Taarifa kwa Vyombo vya habari kutoka IKULU juu ya Katiba Mpya

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI

KamaKatiba Inayopendekezwa ni mbaya, hiyo nzuri ikoje?
auliza Rais Kikwete


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikweteamewashangaa watu wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya,akiuliza kuwa kama Katiba hiyo ni mbaya basi hiyo nzuri ikoje?

Aidha,Rais Kikwete amesema kuwa Katiba inayojali makundi yote ndani yajamii, kama ilivyo Katiba Inayopendekezwa, kamwe haiwezi kuwa Katibambaya.

Rais Kikwete ameyasema hayo nyakati tofauti leo, Ijumaa, Oktoba 10, 2014,wakati alipozungumza na wananchi katika maeneo mbali mbali ya Mkoa waMwanza, ambako anafanya ziara ya siku tatu ya kikazi kukagua nakuzindua miradi ya maendeleo.

Akizungumza na mamia kwa mamia ya wananchi mjini Kisesa ambako ameweka jiwe lamsingi la ujenzi kwa kiwango cha lami na Barabara ya Usagara-Kisesa,Rais Kikwete amewataka wananchi kuwapuuza watu wachache wanaodai kuwaKatiba Inayopendekezwa ni mbaya na badala yake wajiandae kuipigiakura ya kuikubali wakati ukiwadia.

"Sijui katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani ya jamiikama hii Katiba Inayopendekezwa. Hakuna aliyeachwa – wavuvi wamo,wajane wamo, wafanyabiashara ndogo ndogo wamo, akinamama lishe wamo,wakulima wamo, wafugaji wamo….kila mtu yumo. Akinamama ndio usisemekabisa wao wamepata hata asimilia 50 kwa 50 ndani ya Bunge."

Ameongeza Rais Kikwete: "Hivi katiba mbaya inakuwa kama inayopendekezwa nakama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa hivi nzuri ikoje?

Rais Kikwete amewambia wananchi: "Watakuja watu kuwashawishi kuwa KatibaInayopendekezwa ni mbaya, wasikilizeni lakini tumieni akili yetu,kama ile hadithi ya mbayuwayu. Jiandaeni tu kupiga kura na kuungamkono Katiba Inayopendekezwa kwa sababu hii ni Katiba nzuri sana."

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

10 Oktoba, 2014
 
Sasa hii press release inaongelea nn? Nahisi kama nimetoka kapa, au inaendelea toleo lijalo?
 
Katiba inayojalimakundi yaliyosahauliwa na kupuuzwa madai yao ni ile iliyowakumbuka wananchi zaidi ya milioni 20 wa dini ya kiislam wanaodai mahakama ya kadhi kwa maridhiano bila kusubiri shari.

Watu wanapokea maoni ya wasanii wa kinengua viuno kwenye majukwaa halafu wanapuuza maoni ya wanazuoni wa kiislam wanaozungumzia hoja ya mahakama ya kadhi.

Hii ni katiba kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
 
hata aibu hana,anawezaje kusimama mbele za watu na kupigia chapuo katiba pendekezwa ilopatikana kitatanisha,rais boga
 
Kikwete hajielewa, na nadhani hakustahili nafasi kubwa kama hiyo. Anaongea kama Diwani, si katika kiwango cha nafasi ya Urais.
Ni huyu huyu unayedai hajielewi ambaye viongozi wa kikundi kinachojiita UKAWA wanakimbilia kwake ili awasaidie katika harakati zao za kisiasa.

Kama hiyo ndiyo hoja yako, basi hawa viongozi wa UKAWA watakuwa hawajielewi zaidi ya Rais Kikwete!.
 
We want a level playing field. Sasa wao wameanza zamani kwa Kinana kuzunguka nchi nzima na yeye Dhaifu ameanza sasa lakini UKAWA wakitaka kufanya mikutano ccm wanawatumia polisi wao kukataza mikutano!! Kama mnajiamini waacheni UKAWA nao wawaelimishe wananchi kuhusu udhalimu wenu!
 
Katiba tuliyonayo sasa imejaa haki za binadamu lakini tunashuhudia watu hawazipati. Kutamka makundi katika katiba hakuifanyi I we bora ikiwa tu hakuna uhakikisho wa kupata haki makundi husika. Kuna vifungu tayari katika katiba vinazuia kudai haki Hizo za makundi! Je uzuri wake ni up?
 
Kurugenzi ya mawasiliano ikulu kumbe nao wahuni, hiyo letter head ya Ikulu kweli? Ama Ikulu ya Kikwete imekuwa uchocholo.
 
Hii kweli ni taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu? Basi kuna tatizo kubwa sana.
 
Back
Top Bottom