Sorry madam (Destination of my enemies)

SORRY MADAM (53)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Shamsa akajikuta akistuka baada ya kumuona
Phidaya akimfwata katika sehemu alipo shikiliwa
na polisi.
“Hawa ndio majambazi eheee?”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali, askari
mmoja akamuitikia, Phidaya bila hata kujiuliza
mara mbili, akamzaba kofi Shamsa, aliye kuwa
akimshangaa, pasipo kuamini kwamba huyo ni
Phidaya au laa, kwa maana wamefanana kila kitu.
Ilibidi baadhi ya askari wamzuie Phidaya
asiendelea kuwashambulia majambazi hao walio
ivamia hospitali yake.
ENDELEA
Shamsa na majambazi wengine watatu
wakaingizwa ndani ya gari tatu tofauti za polisi,
tukio hilo Sa Yoo aliweza kulishuhudia ila hakujau
ni kitu gani kimetokea hadi Shamsa kukamatwa na
askari, isitoshe akiwa katika mavazi ya unesi,
wakati si mavazi ambayo alikuwa nayo.
Gari za polisi zilizo beba wahalifu zikaondoka Sa
Yoo naye akaingia kwenye gari lake na kuzifwatilia
hadi kituoni. Shamsa na waalifu wengine wawili
wakaingizwa mahabusu, kusubiria mahojiano
yatakayo fwanywa dhidi yao.
Akilini mwa Shamsa kumbukumbu za Phidaya,
zilizidi kujirudia kichwani mwake. Hakuelewa ni
jambo gani ambalo limetokea hadi Phidaya kuwa
hai.
“Au sio yeye?”
Alijiuliza mwenyewe, huku akiwa amesimama
kwenye moja ya kona ya mahabusu, huku
mahabusu wezake wengine wakike wakiwa
wamejilaza, kwenye sakafu.
“Kwa usiku huu hautaweza kumuona”
Askari mmoja alimueleza Sa Yoo, ambaye alihitaji
kukutana na rafiki yake ili amuhoji kuhusu jambo
lililo jitokeza muda mchache ulio pita. Sa Yoo kwa
haraka akampigia simu daktari wa Shamsa,
akamueleza kila kitui kilicho tokea, daktri hiyo aliye
kabidhiwa jukumu la kumuangalia Shamsa, kwa
haraka akafika kituo cha polisi akiwa ameongozana
na mwanasheria wake kuhakikisha kwamba
Shamsa anaachiwa huru.
***
Maisha ya madam Mery yalizidi kuwa mazuri kadri
siku zilivyo zidi kwenda, jeraha la risasi aliyo
pigwa na Manka lilisha pona muda mrefu sana.
Maisha yake aliamua kuyahamishia mkoani
Mwanza, ambapo alifanikiwa kufungua mgahawa
mmoja mkubwa wa kisasa, ambao kwa siku una
uwezo wa kuhudumia wateja mia tisa hasi alfu
moja kwa siku.
Umaarufu wa mgahawa wake uliendana moja kwa
moja na jina lake, jumba kubwa la gorofa la
kifahari, lililopo maeneo ya majango mapya.
Aliliwekea ulinzi mkali kutoka katika mashirika
mawili tofauti yanayo jishuhulisha na ulinzi. Uzuri
wake uliwanyima usingizi wanaume wengi wa jijini
Mwanza, umri wa miaka arobaini na moja alio nao,
kwa haraka haraka ukimtazama utahisi ni
msichana mwenye umri wa miaka ishirini na tano.
Kwa siku hiyo, madam Mery alijawa na furaha sana
moyoni mwake, pale alipo toka katioka banki ya
Bacrays, na kukuta kiasi cha miliomi moja dola za
kimarekani zikiwa zimeingizwa kwenye akaunti
yake hiyo.
“Ranjiti nitakutesa hadi kufa kwako”
Madam Mery alizungumza baada ya kupokea risiti
yake inayo onyesha kiasi hicho kikubwa cha pesa
kikiwa kimeingizwa kwenye akaunti yake. Kwa
mwendo wa madaha akaanza kutembea huku
mlinzi wake wa kike akiwa ameibeba pochi lake
kubwa. Wakaingia kwenye gari, walipo muacha
dereva wake.
“Nirudishe nyumbani nahitaji kupumzika kwa sasa”
“Sawa madam”
Safari ya kutoka benk hadi nyumbani kwake
iliwachukua dakika ishirini, geti kubwa linalo
funguliwa na umeme likafunguka. Gari yake aina ya
Hammer, likaingia na dereva akalisimamisha
kwenye maegesho ya magari, ambapo kuna gari
nyingine nne za kifahari zikiwemo, Range rover
sport, Aud Q7, Ferrari spider na BMW X6. Milinzi
wake kwa haraka akashuka na kumfungulia
mlango.
“Lete tu pochi pumzika”
Madam Mery alizungumza huku akiichukua pochi
yake kwa mlinzi wake huyo, akaelekea ndani, alipo
pokelewa na mfanyakazi wake wa ndani.
“Mama utakula nikuandalie chakula?”
Hapana sijisikii kula”
Kwa furaha ambayo madam Mery anayo,
hakutamani siku hiyo kuweza kuingiza kiu
chochote mdoni mwake, kwani utajiri wake unazidi
kuongezeka mara dufu, akaingia chumbani kwake,
ajitupa kwenye tanda lake kubwa linalo nesa nesa.
“Mery sasa hivi mimi ni milionear”
Alizungumza huku akiliachilia tabasamu lake pana,
akakaa kitako, akaichukua rimoti ya Tv yake kubwa
ilipo ukutani, akaiwasha na kuanza kutafuta chaneli
ambayo ina kipindi kizuri cha kutazama. Chaguo la
chaneli likaangukia katika chaneli ya ITV, ambapo
amekuta mwenyekiti wa chama cha upinzani cha
TDPP(Tanzania Democras People Party), bwana
Kibwila, akizungumza na waandishi wa habari.
Masikio na macho ya Madam Mery yote yakaelekea
kwenye Tv yake, mapigo ya moyo yakaanza
kumdunda pale alipo muona Manka akiwa pembeni
ya kiongozi huyo.
“Huyu mtoto amefwata nini kwenye hichi chama?”
Madam Mery aalijiuliza huku akiongeza kidogo
sauti ya Tv hiyo. Mwenyekiti wa chama hicho
bwana Kibwila, akafikia wakati wa kumtangaza
mgombea uraisi wa chama chake.
“Mgombea wetu atakaye ipeperusha bendera ya
chama chetu atakuwa ndugu Godwin, gererali
mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania”
Madama Mery, akahisi kizunguzungu kikali kikitaka
kumchukua, baada ya kulisikia jina la Mzee
Godwin, kwa kudhibitishiwa kwamba mwenyekiti
huyo hajakosea kabisa, akaonyesha picha ya Mzee
Godwin, hapo ndipo furaha yote ya Madam Mery
ikayeyuka kama barafu liwekwapo juani.
***
Taratibu Rahab akamfikia Raisi Praygod kwenye
mlango alipo simama, kwa haraka akamkumbatia,
na kuanza kumwagikwa na machozi jambo lililo
mshangaza raisi Praygod.
“Mume wangu nisamehe”
Rahab alizungumza huku machozi yakimwagika,
raisi Praygod, alizidi kuendelea kushangaa,
kumuona Rahab akiwa amerejea katika hali ya
kawaida. Rahab, hakusita kuanza kuzinyonya lipsi
za mume wake, joto la hisia za kimapenzi likaanza
kupanda katikati yao. Kila mmoja akajikuta akiwa
na hamu ya kupata penzi la mwenzake, ambalo
walilikosa kwa kipindi fulani. Ndani ya dakika
kadhaa wote wawilili wakajikuta wakiwa hawana
nguo katika miili yao.
Kila mmoja alipo hakikisha kwamba amemuandaa
mwenzake vya kutosha, mechi ikaanza, si raisi
wala Rahab aliye onekana kuchoka, kila mmoja
alihakikisha kwamba anampa mwenzake kile kitu
roho inapenda, huku wote wakiwa wamejawa na
furaha mioyoni mwao.
***
Iliwalazimu Black Shadow kuhamishiwa katika
chumba kingine cha siri, kilichopo chini ya ardhi
ndani ya hospitali hiyo. Kazi hiyo ilifanywa na
dokta Ranjiti na wasaidizi wake, usiku huo huo,
baada ya tukio la uvamizi kutokea katika hospitali
yake. Polisi wakatoa tamko kwa watu ambao
walijitokeza kumuombea shujaa huyo, kwamba
warudi majumbani kwao na kuanzia siku hiyo watu
hawata ruhusiwa kuja kujazana katika hospitali
hiyo, hadi pale afya ya Black Shadow itakapo
imarika.
Lilikuwa ni pigo kwa mashabiki wa Black Shadow,
ila hawakuwa na jinsi, ni lazima waweze kutii
tamko hilo la askari. Ulinzi ukazidi kuimarishwa
kwenye hospitali hiyo, hata dhiara ya raisi,
ikakatishwa hadi pale mambo yatakapo kuja kuwa
sawa ndipo raisi aweze kumtembelea mpiganaji
huyo.
Uwepo wa Black Shadow katika chumba cha siri
ulijilukana kwa watu wachache tu akiwemo
Sabogo, ambaye yeye pekee ndiyo alipewa ruhusa
ya kwenda kumuona Black Shadow katika chumba
hicho. Asubuhi na mapema, Sabogo akawa yupo
ndani ya chumba hicho cha siri kilicho jaa taa
nyingi zenye mwanga mweupe.
Sabogo akatoa kinyago kingine kilicho tengenezwa,
kwa ajili ya Black Shadow, akamvua kinyago cha
mwanzo na kumvalishi kingine kipaya lilicho mkaa
vizuri, alipo hakikisha rafiki yake yupo salama,
akatoka ndani ya chumba hicho na kurudi kwa
daktari mkuu wa hospitali bwana Ranjiti.
“Itamchukua muda gani hadi kupata fahamu?”
“Itamchukua kipindi kidogo, ila kutokana bado
tunaendelea kumuangalia kwa usalama mkubwa,
basi tumuombe Mungu, kila jambo litakwenda
sawa”
“Sawa dokta ila hakikisha kwamba hakuna mtu
ambaye atagundua kwamba yupo chumba cha siri”
“Usijali kwa hilo”
Yote yakiwa yanazungumza ndani ya ofisi ya dokta
Ranjiti Phidaya aliweza kuyasikia akiwa nje ya
mlango, moyo wake ulizidi kumsumbua kila alipo
fikiria juu ya donge nono ambalo polisi
walilitangaza kwa mtu ambaye angelisaidia jeshi
hilo kumkamata Eddy.
Phidaya akarudi kwenye ofisi yake akiwa na
mawazo mengi, akilini mwake akaanza kulifikiria
tukio la jana alipo weza kuiona sura ya Black
Shadow, pili akafirikiria jinsi, majambazi walivyo
vamia kwenye hospitali yake, na kutaka kumuua
Black Shadow.
“Ina maana wanamjua kwamab ni Eddy nini?”
Phidaya alizungumza huku akinyanyuka kwenye
kiti chake na kuanza kuzunguka zunguka ndani ya
ofisi yake.
“Ngoja nikamueleze kila kitu mume wangu”
Phidaya alizungumza, kwa haraka akaanza kupiga
hatua hadi mlangoni kwake, akavuta kitasa cha
mlango huo, akaufungua na kuanza kutembea
kuelekea katika ofisi ya mume wake.
***
Baada ya Sabogo kutoka ofisini kwake, dokta
Ranjiti, akawasha Tv yake, moja ya taarifa aliyo
ikuta ni jinsi hospitali yake ilivyo vamiwa. Ila kati
ya majambazi walio kamatwa, mmoja wao
akamstua kidogo. Akajikuta akisimama kabisa na
kwenda kuikodolea macho Tv hiyo. Jina la Shamsa
Eddy, ndio kabisa zikazidi kumpagawisha. Na moja
ya picha ikapita kwenye taarifa hiyo ya habari jinsi
mke wake alivyo mtandika kofi jambazi huyo wa
kike.
‘Mungu wangu siri inakwenda kufichuka’
Dokta Ranjiti alizungumza huku kijasho kikianza
kumpiga na mapigo yake moyo yakizidi kwenda
mbio. Akaanza kujipapasa kuitafuta simu yake ya
mkononi sehemu alipo iweka, kwa bahati nzuri
akaikuta kwenye koti lake, akaichomoa kwa haraka
na kuminya baadhi ya namba kisha akaiweka
sikioni, baada ya muda ikapokelewa upande wa
pili.
“Ehee mkuu habari yako bwana”
‘Salama vipi dokta nikusaidie nini?’
“Naamini hao majambazi walio kuja kuvamia
hospitalini kwangu wapo mikononi mwako”
‘Ndio na wanaendelea kufanyiwa mahojiano, ila
huyu mmoja wa kike hana hatia ndio tumemuachia
mida hii’
“Mungu wangu…….!!!”
‘VVipi kuna tatizo kwani?’
“Aha…ahaaa hapana”
‘Basi kila litakalo kuwa linaendelea nitakujulisha’
“Sawa mkuu”
Dokta Ranjiti baada ya kukata simu alipo maliza
kuzungumza na mkuu wa kituo cha polisi, akili
yake ikaanza kufanya kazi kama compyuta pale
inapo tafuta, majina yaliyo hifadhiwa kwenye
kumbukumbu zake. Kwa haraka mkumbukumbu
zake zikatua kwenye moja ya mtu ambaye kazi
zake ni umafia na huzifanya kazi za matajiri wengi
ndani na nje ya Japani, pasipo kukosea wala
kukamatwa na askari polisi kutokana na
kujibadilisha badilisha sura na yeye huwa mara
nyingi huwa ndio mtu anaye mfanyia upasuaji wa
kumbadilisha sura.
“Ndio Kim upo wapi?’
‘Yokoma, vipi kuna tatizo dokta?’
“Ndio kuna tatizo bwana, kuna binti anaitwa
Shamsa Eddy nahitaji uweze kumuondoa dunia”
‘Amekufanyaje tena dokta?’
“Ni binti ambaye anaitambua siri ya yangu juu ya
mke wangu Phidaya, si unatambua kwamba huyu
Phidaya ni mwanamke niliye mpora waziri mmoja
nchini Tanzania”
‘Yap nalitambua hilo ulisha wahi kuniambia’
“Ndio basi binti huyo ni kati ya wale majambazi
walio kamatwa jana na polisi na yeye anamtambua
vizuri Phidaya kutokana ni mama yake”
Mazungumza ya simu ya dokta Ranjiti yakamfanya
Phidaya kusimama nje ya mlango, aliweza kusikia
kila kitu alicho kizungumza mume wake, ila
hakuweza kusikia mazungumzo na mtu wa pili.
‘Phidaya kutokana ni mama yake’
Maneno hayo yakaanza kujirudia kwa nguvu akilini
mwake, machozi yakaanza kumlanga lenga
Phidaya, hakuona haja ya kuendelea kukaa
mlangoni mwa mume wake kwa haraka akaanza
kutembea kurudi ofisini mwake. Akaufunga mlango
wake kwa ndani, akavuta kiti chake, akawa kama
mtu aliye changanyikiwa mara kadhaa akijiuliza
maswali mengi kuhusiana na kitui alicho kisikia.
“Shamsa Eddy”
‘Ni binti ambaye anaitambua siri yangu juu ya mke
wangu Phidaya’
Phidaya akajikuta akizidi kuyakumbuka maneno ya
mume wake bwana Ranjiti, kiu na hamu ya
kumuona Shamsa, ikaanza kumjaa moyoni mwake,
kwani anatambu ni kati ya majambazi ambao
walikamatwa jana na ni yule aliye mtandika kibao
jana usiku. Kwa haraka Phidaya akavua koti lake
na kuvaa koti la baridi, akajifutamachozi usoni
mwake, wala hakuhitajki tena kuzungumza na
mumewe kwa kitu alicho wahi kukiona. Kwani roho
ya kumchukia mwanume huyo ilianza kumvaa.
Swali ambalo mara kwa mara alijiuliza kichwani
mwake, kwamba yeye ni nani, taratibu alihisi
linaanza kupata jibu.
“Lazima nijijua mimi ni nani”
Phidaya alizungumza peke yake huku akitembea
kwenye kordo ya kuelekea nje ya hospitali.
***
Kwa juhudi za mwana sheria aliye msimamia
Shamsa, kwenye mahojiano kati yake na polisi,
yalizaa matunda, kwani hadi inatimu alfajiri tayari
Shamsa alionekana kwamba hana hatia kutokana
na maelezo yake aliyo yatoa. Uchunguzi ulio
fanywa kwa nesi ambaye aliuawa na Shamsa,
ulionyesha kwamba hakuwa ni nesi wa hospitali
hiyo kutokana na kukutwa na michoro mingi
(tattoo) mwilini mwake.
Pia katika kubanwa kwa waalifu wawili wa kiume
walio kamatwa, walidhibitisha kwamba Shamasa
sio mwenzao, hilo pia lilichangia kwa Shamsa
kuachiliwa huru.
“Inabidi sasa twende nyumbani ukapumzike”
Sa Yoo alizungumza mara baada ya Shamsa
kuachiliwa huru, kwani naye pia alishinda kituoni
hapo kuhakikisha kwamba rafiki yake anaachiwa
huru.
“Hapana nahitaji kwenda hospitali kumuona Black
Shadow ndio niweze kwenda nyumbani’
Kutokana Shamsa ni mtu wa kung’ang’ania
maamuzi yake mwanzo mwisho, Sa Yoo na daktari
hawakuwa na hiyana zaidi ya kuanza safari
kuelekea katika hospitali aliyo lazwa Black
Shadow. Akilini mwa Shamsa hakumfikiria Phidaya
kutoka alihisi labda alimfananisha, isitoshe tayari
walisha mzika mama yeka huyo. Kutokana ni
asubuhi, barabara ilijaa foleni nyingi, kwa hiyo
iliwachukua muda mwingi sana hadi kuweza kufika
katika hospitali hiyo. Wakiwa getini, wakapishana
na gari aina ya Aud A4. Hakuna aliye weza
kuifwatilia sana, haswa Shamsa ambaye muda
wote alimuwaza Black Shadow wake.
Wakaegesha gari walilo jia kwenye maegesho ya
hospitalini hapo, Shamsa akawa wa kwanza
kushuka kwenye gari huku akifwatiwa na Sa Yoo
pamoja na daktari wake.
Kila nesi aliye muona Shamsa, alijikuta
akimuogopa sana, kwani kila mmoja anatambua ni
miongoni mwa majambazi walio sababisha kifo
cha nesi mwezao aliye pigwa risasi jana usiku
akijaribu kuyaokoa maisha yake.
“Daktari mkuu yupo wapi?”
Sa Yoo alimuuliza nesi wa mapokezi, aliye baki
akimtumbulia macho Shamsa asijue ajibu nini.
“Dada nakuuliza daktari mkuu bwana Ranjiti yupo
wapi?”
“Ahahaa ameetoka”
“Una uhakika?”
Shamsa alimuuliza nesi huyo huku akiwa amekazia
jicho.
“Yupo ofisini kwake”
Sa Yoo alijikuta akiangua kicheko, baada ya
kumuona nesi huyo akiwa anababaika babaika,
wote watatu wakamuaga nesi huyo na kuelekea
katika ofisi ya bwana Ranjiti.
***
Gafla Phidaya akajikuta akifunga breki za gari lake,
alihisi kama mtu aliye muona kwenye gari aliyo
pishana nayo getini, hajakosea.
”Ndio yeye”
Alizungumza huku akikunja kona ya haraka na
kunza kurudi hospitalini kwa mwendo wa kasi,
haikumchukua muda tayari akawa amesimama
kwenye geti la kuingilia hospitalini kwake. Askari
wakamfungulia geti hilo kuwa, kwa haraka
akalisimamisha gari lake kwenye maegesho, kisha
akashuka na kuanza kutembea kwa kasi kuelekea
ndani. Akakuta manesi wa mapokezi wakiwa
wanajadiliana kitu, walipo muona kila mmoja
akajifanya kama anaendelea na kazi zake.
“Kuna nini hapa?”
“Hakuna kitu madam”
“Muna nidanganya eheee?”
“Madama kusema kweli yule jambazi wa kike
amekuja tena, na sasa hivi ameelekea ofisini mwa
mume wako”
“Muna sema kweli?”
“Ndio”
Phidaya akaanza kukimbia kuelekea ofisini mwa
mume wake na kuwaacha manesi hao
wakimshangaa boasi wao, Phidaya bila hata
kubisha hodi akaufungua mlango wa ofisi ya mume
wake, macho yake yakagongana na macho ya
Shamsa, aliye aliye geuka kutazama mtu aliye ingia
ndani ya ofisi ya daktari bila kubisha hodi.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 54 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (54)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Akakuta manesi wa mapokezi wakiwa
wanajadiliana kitu, walipo muona kila mmoja
akajifanya kama anaendelea na kazi zake.
“Kuna nini hapa?”
“Hakuna kitu madam”
“Muna nidanganya eheee?”
“Madama kusema kweli yule jambazi wa kike
amekuja tena, na sasa hivi ameelekea ofisini mwa
mume wako”
“Muna sema kweli?”
“Ndio”
Phidaya akaanza kukimbia kuelekea ofisini mwa
mume wake na kuwaacha manesi hao
wakimshangaa boasi wao, Phidaya bila hata
kubisha hodi akaufungua mlango wa ofisi ya mume
wake, macho yake yakagongana na macho ya
Shamsa, aliye aliye geuka kutazama mtu aliye ingia
ndani ya ofisi ya daktari bila kubisha hodi.
ENDELEA
Macho yakamtoka dokta Ranjiti, akimkodolea mke
wake. Phidaya akamtizama kwa muda Shamsa
kisha akapiga hatua hadi alipo kaa mume wake,
akambusu shavun kisha akawasalimia wageni alio
wakuta ndani ya chumba hicho, hapo ndipo
Shamsa alipo amini kwamba huyu si Phidaya
anaye mtambua, na Phidaya alisi walisha mzika.
“Kama nilivyo waeleza, kwa sasa hatuto ruhusu
mgonjwa kuonewa na mtu wa aina yoyote,
kutokana na tukio ambalo limejitokeza jana”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akiwataza Shamsa
na Sa Yoo pamoja na daktari wa Shamsa.
“Ila dokta kumbuka pasipo mimi, jana Black
Shadow, angefariki dunia je mungekuwa na lipi la
kuzungumza katika jamii, ni kwamba ulinzi wenu ni
wakipumbavu ehee”
Shamsa alizummgumza kwa hasira, kila mmoja
ofisini hususani dokta Ranjiti alibaki kimya.
“Samani binti kwani huyo Black Shadow ni nani
kwako?”
Phidaya alizungumza kwa sauti iliyo zidi
kumchukiza Shamsa.
“Hakuhusu”
“BInti jibu lako lingekuwa ni msaada kwako, ila
kama hayanihusu sawa”
“Hembu sikiliza wewe mwanamke, hunijui na wala
hunitambu vizuri mimi, nimehatarisha maisha
yangu kwa ajili ya mpenzi wangu, kwa hiyo kaa
mbali na mimi”
Shamsa alizungumza huku akisimama, kwa jazba
hadi Sa Yoo na daktari wakamzuia.
“Ahahaa kumbe ni mpenzi wako ni kitu gani
ambacho kinakufanya unapanic, wenye maamuzi ni
sisi, unaweza kumuona huyo Black Shadow au
usimuone sawa binti”
PPhidaya alizungumza huku akimpandisha na
kumshusha Shamsa, aliyezidi kukasirika akarusha
kibao ambacho Phidaya aliweza kukiona na kurudi
nyuma.
“Weweeeee unataka kunipiga”
Phidaya alizungumza huku akijiweka sawa kwa
mashambulizi, kwa haraka dokta Ranjiti
akamshikilia mkewe. Sa Yoo na daktari kazi ikawa
ni kumshikilia Shamsa.
“Phidaya mke wangu tuilia basi, mbona unataka
kunidhalilisha mbele za wageni”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya ukali. Jina
la Phidaya likamstua Shamsa na kujikuta hasira
yake ikishuka, kwa haraka akili yake akaipelekea
katika kumchunguza Phidaya kuanzia juu hadi
chini, hakuwa na tofauti yoyote na mama yake
waliye mzika. Shamsa alipotaka kuzungumza kitu
kwa haraka Phidaya akamkonyeza pasipo dokta
Ranjiti kumuona, mkonyezo huo ndio ukampa
Shamsa ishara kwamba huyo ni Phidaya mama
yeke, kwani ni mara kadhaa Phidaya alitumia
kuwakonyeza yeye na Juio, pale anapo waaga
kwenda mahali fulani.
“Phidaya mke wangu nakuomba uende ofisini
kwako tafadhali”
“Nakwenda ila wageni kama hawa sihitaji kuwaona
kwenye hospitali yetu”
“Sawa mke wangu nimekuelewa”
Phidaya akatoka na kuwaacha watu wote ndani ya
ofisi wakikodolea macho hadi alipo ufunga mlango
wake. Dokta Ranjiti akashusha pumzi nzito na
kukaa kwenye kiti chake, ikambidi achukue rimoti
na kuongeza upepo mzuri(A.C).
Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita baina yao,
ikabidi dokta Ranjiti kuuvunja ukimya huo.
“Naombeni munisamehe kwa yale yaliyo tokea kwa
mke wangu”
“Hakuna tatizo si unajua mambo ya wanawake
bwana”
“Kweli wanawake ni viumbe ambao tunatakiwa
kuishi nao kwa akili sana”
“Hembu acheni unyanyapaaji wenu, nyinyi pia
munatakiwa tuishi na nyinyi kwa akili”
Sa Yoo alichangia mada ya madaktai wawili hao,
muda wote Shamsa alimuwazia Phidaya, alama
zote ambazo Phidaya alikuwa nazo, huyu naye pia
anazo. Swali imekuwaje kuwaje hadi awe hai, pili
imekuwaje hadi aolewe na dokta Ranjiti.
‘Kuna kitu’
Shamsa alijisemea kimoyo moyo, akainyanyua sura
yake na kumtazama dokta Ranjiti, jinsi anavyo
zungumza na daktari mwenzake pamoja na Sa
Yoo.
‘Huyu kuna jambo analificha’
“Shamsa, Shamsa, Shamsa”
Sa Yoo aliita, ikabidi amtingishe kidogo Shamsa,
maana hakusikia jinsi anavyo muita.
“Eheeee…..”
“Vipi mwenzetu haupo nasi”
“Ahaa hamna, mumefikiwa wapi?”
“Tumekubaliana na daktari kwamba mgonjwa
atakapo zinduka basi atatupigia simu na kuja
kumuona”
“Ahaaa sawa”
Wakaagana na dokta Ranjiti, huku Shamsa
akiendelea kukiumiza kichwa chake kwa maswali
lukuki kuhusiana na mama yake huyo. Wakatoka
nje ya ofisi hiyo, wakiwa wanasindikizwa na dokta
Ranjiti jambo ambalo si lakawaida kwa daktari
huyo kulifanya kwa wageni wake.
Akawasindikiza hadi sehemu ya maegesho ya
magari ambapo Shamsa, Sa Yoo na daktari wao
wakaingia ndani ya gari hilo na kumuacha dokta
Ranjiti akiwasindikiza kwa macho.
Mambo yote yaliyo kuwa yakifanyika, Phidaya
aliweza kuyaona akiwa amesimama dirishani,
machozi yalimwagtika kumuona binti anaye
utambua ukweli kuhusu yeye akiwa anaondoka
katika eneo hilo la hospitali.
‘Ohh Mungu wangu nisaidie nikutane naye tena’
Phidaya alizungumza huku akilishuhudia gari hilo
likitoka getini na kuingia kwenye barabara yenye
magari mengi sana na kutokomea kwenye upeo wa
macho yake.
“Ina maana hawajatambuana?”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akiwa anarudi
ndani kwenye ofisi yake, hakuhitaji kuyapa mawazo
yake asilimia mia moja kwamba hawajafahamiana.
Nafasi nzuri aliyo kuwa nayo kwa sasa ni
kuhakikisha kwamba maisha ya msichana huyo
yanatoweka dunia. Kutona na akili yake kuto kuwa
sawa hakuona haja ya kuendelea kukaa hospitalini
kwake, akampigia simu Kim, waonane kwenye
moja ya mgahawa. Dokta Ranjiti akiwa anatoka,
akakutana na Phidaya mlangoni.
“Vipi baby unatoka?”
“Ndio kidogo kuna mtu nahitaji kwenda kuonana
naye”
“Wapi?”
“Ahaa ni hapa hapa mjini, kukiwa na tatizo nipigie
nitakuja”
Dokta Ranjiti akambusu Shamsa mdomoni na
kuanza kutembea kwa mwendo wa kujihami hami
kwa mara kadhaa aligeuka nyuma na kumtazama
mke wake, ambaye aliendelea kumtazama kwenye
kordo hiyo ndefu hadi pale alipo kunja kona na
kuingia kwenye lifti.
“Kuna kitu anahitaji kukifanya huyu”
Phidaya alizungumza huku akiwahi kuingia ofisini
kwake kwenye dirisha lililo elekea kwenye
maegesho ya magari. Dakika moja mbeleni
akamuona mume wake akiwa anaingia kwenye gari
lake na kuondoka hospitalini hapo. Kwa haraka
akakaa kwenye kiti chake na kuifungua laptop yake
aina ya ‘Mac Book Air’. Akaingia kwenye moja ya
mtandao ambao unaweza kukupa ramani ya gari
unalo hitaji kujua linakwenda wapi, ikakuonyesha
kupitia satelaiti. Huduma hiyo ya haraka, Phidaya
aliweza kujibiwa kila kitu na ndani ya dakika mbili,
ramani iliyo jitokeza kwenye kioo cha lapotop yake
hiyo, alama nyekundu ilionekana ikiashiria ndio
gari la mume wake, linavyo tembea.
Kwa haraka Phidaya akatoa simu yake na kumpigia
kijna wake aitwaye Lee Si.
“Kuna ramani nakutumia hakikisha kwamba
unalifwatilia gari la mtu huyo na hadi sehemu
anapo ingia hakikisha kwamba unmfwatilia”
“Sawa madama”
“Ila hakikisha muhusika hatambua kwamba
unamfwatlia?”
“Sawa madam”
Phidaya akaituma ramani hiyo kwa kijana wake
ambaye mara nyingi huwa anamtumia katika
maswala yake binafsi ikiwemo ulinzi wake, pale
anapokuwa anakwenda katika sehemu za mbali.
***
Karibia umma wa Watanzania wote walijikuta
wakipigwa na butwaa, baada ya chama pinzani cha
TDPP(Tanzania Democras People Party),
kumsimamisha Mzee Godwin, wapo wananchi
walio mkubali kutokana na kusikiliza vizuri hotuba
ya mwenye kiti wa chama hicho bwana Kibwila,
akimuelezea Mzee Godwin kuanzia mwanzo wa
matatizo yake hadi mwisho, huku akilaumu
kwamba matatizo yote hayo yamesababisha na
waziri mkuu mstaafu aliye kuwa mke wake.
Wananchi wengi wakatokea kuhuzunishwa na
historia hiyo ambayo imetengenezwa huku vitu
vichache sana vikiwa na ukweli ndani yake.
Mgawanyiko wa kisiasa ukaanza kutokea ndani ya
chama tawala cha TSD(Tanzania Society
Development), viongozi wa ngazi za juu mmoja
baada ya mwengine akaanza kuhamia katika
chama cha upinzani cha TDPP. Wengi wao wakiwa
ni wanachama wa siri wa kundi la D.F.E(Destinati
on of my Enemies). Wananchi pasipo kujielewa
husasani vijana wakajikuta wakiwafwata viongozi
walio kuwa wakiwapenda na kujiunga na chama
pinziani.
Maelefu ya wananchi wakaingia katika chama cha
DTPP. Hali ya kiasiasa ikazidi kuwa tumbo joto
kwa chama tawala cha TSD. Wananchi wengi walio
kusanyika katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es
Salaam, wakiwa ni wanachama wa chama cha
DTPP, hamu yao kubwa waliyo nayo ni kumuona
mgombea wao uraisi Mzee Godwin. Helcoptar
zipatazo nne, zikatua kwenye viwanja hivyo, huku
helecoptar moja ikiwa imewabeba Fetty, Halima,
Anna. Agnes, Jackline na Manka wote wakiwa
wamevalia suti nyeusi, miwani nyeusi, gloves
nyeusi na kila mmoja aliweza kuichomeka bastola
yake kiunoni mwake na kuifunika na koti lake.
Fetty na Halima wakaisogelea helcoptar aliyo
panda mzee Godwin, wakafungua mlango. Mzee
Godwin akavuta pumzi nyingi kisha akashuka.
Wananchi wengi wakaanza kumshangilia kwa
furaha, Manka na wezake wote wakamzunguka na
kumuwekea ulinzi, ambao kila mtu alifurahia kuona
walinzi wa kiongozi huyo wakiwa ni wanawake
shupavu.
Mzee Godwin akaanza kuwapungia wananchi
mkono kila alipokuwa anakatiza, wamama, vijana
na wababa walijitokeza katika viwanja hivyo huku
kauli mbio ya chama hicho ikisema kwamba
TUNATAKA MABADILIKO.
Mzee Godwin akapokelewa na viongozi wa chama
hicho, ambao wengi wao leo ndio waliweza kumtia
machoni mwao. Kwa nguvu kubwa ya pesa aliyo
kuwa nayo mzee Godwin basi hapakuwa na
kiongozi ndani ya chama aliye weza kwenda naye
kinyume hata kidogo, kwani kila mmoja alipenda
pesa yam zee Godwin, ili ajikimu kimaisha yeye na
familia yake.
Manka na wezake, wakasimama jukwaa zima
wakiimarisha ulinzi kwa Mzee Godwin, macho yao
yote yalikuwa yakitazama tazama kila kona
kuhakikisha kwamba hakuna jambo baya ambalo
litampata kiongozi wao huyo.
***
Macho ya Rahab hayakung’atuka kwenye kioo cha
Tv kubwa iliyopo sebleni, viongozi kadhaa
akiwemo mume wake, nao waliweza kukusanyika
katika sebule hiyo ya ikulu kufwatilia mkutano
mkubwa wa chama cha upinzani. Rahab aliweza
kuwatambua wezake vizuri na hakuhitaji
kuzungumza chochote kwa viongozi waliomo ndani
ya seble hiyo wakifwatilia mkutano huo. Kwani
wengi wao wanatambua wasichana walio kuwa
magaidi walisha fariki wakiwa mikononi mwa jeshi
la Wamarekani.
“Mkuu wanaonekanawamejipanga sana hawa”
Makamu wa raisi alimuambia raisi Praygod
ambaye muda wote aliendelea kuikazia macho Tv
hiyo.
“Ni kweli, ila na sisi inatubidi tujipange sana, kwa
maana safari hii wananchi wana uelewa mkubwa”
“Kweli muheshimiwa”
“Ila huku kiongozi wao si mtuhumiwa?”
“Ndio ni mtuhumiwa ila kwa sasa vithibitisho vya
kumkamata hatuna, tayari amesha watek watu
wengi”
“Kazi ipo”
“Ila niwatoe hofu, lazima tutashinda kwa maana
wananchi bado wanaimani na sisi”
“Kweli kweli”
Viongozi wengine wakajikuta wakipiga makofi,
wakimpongeza mwenyekiti wao wa chama kwa
kauli aliyo izungumza.
Kichwani mwa Rahab, akawa anachanganua ni jinsi
gani anaweza kukutana na rafiki zake hao pasipo
kustukiwa, isitoshe kwa wakati huu ulinzi juu yake
umeimarishwa kupita maelezo. Wakaendelea
kutazama mkutano huo unao rushwa moja kwa
moja kwenye televishion ya Star Tv, hadi ukaisha.
Raisi Praygod wakamuomba Rahab awapishe ili
wazungumze mambo ya kufanya katia wakati huu
mgumu wa kuelekea kampeni.
Ikawa ni nafasi kwa Rahab, akaingia chumbani
kwake, akavaa sweta jeusi pamoja na suruali
nyeusi, akachukua miwani nyeusi, kisha chini
akapigilia viatu virefu vya kisasa aina ya Travota.
Alipo hakikisha kwamba yupo poa, akatoa simu
yake na kumpigia Priscar.
“Andaa gari binafsi nahitaji kutoka, nilikute nje ya
ikulu”
“Sawa mdam”
Rahab akatoka chumbani kwake huku miwani akiwa
ameificha kwenye mfuko wa sweta lake,
akafanikiwa kutoka nje pasipo mume wake
kumuona, kwani aliweza kuwapita sebleni na
kuwakuta wakiwa katika mjadiliano mkali sana.
Akatembea hadi kwenye geti la kutoka nje ya ikulu.
“Madam ni jukumu letu kuhakikisha kwamba
tunakulinda kila unapo kwenda”
Mlinzi wake mpya mmoja alizungumza.
“Hata nikienda chooni pia munataka kunilinda
humu ndani?”
“Hapana sio hivyo madam”
“Sikieni mimi ninakwenda kukimbia kimbia sihitaji
ulinzi kwa maana ninaweza kujilinda mwenyewe
sawa”
Rahab alizungumza kwa sauti ya ukali hadi walinzi
wake hao wakatingisha vichwa kwamba
wamemuelewa, akatoa nje ya geti na kuanza
kujifanya kama mtu anaye fanya mazoezi ya
kukimbi, alipo kunya kona akalikuta gari jeusi aina
ya KIA likiwa limesimamishwa.
Akalifwata akafungua mlango na kuingia, akamkuta
Priscar akiwa amejiandaa, kwa safari atakayo
ambiwa na bosi wake huyo.
“Twende hapo Serena”
“Sawa madam, ila leoumetokelezea”
“Hahaa, usiniambie”
Rahab alizungumza huku akiwa anajitazama
kwenye kioo cha pembeni cha gari hilo,
akatabasamu kweli alipo jiona amependeza na si
rahisi kwa mwananchi wa kawaidia kuweza
kumtambua kwamba ni mke wa raisi.
Hawakuchukua muda sana kufika katika hoteli ya
Serena, akashuka na kuanza kuelekea mapokezi
huku akimuomba Priscar amsubirie ndani ya gari.
“Chumba walichopo walinzi wa mzee Godwin ni
kipi?”
Rahab alimuuliza msichana wa mapokezi aliye
onekana kumkodolea macho, ikambidi Rahab
kuivua miwani yake, hapo kidogo msichan huyo
wasiwasi ukamtoka baada ya kugundua kwamba ni
mke wa raisi.
