Swali: Hivi mikanda ya video ya mazishi huwa watu wanaangalia lini?

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Michango na gharama za matumizi ya shughuli za kijamii kwa siku hizi ni maajabu!
Mtu akiugua, watu wanavuta miguu sana kuchangia matibabu.Akifa ndio utashangaa budget zinatengenezwa na michango kuitishwa.
Kinachonishangza ni ile budget ya kupiga picha za video za tukio zima.Hii iko hadi vijijini!
Cha kujiuliza - hivi, watu hasa wafiwa huangalia lini hii mikanda na kwa kuangalia inamaanisha nini?
 
Mzee hapo kazi ipo maana siku hiyo sijui utakuwa una hamu ya kulimwaga chozi au umem-miss mpendwa wako?
 
Hata leo nimetoka kwenye mazishi tuliyofanya hapa mtaani kwe2 na kuwepo vi2 kama hivyo na watu wamejigaragaza sana na video ikawa inachukuliwa nikakosa jibu ya kwmb wataangalia lini haya matukio. Lakini imekuwa desturi sasa hv sana ktk jamii yetu.
 
Swali zuri sana niliwahi kujiuliza nilipoona wapiga picha wakijipanga wakati wa kumchukua marehemu.kiukweli zile picha huwa zinatia simanzi sana kiasi wale watu wa karibu ni vigumu kuziangalia tena.Ila ndio hivyo tena ni utamaduni mpya tumeiga so baadae pengine itazoeleka lakini wabongo tunacomplicate kila tukio siku hizi hakuna jambo dogo,haina tafsiri kuwa tumepiga sana hatua kiuchumi bali kuna kaulimbukeni maana kuna vitu endelevu ambavyo tungeweza kuwekeza kwa hizo gharama.
 
Hata miye huwa naona sielewi wataangalia lini jamani. Wabongo bana.
Si ajabu ni mambo ya kuiga kwenye movies haya.
Tz watu wanajifunza kila kitu kutoka movies hata visivyo na maana kama kuvaa majaketi ya winter huku jua kali la tropikali .
 
na wengine na sare kabisa....wanavaa..
t shirt za picha ya marehemu
na kushonesha nguo kabisa
halafu unakuta 'marehemu' alikuwa na maisha ya 'kubangaiza' tu
 
ndugu wapo ulaya wameshindwa kuhudhuria ndo watakuja kuangalia!!!just jokin!ila kiukweli hii tabia inashangaza!
 
Hata mimi kwa ukweli haya matukio huwa yananishangaza sana. Hapo zamani watu walikuwa wanazikwa mbali na maeneo yao ili kupunguza majonzi kwa wafiwa watapo ona kaburi la Mpendwa wao, sasa sijui kama wakati huo kuona kaburi linakukumbusha simanzi sasa sijui hili la kuangalia shughuri nzima ya mazishi ya mpendwa wako linakaaje. Jibu nililopata ni kwamba watu siku hizi tuna sifa sana haswa katika mikusanyiko ya watu hivyo Kuanzia Katika Harusi za siku hizi, Misiba hata kipaimara ni kuoneshana ufahari Mavi ambao hauna tija.
 
Lakini hii ya kuchukua picha (si video) imekuwepo tokea zamani sana au mimi ndo sijui?
 
Nchi kama RSA,siku ya kurudi kutoka mazikoni inakuwa ni kama shughuli fulani hivi bila kusahau Msumbiji hasa kusini mwa nchi ile,siku ya tatu baada ya kurudi makaburini kunakuwa na mishemishe fulani hivi kwahiyo suala la mazishi linategemea jamii husika.

Ila kuhusu kuchukua tukio zima kwa kutumia kideo,huwa unaangalia siku uliyomkumbuka huyo aliyekufa.Nalog off
 
Ukwel ni kwamb akuna umuhim wowote na ndugu wa familia husika uwa awapendi kuziangalia<baba,mama ,watoto na jamaa waliozaliwa tumbomoja na marehem>wanakamati weng wanapenda makuu.picha muhimu za kuangalia ni zamatukio ya marehem alipokuwa bado angali ahi.mimi tangu mama yangu afariki 09 sijawa kuangalia iwe mkanda au picha matukio ya msiba japo kuna WANAFIKI uwawanaulizia mkanda/picha za matukio ya mazish.
Msiba usikie kwa jirani kamwe auzoeleki!
 
Hata miye huwa naona sielewi wataangalia lini jamani. Wabongo bana.
Si ajabu ni mambo ya kuiga kwenye movies haya.
Tz watu wanajifunza kila kitu kutoka movies hata visivyo na maana kama kuvaa majaketi ya winter huku jua kali la tropikali .
hapo kwenye bluu una ugomvi na wasanii wetu,jiandae kujibu mapigo.&#607;&#607;o &#387;o&#1503;&#592;u
 
Back
Top Bottom