kutoa ushauri zaidi ya ugomvi na uchokozi. Kwani haujawahi kusikia mwanaume anaogopa kurudi nyumbani kwa sababu ya ukorofi wa mkewe? Hapa ndipo asilimia kubwa ya nyumba ndogo huzaliwa.

Kama vile mwanamke alivyopewa uwezo wa kushawishi, kuvumilia, na kumudu mikiki mikiki ktk mahusiono, ile nguvu ikigeuka hutumika ktk ugomvi na uchokozi.

Hakuna mtu anayezaliwa na tabia mbaya. Tabia ni matokeo ya malezi na makuzi anayopata mtu kutoka ktk mazingira anayoishi. Uchaguzi anaofanya ktk kila jambo ndio unaoumba tabia yake. Kwa kifupi tabia inaumbwa na kile unachochagua kuamini, kufanya na kutofanya ili kujiweka ktk nafasi unayodhani itakupa usalama na unafuu wa kuendesha maisha yako na ya wengine (au dhidi ya wengine). Ni namna unavyochagua kufanya ili uwe namna unayodhani itakuwezesha kuishi bila kizuizi kitakachokuzuia kuendelea kwako mbele au kufanikisha kwako mambo. Kuna tabia njema au nzuri na tabia mbaya, zote huumbwa kwa uchaguzi tunaofanya kila siku juu ya mambo yanayohusu maisha yetu.

Hata hivyo tabia huwa tabia baada ya kurudia rudia kufanya jambo fulani ulilolichagua. Tendo fulani likishakuwa mazoea hugeuka na kuwa tabia ya mtu. Kwa mfano, nilipokuwa mtoto mdogo nikisoma shule ya msingi, niliona namna wanafunzi wenzangu wanavyoishi kwa raha, walinunua kila walichokitamani lkn kwa upande wangu haikuwa hivyo kutokana na uwezo wangu. Lkn pamoja na hayo bado nilitamani niishi kama wao lkn sikujua ni kwa namna gani ningeliweza kufanya hivyo.

Siku moja nilitumwa dukani kwa baba kufuata vitu fulani. Nilifika nikamwambia muuzaji, alipokuwa kaenda kunishughulikia bahati mbaya aliacha droo ya pesa wazi. Nilipoziona nilikumbuka matamanio yangu ya kuwa na maisha kama wenzangu wengine huko shule, nilijaribiwa kuiba kwa mara ya kwanza. Nilichukua kiasi cha pesa na kukificha. Kesho yake nilipoenda shule nilitanua kama wenzangu lkn nikiwa na hofu ya kugundulika.

Nilipoona nimeweza kuishi kama wengine, licha ya kuwa na hofu ya kugundulika nilitamani kudokoa pesa tena. Nilienda tena, nikadokoa, taratibu kurudia rudia tendo hili la udokozi, nilianza kuzoea hadi ikawa tabia yangu. Hata kama nikipewa pesa bado tu nitadokoa, na kwa sababu ilifanya tabia nilianza kudokoa kila kilichokuwa mbele yangu kinachouzika ili nipate pesa.

Nilianza kuiba hata kwenye maduka mengine. Nilikuwa jasiri kufanya hivyo sasa tofauti na mwanzo kwa sababu imeisha kuwa tabia. Japokuwa nilipigwa sana kwa tabia hiyo lkn sikuweza kuiacha. Nilijitahidi nikashindwa, mpaka pale nilipokuja kuokoka, ndipo nilipofanya maamuzi ya kuacha kwa kuchagua kutoiba na badala yake kuomba. Kuiba ikawa sio tena tabia yangu ila kuomba kila ninapokuwa na uhitaji ndio ikawa tabia yangu.

Mwanzoni nilikuwa na uwezo wa kuchagua kutokuiba lkn baada ya kuwa tabia yangu siwezi kuchagua kutokuiba, nalazima kuiba tu hata kama ninacho, mpaka nilipokutana na Neema ya Mungu ndipo kwa neema yake aliniwezesha Nami nikiwa nimekusudia kuacha kabisa. Nilipokuwa tayari kuacha Neema yake iliniwezesha.

Namna hii hii ndivyo ilivyo kwa tabia ya ugomvi na uchokozi kwa mwanamke, huanza na kuchagua kwa kujua au kwa kutokujua.

Tabia sio bahati mbaya, haitokei kwa bahati mbaya, ni marudio ya tendo lile lile yanayopelekea mazoea na mazoea kujenga tabia.

Sasa tuangalie tabia ya ugomvi na uchokozi hujengwaje: Mambo yafuatayo yakitendwa kwa kurudia rudia hujenga tabia ya ugomvi na uchokozi, na ndio dalili za mtu mgomvi na mchokozi.

