Sorry madam (Destination of my enemies)

SORRY MADAM (34)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Raisi Praygod akiwa amejilaza chali huku akihema
kama mtu aliye fukuzwa, akajikuta akishangilia
kimya kimya kwa Eddy kuweza kufariki. Akashuka
kitandani na kujinyoosha, kabla hata hajapiga
hatua mbele simu ya mke wake iliyo anguka chini
ikaingia ujumbe wa maandishi, akaiokota taratibu
na kuirushia kitandani, akapiga hatua mbili
kuelekea bafuni, ila roho yake ikasita, akarudi hadi
kitandani na kuichukua simu ya Rahab. Pasipo
kujishauri mara mbili akaufungua ujumbe ambao
jina limejitokeza kwa ufupi ‘SAM’. Akatingisha
kichwa mara mbili kuyaweka macho yake sawa,
kurudia kuusoma ujumbe huo wa meseji.
{MADAM EDDY, AMEPIGWA RISASI YA MGUU NA
ANAHITAJI DAMU NIMUWEKEE YAKWANGU?}
“EDDYYYYYY………………………???”
Raisi Praygod akabaki akiwa amejiuliza, kugeuza
shingo yake nyuma akamkuta Rahab akiwa
amesima nje ya mlango wa bafuni akijifuta maji
kwa taulo.
ENDELEA
Raisi Praygod baada ya kugundua kwamba Rahab
hajastuka kwa lolote kwa haraka akaifuta meseji
hiyo kisha akaizima simu na kuirudisha kimya
kimya na kuirudisha kitandani.
“Baby kaoge upumzike”
Rahaba alizungumza kwa sauti ya upole, huku
akipiga hatua za kuelekea kwenye kabati kubwa
kubwa, akatoa kigauni kidogo cha kulalia, na
kumuacha mume wake akielekea bafuni kuoga.
Msongo wa mawazo ukaanza kukiumiza kichwa
cha raisi Praygod, kwani haelewi kama Eddy
amekuwa vipi hai. Akafungulia bomba taratibu maji
yakaanza kumwagikia mwilini mwake huku
akiendelea kujiuliza maswali ambayo mengi
alijikuta akiwa amekosa majibu. Akamaliza na
kurudi chumbani kwake na kumkuta Rahab akiwa
tayari amesha jilaza kitandani huku akiwa
amejifunika shuka kubwa na zito.
“Vipi ulali leo?”
“Nahitaji kutoka tena”
“Unakwenda wapi saa hizi mume wangu”
“Kuna kazi nahitaji kuweza kuifanya ofisini mara
moja”
“Mmmmm……Haya mwaya”
Rahab akajigeuza upende wa pili wakitanda, raisi
Praygod akavaa nguo za mazoezi(track suit), kisha
akatoka ndani ya na kuelekea ofisini kwake.
“Nahitaji twende Muhimbili kuutazama mwili wa
waziri Eddy”
Raisi Praygod alimuambia Lube, wote kwa pamoja
wakatoka usiku huo huo, akachukua walinzi
wengine wanne wakaondoka ndani ya ikulu
***
Uvamizi wa jeshi katika jumba la waziri wa ulinzi
mstafu anaye sadikika amefariki katika jaribio la
kuteka jengo la biashara la Mlimani city, ukazidi
kusonga mbele ikiwa ni amri kutoka kwa amiri
jeshi mkuu raisi Praygod Makuya, akiamini katika
jumba hilo kuta kuwa na mambo ya siri ambayo
serikali kama serikali hawayafahamu.
Upelelezi ukazidi kufanyika kila kona ya jumba hilo,
kitu kilicho zidi kuwapa mashaka wanajeshi hao ni
damu iliyo kutwa ndani ya gari lililo kuwa na
baadhi ya silaha katika maeneo ya maegesho
katika jumba hilo.
“Muheshimiwa kuna dalili ya uhai wa watu humu
ndani”
Mwanajeshi mmoja alizungumza mara baada ya
kutafuta kila sehemu ila hawakuona mtu wa aina
yoyote.
“Endeleeni kutafuta kila konaaa”
“Sawa Captain”
Wanajeshi wapatao ishirini na tano kama walivyo
agizwa na mkuu wao wa kikosi wakazidi kufanya
uchunguzi huku wakichangua changua kila chumba
kuangalia kama kuna mtu kwani damu hiyo
inaonekana ni mbichi kabisa. Wasiwasi mwingi
ukazidi kumjaa Samson, kwani endapo chimba
hicho cha siri kilichopo chini ya ardhi kikifahamika
basi inaweza ikawa ni shida kwao. Akatoa simua
yake mfukoni na kupigia Rahab ila hakupatikana
hewani, akajaribu kupiga zidi na zaidi ila namba
haikupatikana.
“Muheshimiwa kuna chumba hapa chini”
Sauti moja ilisikika nje ya mlango wa chumba
hicho, macho ya Samson akayeelekezea mlangoni,
mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio,
akamtazama Eddy, ila bado hajazinduka kutoka
kwenye kupoteza fahamu. Samson akaiwahi swichi
ya ukutani na kuzima taa zote, macho yake
yakabadilika, na kuwa katika hali ya kutisha.
Kaptain wa kikosi akafika hadi nje ya chumba
hicho alipo itiwa na wanajeshi wake. Chini ya
mlango huo kuna matone kadhaa ya damu
yakiashiria kwamba mtu huyo ameingia ndani ya
chumba hicho.
“Vunjaa mlangoo”
Kiongozi huyo alitoa amri, iliyo anza kutekelezwa
mara moja kwa vijana wake kuurukia mlango huo
kwa kutumia mabega yao. Samson akasimama
katikati ya mlango huo akimsubiria atakaye anza
kuingia ndani basi atakuwa ni alali yake.
***
“Nini…………..”
Mzee Godwin aliuliza kwa hasira huku akiwa
ameiweka simu yake sikioni.
“Ndio muheshimiwa yule kijana amekamatwa na
polisi na sasa yupo katika uchunguzi”
“Pumbavu wewe, hakikisha huyo kijana
hazungumzi kitu cha aina yoyote na ikishindikana
basi muuee”
“Ila muheshimiwa kijana huyo si wakwetu ni wa Al-
Shabab na endapo tukimuua si itakuwa ni
mtafaruka?”
“Nimekuambia muue”
Simu ikakatwa, bwana Mgwira, akabaki akiwa
ameishika simu yake kwa wasiwasi asijue ni nini
cha kufanya kwani tayari amesha pokea oda kutoka
makao makuu kwa bosi wake. Bwana Mgira
akatazama saa yake ya mkononi na kukuta ni saa,
kumi na moja alfajiri na ninusu saa tangu aingie
nyumbani kwake akitokea ofisini ya raisi akiwa
kama miongoni mwa washauri wa ngazi ya juu wa
raisi Praygod. Bwana Mgira kwa haraka
akakumbuka mkuu wa polisi wa kanda maalumu ni
rafiki yake wa muda mrefu kwa haraka akaitafuta
namba ya muheshimiwa huyo anaye amini wakati
huu bado atakuwa macho kutokana na jukumu zito
walilo toka kulifanya masaa machache ya nyuma.
“Ndio muheshimiwa”
Sauti nzito ilisikika kutoka upande wa pili wa simu.
“Huyu mtuhumiwa muliye mshikilia ameweza
kungumza kitu chochote?”
“Bado muheshimiwa, ila vijana wanazidi kumbana,
ili aweze kusema kwamba kundi la waziri Eddy,
lipowapi”
“Kwai inavyo wezekana kukawa na walio salia
katika kundi hilo kwa maana kiongozi wao ndio
huyo amesha kufa?”
“Hilo sina uhakika nalo kutokana bado mtuhumiwa
hajazungumza kitu chochote hadi sasa hivi japo
bado anapewa mateso makali ila hajazungumza”
“Basi kuna kuna……..”
Bwana Mgwira akajing’ata ng’ata akitamani
kuzungumza jambo.
“Vipi kuna tatizo?”
“Hapana, basi hakikisheni anazungumza kwa
maana hali ya usalama bado si shwari ndani ya hii
nchi”
“Usijali muheshimiwa hilo nalo tutalifanyia kazi
hapata kuwa na shida yoyote.”
Bwana Mgwira Akaka simu na kushusha pumzi
nyingi akiwa anajiuliza ni jambo gani aweze
kulifanya kwa Briton aliye shikiliwa na jeshi la
polisi. Waz likamijia kichwani na kujikuta
akitabasamu huku akiitazama simu yake.
***
Taratibu macho ya Shamsa yakaanza kufunguka,
akaanza kutazama kila sehemu kuona ni wapi
alipo. Kando yake upande wakulia akaona kitanda
ambacho amelazwa mama wa makamo kidogo,
kageuka upande wa kushoto na kukuta kitanda
kingine kikiwa kimekaliwa na mama mmoja huku
binti mdogo akiwa amelala kwenye kitanda hicho
akiwa ametundikiwa dribu la maji. Shamsa
akajaribu kunyanyuka ila maumivu makali yakapita
kwenye tumbo lake na kujikuta akirudi tena na
kulala kama alivyo jikuta awali.
Kumbukumbu ya mwisho ikamjia kipindi alipo
jikuta akiwa amepigwa teke zito la mwisho na
Eddy, lililo mfanya kuwa katika hali hiyo aliyo kuwa
nayo kwa kipindi hichi. Machozi ya yakaanza
kumwagika pembezoni mwa macho yake,
hakuamini kama Eddy aliye kuwa akimpenda na
kumchukulia kama baba yake amebadilika na kuwa
jambazi wa kuweza kutoa roho za raisi wasio na
hatia. Akiwa katika hali hiyo akapita nesi karibu na
kitanda chake, akalazimika kumuita ili kumuhoji
baadhi ya maswali.
“Eti nesi hapa nipo wapi?”
“Hapa ni Muhimbili hospitali ya Taifa, Muhimbili na
hii ni wodi ya watu walio pata matatizo kwenye
tukio la ligaidi Mlimani City”
“Ahaa sawa asante”
Nesi huyo akaondoka ila kabla hajafika mbali
Shamsa akamuita tena na kurudi hadi kilipo
kitanda cha Shamsa.
“Hivi yule kiongozi wa watekaji yupo wapi?”
“Nani………. Waziri Eddy Godwin?”
“Eheee”
“Yule ameshakufa aliuwa kwa na mwenzake aliye
kuwa akishirikiana naye”
“Nini?
“Ndio amekufa mbona unashangaa sana?”
“Ahaa ahaha hapana”
Shamsa alizungumza huku machozi yakianza
kumlanga lenga tena, nesi huyo akandoka na
kumuachia Shamsa simanzi kubwa, na likiwa ni
moja ya pigo jengine kubwa sana, kwani mtu
anaye mtemea ndio hoyo tayari amesha iga dunia.
Shamsa taratibu akaanza kushuka kitandani huku
maumivu makali yakiendelea kumsumbua kwenye
tumbo lake, akaanza kutembea huku akiyumba
yumba mara kadhaa akalazimika kuweza
kujishikiza kwenye baadhi ya vitanda hadi
akafanikiwa kutoka nje ya wodi hiyo ya wanawake.
Akatazama eneo zima nje ya wodi hiyo, idadi
kubwa ya watu mchanganyiko ipo nje ya wodi
hiyo, wengine wakiwemo ni ndugu na jamaa walio
kuja kuwatembelea ndugu zao.
“Raisi amekuja yupo mochwari kule”
Madaktari wawili walio pita kwa mwendo wa kasi
huku wakiwa wamevalia makoti meupe walipita
karibu na Shamsa wakizungumza mada iliyo
mfanya Shamsa, kuichambua kwa haraka kichwani
mwake na kugundua ujio wa raisi Praygod Makuya
kwenye hospitali hiyo ni kuweza kutazama mwili
wa aliye kuwa miongoni mwa watumishi wake
waadilifu ndani ya serikali yake waziri wa ulinzi
bwana Eddy Godwin.
“Wewe, wewee”
Shamsa alimuiita kijana mmoja aliye simama
karibu yake, kwa sauti ya unyonge inayo ashiria
kwamba bado ni mgonjwa, kwani hata sura yake
inaashiria kuonekana ni mtu anaye sumbuliwa na
maumivu makali kwenye moja ya maeneo ya mwili
wake. Kijana huyo akasogea hadi sehemu alipo
Shamsa ili kumsikiliza ni haja gani aliyo kuwa
nayo
“Eti mochwari ni wapi?”
“Ni kule”
Kina huyo alimuonyesha kaskazini mwa sehemu
hiyo waliyo simama kwa kutumia kidole, Shamsa
akajaribu kupiga hatua moja mbele, ila akayumba
sana hadi kijana huyo akamdaka.
“Dada upo sawa kweli?”
“Ndio nipo sawa”
“Hapana dada haupo sawa”
Kijana huyo alizungumza kwa msisitizo, kwa
maumivu makali ya tumbo taratibu Shamsa
akajikuta miguu yake ikianza kumuishia nguvu,
taratibu akajikuta akikalishwa chini kwa msaada wa
kijana huyo aliye msihikilia mwili wake ili
asianguke.
“Muheshimiwa huu si mwili wa waziri Eddy
Godwin. Mtu huyu alivalia sura ya bandia ili
kuweza kuitumia katika uhalifu wake ili kumshafulia
muheshimiwa waziri mstaafu”
Mkemia mkuu wa serikali alizungumza huku mwili
wa Lukuma ukiwa umelazwa juu ya meza iliyopo
ndani ya chumba cha uchunguzi, huku sura yake
halisi ikiwa imeonekana na sura bandia inayo
fanania na sura ya waziri Eddy ikiwa imesha
tolewa.
‘Ina maana huyu mshenzi bado yupo hai?’
Raisi Praygod alizungumza kimoyo moyo huku
akiutazama mwili wa Lukuman kwa hasira kali
“Irudisheni sura yake halisi na mutangaze waziri
Eddy Godwin amefariki dunia. Hii si ombi bali ni
amri”
Raisi Praygod alizungumza kwa msisitizo kisha
akatoka ndani ya chumba hicho kwa hasira na
kumuacha mkemia mkuu wa serikali akiwa
ameduwaa uamuzi huo ulio chukuliwa na
muheshimiwa raisi.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 35 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (35)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
‘Ina maana huyu mshenzi bado yupo hai?’
Raisi Praygod alizungumza kimoyo moyo huku
akiutazama mwili wa Lukuman kwa hasira kali
“Irudisheni sura yake halisi na mutangaze waziri
Eddy Godwin amefariki dunia. Hii si ombi bali ni
amri”
Raisi Praygod alizungumza kwa msisitizo kisha
akatoka ndani ya chumba hicho kwa hasira na
kumuacha mkemia mkuu wa serikali akiwa
ameduwaa uamuzi huo ulio chukuliwa na
muheshimiwa raisi.
ENDELEA
***
Vishindo vikazidi kusikika nje ya mlango wa
chumba cha siri walimo Eddy aliye poteza fahamu
pamoja na Samson ambaye macho yake yote
ameyaelekezea kwenye mlango huo, gafla mlango
huo ukafunguka, na wanajeshi wane wakajikuta
wakiingia ndani pamoja na mlango huo. Samson
kwa haraka akaanza kuwashambulia wanajeshi hao
kwa kuwavunja shingo zao, huku baadhi yao
wakitoa vilio vya maumivu makali. Wanajeshi
wengine walio kuwa nje wakajikuta wakifyatua
risasi hovyo hovyo pasipo kujua ni nani anaye
washambuli. Samson akatoka kwa mwendo wa
kasi na kupita katikati yao na kuanza
kuwashambulia kwa kuwaua kinyama pasipo
huruma. Idadi ya wanajeshi wote walio weza kufika
nyumbanbi kwa Eddy, wakauawa.
Bila ya kupoteza muda Samson akarudi ndani ya
chumba na kumchukua Eddy aliyekuwa
amemuhifadhi kwenye sehemu ambayo haikuwa ni
raisi kwa risasi kuweza kumfikia. Akamuingia
kwenye gari yao na kuondoka maeneo ya jumba
hilo la kifahari.
Kila simu ya upepo iliyokuwa ikipigwa kwa
kiongozi wa kikosi hicho kujua ni nini kinacho
endelea katika eneo hilo haikuweza kupokelewa,
ikabidi watumwe wanajeshi wengine watano
kwenda kutazama ni kitu gani ambacho
kinaendelea kwenye eneo la tukio. Wanajeshi walio
fika kwenye eneo la tukio hawakuamini macho yao
kuwakuta wezao wote wakiwa wamelala chini huku
wakiwa wameuwa kifo kinacho onyesha muuaji
hakuweza kutumi silaha bali ni kitu chenye ncha
kali kama kucha, zilizo weza kuwaparuza wengi
wao kwenye sehemu mbalimbali za miili yao.
***
Mkemia mkuu wa serikali bwana Ignatus Mkama,
hakuwa na jinsi yoyote yakufanya kwani amri aliyo
pewa na raisi Praygod alilazimika kuweza
kuitekeleza mara moja. Akaitisha mkutano na
waandishi wa habari walio weza kuweka kambi
katika hospitali ya muhimbili kujua ni kitu gani
kinacho endelea kuhusiana na kifo cha waziri wa
ulinzi Eddy Godwin.
“Nimedhibitisha ya kwamba aliye kuwa ni waziri wa
ulinzi na mtoto wa waziri mkuu mstafu. Eddy
Gdowin, amefariki dunia”
Waandishi wa habari wa magazeti, redio na
televishion hawakusita kuuliza maswali kwa bwana
Ingatus Mkama.
“Je kifo chake kimesababishwa na nini?”
“Kifo chake kimetokana na kupigizwa chini sehemu
ya nyuma ya kichwa chake, ambapo kulipelekea
mpasuko mkubwa kwenye ubungo wake na damu
iliweza kuvuja na kupelekea ubongo wake kuweza
kuganda na ndipo mauti yalipo chukua mauti yake”
***
“Kijana usipo weza kuzungumza kitu cha aina
yoyote hakika unaweza ukafia katika mikono yetu”
Mmoja wa askari wapelelezi aliye ingia kwenye
chumba cha mahojiano kumuhoji Briton huku
akiendelea kumzunguka Briton aliye kalishwa
kwenye kiti huku miguu na mikono yake ikiwa
imefungwa pingu.
Briton hakuzungumza kitu cha aina yoyote tangu
akamatwe kwenye chumba hicho, macho yake
makali na yaliyo jaa dharau akaendelea kumtazama
mpelelezi huyo ambaye mara kadhaa alimuhoji
maswali ambayo hakuwa tayari kuweza kujibu.
“Ninaimani wapo watu ambao wapo nyuma yako si
ndio, hembu niambie ni kina nani hao ili niweze
kuwatambua”
“Nina weza kukuamini?”
Briton alimuuliza mpelelezi huyo ambaye kwa
haraka akaweza kukaa kwenye kiti kilichopo mbele
ya meza kumsikiliza Briton aliye patiwa matesi
makali ila hakuweza kuzungumza kitu cha aina
yoyote.
“Ndio kwa maana mimi siwezi kuwa kinyume na
wewe, na ukiniambia ukweli basi nina uhakika
nitakuwa upande wako”
“Kwa maana sisi tunahitaji watu ambao wapo
nyuma yako, au unahitaji kusema kwamba waziri
Eddy ndio alikuwa kiongozi wenu mkubwa au?”
Briton akatabasamu na kucheka kichoko kidogo
cha dharau, akakitazama chumba chote na kukuta
kameza mbili za ulinzi zikiwa katika kona tofauti
katika chumba hicho, kwa uzoefu wake akatambua
kabisa mazungumzo hayo yanarekodiwa na
kutazamwa na watu wengi, waliopo nyuma ya kioo
kikubwa ambacho hakionyeshi nje ila watu wa nje
wanaweza kuona ndani.
“Kuna mtu nahitaji kuonana naye hapa hapa ndani
ya Tanzania”
Maneno hayo ya Briton alipo kuwa akiyazungumza
Bwana Mgwira naye ndio alikuwa amefika kwenye
ofisi ya kusikilizia mahojianop hayo yanayo fanywa
upande wa pili wa chumba hicho.
“Ni nani huyo?”
Mapigo ya bwana Mgwira yakaanza kumuenda
mbio, kwani hakujua ni nani ambaye Biton
anakwenda kumtaja, na endapo atakuwa ni yeye
basi siri ya D.F.E inaweza kufichuka kwani yeye
naye anaweza kufanyiwa mahojiano ili kuzungumza
ana mahusiano gani na Briton.
Briton akakaa kwa muda huku akianza kukumbuka
baadhi ya matukio yaliyo tokea kipindi cha nyuma
akiwa ndio anaingia kwenye kundi la Al-Shabab
akiwa kijana mdogo, akamkumbuka jinsi alivyo
weza kuishi na Shamsa, hadi wakapotezana
kwenye moja ya kazi ambayo walipewa kwenda
kuvamia moja ya nyumba iliyo sadikika kwamba
ina watu wanao tafutwa na bosi wao katika kipindi
hicho. Akakumbuka pia jinsi jana usiku alivyo weza
kukutana na Shamsa anaye amini ni wake.
Akakumbuka jinsi Shamsa alivyo muita Eddy baba,
taratibu picha ikaanza kumjia kichwani mwake na
kuamini kwamba mtu aliye weza kuishi na Shamsa
kwa kipindi chote hicho ni Eddy.
Briton akashusha pumzi nyingi huku akimtazama
mpelelezi huyo, taratibu akajinyoosha, huku
maumivu makali ya kipigo alicho kipata
yakiendelea kuutesa mwili wake.
“Nahitaji kuonana na binti mmoja hivi, yupo ndani
ya Tanzania”
Bwana Mgwira akashusha pumzi nyingi kusikilizia
ni nani huyo binti.
“Anaitwa nani?”
“Shamsa”
“Shamsa……Ila ndani ya Tanzania wasichana waoa
itwa Shamsa ni wengi?”
“Nalijua hilo, ila nahitaji kuonana na huyo la sivyo
hakuna chochote ambacho munaweza kukijua
kuhusiana na mimi, mutanipiga hadi nife, ila sinto
kuwa tayari kuzungumza chochote”
Briton akakaa kimya na kuwaahia kazi nzito
wapelelezi walio pewa kazi ya kuweza kumpeleleza
na kuweza kupata ukweli kuhusiana na kazi yake
ya kigaidi anayo ifanya.
***
“What……..!!!!?(Nini…………..!!!!?)
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa katika hali
ya mshangao
“Ndio muheshimiwa wanajeshi wote wameuawa”
“Wameuawa kivipi?”
Raisi Praygod alibabaika huku akiwa ndani ya gari
akielekea ikulu akitokea hospitali ya Taifa.
“Hata sisi wenyewe hatufahamu muheshimiwa”
“Dereva geuza gari tunaelekea nyumbani kwa
waziri Eddy”
Raisi Praygod alizungumza huku akiikata simu
hiyo, kichwani mwake alihisi kuchanganyikiwa.
Mawasiliano yakafanywa kwa madereva wote
walipo kwenye msafara wa raisi, gari zote nane
zilizo ongezeka baada ya walinzi wengine
kugundua raisi aliondoka ikulu kisiri pasipo wao
kujua, zikageuzwa kwa mtindo ulio wafanya
wananchi wengi walio kuwa karibu na barabara
hiyo kushangaa, kwani ziligeuzwa kwa mwendo wa
kasi sana.
Ving’ora vya gari zote zilizo tangulia mbele
vikawashwa, madereva wote wagari zilizopo
barabara ambayo raisi Praygod anapita,
walizisogeza pembeni gari zoa, ikiwa ni amri
endapo msafara wa raisi unapo pita.
Haikumchukua muda sana Raisi Praygod akafika
kwenye jumba la Eddy akiwa na msafara wake na
walinzi wakutosha, waandishi wa hhabari pamoja
na wananchi walio kuwa karibu na eneo la jumba
hilo waliweza kukushanyika nje ya geti kubwa
wakishuhudia tukio jengine ambalo hapakuwa na
aliye elewa ni kitu gani kilicho tokea, huku baadhi
yao walio hojiwa na waandishi wa habari walidai
kwamba walisikia milio ya risasi majira ya alfajiri,
ila hawakuweza kutoka kohofia maisha yao, kwani
tukio la jana tu liliweza kuwaogopesha kila mmoja
aliye sikia au kuadisiwa.
Raisi Praygod moja kwa moja akapelekwa kwenye
maiti zilizo funikwa za wanajeshi walio weza
kupoteza maisha, ikafuniliwa maiti moja iliyo weza
kutolewa koromeo, Raisi Praygod akajikuta
akifumba macho pasipo kupenda kwa maana maiti
hiyo inatisha sana.
“Muheshimiwa hadi sasa hivi hatujaweza kujua ni
nani aliye weza kufanya tukio hili kwa maana
hapakuwa na alama yoyote ya risasi kwenye miili
ya maiti zote”
“Hakikisheni munatafuta na kutambua ni nani aliye
weza kuhusika na haya mauaji”
“Sawa muheshimiwa”
***
Habari za kifo cha waziri Eddy, zikapokelewa kwa
mitazamo tofauti toafauti na wananchi wa Tanzania,
wengine waliweza kushangilia kwa kifo hicho
kilicho dhibitishwa na mchunguzi mkuu wa serikali
na kutangazwa hadharani kupitia vyombo vya
hatai.
Wananchi wengine waliweza kuipokea taarifa hiyo
kwa unyonge haswa wale wana mtambua waziri
Eddy. Baadhi yao wakabaki na maswali mengi
wakijiuliza ni kwanini kiongozi huyo aliweza
kufanya tukio hilo la kuwaangamiza wananchi
wasio kuwa na hatia. Shamsa akawa ni miongoni
mwa wananchi walio weza kushuhudia taarifa hiyo
kwenye sehemu hiyo aliyo kaa, yenye Tv ndogo
kwa ajili ya watu wanao jipumzisha katika eneo
hilo.
Shamsa akajikuta akipata nguvu na kunyanyuka,
kijana aliye kuwa akimsaidia tayari alisha ondoka,
baada ya kuitwa na baba yake walio fika kutazama
dada yake aliye jeruhiwa katika tukio la kigaidi
Mlimani City. Akaanza kutembea kuelekea kwenye
chumba cha kutazama maiti, akajitahidi kutembea
hivyo hiyo, akijkaza kikike. Alipo hisi kuchoka,
alitafuta sehemu akapumzika kwa dakika kadhaa
kisha akaendelea na safari yake hiyo hadi
akafanikiwa kufika kwenye jengo hilo la kuhifadhia
maiti, akakuta watu wengi wakiwa wamekaa
kwenye eneo hilo, baadhi yao wakimwagikwa na
machozi akatambua kwamba hao ni miongoni mwa
watu walio ondokewa na ndugu zao.
Ulinzi mkali wa polisi ulizidi kuimarishwa eneo
zima eneo hilo la jengo la kuhifadhia maiti,
hususani katika chumba alicho lazwa Lukuma
ambaye anasidikika kuwa ndio Eddy.
“Samahani dokta”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya kinyonge sana.
“Bila samahani?”
“Nahitaji kuona maiti ya baba yangu?”
“Kusema kweli mimi sihusiki na sehemu hii, kwa
kukusaidia nenda pale kwenye dirisha la mapokezi
ukizungumza utaweza kuonyeshwa maiti yako”
Daktari huyo baada ya kuzungumza hivyo
akaondoka zake na kumuacha Shamsa akitazana
kundi kubwa la watu walio kusanyika kwenye
dirisha hilo, kila mmoja akijaribu kujua kama
ndugu yake yupo kwenye jumba hilo. Akajikongoja
hadi kwenye dirisha hilo, akasimama kwa muda
kutazama kama anaweza kupata msaada wa
kuuliza jina la Eddy, lengo lake kubwa ni
kuhakikisha kwamba anamuona Eddy aliye fariki,
kwa bahati nzuri akafanikiwa kupata kijiupenyo
akafanikiwa kufika kwa dirishani.
“Namuulizia Eddy Godwin”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya chini
“Nani hembu zungumza kwa sauti ya juu usilete
lete mapozi”
Jamaa huyo aliye onekena kuchoshwa na kuti
kubwa la watu alizungumza kwa hasira
“EDDY GODWIN”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya juu, na
kumfanya jamaa huyo kuanza kuchambua faili lake
kwa haraka, akihisi binti huyo atakuwa anamuulizia
Eddy mwengine kwani Eddy anaye mfahamu yeye
anahisi ahusiani na binti huyu mwenye asili ya
kiarabu.
“Binti hakuna jina kama hilo”
“Baba yangu ni waziri aliye kufa Eddy Godwin,
unataka kusema humjui wewe”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya ukali huku
machozi yakimlenga lenga, na mkono wake mmoja
akiwa amejishika tumboni mwake akijaribu
kuyazuia maumivu makali anayo yapata. Baadhi ya
watu waliyo yasikia maneno ya Shamsa wakajikuta
wakimtazama marambili mbili, wengine wakianza
kunong’onezana na mmoja wao akaropoka
“Jamani huyu ni mototo wa gaidi”
Kitendo cha jamaa huyo kuzungumza hivyo
akamfwata Shamsa kwa nyuma na kumsukumia
pembeni, na kuanza kuzua vurumai, iliyo wabidi
polisi kuweza kuwahi katika eneo la tukio na
kumchomoa Shamsa, aliye anza kushambuliwa
kwa makofi na mangumi na wananchi hao walio
kuwa na hasira dhidi ya Eddy Godwin aliye waulia
ndugu zao.
***
“MAUAJI MENGINE YAKUTISHA YATOKEA KWENYE
JUMBA LA MAREHEMU WAZIRI EDDY GODWIN”
Taarifa hiyo ikamfanya Rahab kunyanyuka kitandani
haraka haraka na kukaa kitako, akachukua romoti
ya tv hiyo iliyomo chumbani kwake na kuiwasha,
akazidi kuikodolea macho Tv hiyo na kutazama
baadhi ya maiti nyingi zikiwa zimefunika kwenye
eneo la kiwanja katika jumba hilo analo lifahamu
vizuri sana.
“Eddy”
Rahab kwa haraka, akaanza kuitafuta simu yake,
akaikuta chini ya mto, akaikuta ikiwa imezima
akaiwasha, kitu cha kwanza kuweza kufanya ni
kumpigia Samson na kumuuliza ni kitu gani kilicho
tokea, Simu ya Samson ikaita kwa muda mrefu na
kukata, akarudia kupiga tena, ikaita na kukata.
Akajaribu kuipiga namba ya Eddy, ila nayo haikuita,
akaitazama saa iliyomo ndani ya simu yake,
ikamuonyesha ni saa nne asubuhi. Kwa haraka
akashuka kitandani na kusimama wima akiwa
amechanganyikiwa, akajaribu kufumba macho yake
kuvuta hisia zake kutambu ni wapi alipo Eddy, ila
hakuweza kuona kitu cha aina yoyote.
“INASADIKIKA MUUAJI WA WANAJESHI HUO NI
KIUMBE AMBACHO SI CHAKAWAIDA, NA UPELELEZI
UNAENDELEA KUFANYIKA ILI KUMPATA MUUAJI”
Maneno ya muandishi wa habari huyo yakazidi
kumchanganya Rahab, akajaribu tena kuvuta hisia
zake kujua ni wapi alipo Eddy, kidogo picha
ikaanza kumjia kwenye hisia zake, akaona jinsi
Eddy alivyo weza kutoka kwenye jumba lake akiwa
ameingizwa kwenye gari na Samson, jinsi Rahab
anavyo jaribu kuvuta hisia zake ndivyo jinsi damu
zilivyo anza kumtoka kwenye pua zake. Hakulijali
la pua kuweza kutoka damu, akazidi kuvuta hisia
zake, akaona jinsi gari aliyo panda Eddy ilivyo
kuwa ikieelekea nje ya mkoa wa Dar es Salaam, ila
gafla picha hiyo ikakata kwenye hisia zake.
Rahab akajitahidi tena na tena kuvuta hisia zake ila
hakuweza kuona kitu chochote, akajaribu kumtafuta
Samson kwenye hisia zake ila hakuweza kuona
kitu chochote. Rahab machozi yakaanza kumlenga
lenga, kwani tayari alihisi hali ya hatari imetokea
kwa Eddy na Samso. Akajaribu tena kuvuta hisia
zake, huku nguvu za mwili zikiwa zimemuishia
kabisa. Picha ya mwisho kuweza kuiona ni gari
kubwa aina ya Scania ilivyo weza kuivaa gari aliyo
panda Eddy na Samson na kusambaratika vipande
vipande na kulipuka na watu wake waliomo ndani
ya gari hilo
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 36 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (36) (Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author) WEBSITE……………………
……… www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Rahab akajitahidi tena na tena kuvuta hisia zake ila
hakuweza kuona kitu chochote, akajaribu kumtafuta
Samson kwenye hisia zake ila hakuweza kuona
kitu chochote. Rahab machozi yakaanza kumlenga
lenga, kwani tayari alihisi hali ya hatari imetokea
kwa Eddy na Samso. Akajaribu tena kuvuta hisia
zake, huku nguvu za mwili zikiwa zimemuishia
kabisa. Picha ya mwisho kuweza kuiona ni gari
kubwa aina ya Scania ilivyo weza kuivaa gari aliyo
panda Eddy na Samson na kusambaratika vipande
vipande na kulipuka na watu wake waliomo ndani
ya gari hilo
ENDELEA
Rahab akafumbu macho yake huku akihema sana,
kwa haraka akaelekea bafuni, akanawa uso wake,
akarudi chumbani na kufuta matone yote ya damu,
kwa haraka akafungua kabati na kuhukua suruali
iliyo mbana kiasi kisha akachukua na tisheti iliyo
mbana na juu akavaa kikoti. Alipo hakikisha yupo
tayari, nywele zake zinazo fika mgongoni,
akazikunja na kuzibana na kibanio. Akafungua droo
yake, akatoa bastola yenye magazine yenye risasi
za kutosha. Akaichomeka kwa nyuma maeneo ya
kiunoni mwake kisha akavaa gloves nyeusi
mikononi mwake, akamalizia na kuvaa kofia nyeusi
pamoja na miwani kisha akatoka chumbani kwake.
Wafanyakazi wa ndani wakabaki kumshangaa bosi
wao jinsi alivyo vaa kwani ni mara chache sana
kuweza kuvaa hivyo. Akatoa simu yake na
kumpigia Priscar.
“Andaa gari tunatoka” “Sawa madam” Rahab moja
kwa moja akaelekea nje akiwa katika mwendo wa
kujiamini, kila mlinzi aliye pishana naye alibaki
kumshanga mke wa raisi imekuaje leo anatoka
hivyo. Akafika kwenye maegesho na kumkuta
Prisca akiwa ndani ya gari aina ya Aud Q5. Rahab
akaingia na kukaa siti ya mbele tofauti na mazoea
ya siku zote kwani anatakiwa kukaa siti ya nyuma
kama kiongozi.
“Madam mbona leo umekaa mbele?” “Endesha gari
kwani kuna tatizo?” “Haha hapana” Prisca
akawasha gari na kuondoka taratibu pasipo kujua
ni wapi anapaswa kuelekea.
