Sheria ya mvuto na hisia katika kuleta jawabu linalostahili

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,692
SHERIA YA MVUTO NA HISIA KATIKA KULETA JAWABU LINALOSTAHILI.

Where concentration is, is where energy flows!"
Mahali ambapo unawekeza mawazo au fikra zako ndiko nguvu hutiririkia

Hii Ni Sheria ya 7 Katika sheria 12 zinazoratibu ulimwengu, awali tuliiona sheria ya 5 ya KARMA , Leo tuisome hii the law of attraction.

👉Hebu fikiria, ni wapi unawekeza sana fikra zako? Mambo gani uwa yanatawala fikra zako? Vitu gani unavitafakari au unaviamini?

Haijalishi unaamini nini? Amini jiwe, ng'ombe, sanamu fulani, Allah, Yehova, Jesus, Krishna, Mahavir, Ganesha, mahoka, mababu, kenge au chochote kile.

Madam umewekeza concentration yako au mawazo yako/ moyo wako huko basi ndani yako kuna nguvu isiyo ya kawaida inaachiliwa kwenda kwa mtu au kitu unachokihusudu/ abudu na kukuunganisha na huyo mtu au kitu ambacho umekipa moyo wako.

Kitu hicho au mtu huyo kwa mantiki hiyo kwako kinafanyika Mungu na kinaweza fanya chochote utakacho.

👉Hayo ndiyo maajabu ya mwanadamu.
Anaumba Mungu wake na kumwabudu na anapata majibu ya maombi yake akiomba kwa uhakika uliozalishwa ndani yake na hiyo nguvu!

Ndio maana huwezi kuwa na dini/ imani Moja duniani hata ufanyeje, kwa sababu kila mtu ana mahali anapoelekeza nguvu zake za asili na KUZIRUHUSU kufanya chochote.

Ukiamini YOTE YANAWEZEKANA kwa sababu nguvu ya kuwezesha vitu kutokea inatokana na wewe. Hata ukiamua kujiabudu kwa dhati basi utaona maajabu na utajitangaza Mungu na kupata wafuasi wa kujiabudu kama Mungu wao.

Tofauti ya nguvu baina ya Mungu huyu na Mungu yule ni kiwango cha mtu husika KURUHUSU NAFSI YAKE KUWA CHANNEL OF POWER!

👉Asilimia kubwa ya wanadamu duniani Leo wanaamini katika Mungu anayeabudiwa kupitia Masihi Yesu Kristo na wanapata matokeo kadiri ya Imani, huku wengine wakiabudu chochote na kupata majibu pia.
Sasa UDHIHIRISHO WA NGUVU NA UWEZA WA MUNGU HUSIKA utategemea si tu huyo Mungu bali kwa asilimia kubwa mwanadamu husika na uwezo wake wa asili huitwao ENERGY/ POWER au unaweza kuita FAITH!

Ndio maana tumekuwa tukiwasisitiza wafia dini wafunguke macho yao wayatazame mambo haya kwa udadisi ndipo ibada zao zitawapa matokeo, kinyume chake wataendelea kushangaa na kujiuliza inakuwaje waabudu kile kinachoitwa mizimu na wachawi wanawapiga gap la nguvu!

Inua kiwango chako cha nguvu uone utendaji wa kile unachokiamini kwa sababu imani zote zinasimamiwa na LAW OF ATTRACTION!

👉Unapokaa mahali fulani ukawa unawaza vitu fulani fulani kwa hofu unakuwa unavivuta viumbike kwenye ulimwengu wako.

Ndio maana kila unachokiogopa lazima hatimaye kikupate!

Kama kila mara unawazia kuwa maskini (hofu ya maisha inakutawala) lazima hali hiyo hiyo ikupate.
Kama unaogopa kusalitiwa na 'mtu wako' lazima hilo likutokee kwa sababu kila unapokuwa na mawazo hasi unakuwa unayavuta kuwa dhahiri kwenye ulimwengu wako.

Uking'atwa na mbu alafu ukawa na hofu kuwa utaugua malaria, hata kama huyo mbu sio Anopheles, lazima uugue malaria!

Watu wanaoogopa sana uchawi, they are vulnerable to its effects.

👉Lazima upambane dhidi ya negativities ndani yako kama unataka kuwa huru kwenye huu uso wa dunia, hata kabla hujawazia maombi!

