Kimsingi watu wa namna hii wanapaswa kubadirika kabla ya mwaka kuisha!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Kuna watu wanakera,wanaudhi na kutia kichefuchefu mno kwenye jamii ya watu waliostaarabika.

Moja ya watu wanaokera ni wafuatao:-

1.WAPIGA MIZINGA

Hawa wao huwa wanadhani kila pesa unawatafutia wao,badilikeni

2.WAAZIMA NGUO & VIATU

Hivi dunia la leo bado mnagongea mavazi?,Unakuta mtu anakuja kukuazima mavazi ukitegemea akimaliza kufanyia shughuli zake hizo za sherehe atakurejeshea lakini anaamua kujikausha kama zake vile!,Kwakuwa watanzania wengi ni waungwana,mtu mwenye chake anaamua kupiga kimya akidhani uenda muazimaji atajiongeza arudishe lakini na yeye bila aibu anaamua kula buyu!,Hizi tabia za kijinga ziacheni huu Mwaka 2023!.

3.WAAZIMA SHELA NA SUTI

Unaweza kudhani uenda natania lakini huwezi amini hadi leo watu bado wanaazima shela na Suti!.

Kuazima si tatizo,tatizo linakuja pale unapopewa Shela ya mtu na wewe kwenda kuipunguza au kuiongeza kama ya kwako halafu shughuli inapokwisha unaicha hivyo hivyo bila kuirudisha kwenye muonekano wake kama mwanzo!,Hizi tabia za kijinga mtaziacha lini!?

Unarudisha Shela ya watu ikiwa imepoteza mng'ao wake na rangi yake ya awali utadhani ulikuwa unaogelea nalo kwenye tope!.Badilikeni acheni Ushamba na Ujinga.

4.WAAZIMA MAGARI

Unakuta mtu mnaheshimiana nae vizuri tu,anakuja kuazima gari yako na huwa wanategea sana wakiona umetoka wanamuwahi mkeo kwasababu wanajua ukiwa safari mkeo akikwambia Baba fulani mtu fulani anaomba gari yako huwezi kuchomoa!.

Mtu anachukua gari ikiwa na mafuta ya kutosha ila yeye atafanyia mambo yake huko aendako lakini bila aibu atarudisha gari ikiwa mafuta yamebaki kibaba,hivi hii tabia ya kidwanzi mtaacha lini?

Kibaya zaidi unachukua gari ya watu unaanza kuzunguka nalo mtaani na kwenye Ma-bar ili kuzongozea wanawake!.

Gari uliichukua safi lakini utalirudisha likiwa chafu bila hata kuona aibu,siku nyingine mkinyimwa magari ya watu mnaanza kutangaza ubaya kwamba fulani ana roho mbaya!.Badilikeni acheni Ujuaji.

5.WAAZIMA CHAJI ZA SIMU.

Kama kuna kitu ambacho mtu anapaswa kuwa mchoyo kukitoa ni chaja ya simu!.

Kuna mtu anaazima chaji ya simu lakini kurudisha ni matanga,wakati anaazima anajua kabisa na wewe hiyo chaja ndiyo unayoitumia lakini atajifanya kama amesahau ili tu uanze kuongea uonekane mbaya!.

Unapoazima kitu kama chaji usitake hadi ufuatwe ndipo utoe,unapoazima hakikisha simu yako ikishajaa mrudishie mwenye chaji yake,huo ndiyo ustaarabu!

Kuna wengine unakuta wanachati na kufanya mambo kadhaa kwenye simu huku chaji ikiwa kwenye soketi,hivyo kuiazima chaji yake hakikisha unairudisha kwa wakati kabla hajaanza kusonya moyoni mwake na kukuona hufai kupewa kabisa hiyo chaji!.

6.WAAZIMA MIAMVULI

Hapa najua mpo wengi ila ngoja niwatwange ili mbadirike wapuuzi nyie!.

Tunajua kabisa kwasasa mikoa mingi ni msimu wa mvua,sasa kumejengeka katabia ambako ni ka kijinga ka kuazima Miamvuli ya watu mkaondoka nayo na mvua ikiisha mnaiacha huko huko makazini na kwenye biashara zenu au na nyie kuigawa kwa watu wengine.

Hivi hii tabia mtaiacha lini,kibaya zaidi kuna mtu ukimpa mwamvuli hadi uanze kumuomba tena kwa kupigishana kelele,unakuta kauacha huko alikouacha na kila siku zinakuwa danadana tu!.