***
Katika barabara itokayo Dar es Salaam, kwenda
mikoa ya Arusha na Tanga, katika kijiji cha Mkata,
ajali moja mbaya na kubwa ya gari ndogo aina ya
Toyota land cruser, ikiwa imegongana uso kwa uso
na gari kubwa aina ya Scania lililo beba mafuta ya
petrol na kusababisha mlipuko mkubwa ulio
pelekea gari zote mbili kuteketea kwa moto. Gari
za zima moto pamoja na askari wa usalama
barabarani na wanao tuliza ghasia, wakafika eneo
la tukio wakiwa makini katika kudhibiti hatari
yoyote ambayo itajitokeza.
Kila aliye shuhudia ajali hiyo alizungumza chake
kutokana na alicho weza kukiona wakati ajali
ikijitokeza, wapo walio dai kwamba ni uzembe wa
dereva aliye kuwa anaendesha gari ndogo wengine
wakadai ni uzembe wa madereva wote kwani gari
zote mbili zilikuwa zikienda kwa mwendo kasi
sana.
Kikosi cha kuzima moto kikajitahidi kuifanya kazi
yake, ila hawakuweza kuwaokoa watu wali kuwemo
kwenye gari ndogo kwani moto uliweza
kuwateketeza muda mrefu sana.
Walicho weza ni kuzima moto, usiendelee kuwaka.
Priscar kwa kufwata maelekezo anayo pewa na
Rahab wakaweza kufika maeneo ya Mkata, na
kuikuta ajli hiyo, kwa haraka Rahab akashuka
kwenye gari na kujipenyeza kat5ikati ya wananchi
walio zunguka eneo hilo hadi akafanikiwa kufika
mbele ilipo angukia gari ya Samson. Machozi na
ya uchungu yakaanza kumwagika. Hakuamini
macho yake kama amewapoteza watu muhimu
sana.
“Samahani mama unatakiwa kurudi nyuma” Askari
mmoja alizungumza huku akimrudisha Rahab aliye
simama pasipo kujali moshi mwingi wa gari hiyo
unavyo muingia mwili mwake. Hakusikiliza kauli ya
askari huyo zaidi akaendelea kusimama akizidi
kuto kuamini kwamba Eddy na Samson wamefariki
dunia.
“No haiwezi kuwa” Rahab alizungumza huku
akigeuka nyuma na kumkuta Priscar akiwa
amesimama kama kazi yake inavyo mlazimu
kufanya pale mke wa raisi anapo kuwa nje ya ikulu
basi anapaswa kumlinda, labda itokee Rahab
akamzuia. Rahab akajikuta akimkumbatia Priscar
ambaye hakujua ni kwanini basi wake huyo analia,
taratibu akampitisha katikati ya watu wanao
mshangaa, kisha akampeleka ndani ya gari.
“Bosi kuna tatizo gani?” “Eddy na Samson
wamefariki”
“Weeeee…………………!!!!” Ikambidi Priscar kushuka
naye kwenda kutazama kwenye gari inayo
malizikia kuteketea kwa moto kama ni kweli
Samson wake, aliye tokea kuanza kumpenda ndio
anateketea kwa moto, Priscar na yeye akajajikuta
akishindwa kujizuia. Machozi yakaanza kumwagika,
ikabidi kumfwata askari mmoja na kumuuliza.
“Kaka ina maana watu wote wamekufa ndani ya hii
gari ndogo?” “Ndio dada, hatukuweza kuwaokoa,
kwani wewe ni nani kwao?” Askari hutyo
aliongezea swali baada ya kumuona Priscar
akimwagikwa na machozi huku akijikaza tu
kuzungumza.
“Ni mume wangu?”
“Hembu ngoja” Askari huyo akamfwata mwenzake
aliye kuwa amesimama pembeni akipima pima
baadhi ya mambop barabarani. Mwenzake huyo
akampa kimfuko cheupe chenye kitu ndani kisha
akarudi alipo simama Priscar. Askari huyo aliye
onekena kumuhurumia Priscar, akatoa simu iliyo
pasuka kioo kidogo ila baodo inafanya kazi.
“Na hii si ni simu yake?”
Alizungumza huku akimpatia Priscar simu hiyo,
Priscar akatingisha kichwa kwamba ni ya Samson,
kwani siku walipokuwa msituni aliweza kumuona
nayo simu hiyo. Na ushahidi mwingine waliweza
kupiga picha ya pamoja kupitia simu hiyo. Katika
kuichunguza akakuta missed call, za bosi wake
ikionekana Rahab alimpigia Samson.
“Hiyo simu iliokotwa na mwananchi, mita chache
kutoka eneo la ajali, alikuwa mwaminifu na
kutukabidhi sisi” “Asante afande” “Ila itabidi
kufanya utaratibu wa kutoa mifupa ndani ya gari,
kwa ajili ya kwenda kuzika” Maneno ya askari huyo
yakamfanya Priscar kuondoka huku akiangua kilio,
ukakamavu wake alio upata katika jeshi,
haumkusaidia kitu kuweza kujizuia kumwaga
machozi kwa mwanaume aliye tokea kumpenda,
isitoshe hakuweza kumueleza kitu kama hicho
kwamba anampenda hadi mauti yalipo weza
kumkuta.
***
Video ya jinsi Briton, Lukuma na mtu aliye valia
mavazi meusi pamoja na kofia kofia lililo mfunika
kichwani mwake, ikafikishwa mbele mkuu wa
kikosi cha Al-Shabab bwana Abdulah Mohamed,
akiwa na kijana wake msaidizi wa kikosi hicho
wakaanza kuitazama video hiyo kwa umakini wa
hali ya juu.
Mara kidogo bwana Abdulah Mohamed akastuka,
kumuona binti anaye mtambua vizuri na ni binti
aliye weza kulelewa na marehemu kaka yake, aliye
kuwa kiongozi wao, baada ya kaka yake kufariki
akashikilia yeye madaraka.
“Huyu si Shamsa?” Alimuuliza msaidizi wake huku
wakiisimamsha video hiyo, katika sehemu ambayo
Shamsa aliweza kuingilia ugomvi huo akionekana
kupambana na Lukuman.
“Ndio yeye bosi” “Ohhh mwanangu, fanya fanya
utume vijana wajue ni wapi alipo mwanangu huyu”
Bwana Abdulah Mohamed alizungumza huku akiwa
na furaha moyoni mwake, kwani kazi moja ambayo
marehemu kaka yake alimuachia ni kuweza
kuhakikisha kwamba ana mtafura Shamsa popote
alipo, ili miaka ya baadae Shamsa anatakiwa
kuridhi kiti chao cha uongozi. Japo Shamsa
hakuwa ni mtoto wa kumzaa wa kaka yake. Ila
alimchukulia kama mwanaye na mambo mengi na
siri nyingi sana aliweza kuambiwa na kiongozi
wake huyo kuhusiana na kikundi hicho chenye
makazi yake makuu mjini Mogadishu Somalia.
“Muheshimiwa tumepata ripoti kwamba yupo
Tanzania”
“Tuma viajan makini, na wahakikishe wanarudi pia
na Briton hapa” Bwana Mohamed alizungumza
huku akiendelea kuitazama video hiyo, alipo ona
jinsi Shamsa alivyo pigwa kipigo kikali na
Lukuman, aliyafumba macho yake na kujihisi
maumivu makali, moyoni mwake. Ila alipo ona
Briton anamvaa, Lukuman na kuanza
kumshambulia basi akaamini kwamba Briton
amefanya jambo sahihi kumuokoa kiongozi wao
huyo mtarajiwa, wanaye mtafura miaka kwa miaka.
Kundi la vijana wanne walio kamilika katika nyanja
zote kuanzia kupambana na uytumiaji wa silaha
wakapewa picha ya Shamsa, na kuihidiawa
aendapo watamleta kila mmoja ataoewa donge
nono la dola za kimarekani laki moja, na agizo
jengine wakaambiwa wahakikishe wanamrudisha
Briton nyumbani na aendelea kutumikia mikono ya
serikali wa Tanzania, pasipo kujua kiongozi mwake
mzee Godwin ameagiza kija huyo auawe akiwa
ndani ya mikono ya serikali ili asitoe siri ya kikosi
chao,
***
Taarifa ya binti wa Eddy, Shamsa kuokolewa katika
miono ya wananchi walio mshambulia kwa hasira,
wakimshutumu ni mtoto wa gaidi, zikaifikia ofisi ya
upelelezi, walio kuwa wameanza msako wa
kufwatilia majina yote ya wasichana wanao itwa
Shamsa, wenye asili ya kisomali nchini Tanzania.
Wakiamini ya kwamba watakuwa ni miongoni watu
wanao husika na kikosi cha Eddy. Ila walipo sikia
kuna mtoto wa Eddy yupo mikononi mwa Polisi na
yeye anaitwa Shamsa, wakapiga picha kwamba
Eddy ndio aliye kuwa kiongozi wa kundi hilo, basi
ikawawia urahisi kuweza kutambua Shamsa huyo
ndio anye hitajika na gaidi waliye mshikilia.
Shamsa akashangaa kuona ulinzi wa polisi
ukingezeka katika kitanda alicho lazwa akiendelea
kupatiwa matibabu ya muhimu na madaktari.
“Eti dada kuna nini?” Shamsa alimuuliza askari
mmoja wa kile aliye simama kando yake akiwa na
bastola kiunoni mwake.
“Hakuna chochote mdongo wangu, ila tunapaswa
kukulinda tu”
“Kwani kuna tatizo juu yangu?” “Hapana, ila kuna
haja ya sisi kuweza kukulinda wewe kwani tuna
amini kuna watu wabaya wanaweza kukufwatilia”
“Ahaa sawa” Shamsa hakutilia mashaka sana,
kwani aliamini ni kweli watu wabaya wanaweza
kumvamia na kuitoa roho yake. Matibabu ya
haraka yakaendelea kufanyika huku akichomwa
baadhi ya sindano za kukata maumivu, ili aweze
kwenda kwenye ofisi za usalama wa taifa
kukutanishwa na gaidi walio mkamata.
Ndani ya masaa mawili, Shamsa akajihisi unafuu
mkubwa, maumivu yote aliyo kuwa akiyahisi
tumboni mwake, yakakatika. Akamueleza nesi aliye
kuwa akimuhudumia kwamba yeye yupo salama tu
na anahitaji kuweza kuondoka hapo hospitalini.
Kutokana nesi huyo anafahamu kinacho endelea,
akamuita daktari na kumruhusu Shamsa kuweza
kutoka katika hospitali, polisi zaidi ya sita
wakaongozana na Shamsa kuelekea maeneo ya
maegesho ya magari kwa madai kwamba
wanamlinda, ila asivamiwe, ila ukweli tayari amsha
anza kuhisiwa kama gaidi kutokana baba yake
Eddy amefanya tukio la kigaidi ambalo kila mmoja
ndani ya nje ya Tanzania ameweza kulishuhudia
kwa macho yake.
“Naweza kumuona baba yangu?”
“Hapana kwa muda huu wananchi wakiweza
kukuona wanaweza kuanzisha vurugu, mwili wa
baba yako ukisha andaliwa basi utaonyeshwa”
Shamsa akatokea kumuamini askari huyo, wa kike
ambaye kwa mara nyingi aliweza kumuuliza
maswali na akayajibu kiufasaha kabisa. Waandishi
wa habari walipo waona Shamsa na askari wakanza
kukimbilia eneo walipo ili kupata japo habari
kuhusiana na binti huyo ambaye wananchi chupu
chupu wamtoe roho wakidai kwamba ni mtoto wa
gaidi. Askari kwa haraka wakamuingiza Shamsa
ndani ya gari na kuondoka naye katika eneo la
hospitali wakiwaacha waandishi wa habari wakipiga
piga picha gari hilo la polisi.
“Munanipeleka wapi?”
“Sehemu ambayo ni salama kwa maisha yako”
“Nipelekeni nyumbani kwanza”
“Hauwezi kwenda kutokana kuna mauaji ya kikatili
yametokea nyumbani kwenu, walipelekwa
wanajeshi kulinda ila wote waliuawa kwa hiyo
inavyo onekana watu hao wana kutafuta wewe”
Kabla Shamsa hajazungumza chochote, askari
huyo akatoa simu yake mfukoni na kumuwekea
Shamsa tukio lililo tokea nyumbani kwao majira ya
asubuhi.
Shamsa akajikuta akishika mdomo kwa mshangao,
kwani maiti nyingi za wanajeshi zimelala chini
zikiwa zimeuawa vibaya sana. Hofu na mashaaka
vikaanza kumtawala, hapo ndipo akaamini kwamba
anapaswa kulindwa na askari wote hao.
Wakamfikisha Shamsa kwenye jengo kuu la ofisi za
usalama wa taifa, wakamkabidhisha kwa kikosi
hicho kisha wao wakaondoka. Shamsa moja kwa
moja akapelekwa kwenye chumba alicho andaliwa
na kikosi hicho, chenye kila huduma kama chumba
cha kisasa.
“Naitwa Pudensia, nitakuwa muhudumu wako kwa
kila jambo ambalo utalihitaji humu chumbani
kwako” Mmama huyo alijitambulisha kwa Shamsa
huku akiwa ameachia tabasamu pana akimtazama
Shamsa.
“Asante” “Umekula?”
“Hapana”
“Utahitaji nikuletee nini?” “Sambusa na chai” “Za
nyama au viazi?” “Nyama” “Ok subiria kidogo”
Mwana mama Pudensia akatoka ndani ya chumba
hicho, Shamsa akabaki akiwa na mawazo mengi ni
kwanini watu hao wabaya wanamfwatilia yeye.
Swali jengine lililo mjia kichwani mwake ni kwanini
Eddy alikwenda kuteka Mlimani City wakatyi
anajitambua ya kwamba yeye ni kiongozi anaye
tazamwa na watu wengi. Machozi taratibu
yakaanza kumwagika kwani hakuamini kwamba
Eddy ndio tayari amesha fariki na kumuacha akiwa
peke yake.
“Eddy kwa nini lakini ulifanya hivyo?” Shamsa
alizidi kulia huku akimlalamikia Eddy kwa maamuzi
ambayo aliyachukua na kumpelekea kufa.
Mwanamama huyo akarejea akiwa amshikilia,
sahani nyenye sambusa nne, chupa ya chai
pamoja na kikombe. Akamuandalia Shamsa kila
kitu na kumkaribsha kula. Shamsa taratibu
akaanza kula huku kichwa chake kikiwa
kimetawaliwa na mawazo mengi sana. Hakujua ni
nini hatima ya maisha yake kwa wakati huu.
Hata ladha ya chai hiyo hakuweza kuipata
mdomoni mwake, akajilazimisha kuinywa hivyo
hivyo ili mradi aimalize chai hiyo, kwani njaa
inamsumbua tumboni mwake. Alipo maliza
Pudensia akamuomba waongozane hadi kwenye
moja ya chumba ambacho kuna mtu anahitaji
kumuona na kumuambia maagizo aliyo pewa na
Eddy. Kwa ujanja alio utumia Pudensia ukamfanya
Shamsa kunyanyuka kwa haraka na kumuomba
waongozane kwenye chumba hicho huku akiwa na
shauku kubwa ya kuweza kumuona mtu huyo ni
nani.
Wakafika katika chumba hicho akaingia na
Pudensia, Shamsa akamkuta gaidi ambaye aliweza
kumuona akipambana na mtua aliye kuja
kuwaokoa. Briton alipo muona Shamsa
akatabasamu, akiamini kwamba mpenzi wake huyo
anaweza kumkumbuka.
“Shamsa ni muda mrefu atuja onana” Briton
alizungumza baada ya Pudensia kutoka ndani ya
chumba hicho.
“Wewe ni nani?” Shamsa alizungumza huku akikaa
kwenye kiti wakitenganishwa katikati yao na meza.
“Ina maana umenisahau Shamsa wangu”
Wapelelezi waliopo nje ya chumba hicho walizidi
kuyafwatilia mazungumzo hayo kwa vinasa sauti
walivyo weza kuvifunga ndani ya chumba hicho.
“Siwezi kumfahamu mtu gaidi kama wewe.
Niambieni ni nini alicho kuambia baba yangu
Eddy”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku
akimwagikwa na machozi, Briton kwa dharau
akatabasamu kisha akajivuta kidogo kwenye kiti na
kumtazama usoni Shamsa
“Baba……..baba gaidi kama Eddy. Ohoooo mimi
ndio niliye weza kumuua, sahamani kwa hilo”
Shamsa akasimama kwa hasira na kumrukia Briton
na wote wakaanguka chini na kuanaza
kumshindilia ngumi za hasira Briton aliye fungwa
pingu miguuni na mikononi.
ITAENDELEA USIKOSE SEHEMU YA 37YA SIMUHILI
 
SORRY MADAM (37)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Wapelelezi waliopo nje ya chumba hicho walizidi
kuyafwatilia mazungumzo hayo kwa vinasa sauti
walivyo weza kuvifunga ndani ya chumba hicho.
“Siwezi kumfahamu mtu gaidi kama wewe.
Niambieni ni nini alicho kuambia baba yangu
Eddy”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku
akimwagikwa na machozi, Briton kwa dharau
akatabasamu kisha akajivuta kidogo kwenye kiti na
kumtazama usoni Shamsa
“Baba……..baba gaidi kama Eddy. Ohoooo mimi
ndio niliye weza kumuua, sahamani kwa hilo”
Shamsa akasimama kwa hasira na kumrukia Briton
na wote wakaanguka chini na kuanaza
kumshindilia ngumi za hasira Briton aliye fungwa
pingu miguuni na mikononi.
ENDELEA
Wapeleezi wawili wa kike wakaingia ndani ya
chumba hicho na kumtoa Shamsa juu ya mwili wa
Briton anaye zidi kupigika na binti huyo.
Ikawalazimu kumtoa kabisa nje ya chumba hicho
na kumpeleka katika chumba chake walicho mpatia
na chenye ulinzi mkali sana.
“Mwanangu mbona umekuwa hivyo?”
Mama Pudensia alizungumza huku akimtazama
Shamsa machoni anaye mwagikwa na machozi
akionekana dhahiri kwamba ana hasira kali iliyo
mpanda, kwani kifua chake kiliweza kutanuka kiasi,
mishipa yake ya shingo inaoenekana vizuri, uzuri
wa sura yake umebadilika sana.
Mambo yote yakiwa yanaendelea, Bwana Mgwira
aliweza kushuhudia tukio hilo akiwa katika chumba
cha kusikilizia mazungumzo yaliyo kuwa
yanafanywa kwenye chumba hicho.
‘Hakikisha hii siku haipiti lazima awe amesha kufa’
Bwana Mgira alimtumia meseji mmoja wa
wapelelezi alio kuwa nao ndani ya chumba hicho
kisha yeye akatoka na kuondoka zake.
***
Kitu kilicho zidi kumuumiza kichwa Raisi Praygod
ni wapi alipo Eddy, ambaye wananchi wengi wote
wanafahamu kiongozi huyo amefariki. Anashindwa
hata kuwatangazia wananchi kwamba Eddy ndio
amehusika na vifo vya wanajeshi hao.
“Sasa hapatunafanyaje?”
Raisi Praygod alimuuliza mshauri wake bwana
Mgwira, wakiwa ndani ya ofisi ya yake.
“Muheshimiwa hapo kusema kweli hatuwezi
kufanya chochote zaidi ya kumtafuta kimya kimya,
pasipo wananchi kuweza kulitambua hilo. Pia
itakuwa ni nafasi ya kipekee kuweza kumuua,
pasipo watu wengine kuelewa”
“Etieee?”
“Ndio muheshimiwa, kwa maana wananchi wanajua
kwamba amekufa. Tunacho kifanya mwili wa yule
mshenzi kule Muhimbili, unazikwa na jeshi kwa
madai kwamba ni gaidi, hakuna muandishi wa
habari atakaye karibia jeneza na kuipiga picha sura
ya Eddy”
“Lakini tukiwabana waandishi wa habari wasifanya
kazi yao, kunaweza kuzuka mambo ya kitata.
Tuwape nafasi tuone itakavyo kuwa”
“Sawa muheshimiwa. Tuachane na hayo, vipi
uchaguzi ndio mwaka huu, umejipangaje kaka”
“Kama kawaidia, miaka mitano ijayo ipo mikononi
mwangu”
Raisi Praygod alizungumza kwa kujiamini, kwani
anatambua kwamba wananchi wengi wa Tanzania
wanamchukulia kwama kiongozi imara na sahihi
katika maisha yao, ila nyuma ya pazia ni kiongozi
katili asiye paswa kushikilia hata hiyo miaka
mitano ya awamu ya pili.
***
“Priscar twende kule kwenye handaki”
“Sawa mdama”
Priscar akazidi kujikaza kuliendesha gai hilo, kwani
wote wawili kila mmoja ana uchungu wake kwa
upande wake, yeye anamlilia Samson, ila bosi
wake anamlilia Eddy. Kwa mwendao wa lisaa moja
na nusu wakawa wamefanikiwa kufika kwenye
handaki ambalo ndipo yalipo kuwa maficho ya
Rahab na kikundi cha wezake walio kuwa wakidili
na maswala ya ujambazi, wa kuua watu kazi hiyo
ikiwa ni amri kutoka kwa raisi Praygod wao
wakiifanya pasipo kujua kwamba ni kazi ya
kiserikali,
Wakashuka wote wawili, huku Rahab akionekana
kuwa na Shahuku kubwa ya kutaka kwenda
kumuona Eddy akiwa ndani ya handaki hilo.
Wakafika ndani, hapakuwa na mtu wa aina yoyote,
Rahab akafungua kila chumba kuhakikisha kwamba
ni kweli hakuna mtu, ila ndivyo jinsi macho yake
yalivyo weza kushuhudia kwamba hakuna mtu wa
aina yoyote katika handaki hilo, akarudi eneo la
sebleni akiwa amechoka, akamkuta Priscar akiwa
ameshika karatasi nyeupe akiwa anasoma yaliyo
andikwa humo ndani huku machozi yakimwagika,
alipo maliza taratibu akamkabidhi Rahab aweze
kuisoma karatasi hiyo.
{Madam R. Samahani sana kwa kile kilicho weza
kujitokeza zidi ya wanajeshi hao, sikuwa na jinsi
zaidi ya kuweza kuwaangamiza ili wasiweze
kumdhuru mwanaume unaye mpenda kwa dhati.
Rahab natambu ya kwamba mapenzi yanauma
sana pale unapo mkosa yule umpendaye, ndivyo
jinsi hata wanafamilia wa wanajeshi nilio waua,
ndivyo wanavyo umia kwa sasa. Madama, asante
sana kwa kuweza kunipa nafasi ya pili ya kuweza
kuishi, ila nikiwa kama si binadamu wa kawaidi,
hali hii inadhidi kunidhuru siku hadi siku pale
ninapo mwaga damu za watu, huwa natamani kila
muda na kila mara niweze kumwaga damu za
watu, natambua maamuzi ninayo yachukua ni
magumu sana ten asana. Ningependa niyachukue
mimi kama mimi mwenyewe na nisimshirikishe
mtu yoyote. Nitakufa kwa ajili ya kuto ua zaidi
kwani kila nikiua ndivyo jinsi ninavyo zidi kupata
nguvu, za kuendelea kuua. Namuacha Eddy ndani
ya handaki hili ukija hakikisha hali yake inakuwa
salama kwani bila ya hivyo anaweza kufariki muda
na saa yoyote. Nakutakia kazi njema. Samson}
Ujumbe huo wa Samson ukazidi kumchanganya
Rahab akajikuta akitoka mbio ndani ya handaki hilo
na kuanza kuita kwa sauti kubwa huku na huko
akiliita jina la Eddy. Milio ya ndega pamoja na
upepo unao vuma ndani ya msitu huo havikutosha
kuweza kusikia sauiti yoyote ya mtu akiliitikia jina
lake. Uchungu mkali ukazidi kumtawala ndani ya
moyo wake, akazidi kuita jina la Eddy ila hapakuwa
na majibu ya aina yoyote. Akajaribu kuweza kuvuta
hisia, ila picha halisi ambayo inamjia kichwani ni
jinsi Samson alivyo weza kuaondoka katika eneo
hilo na gari lake, akiwa amefika eneo la barabara
kuu, kuna mzee wa makamo alimsimamisha na
kumuomba lifti, japo Samson kwa mara ya kwanza
aliweza kukataa, ila mzee huyo alijaribu kuweza
kumsihi sana kwamba anahitaji lifti. Samson
ikambidi kumfungulia mlango mzee huyo mwenye
mvi nyingi kichwani mwake, kisha akaondoka
naye. Mwendo kasi wa gari anayo iendesha
Samson kukamfanya mzee huyo kuanza
kumuomba Samson aweze kupunguza mwendo
huo, ila Samson hakuhitaji kuweza kupunguza,
zaidi na zaidi ndivyo jinsi alivyo zidi kuongeza
mwenda kasi hadi mzee huyo akaanza
kumwagikwa na machozi.
Simu ya Samson ikaanza kuita, alipo ona ni jina la
Rahab, akaiacha simu hiyo iite hadi ikakatika,
ikapigwa tena, ikaita hadi ikakatika, ikapigwa kwa
mara kadhaa ila Samon hakuweza kuipokea zaidi
alipo ona inampigia kelele, akafungua kioo cha
upande alipo kaa mzee huyo, kisha akaitupia
kwanye nyasi nyingi zilizopo kandokando ya
barabara, kurudisha macho yake barabarani,
kufumba na kufumbua gari yake ikagongana uso
kwa uso na gari la mafuta, likauburuzwa kwa urefu
fulani, huku tanki lake la mafuta likiwa limetoboka
na kumwaga mafuta. Mikwaruzo ya ya vyuma
vyuma kwenye lami, vikazalisha cheche, zilizo
ingia kwenye mafuta ya petrol na kusababisha
mlipuko mkubwa, ulio pelekea gari hiyo kurushwa
pembeni ya barabara na kuendelea kuteketea kwa
moto.
“Am sorry madam” (Samahni bibie)
Yalikuwa ni maneno ya mwisho ya Samson kabla
hajafariki kabisa. Kwa hasira Rahab akajikuta
akipiga kelele kali, hadi miti ikatingishika, huku
ndege wakipupuruka kwa woga wa sauti hiyo
ambayo hawakuwahi kuisikia. Priscar naye
akajikuta akianguka chini na kupoteza fahamu,
kwani hakuweza kustahimili mtingisho na nguvu
ambayo inazunguka ndani ya msitu huo.
***
Kwa kupitia kifaa maalumu kilichomo ndani ya
mwili wa Briton, maeneo ya mgongoni mwake,
vijana wanne wa Al-Shabab waliweza kugundua ni
jengo gani ambalo Briton yupo. Kila mmoja akiwa
na simu yake yenye uwezo ya kuonyesha alama
nyekundu sehemu Briton alipo, wakajigawa wawili
wawili, kwenda kulisoma jengo hilo kabla hata
wajafanya uvamizi majira ya usiku, kwani muda wa
sasa ni jioni.
Pasipo kustukiwa wakalichunguza gorofa hilo,
walipo hakikisha kwamba ulinzi wa eneo hilo
umeimarishwa sana, ikabidi warudi kwenye
nyumba ya wageni walipo fikizia kuendelea
kupanga mipango yao.
Kila mmoja alihakikisha anajiandaa vizuri, kwani
hawakuhitaji zoezi hilo liweze kuwachukua muda
mrefu, wakiwa katika kutazama luninga iliyomo
ndani ya chumba hicho, wakaona taarifa
ikiwaonyesha binti waliye agizwa akiwa kwenye
ulinzi mkali wa askari na kuingizwa kwenye gari.
“Watakuwa wamempelea kwapi?”
“Nahisi kwenye kituo kikubwa cha polisi”
“Una uhakika huo?”
“Ndio kwa maana hawezi kupelekwa eneo jengine
lolote zaidi ya kuwa katika kituo kikuu cha polisi”
“Basi nyinyi wawili mutaenda katika kituo cha
polisi usiku huu, kisha na sisi wa wili tutakwenda
kumkomboa bosi”
“Sawa mkuu”
Mipango ya vijana hao wanao jiamini kupita
maelezo ikakamilika vizuri majira ya saa mbili
usiku wakatoka vijana wana kwenda kwenye kituo
cha polisi, wakiwa na lengo la kwenda kuhakikisha
kwamba wanatoka na Shamsa, wakiwaancha wezao
wanao kwenda kwenye jengo la alilo shikiliwa
Briton.
***
“Mama Pude”
Shamsa aliita kwa sauti ya unyonge huku
akimgeukia mama huyo aliye kaa karibu naye
kwenye kitanda.
“Ndio mwanangu”
“Nahitaji kwenda kuzungumza na yule kijana tena”
“Una uhakika huto fanya vurugu tena?”
“Ndio ninauhakika”
“Basi ngoja”
Pudensia akapiga simu kwa mkuu wa upelelezi
kumtaarifu kwamba binti huyo anahitaji kwenda
kuzungumza na gaidi waliye mkamata. Ofisi nzima
kila mmoja akajiweza sawa kuweza kusikiliza
mazungumzo yao, kisha Shamsa akaruhusiwa
kwenda kwenye chumba cha mahojiano. Shamsa
alipo ingia kwenye chumba hicho akasimama
mlangoni kwa muda huku akimtazama Briton.
Akilini mwake akawa amepata jibu kwamba mtu
huyo kuna sehemu amesha wahi kumuona, japo
hana uhakika naye sana.
Akatazama kamera za ulinzi zilizomo ndani ya
chumba hicho, kisha taratibu akaanza kupiga hatua
kuelekea kwenye kiti kilicho wazi, akakaa na
kutazamana na Briton aliye mvimbisha maeneo ya
jichoni kwa ngumi alizo weza kumpiga.
Shamsa akaazidi kumtazama Briton, kwa umakini,
akamtazama sehemu ya kushoto chini kabisa ya
shingo yake, hapo ndipo alipo weza kumkumbuka
kwamba mtu huyu ndio aliye weza kumsaidia
maisha yake kipindi alipo kuwa anaanza kuingia
katika kambi ya Al-Shabab.
“Briton……..!!!”
Shamsa aliita kwa sauti ya chini, huku akimtazama
Broton, aliye achia tabasamu pana huku akitingisha
kichwa akimuashiria kwamba ndio yeye. Shamsa
akajikuta machozi yakimwagika, matumaini yake ya
kuweza kupata mtu anaye mjali yakaanza kufufuka
taratibu moyoni mwake. Wapelelezi wakabaki
wakishangaa, kumuona Shamsa analia, kila mmoja
akatega sikio lake huku wakitazam kupitia kioo
kikubwa kinacho watenganisha na chumba
walichopo Shamsa na Briton.
Shamsa akataka kusimama kwenda kumkumbatia
ila Briton akawahi kumshika mkono, na
kumkonyeza kumzuia asifanye hivyo kwani ni
hatari kwake.
“Kwanini lakini umefanya hivyo?”
“Nimekuja kukuchukua turudi nyumbani, Tanzania
si kwenu Shamsa”
Shamsa akabaki kimya, Briton akaipeleka mikono
yake, iliyo fungwa pingu taratibu usoni mwa
Shamsa na kuyafuta machozi yanayo mwagika
Shamsa.
“Uliniacha kipindi chote nikiwa ninateseka na
kuhangaika, sasa ni muda wa kurudi nyumbani
Sh…….”
Kabla hata Briton hajamalizia sentesi yake zaa za
jengo zima zikazima, ving’ora vya hatrari vikaanza
kulia ndani ya jengo zima, huku milio ya bunduki
kutokea nje ikianza kurindima.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 38 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (38)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Nimekuja kukuchukua turudi nyumbani, Tanzania
si kwenu Shamsa”
Shamsa akabaki kimya, Briton akaipeleka mikono
yake, iliyo fungwa pingu taratibu usoni mwa
Shamsa na kuyafuta machozi yanayo mwagika
Shamsa.
“Uliniacha kipindi chote nikiwa ninateseka na
kuhangaika, sasa ni muda wa kurudi nyumbani
Sh…….”
Kabla hata Briton hajamalizia sentesi yake zaa za
jengo zima zikazima, ving’ora vya hatrari vikaanza
kulia ndani ya jengo zima, huku milio ya bunduki
kutokea nje ikianza kurindima.
ENDELEA
Halikuwa ni jambo la kushangaza kwa Briton kwani
alitambua muda wowote na saa yoyote ni lazima
wezake watakuja kumuokoa katika jengo hilo.
Shamsa akasimama wima baada ya mlango wa
chumba walichopo kufunguliwa, walinzi watatu
walio shikilia tochi, waliingia huku wakihitaji
kuweza kuweka ulinzi kwa Briton pamoja na
Shamsa, huku walinzi wengine wakiendelea
kupambana nje na magaidi walio jipanga vilivyo
kwani silaha zao, zina uwezo wa hali ya juu huku
wakiwa wamevalia miwani ambazo zinawasiadia
kuona usiku vizuri gata kama kuna giza zito.
Kitendo cha mpelelezi mmoja kuweza kumshika
Shamsa mkono wake wa kulia, ikawa ni kosa
kubwa kwa kijana huyo kwani Shamsa, alijigeuza
haraka, kwa kutumia mkono wake wa kulia,
akamkaba kabala mpelezi huyo, bila hata ya
kumuonea huruma akamvunja shingo.
Kishindo cha mwenzo kuanguka kikawastua
wapelelezi wengine ambao wamemuweka kati
Briton, wakajaribu kumulika alipo anguka
mwenzao, wakakuta Shamsa ananyanyuka huku
akiwa amesha ichomoa bastola iliyo kuwa kiunoni
mwa mpelelezi huyo.
Risasi kadhaa zikatua vifuani mwa wapelelezi hao,
walio simama pembeni ya Briton, kisha kwa haraka
Shamsa akamfwata Briton na kumkumbatia kwa
nguvu. Wakajikuta wote wawili wakiikutanisha
midomo yao na kuanza kupeana mabusu mazito
mazito, kuto kujali kwamba wapo kwenye hatari
kubwa.
“Tafuta funguo unifungue”
Briton alizungumza huku akimuachia Shamsa, aliye
anaza kupekua mifuko ya wapelelezi hao walio
ingia mmoja baada ya mwengine. Kwa bahati nzuri
akafanikiwa kuipata funguo hiyo kwa mmoja wa
wapelelezi wanao endelea kuwamgikwa na damu
mwili ni mwake kwa risasi zilizo weza kumpata.
Kwa haraka Shamsa akamfungua Briton na kumpa
moja ya bunduki aina ya SMG, walio ingia nazo
hao wapelelezi.
“Upo vizuri?”
Shamsa alizungumza huku akiwa anatazama
mlangoni
“Ndio”
“Tutoke”
Kwa umakini mkubwa wakatembea hadi mlangoni
ambapo, Shamsa akachungulia, akashuhudia jinsi
wapelezi wakipambana na watu ambao
wamewavamia. Bila ya kupoteza muda Shamsa na
Brito wakawa na kazi moja ya kuhakikisha kwamba
wanatoka ndani ya jengo hilo na kila aliye weza
kujipendekeza kwao ni lazima mauti yatamkuta.
