Sumu ya sera ya majimbo ya Dr. Slaa na Mbowe kuwaua wabunge wa CHADEMA

mkuu, mbona hujaeleza ni kwa namna gani sera hiyo itafanya kazi kwa tanzania hasa katika wakati huu ambao wanasiasa wamegawanyika kwa misingi ya dini na ukabila?

Hayo ya ukabila na udini kwetu sisi tunayasikia huko MAGAMBANI. Huku vijijini tulipo waislam na wakrito tuna shereheka pamoja na tunahuzunika pamoja. Ni mzaliwa wa Thame, ninaishi tanga na nimeoa mmatumbi.

Udini sijauona na wala ukabila sijautia machoni. Vyote hivyo navisikia kwenye majukwaa kila MAGAMBA wanapo hutubia. Na cha kushangaza hakuna hata mwananchi wa kawaida tunaloliona hilo.

Hilo nadhani mnalo huko ndani MAGAMBANI mwenu.

Kwa ufupi tunachi hitaji ni kupata chama cha siasa kitakacho unda serikali itakayo tutoa hapa tulipo fikishwa na MAGAMBA. Na hakuna chama kingine zaidi ya CHADEMA. Tumezisoma sera zao na tuna hakika wanaweza. Kwani hata viongozi wao wana dhamira ya dhati kuliko chama ambacho kimashakuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 51 lakini hali ndiyo hii ya umasikini uliyo tamalaki.
 
Wadau, hivi karibuni, viongozi wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa walitangaza mpango wa Tanzania kuongozwa katika Mfumo wa Majimbo. Katika nadharia yao hiyo, ni kwamba nchi ya Tanzania itagawanywa katika Majimbo ili kuharakisha shughuli za maendeleo.

Wametolea mfano kuwa mataifa mengi ikiwa ni pamoja na Marekani yameendelea kwa vile kuna majimbo ambayo yana mamlaka ya kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika majimbo yao. Kwa mujibu wa nadharia yao hiyo ni kuwa Tanzania itakuwa na mamlaka mbili za kiutawala.

Kutakuwa na serikali kuu ambayo itakuwa na wajibu wa kushughulikia masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama sambamba na ushirikiano wa kimataifa. Aidha, kutakuwa na serikali za majimbo ambazo zitakuwa na jukumu la kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Katika kutekeleza hilo, CHADEMA wameanzisha kampeni za kueneza hoja yao hiyo kwa wananchi huku ikiwashawishi wakatae raslimali zao kutumika kwa manufaa ya Taifa. Mathalan, baada ya OPERESHENI OKOA KUSINI kutokuwa na mafanikio, viongozi wa CHADEMA waliwashawishi viongozi wa vyama vingine vya upinzani katika mikoa ya Lindi na Mtwara ili waanzishe kampeni ya kupinga mradi wa Taifa wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam chini ya kauli mbiu GESI KWANZA, VYAMA BAADAYE, HAPA HAKITOKI KITU. Kudhihirisha hilo, bendera ya CDM ilipeperushwa wakati wa maandamano yaliyofanyika Desemba 2012 na Januari 2013.