Kama ukiazima mwamvuli wa mtu hakikisha unamrejeshea baadae baada ya mvua kuisha kwasababu aliununua kwa ajili ya kujikinga na mvua,usitake aliyekuazimisha akakuona mtu usiyemstaarabu!.

Kuna wengine wanakwambia mvua ikiisha mwamvuli unakuwa mzigo mzito kuubeba,acheni huu ujinga,hakikisheni mnapoazima kitu cha mtu mnarudisha!.

7.WAAZIMA MAFYEKEO/KWANJA.

Hivi vitu huwezi amini vimewakosanisha majirani sehemu tofauti tofauti hadi leo hawaongeleshani!

Kwanini kama unajua wewe si mtunzaji uazime kwanja/Fyekeo la mwenzako?,Unapoazima kitu cha mtu hakikisha unakitunza na ukimaliza matumizi nacho hakikisha unamrejeshea mwenye nacho!.

Kama unajua si mtunzaji basi usiazime cha mtu kwasababu utasababisha uonekane si muungwana!.

8.WAAZIMA VYOMBO VYA KUPIKIA & KUPAKULIA

Kuna ambao unakuta inapotokea kwake sherehe anakuja kuazima kwako vyombo vya kupikia na kupakulia lakini sherehe ikiisha anarudisha vyombo vikiwa vimepungua,eidha utakuta sahani amevuja au amepoteza visu au vijiko!.

Kama unajua huwezi kutunza vitu ulivyo azima kwanini uazime?

Hakikisha vitu ulivyoazima unaviorodhesha kwenye daftari ili vikiharibika au kupotea unamnunulia vitu vyake aliyekuazimisha ili muendelee kuwa na ushirikiano kama awali,lakini tofauti na hapo utaonekana si mstaarabu na hata siku nyingine ukienda kuazima huwezi kupewa!

9.WAAZIMA MIZIKI & TV

Hawa wao huwa wanakuja kistaarabu sana,lakini ukishawapa na wakishamaliza sherehe zao huko unakuta wanarudisha mali yako ikiwa na mapungufu tofauti na Mwanzo,hasa TV nyingi sana unakuta zinaunguzwa na kuvunjwa,sasa unakuta unajiuliza mwaswali mwengi sana usiyopata majibu!.

Wewe unakuta umekaa na TV au Redio yako miaka zaidi ya 5 lakini ukimpa mvurugaji ndani ya masaa kadhaa tu lazima itarudi ikiwa imeungua au ikiwa imeharibika,kibaya zaidi bila hata aibu wanataka wewe ndiyo utengeneze wakati waliazima wao.

10.WAAZIMA CHUPA(MAKRETI) ZA BIA & SODA

Unamuazima mtu chupa zako au kreti la bia au soda lakini wakati wa kurudisha anarudisha zikiwa pungufu,hivi hizi tabia mtaacha lini?

Mtu ameamua kukuheshimu kakuazima kreti lake liwe la Bia au soda,wewe unatumia kwenye sherehe zako na hujali na kuthamini kile alichokupa mtu huyo,sherehe inaisha wala hujali tena unawatuma watoto wamrudishie mtu huyo kreti lake likiwa pungufu,mwenyewe akikupigia simu kukuuliza unaanza blah blah nyingi,kwanini usimnunulie ukafidia zilizopotea na kupasuka ili uendelee kuaminika?

Hivi haya mambo ya kudharau dharau mali za wenzenu mtaacha lini wakuu?

Sijajua ni lini kama taifa tutakuwa wastaarabu kwenye vitu vidogo vidogo!.

BADILIKENI!.

Siga okwamba mwana wa mai nikale ku kitebhe nitegelesye amasango ku chalo kunu!
 
Waazima chaji uwa nakupa neno kwanza ndio nakupa,, hawa ninaoshinda nao asbh mpk jioni, niliwakusanya wote ambao tunashare chaja, nikawachangisha nikanunua chaji… so tunayo ya umoja ambayo haitakiwi kutoka nje ya mlango
 
Charger ya simu.
Moja ya vitu vinakufanya usionekane smart huwa ni kutegemea charger za kuazima.

Watu wengi ambao ni very smart hawezi kosa charger wakati ana simu labda kwa dharura kubwa.

Mi vitu ambavyo siwezi safiri bila hivyo ni charger na powerbank. Kuna chagrer ya nyumbani hiyo huwa haimove na kuna charger kwenye begi ninapokuwa kwenye pilika.

Huwa ni kosa kwangu simu kutokuwa hewani.
 