Hii Kanuni inasisitiza kuwa vitu vyote vinavyotikisika katika masafa sawa huvutana na hatimaye kukaa pamoja (Like attracts like)

Kwa binadamu kila kitu kina-vibrate (tikisika) katika frequencies (masafa) fulani ambazo hutafsiriwa na brain.

Human brain inatikisika katika masafa makuu matano (tutakujaga kuyaongelea huko mbeleni)

Kwa Kanuni hii ufahamu wako ndio unaovuta mazingira yako, yaani mawazo yako ya kina (subconscious mind) ndio yanayovuta mazingira yako ya nje!

👉Ukiona kila mara unapambana na wachawi kwenye ndoto au unalogeka kwa urahisi ujue ni kwa sababu ya law of attraction, yaani kwenye ubongo wako umejaza fikra za mambo ya kichawi-chawi. Wewe na wachawi/ uchawi mna-vibrate in the same frequencies!

Unakuta mtu kila wakati anawaza kuhusu ugumu wa maisha, kukosa kazi, kutoolewa, kupata ajari nk... Kitendo hicho kinaufanya ubongo wako kuanza ku-vibrate kwenye masafa ya hizo vitu ili viwe halisi. Ndio maana ukitaka kujua yaliyoujaza moyo wako/ brain yako, fikiria kuhusu ndoto unazoota mara kwa mara. Ndoto ni kama kioo kinachokuonesha mawazo yaliyojaa kwenye subconscious mind yako.

Baada ya muda mambo unayoyaota kila mara lazima yadhihirike kwako ili kui-prove law of attraction; like attracts like!

Ukitaka kujiepusha na mambo mabaya mabaya, hakikisha kila mara unakuwa positive kichwani; usiruhusu ubongo wako kuingiza vitu vya ovyo ovyo vinavyokuogopesha, kukutisha na kukuvunja moyo au kukukatisha tamaa.
Jiepushe na makundi yasiyofaa, movies za kutishatisha na mambo yanayofanana na hayo.

👉Tukirudi Katika biblia ukisoma MATHAYO 6:9-10 Yesu anawafundisha wanafunzi wake kusali, akisema👇
"Ufalme wako UJE. mapenzi yako yatimizwe HAPA DUNIANI Kama HUKO MBINGUNI

Hii inamaanisha waombaji wanawajibika kumuomba baba Mungu(Asili) UFALME wake UJE Dunuani Kama ulivyo huko mbinguni ili yaliyopo Mbinguni(Katika fikra) yaonekane dhahiri DUNIANI, Kwenye maisha halisi ya wanamaombi.

Lakini, swali ni JE, HAWA WANAMAOMBI WANA-ENJOY MAISHA KAMA HUKO MBINGUNI AU WANATESEKA NA KUSUBIRI KWENDA MBINGUNI WAKIWA HOI BIN TAABANI KAMA LAZARO❓

Kwenye hiyo kauli ya Yesu ya kuuleta Ufalme wa Mungu duniani na kusababisha "duniani (kuwa) kama mbinguni" ametumika kuzungumzia👉 THE LAW OF ATTRACTION (AS ABOVE SO BELOW) Yani Kama ilivyo juu ndivyo ilivyochini.

👉Kwamba kila kitu kilichopo kwenye ulimwengu wa roho kinapaswa kuvutwa na kuwa halisi duniani, kwenye macho ya nyama.

Ulimwengu wa roho (higher dimensions, mbinguni) ni mahali ambapo kila kitu kinapatikana, chochote kile ambacho kiliwahi kuwepo, kilichopo na kitakachokuwepo, vyote vipo kwenye Ulimwengu wa roho!

Mema na mabaya, uzima na mauti, afya na magonjwa, utajiri na umasikini, baraka na laana nk, vyote vipo huko. Ukivitaka vinakuja; hicho ndo sheria ya uvutano (law of attraction) humaanisha!
Ukitaka mali zivute zije. Ukitaka ufukara uvute uje.

Kutaka na kuomba au kusali maana yake ni moja!
Yesu alipotaka mtini unyauke, ulinyauka bila kujali huko kunyauka kulisababishwa na nini! (Marko 11:14,20) tambua Hilo ni fumbo

Na wewe ukitaka mwembe unyauke unanyauka tu chap, kama ambavyo umetaka kuwa hivyo ulivyo!