***
Pikipiki aina ya boksa ikasimama mbele ya kituo
kikuu cha polisi, vijana wawili walio ficha nyuso
zao kwa vinyago maalumu, wakashuka wakiwa na
bunduki aina ya AK47, pamoja na mabomu ya
kurusha kwa mkono(Granade). Shambulizi la
kwanza, wakarusha mabomu hayo ya kituo hicho,
mlipuko mzito ukatokea ndani ya kituo hicho huku
kukisikika kelele za maumivu makali kutoka kwa
watu walimo ndani ya kituo hicho. Mmoja
akasimama nje na kuanza kushambulia askari
ambao walikuwa nje, mmoja akaingia ndani ya
kituo hicho kwa lengo la kwenda kumchukua
Shamsa mahali popote alipo fichwa. Askari ambao
wengi wamejeruhiwa na bomo hilo wakajikuta
wakimaliziwa kwa risasi za gaidi huyo asiye na
huruma.
Askari walipo nje wakazidi kupambana na gaidi
ambaye amesimama nje ya kituo chao akiwa
amejibanza kwenye moja ya gari za polisi. Idadi ya
polisi wengine ikazidi kuongezeka kituoni hapo
kuongeza nguvu yta ziada. Gaidi aliye ingia ndani
ya kituo akaanza kutafuta chumba kimoja baada ya
kingine kuangalia kama Shamsa yupo, na endapo
anawakuta mahabusu, akawatwanga risasi wote
pasipo kuwa na huruma.
Gaidi aliyepo nje ya kituo kwa bahati mbaya,
akazidi nguvu na askari na kupigwa risasi nyingi
sana mwilini mwake na kupoteza maisha, askari
walio jipanga kikamilifu wakaanza kuingia ndani
kwa umakini mkubwa huku wakiwa wameshika
silaha zao. Gaidi aliyomo ndani ya kituo pasipo
kuweza kujua nje tayari mambo yamesha kuwa
mabaya, akaendelea kupita chumba kimoja hadi
kingine, ofisi moja hadi nyingine kuhakikisha
kwamba wanatoka na Shamsa, akiwa anatoka
kwenye moja ya ofisi, risasi moja ikampiga kwenye
mguu wake ulio kuwa umetangu lia mbele kwenye
kupiga hatua ya kutokea ndani ya chumba hicho.
Akarudi ndani huku akiwa analalama kwa maumivu
makali, akaichomo magazine yake na kuweka
nyingine iliyo jaa risasi, Akachomoa bomu moja
lililo salia, alilokuwa amelining’iniza kwenye jaketi
la kuzuia risasi. Akalishikilia vizuri kisha akalitupia
sehemu ambayo polisi wapo, kamanda mmoja
mrefu kwenda juu, alipo liono bomu hilo, hata
kabla halijasimama, ili kuachia mlipuko, akalipiga
teke na kulirudisha ndani ya chumba lilipo tokea.
Mlipuko mzito ukatokea ndani ya ofisi hiyo na
kumuangamiza gaidi huyo, hali ilipo anza kutulia
taratibu askari wakaanza kujongea kwenye ofisi
hiyo, wakaukuta mwili wa gaidi huyo ukiwa
umechakaa kwa mlipuko wa bomu hilo la kurusha
kwa mkono.
***
Majira ya saa tano usiku Priscar akastuka, kutoka
usingizini na kumkuta Rahab akiwa amekaa
pembeni yake. Taraibu akajinyanyua kitandani na
kutazama kila mahali ya sehemu walipo ila kidogo
kuna tofauti japo amelala juu ya kitanda.
“Madam nipo wapi?”
Rahab akamtazama kwa muda Prisacar anaye
endelea kudodosa dodosa ndani ya chumba hicho
ili mradi avute kumbukumbu na kutambua kwamba
ni wapi alipo, ila hakuweza kutambua ni sehemu
gani alipo.
“Upo sehemu salama”
“Hapa ni wapi?”
“Ni ndani ya handaki ambalo uliingia kwa mara ya
kwanza ila hakuweza kufika ndani ya chumba
chake hata kimoja”
Priscar akatazama saa yake ya mkononi kukuta
muda umekwenda sana, kwa haraka akakurupuka
na kushuka kitandani akionekana kuchanganyikiwa
.
“Madam ikulu……………..!!!!!?”
“Kuna nini?”
“Fanya twende”
Rahab akatabasamu huku akiendelea kumtazama
Priscar anaye onekana kuweweseka kwa wenge
lililo mjaa.
“Leo haturudi”
“Ahaaa madam, kibarua change kitaota nyasi
kumbuka kwamba mimi nimepewa dhamana ya
kukulinda wewe popote utakapo kwenda na
kuomba basi twende”
“Nimekuambia kwamba hakuna kuondoka,
nimekuandalia chakula sebleni twende ukale”
Rahab akatangulia kutoka ndani ya chumba hicho,
Priscar na yeye akafwata kwa nyuma huku
akionekana kuwa na maswali mengi sana juu ya
bosi wake huyo. Akakuta meza ya chakula ikiwa
imeandaliwa vizuri, huku vyakula pamoja na
vinywaji vikiwa vimo juu ya meza hiyo.
“Madam umevitolea wapi hivi vyakula?”
“Nilikwenda kuvinunua, kwa ajili yetu. Mimi
nimesha kula bado wewe”
Priscar akakaa na kuvuta meza huku akiendelea
kuvitazama vyakula hivyo, Rahab akawasha Tv
iliyomo ndani ya chumba hicho, kuangalia ni nini
kinacho endelea.
‘SHAMBULIZI KITUO KIKUU CHA POLISI CHAUA
ASKARI KUMI NA MOJA HUKU MAGAIDI WAWILI
NAO WAKIPOTEZA MAISHA’
Habari hiyo ikamfanya Priscar kukisitisha kidogo
kijiko kuto kuingia mdomoni mwake na kuitazama
taarifa hiyo ambayo imemuacha mdomo wazi.
“Masikini weee tazama askari wa watu walivyo
kufaa”
Priscar alizungumza kwa sauti ya huruma, Rahab
akawa na kazi ya kutabasamu kwani damu yake
tayari imesha anza kufanya kazi mwilini mwa
Priscar.
***
Shamsa na Briton wakafanikiwa kufika chini ya
gorofa, ambapo maiti nyingi za askari wanao linda
jengo hilo zimesambaa kila mahali, wakaanza
kukimbia kwenye moja ya barabara yenye giza ili
kuto onekana na askari. Wakafanikiwa kupata
usafiri wa bajaji ambao moja kwa moja
ukawapeleka hadi maeneo ya bahari beach,
kutokana hapakuwa na aliye na pesa mfukoni
mwake ya kumlipa dereva huyo wa bajaji, gafla
Shamsa akapiga dereva huyo maeneo ya nyuma ya
shingo yake na kumfanya apoteze fahamu.
Wakaona viboti vidogo vya watalii, vikiwa
vimesimamishwa ufukweni, kwa haraka wakaingia
kwenye moja ya kiboti na kukiwasha, wakaondoka
na kutokomea kusipo julikana
Magaidi walio ingia katika jengo la usalama wa
taifa, wakajikuta wakizidiwa nguvu, na kuwekwa
kati, huku silaha walizo kuwa nazo zikiwaishia.
Hapakuwa na aliye tamani kuweza kukamatwa na
kikiko hicho walicho weza kukifanya ni kujilipua
kwa mabomu ambayo waliyavaa miilini mwao na
huo ndio ukawa ni mwisho wa maisha yao.
***
Msakao mkali ukazidi kufanyika katika maeneo
yote na kuingi mipakani mwa Tanzania, kwenye
vituo vya mabasi pamoja na bandari, msako
ukaendelea kufanyika kuwatafuta Shamsa pamoja
na Briton walio toroka katika jengo la usalama wa
taifa. Kazi hiyo haikufanywa na askari polisi pekee
bali vikosi vyote vya ulinzi vikaingia kazini.
Hapakuwa na muda wa kuweza kupumzika, boti
nyingi za ulinzi pamoja na na helicopter za kijeshi
zikaendelea kufanya doria kwenye maeneo yote ya
nchi kavu pamoja na majini.
Amri kutoka kwa raisi, iliwaruhusu vikosi hivyo vya
majeshi kuwaua Briton na Shamsa pale watakapo
weza kuwakamata kwani hakuhitaji mlolongo wa
mauaji wa wanajeshi wake na raisi uzidi kuendelea
ndani ya nchi yake, hofi ya kiusalama ikazidi
kutanda kwa wananchi wa Tanzania, kila mmoja
hakuhitaji kwenda mbali kabisa nyumbani kwake
kuhofia usalama wake pamoja na familia yake.
Baadhi ya huduma za kijamii, hususani kwa
wafanya biashara wadogo wadogo na wakubwa,
walijikuta wakiingia katika hofu ya kuto kufungua
maduka yao, huku kukiwa na taarifa kwamba Al-
Shabab wameingia jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya ujumbe mfupi wa maneno(meseji),
zilisambaa baina ya mfanya biashara mmoja hadi
mwengine, wakitarifiana kuto kuyafungua maduka
yao pale kutokapo pambazuka kwani kufanya hivyo
yanaweza kutokea maswala ya Mlimani City.
Hadi kuna pambazuka asubuhi hapakuwa na kauli
yoyote kutoka serikalini, jambo lililo pelekea watu
wengi kujawa na hofu zaidi. Foleni ambazo
zimezoeleka kuonekana kwenye barabara za jiji la
Dar es Salaam hazikuwepo kabisa, Magari moja
moja ya wananchi wanao jiamini ndio yalkiyoweza
kukatiza katika barabara hizo. Mabasi ya mikoani
hayakuweza kuingia ndani ya jiji la Dar es Salaam,
wala mabasi ya ndani ya jiji kutoka nje ya jiji la
Dar es Salaam.
Kiufupi hali ya amani ilipotea kabisa, kwani hata
tetesi za chini chini zilidai kwamba mke wa raisi
amepotea na inasadikika ametekwa.
“Kama mke wa raisi amete kwa wewe je? Hembu
kalisha makalio yako hapo mume wangu na kama
ni hiyo kazi bora tu ufukuzwe, ila sinto hitaji kuona
ninakupoteza wewe mume wangu sawa”
Dada mmoja mjamzito alisikika akizungumza huku
akiwa amesimama katikatai ya mlango akimzuia
mume wake kutoka nyumbani baada ya kumaliza
kujiandaa kwenda kazini.
“Lakini mke wangu…..”
“Hakuna cha lakini hapo, wewe unahitaji mimba
yangu itoke si ndio”
Ikabidi jaama kuwa mpole na kuanza kuvua nguo
moja baada ya nyingine na kurudi chumbani huku
akiwa analalamika sana.
***
“Muheshimiwa bado mke wako hajarudi na kila
tukipiga simu yake na mlinzi wake, hazipatikani”
Habari hiyo ikazidi kumchanganya Raisi Praygod
aliye jikuta akizunguka zunguka ndani ya ofisi yake
kama mtu aliye changanyikiwa. Hapakuwa na
amaini kwa kila aliye fanya kazi kwenye ofisi yake,.
Kwani kila taarifa inayo letwa ni mbaya kupindukia,
vikosi vya uvamizi vinavyo vamia majengo ya
serikali, vilizidi kumchanganya Raisi Praygod huku
akiwa na hofu ya kuuendea uchanguzi kwani
wananchi wengi watapoteza imani na serikali yake
iliyopo madarakani.
“Hakikisheni munamtafuta mke wangu popote alipo
sawa”
“Sawa muheshimiwa”
“Muheshimiwa kuna simu yako”
Mmoja wa sekretari wake wakamuita, raisi Praygod
akaiendea meza yake na kuchukua mkonga wa
simu na kuuweka sikioni na kuusikilizia ni nani
anaye ipiga simu hiyo.
“Haloooo mr president”
Sauti nzito na yenye mikwaruzo ilisikika upande wa
pili wa simu hiyo na kumfanya raisi Praygod
kuweza kustuka.
“Ni nani wewe mwana haramu?”
“Hahahahaha president Praygod, umenisahau mara
moja hii. Ok sina muda mwingi wa kupoteza ila
tangu waziri wako wa ulinzi atokemadarakani na
kufariki, inchi yako haina amani. Hujiulizi kwa nini
muheshimiwa raisi”
Sauti hiyo ikasikika kwenye vipaza sauti vyote
vilivyomo kwenye ofisi ya raisi Praygod, watu wote
waliomo ndani ya ofisi hiyo wakaacha kazi
walizokuwa wakifanya na kuisikiliza sauti hiyo
yenye mikwaruzo ya kutisha.
“Washa televishion yako”
Mmoja wa wafanyakazi wa ofisini akawasha Tv
kubwa iliyomo ndani ya chumba hicho cha raisi
Praygod, macho yao yote yakatua kwenye bomu
kubwa la nyuklia. Lililo tegwa vizuri kwenye
vishikizo vyake.
“Hilo ni bomu lenye uwezo wa kutembea kwa spidi
1,000,000 ndani ya dakika moja, hilo ni Russian
bomu, ambalo limeandaliwa mahususi kuja kwenye
nchi yako na kutua katikati ya jiji la Dar es
Salaam”
Raisi Praygod akajikuta jasho likimwagika,
wasiwasi mwingi ukamtawala, mapigo ya moyo
yakazidi kumuenda mbio mithili ya mtu aliye
kimbia kwa umbali mrefu pasipo kupumzika.
Akajikuta akipunguza uzito mwilini mwake,
akalivua koti alilo livaa, na kubakiwa na shati.
“Ukihitaji bomu hilo lisije kwenye nchi yako, kuna
mambo mawili unahitaji kuyafanya.”
“Moja, hakikisha kwamba unaurudisha uhai wa
Eddy Godwin”
“Mbili ndani ya masaa 48, Eddy awe amerudi
madarakani la sivyo bomu hili litaisambaratisha
ikulu yako”
Simu hiyo ikakata, huku video iliyo kuwa
inaonekana kwenye tv hiyo ikapotea na kubakisha
mwanga wa bluu wa tv hiyo kubwa, watu wote
waliomo ndani ya ofisi hiyo wakabaki wakimtazama
raisi Praygod azungumze kitu juu ya hilo.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 39YA SIMUHILI HII. ENDELEA
 
SORRY MADAM (39)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Moja, hakikisha kwamba unaurudisha uhai wa
Eddy Godwin”
“Mbili ndani ya masaa 48, Eddy awe amerudi
madarakani la sivyo bomu hili litaisambaratisha
ikulu yako”
Simu hiyo ikakata, huku video iliyo kuwa
inaonekana kwenye tv hiyo ikapotea na kubakisha
mwanga wa bluu wa tv hiyo kubwa, watu wote
waliomo ndani ya ofisi
hiyo wakabaki wakimtazama raisi Praygod
azungumze kitu juu ya hilo.
ENDELEA
Jasho jingi likazidi kumwagika raisi Praygod,
hakuwa na jambo la kuweza kuzungunza na wala
hakuweza kutambua ni wapi alipo Eddy.
"Muheshimiwa Eddy si amesha kufa sasa
itakuwaje?"
Mmoja wa wafanyakazi wake walinuuliza
"Yupo hai"
Kila mmoja akabaki akiduwaa, baada ya kulisikia
hilo swala, raisi alipo ligundua hilo akakohoa
kidogo.
"Endeleeni na kazi"
Akatoka ndani ya ofisi yake na kuelekea katika
eneo lake la kulala, kichwani mwake akazidi
kujiuliza ni nani aliye weza kuufanya mchezo huo
kwani wataalamu wake walipo jaribu kutafuta ni
eneo gani simu hiyo ya vitisho ni wapi ilipo tokea
hawakuweza kuipata. Kitu kilicho zidi kumuumiza
zaidi ni wapi alipo kuwepo mke wake kipenzi
Shamsa, kwani inasadikika tangu atoke jana majira
ya asubuhi kutokana na taarifa aliyo pewa,
hakuweza kurejea kabisa hadi majira haya ya
asubuhi.
Akafungua moja ya droo yake na kutoa vidonge
viwili na kuvimeza pasipo hata kunywa maji,
akavisukumiza kwa mafumba kazaa ya mate kisha
akasimama mbele ya kioo kikubwa kilichopo
mbele ya chumba chake na kujitazama uso wake
ulio jaa wasiwask, iliyo changanyikana na hasira
kali sana.
"EDDY, EDDY, EDDY"
Raisi Praygod alizungumza huku jazba ikizidi
kuongezeka kifuani mwake. Taratibu akakisogelea
kitanda na kujilaza, huku akihema taratibu taratibu.
***
Mwanga mkali wa jua ukaanza kupenya kwenye
macho ya mtubaliye lala kitandani huku mwilini
mwake akiwa amebakiwa na boksa tu. Akajaribu
kunyanyuka kitandani ila maumivu makali ya paja
yakamfanya kurudi tena kitandani. Kwa sekunde
kadhaa akatumia kuchunguza kufahanu ni wapi
alipo, ila ikawa ni swali gumu sana Kwakwe
kuweza kufahamu alipo, kwani chumba hicho
kimetawaliwa na mitambo mingi ya kushangza.
Kitanda alicho lalia pembeni yake kuna bomba lililo
ning'inizwa dripu ya maji iliyo peleka mrija wake
moja kwa moja hadi kwenye mkono wake wa kulia
na kisindano kidogo kilicho weza kuunganishwa na
mrja huo, kimeingia moja kwa moja kwenye
mshipa wake wa damu.
"Hapa ni wapi?"
Alizungunza huku akijaribu kujikaza kunyanyuka,
mguh wake ulio fungwa bandeji zilizo badikika
rangi kutokana na dawa akiyo pakwa, ukazidi
kumuuma. Akiwa katika kutazama tazama mlango
wa chumba hicho kikubwa kinacho onekana
kwamba kipo juu ya gorofa kubwa, ukafunguliwa.
Akaingia mwanaume aliye valia koti jeupe pamoja
na miwani kubwa kiasi. Katika kumtazama kwa
haraka haraka ni lazima utagundua kwamba mtu
huyo ni daktari.
"Karibu tena duniani Mr Eddy Godwin"
Mtu huyo mwenye asili ya kizungu izungumza
kiswahili sahihi kilicho mshangaza hata Eddy
mwenyewe.
"Wewe ni nani?"
Lilikuwa ni swali la kwanza la Eddy huku akimkazia
macho daktari huyo aliye zidi kupiga hatua
kumfwata katika kitanda alicho lala.
"Kuna hofu ya kuhofia, mimi ni rafiki yako wa
karibu. Naitwa dokta William"
Alizungumza huku akigeuza geuza dripu linalo
endelea kushusha maji kwenye miishipa ya Eddy.
"Unajisikiaje?"
"Nina maumivu kwenye mguu. Kwanza hapa ni
wapi?"
"Hapa upo Mosscow Russia"
"Nilifikaje hapa?"
Eddy aliiza huku akizidi kumkazia macho daktari
huyo kwani jibu lake tayari lilianza kumpa wasiwasi
mkubwa.
"Nilikutoa Tanzania siju chache za nyuma. Niweza
kukufwatilia wewe kwa ukaribu mkubwa hadi
nikafanikiwa kukupata"
"Ulinijuaje mimi?"
"Nilikujua kupitia mama yako, alikuwa ni rafiki
yangu wa karibu sana. Kiufupi mama yako alikuwa
ni mwema sana kipindi nilipo kuwa nikiifanya kazi
ya kuwafundisha madktari wa jeshi nchini
Tanzania.
"Usiwe na shaka kwani Tanzania ni moja ya nchi
niliyo ipenda sana na ni nchi ambayo viongozi
wake baadhi ni wakatili sana wakiongozwa na raisi
Praygod"
Eddy akastuka kusikia jina jilo, katika
kumchunguza chunguza dokta William kwa haraka
haraka akatambua kwamba ni mtu ambaye hakuwa
na nia mbaya sana kwake japo hakuhitaji kuliamini
hilo kwa asilimia mia moja.
"Nil stori ndefu sana mimi na Tanzania pamoja na
viongozi wake na sasa nipo katika mpango wa
kuhakikisha kwamba nina lipa kisasi kwa nchi
hiyo."
"Kwa nini unahitaji kulipa kisasi?"
Dokta William akaivua miwani yake taratibu, kwa
mbali machozi yakawa yanamlenga lenga,
hakuhitaji kuzungumza kitu cha aina yoyote.
Akaondoka na kusimama kwenye moja ya mashine
inayo ongozwa na kompyuta aina ya Laptop.
Akaanza kuiminya minya batani zake kwa mwendo
wa kasi akionekana kuseti baadhi ya vitu katika
mtambo huo. Kila alivyo zidi kuminya batani za
kumpyuta hiyo asira dhidi ya Tanzania hususani
raisi Praygod zikazidi kumpanda mara dufu.
***
Kwa mwendo wa boti waliyo kuwa nayo,
haikuwasaidia sana kuweza kupasua mawimba
makubwa ambayo yanaendelea kuikumba bahari ya
hindi mara mwa mara. Upepe mkali na wenye
nguvu wa kuyumbisha hata meli kubwa ulizidi
kuirusha boti hiyo waliyo panda Shamsa na Briton
kutoka upande mmoja kwenda mwengine.
Halo hiyo kikaifanya boti hiyo kuzima gafla, hofu
ya kufa ndani ya maji ikaanza kumtawala Shamsa
ambaye kwa Mara kadhaa alionekana kumkumbatia
Briton huku akilia sana. Alihisi hakuwa na bahati
ya kuishi jwani familia yake aliyo kuwa akiitegemea
tayari ilisha fariki kuanzia Eddy hadi mtoto wake
Junio.
"Bray tunakufa mpenzi wangu"
"No hatuwezi kufa, tusonge Mbele"
Briton alizungumza huku akiendelea kujitahidi
kuhakikisha kwamba boti huyo inasonga Mbele.
Bahari ikazidi kuchafuka, hats akari ambao
walikuwa doria katika maji waka waliamriwa
kughairisha msako huyo kwank hali ilitisha sana.
Mvua taratibu ikaanza kunyesha jambo lililio zidi
kuwachanganya Briton na Shamsa. Radi zikaanza
kutawala kila kona. Gafla boti yao ikabenuliwa na
kuzamishwa ndani ya maji, kila mmoja akaangukia
upande wake. Hali ikazidi kuwa mbaya kwani radio,
mawimbi Na upepeo vikazidi kuongezeka kadri ya
muda ulivyo zidi kwenda ndivyo ikawa afadhali ya
dakika moja nyuma.
Kila mmoja alijikuta akiwa katika upande wake,
baridi kali ikazidi kuunynyasa mwili wa Shamsa,
maumivu makali ya tumbo yakarejea gafla mwilini
mwa Shamsa na kumfanya aanze kuishi wa nguvu,
dakika kadhaa mbeleni akapoteza fahamu.
***
Hali ya usalama ikazidi kuimarishwa maeneo mbali
mbaali ndanj na nje ya jiji la Dar es Salaam.
Wanaanchi kupitia katika vyombo vya habari.
Video, redio na magazetini raisi Praygod
akatangaza hali ya usalama katika maeneo yote
yanchi, akiendelea kuwahakikishia kwamba hakuto
kuwa na jambo lolote bays litakalo weza
kujitokeza. Wanaanchi pamoja na wafanya biashara
wakarudi katika maeneo yao ya kazi.
Kitu kilicho zidi kimchanganya raisi Praygod ni
wapi alipo mke wake kipenzi Rahab. Msako wa
kuhakikisha kwamba mke wa raisi anapatikana
ukazidi kuendelea. Kwa siku ya pili mfululizo
hapakuwa na askari akiye weza kulaza kichwa
chake kwenye kitanda chake kama ilivyo siku za
nyuma. Kuanzia wakuu wa majeshi hadi waliopo
ngazi za chini, kazi ikawa ni kuhakikisha kwamva
mke wa raisi anapatikana. Hapakuwa na mtu
mwenye wazo la kujua kwamba mke wa raisi yupo
kwenye pango ambalo lilitumiwa Na waasi
wanawake ambao kwa sasa baadhi yao wapo
katika mikono ya wamarekani.
"Madam tutaendelea kukaa humu hadi lini?"
"Hadi siku ambayo nitaamua mimi kutoka ndani ya
handaki hili"
"Ika utakuwa unampa wasiwasi muheshimiwa
raisi"."Nalitambua hilo ila sinto hitaji kurudi ikulu
hadi nihakikishe ninampata Eddy, iwe kwa kuua au
kufanya lolote ni kuhakikisha kwamba tunampata
Eddy"
Priscar hakuwa na kitu chochote cha kuzungumza
zaidi ya kuyasikiliza matakwa ya bosi wake.
"Ila kuna kitu kimoja nahitaji tuweze kukifanya kwa
pamoja"
"Kitu gani madam"
"Nilazima kuhakikisha kwamba tunapata pesa tena
pesa ya kutosha"
"Kama ni pesa mbona mume wako anazo za
kutosha?"
"Ndio anazo ila nitahitahi za kwangu, BOT ipo
kwenye mpango wangu wa kuchukua pesa zote
zilizomo ndani ya benki hiyo"
Rahab izungunza huku akiishika bastola yake,
akiigeuza upande mmoja hadi mwingine, heshima
ya kuwa mke wa riasi akaiweka kando na kuamua
kurudi katika kazi yake aliyo kuwa akiifanya miaka
kadhaa ya nyuma.
***
Mpango wa kuwahamisha wafungwa watatu, ambao
wanachuliwa kama magaidi katika nchi ya
Marekani. Ikawadia, vikosi vyabulinzi vilivyo
kabidhiwa kazibya kuwatoa wafungwa hao ambao
ni Fetty, Halima na Anna. Ulinzi mkali
ukaimarishwa kuanzia kwenye helcoptar zao
wakihakikisha kwamba hakuna jambo lolote ambalo
litaweza kujitokeza. Helcoptar zipatazo sita zilizo
jaa askari wa kikosi cha FBI, zikazidi kukizunguka
eneo la kikosi, huku ndege moja kubwa inayo
tumika kubeba wafungwa kuwatoa katika gereza
hilo, ikawekwa tayari.
Ulinzi ndani ya gereza ukazidi kuimarika. Fetty,
Halima na Anna wakawekwa tayari kwa kutolewa
katika vyumba vyao maalumu walivyo kuwa
wamefungiwa kwa kipindi chote hicho. Walifungwa
pingu mikononi na kufungwa cheni ngumu kwenye
miguu yao. Kila sehemu walipo pita wafungwa
wezao waliweza kuwashangilia kwa jinsi wanavyo
tolewa kwenye gereza hilo. Japo miili yao
imedhohofika sana ika tayari walisha jijengea
umaarufu mkubwa ndani ya gereza hilo. Hii
nikutokana na msaada ambao mara kadhaa
waliweza kuwapatia wafungwa wezao ambao mara
kadhaa walikuwa wakionewa vikali wa wasichana
wengine wababe ndani ya jengo hilo. Kabla
hawajafikishwa nje kulipo na uwanja mkubwa sana
wa ndege. Wakavalishwa vigunia vyeusi
wakatolewa nje ya gereza wakiwa katika ulinzi
mkali, wakizungukwa na askari walio jazatiti kila
idara, ili kuhakikisha tu kwamba magaidi hao
ambao ni tishio hawawezi kufanya kitu chochote
cha ajabu.
Wakiwa njiani wakielekea kwenyebuwanja wa ndege
katika eno hilo, gafla moja ya helcoptar ikalipuliwa
hewani na kuwafanya askari na watu wote kustuka
ni kitu gani kilicho tokea huku askari wapatao kumi
na mbili, walio kuwa wakiwasindikiza Fetty, Halima
na Anna, wakawazingira na kuwalaza chini huku
mitutu yao ya bunduki wakielekezea juu na pande
zote kutazama maadui wapo eneo gani.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 40YA SIMUHILI HII. ENDELEA
 
SORRY MADAM (40)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Wakiwa njiani wakielekea kwenye uwanja wa ndege
katika eno hilo, gafla moja ya helcoptar ikalipuliwa
hewani na kuwafanya askari na watu wote kustuka
ni kitu gani kilicho tokea huku askari wapatao kumi
na mbili, walio kuwa wakiwasindikiza Fetty, Halima
na Anna, wakawazingira na kuwalaza chini huku
mitutu yao ya bunduki wakielekezea juu na pande
zote kutazama maadui wapo eneo gani.
ENDELEA
Ukimya wa dakika kadhaa ukapita huku macho ya
askari yakitazama jinsi helcoptar iliyo lipuka
ikimalizikia vipande vipande kutua chini. Hapakuwa
na askari aliye weza kutoka kwenye helcoptar iliyo
lipuka, uangalizi wa kitu kilicho ipelekea helcoptar
hiyo kulipuka ukazidi kufanyika kwa haraka na
uamkini. Rada zote nje ya gereza zikaendelea
kuangaza kila sehemu ya kona ya gereza hilo
lililopo kwenye kisiwa ambacho hakina makazi ya
watu zaidi ya gereza hilo pekee.
Wakawasimamisha Fetty, Halima na Anna,
wakaendelea kusonga mbele tena kwa mwendo wa
kukimbia na si kutembea huku askari kadhaa
wakiwa wamewashikilia kwenye mikono kuwasaidia
kuweza kukimbia pasipo kuanguka kutokana
hawaoni kitu chochote cha mbele. Wakawaingiza
ndani ya ndege hiyo, kila askari akazidi kuimarisha
ulinzi kuhakikisha ndegehiyo haishambuliwi kwani
hali ya hatari imesha anza kutwala kwa kila
mmoja. Gafla askari mmoja baada ya mwengine
wakaanza kuanguka ndani ya ndege huku risasi za
vichwa zikiwa ndio halali yao. Mianguko hiyo
ikazidi kuwapa matumaini Fetty na wezake
wakiamini anaye fanya msaada huo ni mtu ambaye
amekuja kuwachukua.
***
Garim nyeusi aina ya BMW X5, ikasimama kwenye
moja ya maegesho ya benki kuu ya Tanzania.
Msichana mrefu iye ziweka nywele zake ndefu
mgoilngoni. Miwani yake ya macho aliyo ivaa,
imezidi kumpendezesha, mkoba wake mkubwa alio
shuka nao kwenye gari unaashiria kwamba
msichana huyo ni mtu mwenye uwezo wa kifedha.
Suti ya rangi ya kaki iliyo mkaa vizuri mwilini
mwake ikilichora umbo lake jembamba kiasi huku
makalio madogo kiasi yakijitokeza kwa nyuma.
"Nimefika"
Msichana huyo alizungumza kwa sauti ya chini.
Akaanza kupiga hatua kwa mwendo wa madaha,
kila aliye muoana alibaki akimtumbulia macho
hususani wanaume ikiwemo na askari kadhaa
àmbao wanaendeleza ulinzi nje ya benki hiyo
inayo heshimika kwa kiasi kikubwa ndani na nje ya
Tanzania. Akakaguliwa kama kawaida ya watu
wanao ingia ndani ya Benji huyo. moja kwa moja
akaelekea katika dirisha la kuhudumia Wateja.
"Dada habari yako?"
"Salama nikusaidie mini?"
"Nahitaji kuonana na meneja sijui inawezekana?"
"Una ahadi Nate?"
"Kusema kweli hapana, ila kama unaweza
kunisaidia nakuomba nionane nae"
Dada huyo akatazamana na muhudumu kwa
sekunde kadhaa, kisha muhudumu huyo
akanyanyua mkonga wa simu iliyopo pembeni
yake, akaminya batani moja Na kumpigia meneja
wake.
"Bosi kuna mgeni hapa dirishani anahitaji kuonana
na wewe"
"Anaitwa nani?"
Kwa haraka dada huyo akaibana sehemu ya kinasa
sauti kwa kutumia kiganja chake kisha akamuuliza
swali binti huyo.
"Paulina Thomas"
"Anaitwa Paulina Thomas"
Meneja huyo taratibu akaigeukia TV kubwa ikiyomo
ndani ya ofisi yake, akaiwasha na kutazama ni
Paulina gani. Kamera ya ulinzi iliyopo kwenye
dirisha hilo ilimchukua Paulina kwa nyuma.
"Muambie atazame camera nimuone"
"Dada hembu geuka utazame hiyo kamera"
Paulina bila ya wasiwasi akageuka, akaitazama
kamera hiyo kwa dakika moja kisha akamgeukia
muhudumu huyo.
"Muambie aingine"
Paulina akaruhusiwa kuingia ndani ya ofisi ya
meneja wa BOT. Akakaribishwa na kukaa kwenye
kiti.
"Nikusaidie nini binti?"
Mzee huyo wa makamu alizungumza huku
akiendelea kumtazama Paulina kwa macho ya
matamanio sana. Paulina akatabasamu, akaiweka
miwani yake sawa kisha akasimama, akafungua
kifungo kimoja cha shati lake, maziwa yake yaliyo
chora alama ya vii kutokana na sidiria yake
kuyabana vizuri yakamfanya meneja wa benki
kushusha pumzi nyingi za uchu, taratibu uume
wake ukaanza kusimama taratibu ndani ya suruali
yake.
***
Taratibu hali ya hewa ikaanza kutulia ndani ya
bahari. Upepo ulio kuwa Mkali ukatulia, mvua
pamoja na radi vikakata. Briton akaanza kutazama
kila sehemu kumtafuta Shamsa ila hakumuona.
Akaanza kumuita kwa nguvu ila hapakuwa na jibu
lolote lililo weza kutokea katika juhudi zake za
kumuita Shamsa. Wasiwasi mwingi ukaanza
kumtawala hisia mbaya za Shamsa kufikwa na
mauti zikaanza kumtawala.
Akaanza kupiga mbizi huku na kule akiemdelea
kumuita Shamsa ila hapakuwa na jibu, Machozi
yakaanza mumwagika, akiwa katika kuendelea
kumtafuta Shamsa, mwanga Mkali wa boti kama
mbili, ukawa unakuja katika eneo ambalo yupo.
Ndani ya dakika kadhaa boti hizo mbili zikawa
zimemzunguka huku mwanga mkali wa taa kubwa
za boti hiyo zikiwa zimemmulika. Amri mmoja iliyo
tolewa na watu walio valia mavazi meusi huku
wakiwa na bunduki mikononi mwao, ni Briton
kutulia kama alivyo na akileta ujinga risasi
zitauchangua mwili wake na itakuwa ni mwisho wa
maisha yake.
***
Machozi yakaanza kumwagika Doktar William,
kumbukumbu za mke wake lamoja na wanae
wawili kuuliwa kikatili nyumbani kwake. Jinsi damu
ya zilivyo kuwa zikiwamwagika wanae walio pigwa
risasi za vichwa. Ndio jinsi alivyo zidi kuhisi
kuchanganyikiwa.
"PRAYGOD NILAZIMA NIKUUE"
Maneno ya dokta William yalisikika vizuri masikioni
mwa Eddy, akajiweka vizuri kitandani akatamani
kuzungumza kitu ila mdomo wake ukawa mzito
kiasi. Hakujua ni kwanini Dokta huyo anazungumza
hivyo.
Akashangaa kumuona dokta huyo akivuruga kila
kitu kilichokuwa juu ya meza hadi laptop yake pia
ilianguka chini.
"Agrhaaaaaaaaaaaaaa"
Dokta William izungumza huku akisimama kwa
hasira macho yake yakimwagikwa na machozi
mengi. Akamtazama Eddy kisha akatoka ndani ya
chumba hicho kwa mwendo wa kasi na kumuacha
Eddy akijiuliza maswali juu ya kitu gani kinacho
endelea kati yake na raisi Praygod.
