Kwa hili la katiba mpya rais Samia atalamba dume

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kwa wacheza karata wanafahamu faida za kulamaba dume na athari za kulamba garasa, nami napenda kumpa wosia Rais Samia Suluhu Hassan kwamba kama atafanikisha upatikanaji wa Katiba mpya, basi atakuwa amelamba dume.

Unapocheza karata ukalamba magarasa lazima upate maumivu ya kiakili na kisaikolojia ya kupoteza mchezo mzima hata kama utakuwa na jockeri moja na magarasa matupu, nami namuombea Rais Samia na Watanzania walambe dume. Nimetangulia kutoa mfano huo kuonyesha namna Rais Samia atakavyowaachia Watanzania kumbukumbu inayoishi legacy) kama atafanikisha upatikanaji wa Katiba mpya yenye ridhaa, maridhiano na mwafaka wa kitaifa na si wanasiasa.

Nasema hivyo kwa sababu mwaka 2012, Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alikuwa na ndoto ya kuwaachia Watanzania alama inayoishi kwa kuwapatia Katiba mpya, lakini safari yake ilishia ukingoni mchakato ulipotekwa na wanasiasa.

Wakati ule wa Bunge Maalumu la Katiba 2014, Watanzania walitamani uchaguzi mkuu 2015 ufanyike tukiwa na Katiba mpya, lakini sote tunafahamu namna maoni ya wananchi yalivyokanyagwa na kufinyangwa na Bunge lile.
Siku zote ukweli una sifa moja kuu, kwamba hata ukiuchukia au kuukataa, haugeuki kuwa uongo, nami nasema suala la kulinda masilahi ya kisiasa ya CCM kwa sehemu kubwa na upinzani kwa sehemu ndogo ndiyo yalivuruga mchakato.

Wengi wa wajumbe wa Bunge lile ambao kwa sehemu kubwa walikuwa ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wale 201, walikengeuka na kufumua maoni yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoku wa chini ya Jaji Joseph Warioba.

Wiki iliyopita, Rais alimwagiza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao maalumu cha Baraza la vyama vya siasa kwa ajili ya kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaii wa mapendekezo ya kikosi kazi alichokiunda.

Lengo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaii wa mapendekezo ya kikosi hicho kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini na pia kushirikisha wadau katika mchakato wa katiba mpya. Mbali na mchakato wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushu-ghulikiwa na mkutano huo ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusu uchaguzi, Tume ya Uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019.

Ninampongeza Rais Samia kwa utashi huu wa kisiasa na dhamira niema kwa taifa letu na ninatamani aishi katika maneno na ahadi yake pamoja na chama chake lakini awe makini asipitie njia ile ile tuliyopita kuanzia 2012-2014 tukakwama.

Napenda nimkumbushe tu kuwa hata Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kutuachia kumbukumbu inayoishi au leg-acy, yaani Katiba mpya, lakini wahafidhina ndani ya CCM wasiotaka mabadiliko wakauteka mchakato.ule na kuuvuruga. Huwa mara moja moja napitia rasimu ya pili ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyowasilishwa katika Bunge la Katiba, sioni tatizo lake, ukiondoa suala la muundo wa Muungano, ambalo hilo tunaweza kutoa uwanja mpana wa maridhiano.

Nina wasiwasi, kama tutapita njia ile ile tuliyopita 2012-2014 tulipokwama, ni dhahiri tunakwenda kukwama tena kama tutawafanya wanasiasa kwa sehemu kub-wa ndiyo watuamulie Katiba tunayoitaka wakati maoni yalishakusanywa. Tunatamani twende kwenye uchaguzi mkuu 2025 tukiwa na Katiba mpya itakayopunguza mamlaka makubwa ya Rais ambayo kwa Katiba ya sasa, amri zake ndio zinakuwa sheria hata kama amri hizo zinavunia Katiba au sheria za nchi.

Tunataka Katiba itakayofanya tuwe na mifumo na taasisi imara zinazofanya kazi kwa weledi na bila 'maagizo kutoka juu' na Katiba itakayolinda haki za raia, zikiwamo haki za binadamu na Katiba itakayofanya kila mtu kuwa chini ya sheria. Kwa maoni yangu, kilichotukwamisha wakati ule na kitatukwamisha tena ni kuacha aienda muhimu ya Katiba kutekwa na wanasiasa ambao ni kundi dogo la watu katika Watanzania milioni 61 ambao kwao jambo muhimu ni madaraka.

Tuiifunze kutokana na makosa na huu ndio utamaduni mzuri kwamba wanasia-sa wasaidie kupiga debe na amsha amsha ya Katiba mpya, lakini wasiuteke mchaka-to huu kwa maslahi yao ya kisiasa ya kubaki madarakani au kutwaa madaraka.
Ushauri wangu, tuunde jopo la wataalamu wapitie rasimu ile ya Jail Warioba na Katiba Inayopendekezwa na kuzioanisha na kurejesha maoni ya wananchi, na kuoanisha mapendekezo yao na yale ya kikosi kazi kilichoundwa na Rais. Baada ya hapo, waje na rasimu ya kwanza tuijadili kupata muafaka wa kitaifa halafu tuipeleke Bunge la Katiba kwa ajili ya kupata baraka.
 
Back
Top Bottom