👉Sisi tumeunganishwa na kila kitu tunachokitaka.
Fikra zetu zinapoanza kutetema (to vibrate) kwenye mtetemo wa kitu fulani, hapo hapo tunaunganishwa nacho.

Huo mtetemo ukiendelea unasababisha mvutano kati yetu na hicho kitu, tunaanza kuvutana hata bila kujua na baada ya muda tunakutana. Ni kazi ya Universe kukukutanisha na unachokitaka ukizingatia sheria ya uvutano!

Kwa mfano, fikra zangu zikianza kuwaza fedha, mawimbi yasiyoonekana yananiunganisha na hizo fedha popote zilipo... Nikiendelea kuwaza tena na tena pesa zinajikuta zimeanza ku-vibrate kwenye mawimbi yangu, yaani Mimi na fedha tunaanza kucheza ngoma inayofanana (to vibrate in the same frequencies)
Mtetemo ukiendelea Mimi na fedha tunaanza kuvutana, yaani kutafutana.
Baada ya MUDA FULANI utasikia nawaambia watu "ile fedha niliyotaka imepatikana!"

Kivipi?
By the law of attraction!

Unapowaza, unapotamka, unapohisi kitu chochote; hayo mawazo, hizo hisia na hayo maneno hukuunganisha na hicho kitu.

Mwalimu Mkuu Yesu amechorwa Katika Biblia akiendelea kufundisha akisema "Ukimtazama mwanamke ukamtamani kingono, tayari umezini naye" (Mathayo 5:28)

Maana yake ni kwamba pale unapomuona mwanamke alafu ukaanza kujenga taswira (figuring out) ya 'shep' lake, sura yake, 'nanilii' yake na mambo kama hayo, frequencies zinaku-connect naye, unajikuta na hali fulani hivi ambayo 'sio kawaida'!

Maana yake ni kwamba spiritually umefanya naye ngono.
Ulimwengu wa roho haujui kutofautisha kati ya reality na imagination!
Huna tofauti na mchizi ambaye alipomuona danga kalipia na kwenda kujimaliza; rohoni mnaonekana the same, kwa sababu ya law of attraction!

Ndivyo inavyokuwa hata ukitamka au ukahisi!

Mawazo yetu, fikra zetu, maneno yetu na hisia zetu vina nguvu ya ajabu ya kutu- connect na tunachokitaka!

Ukianza kuwaza kufa, au ukawa kila mara unasema habari za kufa kufa au habari za wafu, unahisi kufa; utashangaa ndotoni unaanza kuona inakuwa kama unavyowaza kila mara na baada ya muda UTAKUFA KABISA na wale waliokuwa karibu nawe watasema "jamaa alijua atakufa alikuwa anatwambia hivyo!"

Ndio maana unashauriwa na Solar Moon (Solo-Mon/ Suleiman) mwenye hekima uhakikishe unachukua taadhari na hisia zako, mawazo na maneno yako (Mithali 4:23)

Hebu jichunguze, we binafsi unavuta vitu gani kuja kwako?

Wadada wengi sana wanavuta "kutokuolewa" badala ya "kuolewa" na ndivyo inavyokuwa!
Unakuta mtu anakwambia ameomba na kufunga sana na kutoa dhabihu nyingi ili aolewe, lakini haolewi!
Ukikaa naye kama saa Moja utagundua anataka kuolewa ni sawa, lakini anaomba kutokuolewa na anapata kirahisi kwa sababu ya mawazo, hisia na maneno yake! Mdomoni anasema anataka kuolewa, lakini moyoni anawaza "hivi itawezekana?"

Wakati mwingine anawaambia wenzake jinsi ambavyo hana uhakika kama atampata mume anayemtaka!
Anaposema hana uhakika maana yake haamini kwa sababu Imani ni kuwa na uhakika!

Sio tu kwenye mambo ya kuoa na kuolewa, bali pia kwenye mambo mengine kama kufanikiwa, kutajirika, kufaulu, kuajiriwa, kuanzisha kampuni, huduma, Kanisa nk.

Watu wengi wanaitumia sheria ya uvutano (law of attraction) kuvuta mambo wasiyoyataka.