***
Kati ya askari kumi walio ingia ndani ya ndege
hiyo ya wafungwa ni askari watatu tu ndio walibaki
wakiwa wamesimama, huku wao ndio wakiwa
wameifanya kazi hiyo ya kuwauwa wezao. Mmoja
wao moja kwa moja akaelekea chumba cha
marubani Wawili wanao irusha ndege hiyo.
"Munaweza kuendelea"
Sauti ya kike ilisikika ikiwaamrisha marubani hao
ambao tayari mashime za ndege hiyo walisha
ziweka tayari na zilikuwa zikinguruma taratibu. Nje
ya ndege hapakuwa na mtu aliye weza kujua kitu
kilicho endelea ndani ya ndege. Kila askari aliye
baki nje ya ndege akawa na kazi ya kuhakikisha
ulinzi unaendelea vuzuri katika eneo zima la
gereza. Wengine waliendelea kuzima moto kwenye
helicopter iliyo anguka. Ndege hiyo ikaanza
kushika kasi taratibu. Dakika chache baadae tayari
ikawa imesha iacha ardhi ya kisiwani na kuanza
kupasua mawingu. Helicopter nyingine za kijeshi
zilizo kuwana na kazi ya kuhakikisha inalinda
usalama wa eneo zima katika tukio zima la
kuwasafirisha wafungwa hao, zikaondoka na kurudi
makao makuu ya FBI. Huku majibu ya uchunguzi
kuhusiana na helicopter iliyo anguka zikidai
kwamba ajali hiyo imetokea kutokana na itilafu
katika katika injini yake. Ila hayakuwa ni majibu ya
kumtosheleza raisi, akaagiza uchunguzi uzidi
kufanyika.
Mstuko mkubwa ukawapata watu wote waliomo
ndani ya ofisi ya makao makuu ya FBI. Mlipuko
mkubwa wa ndege ya wafungwa, wanayo ifwatilia
kupitia mitambo ya satellite ikawafanya kila mtu
kubaki mdomo wazi. Vipande vidogo vidogo vya
ndege hiyo vikazidi kuchanguka na kupotelea
hewani na hapakuwa na mtu aliye weza kutoka
ndani ya ndege hiyo.
***
Paulina akafungua kifunguo cha pili cha shati lake
na kuifanya sidiria hake nyeupe kuonekana vizuri,
maziwa yake yakajitokeza vizuri kifuani mwake,
taratibu akaweka mikono yakemiwili kwenye meza.
Macho ya meneja yakatua kwenye kifua cha
Paulina.Hapakuwa na mtu aliye zungumza zaidi ya
meneja kutetemeka kwa hisia kali za mapenzi.
Meneja akameza tena fumba la mate, akatamani
kuusogeza mdomo wake hadi kwenye maziwa ya
Paulina ila akasita kidogo.
"U...uuu unata..ka nini binti"
Meneja alibabika huku akianza kumwagikwa na
jasho la mabaha mwilini mwake, akazidi kuibana
miguu yake kuuzuia uume wake usizidi
kugombana na nguo yake ya ndani.
"Unajua nini nataka"
Paulina akafungua kifungo cha tatu cha shati lake,
maziwa yake pamoja na tumbo lake vikaonekana
vizuri. Paulina akauchukua mkono wa kulia wa
meneja na kuukandamiza kifuani mwake,
akamshikisha maziwa meneja, akabaki akiwa
ameduwaa huku akihema. Gafla Paulina akamshika
meneja Shingo yake, akamgandamiza kichwa
chake kwenye meza kwa nguvu na kumuachia. Paji
zima la uso wa meneja likawa linavuja damu nyingi
na kumfanya atoe kilio cha maumivu.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 41 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (41)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
"Unajua nini nataka"
Paulina akafungua kifungo cha tatu cha shati lake,
maziwa yake pamoja na tumbo lake vikaonekana
vizuri. Paulina akauchukua mkono wa kulia wa
meneja na kuukandamiza kifuani mwake,
akamshikisha maziwa meneja, akabaki akiwa
ameduwaa huku akihema. Gafla Paulina akamshika
meneja Shingo yake, akamgandamiza kichwa
chake kwenye meza kwa nguvu na kumuachia. Paji
zima la uso wa meneja likawa linavuja damu nyingi
na kumfanya atoe kilio cha maumivu.
ENDELEA
"Unajisikiaje?"
Paulina alimuuliza meneja wa benki ambaye
kichwa chake kilisha anza kuvuma milio ambayo ni
ya ajabu ajabu ambayo yanatokana na maumivu
makali sana ya kubamizwa kwenye meza yake.
Paulina akajifunga vifungo vya shati lake na
kujiweka sawa. Akazunguka upande wa pili wa
meza na kumshika shati meneja, akamnyanyua juu
na kumsogeza karibu na uso wake.
"Nahitaji pesa"
Paulina alizungumza kwa kujiamini sana.
"Pesa! Pesa gani?"
"Priscar fanya kazi iliyo kupeleka hapo"
Sauti ya Rahab ilisikika kupitia kinasa sauti alicho
kivaa masikioni make. Hakuwa Paulina kama alivyo
jitambulisha ila ni Priscar aliye panga mpango na
Rahab kufanya uvamizi wa kimya kimnya. Huku
Priscar akiwa amevaa sura ya bandia ambayo si
rahisi kwa mtu kuweza kumfahamu.
Kwa amri aliyo pewa na Rahab, Moja kwa moja,
akamuamrisha meneja kuelekea kwenye chumba
ambacho kinahifadhiwa mali nyingi za benki
ikiwemo pesa nyingi sana. Pasipo mtu yoyote
kuweza kufahamu ni kitu gani kinacho endelea
huku damu zilizo kuwa zimejaa usoni make zikiwa
zimefutwa na Paulina au Priscar.
Chumba kilicho jaa droo nyingi za chuma zenye
mamba kwa kila droo meneja akaanza kufungua
droo moja hadi nyingine. Huku mapigo ya moyo
yakimuenda kasi sana, kwa vitisho ambayo aliweza
kuvipata.
Priscar akawa na kazi ya kukusanya madini yenye
thamani kubwa, hakuhitaji Kuchukua pesa kutokana
na kuhofia kustukiwa.
"Nakuomba mumuachie mwangu tafadhali"
Meneja alizungumza katika hali ya majonzi kwani
kwa kipindi alipo kuwa ofisini kabla ya kutolewa
kwenye ofisi hiyo. Alipewa simu na kuzungumza
na mtu ambaye amemteka mwanae wa kike kipenzi
na wapekee.
"Nilazima kutoka hapa tuondoke pamoja"
"Nipo tayari katika hilo"
Priscar alipo hakikisha amechukua madini yenye
thamani si chinj ya bilioni moja ya kitanzania.
Akaifunga pochi yake, wakatoka katika chumba
hicho ambacho mara nyingi huingia watu .atajiri
wanao sadikika kuweka thamani ya pesa zao katika
mfumo wa madini ambayo huwa na thamani sawa
na pesa ambazo wanaziweka.
Wakatoka nje pasipo mtu yoyote kuweza kustukia
swala lililo tokea. Wakaingia katika gari la Priscar
na kuondoka naye kuelekea katika eneo ambalo
yupo Rahab akiwa amemshikilia mtoto wa kike wa
meneja wa benki.
***
Msako wa kumtafuta mke wa raisi ukazidi
kuendelea kufanyika, hapakuwa namkuu wa jeshi
aliye weza kulala. Kila mmoja alihakikisha kwamba
anakiamrisha kikosi chake katika kuwatafuta watu
ambao wamemteka mme wa raisi. Uvumilivu
ukawashinda jeshi na kuamua kutangaza hadharani
zawadi nono kwa mtu ambaye atafanikisha
kukamatwa kwa watekaji walio mchukua mke wa
raisi. Hapakuwa na aliye kuwa na hisia kwamba
mke wa raisi hajatekwa na yupo kwenye maficho
ya handaki ambalo siku za nyuma alikuwa
akilitumia yeye na wezake wakiwa katika kujificha
kipindi wakifanya shuhuli za kijambazi.
Mawazo yakazidi kumkondesha raisi Praygod,
uchangamfu wake ulipotea kwa watu wake wa
karibu. Hapakuwa na mtu aliye weza kuzungumza
jambo la kumfurahisha, akili yake yote ipo kwa
mke wake kipenzi. Hata baadhi ya kazi za
kiserikali zikaanza kumshinda kufanya. Ikamlazimu
makamu wa raisi kuweza musimamia baadhi ya
amjukumu.
"Muheshimiwa kuna mgeni anahitaji kukuona"
Sekretaari wake alimuambia raisi Praygod aliye
jiinamia kwenye meza yake mawazo yakizidi
kumpelekesha puta.
"Sihitaji kuonana na mtu kwa wakati hu"
"Ila amesema ni muhimu sana"
Kwa jicho alilo mtazama sekretari wake lilimtosha
kufahamu kwamba rahisi haitaji kuzungumza naye.
Taratibu mama huyo akatoka ofisini kwa raisi
Praygod na kurudisha jibu kwa mkemia mkuu,
bwana Ingnatus Mkama.
Jibu hilo likafedhesha mkemia wa serikali kwani
alihitaji kumjulisha juu ya mazishi ya Lukuman
ambaye ana wiki kadhaa akiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti, huku watu wengi wakiamini
kwamba ndio Eddy.
"Nitafanya ninacho kifahanu"
Mkemia mkuu akizungumza na kuamua kuondoka
akiwa amechoshwa sana skendo ambayo rafiki
yake wa karibu bwana Eddy Godwin, zinaendelea
kumtafuna kwenye jamii akioneka si mtu mwema
kwao.
***
Shamsa hakuwa na jinsi yoyote zaidi, ya kuendelea
kujitahidi kuogelea kuyaokoa maisha yake.
Hakuhitaji kufia baharini. Ni bora kufili mbali na si
kwenye bahari. Chuki dhidi ya Tanzania ikaanza
kumjaa moyoni make. Furha ya maisha aliyo kuwa
nayo kipindi cha nyuma imepotea. Akazidi
kukumbuka Eddy kwa msaada alioweza kumpatia.
Akimchukulia na kumpenda kama mwanae
Kadri jinsi alivyo zidi kwenda ndivyo jinsi Shamsa
alijikuta akichoka. Njaa kali ikazidi kumtesa
tumboni make, uwezo na kasi ambayo alikuwa
anaitumia katika kuogelea ikaanza kupungua
taratibu. Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi na ndani ya
dakika kumi mbele akajikuta akipoteza fahamu
kabisa. Boti moja iliyo jaa watu wembamba kasi
huku nywelie zao zikiwa zimenyongorotana,
wakasimama karibu na ulipo mwili wa Shamsa
unao elea juu ya maji. Mmoja wao akamkabidhi
mwenzake bunduki yake, kisha yeye akajitosa
ndani ya maji.
Wakamuokoa Shamsa na kumuingiza ndani ya boti
na kuondoka naye. Kila mmoja wao ndani ya boti
hiyo aliweza kumtambua binti huyo, moja kwa
moja wakampeleka kwenye makao makuu yao ha
Al-Shabab. Moja kwa moja wakampeleka kwa
Kiongozi wao bwana Mohammed Abdulah.
"Briton hamujampata?"
"Hatujampata kiongozi, huyu amekuwa kama
bahati kwani kwenye patrol yetu ndio tumeweza
kumpata Shamsa"
Kwa upande mmoja ikawa ni furaha kwa bwana
Mohamed Abdulah na kwa upande mwingine
imawa ni huzuni, kubwa kwa kumpoteza kijana
wake aliye mtegemea kuliko yoyote, japo habari za
vijana wake wengine alio watuma nchini Tanzania
alizipata kwamba wamepoteza maisha. Shamsa
akapatia watibabu yote ya muhimu huku daktari
akitoa majibu yaliyo mridhisha bwana Abdulah
Mohammed.
"Kwahiyo umesema kwamba hali yake itakuwa
nzuri"
"Ndio muheshimiwa atakuwa salama, akizinduka
hapa kila kitu kitakuwa sawa"
Wakamuacha Shamsa katika chumba maalumu cha
matibabu kisha yeye na daktari wakatoka ndani ya
chumba hicho.
***
Hali ya Eddy ikazidi kuhimarika siku hadi siku,
huku dokta William akizidi kumuhudumia jeraha
lake hadi likapona kabisa. Dokta William
akamtafutia Eddy, mwalimu wa kumfundisha
maswala ya kujilinda katika maisha yake ya
baadaye. Eddy akazidi kupiga tizi na kujifunza
mbinu mbalimbali za kuweza kupambana kwanza
kutumia mwili wake ikiwa akipatiwa ujuzi wa kareti
pamoja na mafuzo ya judo. Alipo weza kuhitimu
kwa wakati mfupi tu, akaingia katika mafunzo ya
taikondo ambayo aliweza kufundishwa na .walimu
mwengine kutoka nchi ya Thailand.
Mafunzo hayo Eddy aliweza kujifunza kwa juhudi
zote, huku akilini mwake kukiwa na hali moja tu ya
kipiza kisasi kwa mzee Godwin aliye weza
kuhusika katika kumuulia familia yake.
Mazoezi hayo yakazidi kuuimarisha mwili wa Eddy.
Haukuwa kama awali alivyo kuwa bali aliweza
kupungua kwa kiasi kikubwa. Kifua chake hadi
tumboni kuliweza kugawanyika katika miraba sita.
Misuli ya mikono yake iliweza kugawanyika kwa
kiasi cha kumfanya muonekano wa mwili wake
kubadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuwa Eddy waziri
tena ambaye hapo awali mwili wame ulisha anza
kunenepa na kutokwa na kitambi. Ila huyu ni Black
Shadow, umri wake wa miaka ishirini na saba
ulimfanya aweze kujitahidi kuhakikisha anafanya
kila jambo katika kuhakikisha kisasi chake
kinakamilika kwa asilimia mia.
"Itabidi usafiri kwenda Japan"
Dokta William alizungumza mara baada ya Eddy
kukamilisha kufanya mazoezi yake katika ukumbi
maalumu ambao ndio anao fanyia mazoezi.
"Kufanya nini dokta?"
"Kule kuna baadhi ya mazoezi ninahitaji uende
kuyafanya kuna mzee mmoja nirafiki yangu wa
kipindi kirefu nahitaji akakupatie mazoezi hayo
ambayo yatakusaidia"
"Sawa dokta, ila ni kwanini usisitishe mpango wa
kuishambulia Tanzania na umshambulie Raisi
Praygod peke yake"
"Hilo pia ninaliwaza kichwani mwangu, ila sintk
hitaji kumuona anaingia katika awamu ya pili ya
uongozi wake hata kama wananchi wake
wanampenda sana.
"Ila unampango gani na Mzee Godwin?"
"Nahitaji kujiweka sawa ndio niweze kuliliza kisasi
japo ni baba yangu ila yeye ndio chanzo cha mimi
kuwa hivi."
Hapakuwa na jambo jengine ambalo dokta William,
alilizunguza zaidi ya kuhakikisha mpango wa Eddy
unakamilika. Siku mbili mbele Eddy akaanza safari
ya kwenda Japan ambapo alipewa maagizo yoye
ya kukutana na mzee huyo ambaye lengo la dokta
William ni Eddy kujifunza mafunzo ya kininja ili
kupapambana na kila mtu ambaye atakuwa ni adui
yake.
***
Serikali ya Marekani iliamini kwamba wanajeshi
wake pamoja na magaidi watatu ambao wikuwa
wakiwasafirsha katika ndege hiyo kubwa ya
wafungwa, wamefariki dunia kwa mlipuko mkubwa
ulio weza kutokea. Hapakuwa na masalia yaliyo
baki ya ndege hiyo kwani kila kitu kilisha potelea
angani. Hapakuwa na aliyeeweza kufahamu
kwamba kuna mchezo wa akili sana ulio weza
kuchhezwa na marubani hao ambao ni miongoni
mwa wanachama wa D.F.E.
Kitu kilicho weza kutokea kipindi ndege hiyo ilipo
kuwa ikipasua mawingu juu angani umbali mrefu
sana kutoka usawa wa bahari. Kati ya askari
ambao walikuja kuwachukua Fetty, Halima na
Anna. Alikuwemo Agnes, Jaquline na Manka. Wote
watatu waliweza kuzifunika sura zao na kuingia
kisiri katika mpango wa kuwasafirisha magaidi hao,
huku wakiwaua askari watatu wanawake ambao
walikuwa kwenye mpangu huo kisha nafasi zao
wakazichukua wao. Ulikuwa ni mpango wa siri
sana wakishirikiana na mkuu wa kikosi cha FBI,
ambaye aliweza mutoa siri zote za mpango mzima
wa tukio hilo lilivyo kuwa limepangwa, ndio maana
alijitahidi kadri ya uwezo wake kuishawishi serikali
kuweza kukiruhusu kikosi chake kusimamjia
jukumu lote la wao kuwasafirisha magaidi hao.
Hata mlipuko wa helcoptar ambayo ilitegeshwa
bomu linalo ongonjwa kwa romoti, ulikuwa ni
mpango wame akishirikiana karibu na Mzee
Godwin mwenye matawi mengi sana duniani na
hapakuwa na jambo alilo weza kupinga na
kushindika.
Ikawabidi Agnes na wezame kuvua kofia ambazo
zilificha sura zao na kubakisha macho yao.
Wakawavua na kina Fetty vigunia vizito vyeusi
walivyo wavisha. Hapakuwa na mtu kati ya Fetty
aliye weza kuyaamini macho yake kumuona
mwenzao waliye potezana naye kwa kipindi kirefu
akiwa amesimama mbele ya macho yao.
Wakanyanyuka kwa furaha na kumkumbatia Agnes.
Machozi yaliyo changanyikana na uchungu
yakawatoka wote wanne.
Agnes ndio alizidi kupatwa na uchungu zaidi kwani
wezake alio wazoea kuwaona ni warembo na
wakakamavu ila leo wamepauka na kukondeana
sana. Huwezi kuwatofautish na watu ambao
hutumia madawa ya kulevya pasipo kupata chakula
cha maana.
"Hatuna muda wa kupoteza tunahittaji kuondoka
hapa"
Agnes alizungumza huku akiyafuta machozi
yanayo tiririka usoni mwake.
"Ila si tupo juj ya ndege?"
Fetty aliuliza kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo hii
nikutoka na kifua anacho ugua kwa muda mrefu.
"Ndio tupo juu ya ndege ila hii jnatakiwa kulipuliwa
kufuta ushahidi, kufa kwenu kutawasaidia ninyi
kuishi kwa amani popote ndani ya dunia hii"
Agnes alizungumza.
Wakaanza kazi ya kuwavua nguo wanajeshi watatu,
kisha nguo hizo wakazivaa kina Fetty na wezame.
Walipo hakikisha kwamba wapo tayari. Ndege
nyingine ambayo ilitumwa na Mzee Godwin yenye
uwezo wa kuto weza kunaswa na Satelait yoyote
duniani, na mara nyingi ndege hizi hutumiwa na
maraisi wa marekani wanapo elekea kwenye zihara
katika nchi zenye usalama finyu na ni maadui kwa
nchi yao ya Marekani.
Ndege hiyo taratibu ikajisogeza na kuganda chini
ya ndege ya waliomo Agnes na wezake. Bomba
kubwa lenye ngazi ndani yake, mainjini walimo
ndani ya ndege hiyo wakaanza kukata katika eneo
ambalo wezao wangelitumia kutoka katika ndege
moja na kwenda katika ndege nyingine.
Zoezi hilo lilichukua dakika kumi, huku makao
makuu ya FBI wakiwa hawaoni kinacho endelea
zaidi ya kuiona ndege yao ikiwa katika hali ya
usalama tu. Injinia mmoja akaingia katika ndege
walipo Agnes, akawasalimia. Pasipo kupoteza
muda wakaingia kwenye ndege iliyo kuja
kuwachukua, wakaungana na marubani walio
shirikiana nao, ambao kabla ya kutoka ndani ya
ndege hiyo. Waliyafungulia matenki yote ya mafuta
na kuyaacha yakimwaga mafuta hewani wakiamini
ndanj ya dakika kadhaa ndege hiyo italipuka na
ndivyo ilivyo weza kutokea ndani ya dakika kumi
na tano ndege hiyo ilichanguka na kuwa vipande
vipande.
***
"Madam ni mini mapngo wako mwengine?"
Priscar alimuuliza Rahab mara baada ya
kumuachia mtoto wa meneja wa benki ya BOT,
waliye mshusha kwenye mataa ya Ubungo kisha
wao wakaondoka na gari yao wakiwa katika sura
za bandia ambazo si rahisi kwa mtu kuweza
kuwafahamu.
"Nahitaji kumuua raisi Praygod kulipiza kisasi cha
Eddy"
Maneno ya Rahab yakamuacha Priscar akiwa
ameduwaa, asijue ni jinsi gani bosi wake anaweza
kusitisha mpango wa kumuua raisi kwani ni hatari
sana kwa maisha yao.
. ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 42 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (42)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
"Madam ni mini mapngo wako mwengine?"
Priscar alimuuliza Rahab mara baada ya
kumuachia mtoto wa meneja wa benki ya BOT,
waliye mshusha kwenye mataa ya Ubungo kisha
wao wakaondoka na gari yao wakiwa katika sura
za bandia ambazo si rahisi kwa mtu kuweza
kuwafahamu.
"Nahitaji kumuua raisi Praygod kulipiza kisasi cha
Eddy"
Maneno ya Rahab yakamuacha Priscar akiwa
ameduwaa, asijue ni jinsi gani bosi wake anaweza
kusitisha mpango wa kumuua raisi kwani ni hatari
sana kwa maisha yao.
ENDELEA
Rahab na Priscar wakaendelea kukaa mafichoni
pasipo kuingia katika mikono ya serikali. Wakiwa
katika sura za bandia waliweza kuzunguka sehemu
moja hadi nyingine ndani ya jiji la Dar es Salaaml
kuangalia ni hali gani inayo endelea katika jamii ya
watanzani wengi ambao macho na masikio yao
wameyapelekea katika hatua za uandikishaji wa
daftari la wapiga kura wakijiandaa na uchaguzi
ambao kwa katiba na sheria ya nchi ya Tanzania
huwa inafànyika mwisho ni mwa mwezi wa Tisa.
Hadi kwa kipindi hicho hakuhitaji kuweza kurudi
ikulu huku kazi yake ikiwa ni jinsi gani anaweza
kupanga mipango yake mipya jinsi ya kumteketeza
mumewe ambaye siku hadi siku anaendelea
kupandisha dau la pesa kwa mtu atakaye saidia
kumpata mke wake ambaye inavyo sadikika
ametekwa wa watu ambao hawajulikanina
hapakuwa na kikundi chochote cha kigaidi
ambacho kimejitokeza na kudai kwamba
wamehuzika na tukio hilo la utekaji.
"Muheshimiwa ni kwanini umeamua uamuzi kama
huu"
Priscar aliuliza baada ya kipande cha taarifa ya
habari kumalizika, kikiwa kimemuonyesha raisi
Praygod akitoa ahadi kwa watu watakao msaidia
kumpata mke wake. Kwa muonekano afya ya raisi
Praygod imepungua sana, hadi kupelekea kuanza
kuonekana kama mzee wa makamo. Rahab
hakujibu chochote zaidi ya kumtazama Priscar.
Rahab akanyanyuka mwenye kiti alicho kalia katika
hotel moja maarufu jijini Dar es Salaam ijulikanayo
kama Kilimanjaro Classic. Akafungua pazia zito
lililopo ndani ya chumba cha gorofa ya tano
kwenda juu. Akatazama jinsi mataa ya baadhi ya
nyumba za karibu na hoteli hiyo zinavyo waka.
"P hujui ni kitu gani alicho nifanyia mume wangu"
"Ni kitu gani alicho kufanyia?"
Machozi yakaanza kumwagika Rahab ambaye Mara
nyingi hakuhitaji kuweza kuikumbuka historia yake
ya nyuma.
"Nikiwa na miaka nane ndipo nilipo weza
kuitambua shida ni kitu gani"
Rahab alizungumza huku akiwa amempa mgongo
Priscar aliye kaa kitandani akisikiliza anacho
kizungumza bosi wake.
"Baba na mama yangu walikuwa ni watu wenye
uwezo mkubwa sana wa kifedha. Walikuwa ni
wamiliki wa miradi mingi sana hapa Tanzania,
ikiwemo hoteli mubwa kama hii."
"Mambo yalikuja kubadilika chini juu juu chini pale
mzee Makuya alipo weza kuingilia katika familia ya
baba yangu. Walikuwa ni marafiki sana na baba
yangu na walishirikiana katika mambo mengi.
Kipindi hicho mzee Makuya alikuwa ni mbunge wa
Dodoma"
Rahab akizungumza huku akijipangusa machozi
usoni mwake, akamgeukia Priscar ambaye
akastushwa baada ya kumuona bosi wake
akimwagikwa na machozi mengi. Akampatia
kitambaa Rahab aliye piga hatua na kukichukua
kisha akakaa kanywe kiti, akajifuta nachozi kisha
akaendelea kuzungumza.
"Mzee Makuya kipindi kama hichi aliweza kumkopa
baba yangu mamilioni ya mapesa kwa ajili
yankuendeshea kampeni zake za ubunge kwa
awamu ya pili.
"Bab alimpatia, alifanikiwa kupita huku kijana wame
Praygod akiwa amemiza chuo huko Marekani"
"Mzee Makuya aliweza kuchaguliwa waziri mkuu,
kutokana na mamlaka yake alianza kumfilisi baba
kisiri siri hadi baba akaparalaizi kwa mistuko
ambayo alikuwa akiilata kutokana na biashara
zame mufilisiwa na serikali pasipo sababu ya
msingi."
"Siri ilikuja mufichuka kwamba rafiki wa baba mzee
Makuya ndio alikuwa mfilisiji mkuj wa mali za
baba, huku kazi hiyo alikuwa akiifanya mwanae wa
kiume ambaye ni Praygod."
"Baba alifariki baada ya nyumba yetu tuliyo ishi
kupigwa mnada na banki wakidai baba alichukua
mkopo benki wa mabilioni ya mapesa wakati kwa
kinywa chair baba alikuwa anachukia madeni na
alishawahi kutuambia kaamba hawezi kukopa kwa
mtu akiogopa deni.
"Mimi na mama tulirudi kijijini kwao, ambapo
tulikimbilia huko baada ya kukosa pa kwenda.
Mzee Makuya alituma watu wake wakiongozwa na
Praygod kuja kumuua mama, ambapo walifanikiwa
kumuua mama, na bibi watu pekee ambao
walibakia kama ndugu kwangu yote him siri
isifichuke"
Rahab alipo fikia hapo machozi yakazidi
kumwagika, hasira ya maji dhidi ya Praygod ikazidi
kuwaka moyoni make.
"Nakumbuka Praygod ndio......ndio aliye mchinja
mama yangu na kichwa chake wakakipelek kwa
baba yake mzee Makuya."
Priscar akabaki akiwa amefumbua mdomo
akishangaa ukatili huo ukiwa umefanywa na raisi
Praygod anaye mfahamu. Akataka kumuuliza
Rahab ni jinsi gani yeye alipona ila akasita
kwanaza na kumuacha alie kwa uchungu hadi pale
atamapo kuwa tayari kuzungumza.
Rahab akajiwema sawa Misha akaendelea
kuzangumza.
"Mimi niliyaona matukio vote hayo nikiwa juu ya
dari lilololo chumbani kulipo tokea mauaji.
Niliweza kumkumbuka vizuri Praygod na sinto kuja
kumsahau. Hata ninavyo zungumza na wewe. Hii
hoteli ilikuwa ni yababa ila imebadiloshwa na kuwa
mali ya raisj Prarygod"
"Baba yake yupo wapi?"
"Sifahamu, laiti angekuwa amefariki basi
tungeweza kujua kifo cha waziri mkuu wa zamani,
ila haijatokea hivyo. Na sikuwahi kusikia siku
Praygod akizungumzia juu ya familia yeke ipo wapi
zaidi ya kusema ipo"
Priscar akashusha pumzi nyingi huku akionekana
kumsitikia bosi wake.
"Nilianza biashara ya kujiuza nikiwa bado binti
mdogo sana ili mradi nipate pesa ya kujikimu
kimaisha. Nilikutana na wanaume wengi cha
ku.shukuru Mungu sikuweza kuadhirika na ukimwi,
ila nilazima niweze kumteketeza Praygod na familia
yeke yote"
***
Agnes nawezake wakafika katika kambia ya mzee
Godwin, hata wenyewe hawakuamini kwa mapokezi
ambayo wamepokewa. Wamechukuliwa kama watu
wa muhimu sana kwenye kambi hiyo. Kitu cha
kwanza muhimu kufanyiwa ni juu ya afya zao.
Madaktari ambao wapo kwenye ngome hiyo
walijitahidi kuifanya kazi yao kiufasaha kuhakikisha
afya za mabinti hao zinakuwa imara. Kadri siku
zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi afya zao zilivyo
zidi kuwa nzuri sana, uzuri wao ukarejea kwa kasi
ya ajabu, si Fetty, Anna wala Halima walio acha
kusiwfiwa na wanaume wa ngome hiyo kwamba
wao nj wazuri zaidi na zaidi.
Baada ya afya zao kuwa fiti kabisa, wakaanza
kufanya mazoezi magumj ya kuwaweka sawa. Kila
mmoja alijitaidi kuitumia nafasi aliyo ipata
kuhakikisha kwamba harudii makosa kama waliyo
wahi kuyafanya kipindi walipo kuwa watumishi wa
bwana Rusev. Hasira yao wote wakaigeuzia kwa
bwana Rusev aliye sababisha maisha yao
kuharibika kwa kiasi kikubwa na asinge mubwa
Mzee Godwin basi wao wangefia gerezani kwani
kila mmoja alisha kata tamaa ya maisha kutokana
na vipigo na manyanyaso waliyokuwa wakiyapata
kutoka kwa wanajeshi hao wakimarekani.
Kikosi chao kikazidi kuongezeka nguvu, huku
Jaquline akiwa mwalimu kwenye baadhi ya
mazoezi. Manka hakuwa nyuma kuhakikisha
kwamba watanzania wezake hao wanafanikiwa
katika mpango mzima wa kumsambaratisha adui
yao, kisha watajua ni nini kinacho fwata katika
maisha yao ya badae.
"Mkuu unafikiria nini juu ya hawa mabinti?"
John limuuliza mzee Godwin wakiwa wamekaa
sehemu ya juu kidogo ya gorofa wakiwa
wanawatazama Manka na wezake wakifanya
mazoezi ya kufa mtu.
"Wamekamilika kisawa sawa"
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa
ametabasamu.
"Ila mpango wao wanao taka kuufanya ni mkubwa
sana ambao utapelekea maisha yao hatarini."
"John kila kitu tunacho kifanya kwenye haya
maisha ni hatari. Kwahiyo usiiogope hatari, cha
kujipanga sasa hivi nikuhakikisha kwamba
ninakuwa raisi wa Tanzania"
John akabaki kimya akimtazama mkuu wake anaye
zidi kuisuka mipango kuhakikisha kwamba
anakuwà raisi wa Tanzania siku za usoni.
***
Kwa kitako cha bunduki alicho pigwa Briton
maeneo ya kichwani, kikamfanya kupoteza fahamu
asitambue ni wapi anapo pelekwa. Ubaridi mkali
wa maji aliyo mwagiwa mwilini mwake huku akiwa
hana guo hata moja, ukamstua kutoka katika
usingizi wa nusu kifo. Mikono yake iliyo chanukiwa
na kufungwa kila upande, kukamfanya azidi kupata
maumivu makali, kwani mwili wake bado umejawa
na maumivu mengi sana ya vipigo vikali alivyo
pewa n wapelelezi wa Tanzania.
Miguu yake nayo imechanuliwa na kufungwa kila
mmoja upande wake. Kwa jinsi alivyo kaa ni kama
ngozi iliyo wambwa kwenye miti ikisubiriwa
kukaushwa na mwanga wa jua. Msichana mrefu
kiasi aliye jazia maeneo ya kiunoni mwake na
kumfanya aonekane na hispi za kutamanisha,
alimtazama Briton anaye zidi kugugumia kwa
maumivu. Pembeni ya binti huyo wamesimama
wanaume wawili wenye bunduki aina ya SMG. Sura
zao zinaonyesha kwamba hao ni wanaume wa kazi
ambao hawahitaji mchezo pale linapo kuja swala la
kazi.
Msichana huyo mrembo mwenye sura nzuri ya
kuvutia, akamsogelea Briton karibu. Kwa kutumia
kucha zake za mkono wa kushoto zilozo ndefu,
akaanza kuzipitisha mwilini mwa Briton huku
akizunguka kumtazama mbele ya nyuma. Bila hàta
ya aibu akamshika Briton sehemu zake siri na
kuanza kuziminya minya.
Hakuishia hapo akazunguka kwa nyuma na kuanza
kuyaminya minya makalio ya Briton aliye jitahidi
kujitingisha asishikwe ila haikuwa rahisi kwa
msichana huyo kumuachia. Zaidi akajikuta makalio
yake yakigeuza kama ngoma, kwani vibao kadhaa
vilitua kwenye makalio hayo.
"Una matako mazuri"
Msichana huyo alizungumza huku akiyafikicha
fikicha makalio ya Briton aliye jikuta akipiga kelele.
Kwa lafudhi ya msichana huyo moja kwa moja,
Briton akatambua kwamba msichana huyo ni
Mkenya.
"Unanifanyaje wewe malaya"
Briton alizungumza huku akiwa amekasirika sana.
Cha kushangaza msichana huyo akayashika
makalio ya Briton na kuyachanua na kuyatazama
katikati. Akatingisha kichwa kisha akayaachia.
"Huyu bado yupo sildi, hajaguswa"
"Anafaa madama"
"Ndio anafaa"
Moyo wa Briton ukapasuka na kuanza kumuenda
mbio alipo yasikia mazungumzo hayo, kitu
ambacho anakiogopa kwenye maisha yake yote ni
kuingiliwa kinyume na maumbile tena na
mwanaume mwenzake. Akazidi kutolea jicho
msichana huyo aliye simama mbele yake kwa
mara nyingine, akajikuta sehemu zake za siri
zikianza kuchezewa na msichana huyo.
"Kamleteni na yule"
Msichana huyo alitoa amri, kwa haraka akili ya
Briton ikamfikiria Shamsa baada ya kumsikia yule.
Jamaa mmoja akatoka na baada ya dakika tano
akarejea na msichana mweusi sana, ila mwenye
umbo matata lenye vigezo vya kila aina. Msichana
huyo aliye valia nguo za ndani tu(chupi na sidiria).
Akasimamishwa mbele ya Briton.
"Mnyonye huyo"
Msichana huyo alipewa amri, ila akasita kidogo.
Bunduki moja nyuma yake ikakokiwa kuashiria
akikatàa atamwagwa ubongo wake kwa risasi.
Taratibu akamsogelea Briton, akaushika uume wa
Briton na kuudumbukiza mdomoni mwake na
kuaanza kuunyonya taratibu jambo lililo zidi
kumkera Briton.
***
Shamsa akayafumbua macho yake na kuanza
kuchunguza ni wapi alipo ila akashindwa kutambu
yupo wapi, kwani chumba hicho hakikuwa na
viashiria vyoyote kwamba yupo wapi. Taratibu
akakaa kitandani hapo, hata kabla dakika moja
haijapita mlango wa chumbani kwake
ukafunguliwa. Macho yake yakatua usoni mwa
bwnaa Mohamed Abdulah anaye mtambua kama
baba yake mdogo wa kumlea.