  • Inawezekana kabisa CDM hawana watu wa kutosha wenye sifa za kuunda serikali kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais, waziri Mkuu, mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya n.k na hivyo kuona kama sera hii ni mwarobaini wa kukidhi idadi ndogo kabisa ya watu wenye sifa hizo ukimwondoa Mwenyekiti wa chama ambaye hata elimu yake ya kidato cha nne haioneshi alisoma shule gani, huku uzoefu wake wa kazi ikiwa ni karani wa benki kuu wakati Baba mkwe wake akiwa Gavana
  • Kwa maoni yangu ni kuwa, kitendo cha viongozi wa CHADEMA cha kuigawa nchi ambayo hawana mamlaka nayo ni uvunjwaji wa katiba na sheria za nchi. Kwamba, nchi ya Tanzania kwa sasa inaongozwa kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ambapo ndani ya katiba ya sasa hakuna kipengele kinachoelezea sera ya majimbo. Kwa kitendo cha viongozi wa CHADEMA kuigawa nchi wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria na kama ingekuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kimabavu, Dr Slaa na Mbowe hivi sasa wangekuwa wapo ndani ya magereza yetu wanasubiri hukumu ya kifo kwa makosa yao ya uhaini
  • Hapana ubishi kuwa mikoa kama Dar es salaam, Tanga, Pwani, Lindi na visiwa vya Zanzibar waumini wake wengi ni waislamu, huku mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Manyara waumini wake walio wengi ni wakristo. CDM wameamua kwa makusudi mazima kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini, hoja ambayo wanajaribu kuwa-preempt CCM kuwa ndiyo wanaeneza udini. Hili linafanyika kwa makusudi hasa ukizingatia kuwa wote wanaopiga kelele za kuwa CCM ni wadini wote wamelelewa na kanisa (SLAA, MBOWE, LEMA, MNYIKA n.k), kwa ushahidi tazameni CV zao kwenye tovuti ya bunge mkajionee, hata machapisho yao ni vitabu vya dini.
  • Kuonesha kwa vitendo kuwa ni wadini kwa kuyaenzi maneno yalioko kwenye vitabu vitakatifu kuwa "KILA MTU ATAUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE" kwani sasa ile mikoa ambayo haina maliasili kama mito, maziwa, milima na madini na iko nyuma kimaendeleo iendelee kuwa maskini na ile yenye maliasili na iko mbele kimaendeleo na iendelee tajiri.

Sera ya Majimbo imeanzishwa kama sehemu ya kuingilia tu mwelekeo halisi ni kuigawa nchi kimkoa. Katika maandalizi ya hilo, CHADEMA wameanzisha Tovuti za kimkoa kama vile Mbeya Yetu, Katavi Yetu, Iringa Yetu, Lindi Yetu, Mtwara Yetu, Dar es Salaam Yetu, Arusha Yetu na Zanzibar Yetu. Mitandao hiyo imeratibiwa na kuendeshwa na CHADEMA kwa lengo la kuhamasisha vijana ambao ndio watumiaji wakubwa kuichukia serikali na kujitambua kimkoa chini ya dhana ya WAGAWE UWATAWALE.

  • Katika kuonyesha kuwa dhana yao hiyo haitekelezeki, viongozi wa CHADEMA na hasa FREEMAN MBOWE na dr WILBROAD SLAA wamekuwa wakitumia mapato ya kitaifa ya CHADEMA kuendeleza majimbo yao ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za kijamii kama vile maji na afya huku akina MNYIKA wakitegemea hoja binafsi bungeni na maandamano kuondoa matatizo yanayowakabili hususan tatizo la maji ubungo. Kutokana na hali hiyo, wabunge wengi wa CHADEMA watapoteza majimbo yao katika uchaguzi wa 2015 kwa vile wananchi wanatambua kuwa wabunge hao hawana uwezo wa kuwaletea maendeleo
  • DR SLAA na MBOWE wamekuwa wakihamasisha maandamano katika maeneo mbalimbali nchini kama mkakati mmojawapo wa kutekeleza sera hiyo ya majimbo. Kwa kutambua athari za maandamano, viongozi hao hawajawahi kuitisha maandamano hata siku moja katika majimbo yao. Mathalan, siku chache zijazo, MBOWE ataitisha maandamano mkoani Mbeya kushinikiza DR KAWAMBWA ajiuzuru. Maandamano pia yanafanyika kwenye wilaya moja ya kanda ya ziwa kupinga kitendo cha nguzo za umeme kuanguka wakati wa mvua nyingi.

Federalism or majimbo seems to be the ultimate governance system for Tanzania. Like multi-party-ism, federalism would open avenues for democracy and good governance. The current centralized governance being perpetuated by few elite and corrupt politicians and businessperson has for long time been used to swindle fellow countrymen of monies from other parts of the nation for selfish gain.

Majority who are poor are being denied an opportunity to participate and contribute to national development. Certainly, majimbo would give a chance to each and every Tanzanian to demonstrate and determine varied development initiatives through participation of all including the majority poor.

