Dkt. Slaa: Nchi yetu inaongozwa kishamba, pamoja na IGA sasa tutadai pia Katiba Mpya ya wananchi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Fuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa waandishi wa habari unaoendelea muda huu ambapo Dkt. Slaa, Mwabukusi na Mbatia wanazungumza.


Wakili Mwabukusi anazungumza
Juzi walitaka kubadilisha makubaliano ya Mkataba huu kati ya Taifa letu na kikampuni ambacho sidhani hata kama BRELA kipo.

Sisi hatushughuliki na Dubai Emirates wala DPW, sisi tunashughulika na Bandari yetu. Wengi wanasema mkataba ule wa kimataifa hivyo una defeat sheria za ndani. Kwa makusudi hawataki kusoma Geneva law of treaty ambayo inafafanua kuwa kwenye hali kama hizi mkataba huu hauwezi kuzidi sovereignty ya nchi. Walitusingizia uhaini wakatutoa, tunaanzia hapo tulipoishia.

Mwabukusi.jpg

Wakili Mwabukusi
Hili tunamkabidhi Mungu upande wa kushughulika na yaliyo nje ya mipaka ya binadamu, lakini yale ya kisheria hatumuachii yeye, tutakabiliana nao.

Kama walidhani wananitisha walifanya kosa kubwa sana, mimi sitishwi. Kama unafuata sheria za nchi nitakuheshimu, kama unatumia cheo sitakuheshimu. Kama nimekosea niadhibu kisheria pasipo kutunga makosa.

Sijui hata kutumia manati, ugaidi nitaifanya nini? Hii IGA nitaipinga, na Mungu atatupa uhai hadi tutakaposherekeka kufutwa kwa IGA. Hatutaruhusu laana hii katika malango ya nchi. Hoja za Bandari hazihitaji risasi, Serikali itujibu kwa hoja.

Sisi tukivunja mkataba watakamata ndege zetu, wao wakivunja mkataba wanaondoka bure. Wenzetu wakatoliki walitoa waraka, tumekubaliana wakati RC wakisoma waraka huu na kujuzana, tuipe Serikali na Bunge siku 30 ili lishughulikiwe.

Wastaafu kama hawawezi kuishauri kwa haki Serikali wakae kimya. Tumetoa siku 30, tunaanza kufanya kazi kubwa ya kufika mikoani, tutakuwa na mikutano 3 kwenye mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya kueleza madhara ya huu mkataba.

Polisi kama wanapenda sana siasa wastaafu, sisi tunazungumza hoja za kisiasa wao wanataka kutuua. Vyombo vya usalama vimsaidie Rais kumuonesha madhira ya mkataba huu, wakae nae kitaalamu wampitishe. Kama wao wanashindwa wasitumie Bunduki, watuite tuzungumze.

Baada ya siku 30 tutaitisha maandamano ya amani na sitojificha, hatutaacha kuandamana hadi IGA iondoke, isipoondoka tutaandamana milele, tutawataarifu Polisi.

IGP Wambura, kama una hoja niite, kaa na wataalamu wako nije tuzungumze, usitume vijana kutukamata usiku kutuweka korokoroni, ukiniita nitafika ili kama ni uchochezi nikuchongee wewe. Hatutaki cheo wala upendeleo wowote.

Quran na Biblia zote zinakemea ufisadi, tukemee mafisadi yote.

Dkt. Slaa anazungumza
Tunawashukuru kwa jitihada za kutotoa japo sisi tulitamani tuendelee kubaki.

Kama uhaini huwa unafanywa kwa namna hii basi tutaufanya sana. Yesu Kristu aliuawa, mimi ni nani nipelekeni tu mnakotaka kama ni kukata shingo nikateni.

Hatuogopi kifo, ilimradi tunajua tunasimamia nini. Hakuna kifo chenye heshima kama kufia ukisimamia maslahi ya nchi yako.
H.E_Dr_Willibrod_Peter_Slaa (1).jpg

Dkt. Willibroad Slaa
Serikali, wananchi, vyama vya siasa hawaelewi kuhusu katiba. Wakizungumza wanazungumzia uchaguzi. Juzi kuna taasisi moja imezungumzia tume huru, watu wanakufa wewe unazungumzia Tume ya Uchaguzi?

Kinachotokea katika nchi yetu ni kichekesho, katiba ya 1977 iliandikwa kama appendix ya CCM, kitu fulani kinachoning'ingia, kitu kisicho na umuhimu. Wananchi hawajawahi kupewa nafasi, hawajawahi kutengeneza katiba yao.

Bunge la CCM lilijigeuza wakawa Bunge maalumu kutengeneza Katiba, tafuta mwaka 1977 CCM walikuwa wangapi? Ni lini mwajiriwa anaandaa mkataba wake mwenyewe? Serikali tunaiajiri sisi, Rais tunamwajiri sisi. Kinachofanyika ni kama Rais anatengeneza mkataba wenye masharti anayotaka yeye.

Katiba hii ya sasa ilijadiliwa kwa saa 2 tu, kama sikosei wabunge walioongewa walikuwa 8 au 9. Tumeona mchezo wa 1977 unataka kujirudia tena kwa hali mbaya zaidi.

Katiba haianzishwi kwa mdomo tu wa Rais, huanzishwa kwa muswada. nchi yetu inaongozwa kishamba. Sasa nawauliza, hivi tunaakili au tumegeuzwa kuwa nyani (kufundishwa umuhimu wa katiba kwa miaka 3). Mimi kwa akili yangu ya kawaida watanata kutupiga.