Tabasamu la bwana Mohamed Abdulah, likamfariji
Shamsa na kujikuta na yeye akiachia tabasamu
pana usoni mwake. Bwana Mohamed Abdukah,
akachanua mikono yake na Shamsa kwa haraka
akashuka kitandani na kumkumbatia bwana
Abdulah. Machozi ya furaha yàkaanza kumbubujika
Shamsa. Hakuamini kwamba amerudi kwenye
familia yake ambayo aliiona mbaya alipo kuwa
mikononi mwa Eddy aliye fariki dunia. Kutokana
hakuwa na pakwenda, matumaini yake ya kuishi
sehemu salama kwa maisha yake ikarejea upya.
"Ulikiwa wapi mwanangu?"
Bwana Mohamed Abdulah alizungumza huku
machozi yakimlenga lenga.
"Am sorry dady"(Samahani baba)
Shamsa alizungumza na kuzidi kukumbatia bwna
Mohamed Abdulah na kumfanya azidi kumwagikwa
na machozi. Baada ya muda wakaachia, Shamsa
akaanza kumuelezea bwana Mohamed Abdulah kila
kitu kilicho tokea kwenye maisha yake na malezi
ambayo aliweza kuyapata kwa kipindi chote cha
nyuma. Katika swala la Eddy kufariki dunia likazidi
kumuumiza Shamsa na kujikuta akikwama kwama
kuendelea kuzungumzia kifo cha Eddy.
Ila ukwi wa jambo hilo bwana Mohamed Abdulah
analifahamu kwa asilimia mia moja kwani kijana
ambaye alivaa sura kama ya Eddy ametoka kwenye
kambi yake, likiwa ni wazo la rafiki yake mzee
Godwin anaye wasaidi kwa mambo mengi kikosi
chake.
Usiku wa siku hiyo sherehe kubwa ikafanyika ya
kumkaribisha nyumbani Shamsa aliye potea kwa
kipindi kirefu. Risasi nyingi zikapigwa hewani ikiwa
ni kama ishara ya kushangilia. Shamsa akazidi
kujiona ni muhimu sana. Ila furaha yake
haikukamilika kwani hakuweza kumuona Briton na
alipo uliza hakupewa jibu la maana, wasiwasi
ukaanza kurejea upya moyoni mwake
***
Eddy akafika nchini Japan majira ya asubuhi akiwa
katika ndege ya shirka la Japan Airline. Ndege
hiyo iliyo fikizia kwenye uwanja wa kimataifa wa
'HUB'. Eddy pamoja na abirka wengine wamashuka
wakaingia kwenye basi ambalo liliwapeleka karibu
kabisa na eneo ambalo abiria wanatokea. Eddy
taratibu akapanga foleni ya kutokea nje, huku kila
abiria akikaguliwa kutoka kwenye uwanja huo.
Ikafika zamu yake ambapo akampatia dada mmoja
mkaguzi hat yake ya kusafiria{Passport). Dada
huyo akaipitisha kwenye mashine maalumi,
akayanyanyua macho yake na kumtazama Eddy
kwa umakini. Dada huyo akanyanyua simu yake na
kuzungumza kijapani ambacho Eddy hakukielewa,
gafla Eddy akaona kundi la polisi likimfwata wakiwa
na mbwa pamoja na bundiki. Kwa mara ya kwanza
alipo watazama alijifariji labda kuna mtu wanaye
mfwata tofauti na yeye. Ila kadri walivyo zidi kuja
ndivyo wakivyo zidi kumlenga yeye huku macho
yao yote wakimtazama, na ndani ya dakika wakawa
wamemzingira Eddy na kumuweka kati, asitambue
sababu ni nini ya askari hao kumzunguka.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 43 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (43)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Eddy taratibu akapanga foleni ya kutokea nje, huku
kila abiria akikaguliwa kutoka kwenye uwanja huo.
Ikafika zamu yake ambapo akampatia dada mmoja
mkaguzi hati yake ya kusafiria{Passport). Dada
huyo akaipitisha kwenye mashine maalumu,
akayanyanyua macho yake na kumtazama Eddy
kwa umakini. Dada huyo akanyanyua simu yake na
kuzungumza kitu ambacho Eddy hakukielewa, gafla
Eddy akaona kundi la polisi likimfwata wakiwa na
mbwa pamoja na bundiki. Kwa mara ya kwanza
alipo watazama alijifariji labda kuna mtu wanaye
mfwata tofauti na yeye. Ila kadri walivyo zidi kuja
ndivyo wlivyo zidi kumlenga yeye huku macho yao
yote wakimtazama, na ndani ya dakika wakawa
wamemzingira Eddy na kumuweka kati, asitambue
sababu ni nini ya askari hao kumzunguka.
ENDELEA
Karibia watu wote walio Karibia na eneo hilo,
macho yao waliyelekezea eneo walipo simama
askari pamoja na Eddy aliye wekwa kati.
"Upon chini ya ulinzi"
Askari mmoja alizungumza kwa lugha ya kingereza
na kumfanya Eddy amkodolee macho pasipo
kuelewa haswa ni nini kosa alilo litenda hadi
akamatwe.
"Kwa kosa gani?"
"Una haki ya kukaa kimya, na si kuuliza maswali.
Mpigeni pingu mpelekeni chumba cha mahojiano"
Kutokana na kuziheshimu sheria za nchi hiyo
ambazo ni kali kwa waalifu wake, Eddy akakubali
kipigwa pingu mikononi mwake. Hakuhitaji askari
hao wamsumbue, kwa mwendo wa taratibu
wakatembea kuelekea katika chumba cha
mahojiano.
Begi la Eddy likawekwa juu ya meza aliyo ikuta
ndani ya chumba hicho. Wakaanza kulipekua,
wakakuta nguo pamoja na pesa ambazo Eddy
alihitaji kuzitumia akiwa katik nchi hiyo. Cha
kushangaza aksari hao watano wakagawana pesa
yake pasipo kumueleza Eddy jambo lolote.
"Hembu niambieni basi kwa nini mumenikamata?"
"Utajua muda mchache ujao ni kwanini
tumekukamata wewe kaa kimya"
Ikamlazimu Eddy kubaki kimya. Hazikupita dakika
nyingi akaingia mwanamama mweusi aliye panda
juu kiasi.
"Mambo Eddy"
Mwanamama huyo alitabasamu huku akivuta kiti
na kukaa. Eddy akajaribu kuvuta hisia zake ni wapi
alipo muona mwana mama huyo, ila hakupata
kumbukumbu yoyote kwenye kichwa chake,
isitoshe mwana mama huyo anazungumza
kiswahili vizuri ikiashiria kwamba yeye ni muafrika
tena Mtanzania.
"Mimi ni balozi wa Tanzania hapa Japana ninaitwa
mama Ngoi"
"Wewe ndio umeagiza nikamatwe?"
"Hapana ila ni amri kutoka iku. Unatakiwa uweze
kurudi nyumbani ukaendelee na majukumu yako
ya kikazi"
Eddy akatabasamu kwa kejeli. Akamtazama mama
huyo kuanzia kichwani hadi kwenye tumbu,
sehemu ya chini ya mwili wake hakuweza kuiona
kutokana na kuzibwa na meza kwa chini.
"Kazi eheeee?"
"Ndio nchi ipo hatarini na katika vitisho vya
kulipuliwa kwa bomu la nyuklia. Wewe ndio unaye
hitajika kurudi katika nafasi yako ya uwaziri.
Matukio ya kijambazi yanatokea kila kukicha,
isitoshe hata mke wa raisi mwenyewe ametekwa
inapata miezi minne sasa"
Eddy akastuka kusikia Rahab ametekwa, akajiuliza
maswali kadhaa kichwani mwake. Ila hakuhitaji
kuonyesha mstuko wake huo kwa maana
anatambua kwamba huo ni uongo kwa Rahab
kuweza kutekwa.
"Nisikilize mama. Sina kitu nilicho kibakisha
Tanzania. Sina familia sina chochote kwa hiyo
sihitaji kurudi. Tafadhali waambie kuwa sihitaji
kurudi Tanzania"
"Tayari maandalizi ya kukurudisha Tanzania
yanaendelea huko nje ya uwanja wa ndege.
Tafadhali hii ni kwaajili ya usalama wako na nchi"
"Hembu kwanza nifungulieni hizi pingu. Hauwezi
kuzungumzw eti na kiongozi wako ukiwa
umenifunga pingu kama muhalifu"
Ushawishi huo wa Eddy ukamfanya mama huyo,
kumuamrisha askari mmoja kufungua pingu za
Eddy pasipo kufahamu kwamba ana dili na mtu wa
aina gani. Akili ya Eddy ikafanya kazi haraka
haraka akifikiria kashfa mbaya inayo endelea ndani
ya Tanzania kwamba yeye ni gaidi aliye teka jengo
la Mlimani City. Moja kwa moja akatambua kitendo
cha yeye kurudi Tanzania nikwenda kuhukumiwa.
Kifungo cha maisha kwani mauaji aliyo yaona ni
makubwa sana. Kazi yake ikaanza kufikiria ni jinsi
gani anaweza kutoroka pasipo kujua ataoroka vipi
ikiwa yeye bado ni mgeni katika nchi ya Japan.
***
Kitendo cha Briton kuendelea kunyonywa uume
wake, kilizidi kumkera ila kwa jinsi biti huyo
anavyo zidi kumnyonya ndivyo jinsi alivyo jikuta
mwili ukimsisimka hadi uume wake ukasimama
kabisa. Cha kushangaza Dada huyo wa kikenya
akaanza mushangilia akiamini mambo yake
yanazidi kuwa mazuri. Akamuamrisha msichana
huyo kuondolewa katika chumba hicho na kubaki
yeye na Briton. Dada huyo pasipo kuwa na aibu,
akaanza kujnyonya uume wa Briton, akazidi
kwenda mbali na hapo kwani akaanza kufanya
ngono na Briton pasipo ridhaa yake. Hasira ya
Briton ilizidi kumpanda ila hakuwa na uwezo wa
kufanya jambo lolote kwajinsi alivyo fungwa
hakuweza kufanya jambo lolote.
Dada huyo alipo maliza matakwa yake,
amawaamuru watu wake kumfungulia Briton,
wakambeba mzoga mzoga hadi ndani ya chumba
kimoja kikubwa, ambapo Briton akamuona mzee
wa makamo mwenye miaka kati ya arobaini na
tano hadi hamsini na tano akiwa amesimama na
bomba la sindano, huku akiwa amevalia koti jeupe
ikiashiria kwamba huyo ni daktari. Briton akiwa
ameshikiliwa hivyo hivyo na majamaa hayo yaliyo
gawanyika kwa misuli mingi. Akachomwa sindano
ya shingoni, ndani ya dakika mbili mbeleni,
usingizi mzito ukamchukua na kulala fofofo asijue
ni nini kinacho endelea.
***
Majira ya saa kumi na mbili jioni. Barabara ya
kuelekea mikoni, kuanzia Ubungo na kwenda
mbele maeneo ya kimara zote na mbezi mwisho.
Imetulia huku askari wa usalama barabarani,
wakifanya kazi ya kusimamisha magari yote
yanayopita katika barabara hiyo. Wakazi wengi
wanao itumia barabara hiyo walisikika wakilaani
kitendo hicho ambacho kinawachelesha wengi
wanao toka makazini, wamisubiria msafara wa raisi
uweze kupita.
Foleni ikazidi kuwa kubwa kiasi cha magari yanayo
tokea, Kariakoo, Mwenge na Tabata kushindwa
kwenda. Ving'ora vya pikipiki za polisi pamoja na
magari hayo vikaanza kusikika jirani kabisa na
mataa ya Ubungo yalipo. Wananchi ambao
walikuwa wamechukia walijikuta wakichomoza
vichwa vyao kwenye magari kutazama msafara huo
ambao mara nyingi husifika kwa gari zake kwenda
kasi na katika mtindo wa kupanua barabara.
"Raisi jioni hii anakwenda wali?"
Mmoja wa wananchi alisikika akimuuliza mwezanke
wakiwa ndani ya basi lao dogo linalo tokea
kariakoo.
"Mmmm nitajulia wapi ndugu yangu wakati hata
ikulu yenyewe sipajui"
Magari hayo yakazidi kupita kwa mwendo wa kasi
huku askari aliye simaama kwenye eneo hilo la
mataa akiyaelekeza magari hayo yanapo hitajika
kwenda. Msafara huo wenye magari kumi na saba,
ukapita ila gari nyengine yenye namba za ikulu,
ikiwa imewasha taa zake ikaongezeka kataka
msafara huo na kuongeza idadi ya magari na
kufikia kumi na nane.
"Mkuu gari zinatakiwa kuwa ngapi?"
Askari huyo wa usalama barabarani alizungumza
kwa simu yake ya upepo akimtaarifu kiongozi wa
msafara, baada ya kuitilia shaka gari hiyo iliyo
ongezeka.
"Kumi na saba. Over"
"Kuna gari moja ya ikulu imeongezeka
muheshimiwa. Una taarifa nayo?"
"Hapana, tutaichukulia uangalizi. Over"
Askari huyo akaanza kuruhusu gari za abiria na
wananchi wa kawaida kuendelea na safari zao.
"Madam nimesha jiunga kwenye msafara"
Priscar alizungumza na Rahab kulitia simu ya
mkononi.
"Umestukiwa?"
"Sidhani, kwa maana niliuwahi msafara"
"Poa kila kitu kinakwenda kwenye mlango"
"Sawa madam"
Simu ikakatwa na Priscar akazidi kuongeza
mwendo kasi wa gari yake.Taarifa ya kuongezeka
kwa gari katika msafara wa raisi. Akielekea katika
handaki alilo pata habari kwamba mke wake ndipo
alipo shikiliwa. Ikaanza kumchanganya, madereva
wote taarifa hiyo wakawa nayo. Mchezo walio
ufanya ni wote kutanua barabara, kisha gari ya
Raisi Praygod Makuya, ikapita mbele kwa mwendo
wa kasi kisha hizi nyingine zikaziba kwa nyuma
jambo lililo amza kumpa wasiwasi Priscar.
***
Kutokana na nguvu aliyo kuwa nayo kwenye kikosi
cha Al-Shabab, Shamsa akamuomba bwana
Abdulah Mohamed kuanzisha oparesheni ya
kumtafuta Briton. Hakuficha chochote kwa bwana
Abdulah Mohamed. Akamuelezea hisia za mapenzi
ambazo anazo kwa Briton.
Vikosi vya kigaidi vya kundi hilo vikiongozwa na
Shamsa, akiwa amerudi upya kwenye kazi hiyo
kwa lengo la kumtafuta mpenzi wake. Vikaanza
oparesheni ya kuteka meli ambazo zinakatiza
katika ukanda wa Somalia. Kila meli iliyo kamatwa
ilifanyiwa upekuzi wa mu mmoja baada ya mwengi.
Kuhakikisha wanamtafuta Briton kwa udi na
uvumba. Zoezi hilo lilizidi kudumu takribani
mwenzi mzima, ila hakufanikiwa kuweza kumtia
machozi Briton. Wazo la Briton kufa maji likaanza
kutawala moyo wake na akili. Kumbukumbu ya
ajali waliyo weza kuipata kipindi walipo kuwa
wanatoroka. Ikazidi kumuogopesha. Unyonge
ukaanza kumtawala na kujiona ni msichana asiye
na bahati. Muda mwingi akawa anautumia katika
kunywa pombe kali na kulewa chakari. Hali hiyo
ikazidi kumsikitisha bwana Abdulah Mohamed.
Ikamlazimu kumtafutia Shamsa madaktari wa
saikolojia kutokea Japan. Madaktari hao baada ya
kumfanyia Shamsa uchunguzi wa kina
wakatambua, akili yake inakwenda
kuchanganyikiwa kwa ajili ya mapenzi.
Wakamuomba bwana Abdulah Mohamed,
kumruhusu Shamsa waende naye Japan kwa ajili
ya matibabu. Ombi hilo kwa mara ya kwanza
likawa gumu sana kwa Bwana Abdulah Mohamed.
Ila kwa jinsi ali ya Shamsa ilivyo zidi kuwa mbaya
hadi kiafya ikamlazimu kumruhusu waondoke naye,
ila akiwa na walinzi wangine wawili wakike. Kwa
usafiri maalumu wa ndege ya Jeti ya kifahari inayo
milikiwa na kikundi hicho ikaanza, kuelekea Japan.
***
Eddy hakuhitaji kufanya makosa ya kurudi
Tanzania kwa wakati huo. Akawatazama askari
waliomo ndani ya kiwanja cha ndege hiyo.
"Naomba niende haja ndogo"
Eddy alimuomba Mama Ngoi ambaye yupo na
baadhi ya askari wa Japan pamoja na Tanzania
wanao mlinda. Eddy akasindikizwa hadi chooni na
askari wawili wa kijapan ambao walibaki nje ya
mlango kumsubiri. Eddy akakuta vijana wawili
masharo baro waliomo ndani ya choo hicho,
kutokana hakuwa na haja ya kwenda kwenye haja
zinazo takiwa kufanyika chooni. Alicho kifanya,
nikuwasogelea vijana hao walio simama kwa
pamoja wakikojoa katika sehemu mbili maalumu
zinazo fanana. Pasipo kuwauliza akawapiga
maeneo ya nyuma ya shingoni kwa kutumia
viganga vyake vilivyo komaa kwa mazoezi.Vijana
hao wakapoteza fahamu. Kwa haraka Eddy akaanza
kumvua nguo mmoja wao. Akazivaa akachukua
koti la mmoja wao na kulivaa vizuri, akachukua na
kofia iliyo mficha vizuri sura yake.
Alipo jitizama kwenye kioo akatabasamu kwani,
amebadilika kwa kiasi kikubwa na si rahisi kwa
askari alio waacha nje ya mlango kumtambua.
Akajipapasa kwenye mifuko ya nguo za kijana aliye
mchukulia nguo. Akakuta noti mbili za dola mia
mia za kimarekani. Akampapasa mwengine na
kumkuta na yen kumi, pesa ya kijapani.
Pasipo kupoteza muda akatoka katika choo hicho
na kuwakuta askari wakiendelea kumsubiria.
Akawapita kwa kujiamini, askari hao wala haku
shuhulika naye waliendelea kupiga stori zao.
Eddy akatoka nje ya uwanja wa ndege, jambo lililo
muumiza kichwa ni hati yake ya kusafira. Hakujua
ataishi vipi ndani ya nchi hiyo kwani akihitaji kulala
kwenye hoteli nilazima kuonyesha hati ya kusafiria.
Kitu kilicho zidi kumuumiza akili zaidi na zaidi ni
kijitabu chake kidogo ambacho kina maelekezo
yote ya sehemu ambayo anatakiwa kwenda.
Akakta taksi iliyo mfwata hadi sehemu alipo
simama. Akafungua mlango wa nyuma wa taksi
hiyo ikaondoka.
"Nipeleke kwenye baa yoyote nzuri"
"Sawa"
Safari haikuchukua muda mrefu, taksi hiyo
ikasimama mbele ya gorofa moja refu. Eddy
akamlipa dereva kiasi alicho kihitaji, akashuka na
kuingia ndani ya gorofa hiyo ambapo kwa
maandishi makubwa ya kijapani yaliyo andikwa nje
hakuweza kujua inaitwaje, ila kwa wingi wa watu
wanao ingia na kutoka katika baa hiyo kubwa,
hakuwa na wasiwasi wa aina yoyote.
Nusu saa, lisaa askari hao wakijapan walibaki nje
ya mlango wa kuingia katika choo hicho. Wakaanza
kupatwa na wasiwasi, kwani mtu waliye ambiwa ni
kiongozi mkubwa nchini Tanzania, hajutoka ndani
ya choo hicho. Ubaya hawakujua ni nini kilicho
endelea kwani waliwazuia watu walio kuwa
wakihitaji kuingia ndani ya choo hicho pasipo
kujua mtu wanaye msubiri ni muda mrefu alisha
ondoka katika eneo la Air port.
Ikabidi askari mmona kufungua mlango wa chooni
hapo, akaingia ndani na kuwakuta vijana wawili
wakiwa wamelala chini huku mmoja wao akiwa
amebakiwa na nguo ya ndani. Huku nguo za Eddy
wakizikuta zikiwa zimetupwa chini. Kwa haraka
akawasiliana na mkuu wao. Haraka haraka
wakafika ndani ya choo wakiongozana na Mama
Ngoi.
"Imekuaje mukamlotezaaa?"
Mama Ngoi alizungumza huku akifoka kwa hasira,
hapakuwa na jibu la kueleweka kwa askari walio
kabaidhiwa jukumu la kumlinda Eddy.
***
Mpango wa Raha kumuua raisi Praygod
ukakamilika. Kitu cha kwanza kukifanya ni kuweza
kumtafuta kijana mmoja wa mtaani, akamuambia
apige simu ikulu, huku akimpatia namba ya simu
ya Raisi. Kijana huyo pasipo kujiuliza mara mbili
mbili, kutokana amekabidhiwa kitita cha laki moja.
Akaifanya kazi hiyo majira ya saa kumi na mbili
kasoro jioni. Akiwa lembeni ya Rahab aliye valia
sura ya bandia.
Kijana huyo aliye jitambulisha kwa jina la Ommy.
Akamueleza Raisi Praygod kwamba ameona eneo
ambalo mke wake amefungiwa, kwenye moja ya
handaki lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Raisi Praygod akaitisha kikao cha dharura na
wakuu wa upelelezi, akaamrisha msafara wa
kueleke nje ya jiji, uandaliwe. Baadhi ya wakuu wa
usalama wakamsihi asiendee, aache vijana
waelekee kwenye eneo hilo. Ila Raisi Praygod
hakuhitaji kusikiliza la mtu. Amri yake
ikatekelezwa, akaingia kwenye magari yaliyo
andaliwa kwa safari hiyo. Huku mengi yakiwa
yamejaa makachero kutoka katika usalama wa
taifa.
Kwa jinsi gari la raisi lilivyo tangulia mbele,
likaanza kumpa hofu raisi Praygod. Akatoa amri
gari ya nyuma inayo wafwata iweze kuzuiwa mara
moja, kisha gari chache ziendele na safari hiyo.
Gari mbili za nyuma zenye makachero wanne
wanne katika kila gari zikapunguza mwendo gafla,
Priscar akajikuta akifunga breki za gafla asizigonge
gari hizo.
Makachero hao walio valia suti nyeusi, wakajirusha
kutoka ndani ya magari yao, wakiwa wamevalia
suti nyeusi. Pasipo kuchelewa wakaanza
kulishambulia gari la Priscar kwa risasi zisozo na
idadi. Kwa bahati mbaya Priscar akiwa katika
harakati za kuirudisha nyuma gari hiyo. Risasi
moja ikampiga begani na kujikuta akipoteza
kontroo ya gari na likadumbukia kwenye mtaro
uliopo pembezoni mwa barabara, nakuwapa nafasi
makachero hao kulisogelea gari lake wakiwa na
bastola zao mikononi.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 44 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (44)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Makachero hao walio valia suti nyeusi, wakajirusha
kutoka ndani ya magari yao, wakiwa wamevalia
suti nyeusi. Pasipo kuchelewa wakaanza
kulishambulia gari la Priscar kwa risasi zisozo na
idadi. Kwa bahati mbaya Priscar akiwa katika
harakati za kuirudisha nyuma gari hiyo. Risasi
moja ikampiga begani na kujikuta akipoteza
kontroo ya gari na likadumbukia kwenye mtaro
uliopo pembezoni mwa barabara, nakuwapa nafasi
makachero hao kulisogelea gari lake wakiwa na
bastola zao mikononi.
ENDELEA
Wananchi waliopo eneo la karibu na gari la Priscar
lilipo angukia, wakajikuta wakikimbia ovyo
kuyaokoa maisha yao kwani hapakuwa na
mwananchi aliye zoea milio ya risasi, wala kujua ni
jambo gani ambalo linaemdelea. Makachero hao
wakazidi kulisogelea gari la Priscar wakiwa makini
sana. Kila hatua waliyo ipiga macho yao yalikuwa
ndani ya gari hilo wakijaribu kumtazama mtu
wanaye mshambulia ni nani.
Machozi ya maumivu yakaanza kumtiririka Priscar
mashavuni make, hakuamini kwamba anakwenda
kutiwa nguvuni na makachero wa serikali. Hakujua
ni kitu gani atazungumza kujitetea pale ambapo
atajulikana kama yeye ni mlinzi wa mke wa raisi
wanaye mtafuta kwa kipindi chote.
Ukunga mkali wa maumivu ukamtoka mmoja wa
makachero, akaanguka chini jambo lililo wastua
wezake na kujikuta wakigeuka nyuma kutazama
kilicho mpata mwenzao huyo, wakamkuta akitokwa
na damu nyingi shingoni zikiruka mithili ya maji
yanayotoka kwa kasi katika bomba la askari wa
kikosi cha zihma moto.
***
Eddy akatafuta sehemu yenye maficho kwenye baa
hiyo yenye watu wengi akakaa, kusikilizia hali
inayo endelea huko nje kwani anaamini ni lazima
msako wa yeye kutafutwa utaendelea. Kutokana
hakuwa ni meejeji sana wa vyakula wanavyo tumia
wajapani, ikamlazimu kuagiza bia ili mradi asafishe
koo lake. Akiwa anaendelea kusubiria kinywaji
alicho agiza. Msichana mrefu wa kijapani aliye valia
kisketi kifupi cheusi na sidiria. Akasimama mbele
ya meza yake huku akijishika shika kifuani mwake
ikiwa ni ishara kwamba yupo kimaslahi ya
kimapenzi.
Eddy akatabasamu kisha akachomoa noti moja ya
yen kumi na kumpa binti huyo, kwa ishara ya
mkono akamuomba aondoke eneo hilo kwani
hamuhitaji kimapenzi. Binti huyo hakuamini
kukabidhiwa kiasi hicho cha pesa kwani kwake ni
kikubwa sana. Ila kilicho mshangaza ni uzuri wa
kijana huyu mweusi akionekana ni mzaliwa wa bara
la Afrika japo hakujua ni nchi gani ametoka.
Bia ya Eddy ikaletwa akaendelea kuinywa taratibu
taratibu. Kitu kilicho anza kumuumiza kichwa ni
kuikumbuka sehemu ambayo anatakiwa kwenda.
Binti huyo baada ya kuachana na Eddy akaamua
kurudi katika chumba ambacho kimetengwa
maalumu kwa machangudoa wote wanao jiuza
ndani ya baa hiyo. Akavalia nguo zake za kawaida.
Akawaaga wezake kwamba anakwenda kumtazama
bibi yake hospitali.
Moyoni mwa msichana huyo wa kijapani alijawa na
furaha kwani biashara hiyo ya kujiuza anaifanya
kutokana na hali ngumu ya maisha. Akafika nje ya
baa hiyo. akatembea hadi kwenye maegesho ya
magari akafika hadi kwenye kagari kadogo aina ya
Vitz. Kabla hajafungua mlango askari wawili
wakamfwata na kumsimamisha.
Mmoja wao akatoa simu mfukoni na kumuonyesha
picha ya Eddy.
"Unamfahamu huyu?"
Binti huyo akastuka kidogo, ila akajitahidi kuuzuia
wasiwasi wake. Akatingisha kichwa pasipo
kuwajibu akimaanisha kwamba hamfahamu mtu
huyo. Askari hawakuwa na lakufanya zaidi ya
kuindoka na kuelekea ndani ya baa huyo
wakiendelea kumtafuta Eddy kwani picha yake
ilisha tumwa kwa kila askari ndani ya Japan
wakimtafuta kama muhamiaji aliye ingia ndani ya
nchi hiyo pasipo kuwa na hati ya kusafiria na
hakuna askari aliye ambiwa kwamba Eddy ni waziri
nchini Tanzania.
Binti huyo akasimama kwa sekunde kazaa njee ya
mlango wa gari lake huku akijishauri kuondoka au
akamtaarifu mwanaume aliye mkarimu kwake. Kwa
haraka akaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya
baa hiyo. Akatazama sehemu alipo kuwa amekaa
Eddy hakuweza kumuona, katika kutazama tazama
akawaona askari hao wakiendelea kuwauliza watu
wengine nani ya baa hiyo. Wasiwasi mwingi
ukamjaa hakujua ni wapi alipo kijana huyo. Kwa
haraka akaelekea nje ya kutazama kama kijana
huyo atakua ametoka ila hakumuona. Gafla watu
wakaanza kutoka ndani ya baa hiyo wakikimbia
wengine wakipiga mayowe, ikamlazimu binti huyo
kurudi tena ndani kuangalia ni kitu gani kinacho
wakimbiza watu.
Akamkuta kijana huyo akimalizia kumpiga teke
moja askari lililo muangusha chini huku mwengine
akiwa amelala juu ya meza iliyo vunjika. Macho ya
Eddy yakakutana na binti huyo akionekana
kumshangaa, bila kujali binti huyo akamuita Eddy
aliye mfwata bila kujiuliza. Wakatoka kwa kukimbia
wakaelekea kwenye maegesho ya magari wakaingia
kwenye gari la binti huyo wakaondoka katika eneo
hilo la baa.
***
Macho ya Shamsa yakatua kwenye picha kubwa ya
Eddy iliyo onyeshwa kwenye moja ya Tv kubwa
iliyopo kwenye uwanja wa ndege alio fikia nchini
Japan.
"Most wanted?"(Anatafutwa?)
Shamsa alijiuliza huku akisimama kwenye benchi
alilo kuwa amekalia. Huku macho yake yakiyasoma
maandishi madogo yaliyo andikwa kwa lugha ya
kingereza yanayopita kwenye taarifa inayo
tangazwa kwa lugha ya kijapani.
"Ina maana Eddy hajafa?"
Shamsa alijiuliza ila hakupata jibu ikaonyeshwa
kipande kidogo cha video kilicho rekodiwa na
camera za ulinzi zilizo kuwa kwenye uwanjaambao
Eddy alifikizia.
"Mbona unashangaa?"
Faktari wa Shamsa alimuuliza baada ya kumuona
anaikodolea macho Tv kubwa iliyopo mbele take.
"Hapana"
Shamsa alijibu, Dokta wake akamkabidhi hati yake
ya kusafiria wakaondoka katika uwanja wa ndege.
Moyoni mwa Shamsa alijawa na furaha sana
kusikia kwamba Eddy yupo hai pili ni uwepo wa
Eddy kuwepo ndani ya Japan. Swali kubwa lililo
muumiza kichwa ni wapi alipo Eddy ndani ya
Japani.
"Tutapitia kwanza hospitali kisha tutakwenda katika
nyumba ambayo nimekupangishia"
"Sawa"
Hawakuchukua muda mwingi wakafika kwenye
moja ya jengo kubwa la hospitalini. Wakashuka na
daktari na kuanza kuelekea ndani ya hospitali hiyo.
Kagari kadogo aina ya Vitz kikawakosa kosa
kuwagonga kikiwa kina simamishwa kwenye
maegesho ya hospitalini hapo jambo lililo mkera
sana daktari wa Shamsa, kwa hasira akatembea
kuelekea ilipo gari hiyo dereva akionekana ni
mwanamke huku Shamsa akabaki akiwa
anamtizama dokta wake ni kitu gani ambacho
anakwenda kukifanya kwa dereva huyo.
***
Eddy na binti huyo wakijapani wakazidi kutokomea
kwa mwendo wa kasi kuondoka katika hospitali
hiyo.
"Unafahamu kijapan?"
Binti huyo alizungumza kwa lugha ya kingereza
huku akizidi kuongeza mwendo kasi wa gari hilo.
"Hapana najua kingereza, kifarasana na kiswahili"
"Ohooo unajua kiswahili, mimi pia najua japo si
sana"
Binti huyo alizungumza kwa lugha ya kingereza.
"Kama unajua kiswahili. Haya Mambo vipi?"
"Mambo mimi ni Poa"
"Unaitwa nani?"
"Naitwa SA YOO. Wewe je unaitwa nani?"
"Mimi naitwa Eddy"
"Jina zuri, tokea wapi wewe?"
"Tanzania"
"Ahaaa najua hiyo nchi. Kumbuka nilikujaga nikiwa
mtoto ndio jifunza kiswahili kule"
"Kwa nini umeamua kunisaidia?"
Kabla binti huyo hajajibu simu yake ikaita. Akaitoa
kwenye mkoba wake moja kwa moja akaipokea
kisha na kuiweka sikioni mwake. Sura yake gafla
ikabadilika baada ya kupokea maelezo kutoka
uoande wa pili wa simu. Akaikata simu yake huku
machozi yakianza kumlenga lenga usoni. Jambo
lililo anza kumpa wasiwasi Eddy.
"Sa Yoo unatatizo gani?"
"Bibi yangu"
Sa Yoo alizungumza huku machozi yakilowanisha
mashavu yake Ikamlazimu kugeza gari lake
akakunja kwenye barabara nyingine na kuliendesha
kwa kasi gari lake akijitahidi kuyapita magari
ambayo yanakwenda kwa mwendo wa taratibu.
Dakika kumi mbeleni wakawa wameingia kwenye
jengo moja kubwa. Kwa haraka akalipitisha gari
lake kwenye maeneo ya maegesho na kuwakosa
kosa kuwagonga watu wawili waliokuwa wakivuka
kuelekea katika upande wa kuingilia katika gorofa
hilo.
***
Majira ya saa tatu kasoro msafara wa magari ya
raisi Praygod Makuya yakaingia kwenye msitu
ambao walielekezwa wanapo patikana watekaji
walio mteka mke wake. Makachero wanao uongoza
msafara huo wakashuka kwenye magari yao kila
mmoja akiwa na bastola iliyo jaa risasi mkononi
mwake. Wakatembea kwa tahafhari kubwa
wakijaribu kuchunguza kila sehemu ya msitu huo
kwa umakini wa hali ya juu. Umakini wao ulizidi
kuongezeka kwani wana kiongozi wao mkubwa wa
nchi. Wakafika hadi eneo la handaki. Makachero
wawili wakaingia ndani ya handaki hilo. Gafla milio
mingi ya risasi ikasikika ndani ya handaki hilo
jambo lililo wachanganya raisi na watu wake walio
baki nje ya handaki.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 45 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (45)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Makachero wanao uongoza msafara huo
wakashuka kwenye magari yao kila mmoja akiwa
na bastola iliyo jaa risasi mkononi mwake.
Wakatembea kwa tahafhari kubwa wakijaribu
kuchunguza kila sehemu ya msitu huo kwa
umakini wa hali ya juu. Umakini wao ulizidi
kuongezeka kwani wana kiongozi wao mkubwa wa
nchi. Wakafika hadi eneo la handaki. Makachero
wawili wakaingia ndani ya handaki hilo. Gafla milio
mingi ya risasi ikasikika ndani ya handaki hilo
jambo lililo wachanganya raisi na watu wake walio
baki nje ya handaki.
ENDELEA
Milio hiyo ya risasi ikawafanya makachero wengine
kumzunguka raisi Praygod Makuya kuzuia hata
kama kuna tatizo baya litatokea waweze kumlinda.
