Sumu ya sera ya majimbo ya Dr. Slaa na Mbowe kuwaua wabunge wa CHADEMA

Wadau, hivi karibuni, viongozi wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa walitangaza mpango wa Tanzania kuongozwa katika Mfumo wa Majimbo. Katika nadharia yao hiyo, ni kwamba nchi ya Tanzania itagawanywa katika Majimbo ili kuharakisha shughuli za maendeleo.

Walau umeelewa umuhimu wake..........ila endelea tu kupinga kwa kuwa wewe ni GAMBA
 
leo ipo kazi na haya maccm si mnaona yalivyotoka humu kuhalalisha upuuz wa mleta mda
Kumbe na wewe umeliona hilo! Nadhan wametumwa sio bure, Ila kwa akili ya maCCM unaweza kuta ni njemba moja mwenye ma ID mengi ameamua kujitekenya na kucheka siku nzima. Ila kwa bahati nzuri hoja zao/zake ni nyepesi na zinahimilika, tutaenda nao/nae mdogo mdogo hadi watapotea, hawa wamesha lose battle, wanang'ang'ana tu ili waonekane wapo. Haya maCCM yamebakia kuwa mapotoshaji tu. Kama ni zile ngumi za utotoni, tunaweza sema sasa hiv yameamua kung'ata. Sioni wakileta mkakati wowote wa chama chao, kazi kubwa kwao imebaki kuwa ni watu wa kupinga tu, inamaana kwao hawana think tanks!!! Shame on them!!
 
mbona mikoa kila siku inagawanywa ....kila kukicha inazaliwa mikoa mipya na wilaya mpya...kama akili yako inafanya kazi kweli mbona husemi kwamba migawanyo hiyo inatugawa kikabila au kidini......maana mpaka sasa iko wazi mkoa kama mbeya- wanyakyusa ,iringa -wanyulukolo,mwanza-wasukuma,kilimanjaro-wachaga n.k mwisho wa siku kila mkoa una kabila fulani kubwa na maisha yanaendelea kama kawaida sijawahi kusikia mtu analalamika mikoa au wilaya zinatugawa kikabila...........uvivu wa kufikiri....

Hii Nchi Ukabila Uko Tangu Enzi za Nyere, Je Mchaga anaweza enda Kugombea Ubunge huko Kagera? Na ishu ya Rasilimali ni Bora Kila Jimbo litumie rasilimali zeke kwa sababu kwa sasa huwezi tofautisha haya

1. Singida Na Shinyanga yenye dhahabu kuna Tofauti?

2. Je Tarime kwenye dhahabu na Muheza Tanga kuna tofauti?

3. Je Kule Mererena kwenye Tanzanite isiyo patika kokote kule kuna tofauti Mpwapwa Dodoma?

4. Je Wananchi wa Ngorongoro kimaisha wanatofautiana na wa Kule Ulambo Tabora?

Kwa Kifupi kwa sasa hakuna tofauti kati ya maeneo yenye rasilimali na maeneo yasiyo kuwa nazo, so ni Bora kila eneo litumie rasilimali zake
 
hapo ndipo kwenye tatizo la uelewa....kuna tofauti kati ya state na constituency....na majimbo kama SIHA,MWANGA, YAMEENDELEA KWA RUZUKU ZA YA CCM AU

wewe unaonaje? nimeeleza tangia mwanzo kuwa kutokana na mfumo kandamizi wa kikoloni, baadhi ya maeneo hasa ya kaskazinI na Dar eslsaam yaliendelezwa kuanzia enzi za kikoloni huku maeneo mengine na hasa ya magharibi na kusini hayakuendelezwa. hata hivyo serikali ilianza kuelekeza nguvu zake katika maeneo hayo ambayo maarufu hujulikana kama maeneo ya pembezoni ambayo hata watumishi huyaona kama ni adhabu wanapopelekwa kufanya kazi. bahati mbaya zaidi wakati serikali ikiendeleza maeneo hayo kwa fedha za serikali kuu kupitia misaada ya wahisani na mikopo, watu wengine wanajitokeza kupinga maeneo hayo baada ya kuona sasa kigoma kunawaka baada ya umeme wa uhakika kupatikana au mtwara kunapitika baada ya barabara kujengwa tena kwa mikopo na misaada ya nje
 
