mkuu, mbona hujaeleza ni kwa namna gani sera hiyo itafanya kazi kwa tanzania hasa katika wakati huu ambao wanasiasa wamegawanyika kwa misingi ya dini na ukabila?
Hayo ya ukabila na udini kwetu sisi tunayasikia huko MAGAMBANI. Huku vijijini tulipo waislam na wakrito tuna shereheka pamoja na tunahuzunika pamoja. Ni mzaliwa wa Thame, ninaishi tanga na nimeoa mmatumbi.
Udini sijauona na wala ukabila sijautia machoni. Vyote hivyo navisikia kwenye majukwaa kila MAGAMBA wanapo hutubia. Na cha kushangaza hakuna hata mwananchi wa kawaida tunaloliona hilo.
Hilo nadhani mnalo huko ndani MAGAMBANI mwenu.
Kwa ufupi tunachi hitaji ni kupata chama cha siasa kitakacho unda serikali itakayo tutoa hapa tulipo fikishwa na MAGAMBA. Na hakuna chama kingine zaidi ya CHADEMA. Tumezisoma sera zao na tuna hakika wanaweza. Kwani hata viongozi wao wana dhamira ya dhati kuliko chama ambacho kimashakuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 51 lakini hali ndiyo hii ya umasikini uliyo tamalaki.