Ikawalazimu makachero wawili kuingia katika
handaki bastola zao zikiwa mikononi mwao. Cha
kushangaza wakawakuta wezao wakiwa
wamesimaa huku wanatetemeka mithili ya watu
walio mwagiwa maji ya baridi na kusimamishwa
kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
Wakajaribu kuwauliza kwa ishara ni kitu gani
kimepelekea hadi wakawa wanafyatua risasi ovyo
ovyo. Ila hakuna aliye weza kutoa jibu kati yao
zaidi ya wao kuendelea kutetemeka. Ikawalazimu
wezao hao wawili kuanza kutembea taratibu ndani
ya handaki hilo kuchunguza ni nini ambacho
kimetokea. Wakaingia kwenye moja ya chumba
ambapo cha kwanza kukutana nacho chini ni damu
nyingi za mwanadamu. Katika kupitisha pitisha
macho yao huku na huku. Wakamkuta mke wa
raisi akiwa amelala juu ya kitanda huku damu
nyingi zikiwa zinamwagika mwilini mwake,
akikaribia kuiaga dunia.
***
Kitu kisicho onekana kikazidi kuwateketeza
makachero walio mshambulia Priscar hadi wote
wakafa.
Katika hali ya kumshangaza Priscar akajikuta
akivutwa nje ya gari na kulazwa pembeni pasipo
kumuona mtu anaye mfanyia mambo yote hayo.
Jeraha la risasi iliyo mpiga ndani ya dakika moja
likawa limekauka na mwili wake ukarudi katika hali
yake ya kawaida.
“Wewe ni nani unaye nifanyia haya yote”
Ilimbidi Priscar kuuliza kwani hisia za kusnikwa na
mtu huyo asiye oenekana kwenye mwili wake mara
kadhaa, anazihisi ila tatizo ni mboni zake za
macho haziwezi kumuona mtu huyo. Hakuna
ambacho aliweza kuambulia kujibiwa. Gari lake
ambalo limeingia kwa nyuma ndani ya mtaro
akashangaa likisitolewa taratibu na kusimamishwa
barabarani. Kisha akajikuta akishikwa mkono wa
kulia akikokotwa hadi kwenye mlango wa kuingilia
ndani ya gari hilo. Mlango ukafunguliwa bila hata
ya kupenda akajikuta akinyanyuliwa na kuingizwa
kwenye gari na kukalishwa kwenye siti ya dereva.
Akafungwa mkanda, gari ikawashwa na mikono
yake ikashikishwa kwenye mskani wa gari hiyo na
mlango ukafungwa. Ikiashiria aondoke katika eneo
hilo haraka iwezekanavyo kwani kuna gari baadhi
za polisi zinakuja kuwapa nguvu makachero wanao
pambana na mtu aliye hitaji kuuvamia msafara wa
raisi.
***
Dokta akamuachia simu Shamsa kisha yeye akazidi
kusonga mbele. Kulifwata gari lililo kosa kosa
kuwagonga. Shamsa kabla hajafika hatua nyingi
simu hiyo ikaita kuangalia vizuri akakuta ni jina la
baba yake, hakuona haja ya kuelekea anapo
kwenda dokta wake. Akaipokea na kuiweka sikioni
mwake.
“Baba habari”
“Ohoo Salama binti yangu, mumefika salama”
“Ndio baba hapa tumefika hospitalini”
“Mbona unazungumza kwa furaha sana?”
“Hpana baba kidogo nimebadilisha mazingira,
kidogo ninafurahi sana”
Shamsa akiendelea kuzungumza na simu tayari
dokta wale alisha fika kwenye gari na kukutana na
binti anaye mfahamu akitokea ndani ya gari hilo
huku akimwagikwa na machozi.
“Sa Yoo unatatizo gani?”
Daktari alimuuliza huku hasira yake ikiwa
imebubujika kifuani mwake mithili ya barafu la maji
liwekwapo juani
“Bibi yangu hali yake ni mbaya”
Dokta baada ya kusikia hiyo na kutokana
anamfahamu vizuri binti huyo pamoja na bibi yake
ambaye pia alisha wahi kumuhudumia katika
maswala ya saikolojia, hakuwa na budi zaidi ya
kuondoka na Sa Yoo wakielekea ndani.
Wakaungana na Shamsa kuingia ndani ya
hospoitali hiyo pasipo Eddy kumjua binti wa tatu
anaye ingia na kina Sa Yoo ni nani, kwani binti
huyo ameziachia nywele zake ndefu kwa nyuma
nakuizuia sura yake kuweza kuonekana vizuri kwa
mbele
Kutokana na uhalifu alio ufanya Eddy, ikamuwia
ugumu kushuka ndani ya gari kuhofia kuingia
mikononi mwa polisi, moja ni lazima astakiwe kwa
kusa la kuwapiga polisi, mbili ni lazima
atakabidhiwa katika ubalozi wa Tanzania aweze
kurudishwa Tanzania, jambo ambalo hakuhitaji
kuweza kulisikia kwa wakati huo.
Sa Yoo na daktari wakakimbilia kwenye chumba
cha wagonjwa mahututi huku wakimuacha Shamsa
akiwa amekaa sehemu maalumu ya mapokezi
akimsubiria mwenyeji wake afike. Shamsa
akaitumia nafasi hiyo kuweza kumfikiria ni wapi
ambapo anaweza kumpata Eddy. Mwanaume anaye
muheshimu kama baba yake, wazo la kurudi
kwenye familia ya magaidi wa Al-Shabab likaanza
kumpotea taratibu kichwani mwake, akaanza
kufikiria kuungana tena na Eddy ambaye aliamini
kwamba amekufa na hilo ndio jambo ambalo
lilimfanya akubali kurudi katika familia ya Al-
Shabab watu walio muulia wazazi wake baba na
mama akiwa mdogo kisha akachukuliwa mateka na
kuwa miongoni mwa askari wakikosi hicho akiwa
mdogo sana.
“Nilazima niwaue Al-Shabab wote”
Shamsa alizungumza huku picha ya askari wa
kikosi hicho ikiwajia jia kichwani mwake. Hasira
dhidi ya kikosi hicho ikazidi kumpanda moyoni
mwake hadi mwili mzima ukaanza kumtetemeka.
Kwa kupitia kioo cha pembeni cha gari alilomo
Eddy, akaona gari mbili za polisi zikija katia
maeneo ya maegesho ya hospitalini hapo.
Wasiwasi mwingi ukazidi kumpanda, akataka
kushuka na kukimbia akaoona itakuwa ni hatari
sana kwake na itakuwa ni rahisi kwa yeye kuweza
kukamatwa na askari hao. Gari hizo zikazidi
kulisogelea gari ambalo Eddy yupo, kwa haraka
ikamlazimu kuweza kuinama ndani gari hilo ili
asiweze kuonekana.
Gari hizo za polisi zikasimama karibu kabisa na
gari alilopo. Wakashuka askari wanne walio valia
nguo nyeusi huku viunoni mwao wakiwa
wamening’iniza pingu pamoja na kuchomeka
bastola zao zilizomo kwenye vifuko maalumu vya
kuchomekea bastola.
Askari hao wakatizama tizama kila sehemu ya
maegesho ya magari hayo wakionekana kwamba
kuna gari wanaitafuta, mmoja wao akaanza kupiga
hatua za kulifwata gari hilo taratibu huku akijaribu
kutazama namba ya usajili ya gari hilo kwani ni
gari lililo mbebea muhalifu anayetafutwa ndani ya
Japan nzima.
***
Miliyo ya risasi ilipo kata ndani ya handaki
makachero wote walio nje ya handaki
wakiongozwa na raisi Praygod wakaingia ndani
huku wakionekana kuwa na shauku kubwa ya
kujua ni kitu gani kinacho endelea ndani ya
handaki. Wakawakuta makachero wa kwanza
wakiwa hai huku wamesimama, hata kabla
hawajawauliza wakawaona makachero wengine
wakitoka ndani ya chumba kimoja huku wakiwa
wamembeba Rahab anaye endelea kuvujwa na
damu nyingi.
Ikabaki nusu Raisi Praygod kuchanganyikiwa baada
ya kumuona Rahab akiwa katika hali hiyo.
“Ah…aaa aahme faafaanyaa nini mke wangu”
Raisi Praygod aliuliza huku mwili ukimtetemeka,
makachero walio tangulia kuingia ndani ya handaki
hilo wakakosa jibu la kuzungumza na fika
wanatambu kwamba wao ndio wameusika katika
kumpiga risasi Rahab baada ya Rahab kuanza
kufanya jaribio la kuwashambulia makachero hao
ila akashindwa na kujikuta akipigwa risasi kadhaa
zilizo mfanya kuingia ndani ya chumba huku hali
yake ikiwa mbaya sana.
Kutokana hapakuwa na jibu kwa makachero hao,
raisi Praygod akatoa amri ya mke wake awaishwe
mara moja kwenye gari wampeleke hospitali.
Safari ya kurudi jijini Dar es Salaam ikaanza huku
gari hizo zikiendeshwa kwa mwendo kasi. Ndani
ya dakika arobaini na tano wakawa wameingia
ndani ya hospitali ya taifa muhimbili huku hali ya
raabu kizidi kuwa mbaya kila jinsi dakika zilivyo
zidi kwenda.
Madaktari wakaanza kazi ya kumuhudumia mke wa
raisi, raisi Praygod akashindwa kuyazuai machozi
yake.kumwagika. Hakujali kama ni kiongozi wa
nchi alicho kihitaji kwa wakati huo ni kusikia mke
wake anaendelea vizuri.
Madaktari ndani ya chumba cha upasuaji
wakafanikiwa kutoa risasi zote sita zilizo ingia
ndani ya mwili wa Rahab.
“Dokta…….”
Nesi mmoja alimuita daktari kiongozi wa
opereshini hiyo, macho yao wote yakatua kwenye
mwili wa Rahab, hapakuwa na mtu aliye weza
kuamini kitu walicho kiona, woga kati yao ukazidi
kutawala madaktari wote sita pamoja na nesi
mmoja waliomo ndani ya chumba hicho. Vidonda
vilivyo kuwa kwenye mwili wa Rahab vilijiziba na
kurudi katika hali ya kawaida.
Kitendo cha Rahab kuyafumbua macho yake yaliyo
mekundu mithili ya damu kikawafanya madaktari
wpte waliomo ndani ya chumba kuanza kukimbilia
mlangoni, kila mmoja akijaribu kuyaokoa maisha
yake. Hadi wanafika mlangoni tayari Rahab alisha
simama wima na kuchomo sindano zote za
madripu zilizo kuwa zimechomwa mwilini mwake.
Kila walipo jaribu kuufungua mlango haukufunguka
na taa zilizomo ndani ya chumba hicho zikaanza
kufifia na kigiza cha mbali kikaanza kutawala ndani
ya chumba.
***
Njia nzima Priscar akajikuta akijiuliza maswali ni
kitui gani kilicho weza kutoke katika muda
mchache uliopita.
“Au naota?”
Swali hilo alilipatia jibu akilini mwake kwamba kila
kitu kinacho tokea kwa wakati huo si ndoto bali ni
hali alisi inayo jitokeza.
“Madam”
Priscar aliwaza sehemu alipo mucha Rahab,
ikamlazimu kuongeza mwendo kasi wa gari lake
kuelekea nje ya jiji la Dar es Salaam. Hadi anafika
katika maeneo ya hamdaki ikamlazimu kusimaisha
gari lake mbali kidogo na sehemu na lilipo
hamdaki, akashuka na kuanza kukimbia kuelekea
sehemu ya handaki, kabla hajalifikia akasikia milio
kadhaa ya risasi ikirindima ndani ya handaki hilo.
Alipo chunguza vizuri akaziona gari za ikulu zikiwa
zimesimama nje ya handaki hilo, huku Raisi
Praygod akiwa wamezungukwa na walinzi wake.
Baada ya milio ya risasi kunyamaza
akawashuhudia walinzi hao wakiongozana na raisi
wakiingi ndani ya handaki hilo. Baada ya dakika
tano mbeleni akawaona wakitoka wakiwa
wamembeba Rahab akionekana akiwa katika hali
mbaya.
Priscar akataka kujitokeza ili akasaidiane nao ila
akaona itakuwa ni hatari kwake, akaendelea
kujibanza kwenye mti huo hadi wakaondoka kwa
kasi katika eneo hilo.
Kudhibitisha ni kitu gani kilicho weza kutokea
ndani ya handaki hilo, kwa haraka akakimbia nje ya
handaki hilo kutazama ni nini kilicho tokea.
Hakuamini macho yake baada ya kukuta damu
nyingi zikiwa chini ya sakafu zikitokea katika
chumba alipo ingia akazidikuta zikiwa nyingi jkuu
ya kitanda. Jasho likaanza kumtirirka akifikiria ni
kitu gani ambacho kimetokea bosi wake.
Kwa haraka akatoka ndani ya handaki na kurudi
alipo liacha gari lake. Akaingia ndani ya gari na
kuanza kuelekea Dar es Salaam akiamini kwamba
ni lazima Rahab atakuwa amepelekwa kwenye moja
ya hospitali iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kwa bahati nzuri akabahatika kuweza kuuona
msafara wa raisi kwa mbali, kwa tahadhari kubwa
akaufwatilia hadi katika hospitali ya Muhimbili.
Magari yalipo ingia katika geti kubwa la Muhimbili
na yeye akalisimamisha gari nje na kushuka na
kuanza kuelekea katika geti. Walinzi wa getini
wakamzuia asiingie ndani ya geti hilo kutokana ni
majira ya usiku.
Akatoa kitambulisho chake, baada ya askari mmoja
kukisoma akamuamuru wezake wamruhusu Priscar
kuingia ndani ya hospitali.
“Samahani nesi kuna mgonjwa ameletwa hapa
dakika mbili zilizo pita amepelekwa wapi?”
“Aliye letwa wakati huu ni mke wa raisi na
amepelekwa chumba cha upasuji”
“Asante”
Shamsa akaondoka na kuanza kutembea kwa
mwendo wa haraka kuelekea kwenye chumba cha
upasuaji, kabla hajafika akawaona baadhi ya
makachero wezake wa ikulu wakiwa nje ya chumba
hicho wakiwa wameimarisha ulinzi mkali nje ya
chumba hicho kuku raisi akimwagikwa na
machozi.
Katika hali ya kustaajabisha Priscar akashuhudia
damu nyingi zikiruka kwenye kioo cha dirisha cha
chumba hicho pasipo hata walinzi walio kipa
mgongo chumba hicho kushuhudia tukio hilo.
Kwa haraka akaanza kukimbia kuelekea kwenye
chumba hicho, makachero wezake wanao mfahamu
wakabaki wakimshangaa, mmoja wao akataka
kumzuia ila akaambuliwa kusukumwa pembeni
hadi raisi aliye kuwa emekaa akanyanyuka
kumshnagaa binti huyo aliye mpa majukumu ya
kumlinda mke wake na akashindwa.
Priscar bila hata kumjali mtu akaupika teke
mlango huo ila haukufunguka, hapo ndipo watu
wote wakatambua kwamba kuna tatizo limetokea
ndani ya chumba hicho baada ya kuziona damu
nyingi kwenye kioo cha mlangoni kikiwa
kimetapakaa damu na mbaya zaidi hawasikii kitu
chochote mutoka ndani ya chumba hicho kilicho
tengenezwa kwa utaalamu mkubwa wa kuto kutoa
sauti nje wala kuingiza sauti ndani pale mlango
unapokuwa umefungwa vizuri.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 46 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (48)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Refa akatoa ishara ya kengele kugongwa, pambano
lianze.
Bao moja zito likatua usoni mwa Eddy, akayumba
mithili ya mlevi wa pombe za kienyeji, akastukia
akinyakuliwa kama mwewe anapo nyakua kifaranga
cha kuku, akazungusha haweni mara kadhaa, na
kutupiwa pembeni. Ukumbi mzima ukanyanyuka
kwa kushangilia. Macho yaliyo jaa ukungu na
kizungu zungu kikali. Yakatua kwa binti aliye
karibu kabisa na ulingo akishangilia kwa nguvu
zote kama wanavyo fanya mashabiki wengine
“Shammm…..”
Hata kabla Eddy hajaimalizia sentesi yake hiyo
akastukia jitu hilo likitua juu ya mwili wake na
kumuangukia mgongoni na kumzidishia maumivu
ya mwili.
ENDELEA
Eddy alajikuta akinyanyuliwa tena juu na kurushiwa
nje kabisa ya ulingo, hapo ndipo kelele za
mashabiki zikazidi mara dufu. Refa rii kwa haraka
akamfwata Eddy na kumuuliza kama anaweza
kuendelea na mchezo huo.
“Ndio naweza”
Eddy al;izungumza huku akijizoa zoa kunyanyuka
katika sehemu aliyo angukia. Akanyanyua kichwa
chake kutazama sehemu alipo kaa msichana aliye
mfananisha na Shamsa, kweli macho wala akili
yake haikuweza kukosea kabisa kwani binti huyo ni
Shamsa. Kushangilia kwake, kukarudisha
kumbukumbu, kipindi wapo katika fukwe za kopa
kabana, nchini Brazil. Alipokuwa akicheza mpira na
mwanaye Junio, huku Shamsa akiwa mshabiki
mkubwa wa Junio.
Uchungu na maumivu kuhusiana na familia yake
iliyo potea duniani. Familia aliyo ihangaikia miaka
kadhaa kuweza kuitia mikononi mwake, ila iliweza
kuiondoka ndani ya siku moja, tena mauaji yaliyo
sababishwa na baba pamoja na dada yake Manka.
Machozi yakaendelea kumwagika, taratibu akaanza
kurudi ndani ya ulingo huku akijipenyeza kwenye
uwazi wa kamba ya chini kabisa. Jitu linalo pigana
naye lililopo muona tu Eddy likamkimbilia na
kutaka kumkumba.
Kwa bahati mbaya haikuwa hivyo tena kwani,
lilijikuta likipita lenyewe na Eddy kumkwepa,
likajibamiza kwenye kamba za ulingo zinazo futika
na kulifanya lirudi kwa kasi sehemu linapo tokea.
Jinsi linavyo kuja kwa kasi ndivyo jinsi macho ya
Eddy yalivyo weza kulitazama kwenye mguu wa
kustoto. Bila hata ya kujiuliza mara mbili, kwa
miguu yake yote miwili, Eddy akajirusha na
kugonga sehemu ya goti la kushoto la jitu hilo.
Sehemu ya goti la jitu hilo, ikapelekea kutenguka
na kugeuka nyuma. Anguko la jitu hilo huku
likipiga mayowe ya maumivu makali, yakapelekea
uwanja mzima kukaa kimya, hapakuwa na mtu
aliye weza kuamini kwa pigo hilo jitu hilo
litaanguka. Watu wa Sabogo, ndio pekee wakaanza
kusikika wakishangilia huku wakilitaja jina la black
shadow.
Madaktari wa dharara wakaingia ulingoni
kulitazama jitu hilo, kila daktari aliye mtazama
mguu wa jitu hilo linalo endelea kulia kama mtoto
mdogo na kupiga piga kiganja chake chake chini
kwa maumivu makali anayo pata. Wakajikuta
wakitingisha kichwa wakimuashiria refarii kwamba
jitu hilo haliweza kuendelea na mashindano hayo.
Refarii bila hiyana akamfwata Eddy na kumshika
mkono wake wa kushoto na kuunyanyua juu
kuashiria kwamba yeye ndio mshindi wa mechi
hiyo. Baadhi ya mashabiki wakajikuta wakibadilisha
msimamo wao na kuanza kumshangilia black
shadow, wengine wakajikuta wakishikilia msimamo
wao na kuanza kuzomea.
Eddy akatoka ndani ya ulingo, taratibua akaanza
kutembea kuelekea sehemu kilipo chumba cha
kupumzikia akisubiria mzunguko unao fwata.
“Kazi nzuri kiongozi”
Sabogo alizungumza huku akimpiga piga Eddy
mgongoni
“Asante”
***
Tukio la mauji ya madaktrari walio kuwa
wakimfanyia upasuaji mke wa raisi, zikazidi
kuwaumiza kichwa watu walio shuhudia tukio hilo
ambalo raisi aliagiza liweze kuwa siri kwa watu
walio weza kushuhudia na endapo mtu ataitoa siri
hiyo basi anaweza kukutana na jambo baya
ambalo hakuwahi kuweza kulipata tangu alipo toka
tumboni mwa mama yake.
Kila mtu alibaki akilinda kinywa chake
kisizungumzie wala kichwa chake kisiliwazie sana
jambo hilo kwani ni jambo la kutisha pili ni jambo
ambalo hata ukilizungumza kwa watu kwamba mke
wa raisi si binadamu, watu watakushangaa. Utata
ukabaki kwa ndugu wa marehemu ambao walianza
kuhoji ni wapi walipo ndugu zoa. Ila uongozi wa
hospitali haukusita kudanganya kwamba
wamewapeleka watumishi wao nje ya nchi kwa
kazi maalumu.
“Jamani ila hata kama ni safari ya gafla mume
wangu angenipigia simu kunijulisha?”
Mamammoja alimlalamikia daktari mkuu aliye bosi
wa mume wake
“Ndio mama Kigadi angekupa taarifa, ila kutokana
hali ya safari hiyo, ilikuwa ni ya gafla sana
hapakuwa na daktari aliye weza kupiga simu.”
Daktari mkuu aliendelea kumuongopea mama huyo
kwani anafahamu kila jambo lililo weza kutokea
“Sawa na wamekwenda nchi gani?”
“Pakistani, kisha watakwenda Iraque huko ndipo
watamalizia kazi yao na kurudi nchini”
Daktari alisemea hivyo akimaanisha nchi zote hizo
mbili ni nchi ambazo hazina amani sana, na lolote
linaweza kutokea hata wakisema kwamba
madaktari wao wamelipuliwa kwa mabomu,
itakuwa si ja,bo la kushangaza sana zaidi
itawauma wana familia ambao bado wanaendelea
kufichwa juu ya vifo vya ndugu zao.
***
Wiki nzima ikakatika, pasipo Rahab kurudisha
fahamu yake. Madaktario maalumu kutoka nchini
Mexco ambao kwa mara ya kwanza waliweza
kumibu Rahab na kugundua tatizo la yeye kuwa na
nguvu za ajabu, wakaweka kambi ndani ya ikulu
wakiendelea kuifwatilia afya ya Rahab, huku wakiwa
wamemuweka katika chumba maalumu.
Hapakuwa na jibu lolote juu ya ugonjwa ambao
unao msumbua Rahab. Raisi Praygod akazidi
kudhohofika kwa mawazo juu ya mke wake.
Moyoni mwake anampenda mke wake kupita kitu
cha aina yoyote. Mapenzi yake juu ya Rahab,
yamemfanya aonekane kama mwendawazimu.
Shuhuli zake zote za uongozi amemuamchia
makamu wake wa raisi. Kitu anacho kiangalia kwa
sasa ni jinsi mke wake anaweza kupona. Kila mara
aliingia kwenye chumba ambacho amelazwa Rahab
na kuwekewa mashine ambazo zinamsaidia
kupulia, na kusoma mapigo yake ya moyo, huku
mirija isiyo pungua sita inayo peleka damu na maji
ikiwa imechomwa mwilini mwake.
“Mke wangu anaweza kupona kweli?”
“Ndio anaweza kupona bado hatujapata kujua ni
kitu gani ambacho kinaweza kumsaidia akapona”
“Jamani naombeni mufanye jitihada zenu mke
wangu aweze kupona”
“Kila jambo muheshimiwa linawezekana ila
kikubwa pia tusisahau kumuomba Mungu ashushe
wepesi wake katika hili”
“Amen atasaidia”
Raisi Praygod alizungumza kwa unyonge huku
akimtazama mke wake aliye lala kitandani,
akionekana kuwa ni nusu mfu
***
“Kiongozi jiweke tayari kwa pambano lijalo”
Sabogo alimuambia Eddy aliye kaa kwenye moja
ya kiti kilichopo ndani ya chumba cha kupumzikia”
“Pesa ya pambano la kwanza mumesha niwekea”
“Ndio ipo”
“Mapambano yatakuwa mangapi?”
“Kwa leo yatakuwa manne kama utashinda yote
kesho itakuwa ni fainali”
“Poa ila ku……”
Eddy akaona anyamaze hakuhitaji kuzungumza
chochote juu ya Shamsa japo anamfahamu vizuri
kama ndio yeye aliye kuwa miongoni mwa
mashabiki ila hakuhitaji kujihusisha naye hadi pale
atakapo dhibitisha kwamba kweli ni Shamsa kwani
hisia za kwamba watu wanafanana duniani zilianza
kumjia kichwani mwake.
Muda wa pambano lake la pili ukawadia, safari hii
kidogo Eddy akawa amejipatia patia mashabiki,
walio mshangilia. Wapo walio anza kumkubali kwa
kuweza kumuangusha jitu ambalo si rahisi kwa
wau kuweza kuamini kama lingepigwa kirahisi kiasi
hicho.
Eddy akaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu
kuelekea ulingoni. Alipo karibia ulingoni akaanza
kutembea kuuzunguka ulingo lengo lake ni kufika
katika sehemu ambayo amekaa Shamsa. Alipo
muona Sa Yoo kidogo akastuka kwani
anamfahamu msichana huyo, ndiye aliye weza
kumsadia kuwakimbia polisi kwenye baa aliyo
fikizia.
‘Ina maana wanajuana au?’
Eddy alijiuliza kimoyo moyo huku akiwatazama
kwa jicho la kuibia, kuna kidoti cheusi kidogo
ambacho kipo shingini mwa Shamsa, hichi ndicho
kilicho mpa uhakika kwamba huyo ni Shamsa. Bila
kuchelewa akaingia uwanjani kumsubiria mpinzani
wake ambaye anakuja kupambana naye.
Mpinzani wa sasa hivi hakuwa na umbo la kutisha
sana, ila amejengeka vizuri kwa misuli yake,
pambano likaruhusiwa kuanza, hapo ndipo Eddy
akagundua kwamba mpinzani wake ana utaalamu
mkubwa wa kupambana. Ikawa ni piga ni kupige,
pambano likazidi kuvuta hisia za mashabiki
waliomo uwanjani na hata wale walipo nje ya
uwanja wanao tizama pambano hilo kupitia
televishion.
Mapigo ya black shadow yakaanza kumstua
Shamsa na kuhisi kuna sehemu alisha wahi
kumuona mtu huyo jinsi anavyo pigana ila
kumbukumbu za haraka hazikufanya kazi kwani
umahiri wa black shadow ukazidi kumchanganya
Shamsa, aliye zidi kuvuta hisia kujua ni nani anaye
pigana kama black Shadow.
Kumbukumbu zake hazikuwepo kabisa juu ya
Eddy, kwani anatambua kwamba Eddy anatafutwa
na jeshi la polisi nchini humo Japan na ningumu
kwa yeye kuweza kushiriki mashindano kama
hayo.
Kitu kilicho zidi kumchanganya ni jinsi black
Shadow anavyo rusha mateke na ukunjaji wake wa
ngumi. Kumbukumbu kadhaa za mwanaume aliye
kuwa akipambana Mlimani City akiwa amevaliaa
koti kubwa lenye kofia iliyo mficha sura yake,
zikaanza kumjia kichwani mwake.
Akakumbuka mwanaume huyo jinsi alivyo kuwa
anapambana na Eddy baba yake. Hapo ndipo
akaanza kupata picha.
‘No hitahitaji kumfahamu huyu mpiganaji’
Shamsa alijisemea kimoyo moyo huku akimtazama
black Shadow aliye mzidi mpiganaji mwanzake
aliye anza kupoteza umahiri wa kupambana na
mwisho kabisa mpiganaji huyo aliangushwa na
black Shadow chini na kushindwa kunyanyuka
kabisa.
Uwanja mzima ukanyanyka na kuanza kuchangilia,
Shamsa naye hakusita kusimama na kumshangilia
black shadow kwani mechi hiyo imeleta msisimko
mkubwa kwa mashabiki wengi, wale ambao
hawakumkubali walijikuta wakimkubali wenyewe.
“Sa Yoo, nimempenda sana yule black shadow”
“Umempenda?”
“Ndio nimependa”
“Umempendaje sasa wakati mtu mwenyewe hata
sura humjui”
“Nihitaji kuweza kuiona sura yake, hata nimuelezee
hisia zangu juu yangu”
“Sasa Shamsa rafiki yangu umechanganyikiwa,
mara moja hii umetokea kumpenda mtu usiye
mjua sura yake”
“Sa Yoo wewe niache tu. Hapa mwili wangu
unachemka kweli kweli”
“Hembu acha masiraha bwana”
“Haki ya Mungu, nahisi si mara yangu ya kwanza
kuweza kumuona huyu mpiganaji?”
“Umemuonea wapi?”
Swali hilo likamfanya Shamsa kuto kulijibu na
kukaa kimya akimshuhudia black Shadow akizama
kwenye mlango wa kutokea katika ukumbi huo
kuelekea kwenye vyumba maalumu vya wapiganaji.
Mapambano yote yaliyo kuwa yamepangwa kwa
watu watakao weza kushinda na kuelekea fainali
siku inayo fwata yakamalizika huku Eddy akiwa
amefanikiwa kushinda mapambano yake yote
mane.
Mpiganaji anayo ogopwa Yong Po naye akafudhu
kuingia fainali huku mapambano yake yote manne
akiwavunja vunja wapiganaji alio shinda nishwa
nao.
Kila watu walio shuhudia mtanange wa siku ya
kwanza wakatamani kushushudia na kesho yake
fainali itakuwaje. Katika watu kutoka ukumbini,
Shamsa na Sa Yoo wakafanikiwa kuelekea katika
vyumba vya wapiganaji wajikijifanya kama
waandishi wa habari. Kwani waandishi ndio watu
pekee ambao wameruhusiwa kuingia katika
vyumba hivyo japo wamejitetea mbele ya walinzi
kwamba wamesahau vitambulisho vyao na hapo
walikuja kama washabiki, ila wanaomba kuweza
kuwahoji washindi.
Kutona na uzuri wao na mapozi kazaa ambayo Sa
Yoo amekubuhu nayo kwenye biashara ya ukahaba
aliyo kuwa anaifanya, ikawawia urahisi sana
kuingia kwenye chumba cha Young Poo, wakakuta
akiwa amezungukwa na waandhishi wengi
wakimuhoji.
Moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha
black shadow, ambacho nacho pia kimejaa
waandhishi wengi wa habari wenye kamera
kurekodia video na kamera za kupigia picha.
Hawakuweza kumuona black shadow zaidi ya
Sabogo na wapamb wengine.
“Wanasemaje?”
Shamsa alimuuliza Sa Yoo kwa kingereza kutokana
hafahamu kijapan wanacho zungumza waandishi
na Sabogo.
“Anasema kwamba black shadow, yupo bafuni
hawezi kuzungumza na waandhishi wa habari”
“Hilo bafu lipo wapi?”
“Nahisi ni huo mlango walio simama mabaunsa”
Shamsa akautazama mlamgo uliopo mota chache
kutoka sehemu walipo simama, wanaume walio
jazia na kukatika miili yao kwa misuli ndio walio
simama kwenye mlango wenye maandishi yanayo
somekaa kwamba ni bafu. Wanaume hao ambao ni
walinzi hawakuhitaji mtu yoyote kuweza kusogelea
mlango huo wala kupiga picha na kama ni
mazungumzo yote ya waandhishi wa habari
yafanyike kwa Sabogo.
“Tutafanyaje sasa?”
“Sijui rafiki yangu itakuwaje”
“Hembu jifanye kama umechanganyikiwa unapiga
makelele”
Shamsa alimshauri Sa Yoo, ambaye kwa mara ya
kwanza alisita ila alipo shawishiwa sana na rafiki
yake aliye tokea kumzoea, akaanza kupiga kelele
huku akigaragara kuelekea kwenye mlango wa
bafu. Mabaunsa hao wawili walio kaa mlangoni
wakalazimika kupiga hatua kadhaa mbele kumzuia
Sa Yoo asiwafwate, wandishi wa habari kadhaa
wakageuka na kamera zao kuchukua tukio hilo.
Shamsa akapata nafasi ya kuufungua mlango huo
na kuzama ndani, lengo lake ni kwenda kumuona
black shadow. Waandishi wa habari baadhi nao
walipo ona mlango umeacha wazi wa bafuni
wakajipenyeza na kuzama ndani.
Kwa bahati nzuri, Shamsa akamkuta Eddy akiwa
tayari amemaliza kuoga na kuvaa nguo zake
pamoja na kinyago chake. Eddy katika kumduwaa,
Shamsa aliye mjia kwa kasi, ndani ya bafu hilo
akiongozana na waandhishi wa habari. Akastukia
Shamsa akimkumbatia kwa nguvu bila hata kusita
Shamsa akaanza kumnyonye denda black shadow,
huku waandishi wakifyatua kamera zao kupiga
picha za kuweka kwenye magazeti yao.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 48 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (49)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Kwa bahati nzuri, Shamsa akamkuta Eddy akiwa
tayari amemaliza kuoga na kuvaa nguo zake
pamoja na kinyago chake. Eddy katika kumduwaa,
Shamsa aliye mjia kwa kasi, ndani ya bafu hilo
akiongozana na waandhishi wa habari. Akastukia
Shamsa akimkumbatia kwa nguvu bila hata kusita
Shamsa akaanza kumnyonye denda black shadow,
huku waandishi wakifyatua kamera zao kupiga
picha za kuweka kwenye magazeti yao.
ENDELEA
Kitendo hicho kikampa Eddy kigugumizi, akataka
kumuita Shamsa ila sauti haikutoka akajikuta
akiugulia tu huku akijaribu kumtoa Shamsa mwilini
mwake.
Mabaunsa na wapambe wa Sabogo wakawa tayari
wamesha ingia ndani ya bafu. Mabaunsa
wakambeba juu juu Shamsa aliye anza kupiga
kelele za furaha.
“I love you black shadow”(Nakupenda black
shadow)
Waandishi wa habari nao wakatolewa ndani ya bafu
hilo. Akabaki Eddy na Sabogo.
“Hao ndio mashabiki kiongozi inabidi uwavumilie
tu”
Eddy hakujibu kitu zaidi ya kubaki kimya,
akimfikiria Shamsa.
‘Huyu mtoto amepatwa na nini?’
Alijiuliza swahi hilo kichwani mwake.
“Kiongozi?”
“Mmmmmmm”
Eddy alistuka kutoka katika dibwi la mawazo mengi
“Huyu binti amekuumiza nini, tumchukulie hatua za
kisheria?”
“Hapana muacheni, na kama inawezekana kesho
nahitaji akae meza ya VIP”
“VIP tena! Au umesha mzimikia tukamlete upate
naye burudani usiku mzima. Kwa maana
anaonekana kama changudoa”
“Fanya kama nilivyo kuagiza kufanya”
Eddy alizungumza kwa sauti nzito hadi Sabogo
mwenyewe akabaki kimya na kutingisha kichwa
akimaanisha kwamba amemuelewa.
Shamsa akamkuta Sa Yoo nje ya ukumbi,
akamkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu rafiki
yake huyo huku akishangilia kama ameokota
kipande cha dhahabu barabarani.
“Vipi nieleze umefanikiwa?”