jamani chama changu CCM,chonde chonde acheni kulazimisha udini na ukabila,utalipeleka pabaya taifa,hivi kumbe kuwa mseminari hlafu baadaye ukawa mwanasiasa ni dhambi?mbona unawashambulia waziwazi mbowe,slaa,myika na lema,eti kwa kuwa tu wengi wao wamesoma seminari school,ugawaji wa majimbo,wao cdm wanasema itarahisisha kusogeza hudima kwa watu,ila wewe unataka kupindisha kwa makusudi kwamba kuna kanda za mikoa ya kiislaam kama ulivyotaja,kwa ufupi wewe ndio mdini,na unakipaka matope ccm,kana kwamba ndio waliokutuma,naomba wakukemee,ni mtu wa ajabu sana wewe.
 
Umeandika upuuzi mtupu na zaidi mnaogopa sana harakati za CDM,endeleeni kupumua kimwisho mwisho wababaishaji nyie Magamba
 
Hii Nchi Ukabila Uko Tangu Enzi za Nyere, Je Mchaga anaweza enda Kugombea Ubunge huko Kagera? Na ishu ya Rasilimali ni Bora Kila Jimbo litumie rasilimali zeke kwa sababu kwa sasa huwezi tofautisha haya

1. Singida Na Shinyanga yenye dhahabu kuna Tofauti?

2. Je Tarime kwenye dhahabu na Muheza Tanga kuna tofauti?

3. Je Kule Mererena kwenye Tanzanite isiyo patika kokote kule kuna tofauti Mpwapwa Dodoma?

4. Je Wananchi wa Ngorongoro kimaisha wanatofautiana na wa Kule Ulambo Tabora?

Kwa Kifupi kwa sasa hakuna tofauti kati ya maeneo yenye rasilimali na maeneo yasiyo kuwa nazo, so ni Bora kila eneo litumie rasilimali zake

hayo maamuzi angeyafanya baba wa taifa na wakoloni. sasa mmeenyonya raslimali zetu sasa mnataka muendelee kunufaika na raslimali ambazo haziishi kama mlima kilimanjaro ambao juzi tu umeingizwa kuwa miongoni mwa maajabu saba ya dunia. hovyo. hapa hatudanganyiki na hiyo sera yenu
 
hiyo mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ndiyo imefanya maeneo mengine ya nchi hii kuwa maskini. hivi unakumbuka jinsi Mbunge wa Lindi viti maalum Riziki Lulida alivyoongea kwa uchungu bungeni akielezea jinshi halmashauri za mikoa ya lindi na mtwara zilivyohujumiwa na wachaga? kwa vile wao maeneo yao yameendelea kwa raslimali za taifa wanataka maeneo mengine yaendelee kwa raslimali gani? FIKIRIA KULE MWADUI SHINYANGA, almasi imeisha yamebaki mashimo tu. fikiria kule bulyanhulu na geita, migodi ipo mbioni kufungwa, madini yameisha na bado mikoa hiyo ipo maskini. je sasa watajengwa na raslimali zipi kama si na gesi ya mtwara?
Mkuu hujafafanua vizuri, umesema mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ndio imefanya mikoa mingine kuwa maskini, ukatolea mfano waShinyanga kwenye madini lakini mkoa ni maskini, fafanua sasa mikoa ya Arusha na Moshi imesababishaje hilo, ilikuwa inachukua madini na kuyapeleka moshi au?, kivipi sasa?, Je, sera ya majimbo isingesaidia wasukuma kunufaika na madini?, unataka sasa wasukuma kwa sababu hawajanufaika na madini wanufaike na gesi ya mtwara, wana mtwara wanufaike na nini sasa?, Umesema pia kuwa mikoa ya kusini imehujumiwa na wachaga, kivipi?, hivi kabila fulani linaweza kuzuia mikoa mingine kuendelea?, Je, hii sio propaganda ya kuleta chuki baina ya makabila?, Je, kwa mikoa hasa ya kusini pamoja na kanda ya ziwa kutopata maendeleo pamoja na kuwa na utajiri wa madini katika uongozi wa ccm wa kulaumiwa ni chadema au ccm?, kweli nchi hii tuna viazi, na katika viazi, wewe ni kiazi.
 
