Ikulu Zanzibar: Taarifa kwa vyombo vya habari

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote Zanzibar kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa suala la Ulinzi na usalama katika maeneo yao Kwani kuna baadhi ya maeneo kuna matukio mengi ya uvunjifu wa amani.

Dk. Mwinyi amewataka viongozi hao kuyashughulikia matukio hayo kwa nguvu kubwa na kuwepo operesheni maalum ya kudhibiti hali ya uvunjifu wa amani hasa maeneo ya Nungwi na Paje.

Rais Mhe. Dk. Mwinyi ametoa Kauli hiyo leo baada ya kuwaapisha Wakuu wawili wa Mikoa na Wakuu watatu wa Wilaya hafla iliyofanyika Ikulu - Zanzibar.

Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe wanatatua kero za wananchi Kwani Wananchi wengi wanapeleka malalamiko yao Ikulu badala ya kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya akitaja Kero kubwa ni za Ardhi.

Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya wametakiwa kutatua na kutenda haki kwa Kero zinazowahusu wawekezaji na wawe sehemu ya utatuzi wa Kero zao. Aidha Dk. Mwinyi amewataka Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kusimamia Halmashauri na Manispaaa zilizo katika maeneo yao na hasa kusimamia suala la usafi wa mazingira na Changamoto za ujenzi wa nyumba ovyo suala linaloanzia ngazi ya Shehia.

Halikadhalika, Rais Dk. Mwinyi akawasihi viongozi wote kwa kwa ujumla kufanya kazi kwa pamoja na kuelewana kwani kuna baadhi yao hata hawazungumzi suala linalodhorotesha utendaji kazi serikalini na akaonya iwapo hapana budi atachukua hatua.

Viongozi walioapishwa leo na Mhe. Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi ni Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Unguja, Mhe. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja.

Wengine ni Mhe. Sadifa Juma Khamis kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati, Unguja, Mhe. Othman Ali Maulid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini, Unguja, Mhe. Cassian Gallos Nyimbo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Unguja

Uteuzi huo umeanza tarehe 16 Novemba, 2023.

IMG-20231120-WA0018.jpg
 
Back
Top Bottom