vinneboy
JF-Expert Member
- Aug 12, 2015
- 478
- 436
- Thread starter
- #21
SORRY MADAM (17)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
. Akiwa gorofa ya kwanza kwenda gorofa ya pili,
akakutana na askari wawili wakishiuka chini,
akaishusha kofia yake chini kidogo, akapisha na
askari hao wakimtazama.
“Ngoja kwanza”
Askari mmoja alizungumza baada ya kushuka
ngazi sita kwenda chini, akatoa picha iliyopo
mfukoni mwake.
“Ndio huyu tunaye mtafuta”
Askari mmoja alizungumza na kuanza kupandisha
kwenda ngazi za juu huku akikimbia, kwa bahati
nzuri akafanikiwa kumuona mzee Godwin
akitembea kwenye moja ya kordo.
“Simama polisii”
Askari huyo alizungumza huku bunduki yake akiwa
amemnyooshea mzee Godwin kwa nyuma.
ENDELEA
“Nyoosha mikono yako juu”
Watu walio karibu na eneo alipo simama Mzee
Godwin pamoja na askari hao walipo nyuma yake
mita chache kutoka sehemu alipo, wakabaki
wakishangaa tukio hilo kwani hawakujua ni kwanini
askari hao wamemshikia mtutu mtu huyo. Taratibu
Mzee Godwin akanyoosha mikono yake juu, huku
akiwa bado hajageuka kuwatazama askari hao.
Askari mmoja akamkonyeza mwenzake amfwate
mzee Godwin, kwenda kumfunga piungu.
Kwa umakini mkubwa askari huyo akaanza
kutembea kwa kunyata huku bunduki yake aina ya
SMG akiwa ameishika vizuri mikononi mwake.
Kitendo cha kumfikia Mzee Godwin, ikawa ni moja
ya kosa kubwa sana, mzee Godwin akageuka na
teke la mguu wa kustoto, lililo mchota askari huyo
miguu yake na kujikuta akianguka kama mzingo na
bunduki yake akiitupia pembeni, kwa uharaka wa
hali ya juu, mzee Godwin, akaichomoa bastola
yake iliyo ichomeka kiunoni mwake kwa nyuma.
Hakuhitaji hata kuwa na huruma na askari aliye
mshikia bunduki, akibabaika. Akapimga risasi moja
ya paja askari huyo, akaanguka huku akilia kwa
uchungu na maumivu makali sana.
Mlio wa bastola yake ukawafanya watu
kutawanyika, si madaktari wala wagonjwa walio
jiweza, kila mmoja akaikoa roho yake, hata
kushangaa kwao kukaingia doa. Askari wengine
walio kuwa kwenye maeneo tofauti ya hospitali,
baada ya kusikia mlio huo wakakimbilia katika
jengo hilo la maabara.
Askari aliye anguka chini, baada ya kuona
mwenzie ametandikwa risasi ya paja na
anaendelea kuhangaika hangaika chini, huku akilia,
akajaribu kurusha teke la chini, ambalo
lilimuangusha mzee Godwin. Askari huyo
akanyenyuka, huku akikunja ngumi, mzee Godwin
akasimama huku akitabasamu, kwani akimuangalia
askari huyo, umri wake wapata miaka ishirini na
tatu hadi tano.
Askari akaanza kurusha ngumi zake, zilizo mkosa
Mzee Godwin, kwani aliweza kuzikwepa zote huku
akiendelea kumuonea huruma kijana huyo. Mzee
Godwin akakimbia kwa kasi, askari huyo akanzanza
kumfukuza, mzee Godwin akafika hadi karibu ya
ukuta, kwa uwezo mkubwa alio kuwa nao
akakanyaga ukutani, na kujigeuza kwa kasi, askari
huyo akakutana na teke zito la kichwa lililo
muangusha chini, na kupoteza fahamu hapo hapo.
“Nice job, kijana”
Mzee Godwin alizungumza huku akijiweka sawa
koti lake. Akiwa katika kordo hiyo, askari mmoja
akajitokeza akiwa na bunduki. Askari akaanza
kufyatua risasi kwa mawenge yaliyo muingia baada
ya kumuona wezake wakiwa wamelala chini,
mmoja akiwa ametulia kimya na mwengine
akiendelea kulia huku damu nyingi zikiwa
zimesambaa kwenye sakafu.
Mzee Godwin, akauvamila mlango ulipo mbele
yake, na kuingia ndani ya chumba hicho, alicho
wakuta madaktari wawili wakiwa wamelala chini ya
meza kwa woga. Mzee Godwin akaufunga mlango
kwa ndani kisha akaichomoa bastola yake.
“Simameni”
Aliwaamrisha askari hao, wakatoka chini ya meza
huku kila mmoja akionekana kuwa ni muoga
kupindukia, kwani haja ndogo ilianza kuitotesha
suruali yake.
“Vueni nguo haraka”
Kila walicho ambiwa ndicho ambacho madaktari
hao waliweza kukifanya, Mzee Godwin naye
akaanza kuvua nguo zake na kubakiwa na nguo za
ndani.