  • Thanks
Reactions: Awo
wewe unaonaje? nimeeleza tangia mwanzo kuwa kutokana na mfumo kandamizi wa kikoloni, baadhi ya maeneo hasa ya kaskazinI na Dar eslsaam yaliendelezwa kuanzia enzi za kikoloni huku maeneo mengine na hasa ya magharibi na kusini hayakuendelezwa. hata hivyo serikali ilianza kuelekeza nguvu zake katika maeneo hayo ambayo maarufu hujulikana kama maeneo ya pembezoni ambayo hata watumishi huyaona kama ni adhabu wanapopelekwa kufanya kazi. bahati mbaya zaidi wakati serikali ikiendeleza maeneo hayo kwa fedha za serikali kuu kupitia misaada ya wahisani na mikopo, watu wengine wanajitokeza kupinga maeneo hayo baada ya kuona sasa kigoma kunawaka baada ya umeme wa uhakika kupatikana au mtwara kunapitika baada ya barabara kujengwa tena kwa mikopo na misaada ya nje
Mnaendelea kucheza ngoma ya Chadema bila kujitambua kazi yenu imekuwa kupinga tu good move CDM.
 
Umeandika upuuzi mtupu na zaidi mnaogopa sana harakati za CDM,endeleeni kupumua kimwisho mwisho wababaishaji nyie Magamba

hakuna cha kuogopa kwani kwa sasa CCM ndiyo inaongoza. mtaishia kupiga majungu tu nyinyi watia porojo
 
thatha kwahiyo hata Marekani yenye mfumo wa majimbo hawana watu wa kuongoza? Think Big wewe! Kichwa kina zaidi ya kufuga nywele!
 
Last edited by a moderator:
mbona mikoa kila siku inagawanywa ....kila kukicha inazaliwa mikoa mipya na wilaya mpya...kama akili yako inafanya kazi kweli mbona husemi kwamba migawanyo hiyo inatugawa kikabila au kidini......maana mpaka sasa iko wazi mkoa kama mbeya- wanyakyusa ,iringa -wanyulukolo,mwanza-wasukuma,kilimanjaro-wachaga n.k mwisho wa siku kila mkoa una kabila fulani kubwa na maisha yanaendelea kama kawaida sijawahi kusikia mtu analalamika mikoa au wilaya zinatugawa kikabila...........uvivu wa kufikiri....

Kweli kilaza ni kama sikio la kufa halisikii dawa. Kugawanya mikoa manake unazidi kupeleka maamuzi kwa watu wengi zaidi. Ukanda manake unazidi kulimbikiza maamuzi kwa mtu/kikundi cha watu wachache, don't you see the difference my dear?
 
Kama umeki-tune kichwa chako kuwapigia magoti SLAA na MBOWE utajua mwenyewe na siyo lazima kila mtu awabudu haw akina VASCO DA GAMA hakini ujumbe utakuwa umewafikia na mkae mkijua kuwa mimi na watanzania wote tumewashtukia. Kwa nguvu zote muda utakapofika tutazunguka nchi nzima kuwaeleza mikakati michafu iliyojificha kwenye sera hii dhalimu dhidi ya watanzania.
watanzania hatuwez kuwa wapuuz kiasi hiki hayo n maon yako na familia yako sio watanzania wote
 
Wametolea mfano kuwa mataifa mengi ikiwa ni pamoja na Marekani yameendelea kwa vile kuna majimbo ambayo yana mamlaka ya kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika majimbo yao.-
for a start ni kweli kuwa mfumo wa majimbo unaleta maendeleo tena level ya marekani.