Akamtajia namba ya chumba ambacho walinzi wa
mzee Godwin wapo, Rahab akaingai kwenye lifti,
akapandisha hadi gorofa ya nne. Akaanza
kutembea kwenye kordo moja nzuri iliyo pabwa na
vioo katika kuta zake. Akafika hadi kwenye mlango,
wa chumba alicho ambiwa na muhudumu,
akagonga mara mbili, mlango ukafunguliwa.
Mtu aliye simama mbele yake, Rahab alimtambua
vizuri sana kwani ni Fetty, taratibu Rahab akavua
miwani yake na kofia la sweta lake.
“What………..!!!!”(Nini……….!!!)
Fetty alizungumza huku akitoa macho ya
mshangao, Rahab akaanchia tabasamu pana,
sekunde kadhaa wakajikuta wakikumbatiana kwa
furaha. Wakaingia ndani, Halima, Anna na Agnes
walipo muona Rahab wakawa kama
wamechanganyikiwa, kila mmoja akaacha alicho
kuwa anakifanya na kwenda kumrukia rafiki yao
huyo waliye potezana naye miaka mingi ya nyuma.
Machozi ya furaha, yaliwatawala kati yao, wote
watano wakajikuta wakikumbatiana kwa pamoja,
jambo lililo wafanya Manka na Jaqline wabaki na
mshangao.
***
Kwa mbali macho ya Eddy yaliyo jaa, ukungu
yakaanza kufunguka. Akaanza kujitahidi kutazama
kwamba ni wapi alipo, ila mwanga mkali wa
sehemu aliyopo, hakuweza kupata jibu. Akajitahidi
kufumbua macho yake kabisa akafanikiwa,
akakigeuza kichwa chake kushoto mwa kitanda
alicho lala, akaona mashine za kupumulia pamoja
na dripu moja la maji, likiwa limening’inizwa juu
kidogo. Akilini mwake akatambua kwamba sehemu
hiyo aliyopo ni hospitalini. Kumbukumbu zake za
mwisho zikampeleka uwanjani, alipo kuwa
akipambana na mpiganaji hodari Young Po.
Akajaribu kunyanyuka ila maumivu makali katika
mbavu zake yakamfanya arudi tena kulala.
Phidaya baada ya kukaa ofisini mwake kwa muda
akaamua kwenda katika chumba cha siri
kumtazama mgonjwa ambaye ni mpenzi wa binti
anaye fahamu ukweli kuhusu yeye. Phidaya
akashuka kwa kutumia lifti hadi chini kabisa ya
chumba hicho akiwa amevalia koti lake yeupe.
Akapiga hatua hadi kwenye mlango wa chumba
hicho akaufungua kidogo ila simu yake mkononi
ikaita. Akakuta ni namba ya kijana wake Lee Si
aliye mpa kazi.
“Umefikia wapi?”
‘Nimeweza kumuona katika mgahawa akizungumza
na mwanaume mmoja anaye onekana ni hatari
sana’
“Ulifanikiwa kuyasikia mazungumzo yao”
‘Ndio nilisikia akipmpa kazi ya kutaka kumuua binti
anaye itwa Shamsa’
“Anataka kumuua Shamsa…..?”
Sauti ya Phidaya ilijipenyeza hadi ndani ya chumba
alicho lazwa Black Shadow. Sauti hiyo haikuwa
ngeni masikioni mwa Eddy, ni sauti ya mke wake
Phidaya, aliye fariki mwaka mmoja nyuma.
‘Au nipo peponi?’
Eddy alijiuliza maswali huku akijitahidi kutega sikio
lake, ila alipo sikia Phidaya anataja jina la Shamsa,
akajihakikishia kwamba yupo dunia, hamu yake
ikawa kubwa ni kumuona mwanamke huyo anaye
zungumza na simu nje ya chuma alicho lazwa.
“Hakikisha unamfwatilia huyo mtu na unanipa
ripoti”
‘Sawa madam’
Phidaya akakata simu, hakuona haja ya kuingia
tena ndani ya chumba hicho kwani taarifa aliyo
pewa imemchanganya, kwani binti anaye muhitaji
ili apate kutambua ukweli wa yeye ni nani, maisha
yake yapo hatarini. Akaanza kupiga hatua kuelekea
kwenye lifti ila kabla hajafika mbali akasikia kitu
cha bati kikianguka kutokea ndani ya chumba cha
mgonjwa, akaanza kurudi kwa kasi na kukuta
mlango aliusahau kuufunga, kwani aliufungua
kidogo kabla ya kupokea simu. Akaufungua mlango
na kuingia ndani, akakuta bomba la kusimamishia
dripu likiwa limeanguka chini, huku mgonjwa akiwa
naye ameanguka chini, akiugulia maumivu
“Mungu wangu…..!! Umezinduka?”
Phidaya alizungumza huku akipiga magoti chini,
akakinyanyua kichwa cha Black Shadow, akakiweka
kwenye mapaja yake, akijaribu kumpa huduma ya
kwanza mgonjwa, macho ya Eddy yaliyo jaa
machozi ya maumivu makali ya mbavu zake zilizo
piga chini, alipo kuwa akijaribu kunyanyuka
kitandani ili kumuona mwanamke mwenye sauti ya
inayo fanana na Phidaya, yakatua usoni mwa nesi
huyo, akajikuta akistuka kwani ni Phidaya
mwenyewe, ndiye aliyepo mbele yake
akimuhudumia.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 55 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (55)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Mungu wangu…..!! Umezinduka?”
Phidaya alizungumza huku akipiga magoti chini,
akakinyanyua kichwa cha Black Shadow, akakiweka
kwenye mapaja yake, akijaribu kumpa huduma ya
kwanza mgonjwa, macho ya Eddy yaliyo jaa
machozi ya maumivu makali ya mbavu zake zilizo
piga chini, alipo kuwa akijaribu kunyanyuka
kitandani ili kumuona mwanamke mwenye sauti ya
inayo fanana na Phidaya, yakatua usoni mwa nesi
huyo, akajikuta akistuka kwani ni Phidaya
mwenyewe, ndiye aliyepo mbele yake
akimuhudumia.
ENDELEA
Kwa haraka Phidaya, akakiweka kichwa cha Black
Shadow chini, akamnyoosha ili asiendelee
kujikunja na kusabaisha nyuzi alizo shonwa
kwenye mbavu kuachia. Akatoa simua yake na
kumpigia daktari msaidizi wa dokta Ranjiti,
akamuelezea hali ya mgonjwa aliyo kuwa nayo.
“Phidaya……”
Black Shadow akajitahidi kumuita Phidaya na
kumfanya astuke na kumtazama mgonjwa wake.
“Unalijua jina langu…..?”
“Phid….aa…ya mk……”
Black Shadow hakumalizia sentensi yake akatulia
kimya akazimia tena. Phidaya akazidi
kuchanganyikiwa ndani ya dakika moja mbeleni
daktari akafika akiwa na dawa maalumu za
kupunguza maumivu, wakasaidia na Phidaya
kumnyanyua Black Shadow na kumrudisha
kitandani mwake. Dokta akamfantia uchunguzi wa
haraka, cha kumshukuru Mungu hapakuwa na
itilafu iliyo weza kujitokeza kwenye mshono wake.
“Amepoteza fahamu kutokana na muumivu makali
sana”
Dokta Yan alimuambia Phidaya aliye onekana kuwa
na wasiwasi mwingi.
“Ila dokta Yan, huyu mgonjwa anaonekana kama
kunijua mimi”
“Kukujua wewe kivipi?”
“Ameniita jina langu la Phidaya”
Dokta Yan akabaki akiwa na mshangao asijue ni
kitu gani kinacho endelea. Kila mara Phidaya
akajikuta akijifuta jasho usoni mwake na kitambaa
chake, mapigo ya moyo wake hayakutulia kabisa
kiasi cha kumfanya ahisi kuna jambo ambalo Black
Shadow analitambua, isitoshe maneno yake ya
mwisho yaliyo katika katika alipokuwa
akizungumza ndio yalizidi kumchanganya.
“Hivi atazinduka kweli?”
“Ndio nesi atazinduka, ila itamchukua kama masaa
mengine tisa hadi kumi, kwa maana sindano
nilkiyo mchoma inapunguza mumivu taratibu
taratibu”
“Isije akawa akaka kwa muda mrefu kama alivyo
kaa?”
“Hapana atakuwa salama tu nesi, ila nikuulize
swali?”
“Uliza tu”
“Mbona una wasiwasi mwingi sana juu ya huyu
mgonjwa tofauti sana na mara ya kwanza?”
“Kusema kweli dokta Yan mimi sielewi kabisa
kichwa change, nahisi kuna kitu ambacho najaribu
kukikumbuka ila nashindwa kujua ni kitu gani
hicho”
Macho yakamtoka dokta Yan, wasiwasi mwingi na
yeye ukamtawala ila akajikaza asiweze kuuonyesha
mbele ya Phidaya. Akamuomba Phidaya aondoke
akaendelee na kazi zake. Phidaya hakuwa na
hiyana yoyote kwa daktari huyo msaidizi wa mume
wake. Akaondoka na kuelekea ofisini kwake
akamuacha Phidaya akiwa amesimama jirani
kabisa na kitanda cha Black Shadow.
Phidaya kwa mara nyingine, akajikuta akianza
kumvua Black Shaodow kinyago alicho kivaa,
akafanikiwa kumaliza kukivua kinyago hicho na
kukishika katika mkono wake wa kushoto. Sura
nzuri ya Black Shadow, ikamfanya aitazame kwa
muda mwingi sana zaidi ya dakika kumi.
Wazo moja likamjia kichwani mwake, akatoa simu
yake na kuingia upande wa kamera kisha akampiga
Black Shadow picha nne, alipo maliza akamvalisha
kinyago chake kama kilivyo kuwa na kutoka zake
ndani ya chumba hicho.
***
“Ndio dokta kuna jambo nahitaji kukuambia”
Dokta Yan, alizungumza kwenye simu yake mara
ya kuingia ofisini kwake na kujifungia kwa ndani.
Simu hiyo iliyopo hewani, anazungumza na dokta
Ranjiti akiwa ndani ya gari akirudi kutoka kwenye
mgahawa alipo kwenda kuonana na Kim.
“Jambo gani hilo?”
“Ni kuhusiana na mke wako”
“Amefanyaje?”
“Nahisi anaanza kuutafuta ukweli juu yake”
“Umelijuaje hilo?”
“Anadai kwamba yule mgonjwa mpiganaji
amezinduka, na amemuita jina lake”
“U…uuu..nasema mpiganaji amezinduka…..?”
“Ndio amezinduka na amemuita mkeo jina lake na
hapa kunaonekana kuna kufamiana”
“Sasa umefanyaje wewe”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akionekana kama
amechanganyikiwa kwa taarifa aliyo pewa.
“Ilinibidi nimchome sindano ya usingizi, ili hadi
utakapo rudi tuweze kujua tunafanyaje”
“Kazi nzuri Yan, nipo njiani nakuja sasa hivi”
Dokta Yan akakata simu na kukaa vizuri kwenye
kiti chake akimfikiria mgonjwa waliye muweka
katika chumba cha siri, kwani yeye ni mtu wa
karibu wa dokta Ranjiti na anafhamu kila kitu
ambacho kimetokea kati ya Phidaya na Ranjiti.
***
Mawazo ya Shamsa yote yakahamia kwa Phidaya,
mwanamke aliye mchukulia kama mama yake,
ambaye alimpatia upendo mkubwa kama alivyo
kuwa amepatiwa kwa marehemu mama yake.
Tangu aweze kuishi na Phidaya kwa miaka zaidi ya
mitatu, alitokea kumpenda mama huyo, kwani wote
asili zao zimeenda na ilikuwa ni vigumu sana kwa
watu kuwatofautisha hao kama si mtu na mama
yake. Asili yao ya kihidi ndio ilizidi kuwafanya
wafanane japo si sana.
“Shamsa una waza nini?”
Sa Yoo alimuuliza Shamsa aliye jilaza kwenye sofa
ndani ya sebule yao, huku miguu yake akiwa
ameiweka juu ya meza kubwa ya kioo iliyopo jirani
naye. Shamsa akashusha pumzi kidogo kisha
akaishusha miguu yake kwenye meza na kukaa
sawa.
“Namfikiria yule nesi kule hospitalini”
“Sasa ndio anakufanya uwe katika mawazo kiasi
hicho, kama ni ugomvi si ulisha isha”
“Hapana si hivyo Sa Yoo”
“Ila ni nini?”
Ýule ni mama yangu”
Sa Yoo macho yakamtoka kama ameona kitu cha
kushangaza sana na chakutisha, taratibu Sa Yoo
akajiweka vizuri kwenye sofa alilo kaa na
kuendelea kumtumbulia macho Shamsa.
“Mbona unanitumbulia macho yako hivyo,
unaniogopesha bwana”
“Hamna Shamsa, nashangaa, inakuwaje yule nesi
awe mama yako?”
“Kweli ni mama yangu, ila cha kushangaza tulisha
mzika, yeye, bibi na mdogo wangu wa kiume
anaitwa Junio”
“Sasa, Shamsa unataka kuniambia siku hizi watu
wanaweza kurudi kutoka wafu au….?”
“Sa Yoo sio hivyo hata mimi nashangaa kwanini
imekuwa hivyo”
“Ahahaa hapana Shamsa bado hujanishawishi”
“Hembu lete Laptop”
Sa Yoo akanyanyuka na kuichukua Laptop ilipoto
kwenye meza ya chakula akarudi nayo na kukaa
kwenye sofa alilipo Shamsa. Akaiweka mezani na
Shamsa akaifungua na kuiwasha, wakasubiria kwa
sekunde kumi na tano ilipo waka, Shamsa akaingia
kwenye mtandao wa ‘google’ akaandika jina lake,
haikuchukua sekunde jina lake likawa limejitokea
kwenye kioo cha laptop hiyo akaingia kwenye
sehemu ya picha, zikafunguka picha nyingi, picha
ya kwanza kabisa kuonekana ni yake akiwa na
Phidaya pamoja na Junio. Macho yakamtoka Sa
Yoo. Akaivuta laptop karibu kudhibitisha picha
anayo inaoa kweli nesi aliye muoana anafanana
kabisa na mtu anaye muona amesimama na
Shamsa. Mwanga wa Laptop hiyo ukaanza kufifia
huku taa nyekundu ndogo ikiwaka chini kidogo ya
kioo hicho.
“Ohoo inaisha chaji, hujaichomeka kwenye kebo ya
umeme hembu inama uivute hiyo kebo”
Sa Yoo alizungumza na Shamsa akafanya kama
alivyo ambiwa, gafla Laptop hiyo ikarushwa mbali
na kuangukia chini, huku kioo cha dirisha la karibu
walipo kaa, likipasuliwa na risasi ambayo imeingia
na kumkosa Shamsa aliye inama chini kuvuta
kebo hiyo na kutua kwenye laptop.
“Sa Yoo inama chini”
Shamsa alizungumza kwa sauti kali, Sa Yoo bila
hata kuuliza akalala chini kabisa ya sakafu.
“Shamsa ni nini hicho”
“Ni risasi hiyo”
Risasi mfululizo zikaanza kumiminika ndani ya
sable yao, meza ya kioo ikapasuliwa, kila mmoja
akawa amelala chini na kujibanza kwa chini
kwenye sofa walilo kuwa wamelalia.
***
Kim baada ya kukabidhiwa kazi na dokta Ranjiti ya
kumuua Shamsa hakuona haja ya kupoteza muda
wala kujipanga kwani mtu ambaye anakwenda
kumuu kwake ni sawasawa na siafu mdogo
ambaye anaweza kuminya minya chini kwa kidole
chake kimoja. Akarudi nyumbani kwake na kuingia
kwenye compyuta yake, akalisaka jina la Shamsa
Eddy, akafanikiwa kulipata, kwa utaalamu wake alio
kuwa nao kwenye maswala ya mtandao
akafanikiwa kufahamu hadi nyumba anayo ishi
binti huyo alipo, hakikisha kwamba amefanikiwa
kumpata, akafungua droo lake kubwa, ambapo
akachukua budnuki yake aina ya L115A3 AWM
yenye uzito usio pungua kilo 16 ikiwa na risasi
zake tano ndani ya magazine. Akaiingiza kwenye
begi lake kubwa, akachukua na bastola zake mbili,
akazichomeka kwa kiunoni kwa nyuma, akajiweka
sawa na kutoka nje ya nyumba yake. Akaliweka
begi lake ndani ya gari lake aina ya Range Rover,
na taratibu akaanza kuondoka kuelekeaeneo la
tukio.
Lee Si, aliweza kumuona Kim akiwa anatoka
nyumbani kwake, kama alivyo agizwa na bosi wake
Madam Phidaya, akaendelea kumfwatilia mtu huyo
ambaye amepewa kazi na dokta Ranjiti.
Kim hakustuka kwamba anafwatiliwa hadi alipo fika
katika eneo la karibu kabisa na nyumba ambayo
anaishi Shamsa. Kwa uzuri karibu na nyumba hiyo
kuna moja ya dorofa linalo endelea kujengwa ila ni
takribani wiki mbili ujenzi wa jengo hilo
umesimamishwa kutokana na uchunguzi unao
fanyiwa mkandarasi wa gorofa hilo.
Kim akapanda hadi gorofa ya tano akiwa na begi
lenye bunduki yake hiyo kubwa, ambayo mara
nyingi anaitumia kwa mauaji ya mtu mmoja
mmoja. Akaitoa bunduki yake hiyo na kuifunga,
akaiweka sawa kwenye moja ya dirisha linalo
elekea kwenye nyumba ya Shamsa.
Kwa kutumia Lensi ya bunduki hiyo akafanikiwa
kuwaona mabinti wawili wakiwa wamekaa kwenye
sofa huku wakionekana vichwa kwa nyuma. Kitu
kilicho mchanganya hakujua kati ya hao mabinti
wawili yupi ni muhusika anaye paswa kuuawa.
Akamlenga shabaha binti wa kwanza upande wa
kushoto kwake, ila binti huyo alipo inama kidogo
aliweza kuina sura yake, na kutambua kwamba sio
ambaye anatakiwa kumuu. Akaihamishia shabaha
yake kwa binti wa kulia kwake, alipo hakikisha
kwamba amemuweka vizuri kwenye tageti,
akafyatua risasi, ila binti huyo aliinama chini kabla
ya risasi hiyo kufika na kutua kwenye laptop
ambayo hapo mwanzo binti huyo alikuwa
ameiziba.
”Shitii…….”
Kim alizungumza huku akiwa ameyakaza meno
yake, kwani tangu aanze kuifanya kazi ya mauaji
hakuwahi kumkosa shabaha yule aliye kusudia
kumuua, hata iweje, ila kwa huyu binti sijui
imekuwaje. Binti wa pili naye akapotea kwenye
tageti yake na risasi aliyo kuwa amemlenga ikatua
kwenye meza ya kioo na kupasuka pasuka. Sofa
ndilo lililo haribu mpango mzima wa Kim kumuua
Shamsa, kila alipo jaribu kuwatafuta hakuweza
kuwaona.
Lee Si, alishushudia mpango mzima ukiwa
unaendelea kwa muuji na wanao paswa kuuliwa,
akiwa amekaa ndani ya gari lake mbali kidogo na
nyumba ambayo ishi Shamsa.
“Hapa ndipo atakapokuwa anaishi yule binti”
Lee Si alizungumza huku akitazama jinsi Kim
akipiga risasa zinazo toka kimya kimya kutokana
na bunduki anayo itumia kufungwa kiwambo cha
kuzuia risasi.
“Hapana naweza kufanya kitu”
Lee Si akawasha gari lake, akakanyaga mafuta kwa
kasi na kwenda kulipaki mbele ya mlango wa
nyumba ya Shamsa, kwa utaalamu mkubwa
akajirusha nje ya gari baada ya kulisimamisha,
akaupiga teke mlango huo na ukafunguka, jambo
lililo washangaza Sa Yoo na Shamsa, hata Kim
mwenyewe akashangaa kuona gari nyekundu ikiwa
imesimama nje ya mlango wa Shamsa.
***
“Vipi mwenzetu tulisikia kwamba unaumwa?”
Halima alimuuliza Rahab huku akijipangusa
machozi ya furaha yaliyo mtiririka usoni mwake.
“Yaa kweli nilikuwa ninaumwa?”
“Nini zaidi”
Fetty alimuuliza Rahab huku akiwa ameupitisha
mkono wake mmoja mabegani mwa Rahab.
“Ahaa ni malaria tu ilinishika nusu iniue”
Rahab aliongopea
“Doo pole sana”
“Sasa mke wa raisi inakuwaje anaumwa Malaria
hadi ikulu kuna mbu kweli?”
Anna alitania huku akicheka, wote wakajikuta
wakiangua kicheko, wakamkaribisha Rahab na
kuketi naye kwenye masofa yaliyomo ndani ya
chumba chao.
“Vipi unatumia kilevi, au ndio umestaarabika Mrs
President”
“Hapana jamani, bado nina dozi musije mukaniua
mwana wa mwenzenu. Haya niambieni yaliyo
wakuta kwa maana nasikia mulikufa nyinyi?”
“Ni kweli kama tetesi ulivyo sizikia kwamba
tumekufa ila ndivyo dunia inavyo jua, ila ukweli
hatujakufa”
Fetty akaanza kuadisia mkasa wa wao tangu walipo
achana, wakiamini kwamba rafiki yao huyo
alikamatwa kwenye tukio la mwisho la wao
kuvamia benki hadi wao walivyo pitia matatizo
mengi pamoja na mateso. Hawakumficha ujuzi
walio upata kwa bwana Rusev, na jinsi alivyo
watelekeza na kuangukia mikononi mwa
Wamarekani. Mateso makali waliyo pitia wakiwa
gerezani hadi kuokolewa na Mzee Godwin na
kurudi tena Tanzania.
Machozi yakamwagika, Rahab, kwani historia hiyo
iliyo wapata wezake imemsikitisha kupita maelezo,
na yeye akawaadisia mambo yote yaliyo mpata
kwenye maisha yake hadi kuolewa na raisi
Praygod, ila kitu alicho waficha wezake na nguvu
zake za ajabu alizo kuwa nazo.
“Ila unampenda huyo mumeo”
Agnes aliuliza huku akiwa amekazia macho Rahab.
“Ahaaa hivyo hivyo tu maisha yanasonga”
“Mmmmm ila kunaonekana ikulu ni kuzuri,
mwenzetu huna hata doa”
Wote wakacheka, Rahab akatambulishwa kwa
Jaquline na Manka. Wakaendelea kupiga piga stori
kuhusiana na mpango wao wa kuingia ikulu kupitia
kura za wananchi.
“Musijali nitahakikisha munaingia ikulu na si
munatambua raisi Praygod ni mmoja wa target
yetu ambaye bado hatujafanikiwa kuiangusha?”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake
wote ndani ya chumba, Fetty akatingisha kichwa
akimaanisha kwamba anakumbuka.
“Basi nitakuwa nikiwaeleza kila kitu ambacho
kitakuwa kinaendelea ndani ya ikulu”
Wote wakampigia makofi Rahab, kila mmoja
akaamini ushindi wa Mzee Godwin kuingia ikulu
upo karibu kuiva.
***
Dokta Ranjiti akasimamisha gari lake eneo la
maegesho na kushuka kwa haraka, akaanza
kutembea kwa kasi kueleka ofisini kwake, akili yake
alihisi inakwenda kuchanganyikiwa, swali kubwa
alilo jiuliza, imekuwaje Black Shadow, alitambue
jina la mke wake. Kila alipo jaribu kuhisi labda
Black Shadow, aliweza kusoma koti la mke wake,
ambalo kila mfanya kazi wa hospitalini kwenye
nguo yake ya kazi huwa kuna jina.
Hilo nalo halikumuingia kabisa akilini, akafungua
ofisi yake na kukaa kwenye kiti chake cha
kuzunguka, kwa haraka akampigia simu dokta Yan,
ndani ya dakika tatu akawa amefika kwenye ofisi ya
dokta Ranjiti.
“Hembu nieleze ilikuwaje kuwaje?”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya chini ya
kunong’oneza, kwani swala hilo ni nyeti sana na
halikupaswa mtu yoyote kuweza kulisikia.
“Kwa madai yake amesema kwamba mgonjwa
alimuita baada ya kuzinduka”
Naye dokta Yan alizungumza kwa sauti ya chini.
“Sasa huyo Black Shadow amemjuaje mke
wangu?”
“Hata mimi sitambui dokta, au anaweza kuwa ni
rafiki wa karibu wa huyo mume wake uliye
niambia?”
“Yaweza kuwa, au unaonaje tukamfunue sura yake,
kwa maana najishangaa tumemfanyia mgonjwa
upasuaji hata kuiona sura yake”
“Hapo kweli umenena dokta”
Dokta Ranjiti akashusha pumzi nyingi, huku
akimtazama dokta Yan, rafiki yake wa muda mrefu
sana. Kwa pamoja wakanyanyuka, na kutoka ndani
ya ofisi kuelekea katika chumba cha siri walipo
mlaza Black Shadow.
Phidaya akaitazama picha ya Black Shadow
kwenye simu yake, akayafumba macho yake kwa
muda mrefu, huku akihakikisha kwamba anajaribu
kumkumbuka mtu huyo, kwani kila alipo jaribu
kuitazama picha hiyo mapigo yake ya moyo
yalimuenda kasi sana.
Kwa mbali sana sauti ya Black Shadow, ikaanza
kumjia kwenye kumbukumbu zake, sauti hiyo
alianza kujitahidi kuifananisha na mtu ambaye
kichwani mwake hayupo. Machozi ya uchungu
akajikuta yakimtoka taratibu. Hakujua ni kwanini
machozi hayo yanamtoka, ila yakazidi kumtoka.
Ikamlazimu kuyafumbua macho yake na kujifuta
tena machozi yake kwa kitambaa.
“Nimekuaje mimi”
Phidaya alizungumza huku akiikodolea macho
picha hiyo, akaanza kuikuza vizuri kuna alama
akaiona shingoni mwa Black Shadow, picha kubwa
akilini ikamjia akamuona mwanaume aliye valia suti
nyeusi akiwa amesimama mbele ya watu wengi,
walio huzuria sherehe ambayo kwenye
kumbukumbu zake, Phidaya hakuijua ni sherehe
gani. Taratibu na kwahisia Phidaya akayafumba
macho yake huku akiendelea kuikumbuka alama
hiyo ya shingoni. Busu lililo mjia kwenye
kumbukumbu zake, alilo lipiga mpiganaji huyo
likamstua kutoka kwenye kumbukumbu zake,
akafumbua macho yake.
Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbia, safari
hii yakiwa na kasi kubwa sana. Akanyanyuka huku
machozi yakimlenga lenga, akili yake ikamtuma
kueleka katika chumba cha siri. Bila ya kupoteza
muda akaanza kukimbia kuelekea kwenye mlango
wenye lifti inayo kushusha chini kwenye chumba
hicho cha siri. Akaingia kwenye lifti iliyo anza
kumpeleka chini taratibu.
Dokta Ranjiti na Dokta Yan, wakaingia kwenye
chumba walicho mlaza Black Shadow,
wakasimama jirani kabisa na kitanda cha Black
Shadow, kwa ishara dokta Ranjiti akamuagiza
dokta Yan amvue, kinyago Black Shdow. Dokta
Yan kwa mikono yake miwili, akamvua Black
Shadow, kinyago chake.
Moyo wa dokta Ranjiti ukadunda kwa kasi kama
mtu anaye jaza mpira wa baiskeli kwa pampu,
macho yakamtoka, jasho likamwagika. Hadi dokta
Yan akaligundua hilo kwa mwenzake.
“Dokta Ranjiti vipi?”
“Hu..yu ndio mume wa Phidaya, anaitwa Eddy”
Kauli ya dokta Ranjiti ikamsimamisha gafla Phidaya
jirani kabisa na mlango wa chumba alicho lazwa
Black Shadow, akaanza kunyata taratibu, hadi
kwenye upenyo mdogo wa mlango huo ulio
rudishiwa, akamuona dokta Yan, akiwa ameshika
kinyago cha Black Shadow mkononi, huku mume
wake dokta Ranjiti mikono yake miwili akiwa
ameikusanya kichwani mwake akiwa katika
taharuki kubwa akimshangaa Black Shadow aliye
lala kitandani hajitambui.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 56 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (56)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Moyo wa dokta Ranjiti ukadunda kwa kasi kama
mtu anaye jaza mpira wa baiskeli kwa pampu,
macho yakamtoka, jasho likamwagika. Hadi dokta
Yan akaligundua hilo kwa mwenzake.
“Dokta Ranjiti vipi?”
“Hu..yu ndio mume wa Phidaya, anaitwa Eddy”
Kauli ya dokta Ranjiti ikamsimamisha gafla Phidaya
jirani kabisa na mlango wa chumba alicho lazwa
Black Shadow, akaanza kunyata taratibu, hadi
kwenye upenyo mdogo wa mlango huo ulio
rudishiwa, akamuona dokta Yan, akiwa ameshika
kinyago cha Black Shadow mkononi, huku mume
wake dokta Ranjiti mikono yake miwili akiwa
ameikusanya kichwani mwake akiwa katika
taharuki kubwa akimshangaa Black Shadow aliye
lala kitandani hajitambui.
ENDELEA
“Sasa tutafanyaje dokta Ranjiti”
Dokta Yan aliuliza huku naye wasiwasi mwingi
ukiwa umeanza kumuingia. Dokta Ranjiti hakuwa
na jibu la kujibu, mwili wake wote unachemka kwa
joto kali, lililo sababishwa na wasiwasi mwingi
sana. Akaanza kutembea kwa hatua kuelekea
mlangoni. Kwa haraka Phidaya akakimbia hadi
kwenye moja chumba kinacho tumika kama stoo
ya kuhifadhia madawa ya hospitali hiyo na
kujibanza humo. Dokta Yan akakirudishia kinyago
cha Black Shadow na kutoka, akamkuta dokta
Ranji akiwa amesimama kwenye lifti akimsubiria
wapandishe juu. Wakaingia wote wawili kwenye lifti
huku kila mmoja akiwaza lake kichwani mwake,
pasipo kujua mambo yote waliyo yazungumza
Phidaya mkewe amayasikia.
Phidaya akachungulia nje akiwa ndani ya chumba
cha stoo alicho ingia, alipo ona kuna usalama kwa
haraka akaanza kutembea kuelekea kwenye
chumba alicho lazwa Black Shadow.
Akafungua mlango na kuingi, kisha akaufunga kwa
ndani kuhakikisha kwamba hakuna mtu ambaye
anaweza kuingia ndani ya chumba hicho yeye
akiwa ndani. Akatembea kwa hatua za taratibu hadi
kwenye kitanda cha Black Shadow, taratibu
akapiga magoti chini, huku akimtazama Black
Shadow, shingoni mwake. Maneno ya mumewe
dokta Ranjiti yakaanza kumjia kichwani, machozi
yakaanza kumwagika, kiasi cha kumfanya ajikute
akiangua kilio cha uchungu sana.
‘Hu..yu ndio mume wa Phidaya, anaitwa Eddy’
Kila maneno hayo yalivyo zidi kujirudia kichwani
mwake ndivyo jinsi hasira yake ilivyo zidi
kumpanda na kumchukia sana mume wake.
“Ina maana huyu ni mume wangu?”
Phidaya alijiuliza huku kiganja chake cha kushoto
kikipapasa kifua cha Black Shadow.
“Imekuwaje Ranjiti akanioa?”
Phidaya hakupata jibu kabisa ya maswali yake, kwa
hasira akasimama na kuelekea mlangoni, hakuona
haja ya kuendelea kukaa na kujiliza kama mtoto
wakati ana uwezo wa kumkabili Ranjiti na
kumuuliza kila kitu ambacho kilitokea kwake.
Akaingia kwenye lifti na kupandisha juu. Kwa
mwendo wa hasira na sura iliyo jikunja Phidaya
akazidi kutembea kuelekea kwenye ofisi ya mume
wake, hata baadhi ya menesi na wafanyakazi
wanao mtambua, walijikuta wakimshangaa.
Akiwa anamalizia kupandisha ngazi ya mwisho, ili
kuanza kutembea katika kordo ndefu ilipo ofisi ya
mumewe, simu yake ikaata, hakuwa mwingine balia
ni Lee Si. Akaiweka sikioni alicho kisikia kikamstua
na kuzidi kuichanganya akili yake.
***
“Nimekuja kuwasaidia”
Lee Si, alizungumza huku akiwa amejibanza
sehemu ambayo si rashisi kwa Kim kumuona
akiwa katika gorofa anapo fanya mashambulizi
yake.
“Tambaeni kwa kuja kwangu huku, haraka”
Shamsa, bila hata kujiuliza, akapiga sarakazi kazaa
kwa kasi na kuangukia sehemu alipo simama Lee
Si. Sa Yoo kila aliposikia mshindo wa kitu kikipiga
kwenye sofa hiyo, alijikuta akipiga kelele za woga,
huku akiendelea kulala chini mikono yake akiwa
ameiweka kichwani mwake.
“Dada nyanyuka twende”
Lee Si, alizungumza huku akimtazama Sa Yoo aliye
endelea kulala chini na kujikunyata. Shamsa
akaangaza macho yake huku na huku, akaiona
bastola ya Lee Si, akiwa ameishika mkono wake
kushoto huku mkono wa kulia akimuimiza Sa Yoo,
kunyanyuka haraka.
Shamsa pasipo kuomba akaibeta bastola ya Lee Si,
kwa haraka akaikoki akaanza kubingiria kuelekea
alipo Sa Yoo, akajibanza kwenye sofa.
“Sa Yoo kimbia nakulinda sawa”
“Mmmmmm”
Sa Yoo alitingisha kichwa na kukataa kwenda
popote hapo chini ya sofa ndio kwenye usalama
wake, kibao kikali kutoka kwa Shamsa kikatua
shavuni mwake, na kumfanya amtumbulie macho
yake makubwa Shamsa.
“Kimbiaaaa”
Shamsa akaitoa mikono yake juu kidogo na kuanza
kufyatua risasi kuelekea kwa Kim aliyopo gorofani.
Tukio hilo likiwa linaendelea Sa Yoo alichomoka
kama mshale na kukimbia kwa Lee Si.
Shamsa kwa haraka naye akimbilia walipo wezake,
huku risasi kadhaa zikimkosa kosa na kugonga
kwenye vitu vingine, wote kwa pamoja wakatoka
nje na kuingia katika gari ya Lee Si. Gari hiyo
ikageuzwa kwa utaalamu wa hali ya juu, na
kuondoka kwa kasi katika eneo hilo.
Kim alipo ona hivyo, akaicha bunduki yake kubwa
na kuanza kushuka kwa kasi kwenye gorofa hilo.
Akafika katika eneo alipo lisimamisha gari lake.
Akaingia na kuanza kulifukuzia gari la Lee Si.
Mwendo kasi wa gari la Kim, likazidi kuwakaribia
Shamsa na wezake, woga mwingi ukazidi
kumtawala Sa Yoo muda wote akiwa ndani ya gari
mapigo ya moyo wake yalizidi kumuenda mbio.
Barabara yenye kona nyingi na iliyopo mlimani,
mithili ya bararaba ya mlima Kitonga iliyopo
mkoani Iringa nchini Tanzania, Lee Si alizidi
kujitahidi kuzikata kona hizo kwa mtindo ambao
alisaidia sana kumuacha Kim kwa umbali kidogo
japo gari la Kim lina uwezo mkubwa wa kukimbia,
kuliko gari anayo iendesha Lee Si.
Kim kila alipo likaribia gari la Lee Si hakusita
kupiga risasi kadhaa zilizo pasua kioo cha nyuma,
Shamsa akatoa magazine ya bastola aliyo nayo,
akakuta ikiwa imebakiwa na risasi mbili tu, na
alipo muuliza Lee Si kama ana magazine ya ziada,
hakuwa nayo. Kim akatoa simu yake mfukoni na
kumpigia bosi wake, kitendo cha bosi wake
kupokea simu, risasi moja kutoka kwa Kim, ikapiga
kioo cha pembeni cha dereva na kumfanya Kim
kuiachia simu yake na kuwahi kuushika mskani,
kuhakikisha gari linarudi barabarani kwani wote
walijikuta wakipiga kelele baada ya gari hiyo
kuyumba na kutaka kujitosa kwenye korongo.
“Sa Yoo hamia siti ya mbele”
Shamsa alitoa mri na wala si ombi, Sa Yoo,
akafanya kama alivyo ambiwa nyuma akabaki
Shamsa mwenye. Akashusha pumzi zote
akanyanya kichwa na kulitazama gari la Kim
linavyo wafwata kwa kasi. Akalifumba jicho lake
moja, akamuweka Kim kwenye mabano ya macho
yake, akafnyatua risasi moja, ikapiga kwenye kioo
cha mbele upande alio kaa Kim, cha kushangaza
kioo hicho hakikuweza kupasuka, zaidi ya kutoa
nyufa chache.
“Mungu wangu”
Sa Yoo alizungumza huku akijibanza chini, Kim,
alipo ona hatari ya binti huyo, akaona asilete
masihara kwani muda wowote anaweza kupoteza
maisha.
“Vipi?”
Lee Si alimuuliza Shamsa
“Gari yake haiingii risasi”
Mambo yote yanavyo endelea Phidaya anayasikia
kupitia kwenye simu kwani simu ya Lee bado ipo
hewani, Risasi kadhaa zikapiga matairi ya nyuma
ya gari ya Lee Si, gari yao ikayumba, na kuanza
kuserereka barabarani, Kim akaongeza mwendo
kasi wa gari lake na kuligonga gari la Lee Si, kwa
kasi kilaanza kushuka kwenye maporomoko
yaliyomo pembezoni mwa barabara na kuwafanya
Shamsa na wezake kupiga kelele za kufa.
***
Mwili mzima ukaanza kumtetemeka Phidaya, ndani
ya sekunde kadhaa hakuweza kusikia kitu chochoe
kutoka kwenye simu hiyo kwani ilikatika na kubaki
akiwa katika alama ya kuuliza. Lee Si kijana wake
na Shamsa ambaye anamtegemea kqatika
kurudisha kumbukumbu zake, ndio hao wamesha
poteza maisha kwenye ajali.
“Hapana hawajafa”
PPhidaya alizungumza huku akibadilisha safari na
kueleka ofisini kwake, akachukua funguo ya gari
lake na kutoka pasipo kusemeshana na mtu wa
aina yoyote. Akaingia kwenye gari lake, kwa haraka
akaondoka katika eneo la hospitali na kwenda
pasipo julikana, lengo lake na kuweza kuhakikisha
kwamba anazungumza na Shamsa
***
Kim akafunga beki za gari lake na kusimama
pembezoni mwa barabara na kulitazama gari la Lee
Si linavyo endelea kuteketea kwa moto. Moyoni
mwake akajawa na furaha kubwa kwani kazi yake
imekuwa rahisi japo iliingia ugumu kidogo.