“Ndio yaani ninafuraha achaa. NAKUPENDA
BLACKKKK SHADOOOOOOWWWWWWWWW”
Shamsa alizungumza kwa sauti kubwa kama
mwenda wazimu. Hata baadhi ya watui wakabaki
wakimshangaa. Kutokana yupo nje ya ukumbi
amboa mpiganaji huyo ametoka kuzichapa ulingoni
muda mfupi ulio pita. Kila mtu akaamini kwamba
binti huyo amechanganyikiwa kwa upendo kama
wanachanganyikiwavyo wasichana wengine wanapo
waonaga watu maarufu duniani.
Njia nzima ndani ya gari Shamsa, aliendelea
kumzungumzia black Shadow. Kumbukumbu ya
jinsi alivyo mrukia black shadow na kumnyonya
denda, zikawa zinamrudia rudia. Hadi ikafikia
kipindi akaanza kuutathini mwili wa mpiganaji
huyo, akiwa hana nguo.
“Huli chakula?”
“Nimeshiba”
Shamsa alijibu huku akielekea chumbani kwake
mara baada ya kufika katika nyuma wanayo ishi na
Sa Yoo. Akaingia ndani kwake na kuufunga mlango
kwa funguo. Haraka haraka akazivua nguo zake
zote na kubaki kama alivyo zaliwa. Akasimama
mbele ya kioo kikubwa cha kabati na kuanza
kujichunguza huku akigeuka geuka akiliangalia
umbo lake lililo jengeka vizuri.
“Mimi mzuri, kesho nawahi mapemaa ukumbini
nimuone black shadow”
***
Ndani ya ndege ya kifahari aina ya Jet, Mzee
Gdowin na John, pamoja na walinzi wao wawili.
Waliendelea kuzungumza mambo mengi kuendelea
kikundi chao ambacho kina watu wengi sana
dunia. Ndege iliendelea kupasua mawingu kuelekea
bara la Asia, ikitokea Amerika ya kaskazini. Ni
safari ambayo imewachukua masaa mengi kadhaa,
ila lengo na zumuni lao ni kwenda kuishuhudia
fainali ya mapambano inayo endelea ndani ya
Japani.
Wametokea kujikuta wakimpenda black shadow,
mpiganaji mwenye ujuzi mkubwa sana katika
maswala ya kupigana, wameona ni vyema
wamchukue huyo ili awe miongoni mwa washirika
wao ili kuzidi kujitanua kwenye kikuni chao.
Mara kadhaa wakajikuta wakitazama baadhi ya
video za mapambano manne ya black Shadow.
Ujuzi wao wa kupigana ulizidi kuwachanganya, na
kutamani ndege hiyo iweze kufika katika muda
mchache. Kwani wanahofia matajiri wengine
duniani wanaweza kujitokeza na kumchukua black
shadow katika mambo mbalimbali, ikiwemo uigizaji
wa filamu.
“Mzee usiwe na hofu tutampata tuu. Nguvu ya kila
kitu tunayo”
John alizungumza huku akimtazama Mzee Godwin
anaye onekana kuwa na wasiwasi mwingi sana.
“Hawa marubani sijui wanaiendeshaje hii ndege,
naona tunachelewa”
“Tutafika tu”
Masaa manne mbele teyeri wakawa wamefika
nchini Japani, majira ya saa nne asubuhi.
Wakapokelewa na mwenyeji wao ambaye moja kwa
moja akawapeleka hadi kwenye hoteli moja ya
kifahari.
“Pambano linaanza saa ngapi?”
Aliuliza mzee Godwin baada ya kupumzika kwa
dakika kadhaa baada ya kufika hotelini.
“Saa nne usiku”
“Ahaa, hatuwezi kuonana na huyo black shadow
muda huu kabla ya pambano?”
Mzee Godwin alimuuliza mwenyeji wao bwana
Jackson Lee.
“Kusema kweli itakuwa ni ngumu kutokana black
shadow yupo kwenye maandalizi ya pambano la
usiku”
“Sawa kila kitu kiwekeni sawa, hata kesho
muutaarifu uongozi wake kwamba ninahitaji
kufanya naye kikao”
“Sawa mueheshimiwa”
***
Kengele ya mlangoni ndio iliyo mkurupusha Sa
Yoo. Akajizoa zoa kitandani kwake na kuiangalia
saa yake ya ukutani na kukuta ni saa tano na
dakika tano asubuhi. Akasimama na kujinyoosha
mara kadhaa huku akipiga miyayo. Taratibu kwa
wenge la usingizi akaanza kutembea kuelekea
mlangoni. Akafika mlangoni na kuminya moja ya
batani ambayo pembeni yake kuna kitivii kidogo
cha ukutani kinacho muonyesha mtu aliyopo nje
ya mlango. Akamuona kijana mmoja aliye valia
tisheni yekundu na kofia nyekundu akiwa
amesimama, huku mkononi mwake akiwa
ameshika boksi.
Uvaaji wa kijana huyo ukamuashiria Sa Yoo
kwamba huyo ni mlete mizigo kutoka katika
kampuni moja kubwa ya kutuma mizigo ndani ya
Japani. Akafungua mlango na kumtazama kijana
huyo.
“Wewe ndio Ms Shamsa?”
“Hapana ila unaweza kusema shida yako”
“Kuna mzigo wake hapa nimeagizwa kuuleta kama
yupo basi nahitaji kuweza kumuona”
“Umetokea wapi?”
“Madam kama wewe si muhusika basi, siwezi
kukuambia kwamba unatokea wapi?”
“Mmmmmm”
Sa Yoo aliguna kisha akaanza kumuita Shamsa
kwa sauti kubwa. Shamsa aliitikia baada ya muda
akatoka akiwa amejifunga taulo akiashiria kwamba
naye ndio kwanza anaamka.
“Kuna mzigo wako hapa”
Sa Yoo alizungumza huku akiondoka mlangoni na
kwenda kujibwaga kwenye sofa na kujilaza
kumalizia malizia usingizi wake.
“Naamini wewe ndio ms Shamsa?”
“Ndio”
“Kuna mzigo wako hapa kutoka kwa Mr Sabogo”
“Mr Sabogo ndio nani?”
Sa Yoo baada ya kusikia hilo jina akakurupuka na
kukimbilia mlangoni akiwa katika sura ya furahja
“Humjui wewe Mr Sabogo, si yule mzamini wa
black shadow”
Shamsa kusikia hivyo akawa kama mtu aliye
changanyikiwa kwa haraka, akasaini kwenye
karatasi maalumu ya kijana huyo kisha wakaagana
naye kijana huyo na kuufunga mlango. Akaanza
kulifungu boksi hilo. Macho yao wote yakatua
kwenye ua zuri jekundu, linalo nukia vizuri, Sa Yoo
akalitoa ndipo wakaziona tiketi mbili zilizo kuwa
chini ndani ya boksi.
“VIP TIKETIIIIIII UUUUUUUUU”
Shamsa alizungumza huku akiruka juu kwa furaha,
Sa Yoon aye akampokonya moja wote wakajikuta
wakiruka ruka kwa kushangilia kupata mualiko huo
kutoka kwa black shadow.
Kila mmoja akawa anaombea muda na masaa
yaweze kukimbia kwa haraka ili wafike ukumbini
kushuhudia pambano ambalo si kwasababu watu
wanalipenda, ila Shamsa anampenda mpiganaji wa
pambano huyo ambaye ni black Shadow
Majira ya saa mbili usiku Sa Yoo na Shamsa
wakawa wamefika katika ukumbi wa mapambano.
Kwa siku hiyo hawakupita katika lango wanalo pita
watu wa kawaidia ila walipita katika lango la
kuingilia katika viti maalumu vya watu wenye hadhi
ya juu. Kila sehemu Shamsa alipo pita alitazamwa
na watu kwani habari za yeye kumbusu black
shadow, zilienea kwenye magazeti mengi. Kwa
msaada wa muhudumu katika sehemu hiyo
maalumu wakaonyeshwa viti vyao vya kukaa,
ambavyo mbele yake kuna kioo kikubwa na
kigumu kinacho onyesha pambano hilo kwa
ukaribu zaidi kutokana na lensi ya mvutano iliyo
tengenezwa kwenye kioo hicho.
“Munatumia kinywaji gani?”
Dada muhudumu aliwauliza, kila mtu akaseme
kinywaji anachho kihitaji. Watu walizidi kumiminika
katika ukumbi, kila mtu aliitafuta siti yake na
kuweza kukaa kusubiria muda muafaka wa
pambano hilo liweze kufika.
Ulinzi mkali ukaimarishwa katika sehemu ya VIP,
mzee Godwin na John ambaye muda wote maisha
yake ni yakusukumwa kwenye kiti maalumu cha
matairi. Wakaingi katika sehemu hiyo.
Wakakaribishwa katika sehemu waliyo andaliwa,
ambapo kuna wadada sita walio valia chupi aina ya
bikini na sidiria wakiwa wamesimama, kwa ajili ya
kuwapa huduma ya kuwachua chua miili yao pale
watakapo kuwa wakiendelea kuliangalia pambano
hilo.
Vipaza sauti vilivyomo ndani ya uwanja vilianza
kutoa sauti ya kike ya mtangazaji wa pambano wa
siku ya leo. Kelele zilizidi kurindima kila mahali,
watu walikuwa kama wameingiwa na pepo la
kushangilia kila walipo sikia jina la black shadow.
Wadada wengi walishika mabango yaliyo andikwa
ujumbe tofauti tofauti wakionyesha hisia zao za
kumpenda mpiganaji huyo, aliye jizolea umaarufu
katika kipindi kifupi tu.
Macho ya Shamsa yakaendelea kutazama huku na
kule, mara kadhaa alijaribu kuyapitia mabango ya
wasichana waliyo yashika, akajikuta akiingiwa na
woga pamoja na wivu wa kumkosa mpiganaji huyo
katika swala zima la mapenzi.
“Anaye kuja kwenu kwa sasa ni BLACK
SHADOWWW”
Uwanja mzima ukasimama huku watu
wakimshangilia. Eddy hakuamini kupata idadi
kubwa ya watu wanao mshangilia, kila alipo pitisha
macho yake huku na kule aliona baadhi ya watu
wakiwa wamevaa mavazi kama yake. Akaanza
kutembea kwa kujiamini kuelekea uwanjani.
Hakusita kupita karibu na washabiki walio kaa
karibu na njia ya kuelekea ulingoni. Akawapa
mikono kuashiria kwamba anawapenda kama
wanavyo mpenda.
Akaingia ulingoni na kuendelea kuzunguka huku
mkono wake mmoja wa kulia akiwa ameunyoosha
juu, kwa ishara ya kuwasalimia watu. Muendesha
shuhuli akamkaribisha Yong Po. Mashabiki wake
nao wakasimama na kumshangilia mpiganaji huyo
anaye sifika kwa kuweka rekodi ya kuwavunja
vunja wapiganaji anao kutana nao. Hakuwa
mwenye mwili mkubwa wa kutisha, ila sura yake
iliyo komaa na yenye upara ulio kolezwa mafuta
hadi unameta meta, ndivyo vilivyo mfanya Eddy
ahofie kidogo. Ili kupoteza hofu hiyo ikambidi Eddy
ashushe pumzi nyingi na kujiweka sawa huku
akinyoosha nyoosha viungo vyake.
Muendesha shuhuli akatoka uwanjani na kuwaacha
Eddy na mjapani huyo aliye komaa sana
akionekana ni mpambanaji wa kipindi kirefu cha
nyuma. Refarii akasimama katikati yao, akawapa
sheria zinazo takiwa kufwatwa, alipo hakikisha kila
mmoja ameelewa sheria hizo. Akaanzisha
mpambano.
Young Po akaanza kuruka ruka huku akiichezesha
miguu yake kwa kasi, jambo lililo mfanya Eddy
kutazama miguu hiyo inavyo kwenda, kwani
hakujua ni muda gani, mpinzani wake huyo
atarusha teke. Kufumba na kufumbua Eddy
akajikuta akiwa ameanguka chini, hakuelewa hata
teke hilo la kifuani amepigwa muda gani.
Eddy akanyanyuka kwa haraka na kupanga
mashambulizi, akarusha ngumi kadhaa baadhi
zikampata Young Po ila baadhi alizikwepa. Yoong
Po hakuwa nyuma, na yeye akaendelea kutupa
mashambulizi ya kustukia kwani tayari alisha weza
kumsoma Eddy kupitia mikanda ya video aliyo
cheza jana. Alimgundua kwamba black Shadow ni
mwepesi sana katika kukwepa, kurusha ngumi na
mateke.
Pambano likazidi kufaana, watu walizidi kushangilia
kila pale mmoja kati ya wapiganaji alivyorusha
makonde kwa mwenzake.
Kila mmoja wa mashabiki hadi inatimu robo saa,
hakuweza kujua mshindi ni nani kwani wapiganaji
hao walijitahidi kila mmoja kufanya awezalo
kuhakikisha kwamba anajibu makonde ya
mwenzake.
Jasho likazidi kuwatirika wapiganaji, hata Shamsa
mwenyewe, japo amekaakatika sehemu ambayo
ina kiyoyozi cha kutosha ila naye jasho lilimwagika
kila alipo shuhudia black shadow anapigwa.
Shamsa akajikuta akiaanza kuingiwa na furaha
moyoni mwake baada ya kuanza kuona black
shadow anamzidi Young Po. Si Shamsa pekee bali
hata mashabiki wa black shadow nao walianza
kumshangilia. Mzee Godwin na John nao
hawakuwa nyuma kumshangilia mpiganaji huyo
waliye muhitaji kwa udi na uvumba. Yong Po
alipigwa ngumi moja takatifu ya shingoni iliyo
muangusha chini na kulala kifudi fudi.
Uwanja mzima ukanyanyuka kwa kushangilia,
refarii akamsogelea Yong Po. Akainama na
kumuuliza kama ana weza kuendelea na pambano.
“Nipatie”
Young Po alizungumza kwa sauti ya tabu, kwa siri
kubwa refa rii, akatoa kidoge kimoja cha kuongeza
nguvu, akampatia Young Po, bila mtu kuona,
Young Poul akakimeza, huku akiendelea kulala
chini kama mtu aliye poteza fahamu. Refa
akasimama na kuanza kuhesabu moja, mbili hadi
alipo fika nane Young Pu akasimama wima. Kila
mtu akashangaa, kumuona Yong Po amesimama.
Eddy aliye anza kujawa na furaha akiamini kwamba
amemshinda mpiganaji mwenzake, furaha hiyo
ikakata, akabaki akiwa ameshangaa.
Refarii akaruhusu pambano kuendelea, Eddy
akamsogelea Yong Po na kumtandika makonde
kadhaa ya nguvu, ila Young Po aliyumba kidogo na
kukaa sawa. Yong Po akaanza kurusha makonde
ambayo kila Eddy alipo jaribu kuyazudia
yalimshinda nguvu. Ngumi nyingi zilitua kifuani
mwa Eddy, akaanguka chini mzima mzima huku
akimwaga damu mdomoni mwake. Shamsa
alisimama huku akiwa amelitoa jicho, la kuto
kuamini anacho kiona. Kila Eddy alipo jaribu
kusimama, alijikuta akianguka chini. Young Po
hakuishia hapo, akamsogelea Eddy karibu,
akamtandika teke moja la mbavu lililo mfanya Eddy
kutoa ukelele mkali wa maumivu. Young Po
akamkalia Eddy mgongoni na kuanza kumshindilia
ngumi za mbavu kwa sehemu aliyo mpiga teke.
Eddy akaendelea kuugulia kwa maumivu huku
damu zikimwagika mdomoni mwake.
Young Po akazidisha ngumi, nyingi, akaona
haitoshi akampiga Eddy kabari ya shingo, huku
mkono wake mmoja ukianza kulivuta maski la
Eddy ili amvue ili sura ya black shadow ionekane
kwa kila mtu, kwani ni watu wengi hawamfahamu
black shadow sura yake jinsi inavyo onekana.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 50 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (50)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Kila Eddy alipo jaribu kusimama, alijikuta
akianguka chini. Young Po hakuishia hapo,
akamsogelea Eddy karibu, akamtandika teke moja
la mbavu lililo mfanya Eddy kutoa ukelele mkali wa
maumivu. Young Po akamkalia Eddy mgongoni na
kuanza kumshindilia ngumi za mbavu kwa sehemu
aliyo mpiga teke. Eddy akaendelea kuugulia kwa
maumivu huku damu zikimwagika mdomoni
mwake.
Young Po akazidisha ngumi, nyingi, akaona
haitoshi akampiga Eddy kabari ya shingo, huku
mkono wake mmoja ukianza kulivuta maski la
Eddy ili amvue ili sura ya black shadow ionekane
kwa kila mtu, kwani ni watu wengi hawamfahamu
black shadow sura yake jinsi inavyo onekana
ENDELEA
Eddy hakukubali hata kidogo kwa kinyago chake
kiweze kuvuliwa usoni mwake, ni bora afe ila si
kinyago chake kuweza kuvuka. Akaanza kuminyana
na Young Po kuhakikisha kwamba hamvui kinyago,
japo kabala inaendelea kumpotezea nguvu na
pumzi ila akazidi kujitahidi kuhakikisha kwamba
kinyago hakivuki.
Young Po akabadilisha zaoezi la kumvua kinyago
Eddy, ila alicho kifanya ni kuzidi kumminya kabari,
macho yakazidi kumtoka Eddy. Damu zikazidi
kumchuruzika pembezoni mwa mdomo wake. Hali
ikazidi kuwa mbaya kwa upande wake. Kila shabiki
wa black shadow akajikuta akiwa katika mshangao
wa aina yake. Wapo walio shika vichwa vyao, wapo
walio shika midomo. Wapo walio yatoa macho yao
wakiwa hawaamini kwamba black shadow
anakwenda kuuawa na Yong Po. Kila anaye
ifahamu historia ya Young Po, aliweza kuutambua
ukatili wake. Wamama wengi na mabinti walijikuta
wakimwagikwa na machozi.
Refarii alipo muona black shadow ametulia kabisa
tuli huku akiwa ameyafumba macho yake akapiga
magoti kwa haraka na kuanza kuunyanyua mkono
wa black shadow juu. Mkono ukarudi chini,
akaunyanyua kwa mara ya pili ya tatu, mkono
ukarudi chini.
Akaanza kuhesabu moja kuelekea kumi.
‘Eddy, Eddy, Eddy’
Sauti ya Phidaya ilianza kusikika masikioni mwake,
kila alipo jaribu kuyafumbua macho yake kutazama
ni wapi alipo Phidaya ila hakuweza kumuona.
Mwanga mkali mweupe, ukampiga machoni
mwake. Akamshuhudia Junio akiwa amesimama
mbele yake amevalia mavazi meupe yanayo ng’aa,
mgongoni mwake akiwa na mbawa mbili nyeupe
na kubwa.
‘Baba bado muda wako. Pambana. Simamaaaaa
upiganeee’
SSauti kali ya Junio, iliyo jaa hali ya kama
mingurumo ya radi iliyo na mwangwi ndani yake,
vikamfanya Eddy kustuka.
“Tis………”
Refa rii hakuimalizia sentensi yake, mara baada ya
kumuona Eddy amestuka na kufumbua macho
yake. Wachukua video camera, walijitahidi kuivuta
sura ya Eddy karibu, watu wanao tizama pambano
hilo kwenye tv kubwa iliyopo ndani ya ukumbi na
televishion wakajikuta wakianza kushusha pumzi.
Eddy kwa haraka akaipeleka mikono yake yote
miwili, shingoni mwake, akaushika mkono wa
Young Po, akanza kuutoa tararibu huku akijitahidi
kujigeuza kutoka chini, ili asimame.
Ukumbi umzima ukasimama kwa kushangilia,
macho yakamtoka Young Po. Hakuamini kwamba
kabala yake ndio inaanza kutolewa taratibu
taratibu. Shamsa akajikuta akimkumbatia Sa Yoo,
na kuanza kumwagikwa na machozi ya furaha.
Mzee Godwin akajikuta akinyanyuka kwenye kiti
alicho kaa na kunza kupiga makofi. John naye
akajikuta akimuomba mpambe wake amfute
machozi ya furaha yanayo mwagika.
Eddy akafanikiwa kuichomoa kabari hiyo, mkono
huo huo wa Young Po uliokuwa umemkaba,
akauvuta vizuri alipo hakikisha kwamba
amekumata kisawa sawa, kwa kutumia goti lake la
mguu wa kuliia, akaubamiza mkono huo, mithili ya
mtu anaye vunya vipande vya mua virefu, vilivyo
ungana. Mkono huo ilio komaa mifupa yake,
ukafanikiwa kuvunjika. Young Po, akaruka na
kuanguka chini huku akiwa ameushikilia mkono
wake ulio vunjika, na kiwiliwili cha mbele cha
mkono huo kikiwa kinaning’inia.
Refa akamsogelea Young Po akamuuliza kama
anaweza kuendelea na shindano. Akatingisha
kichwa kwamba hawezi kuendelea. Refa akaruhusu
kengele ya ushindi igongwe na mpambano ukawa
umemalizika. Ukumbi mzima ukafura kwa kelele za
kushangilia. Hata wale ambao ni mashabiki wa
Young Po nao wakahamia kwa black Shadow.
Fataki nyingi zinazo mwaga karatasi nyinginyingi
zikaanza kupigwa hewani, ulingo mzima
ukatawaliwa na mvua ya vikaratasi.
Eddy akatabasamu huku akiwapungia mashabiki
mkono kushoto huku mkono wa kulia ukiwa
umeshika eneo ambalo mbavu zake zinauma.
Maumivu makali ya mbavu, yakamfanya Eddy
kuanguka gafla uwanjani. Madaktari ambao
wanamuhudumia Young Po, baadhi wakamuwahi
Black Shadow. Kila daktari aliye mgusa black
Shadow kwenye kifua chake akajikuta akishtuka
kwani, mapigo ya moyo hayafanyi kazi kabisa.
Heka heka za kumuwahisha hospitalini black
shadow zikaanza, kila shabaki akawa na hamu ya
kujua ni kitu gani kimepata black shadow. Machela
ikaletwa ulingoni, akawekwa vizuri, akawekewa
kifaa cha kumsaidia kupumua. Madaktari wakaanza
kumtoa black shadow ukumbini. Mashabiki
wakapiga makofi wakionekana kumuheshimu black
shadow, aliye poteza fahamu.
Akaingizwa kwenye gari ya wagonjwa na
kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
Shamsa na Sa Yoo wakaingia kwenye gari lao
mara baada ya kutoka uwanjani kwa haraka na
kuanza kulifukuzia gari la wagonjwa linapo elekea.
“Sa Yoo ongeza mwendo”
Shamsa alizungumza huku akijipangusa machozi
usoni mwake. Sa Yoo akazidi kuongeza mwendo
kwani anazitambua hisia za rafiki yake juu ya
mpiganaji huyo.
Wakafanikiwa kufika katika hospitali ambayo
walilishuhudia kwa mbali gari la wagonjwa likiingia.
Wakashuka kwa haraka na kuelekea mapokezi,
wakakuta waandishi wa habari wachache wakiwa
wanamalizia malizia kumpiga picha black shadow
aliye ingizwa kwenye chumba maalumu cha X
rays.
Waandishi wa habari walipo muona Shamsa na
kugundua ni binti ambaye wanahisi ni mpenzi wa
black shadow, wakamgeukia na kuanza kumpiga
picha jinsi anavyo lia.
Kwa haraka Sa Yoo, akavua kikoti chake na
kumfunika Shamsa kichwani ili waandishi
wasiendelea kumpiga picha anavyo mwagikwa na
machozi kisha akamtoa rafiki yake na kumpeleka
katika chumba maalumu cha kusubiria majibu.
“Jikaze tu Shamsa atakuwa salama”
Sa Yoo alizungumza huku akikiweka kichwa cha
Shamsa begeni mwake na kuendelea
kumbembeleza aache kulia
***
Harakati za uchaguzi zikaanza kuendelea
kuendelea katika nchi ya Tanzania. Vyama mbali
mbali vikaendelea kujipanga jinsi gani wanaweza
kuongoza maeneo mbali mbali kupitia viongozi
wao ambao watawapitisha katika vikao vyao
mbalimbali ambavyo wanapaswa kuvifanya. Chama
cha TSD(Tanzania Society Development), kinacho
ongozwa na mwenyekiti wake Raisi Praygod
Makuya. Kikajikuta kikiwa katika wakati mgumu
sana baada ya mwenyekiti wake kukataa kuendelea
kuongoza muhula unao fwata kwa madai ya
kumuuguza mke wake ambaye haijulikani ni lini
anaweza kuamka na akafariki.
Wazee wa chama na wenyeviti wa chama wa mikoa
wakakutana katika ukumbi wa hoteli kubwa ya
Serena kufanya mkutano wa kumuomba
mwenyekiti wao aweze kukubali kugombania tena
kwa maana wananchi bado wanamkubali sana,
kwani kwa miaka yake mitano aliyo kuwa
madarakani nchi ya Tanzania imeweza kupiga
hatua katika sekta nyingi sana, japo kuwa kuna
mapungufu machache yaliyo jitokeza katika kipindi
chake ikiwemo ujambazi, ugaidi na mambo mengi
mabaya.
“Kusema kweli, niliyo yafanya nimeyafanya kwa
msaada wenu ninyi. Ila kwa sasa akili yangu haipo
sawa kabisa katika kuendelea na uongozi.
Tumsimamisheni mtu mwengine basi aweze
kugombania uraisi”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwatazama
wanachama wezake walio jawa na sura za huzuni.
“Ila muheshimiwa wewe ndio mtu ambaye unafaa,
kusimama katika chama. Hatukuwa na mawazo ya
kumfikiria mtu mwengine kusimama kwenye
chama kugombania nafasi hii”
“Makamu wangu si yupo?”
“Muheshimiwa tunamuheshimu makamu wako wa
raisi, ila kumbuka yule alikuwa ni chaguo lako na
si chaguo la wananchi ukisema kwamba
tumsimamishe mtu mwengine, chama hiki kitakufa
katika dira ya siasa”
Wakaendelea kumbembeleza raisi Praygod Makuya
hadi akakubaliana nao kusimama tena katika
muhula mwengine wa kugombania uraisi.
Wanachama wezake wakajikuta wakijawa na furaha
mioyoni mwao. Ila raisi Praygod hakuwa na furaha
sana moyoni mwake kwani mke wake hali yake
bado inaendelea vilevile. Madaktari bingwa kutoka
nchi mbalimbali kubwa duniani. Waliweza kuingia
ndani ya Tanzania kwa lengo la kumtibu Rahab, ila
mbinu zao za kumtibu hazikuzaa matunda kwani
hali ya Rahab haikuweza kubadilika jambo lililo zidi
kuwachanganya sana madaktari.
***
Chama pinzani cha TDPP(Tanzania Democras
People Party), hadi wakati huu hakikuwa na
mgombea wa uraisi. Chama hicho kilicho jipatia
umaarufu mkubwa kwa wananchi wa wafuasi
wengi, bado kilijikuta kikiendelea kumsikilizia
mgombea atakaye simamishwa na chama tawala
cha TSD. Chama hicho kikajikuta kikijipatia fedha
nyingi kutoka kwa wadhamini wanadada walio
jitambulisha kwamba wao ni wafanya biashara
kutoka Marekani. Japo wao ni watanzania ila
waliwaomba viongozi wa TDPP, kukubali msaada
wao lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba
wakakitoa chama tawala madarakani.
Manka akiwa ndio kiongozi wa wezake, wakiwa
ndani ya mkutano wa chama cha TDPP, wakatoa
mchango wa bilioni tano za kimarekani, ili
kukiwezesha chama hicho kuweza kupambana
katika kukitoa chama tawala madarakani.
Ukumbi mzima ukalipuka kwa furaha, wanachama
na viongozi wao wakajikuta wakishangilia kwa
furaha, kwani ni msaada wa pesa nyingi sana.
Hapakuwa na aliye weza kutambua ni nini mpango
wa mabinti hao ambao wameungana nao na kuwa
ni kitu kimoja
***
Madaktari wakagundua kwamba black Shadow
amevunjika mbavu mbili, wakamtoa ndani ya
chumba cha kupigia X rays na kumuwahisha katika
chumba cha Oparesheni. Sabogo na wapambe
wake tayari wakawa wamesha fika katika hospitali
hiyo na kuendelea kusikilizia kitu kinacho endelea,
japo upande mmoja wana furaha ya ushindi
mkubwa walio upata, ila kwa upande mwengine
wamepata huzuni kwani mpiganaji wao yupo katika
hali mbaya.
Kitu kilicho muumiza kichwa Sabogo ni jinsi ya
moja ya makubaliano yake na black shadow,
ambayo hakupenda sura yake ionekane na mtu
yoyote, mbaya zaidi anatafutwa ndani ya Japani
nzima.
“Bosi sasa itakuwaje?”
Mmoja wa wapambe wa Sabogo alimuuliza bosi
wake juu ya hilo.
“Inabidi nizungumze na daktari wa oparesheni”
“Sawa”
Kwa bahati nzuri kuna nesi alitoka kwenye chumba
cha upasuaji, kwa haraka Sabogo akamsimamisha,
ila akajikuta akiwa amemkodolea macho pasipo
kuzungumza kitu cha aina yoyote. Uzuri wa nesi
huyo, ulimfanya mpambe wa Sabogo, atambue
kwamba bosi wake amepata udhaifu fulani kwa
nesi huyo. Sabogo akastuka kidogo baada ya
kugongwa bega kidogo na mpambe wake.
“Nakusikiliza kaka, nina haraka nahitaji kwenda
nilipo agizwa”
“Ahaaa……aaha…a..Nilikua nasema, nasema eti,
nakuomba usimtoe kinyago mgonjwa wetu”
“Kwa nini, inabidi tumtoe kinyago chake ili
kuhakikisha kwamba mfumo mzima wa damu
katika mwili wake unakwenda vizuri”
Macho ya Sabogo yakatua upande wa kushoto
mwa kifua cha nesi huyo na kusoma jina lake,
mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio.
“Nesi Phidaya”
“Ndio nakusikiliza”
“Nakuomba sana musimtoe kinyago chake
mpiganaji”
“Tutaangalia, naona muda hauniruhusu”
Nesi Phidaya akaondoka na kumuacha Sabogo
akiwa amebaki amemkodolea nesi huyo macho
hadi akapotelea kwenye kona na kushusha pumzi
nyingi.
“Bosi mbona kama unamshangaa huyu nesi
umependa nini?”
“Hapana kama ninamfahamu?”
“Una mfahamu!!!”
“Ndio nimesha wahi kumuona”
“Kumuona wapi?”
Sabogo akasogea pembeni kwenye viti vya plastiki
vilivyo jengewa kama benchi wakakaa na mpambe
wake ambaye ndio msiri mkubwa na mshauri wake
kwa miaka mingi.
“Kuna siku black shadow, alinisimulia historia yake
ya nyuma”
“Historia gani?”
“Kuhusiana na ndoa yake pamoja na familia yake
ambayo ilisha toweka duniani. Ila kitu kinacho
nishangaza ni huyo msiachana. Anafanana sana na
mke wa Eddy”
“Eddy!!! EDDY ndio nani?”
Sabogo akajikuta akipata kigugumizi kwani moja
ya mambo ambayo black shadow alimueleza ni juu
ya jina lake halisi na hakulihitaji jina lake hilo mtu
kulifahamu. Sabogo akakiinua kicha chake chenye
mawazo mengi, akastuka kuona macho yake
yamegongana na nesi Phidaya ambaye
amesimama sekunde kadhaa akiwasikiliza
mazungumzo yao.
“Unamfahamu Eddy wewe?”
Nesi Phidaya alimuuliza Sabogo aliye baki
akimtumbulia macho asijue ni nini azungumze.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 51 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (51)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Kuhusiana na ndoa yake pamoja na familia yake
ambayo ilisha toweka duniani. Ila kitu kinacho
nishangaza ni huyo msiachana. Anafanana sana na
mke wa Eddy”
“Eddy!!! EDDY ndio nani?”
Sabogo akajikuta akipata kigugumizi kwani moja
ya mambo ambayo black shadow alimueleza ni juu
ya jina lake halisi na hakulihitaji jina lake hilo mtu
kulifahamu. Sabogo akakiinua kicha chake chenye
mawazo mengi, akastuka kuona macho yake
yamegongana na nesi Phidaya ambaye
amesimama sekunde kadhaa akiwasikiliza
mazungumzo yao.
“Unamfahamu Eddy wewe?”
Nesi Phidaya alimuuliza Sabogo aliye baki
akimtumbulia macho asijue ni nini azungumze.
ENDELEA
Sabogo akatingisha kichwa akionekana kukataa
kwamba amfahamu Eddy.
“Eddy ninaye mzungumza ni rafiki yangu ambaye
nilisoma naye”
Sabogo alidanganya, Phidaya akamtazama kwa
muda Sabogo kisha akandoka pasipo kuzungumza
kitu chochote.
“Bosi”
Mpambe wa Sabogo alimuita bosi wake aliye
onekana kuwa na wasiwasi kidogo.
“Nini?”
“Huyo Eddy ni nani?”
“Ehee tuachane na hizo story”
Sabogo alizungumza huku akiondoka kuelekea
kwenye chumba cha mapumziko, akiwa anafikiria
ni kitu gani ambacho kitatokea pale black shadow
atakapo onekana sura yake.
Daktari mmoja kwa kutumia mkasi akaanza
kuzichana nguo za Black Shadow ambazo
zimembana sana mwilini mwak. Alipo maliza
kuzichana suruali akafwatia nguo ya juu. Nesi
Phidaya akaingia akiwa na kiboksi kidogo alichyo
agizwa na daktari mkuu wa opareshini ambaye ni
mume wake bwana Ranjiti.
“Mbona umechelewa wakati hali ya mgonjwa si
nzuri?”
Alizungumza bwana Ranjiti huku akianza
kuupitisha mkasi wake kwenye mikanda ya
kinyago alicho vaa Black Mask.
“Samahani dokta”
Nesi Phidaya alizungumza huku akikiweka kiboksi
hicho cha dawa kwenye sinia kubwa lililo jaa
mikasi na visu visogo vidogo. Kabla hajamalizia
kukata mikanda miwili ili kuifunua sura ya black
Mask, nesi Phidaya akamshika mumewe mkono
hadi madaktari wengine wawili wakashangaa.
“Vipi?”
“Meneja wa huyu mpiganaji ameniomba tusimvue
kinyago chake?”
“Kwa nini?”
“Hakunieleza ni kwa nini, ila amenisisitiza kwamba
tusimvue”
Bwana Ranjiti, akashusha pumzi kidogo huku
akimtazama mke wake machoni, kutokana
anamuamini na kumpenda sana mke wake kuliko
kitu chochote, akalisikiliza ombi la mkewe.
Wakaanza kazi ya kuchana sehemu ya mbavu za
Black Shadow, ambazo zimevunjika. Kazi ya
Phidaya ikawa ni kuwakabidhi madaktari kila
wanacho kihitaji katika kazi hiyo ya upasuaji.
Oparesheni ikachukua takribani masaa manee hadi
kumalizika. Dokta Ranjiti na mwenzake mmoja
wakamtoa Eddy katika chumba cha upasuaji
wakimuacha Phidaya na daktari mwengine
wakisafisha safisha vifaa na chumba kwa ujumla.