“Wewe kikojozi vaa hizi”
Akamrushia daktari nguo zake, kisha yeye
akachukua nguo za daktari mwengine. Alipo maliza
kuvaa mavazi hayo ya kidaktari pamoja na miwani,
akamuamrisha daktari huyo kuvaa, kofia yake aliyo
kuwa ameivaa.
Gari za polisi wa vikosi vya kutuliza ghasia F.F.U,
zikazidi kuongezeka katika hospitali ya muhimbili,
hii ni baada ya kupata habari kwamba, gaidi Mzee
Godwin ameweza kuonekana katika hospitali hiyo
na kuwashambulia askari wawili. Wananchi walipo
katika eneo la hospitali wakawekwa chini ya ulinzi
mkali, hapakuwa na aliye ruhusiwa kuingia ndani
ya hospitali, wala aliye ndani ya hospitali
hakuruhusiwa kuweza kutoka nje. Hii yote ni
kuhakikisha gaidi wao hajichanganyi na wananchi
na kuweza kutoweka katika eneo la hospitali.
***
Nguvu na umahiri wa kikosi cha bwana Rusev
kikazidi kuongezeka siku hadi siku, akazidi
kuchukua vijana mbali mbali katika mataifa ya
kiafrika, akawaingiza katika kikosi chake ili
kuhakikisha mipango yake anayo ipanga
inakwenda vizuri sana.
“Muheshimiwa mipango yako ni nini?”
Mshauri wake wa karibu alimuuliza bwana Rusev
mara baada ya vijana zaidi ya ishirini kutoka nchi
ya Afrika kuweza kuingizwa kwenye kambi yake,
iliyopo chini ya bahari.
“Nahitaji kuifanya dunia nzima kuwa na kiongozi
mmoja tu, ambaye ni mimi”
“Ila muheshimiwa itawezekana kweli, kutokana
mataifa mengi yana nguvu sana”
“Kwa ukimya ambao tumeufanya tangu kifo cha
Pual Hennry Jr, sasa ninakwenda kuitingisha dunia.
Nahitaji ndoto za Adolf Hitler niweze kuzitimiza
mimi”
Bwana Rusev alizungumza huku akitabasamu.
Akiendelea kuwaangalia vijana hao, wakinza
kupatiwa mafunzo maalumu katika ngome yake,
ambayo ni ngumu sana kwa mtu kuweza
kuifahamu.
Simu ya mshauri wake, ikaingia ujumbe wa video
ulio mstua sana, ikabidi amuonyeshe bosi wake
bwana Rusev.
“RUSEV, RUSEV RUSEV, Umenimiss eheee”
Sauti na sura ya Jaquline, vinaoenekana kwenye
simu hiyo. Bwana Rusev akajikuta akiitumbulia
macho video hiyo aliyo tumwa na muda mchache
ulio pita.
“Huyu Malaya yupo hai?”
Bwana Rusev alizungumza kwa hasira huku
akiendelea kuitazama video hiyo.
“Najua utashangaa, kuniona nipo hai.
Hahahaaaaaa, ngoja niende kwenye point muhimu.
Niliapa kwamba nilazima nitakuua, na hii ni moja
ya ahadi nitakayo ifanya siku na muda wowote.”
“Ila kabla ya kufanya hivyo kutana na mgeni rafiki
yako mpendwa”
Video hiyo ikasogezwa pembeni, ambapo bwana
Rusev akaiona sura ya Agnes akitabasamu.
“Umewaacha wezangu wamekwenda jela kwa ajili
yako, sasa tambua kazi ni moja tu. Tutakupeleka
kuzimu mw………”
Bwana Rusev kwa hasira akaizima video hiyo ya
vitisho kutoka kwa mabinti ambao anawatambua
vizuri sana.
“Muheshimiwa ut…..”
Bwana Rusev akamtandika ngumi nzito mshauri
wake huyo, kisha akaondoka kwa hasira na
kuwafanya baadhiya askari wake kushangaa tukio
hilo.
***
Mzee Godwin kuchungulia dirishani, akaona askari
wengi wakiwa wamemiminika katika eneo la
hospitalini, wakiwa na silaha nzito pamoja na
mbwa wakali.
“Shitii”
Mzee Godwin alizungumza huku akijikuna kichwa
chake
“Shika meza huko”
Aliwaamuru madkatari hao kuisukumia meza hiyo
kubwa kwenye mlango, kwani alihisi muda wowote
mlango unaweza kuvunjwa na askari walipo nje.
“Laleni chini”
Mzee Godwin aliendelea kuwaamrisha madaktari
hao walio tii, kwani pasipo kuweza kufanya hivyo
wanaweza kupoteza maisha yao. Katika
kukichunguza chumba, kwa bahati nzuri akaona
sehemu ya juu kuna sehemu inaweza kufunguka.