  1. Kutopenda suluhu (kutosamehe): Inapotokea umeumizwa kwa kufanyiwa jambo ambalo unasadiki ni baya, na aliyekukosea akaja kutafuta suluhu nawe ukachagua kutokumsamehe, iwapo tendo hili litajirudia rudia kwako na kuwa ni mazoea yako ya kutotaka suluhu basi yatakujengea tabia ya kutosamehe na kutotaka suluhu. Tabia hii upelekea wewe kuwa mtu wa kutaka ugomvi, chokochoko, shari na uchokozi. Kutotaka suluhu na kutosamehe ni dalili ya mtu mgomvi, maadamu wameishagombana anataka waendelee kuwa wagomvi, kwa hiyo atakuwa mgomvi na mchokozi.
  2. Kutunza hasira moyoni :Kama utachagua kuwa na hasira na kuitunza moyoni, basi kujirudia rudia kwa tendo hilo kutapelekea mazoea yatakayojenga tabia hiyo. Kuwa na hasira hupelekea ugomvi na uchokozi, mtu mwenye hasira ni mgomvi. Ugomvi uchochewa na hasira, hasira ni injini ya ugomvi, mtu mwenye tabia ya hasira ni mgomvi. Hasira ikiwa ni tabia yako basi ugomvi ni tabia yako.
  3. Ubishi. Ubishi unatokana na hali ya kupingana na mwingine, mtu aliyezoelea Ubishi hupinga kila kitu cha mwingine kwa kutaka kila kitu chake kipite hata kama si chema na hata kama roho yake itamsuta, yeye atabisha tu japokuwa ukweli uko wazi. Na matakwa yake au wazo lake lisipopita atazua ugomvi. Kwa hiyo mwanamke yeyote mbishi ni mgomvi na mchokozi. Msipobishana ataanzisha mada ili mbishane na hatimaye mgombane. Ubishi hujenga tabia ya ugomvi na uchokozi.
  4. Ubinafsi na choyo :Mtu mbinafsi wakati wote ni mchoyo, na kwa sababu hiyo kila anachofanya ni kwa manufaa yake, na kile wanachofanya wengine atataka wafanye kwa ajili yake. Akiona wengine wanafanikiwa atatafuta kuwa kizuizi kwao, akiona hatendewi mambo atatafuta kutaka kutendewa bila kujali wengine wanajisikiaje na bila hata kutaka kujua kwa nini hajatendewa. Na hapa ndipo ugomvi na uchokozi huanza. Mwanamke mbinafsi na mwenye choyo huwa mgomvi na mchokozi kwa sababu hutafuta kwa lazima bila kujali hali, mazingira na uwezo kutimiliziwa mahitaji yake, na ikishindikana huzua ugomvi. Choyo na Ubinafsi ni tabia za mtu mwenye tabia ya ugomvi.
  5. Kutafuta kumtawala na kutawala matendo ya mwenzi wako. Mwanamke anayetafuta kumtawala mumewe na kutawala kila tendo analofanya, ikitokea mumewe akafanya tofauti ni ugomvi. Tabia hii hujenga tabia ya ugomvi na uchokozi kwa mwanamke.
  6. Kukosa unyenyekevu na utii. Asiye mnyenyekevu na mtii kwa mumewe ni mgomvi na mchokozi. Tabia ya kutokutii na kutokunyenyekea hujenga tabia ya ugomvi na uchokozi.
  7. Kutotosheka na kutoridhika :Mtu mwenye tabia ya Kutotosheka na kutoridhika na kile anachopokea na kupata kwa mumewe atakuwa mgomvi na mchokozi. Pia kutoridhika kutapelekea manung'uniko na lawama zisizo na sababu, hali hii hupelekea ugomvi.

KWA MWANAUME, HEBU JIULIZE MASWALI YAFUATAYO
  1. Je, iwapo nitaoa mwanamke mgomvi, mchokozi nitaweza kuishi naye, au nitaweza kumbadilisha?
  2. Je, ikitokea nimeoa mwanamke mgomvi, mchokozi nifanye nini?
  3. Je, ndoa yangu inaweza kuwa na amani nikiwa nimeoa mwanamke mgomvi, mchokozi?

Mtu aliyeoa mwanamke mgomvi, mchokozi ni vigumu kuishi naye kwa sababu hawezi kumbadilisha kutoka kuwa mgomvi na kuwa mwanana, mtulivu. Japokuwa kwa uvumilivu mwingi, anaweza kuishi naye, (na hii ni mara chache sana) bado hawezi kuwa na amani mpaka Mungu ameingilia kati kwa rehema zake.

Mithali 27:15 - 17;
"Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi,
Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;
Atakaye kumzuia huyo huzuia upepo;
Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta.
Chuma hunoa chuma;
Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake."

