Swali: Hivi mikanda ya video ya mazishi huwa watu wanaangalia lini?

Michango na gharama za matumizi ya shughuli za kijamii kwa siku hizi ni maajabu!
Mtu akiugua, watu wanavuta miguu sana kuchangia matibabu.Akifa ndio utashangaa budget zinatengenezwa na michango kuitishwa.
Kinachonishangza ni ile budget ya kupiga picha za video za tukio zima.Hii iko hadi vijijini!
Cha kujiuliza - hivi, watu hasa wafiwa huangalia lini hii mikanda na kwa kuangalia inamaanisha nini?

Katika kijiji chetu vitu hivyo havipo. Mchango katika msiba ni vyakula vilivyopikwa kutoka katika kila familia ya eneo husika. Watanzania sasa hivi hasa wa mijini tumekuwa magwiji wa kuiga mambo/matumizi mbalimbali yasiyo na tija. Hivi, fikiria michango ya kitchen party/ send off / arusi na matumizi yake. Gharama hizi zinawasaidia nini maharusi kama siyo kuwaacha na madeni yasiyo na tija? Kuna haja ya Watanzania tufanye maamuzi ya magumu ya kupiga vita michango hii ili tuchangishane kusomesha watoto au kupeana mitaji ya mwanzo (seed capital) kwa wajasiliamali wanaoibukia.
 
Ni kuiga wazungu basi hakuna lingine hapo

Ni kweli tunaiga ila wenzetu mazishi yao jeneza huwa limefunikwa na watu wanalia ila hawapigi mayowe. Yaani ukiangalia video au picha, ndio inahuzunisha ila haiogopeshi. Sasa ssisi kibongobongo tunampiga marehemu picha ndani ya jeneza tena wanamkuza kabisaa......nilikwenda kumpa pole ndugu yangu mmoja alifiwa basi ile nafika tu napewa album(sikuwepo kwenye mazishi), kwani niliweza kuangalia basi? nimefungua kurasa mbili tu nikafunga, hata ndugu yangu mwenyewe hakuweza kutizama. So maybe its ok kupiga picha ila upigaji uzingatie kumstiri marehemu.
 
siku hizi wanaweka na bendi kabisa ya kutumbuiza wakati wa mazishi, wanatengeneza t-shirt imekuwa mashindano kama vile harusi ya kifahari na kabwela
 
starling..........
story by.......
scirpt writer........
casting..1,2,3,4,5,6,7,
director.............
makeup............
sound......
editor.........
location........
etc.etc.........

the end
 
hayo ya mikanda mimi nimejiuliza sana sijapata jibu..............................
watu wanaenda salon kushonea weaving na mambo mengine ya urembo............. hapo kafiwa na baba, mama, kaka etc......
yaani siku hizi ladha ya misiba imepotea kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Unazungumzia kupoteza ladha au maana jamani lol
 
Hizi video zinaweza kusaidia uchunguzi/upelelezi kwa vifo venye utata!

Je umewahi kusikia hata kesi moja ilitolewa ushahidi wa mkanda wa video?

unaangalia mkanda wa mazishi ili ukumbuke nini? ...binafsi sioni sababu ya vdeo. Kwenye mazishi,ni umbea tu baada ya mazishi oh, mbona nimeangalia mkanda sikukuona kwenye mazishi ya babangu...nk. Harusi ,b.day sawa .

Huweza kuchochea uhasama...pwenti hii!

Ni kweli tunaiga ila wenzetu mazishi yao jeneza huwa limefunikwa na watu wanalia ila hawapigi mayowe. Yaani ukiangalia video au picha, ndio inahuzunisha ila haiogopeshi. Sasa ssisi kibongobongo tunampiga marehemu picha ndani ya jeneza tena wanamkuza kabisaa......nilikwenda kumpa pole ndugu yangu mmoja alifiwa basi ile nafika tu napewa album(sikuwepo kwenye mazishi), kwani niliweza kuangalia basi? nimefungua kurasa mbili tu nikafunga, hata ndugu yangu mwenyewe hakuweza kutizama. So maybe its ok kupiga picha ila upigaji uzingatie kumstiri marehemu.
Humdhalilisha marehemu jamani! Hata mimi hili nalikubali sana. Inasikitisha na kukasirisha maana hakuna kumsitiri marehemu.

starling..........
story by.......
scirpt writer........
casting..1,2,3,4,5,6,7,
director.............
makeup............
sound......
editor.........
location........
etc.etc.........

the end

Jamani wewe! Ni sinema kumbe!
 
Je umewahi kusikia hata kesi moja ilitolewa ushahidi wa mkanda wa video?

Huweza kuchochea uhasama...pwenti hii!

Humdhalilisha marehemu jamani! Hata mimi hili nalikubali sana. Inasikitisha na kukasirisha maana hakuna kumsitiri marehemu.

Jamani wewe! Ni sinema kumbe!

sindio maana yake? Unakuta mzee wa famili umekaa sittng room unauza watoto :hivi leo tuangalie mkanda upi?maana ule wa marehemu babu yenu mie nimeuchoka.hata ule mkanda wa shangazi yenu sio mkali kama huu wa marehem mama yenu. Utasikia na watoto nao ah! Baba sie tunataka mkanda wa marehem mdogo wetu.unakuta na uko wenyewe sasa mkubwa ma movi nayo ya kumwaga!
 
Back
Top Bottom