Bunge limegeuka kuwa sehemu ya Serikali badala ya kusimama upande wa wananchi na tutasimama na vyama vinayotetea wananchi. Katiba inatoa tafsiri ya mali za taifa na zinalindwa vipi.

Sisi tumesema pamoja na IGA, katiba ni ajenda yetu ya pili na tunamuambia Rais ndani ya siku 30 tulizotoa tuone mwelekeo wa katiba mpya ya wananchi, katiba ni mali ya wananchi.

Unapomsikia Rais anasema anamuweka Waziri kwenye wizara fulani halafu anamwambia wewe unakifua na kumuandaa kwa mambo yanayokuja (uchaguzi) unakuwa huoni nia njema. Halafu unamsikia Rais anasema atatoa bilioni 125 kwa polisi kwa ajili ya jukumu hiko, kwani Kazi ya polisi kwenye uchaguzi ni nini?

Mdude Nyagali anazungumza
Wakina nani walistahili kupewa kesi ya uhaini na kunyongwa kati yetu sisi tunaopigania maslahi na wale walioenda Dubai? Nataka nizungumze hapa kwanini tunataka maandamano ambayo tunaona kuwa ndio solution.

Tena mkome kutupa kesi za uhaini, sisi sio waoga. Tulionesha ustaarabu, tulipopiga kelele tukaenda mahakamani, hukumu mliiona, majaji wakaniri kwamba mkataba ni mbovu lakini wamefungwa mikono.

mdude-chadema.jpeg

Mdude Nyagali
Kama mahakama yenyewe imekiri ubovu wa mkataba lakini wamefungwa mikono, manataka sisi tufanye nini kunusuru rasilimali zetu? Mkataba huu unaandaa watanzania kuwa manamba, wao ndo wataamua nani awe Rais wa nchi hii, tutakuwa tumeolewa sisi.

Nchi hii itakuwa koloni, halafu mimi kijana nikae kimya? Nataka nitoe tamko rasmi Serikali ifute huu mkataba, na wakati tunasubiri siku 30 tunaenda kwenye mikutano ya hadhara kuandaa wananchi kwa maandamano ya nchi nzima.

Tumesema kwamba maandamano haya yatatokea nchi nzima, hayajawahi kutokea nchi tangu uhuru, yataibadilisha nchi hii.

IGP wambura, mimi level ya kutishwa na polisi imeshapita miaka 10 iliyopita. Namwambia anayemtua kwamba aje hadharani kujibu hoja zetu, kama ameshindwa kuwajibika urais sio uchifu anaweza kujiuzulu aje mwingine. Polisi nawajua kama ninavyojua sehemu zangu za siri.

James Mbatia anazungumza
Mambo yapo wazi, dunia ya leo ni kusikilizana, meza ya mazungumzo, tukubaliane kwa pamoja. Mahali popote kwenye migogoro, ukishindwa ku manage inaleta matatizo.

Tukubaliana turudi tukae tuzungumze, suala la DPW ni janga la Taifa, suala la Katiba Mpya ni janga la taifa. Sisi watanzania tuje kwenye meza ya Mazungumzo.

JAMES MBATIA.jpg

James Mbatia
Ninamuomba Rais na kumshauri asikilize kilio cha watanzania, asikiliwe watanzania wanavyoipenda na kuililia nchi yao.

Sisi wote ni watanzania, ni watoto wa mama Tanzania. Hatuna haja ya kutumia vibaya vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Fuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa waandishi wa habari unaoendelea muda huu ambapo Dkt. Slaa, Mwabukusi na Mbatia wanazungumza.


Wakili Mwabukusi anazungumza
Juzi walitaka kubadilisha makubaliano ya Mkataba huu kati ya Taifa letu na kikampuni ambacho sidhani hata kama BRELA kipo.

Sisi hatushughuliki na Dubai Emirates wala DPW, sisi tunashughulika na Bandari yetu. Wengi wanasema mkataba ule wa kimataifa hivyo una defeat sheria za ndani. Kwa makusudi hawataki kusoma Geneva law of treaty ambayo inafafanua kuwa kwenye hali kama hizi mkataba huu hauwezi kuzidi sovereignty ya nchi. Walitusingizia uhaini wakatutoa, tunaanzia hapo tulipoishia.

Hili tunamkabidhi Mungu upande wa kushughulika na yaliyo nje ya mipaka ya binadamu, lakini yale ya kisheria hatumuachii yeye, tutakabiliana nao.

Kama walidhani wananitisha walifanya kosa kubwa sana, mimi sitishwi. Kama unafuata sheria za nchi nitakuheshimu, kama unatumia cheo sitakuheshimu. Kama nimekosea niadhibu kisheria pasipo kutunga makosa.

Sijui hata kutumia manati, ugaidi nitaifanya nini? Hii IGA nitaipinga, na Mungu atatupa uhai hadi tutakaposherekeka kufutwa kwa IGA. Hatutaruhusu laana hii katika malango ya nchi. Hoja za Bandari hazihitaji risasi, Serikali itujibu kwa hoja.

Ivi vikosi maalum kwann hawa mbwa koko amuwapigi risasi ,wanaleta taaruki kwenye ardhi ya amani
 
Naona chama kipya cha siasa kikitangazwa hapa.
Bila shaka, wapo ccm ambao hawaridhishwi na mwenendo wa chama chao pia watajiunga kwenye hiki chama kipya kabla ya 2024.
Chama kipya kufanya kazi lazima kwanza kisajiliwe na mamlaka husika. Itabidi wakamilishe taratibu hizo za kisheria.
 
Back
Top Bottom