Elections 2010 Slaa aunguruma Mwembeyanga, LIVE TBC1

Siyo Uwanja Mkubwa sana lakini unatosha. Unatumika kwa mpira wa miguu na burudani nyingine na kichanga kitupu. Wasiwasi wangu pale simu yako ya gharama acha nyumbani maani sisi wenyeji wa mitaa ya Bububu tunajua habari yake
 
Ufupi wa mambo ni kuwa dkt.Slaa kaisha kabisa.Nikisema hivyo ni katika kila hali hata ya kiafya.

Kutokana na fani yangu naweza kusema kuwa dkt.Slaa ana tatizo la hypertension.Kampeni ziishe akapumzike kabla hajaanguka kwenye majukwaa.

Fani gani wewe, labda ya rural Medical officer!!!

Mgonjwa si anajulikana!!!
 
Dk Slaa ataongea na wana-Dar es Salaam na taifa kwa ujumla kwenye viwanja vya Mwembeyanga kuanzia saa 9 mchana. TBC watarusha live. Kabla ya kwenda Mwembeyanga atahutubia Manzese kuanzia saa 5 asubuhi hii.
 
Good Dr wa ukweli, tunakukaribisha Ikulu make sisi ndo waamuaji. Mwaka huu kieleweke
 
Ss sijajua kampeni zitaanza sa ngapi!! Lkn vyovyote vile lazima niwepo pale, the finest ondoa shaka kuhusu kiwanja, kiwanja ni kikubwa, ufanyefanye kazi zako twende tukamsikilize rais wetu mtarajiwa.

Heshima Suzane karibu jamvini.
 
Mkutano wa DR W P SLAA LIVE TOKA MwembeYanga

Nawakaribisha katika mkutano wa Mgombea uraisi kwa tiketi ya chadema DR W P SLAA unaofanyika hapa Kwenye uwanja wa Mwembe yanga watu wamejaa kweli kweli , kumefurika na kutia fora – Kuna watu wa aina mbalimbali hapa kuanzia wazee , vijana na wale watu wakati , kuanzia wamachinga mpaka wauza mitumba walioacha biashara zao kwa muda kwa ajili ya kuja kumwona dr slaa akinadi sera zake uwanjani hapa

Kwa wale walio mbali na maeneo haya wanafuatilia mkutano huu wanaweza kutazama TC1 Kuanzia saa 9 Kamili , wengine wanaweza kufuatilia kwa njia ya mtandao kama hii .

Kwa wale wanaopenda kuchangia Kampeni hizi wanaweza kutembelea blogu yetu kwa anuani www.marafikiwaslaa.blogspot.com kama una habari zaidi unaweza kututumia kupitia friendsofslaa@gmail.com

Wale wanaopenda kuchangia mkakati wa kutengeneza vipindi vya TV vinavyoendelea kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya TV na radio wanaweza kuchangia kupitia namba

+255766334049 MPESA
+255786806028 ZAP

Kama unataka Fulana za DR SLaa na Kofia zenye sahihi yake wasiliana na 0714 667026
 
Haki ya mama hata sie tulio kikazi West Africa tutasikiliza Mwembe Yanga! Hapa napata ITV vipi nao watarusha matangazo?
 
MwembeYanga in Uwanja mkubwa hata hivyo nina wasiwasi kama utatosha maana ile nyomi ya viwanja vya Tanganyika Parkers ilinitisha. Kumbukeni Temeke is one of highly populated areas in Dar

Hakuna Marefu Yasiyokuwa na Ncha.
 
Back
Top Bottom