Akatazama pande zote za barabara hakuona mtu
gari yoyote inayo kuja katika eneo hilo. Akarudi
kwenye gari lake na kuingia, akaondoka kwa
mwendo wa kasi huku akivua gloves zake nyeusi
alizo kuwa amezivaa kwenye viganja vyake.
Akachomoa simu yake kwenye mfuko wa suruali
yake na kuchagua namba ya dokta Ranjiti, akaipiga
na kuiweka simu yake sikioni.
“Ndio dokta”
‘Vipi umefanikiwa kumaliza kazi?’
“Ndio kila kitu kimekwenda kama nilivyo tarajia”
‘Basi nakuomba tuonane kwenye karakana yangu
mida hii kuna kazi ninahitaji kuweza kukupatia”
“Sawa mkuu”
Kim akakata simu, na kuirudisha mfukoni, mwendo
wa dakika kumi na tano mbele akapishana na gari
za polisi nne pamoja na gari mbili za zima moto
zikiwa zinaelekea katika eneo walipo pigiwa simu
na wasamaria wema kwamba kuna gari ndogo
imepata ajali na kuteketea kwa moto.
“Mumepoteza”
Kim alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa
gari lake na kuzidi kutokomea, safari hii akielekea
kwenye karakana la dokta Ranjiti.
***
Muda wote tangu watoke hospitalini, macho yao
yote ni kwenye lango kubwa la karakana, analo
hifadhia ndege zake nne za kusafriria masafa
marefu na mafupi. Dokta Ranjiti yeye wasiwasi
haukuweza kupungua hata kidogo ila kwa upande
wa dokta Yan, wasiwasi ulisha muisha kwa kile kitu
walicho kizungumza njia nzima kwenye gari walipo
kuwa wakitoka kuelekea kwenye karakana hilo.
Hospitali hawakukaa kabisa baada ya kutoka katika
chumba cha siri, roho ya mauaji juu ya watu
wanao taka kumfanya amkose Phidaya ikaendelea
kumtesa kiasi cha kuchukua maamuzi magumu
kwa watu hao. Simu aliyo pigiwa na Kim kwamba
ameifanya kazi ya kumuua Shamsa. Imekamilika,
kidogo ikazidi kumpa matumaini ya ushindi na
kumtoa wasiwasi alio kuwa nao. Utajiri wake
akaona si kitu mbele ya penzi lake kwa Phidaya
mwanamke aliye chukua asilimia kubwa sana ya
maisha yake. Tangu siku ya kwanza kuweza
kumuona katika hospitali ya Aghakani nchini
Tanzaia, alipo letwa hajitambui, alichanganyikiwa
sana. Kikwazo cha yeye kumpata Phidaya kilikuwa
ni mume wake pamoja na mama yake mke, ila kwa
kazi aliyo weza kuifanya alifanikiwa kumchukua
Phidaya pasipo mtu yoyote kugundua, japo watu
wengi waliweza kuhudhuria mazisha yake.
Dokta Ranjiti akastuka kutoka katika dibwai la
mawazo la jinsi alivyo mpata Phidaya, baada ya
kusikia honi ikipigwa nje ya karakana yake yenye
ukubwa wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu.
Wafanyakazi wa eneo lake wakalifungua geti la
eneo hilo, ambapo gari ya Kim ikaingia na
kuwafwata hadi walipo simama, naye Kim
alilisimamisha gari lake pembeni na kushuka.
Wakaalimiana na moja kwa moja wakaelekea
kwenye moja ya ndege kwa ajili ya mazungumzo
muhimu. Wote watatu wakajifungia ndani ya ndege
hiyo na kuanza mazungumzo yao.
“Ninacho hitaji mimi ni kumzika huyo Black
Shadow, apotelee mbali kabisa”
“Ila huoni kama inaweza kuleta skendo chafu kwa
hospitali yako, na kupelekea uchunguzi ukafanyika
dhidi yako dokta?”
Swali la Kim, likamfanya dokta Ranjiti kukaa kimya
na kukosa cha kuzungumza, dokta Yan
akajikoholesha kidogo kisha akatoa na yeye wazo
lake.
“Unaonaje ukafanya kama uvamizi na kumchuku
mgonjwa na ukaondoka naye na kwenda kumzikia
mbali kabisa”
“Uvamizi kwenye hospitali yenu?”
“Ndio, tutahakikisha kwamba walinzi hawastukii
hilo swala, na wewe utatoka naye, tunacho kihitaji
ni wewe kumzika, au kumchoa moto ateketee
kabisa ushahidi wake usionekane”
“Sawa nimewaelewa wakuu wangu, ila nahitaji
fungu langu muliandae mapema”
“Sikia Kim nipo tayari kukupa kiasi chochote cha
pesa, ili mradi huyo mwanaharamu afee. Siwezi
kumpoteza mke wangu kwa mpumbavu mmoja”
“Sawa dokta nimekuelewa, kazi inaanza saa ngapi?”
Wote wakatazamana na dokta Yan akatoa jibu,
wakakubaliana, wakaagana na Kim, mioyoni mwao
wakiwa wamejawa na amani wakisubiria utekelezaji
wa kazi yao kuweza kufantika mara moja.
***
Phidaya, akasimamisha gari lake kwenye moja ya
kituo cha kuongeza mafuta, akamuomba
muhudumu wa kituo hicho kilichopo pembezoni
kidogo mwa mji kumuongezea mafuta kwenye gari
lake.
“Chooni hapa ni wapi?”
Mfanyakazi huyo alimuonyesha Phidaya akashuka
na kuelekea katika sehemu ya vyoo alivyo
onyesha, kutokana haja ndogo ilimsihika akaona
ajisaidie kwenye moja ya choo cha kike. Akamaliza
haja yake, akatoka na kusimama kwenye moja ya
sink la kunawia mikono.
“Yaani naona hata huruma, sijui kama atakuwa
amepona mtu mule ndani”
Mwana mama mmoja alizungumza na simu yake
huku akiwa ameibana kwenye sikio lake, huku
akisadiwa na bega lake la kulia, huku mikono yake
akinawa kwenye moja ya sinki.
“Yaani nimefika pale, nikakuta moshi mwingi, sasa
nikawa najiuliza ni kitu gani kinatokea kwenye lile
korongo, kushuka na kwenda kutazama hivi
nikakuta gari likiteketea kwa moto. Mwanao
akanishauri tuwapigie polisi, basi ndio tumewaacha
wapo eneo la tukio wakiwa na zima moto”
“Haya mwaya mume wangu, nakupenda, sisi ndio
tupo njiani tunarudi”
Mwana mama huyo alipo maliza kunawa akaitoa
simu yake aliyo kuwa ameibana na kuirudisha
kwenye kipochi chake. Phidaya hakusita kumuuliza
ni kitu gani alicho kuwa anakizungumzia kwenye
simu.
“Ni ajali ya gari moja ndogo nimeikuta inateketea
kwenye maporomoko kwenye milima ya Kishing”
“Hiyo gari ina rangi gani?”
Phidaya aliuliza huku mapigo ya moyo yakimuenda
mbio, hakutamani kuweza kujibiwa kama jibu analo
lifikiria kwamba gari hilo ni la rangi nyekundu.
“Lile gari ni larangi nyekundu hivi. Yaa ni larangi
nyekundu”
Phidaya akahisi kama haja ndogo inaanza kumtoka
tena, akashusha pumzi na kutoka pasipo hata
kumuaga mama huyo, kutokana barabara aliyopo
sio mbali sana na barabara inayo kwenda kwenye
milima hiyo, akaingia kwenye gari lake na kulipa
pesa aliyo aliyo paswa kulipa. Akaondoka kwa kasi
hata muhudumu aliye kuwa akimuhudumia akabaki
akiwa anashangaa
Kwa mwendo kasi wa gari yake, na umahiri wa
kuliendesha gari hilo, akafanikiwa kufika katika
eneo la tukio ambapo alikuta watu wengi
wakiwemo waandishi wa habari, askari wa ulinzi na
kikosi cha zima moto wakiwa wamelizunguka gari
lililo pondeka pondeka.
Phidaya aliweza kuligundua gari hilo kwani ni
miongoni mwa magari yake anayo ya penda na
nigari ambalo alimpatia kijana wake kwa ajili ya
matumizi yake binafsi. Nguvu za miguu akahisi
kwamba zinakwenda kumuishia, kwa ishara
akamuita mmoja wa askari aliye weza kugongana
naye macho alipo kuwa akitazama tazama watu
waliopo katika eneo hilo.
“Madam umefwata nini huku?”
Uzuri polisi huyo aliweza kumtambua Phidaya kwa
haraka kwani ni miongoni mwa askari ambao
waliweza kuhusika katika oparesheni ya
kuwakamata majambazi walio vamia hospitali yake
siku chache zilizo pita.
“Nilipigiwa simu kwamba gari ya kijana wangu
imepata ajali, mwili wake upo wapi?”
“Kusema kweli, ndani ya gari hatukukuta mwili wa
mtu yoyote. Hata tulipo jaribu jaribu kutazama
pembeni kuona kwamba labda mtu au watu walio
kuwemo ndani ya gari hilo watakuwa wameangukia
pembeni hatukuweza kuwapata”
“Unasema kweli?”
“Ndio Mrs Ranjiti, siwezi kukutania”
Kidogo hata nguvu za miguu zikamjia Phidaya,
akajikongoja kongoja kwenda kuchungulia kwenye
korongo hilo huku akiongozana na askari huyo
sehemu alipo onyeshwa gari ilipo kutwa, alijikuta
akitoa macho kwani ina umbali mrefu sana.
‘Sasa kama wametoka watakuwa wapi’
Phidaya aliiuliza huku akiendelea kuchhungulia
chungulia bondeni kwenye korongo hilo.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 57 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (57)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Kusema kweli, ndani ya gari hatukukuta mwili wa
mtu yoyote. Hata tulipo jaribu jaribu kutazama
pembeni kuona kwamba labda mtu au watu walio
kuwemo ndani ya gari hilo watakuwa wameangukia
pembeni hatukuweza kuwapata”
“Unasema kweli?”
“Ndio Mrs Ranjiti, siwezi kukutania”
Kidogo hata nguvu za miguu zikamjia Phidaya,
akajikongoja kongoja kwenda kuchungulia kwenye
korongo hilo huku akiongozana na askari huyo
sehemu alipo onyeshwa gari ilipo kutwa, alijikuta
akitoa macho kwani ina umbali mrefu sana.
‘Sasa kama wametoka watakuwa wapi’
Phidaya aliiuliza huku akiendelea kuchhungulia
chungulia bondeni kwenye korongo hilo.
ENDELEA
Phidaya hakuhitaji kuondoka katika eneo hilo hadi
apate ripoti ya mwisho kutoka kwa Polisi kwamba
kijana wake Lee Si pamoja na Shamsa
hawakuwemo kwenye ajali hiyo. Hadi yanatimu
majira ya saa nne usiku, baridi ikiwa kali katika
eneo la eneo hilo pamoja na ukungu mwingi, ulio
tanda kila mahali hapakuweza kuonekana mtui wa
aina yoyote aliye kuwamo kwenye ajali hiyo.
Jambo hilo kwa upande mmoja liampa matumaini
makubwa sana Phidaya. Akaagana na mkuu wa
polisi aliye fika katika eneo hilo kushuhudia kazi ya
vijana wake. Kwa usalama na kutona ni usiku sana,
Phidaya akapewa gari mbili za polisi ziweze
kuongozana naye hadi takapo fika mjini, gari
mmoja ikatangulia mbele, huku ikiwa na askari
wawili na gari moja ikafwatia kwa nyuma nayo
ikiwa na askari wawili.
Safari yao haikukumbwa na tatizo la aina yoyote
hadi walipo mfikisha Phidaya kwenye jumba lake la
kifahari, lenye ulinzi madhubuti. Akaagana na
askari hao wakimuahidi watampatia ripoti kwa kila
jambo ambalo litatokea kwa wakati wowote katika
uchunguzi wanao endelea kuufanya juu ya chanzo
cha ajali hiyo. Mfanyakazi wake wa ndani,
akampokea koti alilo livua na kulishika mkononi,
taratibu Phidaya akangoza hadi kwenye meza ya
chakula na kuketi.
“Dokta hajarudi?”
Phidaya alimuliza mfanyakazi wake wa ndani baada
ya kukuta hapakuwa na chakula ambacho
kimeweza kuguswa.
“Hajarudi bado”
“Hembu nitolee simu kwenye hilo koti langu”
Mfanyakazi wake akafanya kama alivyo agizwa,
Phidaya akaipokea simu yake hiyo, kitu cha
kwanza alipo minya batani ya kuwashia mwanga
kwenye simu yake hiyo aina ya Iphone 6,
akakutana na sura ya Black Shadow. Kwa haraka
kumbukumbu zake zikarudi kwa mgonjwa huyo.
Akakurupuka kwenye kiti kama kichaa, hata kula
hakutamani tena, akatoka nje na kuingia kwenye
gari lake, walinzi wa getini wakamfungulia geti na
kuondoka kwa mwendo wa kasi sana akiwahi
hospital;ini.
***
Majira ya saa tano kasoro usiku, Kim akiwa
amevalia mavazi ya udaktari, pamoja na kitambaa
cha kijani alicho jifunga puani na kuziba mdomo,
huku kikiwa kimembakisha macho tu. Akaanza
kutembea kuelekea kwenye kordo inayo kupeleka
kwenye litio ya kushukia kwenye chumba cha siri.
Mavazi yote aliyo yavaa aliweza kukabidhiwa na
dokta Yan. Huku dokta Ranjiti aki nje kabisa ya
hospitali yake gari lake akiwa amelisimamisha
sehemu ambayo anaweza kuliona geti la
hospitalini kwake na endapo gari ya kubebea
wagonjwa litatoka, basi ataungana nalo
kuhakikisha kwamba Black Shadow wanamuua na
kumzika.
Hapakuwa na nesi wala mtu aliye weza kumstukia
Kim, kutokana na jinsi alivyo vaa. Anaonekana
kama daktari anaye toka katika chumba cha
upasuaji. Kim akashuka na lifti hadi kwenye
chumba ambacho amelazwa Black Shadow,
akatembea kwa tahadhari kubwa hadi kwenye
chumba ambacho ameelelezwa atamkuta Black
Shadow.
Macho yake yakatua kitandani ambapo alitegemea
kumkuta Black Shadow ila haikuwa hivyo kwani
hakuwepo, kilicho bakishwa hapo ni kitanda na
mashuka pekee. Akahisi labda amekosea, akatoka
na kuanza kukagua vyumba vingine viwili,
hakukuta kitu zaidi ya maboksi yenye dawa tu.
“Shitii…….”
Kim alizungumza kwa hasira huku akiitoa simu
yake mfukoni akampigia dokta Ranjiti, hazikupita
hata sekunde tano simu ikapokelewa.
“Vipi umefanikisha?”
Lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa dokta Ranjiti
mara tu alipo pokea simu ya Kim.
“Mbona hayupo mgonjwa mwenyewe”
“Uuuu….unasem…aje?”
“Hayupo nimeingia kwenye chumba mulicho
niagiza nimekumta hayupo”
Dokta Ranjiti hakuonge kitu chochote zaidi ya
kukaa kimya, Kim akakata simu na kumpigia dokta
Yan, naye akaonekana kushangazwa na taarifa
hiyo, kutokana yeye yupo ndani ya hospitali kwa
haraka akashuka hadi kwenye chumba,
akadhibitisha kwamba Black Shadow hayupo. Kila
mmoja akili yake ikajikuta akichanganyikiwa haswa
dokta Yan, kwani kwa ugonjwa alio kuwa nao Black
Shadow ni vigumu sana kwa yeye kuondoka hapo
hospitalini na isitoshe amemchoma sindano ya
usingizi inayo chukua masaa mengi sana hadi
kuisha kwake mwilini.
***
Dokta Ranjiti, akataka kuliwasha gari lake na
kwenda hospitali ila alipo liona gari la Phidaya
likiingia katika geti la hospitalini, akasitisha zoezi
lake la kwenda hospitalini, kwa jinsi alivyo
changanyikiwa akahisi akili yake ikitaka kupasua
kichwa chake, japo ndani ya gari lake kuna hewa
ya kiyoyozi, ila jasho lilimtiririka usoni mwake
kama mtu aliye kimbia mbio ndefu.
Phidaya akasimamisha gari lake kwenye
maegesho, kwa haraka akashuka na kuanza
kutembea kwa mwendo wa kasi kuelekea ndani.
Hakuhihitaji kusemeshana na mfanyakazi yoyote,
akili yake kwa wakati huo inamfikiria Black Shadow
tu. Akiwa kwenye kordo akapishana na Kim akiwa
ameifunika sura yake, hakumtilia maanani sana.
Akaingia kwenye chumba chenye lifti, akashuka
chini, akaanzaa kukimbia hadi kwenye chumba
alicho lazwa Black Shadow.
Macho na sura yake vikabadilika, gafla baada ya
kukuta kitanda kikiwa hakina mgonjwa, dura ikajaa
mikunjo, macho yakamtoka. Mwendo kasi ukaisha,
akajikuta akianza kutembea kwa taratibu kukifwata
kitanda hicho. Dokta Yan aliweza kumuona
Phidaya akiingia ndani ya chumba alilichokuwa
amelazwa Black Shadow, yeye akiwa kwenye moja
ya stoo, mara baada ya Kim kuondoka, aliingia
kutafuta tafuta, kwani naye akili yake
ilichanganyikiwa. Kwa woga wa kumuogopa
Phidaya akajibanza kwenye maboksi mengi ya
dawa akihofia kuonekana kwa maana kesi nzima
itamuangukia yeye.
Phidaya akajikuta akiishiwa nguvu za miguu na
kujikalia kitandani, hakujua alie, acheke au afanye
nini kwa wakati huo, akili yake ikakosa kabisa
maamuzi ya kufanya hali ya hatari ikamjaa moyoni
mwake. Taratibu akajikuta akilala chali kwenye
kitanda hicho na kutazama feni lililopo juu kwenye
chumba hicho linavyo zunguka taratibu taratibu.
***
Kitendo cha gari kuanza kwenda chini, kwenye
makorongo, Shamsa akaona kupiga kelele haita
kuwa jambo la msaada kwao, kwa haraka
akajirusha kwenye siti ya mwisho alipo Sa Yoo,
anaye endelea kupayuka kwa makelele. Kutokana
kioo cha nyuma cha gari hilo kimepasuka kikampa
upenyo mzuri wa yeye kujitoa kwa haraka,
akamshika mkono Sa Yoo, akamchomoa kupitia
katika upenyo huo. Lee Si alipo ona juhudi za
wasichana hao zimezaa matunda na yeye bila
kusubiria gari kufika chini kabisa, akafungua
mlango na kujitosha nje na kuanza kubingiria
kwenye majani marefu. Sa Yoo na Shamsa nao
waakendelea kubingiria kwenda chini
wakiporomoka kwenye majani marefu. Cha
kumshukuru Mungu Shamsa akabahatika kushikilia
kijimti kilicho mzuia kwenda chini, hivyo hivyo
ikawa kwa Sa Yoo. Kwa umahiri wa mazoezi aliyo
nayo Lee Si, akafanikiwa kujizuia kwenye moja ya
jiwe.
Mlipuko wa gari hilo, uliwastua kila mmoja wao.
Kila mmoja aliweza kulishuhudia gari hilo
likiteketea kwa moto, kutokana na nyasi nyingi
zilizo kuwepo katika eneo hilo, adui yao Kim,
hakuweza kuwaona kwa urahisi akaamini kwamba
wameteketea kwa moto. Wakasubira kwa muda
hadi walipo sikia mngurumo wa gari la adui yao
Kim lilipo ondoka ndipo na wao walipo anza
kufanya jitihada za kupandisha kilima hicho.
Haikuwachukua muda sana, wakafanikiwa kufika
juu barabarani, wakaanza kutembea kwa miguu
wakirudi kutokea mjini, kwa mwendo wa dakika
tano, wakafanikiwa kusimamisha gari la mizigo,
wakapewa lifti iliyo wafikisha hadi mjini kabisa.
Muda wote walitembea kwa kujihami wakihofia
kuonekana na adui yao kwani hawakutambua
kwamba ni sehemu gani anapatika. Wakaelekea
katika nyumba ambayo Sa Yoo, alikuwa akiishi na
bibi yake, na baada ya msiba wa bibi yake aliicha
na kwenda kuishi na rafiki yake Shamsa.
Kila mmoja akaanza kutibu majeraha ya mwilini
mwake, hususani Sa Yoo, yeye ndio amepata
mikwaruzo mingi sana, sehemu za mikononi na
migongoni.
“Shamsa hivi umejifunzia wapi mbinu zote zile?”
Sa Yoo aliuliza huku akitabasamu, Shamsa,
hakumjibu kitu chochote zaidi ya kutabasamu na
yeye.
“Haki ya Mungu nilijua leo nakufa, yaani ahaa wee
acha tu. Ila kusema kweli asante rafiki yangu
Shamsa, kwa maana ningekuwa sasa hivi sijui nipo
kuzimu au laa”
“Unapaswa kuwa mwana mazoezi”
“Na kamwili haka kweli nifanye mazoezi gani
mimi?”
“Ya kujilinda”
Muda wote wa mazungumzo Lee Si hakuzungumza
kitu chochote, aliendelea kusikilizia maumivu ya
vidonda vyake. Hata wazo la kumpigia simu bosi
wake kumpa taarifa kwamba wapo salama wala
halikuwepo akilini mwake, aliendelea kumshukuru
Mungu kwa jinsi alivyo fanikiwa kutoka kwenye
ajali hiyo.
Shamsa na Sa Yoo wakaandaa chakula, majira ya
saa mbili usiku wote kwa pamoja wakajumuika
mezani na kuanza kula.
“Wewe unaitwa nani?”
Sa Yoo, alimuuliza Lee Si, baada ya kumuona
akiwa ametawaliwa na mawazo mengi kichwani
mwake hata chakula hakukila kwa furaha.
”Lee Si”
“Asante pia kwa kutusaidia”
“Nanyi asanteni”
“Mimi naitwa Sa Yoo, huyu anaitwa Shamsa”
“Lee kwa nini uliamua kuhatarisha maisha yako na
kutusaidia sisi”
Shamsa alimuuliza Lee Si.
“Ilikuwa ni moja ya kazi yangu niliyo weza kupewa
na bosi wangu”
“Bosi wako ndio amekupa kazi ya kuhatarisha
maisha yako?”
“Hapana bosi wangu aliweza kunipa kazi ya
kukulinda wewe”
“Mimi…….!!”
Shamsa alishangaa huku wakitazamana na Sa Yoo,
kisha akamtazama Lee Si kwa macho hayo hayo
ya mshangao
“Ndio bosi wangu ndiye aliye niagiza”
“Anaitwa nani?”
Sa Yoo alidakia mada
“Anaitwa Madam Phidaya mke wa Mr Ranjiti”
Shamsa akastuka kidogo, kijoko alicho kuwa
akikipeleka mdomoni kikiwa na chakula akajikuta
akikishusha taratibu na kukirudisha kwenye sahani
yake.
“Laiti kama nisinge kulinda basi leo hii
mungekuwa nyote walili maiti hususani wewe
Shamsa”
Sa Yoo na yeye macho yakamtoka, kwa jinsi
macho yake yalivyo na ukubwa fulani na yaduara,
kwa jinsi yalivyo mtoka hadi Lee Si akacheka
kidogo.
“Unacheke sisi kufa?”
Sa Yoo aliuliza kwa woga
“Hapana siwacheki, ila nimecheka kwa jinsi ulivyo
yatoa macho yako”
“Sa Yoo una simu hapo?”
“Sina simu si tumeacha nyumba ile kule”
“Na wewe Lee Si”
“Sina nahisi simu yangu imeteketea kwenye moto
kwa maana niliiangusha ndani ya gari”
“Kwani simu unaitaka ya nini na wewe?”
“Nahitaji tumpigie mama”
“Mama……!!”
“Ndio mama, Phidaya ni mama yangu”
Lee Si, habari aliyo isikia nayo ni mpya masikioni
mwake,naye akajikuta akishangaa. Taratibu picha
ya mazungumzo ya dokta Ranjiti na Kim ikaanza
kumjia taratibu kichwani mwake.
“Sasa naanza kupata picha”
Lee Si alizungumza huku akitingisha kichwa chake
“Picha gani?”
“Mpango wote wa wewe kuuliwa ameupanga mume
wake dokta Ranjiti?”
“What……?”(Nini…….?)
“Ndio, kitu kinacho takiwa kwa sasa hivi ni wewe
kuwa makini kwani maisha yako yapo hatarini”
“Eheee hanijui huyu, ameingia pabaya”
Shamsa alizungumza huku akiacha kula na
kunyanyuka, akaanza kutembea kwa haraka
kuelekea nje, wezake nao wakamfwata huku Sa
Yoo akimuita.
“Unakwenda wapi sasa?”
“Nakwenda kuonana na huyo Rnjiti”
“Nisikilize Shamsa, peke yako huwezi kupambana
na Ranjiti, ni mtu mwenye pesa sana na endapo
atakuona tena atakuua”
Lee Si alizungungumza huku akimzuia Shamsa
aliye jawa na hasira, hakujua ni kwa nini daktari
huyo anahitaji kumuu kwani hapakuwa na jambo
lolote baya alilo weza kumfanyia daktari huyo. Lee
Si akafanikiwa kumzuia Shamsa na kumrudisha
ndani. Wote watatu wakakaa kwenye meza moja
kwa mazungumzo zaidi.
“Kwa nini anataka kuniua”
“Nilisikia akizungumza na mtu aliye mpa hii kazi,
kwamba wewe unatambua siri ya Phidaya”
“Siri…..! Siri gani?”
“Sijajua, ila nahisi kuna jambo ambalo Phidaya
mwenyewe anahitaji kulitambua, ndio maana
akaamua kukutafuta wewe ili uweze kumueleza
ukweli”
Shamsa akashusha pumzi nyingi, kila kitu anacho
kisikia kwa wakati huu kinamchanganya akili yake.
“Nahitaji kuonana na mama”
“Kwa leo itakuwa ni ngumu kuonana naye, kwa
maana usiku huu atakuwa yupo nyumbani kwake”
“Kwani sasa hivi ni saa ngapi?”
Sa Yoo akasimama na kuingia kwenye chumba
chake, akaitazama saa ya ukutani kisha akarudi
sebleni
“Ni nne na dakika tano”
“Atakuwa amesha toka hospitalini”
Lee Si alisisitiza. Kutajwa kwa hospitalini, Shamsa
akamkumbuka Black Shadow wake.
“Mungu wangu……!!”
“Nini?”
“Black Shadow lazima yule dokta atamuua, si
anatambua kwamba yule ni mpenzi wangu, ili
kuendelea kufivha mauvo yake atamuua tu”
“Ohooo sasa itakuwaje?”
“Itabidi twende hospitalini haraka”
Wote watatu wakakubaliana kwa pamoja wakatoka
nje na kukodisha taksi, iliyo wapeleka hadi
hospitalini. Taksi yao ikasimama pembeni na
kulipisha gari la wagonjwa linalo toka kwenye
hospitali hiyo, huku Kim akiwa ndio derava wa gari
hilo, cha kumshukuru Mungu hapakuwa na mtu
aliye weza kulifwatilia gari hilo la wagonjwa wala
Kim, kuifwatilia taksi hiyo kwani Kim moyoni
mwake amejawa na hasira sana, kwani kazi yake
haijakwenda kama alivyo kusudia. Gari hilo lilipo
toka taksi nayo ikaruhusiwa kuingia, moja kwa
moja ikaenda kusimama kwenye maegesho ya
magari. Lee Si akatoa waleti yake, mfuko wa
nyuma wa jinzi alilo vaa. Akampa dereva taksi kiasi
anacho wadai, kisha akashuka kwenye taksi, akiwa
eneo hilo akaliona gari la Phidaya likiwa kwenye
maegesho yake ya kila siku.
“Madam yupo ndani, gari yake hiyo hapo”
Lee Si alizungumza huku akianza kutembea kwa
hatua ndefu kuelekea ndani ya hospitali huku
akifwatwa nyuma na Sa Yoo na Shamsa.
“Ohoo mjukuu wangu Lee Si mbona umeadimika
siku hizi upo wapi?”
Bibi Eyna, alizungumza huku akiweka ndoo yake
na ufagio wake wa kusafishia sakafu chini.
Akamkumbatia Lee Si, kijana anaye mchukulia
kama mjukuu wake.
“Nipo bibi, madam alinipa kazi kidogo nikawa
nimebanwa banwa”
“Mbona umechubuka chubuka, alafu ni nyote
watatu mumepatwa na nini?”
“Ahaa bibi nitakuambia badaye, vipi madam
Phidaya yupo ofisini kwake?”
“Hapana nilimuona kwenye kordo akielekea
chumba cha siri huko chini”
Bibi huyo alizungumza kwa sauti ya chini chini
asisikike
“Kipo wapi hicho chumba?”
“Mmmm unataka kwenda kufanyaje?”
“Bibi ni historia ndefu ila nipeleke kwenye hicho
chumba alafu mambo mengine yatafwata baadaye”
Kutokana bibi huyo anamuamini sana Lee Si
akakubaliana naye, wakaongozana hadi kwenye
mlango wa chumba chenye lifti ya kushuka chini
kwenye chumba cha siri.
“Na hawa wanakwenda?”
“Ndio bibi niwageni wake”
“Nakuomba usinitaje Lee Si nisije nikafukuzwa kazi
mie”
“Huwezi bibi Eyna kufukuzwa mimi nipo”
Bibi huyo akatazama pande zote za kordo
hapakuwa na mtu akawaruhusu vijana hao kuingia
kisha yeye akajifanya kama anafagia fagia maeneo
hayo. Lee Si, Shamsa na Sa Yoo, wakashuka hadi
chini kabisa kwenye chumba kwa kutumia lifti.
Wakaanza kushangaa shangaa kwani ndani ya
chumba hicho kuna taa nyingi na kiyoyozi kikali
kidogo. Milango mitatu iliyopo mbele yao kidogo
ikawapa utata wa kujua ni chumba gani wanapaswa
kuingia. Ila kuna chumba amacho waliona mlango
wake umerudishiwa. Wakapiga hatua hadi kwenye
mlango huo, Lee Si, akausukuma kidogo ndani, na
kuchungulia, akamkuta Madam Phidaya akiwa
amejilaza juu ya kitanda.
“Yupo huku”
Wote wakaingia na kumfanya Phidaya akurupuke
kitandani na kukaa kitako. Phidaya hakuamiani
macho yake alipo muona Shamsa na wezake. Kwa
haraka akanyanyuka na kumkimbilia Shamsa
wakakumbatiana. Phidaya akajikuta akiangua kilio
kilicho mfanya hata Shamsa mwenyewe kulia.
“Mama”
Shamsa aliita kwa unyonge, taratibu Phidaya
akamuachia Shamsa na kumtazama usoni akiwa
haamini jina alilo itwa kwa haraka akamshika
mkono, wakaka kitandani.
“Shamsa niambie unakumbuka nini kuhusu mim?”
Phidaya alizungumza huku akilia kwa uchungu
“Wewe ni mama yangu”
“Kweli……?”
“Ndio mama”
Phidaya akajipapasa kwa haraka, hakuiona simu
yake, akanyanyuka na kukuta akiwa ameikalia,
akaingia upande wa kuhifadhia picha na kuitafuta
picha ya Black Shadow aliyo mpiga akiwa hana
kinyago.
“Huyu je ni nani?”
Phidaya alizungumza huku machozi yakiendelea
kumtiririka, Shamsa alipo ishika simu na kuiona
picha ya Eddy akastuka, kidogo kwa sekunde
kadhaa akaikuta akiwa kimya.
“Niambie Shamsa mwanangu, huyo ni nani?”
“Huyu ni baba. Baba Eddy”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimwagika.
Phidaya akaachia ukunga ulio mfanya Shamsa
kumkumbatia kwa haraka na kuanza
kumbembeleza.
“Wamemumua baba yako”
Phidaya alizungumza huku akiwa emekumbatiwa.
“Kina nani hao mama”
“Ranjti na wezake, ndio wamemuua. Baada ya
kugundua kwamba Black Shadow ni mume wangu”
“Eheeeeeeeeee…….!!!!”
Shamsa alijikuta akimuachia Phidaya na kusimama
huku akimtazama kwa mshangao, Lee Si na Sa
Yoo nao wakabaki na mshangao kuyasikia maneno
hayo.
“Ndio Black Shadow ndio huyo baba yako Eddy”
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 58 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (58)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Niambie Shamsa mwanangu, huyo ni nani?”
“Huyu ni baba. Baba Eddy”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimwagika.
Phidaya akaachia ukunga ulio mfanya Shamsa
kumkumbatia kwa haraka na kuanza
kumbembeleza.
“Wamemumua baba yako”
Phidaya alizungumza huku akiwa emekumbatiwa.
“Kina nani hao mama”
“Ranjti na wezake, ndio wamemuua. Baada ya
kugundua kwamba Black Shadow ni mume wangu”
“Eheeeeeeeeee…….!!!!”
Shamsa alijikuta akimuachia Phidaya na kusimama
huku akimtazama kwa mshangao, Lee Si na Sa
Yoo nao wakabaki na mshangao kuyasikia maneno
hayo.
“Ndio Black Shadow ndio huyo baba yako Eddy”
ENDELEA
Shamsa akajihisi kama nguvu zikimuishia, taratibu
akarudi kitandani na kuketi pasipo kuzungumza
kitu cha aina yoyote. Kila mmoja akabaki kimya,
wakikosa kitu cha kuzungumza. Maumivu makali
ya mapenzi yakamtawala Shamsa moyoni mwake,
hakuamini asilimi kwamba Eddy ndio Black
Shadow. Yote nikutokana na mapenzi mazito aliyo
kuwa nayo kwa mpiganaji huyo.
“Mama sio kweli, Black Shadow hawezi kuwa
baba”
Maneno ya Shamsa yalimshangaza kila mmoja
wao. Mambo yate yakiwa yanaendelea dokta Yan
aliweza kuwaona, kwa tahadhari kubwa akaanza
kutoka kwa kunyata huku mwili mzima
ukimtetemeka akafanikiwa kufika kwenye lifti
pasipo kuonewa na mtu yoyote, akaingia na
kupanda juu. Kitendo cha kutoka katika chumba
hicho akakutana na bibi Eyna. Hakumsemesha kitu
cha aina yoyote zaidi ya kumpita kama hajamuona.
Akingia ofisini kwake na kujifungia kwa ndani, kwa
haraka akachukua simu yake na kumpigia dokta
Ranjiti.
***
Dokta Ranjiti akiwa barabarani ndani ya gari lake
huku akiongozana na gari ya wagonjwa inayo
endeshwa na Kim wakielekea kwenye karakana
yake, simu yake ikaita. Taratibu akaitoa mfukoni
mwake, alipo kuta ni dokta Yan akaipokea na
kuiweka sikioni.
“Dokta mbona yule msichana hajakufa?”
“Msichana gani?”
“Yule mtoto wa Phidaya”
“Unataka kuniambia Shamsa yupo hai?”
“Ndio nimemuona akiwa na yule binti aliye kuja
naye ofisini kwako siku ile”
Akili ya dokta Ranjiti ikazidi kuchanganyikiwa, kila
taarifa anayo ipata kwa sasa ni mbaya zaidi ya
ubaya
***
Kampeni za vyama vya upinzani na chama tawala
nchini Tanzania, vikazidi kupamba moto. Mzee
Godwin kila siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi
alivyo zidi kupata umaarufu kwa wananchi wengi
wa Tanzania. Maneno yake matamu yakazidi
kuwapagawisha wananchi wengi. Kadri siku zilivyo
zidi kwenda ndivyo chama tawala kilivyo zidi
kupoteza umaarufu wake. Mzee Godwin kwa pesa
aliyo kuwa nayo aliweza kuteka sehemu muhimu
zenye ushawishi mkubwa wa watu wakiwemo
wasanii wa muziki pamoja na wasanii wa filamu.
Siku zikazidi kukatika na kuyoyoma. Siku ambayo
wananchi wengi waliweza kuisubiria kwa hamu
kubwa ikawadia. Tarehe ishirini na tano ya mwenzi
wa kumi, wananchi wengi katika maeneo
mbalimbali ndani ya Tanzania, wakajitokeza katika
vituo zaidi ya elfu tatu vya kupigia kura.
Zoezi hilo lililo funguliwa saa kumi na mbili
asubuhi wananchi wakaanza kuwapigia kura,
madiwani, wabunge na raisi ambaye walihitaji
kuweza kumsimamisha madarakani.
Masaa yalizidi kuyoyoma hadi saa kumi na mbili
jioni, wananchi wengine wakaba bado hawajapiga
kura, hii ni kutokana na wananchi wengi sana
kujitokeza katika zoezi hilo. Tume ya taifa
ikaongeza siku iliyo fwata yaani tarehe ishirini na
sita, wananchi waendelea kupiga kura wale ambao
walikosa kupiga kura katika siku ya kwanza.
Usimamizi wa kura uakazidi kusimamiwa
kikamilifu, kuhakikisha kwamba hakuna chama
kinacho ingia katika kashfa ya kuiba kura.
Siku ya pili zoezi lilizidi kwenda vizuri kwenye
vituo vyote vya nchini Tanzania. Zoezi la kuhesabu
kura likaanza, kila kituo kikatuma hesabu katika
tume kuu ya uchaguzi. Matokeo yote ya uraisi
katika vituo vyote zaidi ya elfu tatu, yakahesabiwa.
Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio,
msimamizi mkuu wa tume ya uchaguzi bwana
Lukas Barnaba. Kwani chama tawala kimetupwa
mbali sana kwa kura zilizo pigwa na wananchi.
Ubaya ni kwamba katika ukumbi wa kuhesabia kura
hizo hapakuwa na mtu yoyote aliye ruhusiwa kuwa
na simu kuhofia kuvujishwa kwa matokeo.
Majira ya saa nne asubuhi, waandishi wa habari
wengi kutoka sehemu mbalimbali, waliweza
kukusanyika katika katika viwanja vya tume ya
taifa. Kila jambo linalo endelea katika viwanja hivyo
yalirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya
televishion na redio. Hata watu wanao miliki blog
pamona na website zao, nao walijitahidi kurusha
matukio yanayo endelea.