Jichunguze tena wewe mwenyewe.

Linapokuja suala la hicho unachokitaka, ni hisia gani unakuwa nazo? Ni mawazo gani yanakujaa akilini? Ni maneno gani yanakutoka?

Yesu alipouambia mti kwamba "tangu leo yasipatikane kwako matunda" hakujua vile itakavyofanyika, alichojua ni itakuwa tu kwani Ulimwengu wa roho unatii sana sana mawazo, hisia, matamshi yetu, hata kama tunaongea kirahisi rahisi!

Mtu akija kwangu akaniambia tatizo lake uwa namuuliza kirahisi, "unataka iweje?" namsikiliza.
Anachosema nakitafsiri, kisha namwambia "hivyo ndivyo itakavyokuwa" na mara zote inakuwaga hivyo.

Kwa mfano, mwanaume mmoja alinambia kuwa watoto wake hawafaulu kabisa mitihani yao anaomba nimwombee.
Nikamuuliza "unataka wafaulu kwa kiwango gani?"
Akajibu "angalau wasipate zero"
Nikamwambia "sawa kuanzia sasa hawatapata zero"

Kwenye mtihani uliofuata akaja ananiambia "wale watoto bado sana, yaani mmoja kapata 23% kwenye Kiswahili na mengine chini ya hapo, Hesabu kapata 4% na mwingine ni yale yale"

Nikamuuliza kwani wamepata zero?
Akajibu "sawa wamejitahidi maana huyo wa kwanza mitihani yake uwa ni masufuri tu, tena kwenye Hesabu hajawahi kupata hata maksi Moja, ila nataka angalau wafaulu"

Nikamwambia wewe umepata ulichokitaka kwa watoto wako kwa sababu ulinambia hutaki wapate zero na hakuna aliyepata zero kwenye masomo yote. Akashtuka na kuniuliza, "sasa nifanyeje angalau nao wafaulu kama wengine?"

Nikamwambia "ondoa maneno 'ANGALAU' na 'KAMA WENGINE' kwani Ulimwengu wa roho wenye kila kitu utakupa hayo hayo unayoyataka (unayoyaomba)"

Akasema "naomba wawe kati ya watano Bora"

Nikamwambia "chukua haya mafuta kila siku asbh kabla hawajaenda shule wapake na kuwaambia hayo maneno na kabla hawajalala fanya hivyo hivyo na kuwatamkia hivyo hivyo, hata watakapofanya vibaya kwenye masomo usiwagombeze na kuwatukana. Akaheshimu maelekezo yangu na akaenda kufanya hivyo hivyo.

Mpaka naandika haya wale watoto wake wawili Jovin na Robert wapo kwenye shule nzuri kidato cha sita maana kwenye mitihani yao ya kidato cha nne walipata division one point 7 na 9! Masomo yote mmoja alipata 'A' zote na mwingine 'A' 5, na masomo mengine 'B' zote! Hao ndio form two walikuwa wanapata masifuri masomo yote!

Law of attraction ita- attract unachowaza, unachotafakari, unachoongea na hata unachoigiza kutenda!

👉Kuna msomaji atasoma kote huko ila ikifika eneo kuhusu mafuta ataona nimemchefua sindio😁, cool down/tulia , hii ni moja wapo ya kitendea kazi, mkazo , kumuamsha mtu ili awe na kianzio Cha kuamini , Yani huyo Mtu hajui kuwa yeye ni nguvu ni kila kitu lakini akili yake, Ufahamu wake unaamini akija kwa Mchungaji au mganga ama shekhe atapona.

Sasa Imani yake inaamini chochote utakachompa utakuwa Msaada , unapompatia maji, mafuta inamwezesha kuamsha Ile sheria ya mvuto(the law of attraction kwani tayari ameanza kuamini kuwa anaenda kufanikiwa na mm ninayempa nimeshayaamuru kumpa kile mpokeaji akitakacho kwani ni kweli akiamini tu uumbaji unafanyika. Ni mchezo wa kisaikolojia kwakuwa watu wengi hawajui hii Siri ya nguvu tulizonazo na kila KITU chetu , tukitakacho kinatoka ndani yetu wenyewe

👉Naligia Mninoi (editor)
👉Rwakiunge DP Rugambwa ..(mwandishi)✍️
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho!