Waandishi wa habari ambao wameweka kambi
wakisubiria kupata ripoti ya hali ya Black Shadow.
Wakaanza kumpiga picha akiwa anapelekwa katika
chumba cha wagonjwa mahututi. Kitanda cha
matairi alicho lazwa Black Shadow kikaendelea
kusukumwa taratibu na msadizidi wa dokta Ranjiti
huku, dokta Ranjiti na yeye akiwa mbele akikivuta
kitanda hicho na kuwaomba waandishi wa habari
kupisha njia. Sa Yoo na Shamsa walipo sikia
kwamba Black Shadow ametolewa katika chumba
cha upasuaji, wakakimbilia hadi kwenye chumba
walicho ambiwa kwamba Black Shadow amelazwa.
Kwa bahati mbaya wakakuta tayari Black Shadow
ameingizwa ndani ya chumba hicho ambacho
haruhusiwi mtu wa aina yoyote kuingia pasipi
idhini maalumu ya daktari.
“Inabidi twende nyumbani”
Sa Yoo alizungumza huku akipiga usingizi kwani ni
majira ya saa kumi na moja alifajiri.
“Wewe nenda siwezi kuondoka hapa hospitalini”
“Kwa nini sasa, wakati unasikia hali ya mgonjwa
inaendelea vizuri?”
“Wewe nenda mimi nitabaki tu hapa”
“Shamsa twenda nyumbani japo mara moja,
tukaoge, kisha nakuahidi rafiki yangu tutarudi tena
hapa”
Sa Yoo akaendelea kumbembeleza Shamsa anaye
onekana kuchanganyikiwa na mapenzi mazito juu
ya Black Shadow, Shamsa akakubaliana na Sa Yoo
kuondoka na baada ya lisaa limoja watarejea katika
hospitali hiyo, ili tu aweze kumuona Black
Shadow.
Nesi Phidaya baada ya kumaliza kufanya usafi
katika chumba cha upasuaji, akaelekea ofisini
kwake ambapo akabadilisha mavazi yake ya kazi,
akapitia ofisini kwa mume wake akamuaga kisha
yeye akaelekea nyumbani, kujipumzisha akisubiria
kuingia tena hospitali usiku. Phidaya moja kwa
moja akelekea chumbani kwake, akaingia bafuni na
kuoga kisha akarudi na kuketi kwenye sofa lililomo
ndani ya chumba chake.
“Mimi ni nani?”
Hilo ndilo swali ambalo siku zote linamuumiza
kichwa Phidaya, kila alipo jaribu kuvuta
kumbukumbu zake za nyuma hakuna kitu ambacho
anakikumbuka. Ila kitu alicho ambiwa na mume
wake kwamba yeye ni Phidaya, ndio jina lake
halisi. Huku jina la baba yake likiwa ni Eddy.
“Phidaya Eddy”
Aliendelea kujiuliza swali hilo, akasimama na
kuanza kutembea hadi kwenye kabati kubwa,
akatoa albamu yenye picha zaidi ya mia tano.
Akaanza kuzitazama moja baada ya nyingine.
Picha zake za harusi na bwana Ranjiti, zilimfariji
sana kila alipo zitazama. Akazidi kujiona ni
mwanamke wa kipekee na mwenye bahati kubwa
sana kwenye maisha yake kutokana na kuolewa na
daktari maarufu nchini Japan na mwenye hospitali
yake inayo tibu watu maarufu ndani na nje ya
Japani.
Uhodari wa mume wake katika swala zima la
upasuaji lilimfanya azidi kumpenda mume wake
huyo japo kiumri mume wake amempita miaka
kumi na tano. Akaibusu picha moja ya mume wake
na kuikumbatia albamu nzima kifuani mwake,
taratibu akajitupa kitandani na kujilaza.
***
Alfajiri na mapema majira ya saa moja asubuhi,
Mzee Godwin akiwa na John pamoja na walinzi
wake, wakakutana na Sabogo meneja wa Black
Shadow, kwenye moja ya ofisi ndogo walio
ichukua katika hoteli waliyo fikizia.
“Hali ya mgonjwa wako inaendeleaje?”
Mzee Godwin aliuliza huku akiwa amemkodolea
macho Sabogo.
“Madaktari wamemaliza upasuaji na anaendelea
vizuri”
“Sawa. Tunaweza kumuona?”
“Hapana, kutokana bado hajarudisha fahamu zake
hakuna mtu ambaye ataruhusiwa kumuona”
“Ok, lengo kubwa la sisi kuja hapa Japan ilikuwa ni
kuonana na yeye. Kutokana hali yake sio nzuri
basi tutaondoka na kurudi America kisha baada ya
siku kadhaa basi tutarejea kuonana naye kwa
maana tunahitaji kuzungumza naye ana kwa ana”
“Hilo halina tatizo, ila kabla ya yote ninahitaji
kufahamu kwamba nyinyi ni kina nani?”
“Sisi ni wafanya biashara kutoka Marekani, na pia
ni watengenezaji wa filamu kwa hiyo tulihitaji
kuzungumza naye kwa maswala ya uigizaji”
John alimuongopea Sabog, ambaye bado
aliendelea kuwa na wasiwasi mwingi moyoni
mwake huku akiwatazama wafanya biashara hao
walio muita asubuhi yote.
“Ahaaa, kama ni hivyo nitahitaji kuzungumza naye
mimi mwenyewe na atakapo kubaliana na ombi
lenu basi nitawapigia simu kuja kukutana naye”
“Sawa, tutakuachia namba za simu kwa
mawasiliano zaidi”
“Sawa”
Mpambe mmoja wa mzee Godwin akatoa kikadi
kidogo na kumkabidhi Sabogo, aliye kipokea
akakisoma vizuri kisha akikitumbukiza mfukoni
mwake. Kabla hajaondoka Mzee Godwin akaomba
wapige picha za ukumbusho na Sabogo aliye
kubaliana na ombi hilo. Kisha naye Sabogo akatoa
simu yake na kumpa mmoja wa wapambe wa mzee
Godwin aliye wapiga picha kadhaa, akachuku simu
yake, wakaagana na kuondoka zke.
Hapakuwa na muda mwengine wa kupoteza ndani
ya Japan, mzee Godwin na John wakiwa na
wapambe wao wakaelekea uwanja wa ndege
wakaondoka kurudi zao bara la Amerika.
***
Kwa siku mbili mfululizo Shamsa na Sa Yoo
waliendelea kusubiri kuruhusiwa kuweza kumuona
Black Shadow ambaye, madaktari waliendelea
kuwazuia watu wasiweze kuingia kwenye chumba
hicho kwani bado hali ya mgonjwa ni mbaya.
Mashabiki wengi wana mshangilia Black Shadow
walijitokeza nje ya hospitali hiyo wakiwa na maua
pamoja na picha kubwa ya Black Shadow, iliyo
wekwa kwenye moja ya bustani katika hospitali
hiyo, wakifanya maombi ya kumuombea mpiganaji
huyo kuweza kupona haraka.
Shamsa na Sa Yoo nao waliungana na mashabiki
hao kukesha nao katika bustani hiyo, kila watu
wakiomba kwa dini yao ili mradi Mungu aweze
kumponya Black Shadow ambaye hadi sasa hivi
hakuna aliye muona sura yake.
Viwanda kadhaa vya nguo ndani ya Japani, vilisha
anza kutegeneza nguo nyeusi zinazo fanana na
Black Shadow. Nguo hizo zilizo tokea kupendwa
na watu wengi ziliuzika kwa gharama kubwa, ila
wananchi walizidi kuzigombani, ili mradi tu mtu
azinunue na kuonekana anafanana na mpiganaji
huyo aliye tokea kutingisha Japani nzima kwa
umaarufu wake.
Macho ya Phidaya yakaendelea kutazama tazama
kupitia kwenye dirisha kubwa la ofisi yake iliyopo
gorofa ya pili kutoka chini, watu wengi walio
jitokeza kwenye bustani ya hospitali hiyo wakiweka
maua mengi kwenye picha kubwa ya Black
Shadow.
“Huyu mpiganaji anapendwa sana ehee?”
Alijiuliza Phidaya huku akiendelea kuwatazama
wananchi hao, wakubwa kwa watoto. Wababa kwa
wamama. Mlango wa ofisini kwake ukafunguliwa na
kumlazimu kugeuka akamuona mume wake
akiingia huku sura yake ikiwa imetawaliwa na
furaha sana.
“Kumbe bado hujaondoka tu mke wangu?”
“Ndio baby, vipi mbona una furaha sana”
“Yaani mgonjwa wetu amezidi kuiongezea
umaarufu hospitali yetu. Nimepewa taarifa kwama
kesho raisi anakuja kumtembelea mgonjwa”
“Weeeeee sema kweli mume wangu?”
“Haki ya Mungu, yaani sikuwahi kufikiria kwamba
ipo siku raisi atakuja kutembelea hapa”
Bwana Ranjiti akamkumbatia mke wake na wote
wakajikuta wakipongezana kwa furaha, kwani ugeni
wa kesho ni mkubwa sana.
“Ila vipi mgonjwa anaendeleaje?”
“Hali yake inazidi kunipa matumaini kwa maana
leo ni tofauti na jana, na juzi”
“Ila si atazinduka?”
“Ndio atazinduka tu”
“Itabidi kabla ya kwenda nyumbani nikamuone”
“Hakuna tatizo.”
Bwana Ranjiti akalisogelea dirisha kubwa na
kuwaangalia wananchi walio jiotokeza kwenye
hospitali hiyo, waandishi wengi wa habari nao
waliendelea kuchukua matukio na kuyarusha moja
kwa moja kwenye vitu vyao vya televishion na
redio. Bwana Ranjiti akajikuta akizidi kufarijika na
kuona kwamba mchango wa mpiganaji wake
umezidi kuipa umaarufu hospitali yake.
Phidaya akamuaga mume wake na kuelekea
kwenye chumba cha wagonjwa mhututi(ICU).
Akavaa mavazi maalumu ya kuingilia ndani ya
chumba hicho. Akaingia na kuufunga mlango kwa
ndani, taratibu akaanza kupiga hatua hadi kwenye
kitanda kilicho zungukwa na mashine nyingi, huku
kila moja ikiwa na kazi yake mwilini mwa Black
Shadow.
Macho yake Phidaya, yakaanza kukichunguza kifua
cha Black Shado, kilicho funikwa nusu kwa shuka
zito, huku nusu iliyo baki ikiwa imewekwa vifaa
maalumu vivili vinavyo msaidia mapigo yake ya
moyo kwenda vizuri.
‘Kwa nini alikataa sura yake isionekane’
Phidaya alijiuliza huku akimkumbuka Sabogo, aliye
msisitiza kwamba sura ya mpiganaji huyo haitakiwi
kuonekana, Taratibu Phidaya akaanza kuupeleka
mkono wake wa kulia katika kinyago cha Black
Shadow kwa lengo la kukitoa ili aweze kumuona.
***
Viongozi wa chama cha upinzani cha TDPP
(Tanzania Democras People Party), wakazidi
kuwaamini Manka pamoja na wezake. Viongozi
watano wa ngazi ya juu, akiwemo mwenye kiti wao
bwana Kibwila.Wakawaalika katika halfa fupi ya
chakula cha usiku katika Kilimanjaro Hoteli.
Viongozi hao walio changanywa na wingi wa pewa
walizo kabidhiwa na wafanya biashara hao wa kike,
hawakuwa na hiyana walipo ambiwa kwamba
wasifike na wake zao katika halfa hiyo waliyo
alikwa kwani pia itakuwa ikizungumzia kuhusiana
na maswala ya kichama na na ni jinsi gani
wanavyo weza kukitoa chama tawala madarakani.
Chakula kilicho andaliwa na wapishi hodari katika
hoteli hiyo, kilianza kutafunwa taratibu na viongozi
hao pamoja na wafanya biashara Manka na
wezake. Kila mmoja alijikuta akikisifia chakula
hicho kwamba nikitamu na wengine wakiri kwamba
hawakuwahi kukila chakula hicho tangu wazaliwe.
Furaha na vicheko vilizidi kutawala katikati yao,
huku wakijadili mambo mengi yaliyo wahi
kujitokeza katika chama hicho hadi kushindwa
kuingia madarakani miaka mitano iliyo pita.
“Jamani natambua kwamba tunahitaji mgombea
mwenye nguvu na atakaye weza kuchukua
madaraka si kweli jamani?”
Fetty alizungumza huku akiwatazama viongozi hao.
“Ni kweli kabisa”
“Pia tunahitaji kiongozi anaye weza kupambana na
kila jambo linalo tokea ndnai ya hii nchi, si
kiongozi kama Praygod ambaye ameshindwa
kupambana na ugaidi ulio sababisha maisha ya
ndugu zetu wengi kupoteza maisha yao”
“Kweli kabisa”
“Basi sisi kama mukitupa ridhaa tutatawapa nyinyi
mgombe ambaye ataweza kupambana na haya
yote”
“Hakuna shida kabisa, kwa maana kama mgombea
atakuwa ni kati ya sisi hapa hakuna tatizo”
Bwana Kibwila alizungumza huku akitabasamu
tabasamu
“Hapana bwana Kibwila, mgombea ambaye
tutamsimamisha kupitia chama chenu atakuwa ni
huyu hapa”
Fetty akamkonyeza Anna aliye shika romoti ya Tv
kubwa iliyomo ndani ya ukumbi huo. Viongozi
wote macho yaliwatoka walipo iona picha ya Mzee
Godwin, kwani kila mmoja anamtambau kwamba ni
gaidi wa kupindukia na inakuwaje wamsimamishe
kama mgombea uraisi wao.
***
Mkono ya Phidaya ikanza kutetemeka kila alipo
karibia kukishika kinyango cha Black Shadow.
Akaurudisha mkono wake nyuma huku akishusha
pumzi nyingi. Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda
mbio kiasi cha kumfanya aogope.
‘Naogopa nini na mimi?’
Phidaya alijisemea kimoyo moyo. Akatoa woga
moyoni mwake kisha akaupeleka kwa kasi mkono
wake hadi kwenye kinyago cha Black Shadow,
akaufungua mkanda wa pili, kisha akaumalizia
mkanda wa tatu. Taratibu akaanza kukinyanyua
kinyago cha Black Shadow, asiye jitambua kwa
kupoteza fahamu, hadi kinyago hicho
akakitenganisha na sura yake. Moyo wake
ukampasuka baada ya kuiona sura ya Black
Shadow. Hofu ikamtawala, macho yakamtoka huku
akiwa amenata kama amegandishwa na sumanku,
kwa mbali akaanza kuhisi haja ndogo ikianza
kumwagika taratibu.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 52 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (52)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
‘Naogopa nini na mimi?’
Phidaya alijisemea kimoyo moyo. Akatoa woga
moyoni mwake kisha akaupeleka kwa kasi mkono
wake hadi kwenye kinyago cha Black Shadow,
akaufungua mkanda wa pili, kisha akaumalizia
mkanda wa tatu. Taratibu akaanza kukinyanyua
kinyago cha Black Shadow, asiye jitambua kwa
kupoteza fahamu, hadi kinyago hicho
akakitenganisha na sura yake. Moyo wake
ukampasuka baada ya kuiona sura ya Black
Shadow. Hofu ikamtawala, macho yakamtoka huku
akiwa amenata kama amegandishwa na sumanku,
kwa mbali akaanza kuhisi haja ndogo ikianza
kumwagika taratibu
ENDELEA
Kwa haraka Phidaya akakirudisha kinyago cha
Black Shadow kama kilivyo kuwa, akaanza
kutembea kwenda nje kwa vishindo. Kabla hata
hajafika mlangoni, akasikia mashine moja ikipiga
mlio, ikamlazimu kugeuka kwa haraka, macho yake
yakatua kwenye mashine inayo hesabu mapigo ya
moyo. Kwa kasi kubwa mapigo ya moyo ya Black
Shadow yakawa yanashuka.
“Mungu wangu?”
Phidaya alizungumza huku akijaribu kukiminya
kifua cha Black Shadow ili mapigo ya moyo
yasishuke, haikuwa kazi rahisi kwake, ikamlazimu
kuminya batani ya dharusa iliyo mtaarifu daktari
mkuu ofisini kwake, kwamba chumba alicho lazwa
Black Shadow kuna tatizo.
Haikupita hata dakika mbili Phidaya akasikia
mlango ukigongwa kwa nje, kwa haraka
akakimbilia kwenye mlango, wakaingia madaktari
wawili akiwemo na mume.
“Kumetokea nini?”
“Mapigo yake ya muyo yamebadilika gafla”
“Washa mashine”
Dokta Ranjiti aliwaamrisha wezake, kwahara
mashine ya umeme inayo tumika katika
kupandishia mapigo ya moyo ikawashwa. Kwa
haraka wakaanza kuigandamiza kifuani mwa Black
Shadow, na kukifanya kifua chake kustuka. Zoezi
hilo wakalifanya kwa dakika kadhaa pasipo
kuchoka, hadi inatimu mara ya ishirini na tano,
mapigo ya moy ya Black Shadow, yakarudi katika
hali yake ya kawaidia, kila mmoja akajikuta
akishusha pumzi ya wasiwasi.
Walipo hakikisha kwamba Black Shadow amerudi
katika hali yake ya kawaidia, wote wakatoka ndani
ya chumba, Phidaya na mume wake wakaelekea
ofisini.
“Baby kuna kitu nataka kukuambia”
Phidaya alizungumza mara baada ya kukaa kwenye
moja ya sofa lililopo ndani ya ofisi ya mume wake.
“Jamb……..”
Kabla Dokta Ranjiti hajamalizia sentesi yake simu
yake ya mezani ikaita ikabidia achukue mkonga wa
simu hiyo na kuiweka sikioni.
“Habari dokta Ranjiti”
Haikuwa ni sauti ngeni sana masikioni mwake.
Dokta Ranjiti akamtazama mke wake kwa macho
ya kuiba kisha akaiweka miwani yake sawa na
kuendelea kumsikiliza mtu aliye mpigia simu.
“Unatatizo gani?”
“Ohooo tatizo, unajua ni nini tatizo langu. Nahitaji
pesa, la sivyo nitamuambia kila kitu Phidaya
mwanamke unaye jifanya kumpenda”
Sauti hiyo ya kike ilimfanya dokta Ranjiti
kumwagika na kijijasho chembamba, hakuweza
kuzungumza jambo lolote mbele ya Phidaya. Woga
wake ulimfanya kuwa mtumwa wa siri kwa mtu
anaye mpigia simu.
“Unahitaji kiasi gani?”
“Ohooo hayo sasa ndio maneno. Najua hospitali
yako kwa sasa inakuingizia pesa nyingi sana.
Nahitaji dola milini moja, uiingize kwenye akauti
yangu ndani ya masaa kumi, la sivyo. Siri inakuwa
dirisha”
Simu hiyo ikakatwa na kumuacha dokta Ranjiti
akiwa katika hali ya mawazo, jambo hilo Phidaya
alilitambua kwamba simu iliyo pigwa imemkosesha
amani mume wake.
“Baby kuna tatizo?”
“Ahaa..ahaa hapana, nahitaji kwenda bank mara
moja”
“Kufanyaje usiku huu?”
“Ahaaa tutazungumza nikirudi”
Dokta Ranjita alizungumza huku akivua koti lake
jeupe na kuvaa koti lake la suti, akachukua funguo
ya gari lake kwenye droo ya mezani mwake,
akampiga busu la mdomoni Phiday kisha
akaondoka na kumuacha mke wake akiwa
hajazungumza kitu alicho kuwa amekusudia
kuzungumza.
***
Macho ya Shamsa yakamshuhudia dokta Ranjiti
akitembea kwa kasi akitoka katika mlango wa
kuingilia hospitalini. Akamuwahi na
kumsimamisha.
“Sahamani dokta, hali ya black shadow
inaendeleaje?”
“Vizuri, ila samahani binti nina haraka nahitaji
kuondoka kunasehemu nawahi”
“Lini atapona dokta?”
“Endeleeni kukesha na kumuombea, samahani
nahitaji kuwahi binti”
Dokta Ranjiti hakuona sababu ya kuendelea
kuzungumza na Shamsa, akaelekea kwa haraka
kwenye maegesho ya magari, akaingia ndani ya
gari lake na kuondoka kwa kasi hadi baadhi ya
watu walikishangaa hicho kitendo.
Shamsa akatazama huku na kule, alipo ona hakuna
mtu anaye mfwatilia, akaanza kutembea kwa
haraka kuelekea ndani ya hospitali, moja kwa moja
akaanza kuchunguza ni chumba gani wanacho
badilishia nguo manesi. Haikumchukua muda
mwingi sana kukipata chumba hicho, akaingia na
kukuta hakina mtu zaidi ya madroo mengi yaliyo
jengwa vizui ndani ya chumba hicho na katika kila
droo kuna mlango na juu yake ukiwa umeandikwa
jina la nesi anaye husika na droo hiyo. Akaanza
kuvuta kitasa cha droo moja baada ya nyengine,
mbili za mwanzo akazikuta zikiwa zimefungwa, ila
ya tatu akakuta ikiwa haijafungwa, akaifungua na
kukuta magauni mawili ya nesi huyo mwenye jina
la Si Ngii. Akachomoa gauni moja na kulipimisha
kwa urefu wa mwili wake, kwa bahati nzuri
limeendana naye. Akazivua nguo zake alizo zivaa,
akalivaa gauni hilo haraka haraka. Nywele zake
ndefu alizo kuwa amezibana kwa nyuma,
akazifungua na kuzimwaga kwa chini, kwa bahati
nzuri ndani ya droo hiyo akaona miwani ya macho
akaichukua na kuivaa. Akazichukua nguo zake na
kuzisokomeza ndani ya droo hiyo. Akaanza
kutembea kueleka mlangoni mwa chumba hicho,
kabla hajafika, mlango ukafunguliwa, akaingia nesi
mmoja anaye onekana kuwa na haraka,
hawakusemeshana kitu zaidi ya kupishana huku
Shamsa kichwa chake akiwa amekielekeza chini.
Akaanza kutembea kwenye kordo ndefu, kuelekea
katika chumba alicho lazwa Black Shadow.
Hakutaka kuinyanyua sura yake juu, kwani alihofiwa
kustukiwa, akazidi kupiga hatua za haraka hadi
kwenye mlango wa kuingila katika chumba cha
wangojwa mahututi. Akashika kitasa cha mlango
huo taratibu akaanza kukishusha chini huku
akitazama kuli na kushoto kwake. Akausukuma
mlango na kuingia ndani, akaurudishia mlango
huo, akageuka na kumtazama Black Shadow,
akiwa amelala juu ya kitanda huku akiwa
amezungukwa na mashine kadhaa. Akaanza
kupiga hatua kuelekea kitandani, hata kabla
hajakifikia kitanda milio mingi ya risasi ikaanza
kusikika nje ya chumba hicho, huku ving’ora vya
hatari vya hospitalini hapo vikianza kulia kwa
nguvu jambo lililo mstua Shamsa na
kumuogopesha sana.
***
Kitendo cha Young Po,kushindwa kutetea taji lake,
kilizidi kumuumiza sana. Kwenye maisha yake
hakuwahi kutarajia kwamba itakuja kutokea siku
atakuja pigwa na mtu katika mapambano ya
ulingoni. Hasira na chuki zikazidi kumpanda kila
alipo utazama mkono wake ulio vunjwa na Black
Shadow.
‘Lazima nifanye kitu’
Young Po alizungumza huku macho yake yakiwa
kwenye Tv kubwa iliyomo ndani ya chumba alicho
lazwa kwenye moja ya hospitali. Alikuwa akitazama
taarifa, kwenye kitua cha Jtv, kilicho kuwa
kikitangaza kwamba siku inayo fwata raisi wa nchi
hiyo atakwenda kumtembelea Black Shadow,
mpiganaji aliye tokea kupendwa na watu wengi.
Wivu ukazidi kumtawala Young Po, kwa haraka
akachukua simu yake iliyopo mezani, akaminya
namba kadhaa kwenye simu, baada ya sekunde
thelathini simu hiyo ikapokelewa.
“Njooni hospitaki sasa hivi”
Young Po akakata simu, baada ya robo saa,
mwanaume mmoja na mwanamke mmoja
wakaingia ndani ya chumba chake. Akawapa
maelekezo ambayo anahitaji yaweze kutekelezwa
usiku huo. Vijana hao hawakua na swali kwani
walimeelewa kazi ambayo wamepewa na bosi wao
huyo. Wakatoka hospitalini moja kwa moja
wakaelekea kwenye makao yao, ambapo,
wakawaelekeza vijana wengine watatu ambao
waliwaacha katika nyumba yao. Mpango wa
kutafuta gari ya wagonjwa, ikaanza. Halikuchukua
muda mrefu sana ndani ya lisaa gari ya wagonjwa
ikaletwa kwenye nyumba yao.
Bunduki zao zilizo jaa risasi za kutosha
wakaziweka ndani ya gari hilo, wkila mmoja
akachomeka silaha ambayo alihisi kwamba
itamsaidia katika kazi hiyo. Wakavalia mavazi ya
udaktari, kisha safari ikaanza kuelekea katika
hospitali aliyo lazwa Black Shadow.
***
Phidaya baada ya mume wake kuondoka, hakuona
haja ya kuendelea kukaa kazini, akavua mavazi
yake ya kazi na kuvaa mavazi aliyo kuja nayo
asubuhi. Akilini mwake akawa anafikiria kuhusiana
na donge nono ambalo polisi walilitangaza kwa
mtu ambaye atatoa ushirikiano wa kukamatwa
muhalifu ajulikanaye kwa jina la Eddy.
‘Lazima nipate pesa hizi’
Alijisemea Phidaya huku akidhamiria kuzipata pesa
kwa kuwatarifu polisi kwamba mtu wanaye mtafuta
ndio huyo Black Shadow aliye lazwa kwenye
hospitali yao. Akaanza kutembea kwa haraka
kuelekea kwenye maegesho ya magari, Akaingia
kwenye gari lake aina ya Aud A4.
‘Hakuna haja ya Ranjiti kujua’
Phidaya alijisemea kimoyo moyo huku akiwasha
gari lake na kuanza kuondoka, getini akapishana
na gari ya wagonjwa ikiingia huku likiwa linapiga
ving’ora. Hakutaka kulifwatilia sana kwa sababu
wapo madaktari wengine ambao watashuhulika na
mgonjwa huyo aliye letwa. Akaingia barabarani na
kuanza kuongeza mwendo kasi wa gari lake
kuelekea katika kituo kimoja cha polisi kilichopo
karibu na hospitali yao.
Ikamchukua dakika kumi kufika katika kituo hicho,
ika kabla hajasimamisha gari lake nje ya kituo
hicho, gari zipatazo kumi za polisi zilianza kutoka
kwenye kituo hicho kwa mwendo wa kasi.
“Mmmm kuna nini?”
Phidaya alizungumza huku akisimamisha gari lake
pembeni akizipisha gari hizi za polisi zipite, zilipo
malizika akaliegesha gari lake kwenye maegesho
ya hapo kituo cha polisi. Akashuka, askari mmoja
wa kike alipo muona Phidaya akamkimbilia hadi
sehemu alipo.
“Madam upo salama?”
Askari huyo alizungumza huku akimshika mkono
Phidaya.
“Ndio nipo salama kwani kuna tatizo gani?”
“Ina maana huna taarifa kwamba hospitalini kwako
kuna uvamizi wa majambazi?”
“Nini…..!!!”
Phidaya akajikuta akimtumbulia macho askari
huyo.
“Hizo gari zilizo toka hapo zinaelekea hospitalini
kwako”
“Twende twende”
Phidaya alizungumza huku akikimbia kwenye gari
lake, huku askari huyo akimfwata kwa nyuma,
wakaingia kwenye gari na safari ya kurudi
hospitalini ikaanza tena kwa mwendo wa kasi
sana.
***
Majambazi hao walio agizwa na Young Po,
wakasimamisha gari lao karibu kabisa na mlango
wa kuingilia ndani ya hospitali, manesi wawili
wakatoka na kuwapokea madaktari hao walio mleta
mgonjwa mmoja aliye lazwa kwenye kitanda cha
matairi wakaanza kumkimbiza ndani pasipo
kufahamu kwamba hao si madaktari. Wakiwa
katikati ya kordo, manesi wakastukia, mgonjwa
wanaye msukuma kwenye hicho kitanda
akinyanyuka huku akiwa na bastola mbili mkononi
mwake.
Manesi hao katika kushangaa, mmoja wao akaona
usalama wake ni bora akimbie, risasi kadhaa
zikamuingia kwenye mwili wake. Milio hiyo ya
risasi ikawastua watu wote walio kuwa ndani na
nje ya hospitali. Watu walio kuja kumuombea
Black Shadow, wote wakajikuta wakianza
kutawanyika kila mmoja akijaribu kuiokoa roho
yake. Baadhi ya walinzi wa hospitali wakakimbila
kwenye eneo la tukio huku wakiwa na bunduki
zao. Majibizano ya risasi baina ya walinzi na
majambazi hao walio fika hospitalini kwa lengo la
kumuua Black Shadow, yakazidi kupamba moto.
Shamsa akafungua mlango wa chumba alichopo,
akachungulia nje, akashuhudia nesi mmoja akiwa
amelala chini, damu zikiwa zinamwagika, watu
walio valia kama madaktari wakazidi
kuwashambulia walinzi wanao pambana nao.
Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio Shamsa,
hakujua afanye nini kwa wakati huo. Hata kabla
hajafikiria kitu kingine, gafla mlango ukapigwa teke,
akaingia msichana aliye valia nguo za kinesi,
mkononi mwake akiwa ameshika bastola.
Shamsa hakuhitaji kufikiria mara mbili kwamba
huyo ni nani, Akarusha teke moja lililo tua mkononi
mwa msichana huyo wa kijapani. Bastola
ikaanguka pembeni, macho makalia ya msichana
huyo, yakampandisha Shamsa kuanzia chini hadi
juu, msichana huyo akaanza kurusha mateke
mazito yaliyo mfanya Shamsa kuanguka chini
sakafuni. Msichana huyo akaanza kupiga hatua za
kuifwata bastola yake ilipo anguka, hata kabla
hajaichukua Shamsa akajirusha na kuwahi
kumdaka mguu msichana huyo na kumuangusha
chini.
Msichana huyo akarusha teke moja la ambalo
Shamsa alilikwepa na kuvuta chini, wakaanza
kubingirishana chini, huku kila mmoja akijitahidi
kukaa juu ya mwenzake, ili amshushie makonde ya
kutosha.
Mbiringishano huo, ukawapeleka hadi kwenye moja
ya mashine, wakajigonga hapo na kuifanya
mashine hiyo kuanza kuyumba yumba na mwisho
ikaanguka chini. Binti huyo alipo muona Black
Shadow akiwa kitandani akajaribu kusimama ili
kufanya agizo alilo tumwa, ila hata kabla
hajamgusa Black Shadow, Shamsa akamvuta na
kumuweka chini, na kuendelea kumshindilia ngumi
nyingi za uso.
***
Majira ya saa nane usiku, Raisi Praygod akiwa
amejilaza kwenye sofa lililopo pembezoni mwa
kitanda alicho lala Rahab, hafla akahisi mtikisiko
kwenye kitanda cha Rahab, ikambidi kuyafumbua
macho yake. Akamkuta Rahab akiwa anajibiringisha
kitandani. Wasiwasi mwingi ukazidi kumtawala
Raisi Praygod Makuya, akasimama kwa woga. Gafla
Rahab akakaa kitako kitandani, akayafumbua
macho yake huku akihema, jasho jingi likimwagika.
“Rahab”
Raisi Praygod alimuuita Rahab, huku akirudi rudi
nyuma, Rahab aliendelea kumuangalia raisi
Praygod pasipo kumsemesha kitu cha aina yoyote.
Taratibu Rahab akaanza kushuka kitandani,
akasimama wima na kuanza kumsogelea Raisi
Praygod aliye anza kurudi nyuma, hadi akagota
ukutana, Rahab akazidi kumsogelea taratibu huku
akiendelea kumkazia macho.
***
Shamsa akazidi kumshindilia ngumi, msichana
huyo ambaye naye alizidi kujitahidi kumzungusha
Shamsa, hadi akafanikiwa kumuangusha chini,
akamkalia Shamsa tumboni, na yeye akaanza
kulipiza makonde ambayo Shamsa alipatia muda
mchache ulio pita. Wakaanza kubiringishana tena
wakiendelea sehemu ilipo angukia bastola. Binti
huyo, anaye onekana amefuzu mazoezi mengi ya
kupigana, akaendelea kumshushia ngumi zilizo
changanyikana na vibao Shamsa, aliye iona
bastola imelala pembezoni mwake.
Askari walio fika eneo la hospitali, wakaanza
kuwatoa watu katika eneo la hospitali, huku
wengine wakiizunguka hospitali kuhakikisha
kwamba hakuna jambazi ambaye anatoka nje ya
hospitali hiyo. Askari sita wakaingia ndani wakiwa
na bunduki zao, walitembea kwa tahadhari hadi
kwenye kordo ambapo waliwakuta walinzi wawili
wa askari wakimpa huduma ya kwanza mwenzao
aliye pigwa risasi. Majambazi wawili walipoteza
maisha na kubaki wawili kwenye kodro, wakiwa
wamejibanza. Mashambulinzi yakaanza upya huku
askari polisi wakishirikiana na walinzi wa
hospitalini wakaendelea kuwashambulia majambazi
hao walio jikuta wakizidiwa nguvu. Askari polisi
wakazidi kusonga mbele, kwa bahati mbaya
majambazi hao wakajikuta wakiishiwa na risasi.
Hapakuwa na jambo jengine la kujitetea zaidi ya
wao kujisalimisha kwa askari hao.
Askari hao wakawafunga pingu majambazi wote
wawili, wakiwa wanawamalizia kuwafunga pingu,
wakastushwa na mlio wa risasi ulio tokea kwenye
chumba kilicho andikwa ICU.
Askari wawili wakavamia ndani ya chumba hicho,
wakamkuta msichana mmoja akijizoa zoa
kunyanyuka, huku akiwa amemuua nesi mwenzie.
Aliye endelea kuvuja damu chini.
Askari hao wakamuamrisha nesi huyo muuaji
kunyoosha mikono yake juu. Nesi huyo hakuwa na
ubishi taratibu akanyanyua mikono yake juu, askari
mmoja akamsogelea na kumfunga pingu kwa
nyuma. Askari hao wakamtoa nesi huyo nje ya
chumba wakamjumuisha na majambazi wengine
wawili. Wakawatoa nje kabisa kwa ajili ya
kuwapeleka kituoni. Shamsa akajikuta akistuka
baada ya kumuona Phidaya akimfwata katika
sehemu alipo shikiliwa na polisi.
“Hawa ndio majambazi eheee?”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali, askari
mmoja akamuitikia, Phidaya bila hata kujiuliza
mara mbili, akamzaba kofi Shamsa, aliye kuwa
akimshangaa, pasipo kuamini kwamba huyo ni
Phidaya au laa, kwa maana wamefanana kila kitu.
Ilibidi baadhi ya askari wamzuie Phidaya
asiendelea kuwashambulia majambazi hao walio
ivamia hospitali yake.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 53 YA SIMUHILI HII.
 
Back
Top Bottom