Kwa mujibu wa nadharia yao hiyo ni kuwa Tanzania itakuwa na mamlaka mbili za kiutawala.-
Kutakuwa na serikali kuu ambayo itakuwa na wajibu wa kushughulikia masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama sambamba na ushirikiano wa kimataifa. Aidha, kutakuwa na serikali za majimbo ambazo zitakuwa na jukumu la kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika maeneo yao.
-Kumbe deep down unauelewa mfumo wa majimbo na unajua jinsi nchi zenye akili zilivyonufaika nayo. Sema unajichizisha tu.

  • Inawezekana kabisa CDM hawana watu wa kutosha wenye sifa za kuunda serikali kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais, waziri -Mkuu, mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya n.k-

  • Kweli CDM ikose watu wa level ya Mulugo, Kawambwa, Wassira, Betty Mkwasa, Joel Bendera, JK, et al.????? Kweli??? Alaf mbona hizi ni argument za kitoto sana kuchambua mada... -Jipange upya... Hii very low level...-

    [*]Kwa maoni yangu ni kuwa, kitendo cha viongozi wa CHADEMA cha kuigawa nchi ambayo hawana mamlaka nayo ni uvunjwaji wa katiba na sheria za nchi.-
    nani anamamlaka nayo sasa?? Kikwete?? Mbona amegawa mikoa na kuanzisha mikoa mipya, walaya mpya hamja sema?? Wanachi wa maeneo hayo walishirikishwa? Katiba inampa mtu moja mamlaka yakubadilisha historia single handedly

    Kwamba, -nchi ya Tanzania kwa sasa inaongozwa kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ambapo ndani ya katiba ya sasa hakuna kipengele kinachoelezea sera ya majimbo.-
    So what?? Mbona katiba ya sass hivi haitambui kuwa Raisi wa Zanzibar anaweza kuanzisha wilaya mpya bila ya ruhusa na kushauriana na Raisi wa JMT...? mbons katiba haiitambui katiba mpya ya Zanzibar na inatumika, au Makamo wa Raisi wa kwanza wa Zanzibar na bado anapata heshima za kitaifa? Au hukona yote hayo kabla hujaja kuleta uchambuzi wako hapa

    [*]Kuonesha kwa vitendo kuwa ni wadini kwa kuyaenzi maneno yalioko kwenye vitabu vitakatifu kuwa “KILA MTU ATAUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE” kwani sasa ile mikoa ambayo haina maliasili kama mito, maziwa, milima na madini na iko nyuma kimaendeleo iendelee kuwa maskini na ile yenye maliasili na iko -mbele kimaendeleo na iendelee tajiri.-
Kwani unafikiri maendeleo yanaletwa nakuwa na maliasili tu?? Au ukiwa huna maliasili basi ndo unehukumiwa umaskini..?

[*]Mathalan, siku chache zijazo, MBOWE ataitisha maandamano mkoani Mbeya kushinikiza DR KAWAMBWA ajiuzuru. Maandamano pia yanafanyika kwenye wilaya moja ya kanda ya ziwa kupinga kitendo cha nguzo za umeme kuanguka wakati wa mvua nyingi.-
[/LIST]
Vipi muasisi Mwl Nyerere unafikiri angekuwa ndo Raisi na katiba yenu hii ya CCM Kawambwa angekuwepo
Bado madarakani mpaka sasa?
 