_20231127_084901.JPG
 
SHERIA YA MVUTO NA HISIA KATIKA KULETA JAWABU LINALOSTAHILI.

Where concentration is, is where energy flows!"
Mahali ambapo unawekeza mawazo au fikra zako ndiko nguvu hutiririkia

Hii Ni Sheria ya 7 Katika sheria 12 zinazoratibu ulimwengu, awali tuliiona sheria ya 5 ya KARMA , Leo tuisome hii the law of attraction.

Hebu fikiria, ni wapi unawekeza sana fikra zako? Mambo gani uwa yanatawala fikra zako? Vitu gani unavitafakari au unaviamini?

Haijalishi unaamini nini? Amini jiwe, ng'ombe, sanamu fulani, Allah, Yehova, Jesus, Krishna, Mahavir, Ganesha, mahoka, mababu, kenge au chochote kile.

Madam umewekeza concentration yako au mawazo yako/ moyo wako huko basi ndani yako kuna nguvu isiyo ya kawaida inaachiliwa kwenda kwa mtu au kitu unachokihusudu/ abudu na kukuunganisha na huyo mtu au kitu ambacho umekipa moyo wako.

Kitu hicho au mtu huyo kwa mantiki hiyo kwako kinafanyika Mungu na kinaweza fanya chochote utakacho.

Hayo ndiyo maajabu ya mwanadamu.
Anaumba Mungu wake na kumwabudu na anapata majibu ya maombi yake akiomba kwa uhakika uliozalishwa ndani yake na hiyo nguvu!

Ndio maana huwezi kuwa na dini/ imani Moja duniani hata ufanyeje, kwa sababu kila mtu ana mahali anapoelekeza nguvu zake za asili na KUZIRUHUSU kufanya chochote.

Ukiamini YOTE YANAWEZEKANA kwa sababu nguvu ya kuwezesha vitu kutokea inatokana na wewe. Hata ukiamua kujiabudu kwa dhati basi utaona maajabu na utajitangaza Mungu na kupata wafuasi wa kujiabudu kama Mungu wao.

Tofauti ya nguvu baina ya Mungu huyu na Mungu yule ni kiwango cha mtu husika KURUHUSU NAFSI YAKE KUWA CHANNEL OF POWER!

Asilimia kubwa ya wanadamu duniani Leo wanaamini katika Mungu anayeabudiwa kupitia Masihi Yesu Kristo na wanapata matokeo kadiri ya Imani, huku wengine wakiabudu chochote na kupata majibu pia.
Sasa UDHIHIRISHO WA NGUVU NA UWEZA WA MUNGU HUSIKA utategemea si tu huyo Mungu bali kwa asilimia kubwa mwanadamu husika na uwezo wake wa asili huitwao ENERGY/ POWER au unaweza kuita FAITH!

Ndio maana tumekuwa tukiwasisitiza wafia dini wafunguke macho yao wayatazame mambo haya kwa udadisi ndipo ibada zao zitawapa matokeo, kinyume chake wataendelea kushangaa na kujiuliza inakuwaje waabudu kile kinachoitwa mizimu na wachawi wanawapiga gap la nguvu!

Inua kiwango chako cha nguvu uone utendaji wa kile unachokiamini kwa sababu imani zote zinasimamiwa na LAW OF ATTRACTION!

Unapokaa mahali fulani ukawa unawaza vitu fulani fulani kwa hofu unakuwa unavivuta viumbike kwenye ulimwengu wako.

Ndio maana kila unachokiogopa lazima hatimaye kikupate!

Kama kila mara unawazia kuwa maskini (hofu ya maisha inakutawala) lazima hali hiyo hiyo ikupate.
Kama unaogopa kusalitiwa na 'mtu wako' lazima hilo likutokee kwa sababu kila unapokuwa na mawazo hasi unakuwa unayavuta kuwa dhahiri kwenye ulimwengu wako.

Uking'atwa na mbu alafu ukawa na hofu kuwa utaugua malaria, hata kama huyo mbu sio Anopheles, lazima uugue malaria!

Watu wanaoogopa sana uchawi, they are vulnerable to its effects.

Lazima upambane dhidi ya negativities ndani yako kama unataka kuwa huru kwenye huu uso wa dunia, hata kabla hujawazia maombi!