Haha emu kuweni serious…
1. Ngo! ngo! Ngo!
2. Nan
1. Ww mpaji mungu fungua mlango
2. Nan bn ww
1. Depal hapa
2. Aaah kuaga serious bas mm nkajua wale wa hela ya taka na sungu sungu
1. Hamna bn! Mpaji naomba nsaidie chaja yako yangu haipeleki tangu Jana hapa sijakusanya assignment afu mwisho saa sita.....na yule lecture alivo sasa
2. Weka hapo uendelee kuchaji mm yenyewe yangu ina 68% sema toa hyo simu ndogo weka yako
1. Sasa hii simu ndogo ya nn Mpaji mungu
2. Ina kazi nyingi wewe
1. Au ndo unatumia kuwasiliana na wifi yangu
2. Wala hata sinaga hzo mbisee
1. Aweeeee navokujua ww

Inaendelea.......🤣
 
Kazii ipo mtaani.. mnaharibu watoto wa watu
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Kuna watu wanakera,wanaudhi na kutia kichefuchefu mno kwenye jamii ya watu waliostaarabika.

Moja ya watu wanaokera ni wafuatao:-

1.WAPIGA MIZINGA

Hawa wao huwa wanadhani kila pesa unawatafutia wao,badilikeni

2.WAAZIMA NGUO & VIATU

Hivi dunia la leo bado mnagongea mavazi?,Unakuta mtu anakuja kukuazima mavazi ukitegemea akimaliza kufanyia shughuli zake hizo za sherehe atakurejeshea lakini anaamua kujikausha kama zake vile!,Kwakuwa watanzania wengi ni waungwana,mtu mwenye chake anaamua kupiga kimya akidhani uenda muazimaji atajiongeza arudishe lakini na yeye bila aibu anaamua kula buyu!,Hizi tabia za kijinga ziacheni huu Mwaka 2023!.

3.WAAZIMA SHELA NA SUTI

Unaweza kudhani uenda natania lakini huwezi amini hadi leo watu bado wanaazima shela na Suti!.

Kuazima si tatizo,tatizo linakuja pale unapopewa Shela ya mtu na wewe kwenda kuipunguza au kuiongeza kama ya kwako halafu shughuli inapokwisha unaicha hivyo hivyo bila kuirudisha kwenye muonekano wake kama mwanzo!,Hizi tabia za kijinga mtaziacha lini!?

Unarudisha Shela ya watu ikiwa imepoteza mng'ao wake na rangi yake ya awali utadhani ulikuwa unaogelea nalo kwenye tope!.Badilikeni acheni Ushamba na Ujinga.

4.WAAZIMA MAGARI

Unakuta mtu mnaheshimiana nae vizuri tu,anakuja kuazima gari yako na huwa wanategea sana wakiona umetoka wanamuwahi mkeo kwasababu wanajua ukiwa safari mkeo akikwambia Baba fulani mtu fulani anaomba gari yako huwezi kuchomoa!.

Mtu anachukua gari ikiwa na mafuta ya kutosha ila yeye atafanyia mambo yake huko aendako lakini bila aibu atarudisha gari ikiwa mafuta yamebaki kibaba,hivi hii tabia ya kidwanzi mtaacha lini?

Kibaya zaidi unachukua gari ya watu unaanza kuzunguka nalo mtaani na kwenye Ma-bar ili kuzongozea wanawake!.

Gari uliichukua safi lakini utalirudisha likiwa chafu bila hata kuona aibu,siku nyingine mkinyimwa magari ya watu mnaanza kutangaza ubaya kwamba fulani ana roho mbaya!.Badilikeni acheni Ujuaji.

5.WAAZIMA CHAJI ZA SIMU.

Kama kuna kitu ambacho mtu anapaswa kuwa mchoyo kukitoa ni chaja ya simu!.

Kuna mtu anaazima chaji ya simu lakini kurudisha ni matanga,wakati anaazima anajua kabisa na wewe hiyo chaja ndiyo unayoitumia lakini atajifanya kama amesahau ili tu uanze kuongea uonekane mbaya!.

Unapoazima kitu kama chaji usitake hadi ufuatwe ndipo utoe,unapoazima hakikisha simu yako ikishajaa mrudishie mwenye chaji yake,huo ndiyo ustaarabu!

Kuna wengine unakuta wanachati na kufanya mambo kadhaa kwenye simu huku chaji ikiwa kwenye soketi,hivyo kuiazima chaji yake hakikisha unairudisha kwa wakati kabla hajaanza kusonya moyoni mwake na kukuona hufai kupewa kabisa hiyo chaji!.