Mnaendelea kucheza ngoma ya Chadema bila kujitambua kazi yenu imekuwa kupinga tu good move CDM.

tumia akili kuelewa wasemacho waungwana.hivi uliwahi kumsikia mbowe na slaa wanaelekeza fedha za ruzuku na misaada wanayopata kupeleka kuendeleza hata ofisi moja nje ya maeneo yao? je unakumbuka ile speech ya mbowe alipomshukuru kikwete kwa kujenga barabara kwenye jimbo lake? msifikirie haya mambo juu juu tu
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza.
 
ujenzi wa barabara moja ya lami unagharimu zaidi ya shilingi bilioni moja. mapato ya halmashauri nyingi kama za Iramba na Tandahimba HAYAZIDI HATA BILIONI moja. ukichanganya mapato ya mkoa wa Lindi na Mtwara kwa mwaka hayazidi hata bilioni 20. ITAHITAJI MIAKA mingapi kukamilisha ujenzi wa barabara katika maeneo yao? huo ni uhuni na wanachokifanya CHADEMA ni kutaka maeneo ambayo kwa sasa yanaendelezwa na serikali bila ya kubaguliwa yaendelee kuwa maskini.
 
Wadau, hivi karibuni, viongozi wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa walitangaza mpango wa Tanzania kuongozwa katika Mfumo wa Majimbo. Katika nadharia yao hiyo, ni kwamba nchi ya Tanzania itagawanywa katika Majimbo ili kuharakisha shughuli za maendeleo.

Wametolea mfano kuwa mataifa mengi ikiwa ni pamoja na Marekani yameendelea kwa vile kuna majimbo ambayo yana mamlaka ya kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika majimbo yao. Kwa mujibu wa nadharia yao hiyo ni kuwa Tanzania itakuwa na mamlaka mbili za kiutawala.

Kutakuwa na serikali kuu ambayo itakuwa na wajibu wa kushughulikia masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama sambamba na ushirikiano wa kimataifa. Aidha, kutakuwa na serikali za majimbo ambazo zitakuwa na jukumu la kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Katika kutekeleza hilo, CHADEMA wameanzisha kampeni za kueneza hoja yao hiyo kwa wananchi huku ikiwashawishi wakatae raslimali zao kutumika kwa manufaa ya Taifa. Mathalan, baada ya OPERESHENI OKOA KUSINI kutokuwa na mafanikio, viongozi wa CHADEMA waliwashawishi viongozi wa vyama vingine vya upinzani katika mikoa ya Lindi na Mtwara ili waanzishe kampeni ya kupinga mradi wa Taifa wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam chini ya kauli mbiu GESI KWANZA, VYAMA BAADAYE, HAPA HAKITOKI KITU. Kudhihirisha hilo, bendera ya CDM ilipeperushwa wakati wa maandamano yaliyofanyika Desemba 2012 na Januari 2013.