Hii Kanuni inasisitiza kuwa vitu vyote vinavyotikisika katika masafa sawa huvutana na hatimaye kukaa pamoja (Like attracts like)

Kwa binadamu kila kitu kina-vibrate (tikisika) katika frequencies (masafa) fulani ambazo hutafsiriwa na brain.

Human brain inatikisika katika masafa makuu matano (tutakujaga kuyaongelea huko mbeleni)

Kwa Kanuni hii ufahamu wako ndio unaovuta mazingira yako, yaani mawazo yako ya kina (subconscious mind) ndio yanayovuta mazingira yako ya nje!

Ukiona kila mara unapambana na wachawi kwenye ndoto au unalogeka kwa urahisi ujue ni kwa sababu ya law of attraction, yaani kwenye ubongo wako umejaza fikra za mambo ya kichawi-chawi. Wewe na wachawi/ uchawi mna-vibrate in the same frequencies!

Unakuta mtu kila wakati anawaza kuhusu ugumu wa maisha, kukosa kazi, kutoolewa, kupata ajari nk... Kitendo hicho kinaufanya ubongo wako kuanza ku-vibrate kwenye masafa ya hizo vitu ili viwe halisi. Ndio maana ukitaka kujua yaliyoujaza moyo wako/ brain yako, fikiria kuhusu ndoto unazoota mara kwa mara. Ndoto ni kama kioo kinachokuonesha mawazo yaliyojaa kwenye subconscious mind yako.

Baada ya muda mambo unayoyaota kila mara lazima yadhihirike kwako ili kui-prove law of attraction; like attracts like!

Ukitaka kujiepusha na mambo mabaya mabaya, hakikisha kila mara unakuwa positive kichwani; usiruhusu ubongo wako kuingiza vitu vya ovyo ovyo vinavyokuogopesha, kukutisha na kukuvunja moyo au kukukatisha tamaa.
Jiepushe na makundi yasiyofaa, movies za kutishatisha na mambo yanayofanana na hayo.

Tukirudi Katika biblia ukisoma MATHAYO 6:9-10 Yesu anawafundisha wanafunzi wake kusali, akisema
"Ufalme wako UJE. mapenzi yako yatimizwe HAPA DUNIANI Kama HUKO MBINGUNI

Hii inamaanisha waombaji wanawajibika kumuomba baba Mungu(Asili) UFALME wake UJE Dunuani Kama ulivyo huko mbinguni ili yaliyopo Mbinguni(Katika fikra) yaonekane dhahiri DUNIANI, Kwenye maisha halisi ya wanamaombi.

Lakini, swali ni JE, HAWA WANAMAOMBI WANA-ENJOY MAISHA KAMA HUKO MBINGUNI AU WANATESEKA NA KUSUBIRI KWENDA MBINGUNI WAKIWA HOI BIN TAABANI KAMA LAZARO

Kwenye hiyo kauli ya Yesu ya kuuleta Ufalme wa Mungu duniani na kusababisha "duniani (kuwa) kama mbinguni" ametumika kuzungumzia THE LAW OF ATTRACTION (AS ABOVE SO BELOW) Yani Kama ilivyo juu ndivyo ilivyochini.

Kwamba kila kitu kilichopo kwenye ulimwengu wa roho kinapaswa kuvutwa na kuwa halisi duniani, kwenye macho ya nyama.

Ulimwengu wa roho (higher dimensions, mbinguni) ni mahali ambapo kila kitu kinapatikana, chochote kile ambacho kiliwahi kuwepo, kilichopo na kitakachokuwepo, vyote vipo kwenye Ulimwengu wa roho!

Mema na mabaya, uzima na mauti, afya na magonjwa, utajiri na umasikini, baraka na laana nk, vyote vipo huko. Ukivitaka vinakuja; hicho ndo sheria ya uvutano (law of attraction) humaanisha!
Ukitaka mali zivute zije. Ukitaka ufukara uvute uje.

Kutaka na kuomba au kusali maana yake ni moja!
Yesu alipotaka mtini unyauke, ulinyauka bila kujali huko kunyauka kulisababishwa na nini! (Marko 11:14,20) tambua Hilo ni fumbo

Na wewe ukitaka mwembe unyauke unanyauka tu chap, kama ambavyo umetaka kuwa hivyo ulivyo!