Viongozi wa vyama mbalimbali nao waliweza
kukusanyika katika viwanja hivyo kushushudia
tukio hilo, kila kiongozi aliye kuwa akigombania
nafasi ya uraisi, mapigo yake ya moyo hayakuweza
kutulia, kila walipo waona watumishi wa tume ya
Taifa, baadhi yao hawakusita kuwauliza uliza kitu
kinacho endelea. Hapakuwa na mtumishi wa tume
ya taifa aliye weza kuto majibu ya kuelewaka kwa
viongozi hao wapatao nane walio kuwa
wakigombani uraisai. Mzee Godwin na raisi
Praygod wao wenyewe tu ndio hawakuweza
kuwauliza watumishi wa uma kwani wanajiamini
sana, hii ni kutokanana vyama vyao kuweza kuwa
na nguvu kuwa ya kisiasa kwa wananchi.
Wakati wa kutaja matokeo ukawadia, mkuu wa
tume ya uchaguzi akasimama kwenye moja ya
sehemu iliyo andaliwa kwa zoezi hilo maalumu
kwa watanzania wote walio weza kupiga kura zao
kuwachangua viongozi wao. Kila mtu macho na
masikio yake aliyaweka tayari kwa kusikiliza majibu
hayo. Ukimya mkubwa ukatawala karibia uwanja
mzima. Mkuu wa tume ya uchaguzi bwana Lukas
Barnaba akawatazama watu walio kusanyika hapo
woga mwingi ukamuingia, macho yake alipo
yakutanisha na raisi Praygod Makuya, ndivyo jinsi
mapigo yake yalivyo kwenda kasi.
“Ndugu Watan…zania”
Bwana Barnaba alizungumza kwa sauti ya kukata
katia, mwili ukazidi kumtetemeka gafla miguu yake
ikaishiwa nguvu na kuanguka chini na kupoteza
fahamu.
***
Phidaya akawaomba Shamsa watoke kwenye
chumba hicho, wakarudi juu huku kila mmoja wao
akiwa na mawazo mengi kichwani mwake. Swali
kubwa ambalo linawachanganya hadi kwa wakati
huu ni sehemu gani ambayo Black Shadow
amekwenda. Kila mmoja alipelekea mawazo yake
kwa dokta Ranjiti. Shamsa aliongoza hadi ofisini
kwa dokta Ranjiti. Ofisini hakumkuta mtu yoyote,
ikawalazimu kuondoka katika eneo la hospitalini
majira ya saa nane usiku. Wakaelekea kwenye
moja ya hoteli ambapo Phidaya aliweza kukodishia
vyumba viwili kwa ajili wajifiche hapo kwa kipindi
kirefu, hadi mambo yatakapo kuwa shwari. Kazi
walivyo kuwa nayo kwa wakati huo ni kuhakikisha
kwamba wanamtafuta Eddy, nchi nzima hadi
wampate.
Phidaya akarudi nyumbani kwake, akiwa katika hali
ya mawazo mengi sana, ukimya nyumbani kwake
ulimuonyesha dokta Ranjiti hajarejea. Chuki yake
juu ya dokta Ranjiti ilizidi kuongezeka kila anapo
mkumbuka kwa tukio ambalo amemfanyia Shamsa
na kumfanyia Black Shadow.
“Lazima naye nimuue”
Phidaya alizungumza huku akijitazama kwenye
kioo cha chumbani kwake.
***
Dokta Ranjiti na Kim walipo ingia kwenye karakana,
dokta Kim akaonekana mwenye hasira kali,
akamkata jicho kali Kim pale alipo shuka kwenye
gari ya wagonjwa hadi Kim akahisi kuna jambo
ambalo limetokea.
“Vipi dokta mbona hivy……..”
Ngumi nzito ikatua shavuni mwa Kim na kumfanya
ayumbe kidogo, akamgeukia dokta Ranjiti kwa
hasira, akataka ajibu shambulizi hilo ila
akakumbuka kwamba mtu huyo ni bosi wake na ni
mtu muhimu sana anaye msaidia katika kuiepuka
mikono ya polisi kutokana na utaalamu wake wa
kutengeneza sura bandia.
“Umesema umemuua yule msichana ilabado wapo
hai ni ujinga gani ulio ufanya weweeee”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa kufoka sana, macho
yalikmtoka, jasho lilimwagika kiasi cha kumfanya
aifungua tai yake na kuitupiakando.
“Ila bosi wamekufa kwenye ajali ya gari?”
“Wewee acha upumbavuuuu. Ona ona hawa ni kina
nani?”
Dokta Ranjiti akampa simu yake Kim, akaona video
fupi ambayo Dokta Yan alimtumia baada ya
kuichukua kwenye chumba cha ulinzi, iliyo
rekodiwa na moja ya kamera za kuingila mapokezi.
Kim hakuamini macho yake kwani video hiyo
iliwaonyesha vijana wote watatu, Shamsa, Sa Yoo
na Lee Si.
“Umefanya nini Kim, na mbaya wamekutana na
Phidaya mke wangu sijui yaani itakuwaje”
Dokta Ranjiti alichanganyikiwa sana.
“Bosi nipe nafasi ya mwisho nitahakikisha
ninawatoa dunia”
“Hakikisha unafanya hivyo”
“Sawa bosi”
Kim alizungumza na kuondoka eneo la karakana,
akiwa amejawa na mawazo mengi kichwani
mwake. Hakujua ni jinsi gani vijana wale watatu
wamezeje kuokoka kwenye ajali ambayo
aliishuhudia kwa macho yake. Moyoni mwake
alianza kupata woga kuwaogopa vijana hao, ila
kutokana ni kazi ambayo amepewa na
inamuingizia pesa akaona ni lazima aifanya ili
maisha yake yaweze kusonga mbele.
Dokta Ranjiti kwa woga alio kuwa nao dhidi ya
mke wake akiamini kwamba atakuwa ameelezwa
kila kitu na Shamsa, walivyo kutana, akaona ni
vyema kuto rudi nyumbani usiku huo, akaingia
kwenye moja ya ndege yake ya kifahari, yenye
kitand kizuri. Akagiza mfanya kazi wake kumletea
chakula, akala na kulala, wala hakukumbuka
kuoga.
***
Majira ya saa mbili asubuhi Sabogo na msaidizi
wake wakafika hospitalini ili kumjulia hali Black
Shadow, kwa bahati nzuri wakamkuta dokta Yan
akiwa anatoka kwenye moja ya chumba
kumtembelea mgonjwa wake. Wakasalimiana naye,
na kumuomba kumuona mgonjwa.
Dokta Yan, akashindwa hata kitu cha kuwajibu,
wawasiwasi wake usoni uliwadhihirisha Sabogo na
msaidizi wake kwamba kuna tatizo ambalo
limetokea kwa Black Shadow.
“Vipi dokta mbona unawasiwasi mwingi?”
“Black Shadow amepotea jana hospitalini”
“Amepotea…….?”
“Ndio hata sisi hatujui amekwenda wapi”
“Kwa…kwa.ni alipata nafuu?”
“Ndio alipata nafuu, sasa ndio hivyo ametoweka na
hadi sasa hivi hatutambui alipo”
Sabogo hakutaka kukubaliana na maneno ya
daktari huyo, kwa urahisi kiasi hicho, bila idhini ya
daktari akaongoza hadi kwenye chumba cha siri
ambapo Black Shadow amelazwa. Kweli akakuta
kitanda cha Eddy kikiwa hakina mtu. Akazidi
kuchnganyikiwa.
“Bosi tunafanyaje sasa?”
“Turudi kambini”
Sabogo na msaidizi wake wakaondoka, wakarudi
katika kambi yake iliyo na vijana wengi wa mtaani.
Akaitisha kikao cha dharura. Akatoa agizo kwa
vijana wake hao kuhakikisha kwamba wanamtafuta
Black Shadow popote alipo kwa madai yake mbele
ya vijana ni kwamba kuna mtu anahusika na
upotevu wa Black Shadow.
Vijana wa Sabogo ambao wengi wao wanaitambua
sura halisi ya Black Shadow, wakaingia mitani na
kuanza kufanya uchunguzi kuhakikisha wanampa
mpiganaji wao.
***
Hadi kuna pambazuka Shamsa hakupata lepe la
usingizi, akilini mwake alizidi kumfikiria Black
Shadow na Eddy. Moyoni mwake akazidi
kujiaminisha kwamba hao ni watu wawili tofauti.
Hisia zake za mapenzi juu ya Black Shadow,
hakuhitaji kuzikatisha kiurahisi, kama alivyo sema
Phidaya kwa maana anaamini kwamba Phidaya
mwenye anahitaji msaada wake wa kuhakikisha
kumbukumbu zake zinamrejea.
“Au sio Phidaya mwenyewe, mbona yule tulisha
mzika?”
Shamsa alizidi kujiuliza maswali ambayo hakujua
hata atajajibu vipi kwa maana hadi sasa hivi na
yeye bado yupo njia panda.
“Umeamkaje?”
Sauti ya Sa Yoo aliye lala pembeni yake, ndio
ilimstua kutoka kwenye dibwa la mawazo,
akageuza kichwa chake taratibu na kumtazama Sa
Yoo anaye piga miyayo ya usingizi.
“Nipo poa vipi wewe?”
“Safi, nimekusikia ukizungumza peke yako vipi
kuna tatizo?”
“Kusema kweli Sa Yoo, hadi sasa hivi sijielewi
kabisa. Sielewi jinsi mambo haya yanavyo kwenda
kwenda”
“Huwelewi nini?”
“Jinsi Black Shadow, nilivyo ambiwa eti ni baba
yangu. Pili ni kuhusiana na huyu mama yangu
Phidaya, yaani nahisi kichwa changu kitanipasuka
kwa mawazo”
“Unajua ni nini rafiki yangu Shamsa. Wewe ndio
uliye baki katika huu mchezo, wewe ndio unaye
takiwa kufumbua ukweli kuhusiana na familia yako”
“Nitaanzai wapi Sa Yoo, wakati mwanaume ninaye
mpenda eti jana ninaambiwa kwamba ni baba
yangu. Mama ambaye tulisha mzika leo yupo hai
tena ni mke wa mtu maarufu hapa Japani, kweli
niambie rafiki yangu mimi nitafanyaje?”
“Mmmmm, ni kweli mwanzo ni mgumu. Ila nina
wazo?”
“Wazo gani?”
“Unaonaje ukajifanya wewe ni Black Shadow”
“Alafu…….?”
Shamsa alijibu huku akicheka
“Usinicheke Shamsa, wazo langu ni zuri sana”
“Ndio nalisikiliza sema mama.”
“Baada ya hapo unaanza kumtafuta dokta Ranjiti
kimya kimya unambananisha. Ninaimani atakupa
wewe ukweli tu”
“Kwa nini umeniambia mimi niwe Black Shadow na
si wewe?”
“Hiii… kwani mimi najua hata kupigana. Fanya
hivyo utafanikiwa rafiki yangu”
Shamsa hakuzungumza kitu zaidi ya kujilaza chali
akitazama juu akilitafakari wazo la rafiki yake
***
Wiki nzima ikakata pasipo Black Shadow
kupatikana, Phidaya alijikuta akikonda taratibu
kwani hofu yake yote ni juu ya mwanau ume huyo
aliye elezwa kwamba ni mume wake. Hakujua ni
lini alikuwa mume wake, ila kwa kauli za Shamsa
aliweza kuamini maneno yake. Kila muda alijikuta
akiitazama picha ya Eddy iliyopo kwenye simu
yake. Mume wake aliye mpigia simu na kumueleza
kwamba yupo Korea Kusini, kikazi, hakuhitaji
kumfwatilia sana. Kwani alizidi kumchukia na
endapo angemuona basi angemng’ofoa shingo
yake.
Hakupenda kukaa kabisa hospitalini kwake, mara
nyingi aliweza kuutumia muda wake kwenda
kutembelea sehemu mbalimbali zenye vivutio ili
kupoteza mawazo yake. Siku ya leo aliamua
kuutumia muda wake kwenda kwenye kituo kimoja
cha watoto yatima. Akiwa na mlinzi wake Lee Si,
walipeleka chakula pamoja na pesa nyingi katika
kituo hicho ili kusaidia watoto hao wenye umri
kuanzia mwaka mmoja hadi kumi na saba.
Macho ya Phidaya yakatua kwa mtoto mmoja, aliye
jitahidi kukumbuka ni wapi alimuona, ila hakilini
mwake hakuweza kupata kumbukumbu yoyote.
Kwa ishara akamuita mtoto huyo ambaye kusema
kweli amefanana sana na Junio, ila si Junio kwani
huyu ni mdogo kwa Junio.
“Unaitwa nani?”
“Black Shadow….”
Jibu la mtoto huyo lilimfanya Phidaya kutabasamu
huku akimtazama mtoto huyo.
“Unamua Black Shadow”
“Ndio namjuaa”
“Umemuona wapi?”
Kidogo mtoto huyo akasita, akamsogelea Phidaya
sikioni na kumnong’oneza
“Nipe ela nitakuambia alipo Black Shadow”
Phidaya ikabidi acheke kidogo kwani mtoto huyo
anaonekena ni mjanha sana.
“Una miaka mingapi?”
“Hiyoo”
Mtoto huyo alionyesha vidole vyake, vinne vya
kiganja cha kulia. Phidaya akatoa noti ya dola mia
na kumpa kijana huyo, kwa haraka kijana huyo
akaificha pesa hiyo kwenye mfuko wake. Ili walezi
wake wasioone kwani anaweza kupokonywa.
Kutokana hawaruhusiwi kukaa na kiasi chochote
cha pesa.
“Unataka kumuona…….?”
Mtoto huyo alizungumza kwa sauti ya chini hata
Lee Si aliye simama pembeni hakusikia zaidi ya
Phidaya peke yake.
“Ndio”
Phidaya naye alijibu kwa sauti ya chini kabisa.
Mtoto huyo akamshika mkono Phidaya
nakumnyanyaua kwenye kiti alicho kuwa amekaa.
“Lee Si nakuja”
“Sawa Madam”
Wakaongozana na mtoto huyo kuelekea kwenye
mabweni wanayo ishi, walezi wakataka kuwafwata
ila Phidaya akawazuia na kuwadanganya kwamba
mtoto huyo anakwenda kumuonyesha bweni na
kitanda anacho lala. Walezi hao wakaamini na
kuwaacha waendelee na safari yao. Kweli
wakaingia kwenye bweni lenye vitanda vingi,
wakazidi kusonga mbele hadi kwenye vyoo vya
ndani kwenye bweni hilo. Wakaingia kwenye moja
ya choo.
“Yupo wapi huyo Black Shadow”
“Ngoja”
Mtoto huyo mwenye upeo mkubwa wa akili,
kakapanda kwenye sinki la choo, ikabidi Phidaya
amsaidie kupanda, kakaitoa picha iliyopo kwenye
ikuta. Phidaya akaona shimo kwenye dogo kwenye
ukuta huo. Mtoto huyo akaingiza mkono wake
ambao upo sawa sawa na shimo hiko. Kuna kitasa
akavuta kwa ndani, Robo ya ukuta wa choo hicho
ukafunguka, hadi Phidaya akaogopa.
“Twende yupo huku”
“Ngoja kwanza mbona kuna giza humo ndani”
Mtoto huyo kwa kumtoa hofu Phidaya akaingia,
akamisha batani kwenye moja ya swichi. Sehemu
ya ndani ikaonekana vizuri. Ngazi nyingi zilizo
shuka chini, zilizidi kumshangaza Phidaya.
Taratibu akapiga hatua za uwoga, akaingia, ndani,
mtoto huyo akaufunga mlango huo ulio kaa kama
ukuta.
“Umepajuaje huku?”
“Babu yangu ndio alinionyesha huku”
“Babu yako”
“Ndio.”
“Kwanza unaitwa nani?”
“Naitwa Soroo”
Walizidi kushuka chini, wakakuta kordo moja ndefu
iliyo jaa taa pembeni kwa juu, mbele yake kwa
mbali kuna mlango wa kuingilia kwenye chumba
kimoja tu kilichopo kwenye eneo hilo. Wakazidi
kupiga hatua, wakiwa umbali fulani kutoka kilipo
chumba hicho, taa zikaanza kufifia. Wote
wakajikuta wakiogopa, gafla taa zote zikazima na
kujikuta wakipiga kelele za woga kwani giza zito
lilitanda kwenye mboni za macho yao.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 59 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (59)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
. Taratibu akapiga hatua za uwoga, akaingia, ndani,
mtoto huyo akaufunga mlango huo ulio kaa kama
ukuta.
“Umepajuaje huku?”
“Babu yangu ndio alinionyesha huku”
“Babu yako”
“Ndio.”
“Kwanza unaitwa nani?”
“Naitwa Soroo”
Walizidi kushuka chini, wakakuta kordo moja ndefu
iliyo jaa taa pembeni kwa juu, mbele yake kwa
mbali kuna mlango wa kuingilia kwenye chumba
kimoja tu kilichopo kwenye eneo hilo. Wakazidi
kupiga hatua, wakiwa umbali fulani kutoka kilipo
chumba hicho, taa zikaanza kufifia. Wote
wakajikuta wakiogopa, gafla taa zote zikazima na
kujikuta wakipiga kelele za woga kwani giza zito
lilitanda kwenye mboni za macho yao.
ENDELEA
Haikupita hata dakika moja taa hizo zikawaka, wote
wakanyamaza na kushusha pumzi zao. Kila mmoja
woga ulimtawala.
“Turudi zetu”
Phidaya alizungumza huku akimshika mkono
Soroo, habari ya kwenda alipo Black Shadow,
ikayayuka moyoni mwake, hakutamani kuona
anafia kwenye sehemu hiyo chini kabisa ya ardhi.
Wakaanza kutembea kwenye kordo kurudi walipo
tokea tena safari hii waliongeza hata mwendo wa
kutembea. Kila mara Phidaya alitazama nyuma
kuona kama kuna kitu kinakuja. Wakazipandisha
ngazi kwa haraka, Soroo akafungua mlango,
wakapita na kutokezea katika choo walicho ingia.
Wakarudishia kila kitu sehemu yake, na kutoka
kwenye mabweni hayo. Moja kwa moja wakarudi
katika sehemu ya mkusanyiko walipo watoto
wengine pamoja na walezi wao.
“Mumefanikiwa kuona kitanda chake?”
Mlezi mmoja alimuuliza, huku akiachia tabasamu
pana usoni mwake.
“Ndio, nimefurahi sana kuona mabweni yao.
Nitahalkikisha kwamba tunaongeza mabweni ili
mumweze kuchukua vijana wengi wamaoishi
kwenye maisha magumu”
“Tutashukuru sana madam”
“Nipo pamoja nanyi. Naona muda wangu hautoshi
basi ngoja niwaache muendelee na majukumu”
Phidaya alijikaza kuzungumza hivyo, ila mwili
mzima alihisi kama umekufa ganzi kwa woga.
Phidaya akamuaga Saroo, na kumuahidi atarejea
kisha akangia kwenye gari lake na kuelekea hotelini
wanap ishi Shamsa na mwenzake. Wakawakuta
wakiwa wanafanya mazoezi ya viungo.
Wakasalimiana kwa furaha, huku Phidaya akimbusu
Shamsa kwenye paji la uso.
“Vipi mbona mupo kwenye mazoezi makali?”
“Kuna kitu mama nahitaji uweze kunisaidia”
“Kitu gani hicho?”
“Nihitaji kutafuta ukweli kuhusiana na kitu
ambacho kilikupata wewe kwa maana inavyo
onekana hukumbuki mambo ya nyuma”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Phidaya
usoni, anaye onekana kumsikiliza kwa umakini
sana.
“Nahitaji kufahamu maeneo ambayo dokta Ranjiti
anapenda kuyatembelea?”
“Kwa sasa yupo Korea Kusini”
“Mama hujanielewa swali langu, yaani sihitaji kujua
yupo wapi ila nahitaji kufahamu maeneo anayo
penda kwenda kutulia”
“Kusema kweli sifahamu, huwa Ranjiti muda
mwingi anapenda kuutumia akiwa hospitalini, na
hata akitoka ni sehemu chache sana ambazo
anakwenda na kurejea”
“Au labda Yan yule rafiki yake aliye kuwa naye
katika chumba cha Black Shadow anaweza
kufahamu maeneo ambayo Ranjiti anapenda
kuyatembelea kwa sana”
“Eheee umenikumbusha mama hivi siku ambayo
uliwasikia wakizungumza kwenye chumba cha
Black Shadow, Yan si alihusika?”
“Ndio lihusika”
“Basi mama nimeshapata kwa kuanzia, kila jambo
kwa sasa litakwenda sawa, niachie mimi hiyo kazi”
“Sawa. Ila unataka kufanya nini?”
“Mama kila kitu nimekuambia niachie mimi,
nikiimaliza kazi yangu nitakuletea ripoti kamili”
“Sawa ila kuwa makini kwa maana hawa watu
mimi wala siwaamini sana”
“Usijali mama yangu, hivi nyumbani kwa Yan si
unapafahamu?”
“Ndio napafahamu”
Phidaya akamuelekeza Shamsa na Sa Yoo
nyumbani kwa daktari Yan, kutokana Sa Yoo ni
mwenyeji sana katika nchi hiyo ya Japan, eneo
hilo alilifahamu.
***
Majadiliano ya dokta Ranjiti, dokta Yan na Kim
ndani ya ndege, yalimchanganya rubani wake
ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo pasipo bosi
wake kuweza kufahamu. Mpango wa kwenda
kumteka Black Shadow, kwenye hospitalini na
kwenda kumuua kwa kumchoma moto. Aliweza
kuisikia vizuri, rohoni mwake akajikuta akishindwa
kuvumilia kuona tukio hilo likiwa linatendeka.
Mzee Yo, aliyasikiliza mazungumzo hayo hadi
mwisho, bosi wake alipo ondoka katika eneo la
karakana kwa haraka akashuka kutoka ndani ya
ndege. Hakumuaga mtu, akapanda pikipiki yake,
iliyo mpeleka moja kwa moja hadi nyumbani
kwake. Kichwani kwake mawazo mengi yalizidi
kukiandama kichwa chake, kila alipo jaribu kufikiria
jinsi ya kumuokoa Black Shadow, alijikuta
akishindwa kupata jibu kabisa.
“Nitafanyaje wakati kazi hii ni hatari sana. Laiti
bosi akitambua nitakuwa sina kazi na pia anaweza
kuniua”
Mzee Yo alizungumza peke yake akiwa chumbani
kwake amejiinamia kwenye sofa lake. Japo ni
rubani wa muda mrefu katika kampuni ya dokta
Ranjiti, ila leo ndio aliweza kufahamu kwamba
dokta huyo ni mtu katili sana. Kila alipo mfikiria
Black Shadow, kijana ambaye ana ujuzi mkubwa
wa kupigana, hadi akamteka kihisia, hakukubali
kuona anakufa mikononi mwa dokta Ranjiti ambaye
amepewa jukumu la kumtibu. Hakuhitaji kufahamu
ni kitu gani ambacho Black Shadow amekifanya
kwa daktari huyo ila kitu alicho kihitaji ni
kuhakikisha kwamba kijana huyo anakuwa hai.
Kwa haraka haraka, akilini mwake akafikiria ni mtu
gani anayeweza kumsaidia katika kazi hiyo, kura
yake ikatua bibi Eyna. Mwanamke aliye kuwa na
mahusiano naye miaka mingi ya nyuma, kabla
hawajatengana. Akakumbuka kwamba bibi Eyna
anafanya kazi katika hospitali ya dokta Ranjit, kwa
haraka akachukua kitabu chake cha kuhifadhia
kumbukumbu. Akaanza kufungua kurasa kadhaa,
akiitafuta namba ya simu ya bibi huyo. Akabahatika
kuipata namba hiyo. Akaingiza namba hizo kwenye
simu yake ya mkononi, akaiweka sikioni simu yake
na kusikiliza, kwa bahati nzuri simu hiyo iliita kwa
muda kisha ikapokelewa.
“Habari yako Eyna”
Sauti ya Mzee Yo, haikuwa ngeni masikioni
mwake, moyo wa bibi Eyna ukajikuta ukikubwa na
furaha kubwa.
“Safi tu Yo habari za siku nyingi?”
“Safi upo wapi kwa sasa?”
“Nipo kazini”
“Naweza kuja kukuona mpenzi?”
“Mmmm jamani, mpenzi si usubiri nikitoka”
“Hapana ni muhimu sana, nahitaji kukuona mida
hii nina hamu sana na wewe”
“Waooo njoo basi nakusubiria”
Mzee Yo, akakata simu baada ya kutumia mameno
ya ulaghai kwa mpenzi wake huyo, ambaye aliweza
kuachana naye kutoka bibi Eyna enzi za ujana
wake hakutulia na mwanaume mmoja. Ndani ya
dakika thelathini akawa amefika katika hospitali ya
dokta Ranjiti, hakupata tabu sana kuweza kukutana
na Bibi Eyna, ambaye alimkumbatia kwa furaha
mara baada ya kumuona.
Japo ni mzee ila bibi Eyna bado ana hulka za
ujana, hakusita kumpiga mzee Yo busu la
mdomoni.
“Baby nimefurahi kukuona jamani”
“Hata mimi, ila unaonekana una joto kali”
Mzee Yo, alitania, huku kiganja chake akiwa
amekiweka shingoni mwa bibi Eyna.
“Ni joto la kulimisi penzi lako?”
“Kweli?”
“Ndio”
“Ninaweza kukupatia ubaraidi wakati huu?”
“Mmmm jamani, mbona unanisisimua”
“ Sikusisimui ila ninacho kizungumza nina
kimaanisha baby”
Mzee Yo, aliweza kuutambua udhaifu wa
mwanamke huyo, kwani anapenda sana ngono
kuliko hata kula ndio maana walishindwana kipindi
cha ujana wao.
“Sasa hapa tutafanyia wapi mume wangu?”
“Kwani hakuna chumba cha siri tukafanya
mambo?”
Bibi Eyna akaichekecha akili yake kwa haraka huku
akifikiria sehemu gani, akakumbuka kwamba ndani
ya hospitali hapo kuna vyumba vya siri ambavyo
vipo ardhini ila havitumiki kwa muda mrefu sasa.
Hakujua uwepo wa Black Shadow ndani ya moja ya
vyumba hivyo, kwani uwepo wa Black Shawod ni
siri iliyopo kwa madaktari wakubwa tu, hata
madaktari wengine hawatambui.
“Hembu kaa hapo niandae mazingira kisha naja
kukuchukua”
“Mazingira gani baby”
“Ngoja kuna vyumba vipo huko ardhini nahisi huko
kutatufaa mpenzi wangu”
Bibi Eyna akaondoka katika eneo hilo akiwa mwingi
wa furaha na amani sana, haraka haraka akaelekea
kweye ofisi ya dokta Ranjiti akagonga kwa muda,
hakuitikiwa, akausukuma mlango na kukuta
haujafungwa kwa funguo. Akachungulia ndani
hapakuwa na mtu, akaelekea ofisi ya Phidaya,
akagonga pia akukuta hakuna mtu. Akaelekea
katika ofisi ya dokta Yan, ambaye ni msaidizi wa
dokta Ranjiti naku huko pia hakukuta mtu. Siku
hiyo akajiona ni mtu mwenye bahati sana, akarudi
sehemu alipo muacha Mzee Yo. Akamuomba
amfwate kwa nyuma.
Wakaingia kwenye chumba ambacho kina lifti iliyo
washusha chini. Kitendo cha kufika eneo hilo, bibi
Eyna akamkumbatia kimahaba mzee huyo na
kuanza kumpiga mabusu mfululizo.
“Baby tulia kwanza tuchunguze kuna weza kukawa
na mtu humu akatuona ikawa tatizo”
“Baby hakuna mtu bwana”
Mzee Yo, akitazama saa yake ya mkononi
inamuonyesha ni saa mbili usiku. Muda wa Black
Shadow kuja kutolewa kwenye eneo hilo ni saa nne
usiku. Kutokana na yeye ni mwanaume rijari,
hakuona vibaya akampatia haki bibi Eyna, haraka
haraka ili kuzidi kumchanganya na kumuweka
karibu pale ataka anza kufanya mpango wake, kwa
maana anatambu lazima Black Shadow yupo
kwenye chumba hicho, kutokana alisikia jinsi Kim
alivyo kuwa akielekezwa chumba alicho Black
Shadow, kila alama aliyo isikia kwenye ndege ipo
kwenye moja ya mlango.
Kwa haraka, akalipandisha gauni la bibi Eyna hadi
kifuani, akamshusha chupi aliyo ivaa, na yeye
akashusha suruali na nguo yake ya ndani.
Agamshikisha ukuta bibi Eyna, bila hata
maandalizi, ya kumuandaa mwenza wake, akaanza
kumpa haki yake. Bibi Eyna, akaanza kutoa miguno
ya mahaba, kwa kasi ambayo anakwenda nayo
Mzee Yo, ilimfanya apagawe na zaidi ya mara nne,
bibi Eyna alijikuta anafika kileleni. Mzee Yo
akafunga goli lake dakika kumi baada ya mchezo
kuanza. Bibi Eyna akajikuta akikaa chini kwa jinsi
alivyo choka kwani ni muda mrefu hajakutana na
mwanaume wa kumpeleka kasi namna hiyo.
Mzee Yo akapandisha nguo zake, akajiweka sawa,
bila ya kupotaza muda akaanza kufungua mlango
ambao alisikia maelekezo yake yakiwa yanatolewa.
Kweli akamkuta Black Shadow akiwa amelala
kwenye kitanda hicho akiwa hajitambui, ili
kuhakikisha ni yeye akamsogelea karibu, kinyago
cha Black Shadow alicho kivaa kilimuhakikishia
kwamba ndio mwenyewe.
“Haaaa…….!!!”
Sauti ya Bibi Eyna ilimstua akageuka na kumkuta
akiwa amesimama kwenye mlango huku mdomo
wake ukiwa mdomoni.
“Shiiiii”
“Huyo si ndio mgonjwa mbaye alivamiwa majuzi?”
Bibi Eyna alizungumza huku akienda kumtazama
Black Shadow kitandani alipo lala.
“Nahitaji kumtorosha hapa hospitalini”
“Kwa nini?”
“Kuna watu wanahitaji kumuua”
Macho yakamtoka bibi Eyna kwa kushangaa
“Usishangae, dokta Ranjiti anahitaji kumua, sasa
nahiyaji tumtoe kiakili pasipo mtu mwengine
kutambu”
“Si unanitafutia matatizo jambo hili likijulikana”
“Una nipenda ua hunipendi?”
“Nakupenda”
“Fanya kama ninavyo hiaji akiendelea kukaa hapa
ninaimani wakuu wako watakuja kumuua”
“Ina maana dokta Ranjiti anahitaji huyu kijana
kumuua?”
“Hilo ni jibu na si swali, hatuna muda wa kupoteza
nilaziama kumtoa humu ndani”
“Sasa utambeba wapi, kwa maana hivi hivi
ataonekena”
Mzee Yoo akatoka kwenye chumba hicho, akaingia
kwenye chumba kingine, ambapo akakuta maboksi
mengi makubwa yakiwa yamepangwa, akalifunua
boksi moja na kukuta likiwa halina kitu ndani yake,
kwa ukubwa wa boksi hilo akamini kwamba
litamsaidia katika mpango wake.
Akarudi nalo kwenye chumba alipo Black Shadow,
akamkuta bibi Eyna akiwa amelifunua shuka lililo
kuwa limemfunika Black Shadow nusu mwili, msho
uliopo kwenye mbavu zake ukmfanya Mzee Yoo
aumize kichwa kufikiria jinsi ya kumuingiza humo.
“Unataka kumingiza kwenye boksi?”
“Ndio”
“Sasa si ataumia sana?”
“Hakuna jinsi, mshike huko miguuni”
Bibi Eyna akamshika Black Shadow miguuni, Mzee
Yo naye akamshika mabegani, taratibu
wakamuingiza kwenye boksi wakimkunya, kidogo,
akalalia ubavu ambao hauna jeraha. Wakaichomo
mirija ya madripu ya maji. Walipo fanikisha zoezi
lao, wakatoboa matundu mawili madogo ya
kuingizia hewa.
“Yo ttukikamatwa?”
“Hatuwezi kukamatwa?”
“Getini tutatokaje?”
“Gari lako si lipo?”
“Ndio lipo”
“Basi utanisaidia kumtoa getini kisha utanipatia
mbele kwa mbele”
“Mmmmmm haya”
Wakalinyanyua boksi kwa umakini, wakaingia nalo
kwenye lifti, wakafika hadi juu, bibi Eyna
akamuelekeza Mzee Yo mlango wa nyuma wa
hospitali hiyo, ambapo kwa bahati nzuri hakuna
kamera za ulinzi. Bibi Eyna akaenda hadi kwenye
maegesho ya magari, ambapo akachukua gari yake
aina ya Toyota hardbody. Akaipeleka hadi eneo
lilipo boksi na mzee Yo, wakalipakiza boksi kwa
nyuma, kisha mzee Yo akaelekea alipo iacha
pikipiki yake. Bibi Eyna akaliendesha gari lake hadi
getini ambapo alisimamishwa na askari wanao
linda hapo getini.
“Bibi leo naona mataka taka yamekuwa mengi
sana”
Askari huyo alimtania bibi Eyna pasipo kutilia
shaka kwamba ndani ya boksi hilo ndani yake kuna
mtu
“Ndio mjukuu wangu, kuna kazi ya usafi nilikuwa
ninaifanya basi nayapeleka dampo”
“Nikusindikize?”
“Hapana kuna sehemu nitapitia kwanza”
“Ahaa sawa bibi niletee pipi”
“Usijalii mwaaaaaaaaaa”
Askari hao walimzoea bibi huyo kwa tabia yake ya
ucheshi, Mzee Yo akashusha pumzi nyingi baada
ya kuona gari la bibi Eyna limeruhusiwa, akawasha
pikipiki yake, akaelekea hadi getini akakaguliwa,
alipo onekana yupo salama akaruhusiwa na
kuondoka.
Akaelekea njia aliyo kwenda bibi Eyna, akalipita
gari lake na kumuomba amfaywa sehemu wanapo
elekea. Wakatoka kidogo nje ya mji, wakaingia
kwenye barabara ya vumbi. Mwendo wa kilimita
mbili, wakasimama kwenye moja ya kilima,
“Tumefika”
Mzee Yo alizungumza huku akizunguka nyuma ya
gari, bibi Eyna naye akazunguka mara baada ya
kushuka, wajalishusha boksi hilo.
“Wewe nenda uwahi kazini kwako”
“Saa ngapi?”
“Saa tatu kasoro”
“Mungu wangu. Ngoja nikuache baby, utanijulisha
kila kitakacho endelea”
“Sawa”
Bibi Eyna akaondoka kurudi hospitalini, Mzee Yo,
akalifungua boksi na kumtoa taratibu Black
Shadow. Kutokana ana nguvu za kutosha
akambeba kiungalifu, taratibu akapenya naye
kwenye mwanya wa mwamba mkubwa uliopo
kwenye kilima hicho. Akawasha taa zilizo onyesha
eneo zima la ndani, ni pango moja kubwa ambalo
anahifadhia vitu vyake vya thamani sana. Ndani ya
pango lake ameweza kuweka huduma muhimu kwa
binadamu, ambazo mtu anaweza kukaa ndani ya
pango hilo hata zaidi ya mwezi mmoja asitoke nje
kabisa.
Akamlaza Black Shadow kwenye moja ya kitanda,
akamfunika na blangeti zito kutokana na baridi kali
iliyomo ndani ya pango hilo.
Alipo hakikisha kuna usalama, akafungu mlango na
kuanza kutembea kwenye kordo ndefu. Akafika
kwenye ngazi kabla hata hajaanza kuzipandisha,
mlango unao fanania na ukuta ukafunguliwa,
akaingia mtoto anaye mpenda kama mjukuu wake
anaye ishi kwenye kituo cha kulele yatima.
“Soroo vipi umefwata nini huku usiku huu?”
“Nimekuja kukuangalia wewe babu kama upo”
“Sawa tena umenirahisishia, nilikuwa ninakuja
huko huko. Ila twende nikakuonyeshe kitu”
“Umeniletea zawadi nini?”
“Wewe twende”
Akampeleka Soroo, hadi kwenye sehemu alipo
muacha Black Shadow. Soroo alishangaa kumuona
mpiganaji hiyo, kwani aliishia kumuona kwenye
luninga tu. Mzee Yo akamuomba mtoto huyo
alicho kiona iwe siri yake asimueleze mtu wa aina
yoyote hata walezi wa chuo chake wanao mlea.
***
Majira ya saa tano usiku dokta Yan akasimamisha
gari lake kwenye maegesho ya nyumbani kwake,
ukimya uliopo kwenye nyumba yake kidogo
ukaanza kumpa wasiwasi, kwani walinzi wake
wanao zunguka zunguka katika eneo la nyumba
yake leo hawapo.
Akazama ndani ya gari, akachukua bastola yake na
kutoka akiwa ameishika vizuri mkononi mwake.
Akaanza kutembea kwa tahadhari kuelekea ndani
ya nyumba yake. Akafungua mlango kwa tahadhari
kubwa, akawasha taa ya ukutani kwake. Macho
yake yakatua sebleni juu ya meza alipo mkuta
Black Shadow amemuwekea kisu cha shingo mke
wake huku mtoto wake wa miaka mitatu akiwa
amezibwa mdomo, na kufungwa mikono na miguu
kwa nyuma na kulazwa sakafuni akiendelea
kubingiria bingiria huku akilia. Dokta Yan akahisi
haja ndogo ikipenyeza kwenye nguo ya ndani huku
taratibu ikishuka kwenye mapaja yake, kwani
hakufikiria kumuona Black Shadow nyumbani
kwake kwa wakati huo wa usiku.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 60 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (60)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Akazama ndani ya gari, akachukua bastola yake na
kutoka akiwa ameishika vizuri mkononi mwake.
Akaanza kutembea kwa tahadhari kuelekea ndani
ya nyumba yake. Akafungua mlango kwa tahadhari
kubwa, akawasha taa ya ukutani kwake. Macho
yake yakatua sebleni juu ya meza alipo mkuta
Black Shadow amemuwekea kisu cha shingo mke
wake huku mtoto wake wa miaka mitatu akiwa
amezibwa mdomo, na kufungwa mikono na miguu
kwa nyuma na kulazwa sakafuni akiendelea
kubingiria bingiria huku akilia. Dokta Yan akahisi
haja ndogo ikipenyeza kwenye nguo ya ndani huku
taratibu ikishuka kwenye mapaja yake, kwani
hakufikiria kumuona Black Shadow nyumbani
kwake kwa wakati huo wa usiku.