  • Inawezekana kabisa CDM hawana watu wa kutosha wenye sifa za kuunda serikali kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais, waziri Mkuu, mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya n.k na hivyo kuona kama sera hii ni mwarobaini wa kukidhi idadi ndogo kabisa ya watu wenye sifa hizo ukimwondoa Mwenyekiti wa chama ambaye hata elimu yake ya kidato cha nne haioneshi alisoma shule gani, huku uzoefu wake wa kazi ikiwa ni karani wa benki kuu wakati Baba mkwe wake akiwa Gavana
  • Kwa maoni yangu ni kuwa, kitendo cha viongozi wa CHADEMA cha kuigawa nchi ambayo hawana mamlaka nayo ni uvunjwaji wa katiba na sheria za nchi. Kwamba, nchi ya Tanzania kwa sasa inaongozwa kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ambapo ndani ya katiba ya sasa hakuna kipengele kinachoelezea sera ya majimbo. Kwa kitendo cha viongozi wa CHADEMA kuigawa nchi wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria na kama ingekuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kimabavu, Dr Slaa na Mbowe hivi sasa wangekuwa wapo ndani ya magereza yetu wanasubiri hukumu ya kifo kwa makosa yao ya uhaini
  • Hapana ubishi kuwa mikoa kama Dar es salaam, Tanga, Pwani, Lindi na visiwa vya Zanzibar waumini wake wengi ni waislamu, huku mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Manyara waumini wake walio wengi ni wakristo. CDM wameamua kwa makusudi mazima kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini, hoja ambayo wanajaribu kuwa-preempt CCM kuwa ndiyo wanaeneza udini. Hili linafanyika kwa makusudi hasa ukizingatia kuwa wote wanaopiga kelele za kuwa CCM ni wadini wote wamelelewa na kanisa (SLAA, MBOWE, LEMA, MNYIKA n.k), kwa ushahidi tazameni CV zao kwenye tovuti ya bunge mkajionee, hata machapisho yao ni vitabu vya dini.
  • Kuonesha kwa vitendo kuwa ni wadini kwa kuyaenzi maneno yalioko kwenye vitabu vitakatifu kuwa “KILA MTU ATAUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE” kwani sasa ile mikoa ambayo haina maliasili kama mito, maziwa, milima na madini na iko nyuma kimaendeleo iendelee kuwa maskini na ile yenye maliasili na iko mbele kimaendeleo na iendelee tajiri.

Sera ya Majimbo imeanzishwa kama sehemu ya kuingilia tu mwelekeo halisi ni kuigawa nchi kimkoa. Katika maandalizi ya hilo, CHADEMA wameanzisha Tovuti za kimkoa kama vile Mbeya Yetu, Katavi Yetu, Iringa Yetu, Lindi Yetu, Mtwara Yetu, Dar es Salaam Yetu, Arusha Yetu na Zanzibar Yetu. Mitandao hiyo imeratibiwa na kuendeshwa na CHADEMA kwa lengo la kuhamasisha vijana ambao ndio watumiaji wakubwa kuichukia serikali na kujitambua kimkoa chini ya dhana ya WAGAWE UWATAWALE.

  • Katika kuonyesha kuwa dhana yao hiyo haitekelezeki, viongozi wa CHADEMA na hasa FREEMAN MBOWE na dr WILBROAD SLAA wamekuwa wakitumia mapato ya kitaifa ya CHADEMA kuendeleza majimbo yao ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za kijamii kama vile maji na afya huku akina MNYIKA wakitegemea hoja binafsi bungeni na maandamano kuondoa matatizo yanayowakabili hususan tatizo la maji ubungo. Kutokana na hali hiyo, wabunge wengi wa CHADEMA watapoteza majimbo yao katika uchaguzi wa 2015 kwa vile wananchi wanatambua kuwa wabunge hao hawana uwezo wa kuwaletea maendeleo
  • DR SLAA na MBOWE wamekuwa wakihamasisha maandamano katika maeneo mbalimbali nchini kama mkakati mmojawapo wa kutekeleza sera hiyo ya majimbo. Kwa kutambua athari za maandamano, viongozi hao hawajawahi kuitisha maandamano hata siku moja katika majimbo yao. Mathalan, siku chache zijazo, MBOWE ataitisha maandamano mkoani Mbeya kushinikiza DR KAWAMBWA ajiuzuru. Maandamano pia yanafanyika kwenye wilaya moja ya kanda ya ziwa kupinga kitendo cha nguzo za umeme kuanguka wakati wa mvua nyingi.

nyinyi si mnasemaga sisiemu itatawala milele sana unalia lia lia nini?,

wakati CDM hawana dola, au umenususa harufu ya CDM kushika dola2015??

kuwa wazi, katika maandiko yako, huweleweki uko wapi?, madhumuni ya post yako nini?? unatoa angalizo??,

tahadhari, ushauri, taarifa, je wewe ni nani??, ni pro cdm au proCCM,

ili kama ni ushauri tujue uelekezwe wapi?? na je nini kifanyike,

vinginevyo unaonekana una wivu wa kike
 
Back
Top Bottom