Katika andiko hili tutaangalia mstari mmoja-mmoja ili tuelewane vizuri. Kwa jicho la ualimu nitakusaidia kuelewa. Tuanze na mstari wa 15. "Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi, ni sawasawa."

Katika mstari huu Biblia inamfananisha mwanamke mgomvi, mchokozi na matone ya mvua yasiyokoma Kutona-tona siku ya mvua nyingi. Huwezi kuzuia matone ya mvua yasidondoke, vivyo hivyo huwezi kuzuia ugomvi mbele ya mwanamke mgomvi, mchokozi. Ugomvi hauepukiki maadamu unaishi na mwanamke mgomvi, mchokozi. Maadamu kuna mwanamke mgomvi, mchokozi, ugomvi lazima utatokea tu. Haiwezekani kuwepo na kiberiti moto ukakosekana, au ukashimdwa kuwashwa. Maadamu kiberiti kipo, muda wowote mtu atakapo kuwasha moto atawasha, na ndivyo ilivyo kwa mwanamke mgomvi, mchokozi, maadamu tabia ya ugomvi na uchokozi inaishi ndani yake lazima atasababisha ugomvi. Kwa hiyo huwezi kuzuia ugomvi maadamu unaishi na mwanamke mgomvi, mchokozi kama vile usivyoweza kuzuia matone ya mvua wakati wa mvua nyingi.

Mstari wa 16; "Atakaye kumzuia huyo (yaani mwanamke mgomvi) huzuia upepo; Na mkono wake wa kuume (mtu atakaye kumzuia mwanamke mgomvi, mchokozi) hukuta mafuta."

Kama ilivyo vigumu kuzuia ugomvi halikadhalika ni vigumu kumzuia mwanamke mgomvi, mchokozi. Kama vile mtu asivyoweza kuzuia upepo, ndivyo asivyoweza kumzuia mwanamke mgomvi, mchokozi asisababishe ugomvi. Hakuna awezaye kuzuia upepo, na hakuna awezaye kumzuia mwanamke mgomvi, mchokozi. Iwapo mtu atajaribu kufanya hivyo, sehemu ya pili ya mstari wetu imesema mkono wake wa kuume mtu huyo utakuta mafuta. Hii ina maana gani? Tabia ya ugomvi na uchokozi ni kama mafuta mengi mwilini mwa mwanamke, hivyo mkono wa kuume ambao ni mkono wa nguvu hauwezi kumshika mwanamke huyo, lazima tu utateleza kwa sababu ya mafuta yale.

Kwa wanaume wote;
Mkono wa kuume unawakilisha nguvu alizonazo mtu. Sasa, naomba unielewe vizuri, mwanaume daima hatumii nguvu zake za mwili kumbadilisha mwanamke, badala yake anatumia maombi, na ubembelezi unaotokana na yeye mwenyewe kubadilika na kunyenyekea. Kama Yesu alivyofanya kwa ulimwengu wote, hakutumia nguvu kuubadilisha ulimwengu, bali alitumia UPENDO; upendo ulimfanya afanane na mwanadamu ili aweze kumtendea mema mwanadamu. Kwa hiyo kwa kuwa mwili wa mwanamke una mafuta badala ya mwanaume kutumia nguvu zake kumbadilisha mwanamke, basi anyenyekee na kutumia mikono yake kumfanyia massage mwanamke, hapo ndipo anaweza taratibu kubadili moyo na tabia ya mkewe. Ukitumia nguvu kumbadilisha au kumzuia, utateleza. Tumia MAOMBI na UPENDO.

Omba kwa Mungu, kisha mpende, na ukimpenda licha ya kuwa ni mgomvi, mchokozi bado utaifanyia mema. Upendo si hisia, Upendo ni maamuzi yanayoambatana na dhabihu ya nafsi yako kwa ajili ya mwenzi wako. Hii ni gharama, kuchagua kumuimbea na kumpenda mkeo mgomvi, mchokozi badala ya kumchukia. Na kwa njia hii ambayo inaambatana na uvumilivu mwingi utamponya mkeo na utaiponya ndoa yako. Maombi hubadilisha vitu, hali, mazingira lakini pia humbadilisha mtu. Upendo pia humbadilisha mtu. Tumia maombi kwa mambo ya kiroho kuondoa roho ya ugomvi na uchokozi kwa mkeo, lkn tumia upendo kwa mambo ya kimwili kuondoa tabia za kimwili alizonazo mkeo za ugomvi na uchokozi. Akijua unampenda atakupenda, na akikupenda, atakutendea mema.

Mstari wa 17; "Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake."