Those terming the system as tribal or religious are only expressing selfish guilt that they have for selfishly capitalizing on national resources for individual and personal gain.

These rich moguls only wish to maintain the status quo to continue to make Tanzanians become desperate and later on seek sectarian handouts.

The government has been dishing out electoral goodies in form of districts, title deeds, loans and resuscitating failed projects and others at this electioneering period in order to win the hearts of the majority poor. Government has taken advantage of the desperation of Tanzanians to use such a tactic to solicit for votes.

On the other hand, centralized governance in Tanzania has contributed to the increase in the number of slum settlements in urban areas.

Majority are denied employment and resources forcing them to migrate to an urban city like Dar es Salaam to seek employment. Sad still employers take advantage of their desperate states to continue to infringe on their livelihoods. Such immigrants are not provided with decent housing, water, medical care, among others yet the same work very hard to put bread on table.

So many ladies are sexually abused and others become prostitutes due to the hard living conditions. Brothels operated by the rich have become a haven for making money at the expense of the victims who are poor and lack options and opportunities in life. This has exacerbated the speedy spread of HIV/AIDS as many choose to sleep around due to the unbalanced economic classes that the centralized government has created.

Thus majimboism would help reverse this demoralizing trend by availing resources equitably to all regions of the nation. This move would encourage many to leave Dar es Salaam for up country towns that have smaller business centers as a way of easing congestion of rural-urban immigrants of the capital city.

All Tanzanians of goodwill have an opportunity to make other fellow citizens live equitably and with dignity for future development and economic prosperity.

God Bless Tanzania
.
 
Mwanzilishi wa hoja hii ana mapungufu makubwa ya kufikiri na kuchambua hoja bila upendeleo, tafakari na uje na sababu zenye uwiano wa ukweli kuhusu mambo unayolalamika. Bahati mbaya sana hawa unaotaka wsome maada hii wana upepo wa kuelewa, lakini mambo yanaonekana hazarani hivyo kuja na uonga wa kizamani hivyo ni kupoteza muda wako
 
Naskitika sana kuona administrator unaruhusu post ya huyu mbaguzi aneendelea kuigawa mikoa kwa misingi ya udini.
 
ujenzi wa barabara moja ya lami unagharimu zaidi ya shilingi bilioni moja. mapato ya halmashauri nyingi kama za Iramba na Tandahimba HAYAZIDI HATA BILIONI moja. ukichanganya mapato ya mkoa wa Lindi na Mtwara kwa mwaka hayazidi hata bilioni 20. ITAHITAJI MIAKA mingapi kukamilisha ujenzi wa barabara katika maeneo yao? huo ni uhuni na wanachokifanya CHADEMA ni kutaka maeneo ambayo kwa sasa yanaendelezwa na serikali bila ya kubaguliwa yaendelee kuwa maskini.
Barabara moja ya lami ndicho kitu gani, nimekuambia hujui lolote hata maana ya sera ya majmbo hujui ndio maana mnasema sera ya majimbo inavunja katiba ya nchi.
 
watu wengine wanajitokeza kupinga maeneo hayo baada ya kuona sasa kigoma kunawaka baada ya umeme wa uhakika kupatikana au mtwara kunapitika baada ya barabara kujengwa tena kwa mikopo na misaada ya nje

Lete ushahidi wa aliyepinga hapa!......otherwise unatunga maneno tu
 
najua mengi kuhusu taifa hili. Chama kikiongozwa na mbumbumbu wengi matokeo yake ndiyo haya. kuja na sera ambazo hawajazifanyia utafiti wa kina
Kwa hilo nakubaliana nawe Taifa linaongozwa na kiongozi Dhaifu sana hatujapata kuona na nafikiriri haitakuja tokea.
 