ENDELEA
“Umefwata nini nyumbani kwangu?”
Dokta Yan alizungumza huku taratibu akipiga hatua
za kusonga mbele huku akielekea sehemu alipo
simama Black Shadow na bastola yake akiwa
ameitanguliza mbele.
“Unajua ni kitu gani kilicho nileta hapa”
Sauti ya kike ndio ilimstua dokta Yan, anatambua
fika kwamba Black Shadow ni mwanaume, huyu
aliye kuja kwake usiku huu ni nani
“Weka silaha yako chini la sivyo nitamchinja mke
wako”
Dokta Yan akayatupia macho yake kwa mke wake
anaye tetemeka mwili mzima. Sura ya woga ya
mke wake iliyo jaa machozi mengi ndio ilimfanya
achukue uamuzi wa bila kupinga kuiweka bastola
yake chini.
“Niambie yupo wapi Black Shadow?”
“Sifahamu kusema kweli”
“Acha uongo wewe na doka Rnjiti mulipanga
kumuu kwa kumchoma moto”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya ukali, macho
yakamtoka dokta Yan kwani hakuamini mambo
hayo kuna mtu anayatambua kati yake yeye, dokta
Ranjiti pamoja na Kim, ambaye wamempa jukumu
hilo.
“Moja, mbili, ta……”
“Nasema nasema usimuue mke wangu”
Dokta Yan, alizungmza huku mwili ukimtetemeka
baada ya kuona kisu alicho kishika huyu Black
Shadow wa kike kikianza kupita kwenye shingo ya
mke wake.
“Ni kweli tulipanga hivyo ila alitoka”
Dokta Yan alizungumza huku akipiga magoti chini
mikono yake yote miwili akiwa amevikusanya
viganja vyake kwa pamoja kwa ishara ya
kumyenyekea Black Shadow huyo.
“Muongo wewe”
“Kweli Ranjiti ndio anayejua ni wapi al……..”
Hata kabla dokta Yan hajamalizia sentesi yake,
risasi moja iliyo ingilia kwenye upenyo mdogo wa
kioo, ikatua kichwani mwa dokta Yan na
kumchangua ubongo, watu wote ndani ya nyumba
wakashangaa. Ukunga mkali wa kelele alio utoa
mke wa dokta Yan ndio ulimfanya Shamsa
kustuka. Macho yake akayatupia dirishani risasi
ilipo tokea hakuona mtu. Kwa haraka akatoka nje
huku akiwa anakimbia, akatizama kona zote ila
hapakuwa na mtu. Kwa haraka akarudi katika
sehemu alipo isimamisha pikipiki yake na
kuondoka kwa kasi katika eneo hilo na kuanza
safari ya kurudi hotelini.
Alipo fika njiani, akavua nguo alizo zivaa na
kubakiwa na nguo za ndani, akafungua begi lake
dogo la mgongoni na kuvaa suruali yake pamoja
na tisheti, akaziweka nguo za Black Shadow ndani
ya kabegi kake na kuendelea na safari yake ya
kwenda hotelini.
Haikumchukua muda sana akawa amefika,
akashuka kwenye pikipiki yake na kuanza
kutembea kwa haraka kuelekea kwenye lifi,
akaminya kitufe cha kufungulia lifti hiyo, ilipo
funguka akaingia huku kichwani mwake akiwa
amejawa na msongamano mkubwa wa mawazo.
‘Ni nani atakaye kuwa amemuua’
Shamsa aliwaza kichwani mwake huku akiwa
ameegemea kwenye lifti hiyo huku macho yake
yote akitazama juu. Alipofika kwenye gorofa ya
saba lifti ikafunguka na kuanza kutembea kwa
mwendo wa kasi hadi kwenye mlango wa chumba
chao, akagonga, baada ya dakika mlango
ukafunguliwa na Sa Yoo.
“Vipi umefanikiwa?”
“Hapana dokta Yan amekufa”
Shamsa alizungumza huku akijibwaga kwenye sofa
na kibegi chake akakitupia pembeni
“Weeee, umemuua?”
“Hapana sijamuua mimi”
“Sasa imekuwaje amekufa?”
“Amepigwa risasi hata mimi sitambui ni nani aliye
fanya hivyo”
Sa Yoo akabaki katika alama ya mshangao kwani
swala alilo lisikia nalo ni jipya masikioni mwake.
***
Hali ya Black Shadow, ikaanza kuleta matumaini
machoni mwa Mzee Yo, aliye amua kuchukua
jukumu la kumtibu Black Shadow kwa dawa za
miti asilia. Baada ya Black Shadow, kuzinduka
kutoka usingizini, Mzee Yoo aliweza kumtuliza kwa
maana muda wote aliweza kuliita jina la Phidaya.
Baada ya kumtuliza kwa muda na Black Shadow
kuweza kutulia, Mzee Yo alimueleza kila kitu alicho
kisikia kwenye ndege kikijadiliwa na madaktari
ambao walikuwa wakimtibu.
Mzee Yo, hakusita kuzungumza jitihada ambazo
alizifanya akiwa miongoni mwa mashabaki wake,
jinsi alivyo mtorosha hospitalini na kumleta huku
mapangoni. Eddy akajipapasa usoni mwake na
kukuta kinyago chake kikiwa kichwani. Kwa
maelezo ambayo Mzee Yo amempatia, aliamini
kwamba huyo ni mtu mzuri kwake na mwenye
busara nyingi. Hakuona haja ya kuendele kukaa na
kinyago hicho, taratibu akakifungua na kukivua.
Mzee Yo, akaonekana kushangaa kidogo, ila
akajizuia kwani sura hiyo mara kadhaa aliweza
kuiona kwenye vitua vya televishion vikidai
kwamba mtu huyo ni mualifu.
“Natambua wewe ni mwema kwangu, huto weza
kuzungumza kitu mbele za watu kitakacho
hatarisha maisha yangu”
Eddy alizungumza kwa sauti iliyo jaa unyonge
mwingi, hadi Mzee Yo akamuonea huruma.
“Ndio, wewe si Eddy unaye tafutwa na polisi”?”
“Ndio ni mimi”
Eddy akaanza kumuelezea Mzee Yo historia nzima
tangu alivyo weza kuingia ndani ya Japani, lengo
lililo mleta ndani ya nchi hiyo hakuweza kulitimiza
kutokana na matatizo ambayo yalimpata. Mzee Yo
akatokea kumsikitikia Eddy kwani ni kijana ambaye
hana hatia, ila nchi yake ndio inamuhitaji yeye
kuweza kurudi kuendelea kutumikia taifa lake.
“Kuna mjukuu wangu anaitwa Soroo, huwa mara
kadhaa anakujaga humu kwenye hili handaki
nakumba asiijue sura yake, na endapo kama
atakuja nakuomba uvae hicho kinyago chako”
“Sawa, hilo halina tatizo”
Siku mbili zikakatiza Eddy akiendelea kutibiwa na
Mzee Yo. Dawa alizo zitumia zikazidi kumpa
unafuu wa kupona, maumivu yakaanza kutoweka
siku hadi siku. Siku ya tatu asubuhi Eddy kwa
mbali alihisi vishindo vya mtu akija ndani ya pango
hilo akipitia njia nyingine, kwa haraka akavaa
kinyago chake kama alivyo ambiwa na Mzee Yo,
aliye toka asubuhi kwenda mjini kuangalia hali
halisi inavyo kwenda. Akamuona mtoto ambaye
moyo wake ukampasuka alipo muona kwa mbali,
mtoto huyo anafanana sana na mwanaye Junio. Ila
huyu anaonekana ni mdogo kwa Junio wake.
Mtoto huyo hakuonekana kumshangaa sana Black
Shadow kutokana alimuona tangu siku ya kwanza.
Mtoto huyo alipo mkaribia Black Shadow
akamsalimia huku akimpa mkono. Taratibu Eddy
akachuchumaa na kuushika mkono wa mtoto huyo,
huku kwa mbali macho yake yakimlenga lenga.
“Marahabaa, wewe ni Soroo si ndio”
“Ndio ni mimi”
Uchangamfu wa mtoto huyo ukazidi kumpagawisha
Eddy, kwani Junio wake naye alikuwa hivyo hivyo,
ila sema ndio hivyo hayupo tena duniani.
“Unaendeleaje?”
“Nipo fiti, vipi mbona umeniuliza hivyo?”
“Juzi babu alikuleta ukiwa unaumwa sana”
“Ahaa nipo safi, umekuja kumfwata yeye?”
“Ndio ila pia nimekuja kukujulia hali wewe”
Uongeaji mwingi wa mtoto huyo huwezi kuamini
kwamba ana umri wa miaka minne. Vitu vingi
aliweza kufanana na Junio ila ni vitu vichache tu
ambavyo hajafanana na Junio. Mchana wa siku
hiyo wakapika chakula cha mchana na Black
Shadow huku wakizungumza mambo mengi sana.
Wakala kwa pamoja na jioni ilipo fika Soroo,
akaaga na kuondoka zake,
Siku kadhaa zikakatika Eddy akiendelea kurudi
katika afya yake, taratibu akaanza kufanya mazoezi
ya kukimbia milimani kujiweka fiti. Kadri ya siku
zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kuwa fiti
sana, urafiki wake na Mzee Yo, ukazidi kukomaa
hadi ikatokea kipindi akamchukulia kama baba
yake, kwani mzee huyo aliweza kumlea na
kumchukulia kama mwanaye.
“Malengo yako ni nini Eddy?”
Mzee Yo alimuuliza wakiwa katika meza ya chakula
ndani ya pango hilo.
”Sina familia kwa sasa, kama nilivyo kueleza mke,
mwanangu na mama yangu walifariki siku moja.
Sitamani kurudi Tanzania kwasasabu ni nchi
ambayo nikirejea nitaumia sana pale nitakapo ona
makaburi ya familia yangu”
“Huna mpango wa kuoa?”
Eddy akatulia kwa muda, kumbukumbu zake
zikarudi kwa nesi aliye weza kumuona kwenye
hospitali aliyo kuwa anatibiwa, nesi huyo aliweza
kufanana sana na marehemu mke wake ambaye ni
Phidaya.
“Kuna nesi mmoja niliweza kumuona kwenye
hospitali niliyokuwa ninatibiwa. Yule nesi amefana
sana na mke wangu. Ukiachilia mbali sana huyu
Soroo naye anafanana sana na mwanangu”
“Kweli……!!!?”
“Kweli, sema mwanangu alikuwa ni mkubwa
kumpita yeye”
“Huyu Soroo, ni mtoto wa marehemu rafiki yangu,
alifariki kwa ajali ya ndege akiwa yeye na mke
wake, basi nikaona nimchuku mwanae na
kumkabidhi katika kituo cha kulelea yatima”
“Hapo analelewa na mara kadhaa huwa ninamleta
huku, sikuweza kuishi naye kutokana sina mke
wala mtoto, isitoshe kazi yangu ni yakusafiri safari
sana”
“Ahaaa ulilo lifanya ni jambo jema. Ila laiti kama
mke wangu angekuwa hai basi ningemchukua
huyu mtoto na kumlea kama mwanangu”
Eddy alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga, taratibu akanyanyuka na kutoka nje ya
pango hilo kupunga upepo.
***
Watumishi wengine wa tume ya taifa kwa haraja
wakamnyanyua bwana Barnaba Lukas, na kuanza
kumpa huduma ya kwanza, watu wote walio weza
kuhuduria kwenye viwanja vya tume kuu ya taifa ya
uchaguzi walijikutwa wakibaki katika hali ya sinto
fahamu, kwani kila mmoja alizungmza yake. Kuna
walio sikika wakisema kwamba atakuwa ametupiwa
jinni, wengine walisema labda alichukua pesa za
watu na matokeo yamekwenda ndivyo sivyo.
Bwana Baraba Lukas akawahishwa hospitali kuu ya
Taifa ya Muhimbili, huku jukumu lake akilichukua
makamu msaidizi. Akili na mawazo ya kumfikiria
bwana Lukasa Barnaba yakafutika vichwani mwa
watu walio kusanyika katika eneo hilo. Mawazo
yao wakayarudisha kwenye matoekeo yanayo
kwenda kusomwa dakika chache zilizo pita.
Makamu wake, Bi Mwenda, hakuhitaji kurembesha
wala kuwa na hofu yoyote juu ya kuyatangama
majibu hayo. Akaanza kuwataja walio pata kura
chache za chini kabisa, kisha akabakisha vyama
viwili vilivyo kuwa na ushindani mkubwa sana.
Akameza fumba la mate kusuuza koo lake,
akaiweka vizuri miwani yake kuziona idadi ya kura
zilizo andikwa kwenye karatasi hilo, bila ya
kujishauri mara ya pili. Akamtaja mshindi wa
uchaguzi huo kwamba ni Mzee Godwin.
Wanachama wa chama DTPP, waliopo katika eneo
la viwanja vya tume ya taifa wakajikuta
wakinyanyuka kwenye viti vyao na kushangilia kwa
nguvu. Kelele na vifijo vikatawala maeneo yote ya
Tanzania. Shangwe na vigelegele, vikazidi kutawala
kwa watu wote walio kiunga mkono chama cha
DTPP, wanachama wa chama tawala walio kuwa
wakimuunga mkono Raisi Praygod Makuya,
wengine walishindwa kuyazuia machozi yao kuona
raisi wao akiwa ameshindwa kwenye kura zilizo
pigwa Tanzania nzima. Wengine walijikuta
wakimbeza raisi wao mpya kwamba ni gaidi,
wengine walijaribu kuleta fujo kwenye baadhi ya
vituo ambavyo walikwenda kupiga kura wakidai
kwamba kura zimechakachuliwa. Ila walicho
ambalia ni kipigo kikali kutoka kaika askari wa
kutuliza ghasia FFU. Na wengine wakajikuta
wakisota maabusu kwa kutokana na kukamatwa.
Raisi Praygod hakuamini kwamba ndio hivyo
ameng’atuka madarakani, mambo aliyo mfanyia
mzee Godwin, yakaanza kujirudia kama mkanda wa
video kichwani mwake, akakumbuka jinsi alivyo
hakikisha kwamba anamsaka kwa udi na uvumba
kama gaidi, leo hii anampisha ikulu gaidi huyo.
‘Si ataniua huyu?’
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa amejilaza
kwenye sofa lake, machozi yakimlenga lenga.
***
Kitendo cha dokta Yan kuuawa kilizidi kumkosesha
amani Shamsa, hata asubuhi kulipo
pambazukafuraha yake haikuwa kama siku
nyingine. Kitu cha kwanza alicho kifanya ni
kuwasha Tv, iliyopo chumbani kwao, akatazama
kitu gani kinacho endelea. Kweli akakuta taarifa ya
dokta Yan kuuawa ikiwa imeshika vichwa vya
habari, huku ikisadikika kwamba muuji aliye fanya
tukio hilo la mauji alikuwa nje ya nyumba hiyo.
Polisi wakatangaza kufanya uchunguzi mkali kwa
daktari huyo kuuawa. Mlango ukagongwa, Shamsa
kwa haraka akayatupia macho yake kwenye mlngo
huo, wasiwasi mwingi ukamjaa na kujiuliza ni nani
ambaye anagonga mlango asubuhi hiyo.
Akanyanyuka na kwenda kuufungua, akamkuta
Phidaya akiwa amesimama nje ya mlango huo
akiwa na wasiwasi mwingi huku amevalia nguo
nyeusi tupu.
“Mama vipi mbona hivyo?”
Shamsa alizungumza baada ya kuufunga mlango
kwa ndani, huku akimfwata Phidaya kwa nyuma
kuelekea kwenye sofa.
“Niambie ukweli mwanangu si wewe uliye muua
dokta Yan?”
Phidaya alizungumza kama mtu aliye
changanyikiwa, kidogo Shamsa akastuka,
akashusha pumzi nyingi chini na kujiweka vizuri
kwenye sofa huku akimgeukia Phidaya.
“Mama amini mwanao wa kike siwezi kufanya
mauji”
Phidaya kusikia kuali hiyo ya Shamsa
akamkumbatia kwa furaha, kwani mpango mzima
wa Shamsa kwenda kwenye nyumba ya dokta Yan,
Phidaya aliuelewa vizuri sana.
“Nisikudanganye mwanangu tangu nilipo sikia
taarifa ya dokta Yan kuuawa basi nilitambua
kwamba wewe ndio umefanya hivyo”
“Hapana mama siwezi kufanya hilo swala”
“Eheee niambie imekuwaje kuwaje”
“Nilikwenda hadi pale lisaa moja kabla sijaingia
nyumbani kwake, niligundua kwamba anaishi na
mke wake pamoja na mtoto wake, nyumba yake
ilikuwa na walinzi wanne hivi….”
“Lengo langu lilikuwa ni kumbana akiwa anashuka
kwenye gari ila nikaona ni wazo baya, nilicho fanya
ni kuwazimisha moto walinzi wote kisha…..”
“Ngoja kwanza, mwanangu. Kuzimisha moto ndio
nini?”
“Hahaa mama, kuwazimisha moto ni kuwazimisha”
“Ahaaa kwahiyo uliwapiga hadi wakazimia?”
“Ndioo, hujakosea”
“Ehee niambie ikawaje?”
Phidaya alizungumza kwa furaha huku meno yake
yote thelethini na mbili yakiwa nje
“Walinzi wenyewe wachovu hao, basi niliingia
ndani na kumbananisha mkewe pamoja na
mwanaye, haikupita muda sana akaja kuingia tu
ndani mtu mzima mwili mzima ulikuwa
unamtetemeka”
“Ila kwa bahati mbaya sikufanikiwa kutambua
Black Shadow ni sehemu gani alipom kwani mauti
yalimpata”
“Mmmm mwanangu unatakiwa kuwa makini, yaani
sitambui nikupe zawadi gani leo”
“Zawadi kwa kazi gani niliyo ifanya?”
“Htahiyo uliyo ifanya ni nzuri?”
“Kwanza dokta Ranjiti amerudi nyumbani?”
“Bado yupo Korea, nilijaribu kumtafuta hewani
namba yake haipatikani, sasa sijajua kama taarifa
za mwenzake amezipata”
“Mmmmm sijui”
“Muamshe na mwenzako twende kwenye maduka
ya nguo mukachague nguo kisha mimi nitakwenda
msibani si unajua inabidi kuwa karibu na
wanafamilia yake”
“Ahaa sawa mama”
Shamsa akamuamsha Sa Yoo, akamueleza juu ya
safari hiyo ya asubuhi, Sa Yoo kutokana na
kupenda kwake kuvaa haraka haraka akaanza
kujiandaa, kwa siku hiyo wala hakutamani kunywa
chai, walipo maliza wote wakatoka kuelekea
kwenye maduka makubwa kwenda kuchagua nguo
watakazo
***
Asubuhi na mapema Mzeee Yoo na Eddy aliye
valia kofia iliyo shuka kidogo na kuuficha uso
wake, huku akiwa amejipachika ndevu za bandia
zilizo mbadilisha muonekano wake, waliianza safari
yako kutoka kwenye msitu wanai ishi kuelekea
mjini, wakiwa kwenye pikipiki. Utaalamu wa
uendeshaji wa pikipiki wa mzee Yo, ulimfanya Eddy
kuufurahia kwani aliweza kwenda kasi sana kupita
hata magari ambayo yamewatangulia.
Wakaingia mjini majira ya saa tatu, habari ya kifo
cha dokta Yan ndio ilikuwa ikizungumziwa kila
mahali walipo pita. Wakaingia kwenye moja ya
mgahawa kujipatia kifungua kinywa.
“Huyu dokta ni mmoja wa madaktari walio kuwa
wakikutibu?”
“Weee”
“Yaa na ndio daktari ambaye alihusika katika
mipango ya kutaka kukuaa. Masikini ya Mungu
katangulia yeye kabla yako”
“Doo dunia hii, alitaka kuniua mim kisa nini?”
“Wala sielewi”
“Mungu amsam……”
Eddy hakuimalizia sentensi yake akamuona nesi
aliye muona hospitalini akitoka kwenye moja ya
duka kubwa la nguo lililopo upande wa pili wa
barabara, akiwa amevalia nguo nyeusi huku
akizungumza na simu. Akaweka kikombe cha chai
taratibu mezani, Mzee Yo naye aliweza
kumshuhudia Phidaya mke wa bosi wake dokta
Ranjiti akiwa amesimama kwenye duka hilo kubwa
maarufu kwa uuzaji wa nguo za kike. Taratibu
Eddy akasimama kutoka kwenye kiti alicho kuwa
amekalia, akaanza kupiga hatua za haraka kuelea
barabarani huku macho yake akiwa amemkazia
Phidaya ambaye yupo bize kwa kuzungumza na
simu.
Gafla hata kabla hajaanza kuvuka barabara, gari
moja jeusi aina ya haisi, likasimama sehemu alipo
simama Phidaya, wakashuka watu wawili walio
valio vinyago vyeusi wakamata kwa nguvu na
kumuingiza ndnai ya gari hilo na kuondoka naye
kwa nguvu, kitendo kilicho shuhudiwa na Eddy
pamoja na Shamsa, kupitia kwenye kioo kikubwa
akiwa ndani ya duka hilo. Eddy akavuka kwa kasi
bilia kujali magari yanayo pita kwenye barabara
hiyo huku Shamsa naye akitoka kwa kasi nje, wote
wawili wakajikuta wakisimama katika sehemu aliyo
tekewa Phidaya na macho yao wakilishuhudia gari
hiyo ikitokomea kwa mbali.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 61 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (61)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Gafla hata kabla hajaanza kuvuka barabara, gari
moja jeusi aina ya haisi, likasimama sehemu alipo
simama Phidaya, wakashuka watu wawili walio
valio vinyago vyeusi wakamata kwa nguvu na
kumuingiza ndnai ya gari hilo na kuondoka naye
kwa nguvu, kitendo kilicho shuhudiwa na Eddy
pamoja na Shamsa, kupitia kwenye kioo kikubwa
akiwa ndani ya duka hilo. Eddy akavuka kwa kasi
bilia kujali magari yanayo pita kwenye barabara
hiyo huku Shamsa naye akitoka kwa kasi nje, wote
wawili wakajikuta wakisimama katika sehemu aliyo
tekewa Phidaya na macho yao wakilishuhudia gari
hiyo ikitokomea kwa mbali.
ENDELEA
Kila mmoja alishusha pumzi, akifikiria cha kufanya,
Sa Yoo, akatoka huku akiwa ameshika mfuko ulio
jaa nguo
“Kumetokea nini?”
Wote wawili wakamtazama Sa Yoo, ambaye kidogo
akaonyesha mstuko baada ya kumtazama Eddy
usoni, Eddy naye aliweza kumtambua Sa Yoo. Ni
binti aliye weza kumsaidia na aliachana naye siku
walipo kwenda hospitalini. Jinsi Sa Yoo alivyo
kuwa akimtazama Eddy machoni huku akimsogelea
taratibu, kukamfanya Shamsa naye kumtazama
mwanaume aliye kuja kusimama naye hapo
akionekana aliliona tukio hilo. Macho yalimtoka
Shamsa, mapigo ya moyo kidogo yakaanza
kumenda mbio, akatamani kuliita jina la Eddy ila
kigugumizi cha gafla kikamfanya aishie kupanua
mdomo wake akimshangaa Eddy.
“Wewe si Eddy?”
Sa Yoo alizungumza huku akibonyea kidogo na
kuchungulia Eddy, usoni mwake kwani kofia yake
iliuziba uso wake kwa kiasi kikubwa. Japo amevaa
ndevu za bandia ila Sa Yoo aliweza kumtambua
haraka na kulitaja jina lake. Eddy hakujibu
chochote iku kuwazugisha akajifanya akigeukia
kule lilipo kuwa linaelekea gari. Macho ya Eddy
yakawashuhudia askari wawili wakija katika eneo
hilo, Eddy hakuona haja ya kuendelea kusiamam
hapo kwani alitambua askari hao wanaweza
kumuharibia siku yake, akatazama barabara pande
zote mbili hapakuwa na gari inayo kuja akavuka
kwa haraka, Shamsa akataka kumfwata ila Sa Yoo
akamzuia kwani kuna gari ambayo ilikuwa inapita
kwa kasi na endapo angepita basi angegongwa.
“Heii miss, mbona huangalii magari?”
Askari mmoja alizungumza huku akimtazama
Shamsa usoni mwake.
“Ohoo samahani maafisa, kidogo ana mawazo?”
“Kwani kuna tatizo kati yenu?”
Askari mwengine aliuliza huku akimtazama Eddy
aliyekuwa akipanda pikipiki, akiondoka na mzee
Yo.
“Ahaaahah hakuna”
Sa Yoo yeye ndio alikuwa mjibuji wa maswali hayo,
kwani Shamsa wakati wote macho yake
aliyaelekezea kwenye pikipiki iliyo kuwa ikitokomea
upande wa pili, ikakunja kona kulia na hakuiona
tena.
“Madam una mawazo sana”
“Eheeee”
Shamsa akastuka kutoka kwenye dibwi zito la
mawazo akimfikiria mtu aliye muna ni Eddy, swali
alilo jiuliza mbona mtu huyo hakuweza kusema
kitu chochote zaidi ya kuondoka. Wazo la Phidaya
kutekwa likamjia upya akilini mwake.
“Mama ametekwa”
“Ametekwa, ametekwa saa ngapi si alitoka nje
kuzungumza na simu?”
“Sa Yoo kuwa muelewa mama ametekwa”
Habari hiyo ikawastua hadi polisi hao, wakaanza
kumuhoji maswali Shamsa, akaelezea jinsi alivyo
weza kushuhudia, askari mmoja akaondoka
kulifwata gari lao na kurudi nalo katika sehemu
alipo mwezake kwa ajili ya kumchukua Shamsa
kwenda naye kituoni kutoa maelezo yakutosha.
Shamsa akamkabidhi Sa Yoo funguo ya gari la
Phidaya na kumuomba awafwate kwa nyuma, na
awasiliane na Lee Si na kumpa habari ya kutekwa
kwa Phidaya. Sa Yoo akaingia kwenye gari la
Phidaya akiwa na fuko lake lililo jaa nguo nyingi.
Akaanza kulifwata gari la polisi kwa nyuma, akatoa
simu kwenye mfuko wa jinzi alilo livaa, akatafuta
namba ya Lee Si kwenye orodha ya majina yake
kweney simu hiyo na kumpigia, siku kwa mara ya
kwanza ikaita na kukatwa, akapiga tena akakuta
simu ikiwa imezimwa kabisa.
“Mmmmmmm……….”
Aliguna Sa Yoo na kuirudisha simu yake mfukoni
na kuzidi kulifwata gari la polisi kwa nyuma hadi
katika kituo kikuu cha polisi nchini Japani
***
Mawazo mengi yakazidi kukisonga kichwa cha
Eddy, akajiona ni mkosaji kushindwa kuzungumza
chochote mbele ya Shamsa, ili kujulikana. Kila
alipo likumbuka busu la Shamsa, machozi
yakamtoka akatambua ni wazi kwamba mwanaye
huyo amempenda, pasipo kujua kwamba
amempenda mtu anaye muheshimu kama baba
yake japo hakumzaa. Jambo jingine lililo zidi
kumchanganya Eddy akilini mwake ni uwepo wa
Phidaya nje ya duka ambalo Shamsa aliweza
kutoka.
‘Ina maana Shamsa na huyu nesi wanajuana?’
‘Na wamejuana vipi? Au ni Phidaya mke wangu?’
‘Mmmm Phidaya wangu amekufa huyu si yeye’
Eddy aliwaza huku akiwa juu ya pikipiki ya Mzee
Yo, ambaye ndio dereva, wakafika kwenye moja ya
soko huku Eddy mara zote akiwa sura yake
ameiweka chini, hakuhitaji kuinyanyua isije watu
wakaistukia kama Sa Yoo ameweza kumtambua
kwa haraka kiasi kile japo kuwa ameweka ndevu
za bandia usoni mwake basi akaamini kwamba
hata mtu wa kawaida anaweza kumtambua na
ikawa ni tatizo kubwa kwake kutokana donge nono
la zawadi ambalo wamelitangaza polisi, kila
mwananchi aliamini kwamba analitamani kulipata.
Baada ya kununua manunuzi walio ona yanatosha,
wakaanza safari ya kwenda mapangoni wanapo
ishi. Mzee Yoo, alikituma kipindi hichi cha likizo
vizuri kukaa mapangoni akifurahia uwepo wa Eddy
aliye mchukulia kama mwanaye wa kumzaa
***
Kitendo cha Phidaya kumueleza Lee Si mpango wa
Shamsa wa kutaka kumvamia dokta Yan usiku,
hakujua ni jambo gani ambalo lingeweza kutokea.
Lee Si alipo maliza majukumu ya kumrudisha bosi
wake nyumbani kwake, akarudi hotelina ambapo
amepangishiwa kwa muda na boasi wake hapo,
kujificha kuepuka uvamizi wa Kim, ambaye hadi
sasa hivi atambui yupo wapi wala ana mpango
gani ambao anahitaji kuweza kuufanya.
Lee Si, akachukua bastola yake, iliyo jaa risasi za
kutosha, akaifunga kiwambo cha kuzia sauti alipo,
hakikisha kwamba majukumu yake yamekamilika,
akajilaza kitandani kwake, mara kwa mara macho
yake akawa anayatupia kwenye saa ya ukutani.
Ilipo jiri saa nne kamili usiku akanyanyuka
kitandani, akavaa mavazi meuzi, kisha akachukua
koti lake kubwa jeusi na refu, akilivaa linamfika
magotini.
Alipo hakikisha yupo vizuri akashuka hadi gorofa
ya chini, akaelekea kwenye maegesho ya magari,
akaingia kwenye gari lake na safari ya kueleka kwa
dokta Yan ikaanza.
Akalisimamisha gari lake mbali kidogo na ilipo
nyumba ya dokta Yan, akalivaa koti lake pamoja na
miwani nyeusi. Akaanza kutembea kwa tahadhari
hadi karibu kabisa na yumba ya dokta Yan. Kitu
kilicho mtisha ni kukuta walinzi wakiwa
wamelundikwa kwenye stoo, hawajitambui, machale
yakaanza kumcheza na kutambua kwamba Shamsa
si msichana wa kawaida kama alivyo kuwa
akimchukulia hapo awali, kwani ni yeye pekee ndio
alikuwa na mpango wa kufika katika nyumba hiyo.
Akajibanza kwenye moja ya ua alipo muona dokta
Yan akishuka kwenye gari lake, akataka kumvamia
ila akasita alipo muona dokta huyo akiwa amejawa
na wasiwasi mwingi sana. Alipo muona dokta huyo
akiingia ndani ya gari lake na kutoka na bastola
akatambua kwamba lazima daktari Yan atakuwa
ameshtukia hali inayo endelea. Kitu kingine alicho
hitaji kujua ni nani aliye ifanya kazi hiyo ya
kuwapiga walinzi, japo ana muhisi Shamsa, basi
akahitaji kudhibitisha kwamba ni yeye, au laa.
Akanyata hadi kwenye dirisha, la kioo, akasikiliza
jinsi dokta Yan akijitetea, akaisikia pia sauti ya
Shamsa, ila katika sehemu alipo simama hakuweza
kumuona Shamza zaidi ya dokta Yan, aliye anza
kupiga magoti taratibu.
Lee Si, hakuhitaji siri ambayo ipo kati ya bosi wake
na mke wake iweze kutoka, kwani anaitambua
vizuri sana, akaikoki bastola yake vizuri, akavuta
jicho moja, akakiweka kichwa cha dokta Yan
katikati ya shabaha yake, na kufyatua risasi moja
iliyo tua kichwani mwa dokta Yan na kumuangusha
chini na kufa hapo hapo.
Hapakuwa na mlio wa risasi hiyo iliyo kuwa ikitoka
kwenye bostola yeke kwani tayari alisha ifunga
kiwambo cha kuzuia risasi. Kwa haraka akaondoka
na kukimbilia kwenye gari lake, akaondoka kwa
kasi na kurudi zake hotelini, kuhakikisha kwamba
Shamsa hawai kufika kabla yake.
Akafika hotelini, kwa haraka akapandisha gorofani
kwake huku koti lake akiwa amelishika mkononi,
akaingia chumbani mwake, akatoa simu yake
mfukoni na kumpigia dokta Ranjiti.
“Bosi nimemaliza kazi”
“Safi kijana wangu, hakikisha na kesho unaifanya
kazi niliyo kuagiza madhubuti”
“Sawa mkuu”
Lee Si, akakata simu akavua nguo zake zote na
kuingia bafuni kuoga.
***
Maelezo ya Shamsa, yakachukuliwa vizuri na
askari wapelelezi, wakamuhoji na Sa Yoo,
akaelekeza alicho kishuhudia, kisha wakaruhusiwa
kuondoka kituoni. Upelelezi wa kupotea kwa mke
wa daktari maarufu nchini Japan bwana Ranjiti,
ukaanza mara moja, ulinzi ukaimarishwa kwenye
sehemu muhimu, kama katika viwanja vya ndege,
bandari na stendi zote za mabasi yaendayo nje ya
mikoa.
Swala hilo likavuja kwa waandishi wa habari ambao
hawakusita kutumi taaluma yao, katika kuwajulisha
wananchi kwamba mke wa dokta Ranjiti amatekwa
na watu wasio julikana. Picha za Phidaya zikaanza
kuonyeshwa kwenye vituo mbalimbali vya
televishion pamoja na kwenye magezeti yanayo
toka majira ya jioni yakiwa yamekusanya habari za
kutwa nzima kuanzia asubuhi hadi jioni.
Habari hizo zilizidi kuwakosesha amani Shamsa na
Sa Yoo, pia walihofia usalama wao kwani
hawakujua ni kitu gani kinaweza kutokea wakato
wowote.
Wakarudi hotelini wakiwa katika mashaka
makubwa, wakiwa wanasubiria lifti ya kupanda
gorofani ifunguke, lifti ya pembeni ikafunguka,
akatoka Lee Si, akionekana mwenye wasiwasi
mwingi.
“Madam mu…muunataka kuniamb….ia amete…
kwa?”
Lee Si, aliuliza akiwa na wasiwasi mwingi sana
usoni mwake.
“Ndio mbona nilikuwa nakupigia simu hupokei?”
Sa Yoo alimuuliza Lee SSi huku akiwa amemkazia
macho na kwajinsi macho yake yalivyo kuwa
makubwa kiasi na makali pale anapo mkazia mtu,
basi Lee Si, akajikuta akizidi kuogopa.
“Nilikuwa nimelala na simu ikawa imezima chaji”
“Mende mkubwa wewe, unajali usingizi kuliko
boasi wako…..”
Sa Yoo alizungumza kwa kufoka huku akiuvuta
mdomo wake, Shamsa akamzuia asimrushie kofi
Lee Si, kwani alimuona hana hatia yoyote kwani
kosa kubwa amelifanya Phidaya kwa kuto mtaarifu
mlinzi wake huyo kwamba anatoka kama anavyo
fanya siku zote. Ikabidi Lee Si, arudi nao,
wakaingia kwenye lifti na kurudi hadi kwenye
chumba wanacho ishi Shamsa na Sa Yoo.
Kila mmoja akakaa kwenye sehemu aliyo ona
inamfaa, mawazo mengi yalizidi kumchanganya
Shamsa, hakujua afanye nini ili kumkomboa mama
yake.
“Wewe unakaa kimya nini sasa, toa mawazo tujue
tunafanyaje”
Sa Yoo alizungumza huku kidole chake akiwa
amemnyooshea Lee Si, aliye kiinamisha kichwa
chake chini, Lee Si akamtazama Sa Yoo kwa
macho yaliyo jaa huruma, hakuzungumza chochote
zaidi ya kuangalia chini tena.
“Tusubirie tuone polisi watatuambia nini”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku
akimtazama Sa Yoo aliye kasirika kwa kununa.
***
Furaha na amani ikatoweka moyoni mwa Eddy,
jambo ambalo Mzee Yo alilistukia mapema,
akajitahidi anampikia Eddy chakula anacho
kipenda, kisha aweze kumfariji mwanaye huyo.
Mzee Yo alipo maziza kupika chakula
akamkaribisha Eddy mezani.
Eddy hakuzungumza chochote zaidi ya kutala
taratibu, mara kadhaa alisikika akisunya, Mzee Yo
akuzungumza chochote hadi walipo maliza kula
chakua.
“Mbona leo una mawazo mengi?”
“Namfikiria yule nesi aliye tekwa?”
“Ahaa yule ni mke wa bwana Ranjiti, kwa jinsi ya
kifo cha dokta Yan kilivyo tokea basi nahisi hapa
kuna mtu anawafwatilia wafanyakazi wake”
“Una taka kuniambia yule nesi ni mke wa daktari
aliye hitaji kuniua mimi?”
“Ndio”
“Hapa kuna jambo ambalo linaendelea na
halieleweki?”
“Kivipi?”
“Si fahamu ila nahisi kuja kitu kinacho endelea
kinacho peleka mambo yote hayo kutoke”
”Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa chini chini”
“Basi nitaomba tuunze kuufa leo hii hii”
“Kwa leo kwako haitakuwa salama, ninaimani sasa
hivi kutakuwa na msakako mkali unaendelea kwa
mtu aliye mteka mke wa dokta”
“Hivi anaitwa nani?”
“Anaitwa Phidaya”
Moyo wa Eddy ukapiga paaa, akahisi labda
hajalisikia vizuri jina alilo tajiwa, akamuomba Mzee
Yo alitaje tena, bila hata kukosea Mzee Yo akalitaja
jina hilo kama lilivyo, akazidi kumchanganya Eddy,
na kumpa hisia ambazo masaa machache ya
nyuma alizikataa na kuamini kwamba mke wake
kwa sasa ni marehemu.
Mzee Yo majira ya jioni akaondoka mapangoni na
kuelekea mjini kuchunguza ni nini kinacho endelea,
huku akiwa ameagiziwa na Eddy kumnunulia nguo
za Black Shadow, ili kurudi kazini kwa lengo moja
kufahamu mke wa dokta Ranjiti ni Phidaya wake au
laa na kama ni Phidaya wake, basi dokta huyo
atatoa maelezo yakutosha juu ya kitu alicho
kifanya hadi kumchukua mke wake.
***
Sindano ya usingizi aliyo chomwa Phidaya mara
baada ya kukamatwa na kuingizwa ndani ya gari,
na watu walio zifunika nyuso zao. Ilimfanya kulala
fofo na kuto kujitambua ni wapi anapo pelekwa.