Sisi tumeunganishwa na kila kitu tunachokitaka.
Fikra zetu zinapoanza kutetema (to vibrate) kwenye mtetemo wa kitu fulani, hapo hapo tunaunganishwa nacho.

Huo mtetemo ukiendelea unasababisha mvutano kati yetu na hicho kitu, tunaanza kuvutana hata bila kujua na baada ya muda tunakutana. Ni kazi ya Universe kukukutanisha na unachokitaka ukizingatia sheria ya uvutano!

Kwa mfano, fikra zangu zikianza kuwaza fedha, mawimbi yasiyoonekana yananiunganisha na hizo fedha popote zilipo... Nikiendelea kuwaza tena na tena pesa zinajikuta zimeanza ku-vibrate kwenye mawimbi yangu, yaani Mimi na fedha tunaanza kucheza ngoma inayofanana (to vibrate in the same frequencies)
Mtetemo ukiendelea Mimi na fedha tunaanza kuvutana, yaani kutafutana.
Baada ya MUDA FULANI utasikia nawaambia watu "ile fedha niliyotaka imepatikana!"

Kivipi?
By the law of attraction!

Unapowaza, unapotamka, unapohisi kitu chochote; hayo mawazo, hizo hisia na hayo maneno hukuunganisha na hicho kitu.

Mwalimu Mkuu Yesu amechorwa Katika Biblia akiendelea kufundisha akisema "Ukimtazama mwanamke ukamtamani kingono, tayari umezini naye" (Mathayo 5:28)

Maana yake ni kwamba pale unapomuona mwanamke alafu ukaanza kujenga taswira (figuring out) ya 'shep' lake, sura yake, 'nanilii' yake na mambo kama hayo, frequencies zinaku-connect naye, unajikuta na hali fulani hivi ambayo 'sio kawaida'!

Maana yake ni kwamba spiritually umefanya naye ngono.
Ulimwengu wa roho haujui kutofautisha kati ya reality na imagination!
Huna tofauti na mchizi ambaye alipomuona danga kalipia na kwenda kujimaliza; rohoni mnaonekana the same, kwa sababu ya law of attraction!

Ndivyo inavyokuwa hata ukitamka au ukahisi!

Mawazo yetu, fikra zetu, maneno yetu na hisia zetu vina nguvu ya ajabu ya kutu- connect na tunachokitaka!

Ukianza kuwaza kufa, au ukawa kila mara unasema habari za kufa kufa au habari za wafu, unahisi kufa; utashangaa ndotoni unaanza kuona inakuwa kama unavyowaza kila mara na baada ya muda UTAKUFA KABISA na wale waliokuwa karibu nawe watasema "jamaa alijua atakufa alikuwa anatwambia hivyo!"

Ndio maana unashauriwa na Solar Moon (Solo-Mon/ Suleiman) mwenye hekima uhakikishe unachukua taadhari na hisia zako, mawazo na maneno yako (Mithali 4:23)

Hebu jichunguze, we binafsi unavuta vitu gani kuja kwako?

Wadada wengi sana wanavuta "kutokuolewa" badala ya "kuolewa" na ndivyo inavyokuwa!
Unakuta mtu anakwambia ameomba na kufunga sana na kutoa dhabihu nyingi ili aolewe, lakini haolewi!
Ukikaa naye kama saa Moja utagundua anataka kuolewa ni sawa, lakini anaomba kutokuolewa na anapata kirahisi kwa sababu ya mawazo, hisia na maneno yake! Mdomoni anasema anataka kuolewa, lakini moyoni anawaza "hivi itawezekana?"

Wakati mwingine anawaambia wenzake jinsi ambavyo hana uhakika kama atampata mume anayemtaka!
Anaposema hana uhakika maana yake haamini kwa sababu Imani ni kuwa na uhakika!

Sio tu kwenye mambo ya kuoa na kuolewa, bali pia kwenye mambo mengine kama kufanikiwa, kutajirika, kufaulu, kuajiriwa, kuanzisha kampuni, huduma, Kanisa nk.

Watu wengi wanaitumia sheria ya uvutano (law of attraction) kuvuta mambo wasiyoyataka.

Jichunguze tena wewe mwenyewe.