Unapoleta hoja kupinga kitu fulani,inabidi uje na hoja za kweli na nzito.sasa thatha wewe una leta hoja ya kitoto kweli ndugu yangu.tambua humu jf wasomi wengi,kwa elimu yangu ya darasa la saba,haki ya mungu haujani convince kuichukia sera ya majimbo.kwanza wewe umeanza kuponda elimu ya mbowe,naomba nikuelimishe elimu ya mbowe has nothing to do with majibo,pili eti cdm hawana watu wa kutawala eg makatibu wakuu rc nk,shame one you simple idiot,hv katibu mkuu si anateuliwa kutokana na elimu yake,kwani mpaka awe chadema.ningeichambua hoja yako yote sema tu natumia simu ka mchina.
 
Hawa ndiyo aina watu tunaowataka humu JF, wenye uwezo wa kupembua na kuchanganua mambo, kuna haja kubwa ya kutafakari kwa kina kuhusu hawa wanasiasa wanakotaka kuipeleka nchi.

kwa upande wa chama kilichokosa ushawishi kama CCM kwenu mwenye propaganda za kipuuzi kama huyo changudoa ni muhimu sana ila kwa chama makini kama chadema tunahitaji vichwa kama akina Dr. Slaa,mbowe,mnyika,lisu na akina mdee na watz wa sasa wanaupeo hao rangi wanaweza kuzitofautisha. pole sana mwana wa kigogo naona tonge kitambo kidogo tu litaingia mchanga
 
Kweli kilaza ni kama sikio la kufa halisikii dawa. Kugawanya mikoa manake unazidi kupeleka maamuzi kwa watu wengi zaidi. Ukanda manake unazidi kulimbikiza maamuzi kwa mtu/kikundi cha watu wachache, don't you see the difference my dear?
Thatha sio kwamba hujui naimani utakuwa umesahau tu, PANYA WENGI HAWACHIMBI SHIMO NA MILUZI MINGI HUMPOTEZA MBWA!!! We are not concerned about the number here, we are concerned about efficiency and effectiveness ya system.

Ili kuwa na maendeleo sio lazima uwe na kundi la viongozi tena wanaofanya duplication of authority/powers. Kumbuka kundi hilo la viongozi wenye madaraka yanayopandiana ndio mwanzo wa kutofanya kazi maana wanacreate kitu kinachoitwa institutional vacuum tena kwa cost kubwa ya walipa kodi.

Unaweza nieleza kazi ya Mkuu wa mkoa, RAS, Mkuu wa Wilaya, DAS, Mkurugenzi wa Wilaya ni nini hasa hapa kwetu??Huoni kama wote hawa wanatumia resources zetu kwa kufanya kazi ya aina moja tu????

Albert Einsten anasema kama ungempa tatizo ili alitafutie ufumbuzi ndani ya lisaa limoja, yeye angetumia dakika 55 kufikiria tatizo halafu angetumia dakika 5 tu kulitafutia ufumbuzi. Mimi naona wewe umetumia dakika 55 kufikiria ufumbuzi na umetumia dakika 5 tu kufikiria tatizo la mfumo wetu wa sasa na ndo maana unaona ni mfumo tunaopaswa kuendelea nao na wala hatupaswi kuuhoji wala kuubadilisha.
 
Federalism or majimbo seems to be the ultimate governance system for Tanzania. Like multi-party-ism, federalism would open avenues for democracy and good governance. The current centralized governance being perpetuated by few elite and corrupt politicians and businessperson has for long time been used to swindle fellow countrymen of monies from other parts of the nation for selfish gain.

Majority who are poor are being denied an opportunity to participate and contribute to national development. Certainly, majimbo would give a chance to each and every Tanzanian to demonstrate and determine varied development initiatives through participation of all including the majority poor.

Those terming the system as tribal or religious are only expressing selfish guilt that they have for selfishly capitalizing on national resources for individual and personal gain.

These rich moguls only wish to maintain the status quo to continue to make Tanzanians become desperate and later on seek sectarian handouts.

The government has been dishing out electoral goodies in form of districts, title deeds, loans and resuscitating failed projects and others at this electioneering period in order to win the hearts of the majority poor. Government has taken advantage of the desperation of Tanzanians to use such a tactic to solicit for votes.

On the other hand, centralized governance in Tanzania has contributed to the increase in the number of slum settlements in urban areas.