Lee Si, akavua kinyago chake na kumuangalia bosi
wake huyo, ambaye kusema kweli ni msichana
mzuri na mrembo sana. Ila kutokana yeye
anafwata maagizo yake kama alivyo ambiwa na
bosi wake, ilibidi kuziweka hisia za kimapenzi
kando na kuangalia kazi ambayo amepewa. Akavaa
kinyago chake. Wakafika kwenye karakana na dokta
Ranjiti, wakaingia ndani Lee Si akambeba Phidaya
begani na kumuingiza kwenye ndege moja iliyo
andaliwa kwa safari ya kuelekea Korea kusini.
Alipo hakikisha amekabidhisha kwa wahudumu wa
ndege hiyo, wanao fwata amri za dokta Ranjiti,
akashuka na kuhakikisha ndege inaondoka eneo
hilo pasipo mchezo wowote kuweza kufanyika.
Marafiki zake alio saidiana nao kwenye kazi hiyo,
akawapa kila mmoja kiasi cha pesa walicho
kubaliana wao wakaondoka kisha yeye akaingia
kwenye gari lake na kurudi hotelini haraka.
Akafika hotelini na kufikiria ni mbinu gani anayo
weza kuitumia kuhakikisha kwamba si Shamsa
wala Sa Yoo anaweza kumstukia kiurahisi. Muda
wote aliweza kusimama dirishani akitazama nje
kuona kama wamerudi, haukupita muda mrefu
sana akawaona wakishuka kwenye gari la Phidaya,
lwa haraka akavaa nguo nyingine tofauti na alizo
kuwa amezivaa wakati alipo kuwa akienda kufanya
kazi yake. Akaingia kwenye moja ya lifti akiwa na
imani kwamba atawawahi Shamsa na Sa Yoo
wakiwa bado hawajaingia kwenye lifti na ndivyo
alivyo wakuta wakisubiria lifti ya kupandishia
gorofani.
***
Dakika chache yangu ndege aliyo pkizwa Phidaya
kuwa hewani, ikaanza kuyumba. Upepo mkali, ulio
sababishwa na hali ya hewa mbaya ukapelekea
ndege kupoteza mawasiliano. Ndege hiyo ya
kifahari inayo ingia abiria wanne pamoja na
wahudumu walili, ikazidi kwenda mrama.
Msukosuko mkali huo uiwafanya wahudumu hao
kujkibamioza kwenye siti, wote wawili kila mmoja
aliliita jina la mama yake. Kwani wanaelewa kitu
kinacho kwenda kutokea kwa wakati huo ni ndege
hiyo kuanguka chini na wote watakuwa marehemu
ndani ya dakika chache zijazo.
Kelele za wasichana hao kwa mbali zikaanza
kupenya masikioni mwa Phidaya aliye jitahidi
kuyafumbua macho yake yaliyo jaa ukungu wa
usingizi. Akafanikiwa kuyafungua macho yake, ila
akastuka kujikuta miguu yake ikiwa juu, huku
kichwa chake kikiwa chini, akiwatazama wasichana
hao wawili wakiwa wamelala kila mmoja sehemu
yake katika sehemu ambayo endapo ndege isinge
geuka basi sehemu hiyo ingekuwa juu. Kitu kilicho
msadia Phidaya kuto kufwatana na wasichana hao
ni mkanda pekee wa siti alio kalio ulio mbana
vizuri kiunoni mwake.
Kabla hata hajafacha chochote akastukia ndege
hiyo ililala ubavubavu na kuanza kwenda kasi
kuelekea chini jambo ambalo naye pia aliweza
kuogopa na kuanza kupiga kelele za kuomba
msaada
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 62 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (62)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Kelele za wasichana hao kwa mbali zikaanza
kupenya masikioni mwa Phidaya aliye jitahidi
kuyafumbua macho yake yaliyo jaa ukungu wa
usingizi. Akafanikiwa kuyafungua macho yake, ila
akastuka kujikuta miguu yake ikiwa juu, huku
kichwa chake kikiwa chini, akiwatazama wasichana
hao wawili wakiwa wamelala kila mmoja sehemu
yake katika sehemu ambayo endapo ndege isinge
geuka basi sehemu hiyo ingekuwa juu. Kitu kilicho
msadia Phidaya kuto kufwatana na wasichana hao
ni mkanda pekee wa siti alio kalio ulio mbana
vizuri kiunoni mwake.
Kabla hata hajafacha chochote akastukia ndege
hiyo ililala ubavubavu na kuanza kwenda kasi
kuelekea chini jambo ambalo naye pia aliweza
kuogopa na kuanza kupiga kelele za kuomba
msaada
ENDELEA
Rubani hakukata tama kuweza kuhakikisha
anaiweka ndege hiyo kwenye hali yake ya kawaida,
kwa bahati nzuri taratibu juhudi zake zikazaa
matumaini, ndege akaiweka sawa, na kuhakikisha
kwamba inaanza kupanda juu taratibu kwani
ilishuka chini kwa kiasi kikubwa na uzuri ni
kwamba ipo katika usawa wa bahari. Ikamachukua
dakika kumi hadi ndege kurudi katika hali yake ya
kawaida. Kila mmoja ndani ya ndege hiyo akawa
anahemea upande wake hususani waudumu wa
ndege ambao mmoja kidogo alipata majeraha
kwenye paji la uso wake.
“Samahani ndugu abiria, kwa hali iliyo jitokeza na
kwa sasa hali imekuwa shwari samani kwa
usumbufu”
Sauti ya rubani ilisikika kwenye kipaza sauti kilicho
fungwa ndani ya ndege hiyo. Phidaya
akaichunguza ndege hiyo na kugundua ni malia ya
mume wake.
“Munanipeleka wapi?”
Phidaya aliwauliza wahudumu, ambao, kila mmoja
anajikanda katika jeraha lake sehemu alipo umia.
“Madam hii ni safari ya Cairo Misri”
“KKufanya nini?”
“Muheshimiwa anakusubiria huku”
“Ina maana yeye ndio aliye niteka?”
Phidaya aliuliza kwa sauti ya hasira huku machozi
yakimlenga lenga. Hapakuwa na muhudumu aliye
weza kulijibu swali hilo, kila mmoja alikaa kimya
huku akiinamisha kichwa chake chini asiitazame
sura ya Phidaya iliyo fura kwa hasira.
***
Wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani
na nje ya mkoa wa Dar er Salaam, wamekusanyika
katika kiwacha cha mpira cha Mwalimu Julius
K.Nyerere. Wengi wao ni wapinzani wa chama
kilicho kuwa kinaongoza nchi, wengi walifika
kushuhudia jinsi raisi mpaya Mzee Godwin
akiapishwa. Ulinzi mkali ukazidi kuimrishwa kila
kona ya uwanja na maeneo ya uwanja. Vyombo
vya kisasa vya ulinzi viliweza kufungwa sehemu
mbalimbali kuhakikisha kwamba hapajitokezi
shambulizi lolote ambalo litahatarisha maisha ya
wananchi walio jitokeza.
Askari polisi nao hawakuwa nyuma katika
kuangalia swala zima la ulinzi, waliweza kubeba
bunduki za moto huku wengine wakiwa na virungu
pamoja na mbwa wanao nusa mabomu.
Shangwe na nderemo zilisikika kila sehemu,
uhasama wa kisiasi tayari ulisha yayuka mioyoni
mwa watu wengi na kujikuta ni wamoja. Wakaanza
kuingia viongozi mbalimbali kutoka maeneo tofauti,
ndani na nje ya nchi, ikiwemo maraisi wa Kenya,
Uganda, Burundi na Rwanda. Nao walifika kuona
kuapishwa kwa raisi mpya kutoka chama pinzani.
Kati ya wananchi ambao waliweza kukusanyika
eneo hilo, Madam Mery naye nimiongoni mwao.
Sura yake aliyo ificha kwa kofia pamoja na nywele
ndefu za wigi alilo shonea, alijiweka katikati ya
wafuasi wa chama cha Mzee Godwin, ili
kuhakikisha kwamba ni Godwin anaye mjua yeye
au laa. Haikupita muda mwingi msafara wa Mzee
Godwin ukaingia, uwanjani, ukiwa katika ulinzi
mkali sana, watu walinyanyuka na kushangilia kwa
furaha sana.
Chuki juu ya Mzee Godwin, ikazidi kuongezeka
moyoni mwa Madam Mery, machozi ya uchungu
yalizidi kumtiririka, kila alipo mtazama jinsi anavyo
punga mkono kwa wananchi. Aliamini wananchi
hawajui maovu ya mzee huyo na endapo
wangeyajua basi wasinge dhubutu kumpa hata
kura moja.
Taratibu za kuapishwa zikaanza, raisi Praygod
akakabidhi cheo na majukumu yake kwa raisi
mpya bwana Godwin, wakakumbatia kila mmoja
akiwa na chuki moyoni mwake ila hawakuzihitaji
kuzionyesha hadharani kwa watu walio kusanyika.
“Nakupa masaa ishirini na nne uwe umefunga
virago vyako na kuhama hii nchi”
Mzee Godwin alimnong’oneza raisi msatafu bwana
Praygod, aliye stuka kwa maneno hayo ambayo
inadhihirisha kwamba bifu kati yao lipo palepale.
***
Mzee Yo akarudisha ripoti kwa Eddy, akamueleza
hali alisi jinsi inavyo endelea kwenye jiji kwa
wakati huu, akamuelezea jinsi askari wanavyo
endeleza msako wao nchi nzima. Vijana wengi
wahuni waliweza kukamatwa na askari. Wengi
waliingizwa kwenye vyumba vya mahojiano
kuhojiwa kwa tukio la utekwaji wa mke wa dokta
Ranjiti.
“Nahitaji kumfahamu huyo dokta Ranjiti”
“Mmmmm nahisi kama picha yake ninayo hapa
kwenye simu yangu”
Mzee Yoo, akatoa simu yake ya mkononi, akaingia
upande wa picha ambapo kuna picha kadhaa
alipiga na bosi wake huyo kipindi cha nyuma.
Akamakabidhi Eddy simu. Moyo wa Eddy ukastuka
kidogo, akasimama kutoka kwenye kiti alicho
kikaa, picha ya daktari huyo haikuwa ngeni
kichwani mwake, akajaribu kuvuta kumbukumbu
kwenye ubongo wake, jibu likatua Tanzania kwenye
hospitali ya Agakgani.
“Huyu daktari nilisha wahi kumuona Tanzania?”
“Tanzania, mwaka gani?”
”Mwaka ulio pita?”
“Basi atakuwa ni yeye”
“Kwa nini unasema ni yeye?”
“Mwaka jana nilimpeleka Tanzania, nikiwa rubani
wake, kisha nilirudi kumchukua baada ya mwenzi
na nusu hivi”
Eddy akahisi akili yake ikipata moto, habari hiyo ya
Mzee Yo, ikaanza kumpa picha ambayo alianza
kuiaminbi kwamba mke wake bado yupo hai na
hajafa.
“Naanza kupata picha mzee wangu”
“Picha gani?”
“Yule mke wa dokta Ranjiti ni mke wangu?”
“Ni mke wako unamaanisha nini?”
“Ni mke wangu mzee, kwani mulimtoa wapi?”
“Mimi nakumbuka kwamba alikuwa ni mgonjwa
ambaye aliingizwa kwenye ndege kulekule
Tanzania na kuletwa huku baada ya muda
akaolewa na dokta”
Eddy akahisi moyo ukitaka kumpasuka kwa wivu,
hakuamini kama mke wake kipenzi anaye mpenda
anaweza kuolewa. Swali jengine lililo muumiza
kichwa, yule aliye zikwa Tanzania, alikuwa ni nani.
Usiku wa siku hiyo Eddy hakuhitaji kulala pasipo
kuhakikisha anainza kazi yaka ya kutambua ni wapi
alipo mke wake. Akavaa nguo zake za kazi(Black
Shadow) Akachukua pikipiki ya Mzee Yo na
kuingia kazini.
‘Phidaya kuwa basi ni wewe mke wangu, sitaku
kuamini kwamba umekufa’
Eddy alizungumza huku machozi yakimwagika,
akazidi kuongeza mwendo kasi wa pikipiki,
akielekea kwa rafiki yake Sabogo. Majira ya saa
tano usiku akawa amefika nyumbani kwa Sabogo.
Akatazama mazingira ya eneo zima, akakut a yapo
vizuri, akapenya dirishani na kuwakuta vijana wa
Sabogo wakicheza karata huku wengine wakinywa
pombe kali.
Wote walipo muona walishikwa na bumbuwazi,
hawakuamini kama mtu ambaye wamemtafuta kwa
wiki kazaa hadi wakakata tamaa leo amesimama
mbele yao. Eddy akatoa ishara ambayo wanaitumia
vijana wa kundi hilo, wote wakaitikia kwa ishara,
wakaamini kwamba mtetezi wao amefika.
Mmoja wao akachomoka kwa kasi na kupandisha
gorofani, akamuita Sabogo, ambaye naye alishuka
kwa kasi huku akiwa na furaha sana, hakuamini
alipo muona Black Shadow akiwa amesimama
mbele yake. Akamkumbatia kwa furaha hadi
kumnyanyua, nyuu kidogo kutokana na yeye kuwa
ni mrefu kuliko Eddy.
“Ulikuwa wapi kaka?”
“Ni stori ndefu ila ninakuomga tukazungumzie
chumbani”
Wakapandisha hadi chumbani, ambapo Sabogo,
akawafukuza machangudoa wawili ambao walikuwa
wakimburudisha kama kawaida yake.
“Ehee niambie kaka?”
“Ndugu yako nashukuru nipo salama, kuna mzee
mmoja alinitorosha hospitali baada ya kutaka
kuuliwa”
“Mzee gani tena?”
Eddy akaanza kumuadisia Sabogo mwanzo hadi
mwisho tukio zima alilo simuliwa na mzee Yo. Pia
akamuelezea jinsi anavyo hisi kwamba Phidaya ni
mke wake. Hilo jambo Sabogo naye akaliunga
mkono, kwani siku ya kwanza kwenda hospitalini
aliweza kuonana na Phidaya, ambaye alimuuliza
kama anamtambua Eddy.
“Ulimjibuje?”
“Nilimuambia kwamba sikufahamu, sikutaka hata
watu waweza kulijua hilo swala”
“Sasa hapo utanisaidiaje rafiki yangu?”
“Kaka ngoja tuanze kufanya uchunguzi tutambue
kwamba mke wako kwa sasa yupo wapi kwa
maama nasikia kwamba ametekwa”
“Nitashukuru kaka, yaani hata kama si mke wangu
nitahitaji kumchukua hivyohivyo ili mradi
anaifanana na mke wangu basi nafsi yangu
itatulia”
“Usijali ndugu yangu nitakusaidia bega kwa bega
kuhakikisha kwamba tunampata mke wako”
***
“Hadi sasa hivi hakuna ripoti yoyote kutoka polisi
na sisi tumekaa tu humu ndani, hatujui madama
anaendeleaje?”
Sa Yoo alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga, Shamsa hakuzungumza kitu chochote wala
Lee Si, wote walishinda macho hadi majira hayo ya
asubuhi. Kila mmoja alijihisi mpekwe isipokuwa
Lee Si, kwani anatambu mpango mzima ambao
alipewa na dokta Ranjiti kama mlinzi wa mkewe.
Simu ya Lee Si ikaingia meseji kupitia mtandoa wa
Whatsapp, akaufungua ujumbe huo na kukuta
picha ya Black Shadow, akiwa na kingago huku
pembeni yake sura yake ikiwa haina kinyago.
Ujumbe wa maneno ukaingia kwenye simu yake,
kutoka kwa dokta Ranjiti
”Hakikisha kwamba unamuua huyo kijana roho
yangu iwe na amani”
Lee Si akashusha pumzi akanyanyua kichwa chake
na kuwatazama Shamsa na Sa Yoo ambao nao pia
walimkodolea macho wakihitaji kujua labda kuna
habari yoyote ambayo ameipata
“Nakwenda chumbani”
Lee Si aliwaaga Shamsa na Sa Yoo, aliye mkazia
macho hadi anatoka kwenye chumba hicho.
“Shamsa ninamashaka na Lee Si”
Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya chini kidogo
“Kwa nini?”
“Yaani mimi wala sielewi, ila moyo wangu umejawa
na mashaka naye”
“Unamdhania vibaya kaka wa watu, laiti kama
angekuwa ni mtu mbaya basi asinge tusaidia ile
siku”
“Mmm haya mwaya ila nikimuona nahisi uzito
fulani, moyoni mwangu”
“Ondoa imani potofi Sa Yoo”
Sa Yoo akanyanyuka na kuaanza kuandaa kifungua
kinywa, alipo maliza wakajumuika kwa pamoja
kupata kifungua kinywa. Walipo malinza wakaingia
bafuni kwa pamoja, akaoga na kurudi seblen,
macho yao wote wakayaelekezea kwenye kioo cha
Tv, kuangalia habari yoyote ambayo inaendelea.
Hapakuwa na abari ambayo waliona inawahusu,
wakazima Tv, akajiandaa na kuelekea kituo cha
polisia kujua ni kitu gani ambacho kinaendelea.
Majibu waliyo pewa polisi yakazidi kuwakatisha
tama, kwa maana waliambiwa bado upelelezi
unafanyika.
“Shamsa mimi nakuomba uanze kumfwatilia Lee
Si, akiwa yeye kama mlinzi wa madam ni lazima
atatambua kitu kinacho endelea”
“Nitamfwatiliaje?”
“Ile siku ambayo wewe ulikwenda kwa dokta Yan,
usiku Lee Si, naye alitoka mara baada ya wewe
kutoka”
“Eheeee”
“Nilimchungulia kwa dirishani na kumuona akiingia
kwenye gari lake na kwenda njia ambayo wewe
ulikwenda, baada ya masaa machache kupita
alirudi kwa haraka na haikupita muda mrefu na
wewe ukawa umerejea. Isitoshe nilikwenda kutega
sikio mlangoni kwake nikamsikia akizungumza na
simu na mtu aliye muita ni bosi”
Sa Yoo alizungumza huku akipunguza mwendo
kasi wa gari analo liendesha kwa maana
mazungumzo hayo anayo yazungumza ni nyeti
sana kwake.
“Ulimsikiaje?”
“Nilisikia akisema kwamba Bosi nimemaliza kazi,
sasa sikujua ni kazi gani, nikahisi labda
anazungumza na madam, ila uliporudi ukaniambia
kwamba dokta Yan amakufa nikaanza kumtilia
mashaka Lee Si”
Shamsa akabaki kimya na kushusha pumzi, yake
maneno aliyo elezwa na Sa Yoo kidogo yameanza
kumfungua akili yake, akamuomba Sa Yoo simu,
akachukua namba ya Lee Si, na kuipiga ikaita kwa
muda, ikapokelewa.
“Upo wapi?”
“Nipo mjini naendelea kutafuta kufahamu ni wapi
alipo madam au kina nani ambao wamehusika
katika kumteka”
“Ahaa sawa badae?”
“Vipi kuna tatizo?”
“Ahaa hapana nilitaka kujua kuwa upo wapi, kwa
maana ulitoka pasipo kutuaga”
“Ahaa nafwatilia fwatilia kujua ni wapi alipo
madam”
“Poa badae”
Shamsa akakata simu na kuachia msunyo mkali,
akaingiza namba ya Lee Si, kwenye call traker,
kuangalia ni wapi alipo, akakuta inmamuonyesha
anaelekea kwenye moja ya mji, akamueleza Sa
Yoo.
“Hiyo sehemu kuna kituo cha watoto yatima”
“Sasa ndio madama atakuwepo huko au anafwata
nini?”
“Hembo ngoja twende”
Sa Yoo akageuza gari na kueleka anapo kwenda
Lee Si, wakiongozwa na ramani kwenye simu ya
Shamsa.
***
Lee Si akafika kwenye kituo cha kulelea watoto
yatima, kwa lengo moja la kumuona Soroo, kwa
mamaana alimsikia akimnong’oneza Phidaya
kwamba anatambua sehemu alipo Black Shadow.
Akashuka kwenye gari lake moja kwa moja
akaelekea kwenye ofisi ya walezi wa kituo hicho.
Akajitambulisha, haikuwa ngumu kwa walezi hao
kuweza kumtambua, kutokana ni juzi tu aliweza
kuja akiwa na bosi wake Phidaya wakilete mizigo.
Akaomba aweze kuitiwa Soroo, akiwaongopea
kwamba kuna zawadi aliweza kukabidhiwa na bosi
wake kabla hajapatwa na matatizo, kutokana
wanamuamini, Soroo akaenda kuitwa
“Ankooo”
Soroo akamkumbatia Lee Si, wakatoka nje ya ofisi
hizo wakiwa wanatembea kuelekea kwenye moja
ya bustani wakaka kwenye moja ya viti.
“Unajua ni sehemu gani alipo Black Shadow?”
Lee Si alimuuliza Soroo, mara baada ya kutoa noti
ya dola mia na kumkabidhi, Sa Yon a Shamsa
waliweza kumuona Lee Si akiwa na mtoto mmoja,
Shamsa alipo jaribu kumkazia macho mtoto huyo
akagundua ni Junio, jambo lililo mfanya ashuke
kwenye gari na kuanza kukimbia kuelekea kule
walipo kaa Soroo na Lee Si
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 63 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (63)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Ankooo”
Soroo akamkumbatia Lee Si, wakatoka nje ya ofisi
hizo wakiwa wanatembea kuelekea kwenye moja
ya bustani wakaka kwenye moja ya viti.
“Unajua ni sehemu gani alipo Black Shadow?”
Lee Si alimuuliza Soroo, mara baada ya kutoa noti
ya dola mia na kumkabidhi, Sa Yon a Shamsa
waliweza kumuona Lee Si akiwa na mtoto mmoja,
Shamsa alipo jaribu kumkazia macho mtoto huyo
akagundua ni Junio, jambo lililo mfanya ashuke
kwenye gari na kuanza kukimbia kuelekea kule
walipo kaa Soroo na Lee Si
ENDELEA
Shamsa akazidisha kasi, hadi karibu na bustani
akasita kidogo kukimbia huku macho yake yote
akiwa amemtupia Soroo, Lee Si, alipo muona
Shamsa akatamani asimame na akimbie, ila
akashindwa na kujikuta akiachia tabasamu pana la
kinafki ili mradi asistukiwe mpango wake. Shamsa
akaanza kutembea hatua za taratibu hadi sehemu
walipo Soroo na Lee Si.Kufanana kwa Soroo na
Junio ambaye kwa sasa ni Marehemu, kukamfanya
Shamsa kulengwa lengwa na machozi.
Saroo akabaki akimshangaa Shamsa aliye piga
magoti mbele yake, hakumjua ni nani aliye kuja.
Soroo akamtazama Lee Si kisha akamtazama
Shamsa, aliye anza kumshika mkono wake wa
kulia. Shamsa akashindwa kujizuia na kujikuta
akiangua kilio huku akimkumbatia Soroo, uchungu
wa kifo cha Junio ukamrejea upya.
“Wewe nani?”
Soroo alimuuliza Shamsa huku ajijitoa mikononi
mwake, Shamsa hakumjibu chochote zaidi ya kulia
kwani hadi sauti wamefanana, Sa Yoo alisimama
kwa mbali akishuhudia hali nzima inavyo endelea.
“Akooo Lee Si eti huyu ni nani?”
“Ahaa ahaa hu…..uuyu…..”
Lee Si alijing’ata ng’ata, hakujua ajibu nini japo
swali alilo ulizwa ni rahisi sana kwake.
“Unaitwa nani mtoto mzuri?”
Shamsa alizungumza huku akijipangusa machozi
yake kwa kiganja chake cha mkono wa kushoto.
“Soroo, wewe unaitwa nani?”
“Shamsa”
“Mbona sasa unalia?”
Shamsa akajitahidi kuachia tabasamu pana, kisha
viganja vyake taratibu vikaanza kupapasa mashavu
yote mawali ya Soroo.
“Nimetokea kukupenda”
“Akoo Lee Si, Shamsa ananipenda kama anti
Phidaya”
Lee Si alitingisha kichwa tu, mdomo wake alijikuta
ukiwa mzito gafla, hata maneno ambayo alipanga
kumshawishi mtoto huyo yote yaliparanganyuka
kichwani.
“Unamjua anti Phidaya?”
“Eheee alikuja siku ile kutuletea vyakula na hele
hapa, akaniambia amenipenda”
“Ahaa basi mimi pia nianakupenda kutokana anti
Phidaya ni mama yangu”
“Ahahaa kweliii?”
“Ndio”
Soroo akajikuta akifurahi sana kusikia maneno ya
Shamsa, akamkumbatia tena na kumuomba
asimame. Mlezi mmoja wa choa baada ya kuona
ujio wa Shamsa, ikamlazimu kufika kwenye bustani
hiyo kuuliza ni kitu gani kinacho endelea. Ikabidi
Lee Si kuchukua jukumu la kumuelezea Shamsa
kwamba ni mtoto wa bosi wake ambaye alikuja
naye siku chache zilizo pita. Mlezi huyo baada ya
kusikia habari hiyo, akafurahi sana na kuomba
kwenye na Shamsa ofisini kumtambulishwa kwa
baadhi ya walezi wa chuo hicho ambao
wanamuheshimu sana Phidaya kama mwanamke
shujjaa aliye jitolea kuwalea watoto hao. Walezi hao
hawakusita kumpa pole Shamsa kwa mama yake
kutekwa, kila mmoja alisikitika sana kwa taarifa
hiyo kwani wameondokewa mtu muhimu sana
kwenye maisha yake.
“Nina imani kwamba atakuwa salama, nahisi watu
hao wanahitaji pesa tu”
Shamsa aliwafariji walezi hao, ambao tukio la
Phidaya kutekwa liliwagusa kwa kiasi kikubwa
sana. Ila mlezi mmoja aakashindwa kustahimili
kuuliza kitu amchacho kinamsumbua moyoni
mwake.
“Mbona weewe na mama yako mumetokea sana
kumpenda Soroo, kuliko watoto wengine?”
“Kusema kweli Soroo amefanana sana na mdogo
wangu, mtoto wa mama, alifariki mwaka jana akiwa
na miaka sita, ndio maana nilipo muona Soroo
kwa mara ya kwanza nilijisikia uchungu sana”
MManeno ya Shamsa yakwafanya baadhi ya
wamama walezi kumwagikwa na machozi, japo ni
maneno machache ila kila mmoja alitambua
uchungu wa kufiwa na mtoto, wakamuangalia
Soroo, mbaye muda wote alijiegemeza mapajani
mwa Shamsa.
Kitendo cha Shamsa kuingia na Soroo ofisini kwa
walezi wa kituo cha kulele watoto, kilimkera sana
Lee Si akanyanyuka kwa hasira kwenye benchi
alillo kuwa amekalia na kwenda kwenye gari lake
huku akimpita Sa Yoo pasipo kumsemesha neon la
aina yoyote. Sa Yoo kama kawaida yake akamkata
Lee Si jicho moja kali, kisha akatabasamu
nakuegemea gari la Phidaya ambalo kwa sasa yeye
ndio analitumia. Lee Si aliweza kuona kitendo
ambacho Sa Yoo amekifanya, hakuhitaji kujibizana
na Sa Yoo, akawasha gari na kuondoka kwa kasi
huku akitimua vumbi kuingia barabarani.
***
Majira ya saa mbili usiku, ndege ya dokta Ranjiti
ikatua wanja wa ndege jijini Cairo nchini Misri.
Phidaya akiongozana na wahudhumu wawili wa
ndege wakashuka na kumkuta dokta Ranjiti akiwa
anawasubiri pembeni yake akiwa Kim pamona na
walinzi wengine wapya watatu.
“Karibu mke wangu”
Dokta Rnjito alizungumza huku akiachia tabasamu
pana, akajaribu kumkumbatia Phidaya, ila
akamzuia na kuongoza moja kwa moja hadi
kwenye gari aina Ranger rover Sport, akaingia na
kumsubiria mume wake amfwate. Dokta Ranjiti
akaingia kwenye gari akiwa amekasirika.
“Kwa nini umeniaibisha mbele ya wafanyakazi
wangu?”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa kufoka akiwa
amekazia macho Phidaya, ambaye hakujali ukali
huo wa dokta Ranjiti
“Umekuwa jeusi sio?”
“Ehee babuee usinipigi……”
Kofi zito likatua shavuni mwa Phidaya, hadi Kim
aliye kaa siti ya mbele ahageuka kungalia kinacho
endelea, akamkuta Phidaya akiwa amejikunyata
huku mikono yake miwili akiiweka kweye shavu
alilo tandikwa kofi zito
“Endesha gari”
Dokta Kim alizungumza huku akijiweka vizuri
kwenye siti, Kim bila pingamizi akawasha gari na
safari ya kueleka kwenye hoteli moja ya kifahari,
ambayo dokta Kim, amepangishwa kwa miezi sita
ikaanza. Ukimya ndani ya gari ulitawala kwa
asilimia mia moja, hapakuwa na mtu aliye
zungumza kitu cha aina yoyote hadi wanafika
hotelini. Taratibu Phidaya akashuka kwenye gari,
baada ya kufunguliwa mlango na Kim, dokta Ranjiti
akamshika mkono na kunaza kutembea naye
kuelekea ndani.
“Hichi ndio chumba chetu tutakacho kaa hapa kwa
miezi sita hadi mambo yatulie ndani ya Japani
sawa mama”
Phidaya hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi
ya kutafuta sofa na kukaa, moyoni mwake akazidi
kumchukia Ranjiti, hakumpenda kama asivyo
mpenda Sheteni.
Taratibu dokta Ranjiti, akaanza kuvua nguo zake
moja baada ya nyingine mbele ya Phidaya hadi
akabakiwa na bukta ya ndani tu.
“Nimekumisi mke wangu”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akipanua mikono
yake na kumkumbatia Phidaya aliye jikalia kwenye
kochi, akimtazama kwa macho makali kuanzia juu
hadi chini. Dokta Ranjiti, akaanza kunyonya shingo
ya Phidaya, kuanzia upande wa kulie kwenda
kushoto, juu kwenda chini.
Phidaya hakutikisika wala kuhisi kitu cha ania
yoyote, mawazo yake yote yapo Japani kwa
mwanaye Shamsa hakujua yupo kwenye hali gani
kwa sasa. Hadi dokta Ranjiti anammalizia kumvua
nguondipo Phidya akastuka, kutoka katika dibwi
zito la mawazo.
“Unataka kufanya nini?”
“Phidaya alimuuliza kwa sauti ya ukali kiasi cha
kumstua dokta Ranjiti aliye katika hisia kali za
kimapenzi
“Ninahamu mke wangu”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya mahaba,
mazito
“Hembu niondolee upuuzi wako, nahitaji kwenda
kuoga”
Phidaya alizungumza huku akitaka kunyanyuka
kwenda bafuni, ila dokta Ranjiti akamzuia.
“Usitake nitumie nguvu”
Dokta Ranjiti alibadilika dakika hiyo hiyo na
kuzungumza kwa sauti ya ukali, Phidaya hakuwa
na jinsi zaidi ya kukubali, mumewe kumfanya
chochote ajisikiacho. Dokta Ranjiti akaanza kulifaidi
tunda la Phidaya, kila alivyo zidi kufanya kitendo
hicho ndivyo jinsi kumbukumbu za Phidaya zilivyo
anza kumrejea kichwani mwake, akaanza
kukumbuka jinsi mwanume wake wa zamani aliye
jengeka kifua, alivyo kuwa akilala juu yake na
kumkumbatia, mihemo yakimapenzi ya mwanaume
huyo ilizidi kumfanya Phidaya kumbukumbu
kurejea na kuiona sura ya mwanaume huyo,
hakuiona sura ya dokta Ranjiti bali aliona sura ya
mwanaume anaye kumbuka kwamba alimpenda
sana kupita maelezo
“Mke wangu unanipenda…….”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akihema akijitajidi
kukipandisha kiliama kirefu kwa kasi
“Ohooo yesssss nakupenda sana mume wangu
EDDY”
Jina la Eddy likamfanya dokta Ranjiti, kasi,
mashamsham yakupandisha mlima mrefu kukatika
gafla, macho yakamtoka hakuamini kwamba
kumbukumbu za Phidaya zimerejea.
***
Raisi mstaafu Praygod, baada ya kukabidhi nyaraka
zote za serikali, kwa Mzee Godwion, hakuona haja
ya kuendelea kukaaa nchini, kwa kutumia ndege
yake binafsi aliyo kabidiwa na rafiki yake kipenzi
Frennando ,yeye na mke wake, Rahab, wakiwa na
walinzi wawili Pricsa na mllinzi wa kiume Emily
wakaianza safari kwenda nchini Misri kwa ajili ya
mapumziko kabla ya kwenda Mexco kuishi.
“Muheshimiwa kwa nini umeamua kuondoka
mapema kiasi hichi nchini?”
Emily alimuuliza raisI mstafu bwana Praygod.
“Kwa sababu ya vitisho vya Godwin”
“Alikuambiaje?”
“Alinipa masaa ya kukaa nchini, sikuhitaji
kulizungumza hilo mapema kwani lingezaa
mtafaruku. Kwa sasa ninahitaji kuituliza akili
yangu, nione kama miaka mingine mitano ijayo
kama nitaweza kushinda uchaguzi”
“KKwa hiyo huto rudi tena Tanzania siku hizi za
usoni?”
“Sijafikiria, au unashauri nini mke wangu?”
“Tuangalie upepo mume wangu”
Rahab alizungumza na kuendelea kucheza game
kwenye simu yake, Priscar hakuzungumza
chochote zaidi ya kuyasikiliza mazungumzo hayo.
“Ila ninawaonea sana huruma Watanzania,
watanikumbuka”
“Kwa nini muheshimiwa?”
“Ahaa matokeo ya kura zao watayaona, tupo sisi
tusikilizie itakuwaje”
Safari yao ilizidi kusonga mbele, wakiendelea
kuzungumza wakijadili mstakabali wa nchi ya
Tanzania unapo elekea, akazidi kuwafumbua
masikio walinzi wake mambo ambayo yalifanywa
na mzee Godwin akiwa jeshini hadi hapo alipo
kuwa, kila mmoja akaonyesha wasiwasi wake juu
ya hali itakavyo kutwa siku chache zijazo.
Wakafika nchini Misri majira ya saa nane usiku,
balozi wa Tanzania nchini hapo akawapokea akiwa
na ulinzi wa kutosha, moja kwa moja wakaelekea
kwenye hoteli kubwa ya kifarahi, iliyo andaliwa kwa
ajili yake apumzike hapo kwa kipindi chote
atakacho yeye na mke wake pamoja na walinzi
wao.
***
Mawazo mengi yakazidi kumuweka Eddy katika
hali ya unyonge, hakutambua ni wapi alipo
Phidaya. Siku zikazidi kuyoyoma, hapakuwa na
matumaini yoyote ya kumuona Phidaya.
“Black Shadow”
Soroo alimuita Eddy mara baada ya kuingia
kwenye pango hilo na kumkuta akifanya mazoezi
ya viongo akiwa amevalia kinyago chake kichwani.
“Naam”
“Umesikia kwamba madam Phidaya ametekwa
nyara?”
“Hapana kwani Phidaya ni nani?”
Eddy alijifanya hajui chochote ili azidi kupata
habari kutoka kwa mtoto huyo aliye anza
kumuamini sana kutokana na upeo wake wa akili
kuwa mkubwa sana.
“Madam Phidaya ni mmoja wa wazamini wa kituo
chetu, anatupatia misaada sana”
“Ahahaa anaonekana ana roho nzuri sana eheee?”
“Ndio ana roho nzuri. Pia ana mwanaye anaitwa
Shamsa alikuja juzi juzi kuniangalia, ila alikuwa
ana lia sana alipo kuwa akinitazama mimi”
“Kwa nini alikuwa analia?”
“Alisema kwamba nafanana sana na mdogo wake,
anaitwa Junio”
Eddy kidogo, akakaa kimya, hakuzungumza
chochote zaidi ya kumtazama Soroo kwenye
mboni ya macho yake, kusema kweli Soroo
anafanana na Junio kwa kiasi kikubwa, tofauti kati
yao ni umri na kimo tu.
“Mbona umekaa kimya……”
“Hamna Soroo, rudi kituoni”
“Babu yupo wapi?”
“Amekwenda mjini”
“Sawa”
Soroo, akampa tano Black Shadow na kuondoka,
machozi yakaanza kumbubujika Eddy usoni
mwake, kila alipokuwa akimtazama Soroo
akiondoka eneo hilo. Kumbukumbu za kifo cha
Junio zikamjia kichwani mwake, akamkumbuka
muuaji aliye husika na kifo cha mwaneye ni
Manka. Eddy akatembea kwa hatua za haraka hadi
kwenye moja ya droo akatoa kitabu chake kidogo
cha kumbukumba alicho pewa na Mzee Yo,
akaliandika jina la Manka kama mmoja wa watu
wanao stahili kufa, huku juu ya jina hilo kukiwa na
majina mawiliya ya mzee Godwin pamoja na dokta
Ranjiti.
***
Akili ya dokta Ranjiti ikazidi kuchanganyikiwa,
baada ya kugundua Phidaya kumbukumbu zake
zinamrejea taratibu. Hakuwa na mbinu yoyote zaidi
ya kuhakikisha anaimarisha ulinzi mkali kwenye
eneo la chumba chake kuhakisha kwamba Phidaya
hatoroki. Huduma zote za simu ndani ya chumba
hicho akazikatisha, hakuhitaji Phidaya awasiliane
na mtu wa aina yoyote.
Phidaya aliweza kulitambua hilo, kwamba mume
wake haitaji akutane na mtu wa aina yoyote,
maisha yake tangu afike Misri na kukaa ndani na
kuangalia Tv pale dokta Ranjiti anapokuwa katika
mizunguko yake ya kukutana na wafanya biashara
wakubwa. Phidaya aliweza kuelewa njama za
mume wake za kukataa yeye kuwa karibu na watu,
akiamini kwamba ni lazima atawasiliana na watu
ambao anawajua na itakuwa ni chanzo cha yeye
kutorokla.