Linapokuja suala la hicho unachokitaka, ni hisia gani unakuwa nazo? Ni mawazo gani yanakujaa akilini? Ni maneno gani yanakutoka?

Yesu alipouambia mti kwamba "tangu leo yasipatikane kwako matunda" hakujua vile itakavyofanyika, alichojua ni itakuwa tu kwani Ulimwengu wa roho unatii sana sana mawazo, hisia, matamshi yetu, hata kama tunaongea kirahisi rahisi!

Mtu akija kwangu akaniambia tatizo lake uwa namuuliza kirahisi, "unataka iweje?" namsikiliza.
Anachosema nakitafsiri, kisha namwambia "hivyo ndivyo itakavyokuwa" na mara zote inakuwaga hivyo.

Kwa mfano, mwanaume mmoja alinambia kuwa watoto wake hawafaulu kabisa mitihani yao anaomba nimwombee.
Nikamuuliza "unataka wafaulu kwa kiwango gani?"
Akajibu "angalau wasipate zero"
Nikamwambia "sawa kuanzia sasa hawatapata zero"

Kwenye mtihani uliofuata akaja ananiambia "wale watoto bado sana, yaani mmoja kapata 23% kwenye Kiswahili na mengine chini ya hapo, Hesabu kapata 4% na mwingine ni yale yale"

Nikamuuliza kwani wamepata zero?
Akajibu "sawa wamejitahidi maana huyo wa kwanza mitihani yake uwa ni masufuri tu, tena kwenye Hesabu hajawahi kupata hata maksi Moja, ila nataka angalau wafaulu"

Nikamwambia wewe umepata ulichokitaka kwa watoto wako kwa sababu ulinambia hutaki wapate zero na hakuna aliyepata zero kwenye masomo yote. Akashtuka na kuniuliza, "sasa nifanyeje angalau nao wafaulu kama wengine?"

Nikamwambia "ondoa maneno 'ANGALAU' na 'KAMA WENGINE' kwani Ulimwengu wa roho wenye kila kitu utakupa hayo hayo unayoyataka (unayoyaomba)"

Akasema "naomba wawe kati ya watano Bora"

Nikamwambia "chukua haya mafuta kila siku asbh kabla hawajaenda shule wapake na kuwaambia hayo maneno na kabla hawajalala fanya hivyo hivyo na kuwatamkia hivyo hivyo, hata watakapofanya vibaya kwenye masomo usiwagombeze na kuwatukana. Akaheshimu maelekezo yangu na akaenda kufanya hivyo hivyo.

Mpaka naandika haya wale watoto wake wawili Jovin na Robert wapo kwenye shule nzuri kidato cha sita maana kwenye mitihani yao ya kidato cha nne walipata division one point 7 na 9! Masomo yote mmoja alipata 'A' zote na mwingine 'A' 5, na masomo mengine 'B' zote! Hao ndio form two walikuwa wanapata masifuri masomo yote!

Law of attraction ita- attract unachowaza, unachotafakari, unachoongea na hata unachoigiza kutenda!

Kuna msomaji atasoma kote huko ila ikifika eneo kuhusu mafuta ataona nimemchefua sindio, cool down/tulia , hii ni moja wapo ya kitendea kazi, mkazo , kumuamsha mtu ili awe na kianzio Cha kuamini , Yani huyo Mtu hajui kuwa yeye ni nguvu ni kila kitu lakini akili yake, Ufahamu wake unaamini akija kwa Mchungaji au mganga ama shekhe atapona.

Sasa Imani yake inaamini chochote utakachompa utakuwa Msaada , unapompatia maji, mafuta inamwezesha kuamsha Ile sheria ya mvuto(the law of attraction kwani tayari ameanza kuamini kuwa anaenda kufanikiwa na mm ninayempa nimeshayaamuru kumpa kile mpokeaji akitakacho kwani ni kweli akiamini tu uumbaji unafanyika. Ni mchezo wa kisaikolojia kwakuwa watu wengi hawajui hii Siri ya nguvu tulizonazo na kila KITU chetu , tukitakacho kinatoka ndani yetu wenyewe

Naligia Mninoi (editor)
Rwakiunge DP Rugambwa ..(mwandishi)
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho!

View attachment 2826383

Back
Top Bottom