“Mukinyanya kichwa tu, ninawapasua ubongo”
Mzee Godwin alizungumza huku akipanda juu ya
meza hiyo, akiendelea kutafuta ni jinsi gani
anaweza kuifungua sehemu hiyo yenye mfuniko
mgumu kiasi. Kwa bahati nzuri akafanikiwa
kufungua mfuniko huo, akachungulia juu ya dari,
akakuta uwazi mkubwa ambao unaweza
kumruhusu yeye kuweza kupita pasipo wasiwasi.
“Hivi ni kwanini tusivunje mlango?”
Askari mmoja alishauri, wezake kwani ni muda
umekatika wamekaa nje ya mlango huo
wakishikilizia kitu kinacho endela ndani.
“Humo ndani kuna madaktari tukifanya hivyo
tunaweza kuwapelekea wakauliwa
“Ila mkuu tutaendela kukaa hapa hadi saa ngapi?”
Hapakuwa na jibu lolote alilo litoa mkuu wao huyo,
anaye hofia maisha ya madaktari hao.
Mzee Godwin akaendelea kufwata njia hiyo iliyopo
juu ya dari, akafanikiwa kufika kwenye moja ya
sehemu yenye upenyo mdogo, akatizama chini na
kugundua ni chumba cha kuhifadhia vitu vya
maabara, akapatizama hapakwa na mtu wa aina
yoyote, Kwa kutumia vidole yake akavingiiza
kwenye matundu madogo ya mfuniko huo kisha
akaufungua, na kuusogeza pembeni. Akashusha
kichwa taratibu na kuchungulia chini, alipo
hakikisha kwamba hakuna mtu yoyote, taratibu
akashuka chini, kimya kimya pasipo kutoa
kishindo cha aina yoyote.
“Shitiii pesa zangu?”
Mzee Godwin akajilaumu sana, kwani kiasi kikubwa
cha pesa amekiacha kwenye koti alilo mvalisha
daktari aliye kuwa akijikojolea kwa woga. Hakuwa
na jinsi tena ya kuweza kurudi katika enoeo hilo,
akachungulia dirishani akakuta eneo hilo lipo kinya,
ila kuna umbali wa gorofa moja chini.
“Hapa nashuka”
Mzee Godwin alijisemea kimoyo moyo, taratibu
akaanza kushuka, kwenye ukuta huo, wenye
vishikizo vidogo vidogo. Akafanikiwa kufika chini.
Sehemu aliyo simama imezungukwa na maua
maua mengi. Akanyata taratibu hadi kwenye
sehemu ya lango la gorofa hilo, akakuta askari
wengi wakiwa wanaendeleza ulinzi.
Akaachana na askari hao, na kuanza kutembele
kuelekea kwenye upande wa jengo la kuhifadhia
damu, akafanikiwa kufika nyuma ya jengo hilo
pasipo kuweza kustukiwa. Akiwa katika
kuchungulai chungulia, akastukia akishikwa bega
kwa nyuma
“Dokta unafany……..”
Baada ya kutazamana na mtu anaye msemesha,
askari huyo akanyamaza gafla, baada ya kugundua
huyo anaye muita daktrai ni gaidi. Mzee Godwin
kwa haraka sana, akaizungusha kwa nguvu shingo
ya askari huyo aliye mtumbulia macho na
kuivunja. Kwa haraka akamvua mavazi askari huyo
na kuchukua nguo zake. Alipo maliza kuvaa nguo
za askari huyo, pamoja na kofia lake aina ya
helment. Akaanza kutembea kuelekea getini kwa
kujiamini sana.
“Vipi unaelekea wapi?’
Askari mmoja alimuuliza baada ya kumuona
akihitaji kufungua mlango wa gari hilo.
“Nahitaji kwenda kuchukua askari wengine”
Mzee Godwin alizungumza huku akibadilisha sauti
yake, kutokana huyo aliye muuliza anacheo
kikubwa zaidi ya mavazi aliyo yavaa, ikambidi awe
mpole kidogo kusikilizia jibu la mkubwa wake
huyo, anaye onekena kuchanganykiwa kidogo.
“Nipeleke kwa waziri wa ulinzi”
“Wapi nyumbani kwake?”
“Ndio muheshimiwa ameniiita”
Mzee Godwin akatii, wakaingia kwenye gari hilo
aina ya ‘Landrove defender’ na kuondoka katika
eneo hilo la hospitalini pasipo hata kustukiwa na
askari yoyote, hata aliiye mpakiza hakuweza
kumtambua.
Kutokana na king’ora alicho kiwasha, magari
mengi barabarani yaliwapisha. Haikuwachukua
muda mwingi sana wakafanikiwa kufika katika
jumba la waziri Eddy, mkuu huyo wa polisi
akashuka na kuelekea katika moja ya hema walilo
kaa viongozi wakubwa. Eddy taratibu akiwa
anatoka sebleni kwake pamoja na Rahab. Macho
yake akaitazama gari ya polisi iliyo fika muda si
mrefu. Askari huyo ambaye ni mzee Godwin
aliyomo ndani ya gari hiyo, alipo yageuza macho
yake kutazama nje yakakutana na Eddy stuka na
kuanza kumtilia mashaka.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 18 YA SIMUHILI HII.