Mkeo ni rafiki yako, mumeo ni rafiki yako. Biblia inasema Chuma hunoa Chuma, haisemi Chuma hubadilisha udongo kuwa Chuma, na wala haisemi Chuma hunoa udongo. Hii ni asili ya Chuma, hunoa Chuma chenzake na haishikamani na udongo daima. Mungu alisema, "Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" Kwa kuwa adamu alikuwa ni mfano wa Chuma, Mungu alimletea Chuma chenzake ili wanoane vizuri.

Uso ni muonekano wa mtu; ni tabia ya mtu, ni utambulisho wa mtu. Kwa hiyo kwa kuwa watu huwa karibu kuna uwezekano wa kubadilishana tabia kupitia mambo mawili; MAOMBI NA UPENDO; mambo haya yakiwa yanasukumwa na mwenendo safi na wa kupendeza wa mtu kwa mwenzi wake. Kwa hiyo basi ikitokea umeoa mwanamke mgomvi, mchokozi, Mwambee, mpende, mvumilie, kuachana mwiko.

Lakini pia ni vizuri kujua kwamba ikiwa ulioa mwanamke mzuri kitabia, baada ya miaka kadhaa ya ndoa yenu akabadilika na kuwa mgomvi, mchokozi tambua ya kuwa na wewe umehusika kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo ukibadilika, atabadilika, ukimuombea, atabadilika, na ukimpenda atabadilika.

Mwisho, oa mwanamke anayefanana na wewe, ili umnoe uso wake na yeye akunoe uso wako. Jua tabia yako, kisha chunguza tabia za mwanamke unayetaka kumuoa, ukijua ni mgomvi, mchokozi, usimuoe. Ni vigumu sana kuishi naye, kuishi naye ni gharama ya dhabihu inayokuteketeza wewe kila siku, inahitaji uvumilivu mwingi na neema ya Mungu.
 
Hiki ni kitabu
Jaribu kusummarize mkuu sisi damu nyeusi ni wavivu kusoma nakala ndefu namna hii labda ingeongelea vitu kama tunda kimasihara...

Nasema uongo ndugu zangu
True hasa hizi zisizo za ngono
 
"Christian WIVES - CW - SOMO: MWANAMKE MGOMVI 🍒Kitabu cha Mithali kinatoa maelezo mengi ya baba akimuasa mwanawe wa kiume 🍒Moja ya jambo lililowekewa angalizo ni dhidi ya mwanamke mgomvi 🍒Kama ambavyo tumekuwa na majirani au jamaa wagomvi,hali kadhalika yaweza kutokea mke aliye ndani ya ndoa kuwa mgomvi “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.” ‭‭Mit‬ ‭21:9‬ ‭SUV 🍒Hili ni pendekezo la kwanza kuwa: mume asiondoke kwenye nyumba kubwa na nzuri anayoishi na mkewe mgomvi,ni heri achague kona ya dari la nyumba hiyo hiyo aishi huko “Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.” ‭‭Mit‬ ‭21:19‬ ‭SUV 🍒Ushauri wa pili kwenye chapter hii hii Mume afadhali kukaa ktk nchi ya nyika kuliko mke mkorofi sifa za mwanamke mgomvi —KIBURI na mashindano “Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.” ‭‭Mit‬ ‭13:10‬ ‭SUV —KUTORIDHIKA ie kuwa na tamaa “Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa; Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi.” ‭‭Mit‬ ‭21:26‬ ‭SUV —KULALAMIKA kwa ajili ya kila jambo( sawa na mvua isiyoisha) “Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;” ‭‭Mit‬ ‭27:15‬ ‭SUV maneno ya mwanamke mgomvi -Maneno makali kwa mumewe -Kumkumbusha mumewe madhaifu na makosa yake ya siku za nyuma -Huuliza kwa dhihaka ie nimekuambia tena na tena nk mambo ya kujirekebisha -anza kuona mambo madogo mazuri anayoyafanya king na umsifie -amua kumruhusu king awe kiongozi wa ndoa yenu(yeye ni kichwa) -epuka kumwambia mumeo maneno makali madhara ya maneno makali -Mith15:1 huchochea ghadhabu -Mith 13:3 huleta uharibifu -Mith 18:19 yanaumiza -Mith 25:10 yanaleta mtazamo mbaya faida za maneno ya upole -Mith 16:24 yanaponya mifupa -Mith 15:2 hugeuza hasira -Mith 12:25 yanaupa moyo furaha -Mith 15:4 yanaleta uhai ~Tr Esther Zakayo | Facebook"
 
Kaka huu ni waraka au mwana kina Tomaso tunapata shida mnatutesa barua hii imenishinda kusoma tupia sammary
 
Sasa unamsema WEMA SEPETU na KAJALA .
 
Kama vile ilivyo shida kwa miguu ya mzee kupanda mlima uliojaa mchanga, ndivo ilivyo kwa mume mpole kuishi na mke mwenye makelele.
 
Back
Top Bottom