“Siwezi kuendelea kukaa humu ndani”
Phidaya alizungumza huku akivaa moja ya suruali
aliyo nunuliwa na mume wake, akavalia na tisheti,
kisha akasimama dirishani, hakuona haja ya
kuvalia viatu kwani akili yake imemtuma kutoroka
kupitia dirishani. Umbali wa gorofa kumi kwenda
chini, haukumtisha alicho kikusudia ni kuhakikisha
kwamba anatoroka ndani ya chumba hicho pasipo
walinzi waliopo mlangoni kufahamu kitu kinacho
endelea. Akafungua vioo vya dirihani, achungulia
chini, kashusha pumzi na kuanza kuutoa mguu
wake wa kulia kwenye sehemu ulipo kanyaga
mguu wake wa kulia, lengo lake alihitaji kwenda
katika dirisha linalo fwata kwa kupita katika kijinjia
hicho. Phidaya alipo hakikisha kwamba ameshikilia
vizuri, akaanza kutambaa kuelekea kwenye dirisha
la chumba cha pili, ila kabla hajafika akajikuta
akigeuka na kuangalia chini, kizunguzuku kikali
kikamshika na kujikuta akipepesuka, mikono na
miguu yake vikapoteza muhimili na kujikuta
akianza kuelea hewani na kwenda chini kwa kasi
kali, kitendo kilicho shuhudiwa na watu wengi
waliopo chini, kila mmoja alishangaa kuona
mwanamke huyo akianguka kutokea gorofa ya
kumi kuja chini.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 64 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (64)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Akafungua vioo vya dirishani, akachungulia chini,
kashusha pumzi na kuanza kuutoa mguu wake wa
kushoto kwenye sehemu ulipo kanyaga mguu wake
wa kulia, lengo lake alihitaji kwenda katika dirisha
linalo fwata kwa kupita katika kijinjia hicho.
Phidaya alipo hakikisha kwamba ameshikilia vizuri,
akaanza kutambaa kuelekea kwenye dirisha la
chumba cha pili, ila kabla hajafika akajikuta
akigeuka na kuangalia chini, kizunguzuku kikali
kikamshika na kujikuta akipepesuka, mikono na
miguu yake vikapoteza muhimili na kujikuta
akianza kuelea hewani na kwenda chini kwa kasi
kali, kitendo kilicho shuhudiwa na watu wengi
waliopo chini, kila mmoja alishangaa kuona
mwanamke huyo akianguka kutokea gorofa ya
kumi kuja chini.
ENDELEA
Macho ya watu wengi yakashuhudia jinsi Phidaya
anavyokuja kwa kasi chini, wakamshindikiza kwa
macho yao hadi kwenye swimming poolm, lililo jaa
maji liliopo chini usawa wa sehemu ambayo
Phidaya aliangukia. Vijana wawili wenye asili ya
kiarabu pamoja na Rahab ambaye alikuwa ameketi
pembezoni mwa swimming pool hilo akipunga
upepo wakajitosha kwenye maji, kila mmoja akiwa
na lengo la kwenda kumuokuoa msichana huyo.
Kwa pamoja wakajikuta wakimtoa kwenye maji,
kidogo Rahab akaonekana kustushwa kidogo na
msichana huyo. Kutokona ni mwanamke
mwenzake Phidaya akaanza kumpulizia hewa,
Phidaya mdomoni mwake kumpa pumzi ya ziada
kutokana kuanguka kwake kumemfanya kuzimia.
Haikuchukua muda Phidaya akastuka, huku
akihema, macho yake yakatua kwa Rahab aliye
muinamia, akashangaa kumuona Rahab kwa
maana ni mtu anye mfahamu, ila bado hakujua ni
sehemu gani ambayo aliweza kumuona mwanamke
huyo.
Wahuduu wa Hoteli pamoja na meneja wa hotelo
hiyo wakafika baada ya kujulishwa na wateja wao
kwamba kuna tukio la ajabu limetokea, katika hoteli
yao, wakakuta Phidaya akiwa amefunikwa na taulo,
kubwa ili kutoa ubaridi mwilini mwake na mwili
nzima unamtetemeka kwa woga.
“Yupo vizuri mpeni hewa musimzunguke”
Rahab alizungumza huku akiwasogeza watu
waliopo katika eneo hilo, hapakuwa na mtu aliye
weza kuamini kwamba mwanamke huyo anaweza
kupona, hii ni kutokana na umbali mrefu alio weza
kutoka hadi chini alipo angukia.
”Mama uaitwa nani?”
Meneje alimuuliza Phidaya, aliye mtazama kwa
macho makali, yalio jaa wekundu ulio sababishwa
na kulia sana.
“Kwa sasa hayupo sawa, labda badae anaweza
kuzungumza”
“Kuna huduma ya dharura labda tuweze
kumuwahisha hospitalini.”
“Hilo pia linaweza kusaidia”
Ikaletwa gari ya wagonjwa, Phidaya akaingizwa
kwenye gari, huku Rahab akiomba na yeye kwenda,
akakubaliwa, kutokana na msaada wake walio
weza kuufanya kwa binti huyo. Haikuwachukua
muda mwingi sana wakawa wamefika hospitalini,
ila kabla Phidaya hajaingizwa katika chumba cha
matibabu, akamuomba Rahab kuweza kuwasiliana
na mtu aliye weza kumtajia namba yake.
“Huyo ni nani?”
“Ni mlinzi wangu”
“Yupo wapi?”
“Yupo Japani”
“Anaitwa nani?”
“Lee Si”
Phidaya alipo maliza kuzungumza hayo, kitanda
alicho lalia kikasukumwa ndani ya chumba hicho
kwa ajili ya uchunguzi zaidi yaw a mwili wake.
***
“Lee Si nina mazungumzo na wewe”
Shamsa alizungumza huku akiufunga mlango wa
Lee Si, baada ya kuugonga kwa muda kasha
ukafunguliwa. Lee Si, akavaa tisheti yake kisha na
kuelekea chumbani kwa Shamsa, akamkuta akiwa
amekaa na Sa Yoo wakimsubiria, sura za
wasichana hao zilimuonyesha Lee Si, kwamba
wana maswali mengi juu yake.
“Nimefika”
Sa Yoo, akamkata jicho Lee Si kisha akamtazama
Shamsa ambaye muda wote alikuwa akifikiria
jambo la kuzungumza.
“Kwa nini unatuzunguka?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Lee Si
usoni
”Kivipi madam?”
“Tuambie madam yupo wapi, ikiwa wewe kama
mlinzi wake ni lazima utatambua kuna kitu kinacho
endelea, la sivyo tutakuripoti polisi na utatuambia
ukweli kuhusiana na sehemu alipo mama yangu”
Lee Si, akatabasamu kwa dharau kicha
akamtazama Shamsa kuanzia chini hadi juu.
Dharau ya Lee Si, ikamfanya Sa Yoo, kuachia
msunyo mkali, huku akilitoa na yeye jicho lake
kubwa fulani kumpandisha na kumshu Lee Si juu
hadi chini.
“Hata mukinipeleka polisi, munahisi nitawekwa
ndani? Siku ambayo mulikwenda kununuliwa nguo
mimi nilikuwepo? Kama jibu ni hapana basi
tambueni kwamba sifahamu alipo madam, na mimi
nikama nyinyi sote hatujui ni wapi alipo”
“Shamsa unaona dharau zake nilizo kuambia, huyu
ni lazima atakuwa anafahamu”
Sa Yoo, alizungumza huku akichukua mto mdogo
wa kochi na kumrushia, Lee Si, na kumbamiza nao
wa uso. Lee Si, akanyanyuka kwa hasira akamfwata
Sa Yoo, sehemu alipo simama, kwa lengo la
kumuadhibu kwa kitendo alicho kifanya ila kabla
hajamfikia, akazuiliwa na Shamsa aliye simama
kwa haraka.
“Unataka kufanya nini?”
Shamsa alimuuliza kwa sauti ya msisitizo huku
akimtazama Lee Si usoni mwake, Lee Si
akamsukumia Shamsa pembeni, akamzaba kibao
kizito Sa Yoo, aliye baki akishangaa. Kitendo hicho
kikamkera sana Shamsa, akanyanyuka na
kumtandika kofi zito Lee Si, aliye mtolea macho
makali Shamsa, akataka kurusha ngumi, ila simu
yake, ikaita, akaitoa kwa haraka mfukoni mwa
suruali yake, kabla hajatazama ni nani aliye piga
simu hiyo, akastukia Sa Yoo, akimpiga teke
kwenye mkono alio shika simu, ikaangukia
pembeni.
Lee Si akamrukia Sa Yoo kwenye kwenye kochi
kabla hajampiga kofi, tayari Sha,sa Alisha jiachia,
na kumrukia, akamuangusha chini na kuanza
kumtandika ngumi mfululizo.
Lee Si hakukubali kuona anapigwa na msichana
huyo alicho kifanya ni kujigeuza, akampiga Shamsa
ngumi moja aliyo izuia kwa mikono yake miwili, Sa
Yoo, katika kuzungusha zungusha jicho lake,
akaiona simu ya Lee Si, ikiita, hakutaka kuujali
ugomvi huo alicho fanya ni kuishika simu hiyo na
kuipokea.
“Haloo”
Sa Yoo, alizungumza huku akikimbilia bafuni na
kuwaacha Shamsa na Lee Si wakiendelea kupigana
“Unazungumza na Rahab Praygod ninatumaini
kwamba wewe ndio Lee Si”
Sa Yoo, ikabidi kuitoa simu hiyo sikioni na
kuitazama namba hiyo akagundua kwamba si
namba ya Japan. Akili yake ikafanya kazi haraka
haraka na kujibu kwamba yeye ndio Lee Si.
“Kuna taarifa ambayo bosi wako Phidaya
ameniambia nikujulishe, kwa sasa yeye yupo
nchini Misri barani Afrika na yupo hospitalini kwa
uchunguzi zaidi wa madaktari hii, ni baada ya
kujaribu kufanya jaribio la kutaka kujiua”
Sa Yoo, akauziba mdomo wake kwa wasiwasi
mwingi, akionekana kustushwa na habari hiyo.
“Alooo unanisikia?”
Rahaba alizungumza baada ya kuona mtu anaye
zungumza naye amekaa kimya.
“Nakusikia, amelazwa hospitali gani?”
Rahab akalitaja jina la hospiali aliyo lazwa Phidaya,
kisha akamuaga Lee Si, kutokana na kumaliza
mazungumzo yake aliyo kuwa ameagizwa na
Phidaya. Sa Yoo, akatoka bafuni na kurudi sebleni,
akamkuta Lee Si, akiwa anavuja damu puani huku
amelala sakafuni na Shamsa amesimama pembeni
yake huku amekunja ngumi na kufura kwa hasira.
“Vipi?”
Sa Yoo, alimuliza Shamsa huku akiwa
amemkodolea macho Lee Si, anaye jizoa zoa
kunyanyuka.
“Siwezi pigana na wazembe mimi”
Shamsa alizunguza huku akiondoka karibu na Lee
Si, aliye kaa kitako sakafuni akiwa haamini kwamba
umahiri wake wa kupigana ameweza kuchezea
kichapo ambacho hakukitarajia kabisa kutoka kwa
binti huyo ambaye kwa mara ya kwanza
alimchukulia binti wa kawaida.
“Nenda chumbani kwako na usije ukarudia”
Kwa haraka Sa Yoo akaituma kwa namba ya simu
kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu
yake, namba ambayo ilipiga kwenye simu ya Lee
Si, kisha akaifuta na kumrushia Lee Si simu yake.
“Besti hiyo puaa ilivyo kaa”
Sa Yoo alimtania Lee Si baada ya kumuona pua
yake ikiwa kidogo kama imepinda, huku damu
zikiendelea kumwagika. Baada ya Lee Si kutoka
chumbani hapo, na Sa Yoo kuhakikisha kwa
kuchungulia mlangoni kwamba Lee Si ameingia
chumbani kwake akamuelezea Shamsa kila kitu
alicho kizungumza kupitia simu ya Lee Si.
“Huyo mtu amesema kwamba anaitwa nani?”
“Rahab Praygod”
Jina la Rahab Praygod halikuwa ngeni masikioni
mwake, ila hakuhitaji, kuliwekea maanani kwa
maana majina duniani yananafanana isitoshe
kwamba mtu mwenyewe aliye ipiga simu hiyo yupo
nchini Misri.
“Inabidi tuondoke”
“Sawa tuanze kufwatilia maswala ya viza”
“Poa”
***
Macho ya Sabogo yaliweza kuwakumbuka Shamsa
na Lee Si, ambao amewaona wakiwa wamesimama
kwenye ofisi za shirika moja la ndege. Kutokana
alisha elezwa na Black Shadow kuhusiana na binti
huyo kwamba ni mwanae hakuona haja ya
kuendelea kuwatazama. Akatembea kwa mwendo
wa haraka hadi walipo, akamgusa Shamsa begani
na kufanya Shamsa kugeuka na Lee Si pia
kugeuka. Wote wakaonekana kumshangaa, Sabogo
kwani ni jitu refu kwenda juu, na wote vimo vyao
wanamfikia kiunoni.
“Ninaweza kuzungumza na nyinyi?”
Sa Yo alikubali kwa kutingisha kichwa kutokana na
woga ulio mvaa gafla. Wakatoka hapo dirishani na
kwenda kukaa nje ya uwanja huo wa ndege
ambapo kuna mgahawa
“Naamini kwamba munanifahamu?”
“Hapana”
Sa Yoo alijibu kwa haraka sana hata kabla Shamsa
kujibu.
“Mimi ni meneja wa Black Shadow ninaimani
kwamba wote munamjua, ninaitwa Sabogo”
“Ahaaa wewe ndio yule ambaye ulituletea tiketi za
kukaa VIP?”
“Ndio mimi haujakosea”
Furaha ikamuingia Shamsa, akaona ni bahati
kubwa sana kuonana na mtu huyo kwa maana
ndoto za kukutana na mpenzi wake ambaye ni
Black Shadow, zinaanza kufufuka upya.
“Black Shadow yupo wapi?”
“Yupo na ninaimani pia atakuwa na furaha
kuonana na nyinyi”
“Ninakuomba utupeleke sasa hivi”
Shamsa alizungumza huku akimshika, mkono
Sabogo.
“Kwa mchana huu ninaimani itakuwa ni ngumu
labda kwa usiku”
“Hata iwe saa nane ya usiku mimi nipo tayari
kuonana naye”
“Sawa kuna sehemu nitawahitaji muje, ila
hakikisheni kwamba munakuja nyinyi wawili peke
yenu tu”
“Sawa”
Sabogo akaawachia namba za simu, hata wazo la
kwenda Misri, barani Afrika, wakaliweka kando
kwanza, moyo wa upendo juu ya Black Shadow,
ukarudi kwa upya kabisa moyoni mwa Shamsa.
Siku hiyo furaha ikamjaa tele moyoni mwake, hata
kumbukumbu alizo ambiwa na Phidaya kwamba
Black Shadow ni baba yake ziliteketea. Hakutaka
kuzipa uzito wa aina yoyote kutokana anaamini
kwamba Black Shadow ni mwanaume mwengine
kabisa na Eddy ni mwanaume mwengine kabisa.
***
Furaha na amani ikamtoweka Madam Mery,
hakujua maisha yake ya hapo mbeleni yatakuwa
vipi, kwani adui yake namba moja ndio huyo
amekalia kiti cha uraisi nchini Tanzania.
“Nitafanyeje?”
Ndio swali ambalo Madam Mery aliendelea kujiuliza
kichwani mwake, akaendelea kuzunguka chumbani
kwake, kitafakari, hakuhitaji siku hiyo kuonana na
mtu wa aina yoyote hata wafanyakazi wake wa
ndani. Kila alilo lifikiria alilipangua, kwani mpango
wake aliona unafeli.
“Eddy, lazima nionane na Eddy ndio mtu pekee
ambaye anaweza kuniunga mkono katika mpango
wangu huu”
Madam Mery alizungumza huku akiifungua Laptop
yake, akaanza kutafuta ni wapi alipo Eddy. Ripoti
ya mwisho ambayo aliipata katika mtandao
kwamba Eddy yupo Japani na nimuhalifu katika
nchi hiyo anatafutwa.
Madam Mery hakuona haja ya kupoteza muda
akakata tiketi kabisa kupitia mtandao, siku iliyo
fwata akapanda ndege hadi Dar es Salaam,
ambapo akakuta tiketi yake ikiwa tayari, apanda
ngege ya shirika la KLM na kuianza safari yake,
ambayo ilimchukua masaa mengi kukaa angani.
Kitendo cha kutoka katika uwanja wa ndege
akamshuhudia Shamsa akiwa na binti mmoja
wakiingia kwenye gari ya kifahari na kuondoka.
Madam Mery hakuhitaji kuweka hisia za kwamba
mtu aliye weza kumuona ni tofauti za Shamsa,
kutokana binti huyo anamtambua vizuri sana na
Alisha wahi kukaa naye na kumueleza siri nyingi
kuhusiana na kikosi cha siri kinacho milikiwa na
mzee Godwin baba yeka Eddy.
Madam Mery akamuomba dereva huyo kulifwata
gari hilo kwa nyuma popote litakapo kwenda,
dereva naye akafanya hivyo kama alivyo agizwa,
gari hilo likafika kwenye moja ya hoteli mabinti hao
wakashuka, Madam Mery naye akashuka na
kumlipa dereva pesa yake akiamini kwamba
atawakuta mapokezi Shamsa na huyo rafiki yake
wa kijapani. Hadi anaingia ndani hakuweza
kuwaona, muhudumu mmoja akamkaribisha, bila
kutaja haja yake, ya yeye kumfikisha hapo,
ikamlazimu kuchukua chumba katika hoteli hiyo
hiyo, akijipa moyo kwamba akiliona gari hilo basi
Shamsa atakuwa amemuona na kama amemuona
Shamsa basi Eddy hato kuwa mbali na atamueleza
kila kitu kuhusiana na Tanzanani.
***
Sabogo, mara baada ya kurudi katika makao yake,
kitu cha kwanza alicho kifanya akampigia simu
Black Shadow na kumuomba aweze kukutana naye
kwenye moja ya gorofa juu kabisa ya gorofa hilo
zinazo pata gorofa, ishirini na tano.
“Kuna nini?”
“Kuna zawadi nimekuandalia”
“Sawa kaka”
Majira ya saa nne usiku, Sabogo akawa ndio mtu
wa kwanza kuweza kufika katika eneo la gorofa
hilo, akawaelekeza Shamsa na Sa Yoo, mara baada
ya kupigiwa simu na wasichana hao. Haikuchukua
muda sana Sa Yoon a Shamsa wakawa wamesha
fika katika kilele cha gorofa hilo.
“Yupo wapi Black Shadow?”
Shamsa alimuliza Sabogo.
“Ninaimani kwamba yupo njiani”
Ikawalazimu wawe wavumilivu waendelee
kumsubiria Black Shadow.
***
Katika kitu ambacho kilitoke kumkera na kumuudhi
Lee Si ni kupigwa na Shamsa, bado hakuwa
anaamini kwamba amechezea kichapo kikali
kutoka kwa binti huyo. Moyoni mwake akajiapiza
kuweza kumuua, iwe isiwe ni lazima awaangamize
hususania cha umbea Sa Yoo.
Akiwa chumbani kwake majira ya usiku, aliweza
kuusikia mlango wa Kina Shamsa ukiwa unafungwa
kwa nje, akatulia kidogo na kuweza kutoka
kuchungulia kuona ni wapi wasichana hao wanapo
elekea, akawaona wakondoka aneo hilo wakiwa
wamevalia vizuri.
“Hii ndio nafasi yangu”
Lee Si alizungumza huku akirudi ndani, akachukua
bastola zake mbili, akiamini kwamba Shamsa na
Sa Yoo, wanakwenda disko kuburudika baada ya
siku yao kuwa mbaya. Akavaa koti lake jeusi
pamoja na gloves nyeusi mikononi mwamke.
Akashuka kupitia lifti hadi chini kabisa na
kuwashuhudia Shasma na Sa Yoo wakiingia
kwenye gari ambalo ni mali ya Phidaya.
Wakaondoka eneo la hoteli kwa haraka na yeye
akakimbilia hadi sehemu ya maegesho alipo liacha
gari lake. Akaingia na kuanza kulifwatilia Shamasa
na Sa Yoo kwa umakini mkubwa pasipo wao
wenyewe kuweza kustukia. Akawashuhudia
wakiingia kwenye moja ya mtaa mbao unasifika
kwa vibaka na uporaji wa mali za raia wema.
Akawashuhudia wakisimamisha gari lao kwenye
moja ya gorofa, wakaingia kwenye gorofa hilo, kwa
haraka na yeye akashuka kwenye gari na kuanza
kupandisha kwenye gorofa hilo. Akaendelea
kuwafwata kwa umakini wa hali ya juu hadi gorofa
ya mwisho, akawaona wakiendelea kupanda juu
ambapo ni juu kabisa.
“Wanakwenda wapi hawa?”
Lee Si, alijiuliza kwani woga ulisha anza kumuingia
na kuhisi kwamba huwenda anavyutwa kwenda juu
zaidi akihisi kwamba amesha stukiwa. Pua yake
aliyo ifunga plasta kubwa nyeupe kutokana na
kipigo kikali, ikaanza kumuuma. Kutokana na hewa
nzito aliyomo katika chumba alicho jificha, kwani
gorofa hiyo halitumiki, na lipo katika harakati za
kuvunjwa na serikali na kujengwa upya kwani ni
moja ya gorofa la zamani ndani ya Japan katika
mji wa Yokohama.
Lee Si akachungulia nje, akamshuhudia mtu anaye
mtafuta siku zote, Black Shadow, akimalizia
kupandisha ngazi kwenda juu walipo elekea
Shamsa na Sa Yoo.
“Bingooo”
Lee Si alizungumza huku akiwa amejawa na furaha
moyoni mwake, akachomo bastola yake moja,
akaikagua inarisasi za kutosha, akakuta magazine
ya bastola hiyo ikiwa na risasi za kutosha.
Akaanza kupandisha kwenda juu kabisa, huku
akinyata. Akakuta mlango wa kufikia juu kabisa
ukiwa wazi kidogo. Akausukuma taratibu,
akachungulia, akamuona Black Shadow akiwa
amekumbatiana na Shamsa aliye jawa na
tabasamu usoni mwake hadi machozi
yakimwagika. Pembeni yake alimuona Sa Yoo
naaye akuwa na furaha, huku jitu kubwa ambalo
hakuwahi kuliona siku hata moja, nalo likiwa
limeshika kitambaa mkononi mwake na kujifuta
machozi.
Lee Si, akainyanyua bastola yake mbele taratibu,
akainyoshea walipo maaduia zake, akawatazama
wote haraka haraka, kisha akaftyatua risasi moja.
Mlio wa bastola ukawastua wote, kila mmoja
mmoja alimtazaa mwenzake kuona risasi hiyo
imempiga nani, kisha wote macho yao wakayatupia
sehemu ilipo tokea risasi hiyo, wakamuona Lee Si
akiwa ameshika bastola, akihitaji kufyatua risasi
ntingine kwao.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 65 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (65)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Bingooo”
Lee Si alizungumza huku akiwa amejawa na furaha
moyoni mwake, akachomo bastola yake moja,
akaikagua inarisasi za kutosha, akakuta magazine
ya bastola hiyo ikiwa na risasi za kutosha.
Akaanza kupandisha kwenda juu kabisa, huku
akinyata. Akakuta mlango wa kufikia juu kabisa
ukiwa wazi kidogo. Akausukuma taratibu,
akachungulia, akamuona Black Shadow akiwa
amekumbatiana na Shamsa aliye jawa na
tabasamu usoni mwake hadi machozi
yakimwagika. Pembeni yake alimuona Sa Yoo
naaye akIwa na furaha, huku jitu kubwa ambalo
hakuwahi kuliona siku hata moja, nalo likiwa
limeshika kitambaa mkononi mwake na kujifuta
machozi.
Lee Si, akainyanyua bastola yake mbele taratibu,
akainyoshea walipo maaduia zake, akawatazama
wote haraka haraka, kisha akaftyatua risasi moja.
Mlio wa bastola ukawastua wote, kila mmoja
mmoja alimtazaa mwenzake kuona risasi hiyo
imempiga nani, kisha wote macho yao wakayatupia
sehemu ilipo tokea risasi hiyo, wakamuona Lee Si
akiwa ameshika bastola, akihitaji kufyatua risasi
nyingine kwao.
ENDELEA
Ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala katikati yao,
hapakuwa na mtu aliye weza kufikiria kitu cha
kufanya kwa wakati huo. Macho ya Black Shadow,
yakamshuhudia, Sabogo, akianza kulegea na
mwisho akapiga magoti chini huku mkono wake
mmoja wa kulia akiwa amelishika tumbo lake.
“Sabogoooo”
Black Shadow aliita kwa nguvu huku akiwa
amemuwahi Sabogo asilale chini kabisa, Lee Si
kwa kiwewe akajikuta akiwa ameduwaa kwani
shabaha yake imekenda tofauti na jinsi ambavyo
alitarajia kuweza kutokea kwa wakati huo., Lengo
lake na nia yake ilikua ni kumuua Shamsa. Kwa
haraka, Shamsa akaanza kumkimbilioa Lee Si
sehemu alipo simama, hakuogopa kama ana risasi
au laa, hasira na uchungu alio kuwa nao ulimpa
ujasiri wa hali ya juu, hatua chache kabla
hajamfikia Lee Si, akaruka hewani na kumpiga teke
moja Lee Si la kifua lililo mrudisha alipo toke
akipitia mlangoni na kujikuta akivaana na Madam
Mery ambaye naye pia alikuwa yupo kwenye
harakati za kuingia katika sehemu hiyo ya juu.
***
Madam Mery akiwa amesimama pembezoni mwa
dirisha la chumba chake, anapunga upepo aliweza
kumuona Shamsa na mwenzake wakiingia kwenye
gari la kifahari majira ya usiku na kuondoka katika
eneo la hoteli hiyo, aliweza kuuona muelekeo
ambao gari hilo limeelekea, kabla hata dakika moja
haijakwisha aliweza kulishuhudia gari jengine
likitoka kwa kasi katika eneo hilo likielekea uelekeo
ambao ndipo lilipo kwenda gari la analo liendesha
Shamsa, kwa haraka akachukua koti lake la kuzuia
baridi na kipochi chake chenye pesa za kutosha,
akatoka nje ya hoteli, akaita teksi mmoja,
akamuelekeza dereva kuelekea upende zilipo toka
gari hizo mbili, kutokana dereva huyo aliweza
kuzishuhudia gari hizo zinapo elekea kwa hareka
akatekeleza jinsi mteja wake alivyo muagiza.
Haikuwachukua muda sana kuweza kuliona gari
zote mbili, wakawa wanazifwatilia kwa ukaribu
huku wakihakikisha kwamba hawagundiliki kwamba
wanawafwata wao.
“Mmmmm”
Dereva taksi aliguna kidogo huku akilisimamisha
gari yake kwenye moja ya kuona.
“Mbona unaguna na umesimama?”
“Huu mtaa zinapo ingia gari hizi mbili, ni mtaa wa
wahuni na watekaji”
“Sasa tunafanyaje?”
“Madam huku hata kwa kiasi gani cha pesa
utaklacho hitaji kunilipa sinto weza kukupeleka, ni
wiki ilipita ndugu yangu, ni dereva taksi naye
aliweza kunyongwa huku huku”
Dereva taksi alizungumza kimsisitizo akionyesha
kwamba, hatoweza kumpeleka Madam Mery katika
mtaa huop unao sifika kwa maswala ya kiunyangaji
na ujambazi. Madam Mery akaisindikiza gari waliyo
kuwa wanaifwata na kuiona ikiwa imesimama
pembezoni mwa gorofa moja. Akafungua pochi
yake na kutoa noti ya dola mia, na kuimkabidhi
dereva.
“Ninakuomba unisubirie hapa sawa”
“Sawa madam”
Dereva huyo alijibu huku akiachia tabasamu
kubwa, kwa maana amelipwa kiasi kikubwa cha
pesa ambacho ni tofauti na kazi ambayo
ameifanya. Madam Mery akashuka kwa haraka na
kuanza kutembea kwa tahadhari katika mtaa huo
ulio tulia sana. Akamshuhudia kijana mmoja
akiingia kwenye gorofa lililopo upande wa kulia
kutoka alipo simamisha gari kijana huyo. Nje ya
gorofa hilo akaiona gari ambayo anaitumia
Shamsa.
“Atakuwa hapa”
Madam Mery alizungumza huku akiongeza
mwendo wa kutembea kulifwata gorofa hilo, ila
mlio wa pikipiki inayo kuja kwa kasi mbele yake,
ukamfanya ajibanze kwenye gari la Lee Si, kwa
maana alisha pewa tahadhari kwamba mtaa huo ni
mtaa wa watu walio chafukwa na roho zao, kwa
hiyo ni vyema ajihadhari kabla ya hatari. Pikipiki
hiyo ikapunguza mwendo, na kusimama pembeni
kabisa mwa gari la Shamsa, kitu kilicho
mshangaza Madam Mery ni kumuona mtu aliye
valia nguo nyeusi kuanzia chuni hadi juu, huku
usoni mwake akiwa amevalia kinyago kilicho
mwacha macho wazi tu. Mtu huyo akatazama eneo
zima la nje hapo, alipo ona hakuna mtu akaingia
kwenye gorofa hilo. Wasiwasi mwingi ukamjaa
Madam Mery, ila akajikaza kusimama, akatizama
sehemu yote ya eneo hilo, kisha akaanza kupiga
hatua za kuelekea lilipo gorofa hilo, lililo chakaa
kwa nje. Kwa mwanga hafifiu wa taa zilizo fungwa
ndani ya gorofa hilo zikamsaidia madam Mery
kuona sehemu anapo elekea, kwa umakini
mkubwa akazidi kuzipandisha gazi, akielekea juu,
akifwata vishindo vya mtu huyo aliye ingia kwenye
gorofa hilo dakika chache zilizo pita. Kutokana na
kutokufanya mazoezi kwa muda mrefu, Madam
Mery akajikuta akiwa amechoka kuzipandisha gazi
hizo, akaanza kuzipandisha kwa mwendo wa
taratibu pasipo kukata tamaa, akiamini kuwa
sehemu anapo eleke ndipo alipo Shamsa.
Akiwa gorofa ya ishirini na tano, akasikia mlio wa
bastola ulio mstua na kumtetemesha mwili mzima,
kijasho chembamba kikaanza kumwagika, sehemu
alipo simama aliweza kuziona ngazi tano zinazo
elekea juu, ambapo kuna mlango mdogo wa
kuelekea juu, ambapo ndipo kulipo tokea mlio huo
wa risasi.
Kitu kilicho mstua madam Mery ni kuisikia sauti ya
mwanaume anaye mtambua hata akiwa usingizini
mwake, hawezi kuisahau sauti hiyo.
“EDDYYYYY…….!!!!”
Madam Mery aliita kwa shauku huku akianza
kuzipandisha nagazi za kueleka katika kimlango
hicho, akiwa katika ngazi ya nne, akastukia
akikubwa na mtu aliye toka kaika mlango huo na
wote wakaanza kubingirika katika ngazi hizo nne
hadi chini.
Shamsa, hakuhitaji kumuacha Lee Si, hivyo hivyo,
akashuka kwenye ngazi hizo, na kumvaa tena na
kuanza kumshambulia kwa ngumi nyingi sana,
tena maeneo ya pua yake, Madam Mery akiwa
anaendelea kuugulia maumivu ya kuanguka huko,
akashuhudia mparangano wa watu wawili
wakipigana kufa na kupona, alipo yaangaza macho
yake kwa umakini akamuona Shamsa, akiminyana
na kijna aliye muona ameteremka kwenye gari na
kuingia kwenye jengo hilo. Hapo ndipo Madam
Mery alipo mshuhudia, Shamsa kwamba ni katili
kwa maana Shamsa, aliporomosha makombora ya
ngumi nzito kwa kijana huyo anaye elekea kukata
roho.
“Anakufa huyu”
Madam Mery alizungumza huku akijizoa zoa na
kusimama, akamshika mkono Shamsa ili asimpige
ngumi kijnaa huyo ambaye ni Lee Si.
“Muache apigwe”
Sauti ya Sa Yoo, ikamfanya Madam Mery alegeze
mkono wa Shamsa, na ngumi nyingine nzito ikatua
puani mwa Lee Si, na kusababisha damu nyingi
kumrukia Shamsa usoni. Wala hakulijali hilo kwa
maana roho ya kikatili ilisha mvaa moyoni mwake,
na ni jambo la hatari sana kama akimuacha Lee Si
hai. Roho ya huruma ikamvaa Madam Mry,
hakuihitaji kumuona kijana huyo akiendelea
kupigwa mbele yake, alicho kifanya ni kumrukia
Shamsa na kumchomoa katika sehemu alipo
mkalia tumboni kijana huyo, jambo lililo
mshangaza Sa Yoo.
“Katokea wapi huyu”
Sa Yoo, alizungumza huku akianza kushuka
kwenye ngazi kwa haraka, akafika katika sehemu
walipo lala Madam Mery na Shamsa, aliye
kandamizwa chini, akiendelea kufurukuta. Sa Yoo
akaanza kumpiga ngumi za mgongo Madam Mery
ili amuachie Shamsa.
“Shamsa nisikilize mimi, mama, achana naye huyu
kijana”
Madama Mry alizungumza kwa sauti kali, hadi Sa
Yoo akastuka na kusitisha zaoezi lake la kuendelea
kumpiga ngumi madam Mery mgongoni.
“Anamjua Shamsa?”
Sa Yoo alijikuta akiropoka huku akiwa ameduwaa,
kwa jinsi Shamsa alivyo banwa na madam Mery
hakuweza kuendelea kukurupuka kwa maana
nguvu zilimuishia na kujikuta akiendelea kulia kwa
harira huku macho yake yakimtazama Lee Si aliye
poteza fahamu.
“Tulia mwanangu tafadhali”
Madam Mery aliendelea kuzungumza huku safai hii
akizungumza kwa sauti ya kumbembeleza Shamsa
aliye tulia tuli.
“Ed…ddy nime…kule nim…..ekuletea zawadi ya
mw….anao”
Sabogo alizungumza kwa sauti ya kukata kata,
huku damu nyingi zikiendelea eneo la kifuani,
puani na mdomoni. Machozi ya uchungu na
maumivu makali yakaanza kumtoka Black Shadow,
hakuamini kama anaweza kumpoteza rafiki yake
kwa namna hiyo.
“Sabogo usiondoke rafiki yangu, baki na mimi”
Black Shadow alizungumza huku machozi
yakimwagika.
“Ha…pana ka..aka muda wan…u ume…efika wa
wa….kuondoka duni….iani. Ikami….lishe famil..ilia
yak….o na, na Phi….dayaaa yupo….h…..”
Black Shadow, hakuimalizia sentesi yake akakata
roho. Black Shadow akabaki akishikwa na
bumbuazi, taratibu akajikuta akivua kinyago chake
na kukitupa pembeni. Machozi yakazidi kumtoka
kila anapomtazama Sabogo usoni mwake.
Madam Mery taratibu akamnyanyua Shamsa na
kumkumbatia, Sa Yoo akabaki kimya asizungumze
chochote.
“Shamsa”
Madam Mery aliita kwa sauti ya upole, huku
akimuachia Shamsa taratibu.
“Beeee”
“Upo sawa mama?”
Shamsa, akanyanyua macho yake na kumtazama
mwanamke huyo, Shamsa akabaki amemkodolea
macho Madam Mery hakujua amefikaje fikaje katika
eneo hilo.
”Umefikaje huku?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Madam
Mery usoni mwake.
“Nitakuambia nimefikaje”
Ukelele wa kulia kwa uchungu ulio tokea juu kabisa
ya gorofa ukawafanya wote watatu kustuka
hususani Shamsa ndio alishtuka zaidi, akajitoa
mikononi mwa madam Mery na kuanza kukimbilia
kuelekea gorofani, huku Madam Mery na Sa Yoo
wakimfwata kwa nyuma. Wote watatu wakamkuta
Black Shadow akiwa amepiga magoti chini, akilia
kama mtoto huku sura yake akiwa ameiinamisha
kwenye mwili wa Sabogo ulio lala chini kwa
kunyooka ukishiria kwamba Sabogo amepoteza
maisha.
“Babyyyy……..”
Shamsa aliita huku akikimbilia sehemu alipo Black
Shadow, na kuwaacha Sa Yoo na Madam Mery
wakiwa wamesimama wasijue ni nini cha kufanya.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 66 YA SIMUHILI HII.
 
Aseee kama naangalia movie hivi
Mkuu una kipaji saanaa hongera saanaa
Post ingine jmn yaan inanoga saanaaa
 
SORRY MADAM (66)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Ukelele wa kulia kwa uchungu ulio tokea juu kabisa
ya gorofa ukawafanya wote watatu kustuka
hususani Shamsa ndio alishtuka zaidi, akajitoa
mikononi mwa madam Mery na kuanza kukimbilia
kuelekea gorofani, huku Madam Mery na Sa Yoo
wakimfwata kwa nyuma. Wote watatu wakamkuta
Black Shadow akiwa amepiga magoti chini, akilia
kama mtoto huku sura yake akiwa ameiinamisha
kwenye mwili wa Sabogo ulio lala chini kwa
kunyooka ukishiria kwamba Sabogo amepoteza
maisha.
“Babyyyy……..”
Shamsa aliita huku akikimbilia sehemu alipo Black
Shadow, na kuwaacha Sa Yoo na Madam Mery
wakiwa wamesimama wasijue ni nini cha kufanya.
ENDELEA
Shamsa akazidi kumsogelea Black Shadow,
taratibu akamgusa begani jambo lililo mfanya
Black Shadow kujiifikiria kwa muda kabla
hajainyanyua sura yake kwa maana anamtambua
vizuri Shamsa kwamba ni mwanae wa kumlea japo
Shamsa hatambui ukweli wa aina yoyote.
‘Liwalo na liwe’
Black Shadow alizungumza huku taratibu
akinyanyua kichwa chake kutoka katika mwili wa
Sabogo aliye iaga dunia kwa kupigwa risasi na Lee
Si. Taratibu Black Shadow akaigeuza sura yake na
kumtazama Shamsa aliye stuka na kuyatoa macho
yake, mstuko huo haukuwa kwa Shamsa peke
yake, bali Madam Mery pamoja na Sa Yoo nao
wakabaki wakimkodolea macho Eddy kwani wote
walili wanamtambua vizuri hususani madam Mery
aliye kuwa mwalimu wa Eddy tangu akiwa kijana
mdogo.
“EDDY………”
Shamsa aliita huku akiwa bado hayaamini macho
yake, mwili mzima Shamsa akahisi unamuishia
nguvu. Taratibu Shamsa akajikuta akianguka
kwenda chini, kabla hajafika chini Eddy akamdaka,
Shamsa akazimia.
“Shamsa, Shamsa, Shamsaa”
Eddy alimuita Shamsa ila hakuitika kwa haraka
Eddy akamnyanyua Shamsa na kumuweka begani
mwake na kuanza kutoka kushuka kwenye jengo
hilo huku Madam Mery na Sa Yoo wakifwata kwa
nyuma wote wakionekana kuchanganyikikwa.