Majority are denied employment and resources forcing them to migrate to an urban city like Dar es Salaam to seek employment. Sad still employers take advantage of their desperate states to continue to infringe on their livelihoods. Such immigrants are not provided with decent housing, water, medical care, among others yet the same work very hard to put bread on table.

So many ladies are sexually abused and others become prostitutes due to the hard living conditions. Brothels operated by the rich have become a haven for making money at the expense of the victims who are poor and lack options and opportunities in life. This has exacerbated the speedy spread of HIV/AIDS as many choose to sleep around due to the unbalanced economic classes that the centralized government has created.

Thus majimboism would help reverse this demoralizing trend by availing resources equitably to all regions of the nation. This move would encourage many to leave Dar es Salaam for up country towns that have smaller business centers as a way of easing congestion of rural-urban immigrants of the capital city.

All Tanzanians of goodwill have an opportunity to make other fellow citizens live equitably and with dignity for future development and economic prosperity.

God Bless Tanzania
.

mkuu, hicho ulichoandika ni nadharia tu na ni hisi9a zako wewe binafsi na si mitazamo ya hao wakuu wako akina mbowe na slaa. walianza toka mwaka 2001 wakati walipolitangaza jimbo la Karatu kuwa jimbo la mfano.raslimali za chama zikawa zinaelekezwa huko. wamechimba visima vya maji kwa ruzuku za chama kwa vile mapato ya Halmashauri ya Karatu yalikuwa hayatoshelezi. wamejenga zahanati pia kwa fedha za chama ambazo wanatoa akina SABODO ambao si wenyeji wa maeneo hayo. kwa nini hawajaelekeza nguvu zao Kigoma kwa Zito ambaye ndiye anatunza heshima ya chama hicho. Mbona hawafanyi hayo Kawe kwa Halima Mdee ambaye amekuwa mtetezi mzuri wa chama bungeni. mnabaguana kwenye chama chenu je mkishika dola hali itakuwaje?
 
mleta thread umechambua kisomi! hongera sana! japo napenda mageuzi lkn sera hii haitufai tanzania. to hell with this majimbo policy!
 
hivi kweli wahaya au wasukuma watakubali kupangiwa mambo yao na wachaga?

Dhambi hizi za ukabila na udini ndizo zinazoiua CCM ....msivokuwa timamu hivi wachaga walio ndani ya ccm na wapenzi wa ccm ambao ni wachaga mnadhani hizo kauli zinawafurahisha,maana yake wachaga wasipewe nafasi hata kama wanasifa,je mnadhani kukosa kula za kabila moja zima la wachaga ccm mtakuwa salama,hivi washauri wenu wa siasa wameishiwa mbinu kabisa zisizoweza kuwagawa
 
Nimeisoma makala yako yote lakini hakuna chochote kipya ulichoandika ambacho hakijawahi kusemwa na ccm na kuandikwa kwenye vyombo vya habari vya mitandao ya kijamii, magazeti, vituo vya redio na televisheni.

Jambo moja kubwa nililoliona katika makala hii ya thatha ni kwamba hii makala umeandikiwa na wakubwa wako wa lumumba na kazi yako imekuwa ni kuja kuibwaga tu hapa JF. Kwa muda mrefu ambao nimekuwa nikisoma threads na comments za Thatha hapa JF, hawezi na hajawahi kutoa comment iliyonyooka kama hii makala pamoja na kuwa hoja zote zilizomo ni propaganda tu ambazo zimekuwa ni sehemu ya mikakati ya ccm kujaribu kuidhoofisha Chadema bila mafanikio.

Kawaambie waliokutuma kwamba wenyewe wako macho hawafumbi macho hata sekunde moja.
 
Last edited by a moderator:
Laiti wamama wa Tanzania wanaolala kwenye wodi hizi wenyewe wanaziitaga "Maisha Plus"
wangekusikia mtu kama wewe jichola3 kiukweli wangetamani wakurudishe tumboni ubaki hukohuko,
maana hukustahili kuletwa"

Ni afadhali hii kuliko kuwanza kuwatenganisha kwa misingi ya ukabila, udini na vipato vyao.
 
Back
Top Bottom