6.WAAZIMA MIAMVULI

Hapa najua mpo wengi ila ngoja niwatwange ili mbadirike wapuuzi nyie!.

Tunajua kabisa kwasasa mikoa mingi ni msimu wa mvua,sasa kumejengeka katabia ambako ni ka kijinga ka kuazima Miamvuli ya watu mkaondoka nayo na mvua ikiisha mnaiacha huko huko makazini na kwenye biashara zenu au na nyie kuigawa kwa watu wengine.

Hivi hii tabia mtaiacha lini,kibaya zaidi kuna mtu ukimpa mwamvuli hadi uanze kumuomba tena kwa kupigishana kelele,unakuta kauacha huko alikouacha na kila siku zinakuwa danadana tu!.

Kama ukiazima mwamvuli wa mtu hakikisha unamrejeshea baadae baada ya mvua kuisha kwasababu aliununua kwa ajili ya kujikinga na mvua,usitake aliyekuazimisha akakuona mtu usiyemstaarabu!.

Kuna wengine wanakwambia mvua ikiisha mwamvuli unakuwa mzigo mzito kuubeba,acheni huu ujinga,hakikisheni mnapoazima kitu cha mtu mnarudisha!.

7.WAAZIMA MAFYEKEO/KWANJA.

Hivi vitu huwezi amini vimewakosanisha majirani sehemu tofauti tofauti hadi leo hawaongeleshani!

Kwanini kama unajua wewe si mtunzaji uazime kwanja/Fyekeo la mwenzako?,Unapoazima kitu cha mtu hakikisha unakitunza na ukimaliza matumizi nacho hakikisha unamrejeshea mwenye nacho!.

Kama unajua si mtunzaji basi usiazime cha mtu kwasababu utasababisha uonekane si muungwana!.

8.WAAZIMA VYOMBO VYA KUPIKIA & KUPAKULIA

Kuna ambao unakuta inapotokea kwake sherehe anakuja kuazima kwako vyombo vya kupikia na kupakulia lakini sherehe ikiisha anarudisha vyombo vikiwa vimepungua,eidha utakuta sahani amevuja au amepoteza visu au vijiko!.

Kama unajua huwezi kutunza vitu ulivyo azima kwanini uazime?

Hakikisha vitu ulivyoazima unaviorodhesha kwenye daftari ili vikiharibika au kupotea unamnunulia vitu vyake aliyekuazimisha ili muendelee kuwa na ushirikiano kama awali,lakini tofauti na hapo utaonekana si mstaarabu na hata siku nyingine ukienda kuazima huwezi kupewa!

9.WAAZIMA MIZIKI & TV

Hawa wao huwa wanakuja kistaarabu sana,lakini ukishawapa na wakishamaliza sherehe zao huko unakuta wanarudisha mali yako ikiwa na mapungufu tofauti na Mwanzo,hasa TV nyingi sana unakuta zinaunguzwa na kuvunjwa,sasa unakuta unajiuliza mwaswali mwengi sana usiyopata majibu!.

Wewe unakuta umekaa na TV au Redio yako miaka zaidi ya 5 lakini ukimpa mvurugaji ndani ya masaa kadhaa tu lazima itarudi ikiwa imeungua au ikiwa imeharibika,kibaya zaidi bila hata aibu wanataka wewe ndiyo utengeneze wakati waliazima wao.

10.WAAZIMA CHUPA(MAKRETI) ZA BIA & SODA

Unamuazima mtu chupa zako au kreti la bia au soda lakini wakati wa kurudisha anarudisha zikiwa pungufu,hivi hizi tabia mtaacha lini?

Mtu ameamua kukuheshimu kakuazima kreti lake liwe la Bia au soda,wewe unatumia kwenye sherehe zako na hujali na kuthamini kile alichokupa mtu huyo,sherehe inaisha wala hujali tena unawatuma watoto wamrudishie mtu huyo kreti lake likiwa pungufu,mwenyewe akikupigia simu kukuuliza unaanza blah blah nyingi,kwanini usimnunulie ukafidia zilizopotea na kupasuka ili uendelee kuaminika?

Hivi haya mambo ya kudharau dharau mali za wenzenu mtaacha lini wakuu?

Sijajua ni lini kama taifa tutakuwa wastaarabu kwenye vitu vidogo vidogo!.

BADILIKENI!.

Siga okwamba mwana wa mai nikale ku kitebhe nitegelesye amasango ku chalo kunu!
TAFUTA HELA WEWE PIMBI! MBONA SISI WA MASAKI HATUNA MAMBO YA KUAZIMANA
 
Back
Top Bottom