Wakafika chini Eddy akataka kupanda pikipiki yake,
ila Sa Yoo akamuomba watumie gari ambalo
walikuja nalo.
“Lete funguo”
Eddy alizungumza mara baada ya kumuingiza
Shamsa ndani ya gari, Sa Yoo akamkabidhi Eddy
funguo na wote wakaingia kwenye gari,
wakaondoka eneo hilo. Hapalukwa na mtu aliye
weza kuzungumza kitu cha aina yoyote, kila
mmoja alimfikiria Shamsa aliye laza kichwa
mapajani mwa Madam Mery huku Sa Yoo akiwa
siti ya mbele mara kwa mara aligeuka nyuma
kuwez akumuangalia Shamsa.
“Unaelekea wapi?”
Sa Yoo aliuliza baada ya kuona wanaelekea nje ya
mji. Eddy hakujibu kitu chochote zaidi ya kuongeza
mwendo kasi wa gari hadi wakafika kwenye msitu
mmoja mkubwa. Eddy akakunja kushoto kwenye
barabara ndogo iliyo jaa nyasi nyingi. Akaongeza
mwendo kasi hadi wakafanikiwa kufika kwenye
pango kubwa, ambapo Eddy kwa haraka akshuka
kwenye gari na kumtoa Shamsa, akambeba begani,
Madam Mery na Sa Yoo wakamfwata kwa nyuma
pasipo kuuliza ni wapi wanapo ingizwa.
Madam Mery na Sa Yoo wakaonekana kushangaa
mazingira ya ndani ya pango hilo lililo jengwa kwa
ndani vizuri na kuna taa nyingi ambazo
zinapendezesha mandhari ya ndnai ya pango hilo.
Eddy akamlaza Shamsa kwenye moja ya sofa,
lililopo sebleni. Akamfungua kifungo cha suruali
yake kisha akamvua tisheti aliyo vaa akabakiwa na
sidiria.
“Mpeni muda wa kupumzika amepoteza fahamu
huyo”
Eddy alizungumza huku jasho likimwagika usoni
mwake, akashusha punzi na kuanza kuwatazama
Madam Mery pamoja na Sa Yoo binti aliye msaidia
kipindi anatafutwa na askari wa hapa nchini Japan.
“Kweli wewe ndio Black Shadow?”
Sa Yoo aliuliza huku macho yake akiwa
amemtumbulia Eddy.
“Ndio mimi”
Eddy akamtazama Madam Mery ambaye
anaonekana anajambo ambalo anahitaji
kuzungumza ila anashindwa kulizungumza kwa
wakati huo kutokana na uwepo wa Sa Yoo. Eddy
baada ya kuligundua hilo akaanza kutembea
kuelekea nje na Madam Mery akamfwata kwa
nyuma.
“Umefikaje huku?”
Eddy alimuuliza Madam Mery kwa sauti nzito iliyo
jaa hasira ndani yake, kwa maana kumbukumbu ya
chanzo cha mtu aliye haribu maisha yake, ikamjia
Eddy kichwani na Madam Mery ndio muhusika
mkuu wa maisha ya Eddy kuharibika wakishirikiana
na Mzee Godwin.
Taratibu Madam Mery akapiga magoti chini, huku
machozi yakimwagika, kwani anamuelewa Eddy
vizuri na anatambua hali aliyo kuwa nayo kwa sasa
ni hali ya hasira na endapo atazungumza jambo
baya basi maisha yake yapo hatarini kuondoka.
“Eddy, ninahaki ya kufa mikononi mwako, nipo
tayari hata sasa hivi maisha yangu yatoke, ila nina
kitu kimoja ninahitaji kuzungumza na wewe kabla
hujaniua”
Madam mery alizungumza kwa sauti ya unyonge,
machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.
Kitendo cha sauti ya Madam Mery kupenya
masikioni mwa Eddy kikazidisha hasira yake na
kujikuta akikunja ngumi, mkono wa kulia huku
mmkono wa kushoto ukimtetemeka sana.
“Sinto hitaji kusikia kitu chochote kutoka kwako,
niliyaacha maisha yako kwa mara ya kwanza kwa
kuheshimu msiba wa mke wangu, mwanangu na
mama yangu. Ila kwa sasa nitakuua kisha atafwata
Godwin”
Eddy alizungumza huku akimgeukia Madam Mery
aliyepiga magoti pembeni yake. Akatamani
alichomoe koo la Madam Mery kwa mkono wake
wa kushoto unao tetemeka kwa hasira, ila akajikuta
mkono huo ukiwa ni mzito sana kufanya jambo
hilo. Madam Mery akatulia kimya, huku macho
yake ameyafumba kwani anatambua ni nini anacho
stahili kufanyiwa. Zikapita sekunde kadhaa za
ukimya, Madam Mery akayafumbua macho yake na
kumuona Eddy akiwa anaondoka kuingia ndani ya
pango hilo na hajamfanya kitu chochote.
“Eddy tunatakliwa kumuua Godwin”
Eddy akasimama, kisha akageuka taratibu na
kumtazama Madam Mery aliye piga magoti. Macho
ya Eddy yaliyo jaa uwekundu wa hasira huku kwa
mbali yakilengwa lengwa na machozi ya hasira,
yakaanza kumpandisha na kumshusha madam
Mery. Kisha sauti mbili moyoni mwake zikawa
zinabishana kwenye kufanya maamuzi. Sauti yake
ya kwanza inamtuma kumuua madam Mery muda
huo huo, huku sauti yake ya piliikimuomba
asifanye mauaji ya mwana mama huyo na
amsikilize kwa kile ambacho Madam Mery anahitaji
kumuambia.
“Tanzania pamoja na raisi Praygod wapo matatani,
muda wowote na saa yoyote wanaweza kupoteza
maisha……”
“Kutokana Godwin amekuwa……….Raisi wa nchini
Tanzania”
“NINI…..?”
Eddy alistuka sana kusikia habari hiyo ambayo ni
mbaya sana ndani ya masikio yake. Akamfwata
Madam Mery kwa kasi hadi sehemu alipo piga
magoti, jambo lililo mfanya madam Mery ajikute
amekaa chini kutokana na kumuogopa Eddy.
“Umesemaje………..?”
“Ni…nini….memee..eeesema baa…ba yak…o Go…
d……win amekuwa raisi wa Tanzania”
Madam Mery alizungumza huku mwili mzima
ukimtetemeka, japo kuna baridi Eddy akajikuta
jasho likimwagika kwa hasira. Kila alicho kifikiria
juu ya Mzee Godwin kilimchanganya akilini mwake.
“Na Phid….aya bado yupo hai”
Maneno ya Madam Mery yakazidi kumumshangaza
Eddy akilini mwake na kuanza kumkumbuka Nesi
Phidaya ambaye alimfananisha na mke wake ila
kitu kilicho mchanganya ni kwamba tayari alisha
mzika mkewe Phidaya.
***
Matajario mazuri ya watanzania juu ya uongozi wa
Raisi GGodwin, yakaanza kupotea kadri siku zilivyo
zidi kwenda. WWengi walitarajia ugumu wa maisha
utapungua ila ndio kwanza ukazidi kuongezeka
mara kumi ya awali walivyo kuwa. Nchi haikuwa ya
watanzania wote bali, ikageuka kuwa nchi ya
watanzania wachache, wenye nguvu ya kipesa na
wenye maamuzi ya kufanya chochote kwa wakati
wowote na kwamtu yoyote. Uonevu ukazidi
kuongezeka kwa wananchi wa hali za chini, watu
wote walio msaidia mzee Godwin kuingia
madarakani, walikabidhiwa madaraka makubwa
ambayo, hata watu wengine walio kua katika
serikali ya raisi Praygod na kumuunga mkono,
waliweza kupigwa chini, huku baadhi yao
wakibambikiwa kesi na kusekwa magerezani, huku
wengine wakifilisiwa na kubaki kuwa masikini
kabisaa.
“Mzee tunatakiwa kidogo tuwajali wananchi, hata
miaka mingine mitano ukigombania uraisi
wakupatie kura zao”
Mshauri wa raisi wa Mzee Godwin, alizungumza
huku akimtazama raisi Godwin usoni mwake. Mzee
Godwin akatabasamu kidogo kisha akaachia
kicheko cha dharau na kumtazama mshauri wake
bwala Mgwira
“Ni nani aliye kudanganya kwamba kutakuwa na
kupiga kura tena nchini Tanzania?”
“Una maana gani muheshimiwa?”
“Maana yangu ni kwamba hakuna mtu ambaye
atanitoa madarakani kwa kupiga kura. Hii nchi kwa
sasa ni yangu na nitaiongoza hadi pale nitakapo
fariki na endapo itatokea nitakufa basi atakaye
tawala atakuwa ni Manka mwanangu kipenzi”
Bwana Mgwira akabaki amemtumbulia macho
mzee Godwin, anaye zungumza kwa kujiamini
sana.
“Nahitaji nchi hii nibadilishe mfumo wa utawala,
uwe utawala wa kifalme na si utawala wa kiraisi”
“Muheshimiwa……………..!!!”
“Ndio, na tena wasiliana na viongozi wote kesho
ninahitaji kufanya nao mkutano sawa”
“Sawa muheshimiwa”
Mzee Mgwira hakuwa na kitu cha kuzungumza
zaidi ya kukubaliana na raisi Praygod ambaye siku
zote akizungumza haitaji mtu yoyote aweze
kukipinga. Manka akaingia kwenye sebule ya baba
yake na kumkuta akiwa amekaa na Mzee Mgwira,
ambaye baada ya kumuona Manka akanyanyuka na
kuondoka, kuwapisha baba na mwana
kuzungumza.
“Baba mbona unaonekana leo una furaha sana?”
“Ninafuraha mwanangu kwa maana nimefikiria kitu
ambacho nina imani kitakuweka wewe kwenye
mazingira mazuri sana”
“Kitu gani hicho baba, wakati unamiliki kila kitu
kwa sasa?”
“Ninakwenda kubadilisha mfumo wa serikali kutoka
katika mfumo wa serikali ya uraisi na kuingia
katika serikali ya ufalme”
Mzee Godwin alizungumza huku akifurahia sana.
“Ufalme, ufalme wa aina gani?”
“Nahitaji kuwa mfalme, nitakuwa nikiongoza katika
maisha yangu yote na hata mimi nikifa basi wewe
mwanangu utatawala katika kiti cha ufalme na
utakuwa ni malkia”
Manka naye aklajikuta akitabasamu na kufurahi
sana, juu ya wazo ambalo baba yake amelifikiria.
Kwa nguvu walio kuwa nayo walijiamini kwamba
kila kitu ndani ya Tanzania ni chakwao.
“Wezako wanaendeleaje?”
“Wapo salama tu, kila mtu anaendelea na
majukumu yake kwenye wizara ambayo
umewapatia”
“Basi wasiliana nao na kesho uwaambie kwamba
nina kikao ambacho kitakuwa kinakwenda
kuihalalisha serikali ninayo ifikiria”
“Sawa baba”
Manka akanyanyuka kwenye sofa alilo kalia
akamsogelea baba yake na kumbusu shavuni na
kuondoka zake sebleni na kumuacha Mzee Godwin
akifikiria mambo yake.
Siku iliyo fwata, mkutano wa viongozi wote ndani
ya serikali ya Mzee Godwin wakakutana kwenye
kikoa ambacho kila mmoja alishangazwa na
ukubwa wa kikao hicho kwa maana tangu uongozi
wa raisi Godwin uanze hajawahi kuitisha kikao
kikubwa kama hicho.
“Habari za asubu”
Raisi Godwin alizungumza kupitia kipaza sauti
kilichopo kwenye meza yake, kila kiongozi aliye
kuwepo kwenye eneo hilo aliitikia. Raisi Godwin
akawatizama viongozi walio chini yake kisha
akakohoa kidogo na kuanza kuzungumza kitu
ambacho alikusudia kukizungumza.
“Ninahitaji kubadilisha mfumo wa serikali”
“Serikali ambayo ninahitaji iwe kwa sasa, itakuwa
ni serikali ya ufalme, na hili swala sinto hitaji mtu
wa iana yoyote kuweza kulipinga hili”
Minong’ono ya chini chini ikaanza kutawala ndani
ya chumba cha mkutano, kila mmoja aliweza
kuzungumza chake juu ya kitu kilicho zungumza
na Raisi Godwin.
“Kuna baadhi ya sekta nitazifuta rasmi kuanzia leo
na sekta ya kwanza itakuwa ni Tume ya taifa ya
uchaguzi”
“Eheee bwana Luka unahitaji kuzungumza nini?”
“Muheshimiwa raisi wazo lako ulilo litoa si baya,
ila itakuwaje kwa hao wananchi ambao tuna
waongoza, watakubaliana kweli na hili?”
“Jeshi tunalo, nguvu ya pesa tunayo ni nani
anayewezakupinga kauli yangu?”
Raisi Godwin alizungumza na kuwafanya viongozi
wote kuwa kimya wasizungumze neno la aina
yoyote.
“Ninaagiza waziri wa mawasiliano, vijulishe
vyombo vya habari namuwatangazie juu ya hili
nililo zungumza sawa”
“Sawa mkuu”
“Na kitu cha mwisho ambacho labda
nitawahurumia wananchi wangu, waweze ku[iga
kura za ndio na hapana kupitisha serikali ninayo
itaka na watakao kataa. NITAJUA NI NINI
CHAKUFANYA”
Raisi Godwin alizungumza na kufunga kikao na
kuondoka ukumbini na kuacha mingong’ono
ikiendelea, kuna walio kubaliana naye na wapo
walio pinga wazo hilo ila walizungumza chichi
chini kuhofia ni kitu gani ambacho kitakwenda
kutokea juu ya maisha yao.
Kama waziri wa mawasiliano, alivyo agizwa,
akaitisha mkutana wa waandishi wa habari, karibia
televishion zote nchini Tanzania zikawa katika
ukumbi huo wa mikutano. Waziri wa mawasiliano
akatoa agizo ambalo limetolewa na raisi Godwin,
hadi waandishi wa habari wenyewe wakaanza
kushangaa kwa taarifa hiyo kwenda kwa wananchi.
Ikawa ni taarifa mpya kwa wananchi, wapo
waliohisi kuchanganyikiwa, ila uhuru wa
kuwakilisha mawzo yao kwenye jamii wanashindwa
kwa maana anaye kwenda kinyume na raisi
Godwin kwa kuweka kitu chochote kibaya kinacho
mfedhahesha raisi basi hufatiliwa na hupotea
katika mazingira ya kutatanisha. Siku na tarehe ya
kupiga kura za kuuweka uongozi wa ufalme
madarakani ukawadia, huku vipengele vya kupiga
kura vikiwa ni NDIO na HAPANA.
***
Hali ya Phidaya, ikazidi kuimarika siku hadi siku,
chini ya usimamizi wa Rahab na raisi mstafu
bwana Praygod aliye fukuzwa nje ya nchi ya
Tanzania. Phidaya akaruhusiwa kutoka hospitali na
kupeleka moja kwa moja katika nyumba ambayo
raisi Praygod aliweza kuinunua kwa ajili ya maisha
yake ya kudumu kwa maana hakuhitaji kurudi tena
nchini Tanzania.
“Kwa nini unasema uhitaji kurudi kwa mumeo
Ranjiti”
Raisi Praygod alimuuliza Phidaya wakiwa katika
meza ya chakula.
“Ranjiti sio mume wangu”
Phidaya alizungumza huku akimtazama raisi
Praygod usoni mwake.
“Una maana gani?”
“Ngoja nimsaidie, huyu ni mke wa waziri wako wa
zamani wa ulinzi Eddy Godwin”
Raisi Praygod akajikuta akiishusha glasi ambayo
alihitaji kunywa fumba la juisi ila akashindwa
kabisa kufanya hivyo, hapo ndipo kumbukumbu za
kumbumbuka Phidaya zikaanza kufanya kazi
kichwani mwake. Kitu kilicho kuwa kikimpa
uhakika kwamba huyu si mke wa Eddy ni kutokana
na msiba ambao hata yeye aliweza kuhudhuria
akiwa kama kiongozi.
“Haiwezekani…….Huyu binti si alisha kufa?”
“Ndio alikufa, ila si kama watu tulivyo dhania, ila
Phidaya yupo hai. Na ndio huyu hapa tuliye kaa
naye hapa”
“Hivi, Eddy yupo wapi kwa sasa?”
“Mara ya mwisho kumuona, alikuwa yupo Japan”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya upole sana
huku machozi yakimlenga lenga
“Itabidi nimtafute Eddy”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwatazama
Rahab na Phidaya.
***
Shamsa akakurupuka kutoka katika usingizi wa
nusu kufa. Akawakuta Sa Yoo, Eddy na Madam
Mery wakiwa wamekaa kimya wakimtazama.
Shamsa akamtazama Eddy, kisha akamtazama
Madam Mery, taratibu akaka kitako akisaidiwa na
Sa Yoo ambaye waketi wote alikaa karibu yake
akimkanda kanda kwa maji ya baridi.
“Umeamka”
Sa Yoo alizungumza huku akitabasamu, Shamsa
sura yake haikuwa na furaha yoyote kila alipo
yatazama mavazi aliyo vaa Eddy, akajikuta
akimkumbuka Black Shadow wake. Ukimya
ukatawala ndani ya sebule hapakuwa na mtu aliye
weza kuzungumza kitu chochote. Sa Yoo,
akatazama tazama ndani ya sebule hiyo akaona tv
kubwa iliyo kwenye moja ya ukuta ndani ya sebule
hiyo. Ili kuvunja ukimya huo akanyanyuka na
kwenda ilipo Tv hiyo na kuiwasha kisha akarudi
kukaa kwenye sofa. Kila mtu akayapeleka macho
yake kwenye Tv hiyo, na kukuta taarifa ambayo
imeishangaza ulimwengu mzima.
‘WATANZANIA WAPIGA KURA YA KUWEKA SERIKALI
YA UFALME NA SI URAISI’
“What…………”
Eddy alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa
alilo kaa na kuisogea ilipo tv hiyo kuisikiliza vizuri
taarifa hiyo kwenye kituo cha televishio na CNN.
“INABIDI NIRUDI TANZANIA KUIOKOA NCHI YANGU”
Eddy alizungumza huku akiitazama picha ya Mzee
Godwin, ikionyeshwa kama raisi aliye hitaji kufanya
mabadiliko hadi ya kiserikali.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 67 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (67)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
‘WATANZANIA WAPIGA KURA YA KUWEKA SERIKALI
YA UFALME NA SI URAISI’
“What…………”
Eddy alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa
alilo kaa na kuisogea ilipo tv hiyo kuisikiliza vizuri
taarifa hiyo kwenye kituo cha televishio na CNN.
“INABIDI NIRUDI TANZANIA KUIOKOA NCHI YANGU”
Eddy alizungumza huku akiitazama picha ya Mzee
Godwin, ikionyeshwa kama raisi aliye hitaji kufanya
mabadiliko hadi ya kiserikali.
ENDELEA
Mikakati ya kuanza safari ya kwenda nchini Misri,
inapo sadikika yupo Phidaya ndipo alipo. Kwa
msaada mkubwa wa Mzee Yo pamoja na Sa Yoo,
wakamuwezesha Eddy kutengenezewa sura ya
bandia ya daktari mmoja bingwa wa kutengeneza
sura hizi hapo nchini Japan.
Eddy akatafutiwa hati ya kusafiria, jambo ambalo
halikuwa gumu sana kwake na baada ya muda
akafanikiwa kuweza kupata hati ya kusafiria. Baada
ya siku mbili mbele safari ikaanza. Eddy akakaa
siti moja na Madam Mery huku Shamsa akikaa na
Sa Yoo aliye omba kusafiri nao. Masaa kadhaa
yakakatika angani wakiwa katika ndege ya shirika
ETHIAD. Wakafanikiwa kufika nchini Misri majira ya
saa tisa usiku. Wakakodi vyumba kwenye moja ya
hoteli ya kitalii. Gharama zote zikiwa juu ya Madam
Mery.
“Sa Yoo ile namba ya mwanamke aliye kupigia
siku ile si unayo?”
“Ndio niliiandika kwenye kijikitabu change”
Sa Yoo akafungua begi lake na kutoa kitabu chake
cha kuhifadhia kumbukumbu na kuanza kuitafuta
namba, haikuchukua hata dakika akafanikiwa
kuipata namba hiyo na kumkabidhi Shamsa, aliye
itazama kwa muda kisha akachukua na kuanza
kuiingiza kwenye simu ya mezani iliyomo ndani ya
chumba chao, hakuhitaji kusubiria kupambazuke
ndio aipige namba hiyo.
“Vipi?”
Sa Yoo aliuliza huku akiwa amemtumbulia macho
Shamsa aliye ushililia mkonga wa siku kwa mkono
wake wa kushoto huku akiwa ameuweka karibu
kabisa na sikio lake.
“Inaita”
Shamsa akaendelea kuisikilizia simu hiyo kwa
muda, ikaendelea kuita hadi ikakatika. Akajaribu
kwa mara mbili zaidi ila haikupokelewa akaamua
kuliacha zoezi hilo.
“Labda huyo mtu atakuwa emelala, tusubiri
asubuhi”
Sa Yoo alishauri, Shamsa akakubaliana na wazo
hilo. Eddy akiwa chumbani kwake, akasikia mlango
ukigongwa, akautazama kwa muda kisha
akasimama na kwenda kuufungua, Akakamkuta
madam Mery akiwa amesimama.
“Vipi hujalala bado?”
Eddy alimuuliza Madam Mery ambaye alitingisha
kichwa akiashiria kwamba hajalala bado. Eddy
akamkaribisha ndani Madam Mery, kila mmoja
akaka kwenye sofa lake akionekana kuwa hana kitu
cha kuzungumza hususani madam Mery ambaye
muda wote kichwa chake alikiinamisha chini.
“Mbona kimya uzungumzi kitu?”
“Eddy kila nikikutazama nafsi yangu inanisuta
sana, bado najiona ni mkosaji kwako”
“Ahaaa hayo mambo yamesha pita, tuangalie ni
kitu gani ambacho tunapaswa kukifanya kwa
wakati huu”
“Ni kweli ila nikiwa kama binadamu, nazidi kujiona
kwamba mimi ni mkosaji, ninaamini ni mambo
mengi ya kinyama ambayo nilikufanyia.”
Madam Mery alizungumza huku machozi
yakimlenga lenga, Eddy akamtazama kwa muda
akajikuta akiingiwa na roho ya huruma, taratibu
akasimama na kwenda kukaa kwenye sofa alilo kaa
madam Merry ambalo linaruhusu wakae watu
wawili.
“Nitazame Mery……”
Eddy alizungumza huku akimshika kichwa Madam
Mery kwa mikono yake miwili huku akimgeuzia
alipo.
“Hapo mwanzo nilikuchukia sana, ila baada ya
kunielezea ukweli nikajua si wewe mwenye
makosa. Wewe umeshurutishwa. Ila adui yetu ni
Mzee Godwin. Tunatakiwa kufanya kitu kwa ajili ya
mioyo yetu. Tuhakikishe kwamba tunafanikiwa
kumtokomeza na safari hii ninahitaji iwe ndio
mwisho wa maadui wangu”
“Eddy nitahakikisha……ninafanya kila utakalo
niambia, itakuwa ni kwaajili ya kufuta dhambi
zangu nilizo kuwa nimezifanya juu yako”
Madam Mery alizungumza huku machozi
yakimwagika, taratibu Eddy akajikuta akimkumbatia
madam Mery aliye zidi kulia kwa uchungu
“Shh………shiiiiii nyamaza usilie”
Eddy akaendelea kumbembeleza madam Mery
hadi, Madam Mery akajikuta akipitiwa na usingizi,
Eddy hakuona haja ya kumsumbua zaidi ya
kumuacha alalie kifua chake. Kutokana na uchovu
mwingi, Eddy naye akajikuta akipitiwa na usingizi.
Sa Yoo na Shamsa hawakulala hadi asubuhi
kunapambazuka. Shamsa akatoka chumbani kwao
na kwenda kwenye chumba ambacho analala Eddy,
alihitaji kumuelezea kuhusiana na namba ya mtu
ambaye wanaamini anaweza kuwasaidia kumpata
Phidaya. Shamsa akashika kitasa cha mlango wa
mlango wa kuingilia ndani kwa Eddy akataka
kupiga hodi ila akasita kwa muda na kukiachia.
Akiawa anajifikiria cha kufanya mlango
ukafunguliwa, akakutana na Madam Mery akiwa
anatoka katika chumba hicho, huku nywele zake
akiziweka vizuri.
“Za asubuhi”
Madam Mery akaanza kumsalimia Shamsa, jambo
lililo mfanya Shamsa kutokujibu kitu chochote zaidi
ya kumkodolea macho Madam Mery yaliyo jaa
maswali mengi.
“Shamsa nakusalimia”
“Aha…aa salama”
Shamsa akajitahidi kuizuia asira yake isijitokeze,
madam Mery hakujua chochote zaidi ya kuelekea
chumbani kwake na kumuacha Shamsa
akimtazama hadi anaingia chumbani kwake.
Shamsa akaingia chumbani kwa Eddy bila ya
kubisha hodi na kumkuta akitoka bafuni kuoga
akiwa na taulo kiunoni mwake.
“Nilihisi umeacha tabia yako kumbe bado unayo
tu”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya kukasikirika.
Jambo lililo mshangaza Eddy
“Tabia gani?”
“Hujui ni nini ulicho kifanya, huyu madam umelala
naye usiku kucha”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga hata Eddy akabaki akiwa ameduwaaa. Moyo
wa Shamsa ulipata maumivu makali kiasi kwamba
akahisi unataka kuchomoka. Alijitahidi kujizuia ila
hisia za mapenzi zilizidi kumuumiza japo
ameutambua ukweli kwa Black Shadow ni Eddy
anaye muheshimu kama baba yake.
“Shamsa, sijalala na huyu madam, alikuja jana
usiku chumbani kwangu kuna mambo tulikuwa
tunazungumza, ndio akapitiwa na usingizi”
Eddu alizungumza huku akiwa amemtazama
Shamsa, aliye jawa na hasira ya dhahiri kwamba
kuna kitu kinamuumiza, moyoni mwake. Shamsa
akajikuta akiachia msunyo mkali na kutoka
chumbani kwa Eddy na kumuacha akiwa
ameduwaa. Eddy hakuhitaji kuliwekee maanani
swala hilo zaidi alicho kifanya, akajiandaa kwa
haraka kisha akatoka chumbani kwake na kuelekea
chumbani kwa Shamsa na Sa Yoo. Akawakuta
wakiwa wamekaa kwenye sofa moja huku Shamsa
akionekana kuwa mnyonge.
“Mbona umekuwa mnyonge kiasi hicho Shamsa?”
Eddy aliuliza kwa sauti ya chini kiasi huku akikaa
kwenye sofa la pembeni. Sa Yoo akamtzama Eddy
kisha akamtazama Shamsa.
“Naona hajisikii vizuri, labda inaweza kutokana na
mabadiliko ya hali ya hewa”
Sa Yoo alijibu huku naye akiwa hajui ni kitu gani
ambacho kinamsumbua rafiki yake huyo, ambaye
kwa sasa amekuwa kama ndugu yake. Madam
Mery akiingia ndani ya chumba hicho huku akiwa
amesha badilisha nguo zake tofauti na alizo kuwa
amezivaa jana kwenye safari. Kabla madam Mery
hajazungumza kitu chochote, mlio wa simu ya
mezani ukawastusha kila mmoja na kujikuta
macho yao yote wakiyageuzia kwenye simu hiyo
inayo endelea kuita kwa muito wa taratibu.
***
Msisimko wa mapenzi ukaanza kumpanda Rahab
aliye lala fofofo, taratibu akayafumbua macho yake
yaliyo jaa uchovu wa usingizi wa usiku kucha.
Akamkuta mume wake, raisi mstafu bwana Praygod
akiwa anaipitisha mikono yake kwenye sehemu ya
kifua chake, kilicho jazia chuchu zilizo jaa vizuri.
“Mmmm…..baby bwanaaa asubuhi yote hii
unaniamsha”
Rahabu alizungumza kwa sauti iliyo jaa mapozi
mengi huku macho yake yakilegea kwa msisimko
huo anao patiwa na mume wake.
“Nina hamu na wewe mke wangu”
“Kweli?”
“Ndio honey”
Raisi Praygod alizungumza huku akiendelea
kuyaminya minya maziwa ya Rahab, kutokana wote
wawili walila usiku huo pasipo kuwa na nguo
yoyote mwilini wakajikuta wakizama kwenye
dimbwi zito la mapenzi. Rahab kama kawaida yake
alihakikisha anampatia mume wake penzi lililo
jitosheleza.
“Ohooo….ooo”
Raisi Praygod alitoa miguno huku taratibu Rahab
akijilaza pembeni ya mwili wa raisi Praygod.
Taratibu Rahab akaupeleka mkono wake kwenye
meza ya pembeni alipo iweka simu yake ya
mkononi. Akaitazama vizuri na kukuta missed call
kadha zilizo ingia majira ya usiku.
“Mmmm namba ngeni”
“Jaribu kuzipiga hizo namba”
Rahab akaanza kuipiga namba ya kwanza, iliyo ita
kwa muda na kupokelewa na sauti ya kike.
“Haloo, jana usiku ulinipigia, nani mwenzangu”
“Naitwa Sa Yoo, niliwahi kuzungumza na wee
nikiwa Japan ukanieleza kuhusiana na swala la
bosi wangu Madam Phidaya kwamba yupo nchini
hapa Misri”
“Waooo, ina maana upo ndani ya Misri”
“Ndio madam, sijui wewe upo sehemu gani?”
“Ila kwa maagizo ya Phidaya aliniambia mtu
ambaye anatakiwa kuonana naye ni Lee Si”
“Ah…….a.aaa..ndio ila Lee Si ameniagiza mimi
kuweza kuja, ila unaweza kumuambia madam
kwamba Sa Yoo nipo hapa ninamtafuta”
“Sawa hembu subiri kama dakika tano, nitakupigia
tena”
Rahab akakata simu na kushuka kitandani, akavaa
gauni lake jepesi na kutoka chumbani kwake na
kwenda moja kwa moja hadi kwenye chumba cha
Phidaya akagonga mara moja mlango
ukafunguliwa, wakakutana na Phidaya ambaye
alikuwa akifanya usafi.
“Za asubuhi Phidaya”
“Salama vipi mbona mapema, na unaonekana
kama kuna tatizo?”
“Hapana sio tatizo, ila nina habari ambayo kidogo
ni njema kwako”
“Habari gani hiyo”
Rahab akaingia ndani na moja kwa moja akaenda
na kukaa kitandani mwa Phidaya ambaye naye
akamfwata na wakaka kwa pamoja.
“Nimepata simu kutoka kwa binti mmoja anaitwa
Sa Yoo sijui unamfahamu”
“Ndi..ndio ninamfahamu, amesemaje?”
Phidaya alizungumza huku akionekana kuwa na
tabasamu pana usoni mwake.
“Ameniambia kwamba yupo hapa nchini Misri
amekuja kuonana na wewe?”
“Yupo wapi?”
“Ohoo sikumuuliza ni wapi alipo, ilangoja niipige
tena ile namba uzungumze naye”
***
Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi Dokta
Ranjiti alivyo zidisha wingi wa vijana wanao weza
kumsaidia kumtafuta Phidaya ndani ya nchi ya
misri. Alikodisha vikundi vitano vinavyo jiusisha
katika swala la uhalifu, na kila kikundi akawa
amekiahidi donge nono la pesa, endapo tu
watafanikisha kumkamata Phidaya akiwa hai. Kila
kikundi kiliweza kupatiwa picha za kutosha zenye
kuionyesha sura ya Phidaya. Upelelezi ulizidi kuwa
mkali katika miji yote.
“Bado hamjampata?”
Dokta Ranjiti alimuuliza mmoja wa viongozi wa
kikundi cha uhalifu
“Bado hatujampata, vijana wanaendelea kumtafuta
kwa udi na uvumba nitahakikisha kwamba
tutampata”
“Hembu harakisheni kumtafuta, au hamtaki pesa
nyinyi”
“Mzee hakuna ambaye hapendi pesa ndio maana
kazi yako tunaifanya usiku na mchana
tutahakikisha kwamba anapatikana”
“Sawa fanyeni hivyo”
Dokta Ranjiti akakata simu, huku hasira ikiwa
imempanda. Akilini mwake alihisi kuchanganyikiwa
, kwani katika maisha yake anampenda mke wake
Phidaya kuliko kitu cha aina yoyote ndio maana
alihakikisha anafanikiwa kuwa na Phidaya katika
maisha yake.
“Bosi kuna simu yako hapa”
Kijana anaye mlinda dokta Ranjiti aliingia ndani ya
chumba cha dokta Ranjiti akiwa na simu mkononi
mwake. Akampatia dokta Ranjiti na kuiweka
sikiooni.
“Nani mwenzangu?”
“Hakuna haja ya kuweza kulifahamu jina langu, ila
mwanamke ambaye unamuhitaji yupo njiani
kuelekea kwenye hoteli ya AHAL, iliyopo katikati ya
jiji la Cairo”
Sauti ya kike ilisikika upande wa pili wa siku, kabla
dokta Ranjiti hajazungumza kitu chochote simu
ikakata. Akajaribu kuitazama namba iliyo mpigia
kwa bahati mbaya akakakuta ni namba private
ambayo si rahisi kwa mtu yoyote kuweza kuipga,
labda mwenye namba hiyo akupigie yeye
mwenyewe.
“Jiandae twende hoteli ya AHAL”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akinyanyuka kwa
haraka kutoka kwenye kiti ambacho alikuwa
amekalia. Wakatoka na mlinzi wake na kuingia
kwenye gari lake, na safari ya kueleka katika hoteli
aliyo elekezwa na msamaria mwema.
***
Simu ikaita na Sa Yoo akaipokea na kuzungumza
na mtu aliye piga kwa bahati nzuri akakuta ni sauti
ya Rahab
“Ehee ulisema kwamba upo wapi?”
“Nipo katika hoteli ya AHAL, gorofa ya ishirini
chumba namba elfu mbili na tisa”
“Sawa tunajiandaa tunakuja hapo mulipo sasa hivi
na Phidaya”
“Sawa nitawapokea”
Simu ikakatwa Sa Yoo akawageukia, Eddy na
wezake huku akiwa na tabasamu pana usoni
mwake.
“Wanakuja”
“Saa ngapi?”
Eddy aliuliza kwa shauku kubwa, kwa mbali
machozi yakimlenga lenga.
“Ameniambia dakika chache watakuwa hapa”
Shamsa hakuonekana kuwa na furaha ya aina
yoyote zaidia alicho kifanya ni kunyanyuka na
kutoka nje ya chumba hicho pasipo kumuaga mtu
yoyote.
“Mbona mwenzako yupo hivi?”
Eddy alimuuliza Sa Yoo baada ya Shamsa kutoka
ndani ya chumba hicho.
“Sifahamu anasumbuliwa na nini, kwa maana hii
hali imeanza asubuhi hii tu”
Hapakuwa na aliye weza kuliwekea maanani swala
la Shamsa, kila mtu kwa wakati huo akawa
anamfikiria Phidaya. Baada ya dakika tano Shamsa
akaingia akiwa katika hali yake ya unyonge.
Hapakuwa na mtu aliye msemesha. Baada ya
dakika tano mbeleni simu ikaita, Sa Yoo kwa
haraka akakimbialia hadi mezani na kuipokea simu
hiyo.
“Tumesha fika kwenye hii hoteli, tupo hapa chini.
Sijui unaweza kuja kutuchukua”
Sauti ya Rahab ilisikika kwenye simu hiyoi
“Sawa basi ninakuja”
Sa Yoo akakata simu na kuwataarifu wezake habari
hiyo, wote kwa pamoja wakatoka kwenye lifti hiyo
na kuanza kushuka kwenda chini.
Rahab na Phidaya wakiwa ndani taksi waliyo jia,
wakaendelea kumsubiria mwenyeji wao kuja
kuwapokea, uzuri ni kwamba Phidaya anamfahamu
Sa Yoo, macho yao kwa pamoja wakawa
wanatazama kwenye mlango wa kutokea kwenye
hoteli hiyo kubwa ya kitalii, yenye wageni wengi
wanao ingia na kutoka.
Meseji ikaingia kwenye simu ya dokta Ranjiti
inayosomeka kwa maandishi makubwa (TUPO
KWENYE TAKSI NYEUPE HAPA KATIKA MAEGESHO
MUHESHIMIWA)
Meseji hiyo ilimtosheleza dokta Ranjiti kuyapitisha
macho yake kwenye maegesho ya magari yaliyopo
katika eneo hilo. Akaiona taski nyeupe iliyopo
kwenye eneo hilo, dokta Ranjiti akashuka kwenye
gari kwa haraka huku bastola yake ikiwa mkononi
mwake. Kwa hatua za haraka anazo zitembea
dokta Ranjiti, akafanikiwa kuifikia taksi hiyo kwa
haraka, pasipohata kuzungumza chochote
akaufungua mlango wa nyuma wa siti hiyo.
Phidaya akastuka macho yakamtoka, mwili mzima
akahisi umemuishia nguvu, alipo iona sura ya
dokta Ranjiti iliyo jaa hasira. Rahab naye akajikuta
akimeza fumba la mate asijue ni nini afanye kwa
maana mdomo wa bastola ya dokta Ranjiti ukiwa
umewaelekea.
“SHUKA NDANI YA GARI”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa hasira kali, bila
hata ya kubisha Phidaya akashuka ndani ya gari,
huku Rahab naye akafwatia kushuka. Dokta Ranjiti
kwa iashara akawaelekeze sehemu ya kuelekea
kwenye gari lake. Macho ya Eddy, Sa Yoo, Shamsa
na Madam Mery wakawashuhudia Phidaya na
Rahab wakiingia kwenye moja ya gari la kifahari
huku nyuma yao akiwepo dokta Ranjiti.
“RANJITIIIIIIIIIIIIIIIIIII…………………….”
Eddy aliita kwa sauti kubwa na kumfanya dokta
Ranjiti kutazama sehemu sauti hiyo inapo tokea,
kwa haraka aliweza kuotambua sauti hiyo ni ya
Eddy, ila sura ni tofauti kabisa, ila macho yake
yalipo muona Madam Mery akiwa nyuma ya mtu
huyo akagundua kwamba kila kitu kimeharibika.
Kwa kiwewe dokta Ranjiti akajikuta akifyatua risasi
kadhaa kuelekea anapotokea Eddy na kusababisha
watu kuanza kukimbia kimbia ovyo kuyaokoa
maisha yao.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 68 YA SIMUHILI HII.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom