LET'S CALL IT A NIGHT

Ronin

Senior Member
Apr 10, 2023
144
610
HII SIMULIZI NIMEISOMA IKANIVUTIA NIKAONA NISHEE NA WATAKAOTAKA KUISOMA.
Haina arosto.
Haina malipo.

Simulizi: Let's Call It A Night
Sehemu Ya Kwanza (1)

Leo ninaianza hadithi hii mpya ambayo nina uhakika itakwenda kukuhuzunisha, kukufurahisha, waliokata tamaa, watajazwa nguvu na hata wale wasiokuwa na matumaini, watapata matumaini mapya.

Ni hadithi ndefu mno ila kamwe haitoweza kukuchosha, kila utakaposoma, utatamani kujua kile kinachofuata siku ijayo. Kuwa nami, kwani pamoja na kukuhuzunisha huko, mwisho wa siku, kuna vingi utavifurahia na kufarijika.
Credit to Nyemo Chilongani

ANZA NAYO....!!!

Dar es Salaam, 2013
Saa 12.30 asubuhi, alamu ya simu ilikuwa ikilia kwa sauti kubwa, Henry akaamka kutoka usingizini, mwili wake ulikuwa na uchovu mwingi huku macho yake yakiwa mazito. Akainuka kitandani pale na kujinyoosha kiuchovu na kisha kuteremka kitandani pale.

Huku akionekana kuwa na uchovu mwingi, Henry akaanza kupiga hatua kuelekea bafuni kuoga. Kwa wakati huo, kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi juu ya kazi aliyokuwa akiifanya, kazi ya uandishi wa habari ambayo ilimpa heshima kubwa nchini Tanzania.

Alikuwa mwandishi wa magazeti yanayotolewa na Kampuni ya Amazon Newspapers iliyokuwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Henry alikuwa amejiwekea heshima kubwa kutokana na kazi hiyo aliyokuwa akiifanya.

Kila siku jina lake lilikuwa likisikika midomoni mwa watu kwamba alikuwa mwandishi bora asiyekuwa na mpinzani nchini Tanzania. Kazi zake, alikuwa akiziandika kwa ufasaha katika mtiririko ambao ulipendwa na kila mtu.

Mbali na uandishi wa magazetini, Henry alikuwa mwandishi wa vitabu vya Riwaya. Katika maisha yake, aliwahi kutoa vitabu vingi vya Riwaya vilivyotikisa sana Afrika Mashariki.

Uandishi wake wa vitabu ukampa fedha nyingi, akafungua biashara lakini kila siku, hakutaka kuacha kazi katika kampuni hiyo iliyokuwa imempa heshima kubwa, Kampuni ya Amazon Newspapers.

Mbali na mafanikio makubwa aliyokuwa nayo, Henry hakuwa ameoa. Mpaka kipindi hiki alikuwa amefikisha miaka ishirini na tano lakini kichwani mwake hakuwa na ndoto za kuoa kabisa.

Alipenda kuishi peke yake kwani alijua kwamba endapo angekuwa na mke, basi kazi zake za kuandika simulizi na kufanya kazi za kampuni zingeshuka na hivyo jina lake kupotea.

Mpaka muda huo, Henry alikuwa ameandika vitabu vya maisha ya watu wengi maarufu wakiwepo wanasiasa, wanamuziki, wanamichezo, wachungaji na watu wengine wengi maarufu.

Vitabu vyote ambavyo alikuwa ameviandika, vilinunuliwa mno kitu kilichoendelea kumpa fedha na heshima kubwa. Waandishi wadogo ambao walikuwa wakichipukia, walikuwa wakimtafuta kwa ajili ya kuwashauri juu ya kipi kilichotakiwa kufanyika ili nao wawe waandishi wazuri kama alivyokuwa.

“Soma sana vitabu, pia jitoe katika kila kitu kuhusiana na uandishi. Mbali na hivyo, jitahidi uwe mtafiti ili ujue mengi katika dunia hii,” alisema Henry mbele ya wanachuo wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha DSJ ambao wengi wao walikuwa wakitamani kuwa mwandishi kama alivyokuwa yeye.

“Mbali na mafanikio yako, kuna changamoto gani ambazo uliwahi kukutana nazo kabla?” aliuliza mwanachuo mmoja.

“Kuna mengi ambayo unakutana nayo kama mwandishi, wakati mwingine unachukiwa kwa kile unachokiandika, waandishi wenzako wa vitabu wataanzisha manenomaneno kwamba simulizi zako si nzuri, zote hizo tunaziita changamoto ambapo mara baada ya kuzisikia, hautakiwi kurudi nyuma, songa mbele zaidi,” alisema Henry.

Siku hiyo alikuwa akiongea maneno mengi kwa waandishi hao, alionekana kuwa mtu wa busara kwani kila swali ambalo alikuwa akiulizwa, majibu yake yalikuwa ni ya kujitosheleza sana.

Henry akaonekana kuwa ‘genius’ japokuwa katika historia ya maisha yake hakuwa na akili nyingi darasani. Wanachuo wengi wakatamani kuwa kama yeye, mafanikio yake yakawafanya waandishi wengi kuona kwamba inawezekana endapo tu utaamua kujituma kwa nguvu zote.

Siku hiyo, Henry alionekana kuwa mhamasishaji mkubwa ambaye aliwatia moyo waandishi wale, mpaka anaaga, bado wanachuo walitamani kuendelea kumsikiliza kwani kila neno alilokuwa akiliongea lilionekana kuwa msaada mkubwa kwao.

Henry akaingia ndani ya gari lake la kifahari aina ya V8 na kuondoka mahali hapo kurudi ofisini. Njiani, mawazo yake yalikuwa juu ya maisha yake ya nyuma, alikuwa kwenye maisha ya kimasikini mno kiasi kwamba wakati mwingine hakuwa akiamini kama kweli yeye ndiye aliyekuwa na mafanikio hayo aliyokuwa nayo.

“Nimetoka mbali sana.” alisema Henry huku akionekana kuwa kwenye hali ya mawazo.

Huku akiwa amefika Magomeni Mikumi, kwenye foleni kuelekea nyumbani kwake Mikocheni B, simu yake ikaanza kuita, alipokiangalia kioo, alikuwa msichana Husna, mfanyakazi wake wa ndani ambaye alikuwa akimthamini kama ndugu yake. Akaichukua simu ile na kuipokea.

“Kuna mgeni anakusubiri,” alisikika Husna.

“Ni nani?” aliuliza Henry.

“Maimartha Paul,” alijibu Husna.

“Kwa nini asingenipigia simu?”

“Anasema alikupigia lakini hakukupata.”

“Sawa, mwambie nakuja, nilikuwa naongea na wanachuo, nipo Magomeni,” alisema Henry na kukata simu.

Maimartha Paul alikuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili aliyekuwa akivuma sana kipindi hicho. Kupitia nyimbo zake za Injili, alikuwa amejijengea jina kubwa lililompa heshima kila sehemu aliyokuwa akienda.

Watu walimfahamu kama mwimbaji ambaye kila alipokuwa akiimba uwepo wa Mungu ulikuwa ukionekana mahali hapo. Nyimbo zake zilionekana kuwa na upako kwani kila alipokuwa akiimba, mapepo yalikuwa yakiwatoka watu, wagonjwa walikuwa wakipona magonjwa yao.

Kupitia nyimbo zake, Maimartha alikuwa amejijengea jina kubwa, kila siku aliendelea kujitengenezea fedha kupitia albamu alizokuwa akizitoa ambazo zilinunuliwa kwa kugombaniwa sana.

Japokuwa Maimartha alikuwa akisali katika Kanisa la Praise And Worship lililopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam lakini ulikuwa umepita mwezi wa nne hakuwa amesali katika kanisa hilo, kila Jumapili alikuwa akialikwa katika makanisa mengine kwa ajili ya kumuimbia Mungu tu.

Baada ya kuishi katika maisha ya mafanikio kwa muda mrefu, Maimartha alifuatwa na Henry na kuambiwa kwamba alitakiwa kuyaweka maisha yake wazi, mbele ya watu ili wapate kuyafahamu kwani kuna wengi kupitia maisha hayo wangeweza kubadilika na kufanikiwa.

Kwa mara ya kwanza, Maimartha alikuwa mgumu kukubali lakini kutokana na kusisitiziwa umuhimu wa kuyaweka maisha yake wazi kupitia vitabu, mwisho wa siku akakubaliana na Henry hivyo kupanga siku ya kuonana.

Siku hiyo alikuwa amekwenda nyumbani kwa Henry, alijaribu kumtafuta simuni lakini hakuwa akipatikana. Hakutaka kubaki nyumbani, alitaka kuonana na Henry uso kwa uso ili aweze kumhadithia maisha yake yaliyopita na hatimae ayaweke kwenye kitabu chake na watu waweze kuyasoma.

“Samahani kwa kuchelewa,” alisema Henry mara baada ya kuingia ndani ya nyumba yake, Maimartha alikuwa kochini.

“Usijali. Sikukupa taarifa ndiyo maana imekuwa hivi,” alisema Maimartha.

Baada ya maongezi machache, Henry akaelekea chumbani, akaoga na kisha kurudi sebuleni hapo kwa ajili ya kuongea na msichana huyo, muimbaji wa nyimbo za Injili.

Mara baada ya kufika sebuleni, Henry akatulia kochini na kuanza kumwangalia Maimartha. Alionekana kuwa msichana mrembo mno ambaye kwa kumwangalia tu, lisingekuwa jambo gumu kugundua kwamba msichana huyo alikuwa amepitia mambo mengi maishani mwake.

Mavazi aliyokuwa amevaa, yalikuwa ni ya heshima kubwa, nywele zake hakuwa amezisuka, aliziweka katika mtindo wa ‘afro’ huku uso wake ukiwa umependezeshwa na miwani yenye rangi nyeusi.

Mbali na hayo yote, msichana huyo alikuwa na mvuto mkubwa, kila wakati alionekana kuwa mtu mwenye furaha japokuwa katika maisha yake alipitia shida nyingi zilizomkatisha tamaa hata wakati mwingine kutamani kujiua.

Kila alipokuwa akicheka au kutabasamu, vishimo viwili vilikuwa vikionekana mashavuni mwake huku kidoti cheusi kikiwa karibu kabisa na mdomo wake. Kwa kifupi, Maimartha alivutia kupita kawaida.

“Nahisi umekuja tuzungumze zaidi kuhusu kitabu chako,” alisema Henry.

“Ningependa kiandikwe, ila naona kama kitanichafua,” alisema Maimartha, hata sura yake tu ilionekana kuhofia kile alichokuwa akitaka kukifanya Henry.

“Kitakuchafua vipi sasa?”

“Unajua mimi ni mwanamuziki wa Injili, sasa mtu asome kwamba ulikuwa na mahusiano na fulani kipindi cha nyuma, huoni kama kitanichafua?” alisema Maimartha na kuuliza.

“Hapana, hakuna kitu kama hicho, kupitia maisha yako nadhani kuna wengi watakwenda kujifunza, wengi watafarijika na wengi watapata nguvu ya kusonga mbele, cha msingi, yaweke wazi kwa ajili ya kuwasaidia wengine,” alisema Henry kwa sauti ya upole kama kawaida yake.

Maimartha akashusha pumzi ndefu na nzito, aliyokuwa ameyaongea Henry yalikuwa maneno ya kweli lakini bado moyo wake ulikuwa ukiogopa. Aliyajua maisha yake ya nyuma, yalikuwa maisha mabovu mno ambayo hakupenda mtu yeyote ayafahamu kwani aliamini kwamba yangemchafua sana.

“Ninaogopa,” alisema Maimartha.

“Nchi yetu ina masikini wengi, kuna watu wengi waliokata tamaa na pia kuna watu wengi sana ambao hawajamjua Mungu, je hautaki kuwaona watu masikini wakifarijika kwa kuamini kwamba kuna siku nao watakuja kuwa matajiri?

Je hautaki kuwaona watu waliokata tamaa wakitiwa nguvu na kusonga mbele? Je hautakiwa kuona wale watu ambao maisha yao hayamjui Mungu waje kumjua? Hebu jifikirie ni kwa kiasi gani utakwenda kuwabadilisha wengi,” alisema Henry, katika kuongea, mara nyingi alionekana kuwa mtu mwenye busara kubwa.

“Maneno yako yananipa nguvu ya kukubaliana nawe, ila naomba nijifikirie juu ya hilo,” alisema Maimartha.

“Maimartha, yaani kipindi chote hicho bado tu haukujifikiria? Umetoka nyumbani kwako mpaka hapa kwangu kwa ajili ya kuanza kazi, bado tu unahitaji muda zaidi wa kujifikiria?” aliuliza Henry kwa sauti ya chini.

“Usijali Henry, nitakwambia tu,” alisema Miamatha.

Henry akashusha pumzi ndefu, maneno aliyoyaongea Maimartha yalimkasirisha lakini hakuwa na jinsi, kwa sababu yeye ndiye alikuwa na uhitaji wa kufanya kazi na mwanamuziki huyo, akakubaliana naye.

Kila siku Henry alikuwa akimsumbua mwanamuziki huyo kwamba ilikuwa ni lazima akiandike kitabu hicho kwa ajili ya kuwafundisha Watanzania mambo mengi, bado Maimartha alikuwa akikataa huku akisisitiza kwamba alikuwa akiogopa kuchafuliwa.

Henry hakutaka kukata tamaa, katika kipindi hicho, mtu pekee ambaye alikuwa akihitaji kuandika historia ya maisha yake alikuwa ni mwanamuziki huyo wa Injili ambaye alikuwa akivuma sana, Maimartha Paul.

Mara kwa mara alikuwa akielekea katika kila kanisa ambalo Maimartha alipokuwa akiabudu na kuanza kuongea naye, huko, aliendelea kumsisitizia kwamba alikuwa akitaka kuandika kitabu cha maisha yake lakini bado Maimartha alikuwa akikataa, sababu kubwa ilikuwa ni kuogopa kujichafua.

“Nina uhakika jina lako halitochafuka bali maisha yako yatakwenda kuwafundisha watu mambo mengi mno,” alisema Henry lakini Maimartha hakutaka kukubaliana naye.

Henry hakujua afanye nini, alijitahidi sana kumwambia msichana huyo juu ya kumwandikia kitabu hicho lakini bado aliendelea kukataa. Kila siku akawa mtu wa mawazo tu, kila alipokuwa akimuona Maimartha katika magazeti, televisheni, alikuwa akijisemea kwamba kuna siku angeweza kuandika kitabu cha maisha ya msichana huyo.

Kila siku ilikuwa ni lazima Henry ampigie simu Maimartha na kuendelea kumuomba kumpa nafasi ya kukiandika kitabu hicho ambacho kilionekana kusubiriwa sana na Watanzania.

Maimartha hakuwa mwepesi kukubaliana naye, bado alikuwa akiendelea kusisitiza kwamba hakutaka jina lake lichafuliwe kwani alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakijiheshimu sana.

“Maimartha....” Henry aliita simuni kwa sauti ya kubembeleza.

“Nakusikiliza.”

“Naomba unikubalie niandae kitabu chako, Watanzania wanatamani kusikia mengi kuhusu wewe, mbali na hiyo, utakwenda kuvuna fedha nyingi mno, zaidi ya milioni mia tano, hauoni hiyo kama ni faida kwako?” alisema Henry na kuuliza.

“Milioni mia tano kuingia zinaweza kuingia, ila kuchafuliwa kwa jina ni vibaya zaidi ya kupokea kiasi hicho cha fedha,” alisema Maimartha.

“Hapana. Nakuhakikishia kwamba jina lako halitoweza kuchafuka,” alisema Henry.

“Haiwezekani Henry, siwezi,” alisema Maimartha na kukata simu.

Henry akabaki na mawazo mengi, ni kweli alikuwa ameandika vitabu vya watu wengi katika maisha yake, watu walimheshimu kwa kazi kubwa aliyokuwa ameifanya, kufanya kazi ya kuandika kitabu cha maisha ya Maimartha, ilionekana kuwa nafasi kubwa zaidi ya kujitangaza na kujizolea sifa.

Maisha ya Maimartha yaliendelea kila siku, kitu ambacho kilikuwa kikimuumiza kichwa kila siku kilikuwa ni kuhusu kuandikiwa kitabu cha maisha yake na Henry. Aliyajua maisha yake yaliyopita, hayakuwa na ushuhuda mzuri, alihofia kwamba inawezekana katika kipindi ambacho angeamua kuyaweka wazi maisha yake ya nyuma basi angeweza kuchafuka na hatimae kuonekana kama Shetani.

Bado aliendelea kusisitiza kwamba kuyaweka wazi maisha yake kitabuni lilikuwa suala gumu kufanyika, kitu alichokuwa akikitaka ni kuona maisha yake ya nyuma kuwa katika ulimwengu wa giza tu.

“Nilimkosea sana Mungu, haiwezekani kuyaweka maisha yangu kitabuni,” alijisemea Maimartha.

Siku ziliendelea kukatika, kwa takribani miezi sita, bado Henry alikuwa akiendelea kumsisitizia Maimartha kwamba alitaka kuandika kitabu cha maisha yake lakini msichana huyo alikuwa akikataa. Hilo lilimuumiza sana Henry, hakutegemea kupata ugumu kama aliokuwa akiupata kipindi hicho.

“Sasa nifanye nini? Mungu, zungumza na Maimartha ili akubali niandike kitabu cha maisha yake,” alisema Henry huku akiangalia juu, kwake, kitendo kile kilikuwa kama kumtazama Mungu kule alipokuwa.

Mara baada ya kuona tangazo kwamba kitabu cha Maimartha kingekuwa mitaani mwaka huo, Watanzania wakajiandaa kwa ajili ya kukisoma kitabu hicho. Japokuwa Maimartha hakuwa amekubaliana na Henry kuandika kitabu cha maisha yake lakini Henry aliamua kuliweka tangazo hilo gazetini ili mradi amuoneshea Maimartha ni kwa kiasi gani maisha yake ya nyuma yangeweza kuwabadilisha watu wengi.

Kila siku ilikuwa ni lazima aendelee kumwambia Maimartha kwamba alitaka kuandika kitabu cha maisha yake lakini msichana huyo alikuwa akikataa.

Alichokifanya Henry, akaanza kuwatumia wachungaji mbalimbali waweze kumuombea apate ruhusa ya kuandika kitabu hicho lakini hiyo wala haikusaidia, bado Maimartha alikuwa akikataa tu.

“Amekataa,” alisema mchungaji Michael Kipute.

“Daah! Nina hamu sana ya kuandika kitabu chake, sasa nitafanyaje?” aliuliza Henry.

“Cha msingi mtafute askofu mkuu, Lutengano, anaweza kukusaidia,” alisema mchungaji Kipute.

Henry akapata kazi nyingine tena ya kumtafuta askofu Lutengano. Katika kipindi hicho, askofu huyo hakuwa nchini Tanzania, alikuwa safarini nchini Uholanzi hivyo Henry alitakiwa kusubiri.

Hiyo wala haikuwa tatizo, wakati akiwa anamsubiri Askofu huyo, huku alikuwa akiendelea kumuomba Maimartha kumwandikia kitabu cha maisha yake, bado muimbaji huyo wa Injili alikuwa akikataa.

Henry akaonekana kuchoka kwani alitumia kila njia ili afanikishe lengo lake alilokuwa ameliweka, kitu alichokiona kwamba kingekuwa na busara ni kumsubiria Askofu Lutengano ili aongee na Maimartha na hatimae amruhusu kuandika kitabu kile.

Baada ya wiki mbili, Askofu Lutengano akarudi nchini Tanzania. Henry hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kumfuata ofisini kwake ambapo huko akakaa na kuanza kuzungumza naye.

“Ninatamani niandike kitabu chake, ila anakataa kunipa ushirikiano,” alisema Henry.

“Unataka nikusaidie nini Henry?” aliuliza Askofu Lutengano.

“Naomba uongee naye, nahisi anaweza kukubali,” alisema Henry.

“Hakuna tatizo, nitaongea naye, ila naomba usimchafue,” alisema askofu.

“Hakuna tatizo, sitoongeza kitu, nitaandika kile atakachoniambia tu,” alisema Henry.

“Basi hakuna tatizo.”

Kidogo, Henry akapata ahueni kwa kuona kwamba askofu angefanikisha kile alichokuwa amemwambia, alichotakiwa kukifanya wakati huo ni kusubiria tu. Kila siku alikuwa akimsikilizia askofu Lutengano ili ampa taarifa juu ya kilichokuwa kikiendelea, naye alikuwa kimya.

Wiki ya kwanza ikakatika, wiki ya pili ikaingia na mwisho wa siku mwezi kukatika, hakupokea simu yoyote kutoka kwa askofu kitu kilichomfanya kumpigia simu ili ajue kipi kiliendelea.

“Nilisahau kumwambia,” alisema askofu Lutengano.

“Ulisahau kumwambia?, Daah! Mbona hili suala linakuwa gumu sana?”

“Usijali, nitaongea naye kesho, nimemualika kanisani kwangu,” alisema askofu Lutengano.

Siku iliyofuata ambayo ilikuwa ni Jumapili, Maimartha akaenda kusali katika Kanisa la Praise And Worship la askofu Lutengano lililokuwa Mikocheni A kwa ajili ya kumsifu Mungu kanisa hapo.

Askofu hakutaka kusahau, alipomuona Maimartha tu, akakumbuka kile alichokuwa ameambiwa na Henry, hivyo alitakiwa kuongea na msichana huyo siku hiyo.

“Kiukweli haitowezekana,” alisema Maimartha.

“Kwa nini?”

“Baba askofu, ninaogopa kuchafuliwa, maisha yangu ya nyuma yanatisha sana,” alisema Maimartha.

“Yaliyopita yamepita Maimartha, hata kama uliua, baada ya kumpa Yesu maisha yako, kila kitu kimepita na tazama yamekuwa mapya,” alisema askofu Lutengano.

“Najua baba askofu, ningependa kila kitu katika maisha yangu kiwe kwenye usiku wa giza, huwa sipendi kukumbuka kuhusu maisha yangu yaliyopita,” alisema Maimartha.

“Yesu atakutia nguvu, naomba ufanye kile Watanzania wanachotaka ukifanye, naamini utakwenda kubaddilisha maisha ya watu wengi,” alisema askofu Lutengano.

Maimartha akawa mtu mwenye mawazo, kichwa chake kilikuwa kikifikiria kuhusu kitabu cha historia ya maisha yake ambacho alitakiwa kumuhadithia Henry ili akiandike na kuanza kukiuza nchini Tanzania.

Kwake lilionekana kuwa jambo gumu lakini kwa sababu askofu Lutengano alikuwa ameingiza mkono wake, Maimartha akajikuta akianza kulegeza msimamo wake na hivyo kumpigia simu henry kumwambia kwamba alikuwa amekubali.

“Asante Yesu, hatimae umekubali baada ya mwaka kupita,” alissema Henry huku akionekana kuwa mwenye furaha tele.

“Kwa hiyo unataka nije kwako lini?”

“Hata sasa hivi.”

“Una muda?”

“Wa kumwaga tu,” alisema Henry.

“Ndani ya nusu saa nitakuwa hapo,” alisema Maimartha na kukata simu.

Henry akaruka juu kwa furaha, hakuamini kile alichokuwa amekisikia, alisota kwa takribani mwaka mmoja akimtaka Maimartha akubali kumwandikia kitabu cha maisha yake, alikuwa amekataa kwa kipindi kirefu lakini mwisho wa siku, alikuwa amekubali.

Shukrani zake zote zikaenda kwa askofu Lutengano kwani aliamini kwamba huyo ndiye alikuwa mtu pekee aliyekuwa amefanikisha jambo hilo, alichokifanya ni kumpigia simu na kuanza kumshukuru.

“Nashukuru sana baba askofu, Mungu akubariki,” alisema Henry.

“Usijali, amani ya Bwana ikutawale.”

“Amen,” alisema Henry na kukata simu.

Muda mwingi macho yake yalikuwa kwenye simu yake ya mkononi, mtu ambaye alikuwa akimsubiria kwa wakati huo alikuwa Maimartha tu. Muda wote moyo wake ulikuwa na kimuemue cha kuwapigia simu waandishi wenzake na kuwapa taarifa kwamba hatimae Maimartha alikuwa amekubali kuandikiwa kitabu cha maisha yake.

Alipotaka kufanya hivyo, akasita, akataka mpaka kuona kipindi atakapoanza kuandika kitabu cha maisha ya msichana huyo ndipo hapo ambapo angewapigia simu waandishi wenzake na kuwaambia.

Simu ilikatwa saa 10:36 jioni, mpaka inafika saa 12:23 jioni, Maimartha hakuwa amefika mahali hapo.

“Mmh!” mbona kachelewa hivyo?” alijiuliza Henry lakini hakupata jibu. Bado alikuwa na presha kubwa ya kumuhoji mwanamuziki huyo wa Injili.

Maimartha alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida, kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi kuhusiana na kitabu cha maisha yake alichokuwa akitaka kukiandika Henry. Moyo wake ulikuwa umegawanyika mara mbili, upande mmoja ulimwambia kwamba alikuwa akienda kujichafua lakini upande mwingine ulimwambia kwamba alikuwa akienda kuwasaidia watu wengine.

Kitu alichokuwa amekiamua ni kuyaweka maisha yake hadharani tu. Ushawishi mkubwa alioupata kutoka kwa askofu Lutengano ulimfanya kuamini kwamba asingeweza kujichafua zaidi ya kuwasaidia wengine.

Hakufikiria fedha, alijua kwamba endapo angeuza kitabu hicho angepata sana fedha nyingi lakini suala hilo hakutaka kulifikiria kichwani mwake, Kile alichokuwa akikifikiria ni maisha yake na maisha ya Watanzania ambao wengi wanaishi katika maisha ya kimasikini.

Barabarani hakukuwa na foleni hivyo ilimuwia urahisi kutoka Tabata kwenda Mikocheni B ila alipofika Ubungo, foleni kubwa ilikuwa mahali hapo.

Hapo ndipo alipopatumia kuendelea kufikiria zaidi. Kichwa chake kilifikiria kila kitu alichokuwa akitakiwa kukifanya. Alipitia katika maisha ya tabu, yaliyojaa msisimko ambayo hakuamini kama yangekwenda kuwafundisha watu zaidi ya kujichafua yeye mwenyewe.

Moyo wake ulikuwa mgumu kukubaliana na suala hilo lakini mwisho wa siku alijikuta akikubaliana na Henry. Alimfahamu kama mwandishi bora ambaye kila siku kazi zake zilikuwa zikisifiwa kila kona. Vitabu vyote ambavyo alikuwa ameviandika mwandishi huyo, vilikuwa katika kabati lake la vitabu, alipenda kila kitu, uandishi wa Henry ulimfurahisha mno.

Leo hii ilikuwa zamu yake, ukiachana na wale wasanii na wanasiasa, zamu yake ilikuwa imefika. Alichokifanya, hata kabla magari hayajaruhusiwa, akachukua simu yake na kumtumia meseji Henry.

“Unajua kwamba sina mtoto?” aliuliza Maimartha katika meseji hiyo, wala hazikupita sekunde nyingi, ikajibiwa.

“Ninajua, kuna nini?” meseji ya Henry ilisomeka.

“Nitakuhadithia mengi tu, nipo hapa Ubungo, foleni kubwa ila baada ya dakika kadhaa nitafika hapo,” aliandika Maimartha.

Wala hazikupita dakika nyingi, magari yakaruhusiwa na foleni ile kuanza kusogea tena. Gari lake ndilo lilikuwa ka mwisha kabisa katika msururu wa foleni ile.

Huku akiwa na mawazo mengi, ghafla kwa mbali akaanza kusikia honi nyuma yake, wala hakutaka kujali sana kwani ni mara nyingi magari hasa ya madereva waliokuwa na haraka walikuwa wakipiga sana honi hata kama kulikuwa na foleni.

Maimartha akapuuzia, alipoona honi zikizidi kusikika tena kadri muda ulivyokwenda zikiwa kwa ukaribu zaidi, akageuka nyuma kuangalia kuna nini, macho yake yakatua katika gari kubwa, gari la mafuta kutoka Ecom ambalo lilikuwa likija kwa kasi hali iliyoonesha kwamba lilikuwa limekatika breki.

Hata kabla hajajua afanye nini, gari lile likalifikia gari lake, likaligonga kwa nyuma, kwa sababu hakuwa amefunga mkanda, akajikuta akikipigiza kichwa chake katika kioo cha mbele cha gari lile, kioo kikapasuka, mwili wake, kuanzia miguuni hadi kiunoni ulikuwa ndani ya gari na kuanzia kiunoni kwenda juu ulikuwa nje, juu ya boneti la mbele la gari yake.

Ilikuwa ni ajali mbaya mno, watu waliokuwa pembeni wakashika vichwa vya, damu zilikuwa zimetapakaa kila sehemu hasa juu ya gari lile. Kichwa cha Maimartha kilikuwa kimepasuka na kufanya damu kutoka kwa kiasi kikubwa.

Watu waliokuwa pembeni mwa barabara ile, kwa haraka wakasogea na kuanza kumtoa pale kwenye boneti, wakamuingiza ndani ya gari la msamaria mwema, canter na kuanza kuondoka ahali hapo.

Mwili wake ulitisha, japokuwa alikuwa supastaa, lakini kwa jinsi alivyokuwa hakukuwa na mtu yeyote yule aliyeweza kumtambua kwani kichwa chake kilijaa damu zilizotapakaa mpaka usoni mwake.

Maimartha alikuwa akitetemeka tu mule garini kama mtu ambaye angekata roho muda wowote ule. Ukiachana na damu zilizokuwa zikitoka kichwani mwake kutokana na kupasuka kwa kiasi kikubwa, mdomoni mwake alikuwa akitokwa na machozi.

Garini, damu zilikuwa zimetapakaa kila sehemu huku nyingine zikiendelea kutoka. Kutetemeka mwili hakukuacha, bado aliendelea kuwa kwenye hali ileile, alionekana kubakiwa na sekunde chache za kuvuta pumzi ya dunia hii.

“Mmmh! Hii noma,” alisema jamaa mmoja aliyekuwa ndani ya hiyo gari hilo lililoanza kuendeshwa kwa mwendo wa kasi kama ambulance kuwahi hospitali.

“Kama atapona, yampasa kumshukuru Mungu maisha yake yote,” alisema jamaa mwingine huku akiuweka mwili wa Maimartha vizuri garini mule. Hakukuwa na mtu aliyejua kwamba msichana yule aliyekuwa amepata ajali alikuwa Maimartha, muimba nyimbo za Injili ambaye alikuwa akitamba na albamu yake iitwayo Hapana Rafiki Kama Yesu.
***
Henry bado alikuwa akiisubiria simu kutoka kwa Maimartha, moyoni alikuwa na presha kubwa ya kutaka kufanya kazi na muimbaji huyo wa Injili kwa kuamini kwamba angelifanya jina lake kuwa kubwa zaidi.

Kila wakati alikuwa akiiangalia simu yake, alikuwa akitaka kuona Maimartha akipiga simu na kumwambia kwamba amekaribia kufika hivyo aache geti wazi. Sekunde zikasogea, dakika zikasonga lakini hakukuwa na simu yoyote ile iliyoingia kutoka kwa Maimartha.

Haikuwa kawaida, alimfahamu vizuri msichana huyo, kila alipokuwa na miadi ya kuonana naye, alikuwa akimuahidi huku kila wakati akimtumia meseji kumpa taarifa kwamba alikuwa amefikia wapi, siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti.

“Amepatwa na nini? Hii si kawaida yake,” alisema Henry.

Hakutaka kuvumilia zaidi, alichokifanya ni kuanza kumpigia simu msichana huyo. Simu ikaanza kuita, kadiri ilivyokuwa ikiita ndivyo alivyokuwa akijipa uhakika kwamba ingepokelewa, iliita zaidi na zaidi, haikupokelewa mpaka ikakatika.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza, akajaribu kupiga tena mara ya pili, kama ilivyokuwa mwanzo ndivyo ilivyokuwa tena, simu ilianza kuita, iliita zaidi na zaidi lakini matokeo yalikuwa ni yaleyale, simu haikupokelewa.

Masaa yalizidi kwenda mbele, mpaka inaingia saa mbili usiku, simu haikuwa ikipokelewa, mwisho wa siku, haikupatikana kabisa. Henry akachukia, kwake ulionekana kama usumbufu, mtu kumwambia kwamba aje, akubaliane naye na mwisho wa siku kutokupatikana simuni, kumlimkasirisha.

“Hawa watu wengine mpaka wanakera, yaani tumekubaliana aje, akasema anakuja, amechelewa, nampigia simu, hapokei, mwisho wa siku kaizima kabisa hiyo simu, huu ni ujinga, kuanzia leo, simtafuti tena, asijifanye yeye ni supastaa zaidi ya raisi,” alisema Henry kwa hasira.

Mpaka usiku mwingi unaingia, bado Henry aliendelea kuwa na hasira, akajikuta akianza kumchukia Maimartha kwa kile alichomfanyia, hakutaka tena kusikia kitu chochote kutoka kwa msichana yule, kitendo kile alichokifanya siku ile kilimkera kupita kawaida.

Kutokupokea simu kwa msichana huyo kulimuoneshea kwamba alikuwa na maringo mengi, akaachana naye, akajilaza kitandani, moyo wake bado ulikuwa na hasira mno, kila wakati alikuwa akiyauma meno yake, hakuamini kama Maimartha alikuwa amemfanyia kile alichomfanyia.

“Yaani ananichomesha mahindi, huu ni ujinga, ngoja kesho akinipigia simu, atajuta kuzaliwa, nitampa makavu live,” alisema Henry kwa hasira na kulala huku bado moyo wake ukiendelea kuwa na hasira tele.

Habari za mitandaoni ndizo zilizomshtua, hakuamini kile alichokuwa akikisoma kwamba muimbaji wa Injili, Maimartha Paul alikuwa amepata ajali mbaya alipokuwa Ubungo. Kwanza akashtuka, usingizi na uchovu wote aliokuwa nao ukapaa, hakuamini kile alichokuwa amekisoma.

Picha ambazo zilionekana katika mtandao ule zilimsikitisha, ghafla, hasira zote alizokuwa nazo juu ya Maimartha zikapotea na huruma kuanza kumuingia.

Alichokifanya ni kuinuka kutoka kitandani, akaelekea bafuni kuoga na kwa harakaharaka akaanza kuvaa nguo zake, kitu alichokitaka kwa wakati huo ni kuelekea katika Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kumuona Maimartha tu.

“Mimi ndiye nimeyataka,” alisema Henry, aliona kwamba yeye ndiye aliyesababisha hayo yote, pasipo kumuita nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya naye mahojiano kuhusu kitabu chake basi asingepata ajali aliyokuwa ameipata.

Mara baada ya kumaliza kujiandaa, Henry akatoka nje ambako akachukua gari lake na kuanza safari ya kuelekea hospitali. Njiani, Henry alikuwa na mawazo mengi, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Maimartha tu, alijiona kuwa yeye ndiye chanzo cha ajali hiyo kitu ambacho kilimuumiza mno.

Kwa sababu hakukuwa na foleni kubwa, wala kufika hospitalini hapo hakuchukua muda mrefu. Kwa sababu haukuwa muda wa kuona wagonjwa, Henry akaonesha kitambulisho chake cha kazi, akaruhusiwa kuingia.

Akaelekea sehemu ya maegesho na kuliegesha gari lake. Kwa sababu hakuwa akifahamu ni sehemu gani alipokuwa amelazwa Maimartha, akamfuata nesi mmoja aliyekuwa akipita karibu yake na kuanza kumuuliza.

“Samahani dada yangu, jana usiku kulitokea ajali maeneo ya Ubungo, msanii wa Injili aligongwa na gari na kuletwa hapa, yupo wodi gani?” aliuliza Henry huku machozi yakianza kumlenga.

“Sina uhakika, ila nenda kule katika Wodi ya Mwaisela,” alisema nesi yule.

“Nashukuru.”

Henry akaondoka mahali hapo na kuanza kuelekea katika Wodi ya Mwaisela. Mwendo wake ulikuwa ni wa harakaharaka, bado kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Maimartha, kwake, kila hatua aliyokuwa akipiga alijiona kwamba yeye ndiye aliyesababisha Maimartha kupata ajali ile mbaya.

“Dada samahani,” alisema Henry, alikuwa amemsimamisha nesi.

“Bila samahani.”

“Ninamuulizia Maimartha, alipata ajali jana.”

“Umeambiwa uje huku Mwaisela?”

“Ndiyo.”

“Hapana, hayupo huku, nenda kitengo cha mifupa, MOI,” alisema nesi huyo.

“Nashukuru.

Henry hakutaka kubaki mahali hapo, akaanza kutembea kwa mwendo uleule wa harakaharaka, kitu pekee alichokuwa akikitaka kwa wakati huo ni kumuona Maimartha tu.

Alipofika huko, waandishi wa habari wengine zaidi ya kumi walikuwa wamekusanyika katika mlango wa kuingilia katika jengo la kitengo cha mifupa, MOI. Kila mmoja alikuwa na kamera mkononi tayari kwa kumpiga picha Maimartha endapo tu angepitishwa nje kuelekea Mwaisela.

“Vipi?” aliuliza Henry.

“Bado anaendelea na matibabu, hali yake mbaya sana,” alisema mwandishi wa Gazeti la Uwazi, Haroun Sanchawa.

“Kwani ilikuwaje?” aliuliza Henry.

“Sijui chochote kile, chanzo kilinipigia simu na kuniambia kwamba Maimartha kaletwa mahali hapa baada ya kupata ajali, zaidi ya hapo, sijui chochote kile,” alisema Sanchawa.

Hakuwa na jinsi, kwa sababu alifika mahali hapo kwa ajili ya kumuona Maimartha na waandishi wengine walikuwa nje, naye ilimpasa kusubiria kama wengine. Muda wote Henry alikuwa akimuomba Mungu kwamba amponye Maimartha lakini zaidi ya hilo, alikuwa akiomba msamaha kwa kuongea maneno mabaya dhidi ya Maimartha katika kipindi ambacho hakutokea nyumbani na alipokuwa akimpigia simu bila kupokelewa.

Muda wote Henry alikuwa akijihukumu, bado alijiona kuwa chanzo cha mambo hayo yote kwani endapo asingempigia simu Maimartha ilimaanisha kwamba asingepata ajali ile aliyokuwa ameipata.

“Nisamehe Mungu,” alisema Henry huku machozi yaliyokuwa yakimlenga yakianza kububujika mashavuni mwake.

Hakufikiria tena kuandika kitabu cha maisha ya Maimartha, kitu alichokuwa akikifikiria mahali hapo kilikuwa ni kumuombea uzima msichana huyo ambaye bado alionekana kuwa na muda mwingi wa kumsifu Mungu.
****
Watanzania hasa wakristo walionekana kama kuchanganyikiwa, taarifa za kupata ajali kwa Maimartha kuliwashtua. Wengi hawakuziamini taarifa hizo kitu kilichowafanya kuelekea hospitalini ili kupata uhakika juu ya kile kilichokuwa kimetokea.

Huko, wakapata uhakika kwamba taarifa ambazo zilikuwa zikiendelea kuvuma hazikuwa tetesi bali zilikuwa taarifa kamili. Hilo likaonekana kuwa kama pigo kwa waimbaji wa nyimbo za Injili na makanisa mengi ya kilokole Tanzania.

Maombezi yakaanza rasmi, katika kila ibada ya Jumapili, washirika wa makanisa mbalimbali wa

likuwa wakikusanyana katika Kanisa la Kilokole la Praise And Worship lililokuwa Kinondoni na kuanza kumuombea Maimartha.

Huyo ndiye alikuwa muimbaji mkubwa na maarufu aliyekuwa amebaki, nyimbo zake zilizojaa uwepo wa Mungu ndizo zilizokuwa zikisikika kila sehemu. Kitu cha ajabu, mara baada ya kupata ajali hiyo, albamu zake zilizokuwa sokoni zikanunuliwa zote.

“Mungu, tunakuomba umponye Maimartha, tunampenda sana,” alisema msichana mmoja huku mkononi mwake akiwa ameshika Biblia.

Kila siku wachungaji walikuwa wakielekea hospitalini hapo kwa ajili ya kumuona muimbaji huyo. Hawakuwa wakiruhusiwa kwani mgonjwa alikuwa akihitajika kupata muda mwingi wa kuwa peke yake kitandani.

Hakuwa amepata fahamu, kwa muda wa wiki nzima, alikuwa kimya kitandani hali ambayo iliwapa wasiwasi mkubwa washirika wa makanisa kwa kudhani kwamba Maimartha alikuwa amefariki japokuwa madaktari hawakutaka kuzungumza ukweli.

Baadhi ya ndugu zake waliokuwa Iringa wakiwepo wazazi wake wakaingia jijini Dar es Salaam, taarifa walizokuwa wamezipata ziliwashtua. Maimartha alikuwa miongoni mwa watoto wao saba, kutokana na kuingiza kiasi kikubwa cha fedha, wao wenyewe walikuwa wamebadilika kwa kujengewa nyumba ya kifahari na shamba kubwa ambalo liliwaingizia fedha kila walipokuwa wakilima na kuvuna.

Mama yake, bi Estelina alikuwa akilia tu, muda wote alionekana kuwa mwenye majonzi. Alimpenda sana Maimartha, kwake alionekana kuwa mtoto wa tofauti aliyekuwa na kiu ya kubadilisha maisha ya watu wengi, wale wasiokuwa wakimjua Mungu, kupitia nyimbo zake wamjue.

Ndoto zake zote alizokuwa nazo zilionekana kufikia tamati, ajali ile aliyokuwa ameipata ilionekana kuwa mwisho wa kila kitu. Hakukuwa na matumaini ya kupona, kitu walichotakiwa ni kumuomba Mungu kwani japokuwa madaktari walikuwa wataalamu wa kuujua mwili wa binadamu, Mungu alikuwa zaidi kwani Yeye ndiye aliyeuumba mwili huo.

Jopo la madaktari kumi walikuwa wamekutana ndani ya chumba cha mkutano kwa ajili ya kuzungumzia hali aliyokuwa nayo Maimartha. Wiki ya kwanza ilikuwa imekwishakatika na hali ya Maimartha ilikuwa vilevile, hakuwa amerudiwa na fahamu zake.

Kila mmoja alikuwa na karatasi juu ya majibu ya vipimo ambavyo vilichukuliwa toka siku ya kwanza msichana huyo alipoletwa hospitalini hapo.

Katika karatasi hizo, pia kulikuwa na majibu ya vipimo vya CT (Computed Tomography) ambacho hutumika kupiga picha kwa watu waliopata mivunjiko kadhaa miilini mwao, hasa uti wa mgongo.

Mbali na hayo, kulikuwa na karatasi nyingine ambayo ilikuwa na majibu ya mwili wa Maimartha. Katika vipimo vyote ambavyo vilifanyika kama x-ray, CT, kipimo cha mwisho kabisa ambacho kilifanyika kilikuwa ni Magnetic Resonance Imaging (MRI).

Hiki kilikuwa kipimo kikubwa na cha mwisho kabisa kufanyika ambacho kilikuwa na uwezo wa kuchunguza kila kitu kuhusiana na mvunjiko kisha kutoa majibu kwa ufasaha zaidi.

Vipimo vyote hivyo, vilitumika katika kipindi ambacho Maimartha alikuwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi. Hakuwa akijitambua, alikuwa kimya kitandani huku akionekana kama mtu ambaye tayari alikwishakufa.

Madaktari hao waliokuwa ndani ya chumba hicho walikuwa kimya, vichwa vyao vilikuwa vikiuma sana kwani mgonjwa aliyekuwa ameletwa alionekana kuwa tofauti kabisa na wagonjwa wengine, huyu alionekana kuwa kwenye hali ya hatari zaidi.

Kila mtu hakuwa akiamini kile alichokuwa akikiona katika karatasi zile za majibu. Hawakuamini kama kungekuwa na mtu ambaye angepatwa na tatizo kubwa kama alilokuwa nalo Maimartha. Kila mmoja alijua kwamba huo ungekuwa mwisho wake.

“Hali imekuwa ni ngumu mno, mpaka sasa hivi sidhani kama huyu mgonjwa tutamuweza,” alisema Dk. Mshana, huyu alikuwa mtaalamu wa mifupa hospitalini hapo.

“Vipimo vinaonesha nini?” aliuliza Dk. Kimosa.

“Uti wake wa mgongo umevunjika, sidhani kama tutaweza, cha msingi, ni bora asafirishwe tu,” alisema Dk. Mshana.

Uti wa mgongo wa Maimartha ulikuwa umevunjika. Hali ilionekana kuwa mbaya kwake kwani watu wote waliokuwa wakivunjika uti wa mgongo ilikuwa ni lazima wapooze huku watu hao wakihitajika kufanyiwa oparesheni ndani ya miezi sita tu, kama ikipita miezi hiyo na bado hali inaendelea basi kupooza huko kutakuwa kwa maisha yake yote.

“Ni lazima tutafute msaada,” alisema Dk. Mshana huku akishusha pumzi ndefu.

“Msaada gani?”

“Asafirishwe kuelekea India kwa matibabu zaidi, vinginevyo, anaweza kufariki dunia,” alisema Dk. Mshana.

Kikao hicho cha kuijadili hali ya Maimartha kilichukuwa masaa matatu, makubaliano ambayo waliafikiana yalikuwa ni Maimartha kusafirishwa na kupelekwa nchini India. Walichokifanya madaktari hao ni kuwasiliana na uongozi wa Hospitali ya Ganga kwa ajili ya kumpeleka Maimartha huko ili aweze kupata matibabu mahali hapo.

“Anatakiwa kusafirishwa na kupelekwa nchini India,” alisema Dk. Kipwate, alikuwa akiwaambia wazazi wake.

“Hilo si tatizo, tunachokitaka ni kuona akipona tena,” alisema mzee Paul.

“Na mimi nataka kwenda huko, nitajigharamia kila kitu,” alisema Henry, mzee Paul na bi Estelina wakapigwa na mshangao kwani hawakuwa wakimfahamu kijana huyo.

“Utaongea na wazazi wake, hilo ni nje ya uwezo wetu,” alisema Dk. Kipwate na kuondoka mahali hapo.

Hapo ndipo Henry alipoanza kuwaambia wazazi hao juu ya mchakato ambao alikuwa nao kwa Maimartha. Hakutaka kuficha kitu chochote kile, aliendelea kuwaambia kwamba hata ajali ile aliyokuwa ameipata, yeye ndiye aliyesababisha hilo kwani Maimartha alikuwa njiani akielekea nyumbani kwake.

Bi Estelina alijikuta akianza kulia tena, maneno aliyokuwa ameyaongea Henry yalimuumiza kupita kawaida. Alimkumbuka mtoto wake, katika kipindi alichokuwa mzima, moyo wake ulikuwa na furaha tele, kila wakati alikuwa mtu wa kufurahi tu lakini ghafla, maisha yake hayo yakawa yamebadilika, furaha aliyokuwa nayo ikapotea maishani mwake.

Maneno ya faraja na pole walizokuwa wakipewa na washirika wa makanisa mbalimbali waliofika hospitalini hapo ziliwaumiza mno, washirika hao walionekana kama watu waliowakumbusha maisha ya furaha ya nyuma waliyokuwa wakiishi na mtoto wao.

“Mungu ni mponyaji, atamponya tu,” alisema kijana mmoja, naye alikuwa muimbaji wa nyimbo za Injili kama alivyokuwa Maimartha.

“Tunaamini hilo, cha msingi ni kuendelea kumuomba Mungu,” alisema mzee Paul.

“Kwani anasumbuliwa na nini?” aliuliza mwandishi wa habari wa Gazeti la Uwazi, Sanchawa.

“Uti wa mgongo wake umevunjika, madaktari wanasema kwamba ataweza kupooza,” alimjibu mzee Paul.

“Poleni sana. Kwa hiyo ndiyo anataka kusafirishwa kuelekea India?” aliendelea kuuliza mwandishi huyo.

“Ndiyo.”

“Mtasafiri lini?”

“Tutasafiri siku ya Jumatano, tuna siku tatu za kujiandaa,” alijibu mzee Paul.

Henry alitakiwa kujiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini India. Kwa sababu alikuwa na vibali vyote, akahangaikia viza, alipopata, kitu alichokuwa akikisubiria kilikuwa ni safari tu.

Kila siku alionekana kuwa mtu wa mawazo, bado kichwa chake kilikuwa kikimuuma kwani kila alipokuwa akiliona jina la Maimartha na picha yake katika vyombo mbalimbali vya habari, moyo wake ulikuwa ukimuuma sana.

Japokuwa hakuwa amesababisha ajali ile barabarani lakini Henry alijiona kwamba yeye ndiye mtu pekee ambaye alitakiwa kubebeshwa mzigo wa lawama kwa kila kitu kilichokuwa kimetokea.

“Mungu, naomba umponye, mzigo huu wa lawama ni mzito mno kuubeba,” alisema Henry huku machozi yakimbubujika mashavuni mwake.

Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilimuumiza zaidi. Hakuacha kwenda hospitalini, kila siku ilikuwa ni lazima kuelekea huko, mpaka kipindi hicho, bado hakukuwa na mtu aliyeruhusiwa kuingia ndani.

“Lakini tunataka japo kumuona,” alisema Henry, alikuwa akimwambia Dk. Mshana.

“Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia humo.”

“Dokta, hawa ni wazazi wake, mimi ni mwandishi ninataka kumwandikia historia ya maisha yake, kweli hatuwezi kuingia na kumuona? Mimi ni Henry, mwandishi wa habari, nadhani unanifahamu, tafadhali dokta, tunaomba kumuona,” alisema Henry huku akijitahidi kumbembeleza Dk. Mshana.

“Mtamuona tu, si kesho ndiyo mnaelekea India, hakuna tatizo, mtamuona tu,” alisema Dk. Mshana.

Siku iliyofuata baada ya kila kuandaliwa, safari ya kuelekea nchini India ikaanza. Wote walikuwa ndani ya ndege ya Shirika la Indians Airlines huku kukiwa na kitanda maalumu ambacho Maimartha alikuwa amelala kimya. Hawakuwa peke yao ndani ya safari hiyo bali Dk. Mshana alikuwa pamoja nao.

Japokuwa alikuwa na kiti chake, muda mwingi Henry alikuwa akielekea karibu na kitanda hicho na kukaa karibu na Maimartha. Kila alipokuwa akimwangalia, uso wake ulitawaliwa na majonzi, hakuamini kama msichana huyo aliyekuwa kitandani alikuwa Maimartha, muimbaji wa nyimbo za Injili ambaye alikuwa akitaka kuandika kitabu cha historia ya maisha yake.

“Mungu, naomba usimchukue Maimartha, mpe nafasi nyingine ya kuishi, japo nafasi moja tu, nadhani ataitumia awezavyo ili kukiandika kitabu cha maisha yake,” alisema Henry.

Machozi hayakukoma kumbubujika mashavuni mwake, kila alipokuwa akimwangalia Maimartha kitandani pale, aliumia kila alipokumbuka kwamba pamoja na uzima tuliokuwa nayo, pia Mungu aliumba kifo, kitu ambacho Maimartha alikuwa akielekea kukutana nacho.

“Usiniache Maimartha,” alisema Henry, shati alilokuwa amevaa lililoanishwa na machozi yake kifuani mwake.

Baada ya masaa kumi, ndege ya Shirika la Indians Airlines ilikuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi uliokuwa New Delhi, hali ya hewa haikuwa tofauti na jiji la Dar es Salaam, joto lilikuwa imetawala jijini hapo.

Gari la Hospitali ya Ganga lilikuwa mahali hapo kwa ajili ya kumchukua Maimartha ambaye mpaka katika kipindi hicho hakuwa amepata fahamu. Abiria wakaanza kuteremka kutoka ndani ya ndege na kuelekea katika sehemu iliyokuwa na mlango wa kuingilia ndani ya jengo la uwanja huo.

Baada ya abiria wote kumalizika, kitanda alichokuwa amelalia Maimartha kikaanza kuteremshwa huku wazazi wake, Henry wakifuata.

Japo kuwa hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika nchini India lakini Henry hakuonekana kuwa na furaha kabisa, muda wote uso wake ulionekana kuwa na mawazo mengi, hakuamini kama siku yake ya kwanza kufika nchini humo ilikuwa ni kumleta msichana Maimartha ambaye alikuwa hoi kitandani.

Baada ya Maimartha kupandishwa ndani ya gari hilo, nao wakatakiwa kupitia katika mlango maalumu ambapo baada ya dakika chache, wakaungana na gari hilo na safari ya kuelekea katika hospitali hiyo kuanza.

Mwili wa Maimartha haukuwa na majeraha makubwa, vidonda kadhaa alivyokuwa navyo vilikuwa vimekwishafishwa, kitu kilichokuwa kimebakia kilikuwa ni kurudiwa na fahamu tu.

Dripu za maji yaliyochanganywa na dawa ziitwazo alendronate (fosamax), ibandronate (bonviva), risedronate (actonel) ziliendelea kupitisha maji katika mwili wake, kwa kumtazama kitandani pale ungeweza kusema kwamba Maimartha alikuwa amelala na angeamka muda wowote ule.

“I want to see her back” (Ninataka nimuone tena)” alisema Henry akimaanishak wamba alitaka kumuona Maimartha akirudiwa na fahamu. “She will come back, let them do their work” (Atarudi tu, waachie wafanye kazi yao)” alisema mmoja wa manesi waliokuwa ndani ya gari hilo.

“We trust them with their treatment, this is not the first time (Tunawaamini na matibabu yao, hii si mara ya kwanza)” alisema Dk. Mshana ambaye aliongozana nao.

Kutokana na idadi kubwa ya watu, foleni za magari ambazo hazikuangalia kama hili lilikuwa gari la wagonjwa au la, walichukua dakika ishirini mpaka kufika katika hospitali hiyo.

Lilikuwa jengo kubwa la ghorofa sita ambalo kwa juu kabisa liliandikwa Ganga Medical Center. Gari likaingizwa ndani ya eneo la hospitali hiyo, manesi wawili wakaanza kulisogelea, machela ikashushwa na machela kushushwa.

Katika kila hatua iliyokuwa ikiendelea mahali hapo, Henry alikuwa akihuzunika tu, hakuamini kama msichana aliyekuwa akipenda sana kusikiliza nyimbo zake leo hii alikuwa kitandani huku akionekana kama mfu anayepumulia mashine ya oksijeni.

Kwa sababu walikuwa wamekwishafanikisha kumfikisha Maimartha hospitalini hapo, kilichofuatia ni kwenda mitaani ambapo huko wakachukua vyumba katika Hoteli ya Banjubanju ambayo haikuwa na gharama sana.

“Mungu, bado nina kazi na Maimartha, kama inawezekana, naomba hata umpe nguvu kwa wiki moja tu, naomba uisikie sala yangu,” alisema Henry.
***
Matibabu yakaanza rasmi hospitalini hapo. Kuumia kwa Maimartha kulionekana tofauti na wagonjwa ambao waliwahi kuletwa hospitalini hapo, yeye alionekana kuumia zaidi.

Uti wa mgongo wake ulikuwa umefunjika mara mbili, mpaka hapo, hali ilionesha
kwamba ajali aliyokuwa ameipata haikuwa ya kawaida, ilikuwa ni ajali mbaya ambayo ingeweza hata kukatisha maisha yake.

Dokta Bingwa wa Upasuaji, Sunil Kushey akachaguliwa kumtibia Maimartha ili
apone haraka hata kabla miezi sita haijakatika kwani kama angechelewa mpaka miezi hiyo kukatika, inamaanisha kwamba angekuwa katika hali ya kupooza maisha yake yote.

Kazi hakuwa ndogo, kila siku Dk. Sunil alikuwa akifika hospitalini hapo, hatua ya kwanza ilikuwa ni kuingia katika chumba cha upasuaji ambapo huko akakutana na wenzake na kuanza kuifanya kazi hiyo.

Japokuwa nchini Tanzania vipimo vilikuwa vimetolewa na majibu kuwekwa wazi lakini hawakutaka kukubali, ilitakiwa vipimo zaidi vifanyike ili kuchunguza kwa undani juu ya uti huo, jinsi ulivyovunjka na chembechembe ambazo zilitoka katika uti wa mgongo.

“Upasuaji huu utachukua miezi mitano mpaka kukamilika,” alisema Dr. Sunil.

“Baada ya hapo, atakuwa kwenye hali yake nzuri? Namaanisha hatokuwa
amepooza?” aliuliza Dk. Malish.

“Bado sijajua, huyu mgonjwa amekuwa ni wa tofauti sana, cha msingi, nitajitahidi kadri niwezavyo,” alisema Dk. Sunil.

Mipira kadhaa ilipitishwa katika mwili wake kwa ajili ya chakula na kujisaidia haja zote. Hakuwa akiongea, bado ukimya wake uliendelea kitandani pale huku akiwa kimya kabisa.

Kila kitu alikuwa akifanyiwa, manesi walikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kila wiki mipira ya chakula na haja inabadilishwa na kuwekwa mingine. Henry, wazazi wa Maimartha na Dk. Mshana waliendelea kufika hospitalini hapo kuangalia hali ya mgonjwa. Huko, hawakuzuiliwa, kila walipokuwa wakienda, waliruhusiwa kuingia ndani ya chumba hicho na kumwangalia mgonjwa wao kitandani pale alipokuwa amelala.

“Naomba unisamehe Maimartha,” alisema Henry huku akiwa akiwa pembeni mwa kitanda alichokuwa Maimartha, alikuwa amemshika mkono.

“Najua bila mimi usingekuwa katika hali hii, nisamehe kwa kila kitu, nisamehe kwa kukuhisi vibaya, nisamehe kwa kukulazimisha kukiandika kitabu cha maisha yako, naomba unisamehe kwa kila nilichokifanya kwako, ninatamani uyafumbue macho yako na uniangalie tena, uangalie ni kwa jinsi gani nimeumia moyoni mwangu, Maimartha...Maimartha...Maimartha amka,” alisema henry huku machozi yakimbubujika mashavuni mwake.

Maneno yake hayakubadilisha kitu chochote kile, bado Maimartha aliendelea kubaki kitandani pale. Kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hali yake kitandani pale ilivyozidi kudhoofika, mwili wake ukaanza kupunguaa jambo lililoonekana kuwatisha hata wazazi wake.

“Mume wangu, Maimartha atakufa,” alisema bi Estelina huku akilia.

“Hatoweza kufa, nyamaza mke wangu,” alisema mzee Paul lakini bi Estelina
hakutaka kunyamaza.

Kila alipokuwa akimwangalia mtoto wake kitandani pale alionekana kuwa kwenye mateso makali, hakuonesha dalili zozote za kupona na kurudi katika hali yake kama kawaida.

“Amka Maimartha, Amka unitazame tena, amka uongee na uimbe tena, Tanzania imeikumbuka sauti yako, amka Maimartha, amka uimbe tena,” alisema Henry kwa maumivu makali moyoni mwake huku akiamini kwamba Maimartha angeweza kuisikia sauti ile na kuyafumbua macho yake. Bado alikuwa kimya, kwa jinsi alivyoonekana kitandani pale, alionekana kama mfu.
 
utaimaliza au ndo habari ya itaendelea

Simulizi: Let's Call It A Night

Sehemu Ya Pili (2)

Matibabu bado yalikuwa yakiendelea kila siku, Maimartha alikuwa kimya

kitandani huku akionekana kama mtu ambaye tayari alikuwa amekata roho. Kila

alipokuwa akimwangalia Maimartha kitandani pale, henry alijisikia uchungu
moyoni mwake.

Ni kweli alikuwa akiwaona watu wengi vitandani wakiteseka, alikuwa akiwachukulia kawaida, kuumwa kwa Maimartha lilionekana jambo zito sana moyoni mwake, alilichukulia kwa uzito tofauti na watu wengine walipokuwa wakiumwa wakiwepo ndugu zake.

Kila wakati swali lake kwa madaktari lilikuwa atapona lini na atayafumbua macho yake lini. Hakukuwa na dokta aliyekuwa akilijua hilo, kitu walichokuwa wakikitaka ni kuendelea na tiba hiyo kama kawaida.

Picha za vipimo vya Magnetic Resonance Imaging (MRI) vikasafirishwa na kupelekwa katika Hospitali ya Ahmedabad Civil ambayo ilikuwa ikipatikana Ahmedabad. Ukiachana na India, hiyo ndiyo ilikuwa hospitali kubwa barani Asia.

Wagonjwa wengi waliokuwa wakishindikana katika hospitali nyingine walikuwa wakipelekwa katika hospitali hiyo ambayo ilikuwa na madaktari waliokuwa wazoefu katika kuzifanya kazi zao.

Walipoyapokea majibu ya vipimo vya MRI kutoka katika Hospitali ya Ganga, walichokifanya ni kumtuma daktari wao ambaye alikuwa mzoefu na matatizo ya mifupa, Amir aende huko kwa ajili ya kumuona mgonjwa huyo, Maimartha.

Alipofika, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuangalia taarifa nzima ya mgonjwa huo hata kabla hajaanza kazi yake. Kila kitu alichokisoma katika ripoti hiyo kilionesha kwamba pamoja na kuvunjika kwa uti wa mgongo, Maimartha

angeweza kupooza na kubaki hivyo maisha yake yote.

“Tunatakiwa kufanya haraka hata kabla miezi sita haijatimia, vilevile tunatakiwa

kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha hizo chembechembe zilizotoka

zinatolewa kuepuka matatizo zaidi,” alisema Dk. Amir.

“Hatua ya kwanza ni ipi?” aliuliz Dk. Sunil.

“Kumchukua tena vipimo vya MRI.”

“Mmmh! Hivyo si tumekwishachukua na ripoti kukutumia?”

“Najua, natakiwa kuanza upya, kwa kufanya hivyo, nadhani itaweza kusaidia na

nitajua tatizo kubwa ni lipi,” alisema Dk. Amir.

Kwa sababu yeye ndiye alikuwa mtaalamu zaidi, hakukuwa na mtu aliyelipinga

hilo, walichokifanya ni kufanya kama alivyosema. Vipimo vya MRI vikachuliwa

kwa mara nyingine tena, majibu yalivyokuja, akagundua tatizo jingine kwamba

mbali na kuvunjika kwa uti wa mgongo, pia picha iliyopigwa ilionesha kwamba

ulikuwa umepinda kidogo.

“Hili ni tatizo ambalo sikuwahi kukutana nalo,” alisema Dk. Amir huku

akionekana kushangaa.

“Tatizo gani?”

“Uti wake wa mgongo umepinda, kazi ya kwanza tunayotakiwa kupambana

nayo ni kuurudisha uti huo kwenye hali yake ya kawaida na matibabu yaanze

rasmi,” alisema Dk. Amir.

“Mmmh! Itachukua muda gani mpaka unyooke?”

“Miezi miwili.”

“Sasa baada ya hapo, tutafanikiwa kumtibia kwa miezi sita? Itakuwa imebaki

miezi minne.”

“Tutaweza tu. Kupinda kwa uti wa mgongo ndiyo tatizo lililoleta tatizo lake la

kutokurejewa na fahamu. Kwanza tushughulikie suala hili,” alisema Dk. Amir.

Usiku hakulala, muda wote alikesha na vitabu vyake huku akiangalia ni kwa

namna gani angeweza kumsaidia Maimartha. Mgonjwa huyo alionekana kuwa

kwenye hali mbaya, alijua fika kwamba alikutana na wagonjwa waliokuwa na

matatizo ya uti wa mgongo lakini kwa Maimartha tatizo hilo likaonekana kuwa

kubwa zaidi.

Kichwa chake kilimuuma, kwa kutumia mitandao mbalimbali ya madaktari

wenzake, hakuweza kugundua namna ya kuurudisha uti wa mgongo wa

Maimartha kama ulivyokuwa, kwake, tatizo hilo likaonekana jipya.

Mbele yake alijiona kuwa na mtihani mkubwa, kufanikisha matibabu ya

Maimartha kulimaanisha kwamba uwezo wake ungekuwa juu zaidi kwani tatizo

hilo lilionekana kuwa jipya kabisa.

Alipekua kila kitu alichoona kufaa kupekuliwa usiku huo lakini wala haikusaidia.

Akajaribu kuufungua mtandao wa Google na kuanza kutafuta labda tatizo la

kupinda kwa uti wa mgongo lilikuwa limeelezewa, napo hakukuta kitu hali

iliyomuumiza kichwa zaidi.

“Nifanye nini sasa? Hivi kweli naweza kushindwa namna hii? Hapana, kusoma

kwangu kwa miaka thelathini halafu tatizo hili kweli nisilitatue, basi bora

nirudishe vyeti endapo tu itatokea kushindwa kulitatua tatizo hili,” alijisema Dk. Amir.

Siku iliyofuata, asubuhi na mapema akafika hospitalini hapo, kitu cha kwanza

alichokifanya ni kuonana na ndegu wa Maimartha na kuanza kuongea nao.

Aliwaelezea tatizo lililokuwa likimsibu msichana huyo, kila mmoja alionekana

kusikitishwa.

“Atapona?” aliuliza bi Estelina huku akilia.

“Atapona tu, cha msingi muendelee kumuomba Mungu,” alisema Dk. Amir.

Kuunyoosha uti wa mgongo wake haikuwa kazi nyepesi, ilikuwa ni kazi ngumu

iliyohitaji umakini wa hali ya juu. Kila siku kazi ilikuwa ni hiyohiyo tu. Madaktari

walikuwa wakikusanyika katika chumba hicho kila siku ambazo Dk. Amir

alikuwa akifika mahali hapo.

Mwezi wa kwanza ukakatika, kwa mbali dalili zikaanza kuonekana kwamba uti

wa mgongo ungeweza kunyooka endapo wangeongeza juhudi zaidi.

Hawakukata tamaa, waliendelea mbele na mwezi wa pili ulipoingia, kazi ilikuwa

imefanyika, uti wa mgongo ulikuwa umenyooka, bila kutegemeam, wakajikuta

wakipiga makofi ya shangwe kana kwamba Maimartha alikuwa amepona.

“Asante Mungu kwa msaada wako, hongera sana dokta,” madaktari wengine

wakajikuta wakimpongeza Dk. Amir.

Wazazi wake, Henry na Dk. Mshana walipopewa taarifa kwamba madaktari

walikuwa wamefanikisha kuunyoosha uti wa mgongo wa Maimartha, wakabaki

wakimshukuru Mungu tu kwani waliamini kwamba yeye ndiye alikuwa dokta

mkuu aliyeujua zaidi mwili wa binadamu kuliko madaktari hao.

“Tunamshukuru Mungu, kwa hiyo atapona vizuri lini?” aliuliza bi Estelina.

“Tuna miezi minne, tusipofanikisha ndani ya miezi minne inamaanisha kwamba

mgonjwa wenu atapooza maisha yake yote,” alisema Dk. Amir.

“Kwa hiyo amepooza?”

“Kila mtu anayepata tatizo hilo ni lazima apooze,” alijibu Dk. Amir.

“Na vipi kuhusu kurudiwa na fahamu zake?”

“Alishindwa kurudiwa na fahamu kwa sababu uti wa mgongo wake ulikuwa

umepinda, tatizo limekwisha, tegemeeni kwamba atarudiwa na fahamu na

kuongea muda wowote ule,” alisema Dk. Amir, wote wakajikuta wakibubujikwa

na machozi, kuambiwa kwamba Maimartha alikuwa amepooza, kuliwaumiza

zaidi ila kuhusu kurudiwa na fahamu muda wowote ule, kidogo kuliwafariji.


Siku ziliendelea kukatika kama kawaida, kila siku Dk. Amir alikuwa na jukumu

la kufika hospitalini hapo na kumtibia mgonjwa wake. Moyoni mwake alikuwa

na imani kubwa kwamba Maimartha angekwenda kurudiwa na fahamu na

mwisho wa siku angepona kabisa.

Mpaka kufikia hapo, jina lake liliendelea kuwa kubwa, kazi aliyokuwa ameifanya

haikuwa ndogo, ilikuwa ni kazi moja kubwa ambayo ilimpa heshima kubwa.

Siku ya kwanza ikakatika, katika mwezi huo wa pili, ulipofika katikati, kama

muujiza, Maimartha akaanza kuyafumbua macho yake na kuanza kuangalia

hapo alipokuwa.

Madaktari walikuwa wamemzunguka, kila alipokuwa akiangalia alipokuwa

hakupafahamu lakini mara ya kuwaona madaktari hao, dripu alizokuwa

ametundikiwa na mashine ya oksijeni iliyokuwa imeziba pua na mdomo wake,

akagundua kwamba alikuwa hospitalini.

Madaktari waliomzunguka, hakukuwa na daktari mweusi, kila mmoja alikuwa

mweupe, hiyo ikaacha maswali kichwani mwake kwamba alikuwa wapi.

“Welcome to the world” (Karibu ulimwenguni)” alisema Dk. Amir huku uso wake

ukipambwa na tabasamu pana.

“Nipo wapi?” aliuliza Maimartha kwa sauti ya chini.

“Just relax....relax,” (Tulia...tulia)” alisema Dk. Amir.

Hapo ndipo ambapo Maimartha akaanza kukumbuka, mara ya mwisho kabisa

alikumbuka kwamba alikuwa ndani ya gari na alikuwa akisikia honi kwa nyuma,

alipogeuka, aliliona gari kubwa la mafuta likija kule alipokuwa, likaigonga gari

lake kwa nyuma, baada ya hapo, hakukumbuka kitu chochote kile

kilichoendelea.

Akaanza kujiangalia, akataka kuitoa mashine ile ya oksijeni, akashindwa

kuunyanyua mkono wake. Hakuishia hapo, akataka kuisogeza miguu yake,

akashindwa kabisa kufanya hivyo jambo lililomfanya kugundua kwamba

alipooza.

“Nimepooza, nimepooza,” alisema Maimartha huku akipiga kelele.

Alichokifanya Dk. Amir ni kuchukua sindano iliyokuwa na dawa ya usingizi na

kumchoma Maimartha, hapohapo akalala usingizi mzito.

Mpaka kufikia hatua hiyo, wakaanza kupongezana, kazi waliyokuwa

wameifanya ilikuwa kubwa iliyohitaji pongezi, hawakuamini kama kweli

walikuwa wamefanikiwa kwa kiasi hicho mpaka Maimartha kurudiwa na

fahamu, kazi kubwa ambayo ilikuwa imebakia ni kumrudisha katika hali yake ya

kawaida.

Walipopewa taarifa kwamba Maimartha alikuwa amerudiwa na fahamu, wote

kwa pamoja wakarukaruka kwa furaha na kukumbatiana, hawakuamini kama

mwisho wa siku Maimartha angeweza kurudiwa na fahamu kwani siku

ziliendelea kukatika na alikuwa kimya.

“Can she talk?” (Anaweza kuongea?) hilo lilikuwa swali la kwanza alilouliza

Henry.

“Yes, she can,” (Ndiyo, anaweza)

“We want to talk to her” (Tunataka kuongea naye) alisema Henry huku

akilengwa na machozi ya furaha. Kwa furaha aliyokuwa nayo moyoni, haikuweza kuelezeka.

Dk. Amir hakutaka kuwaruhusu muda huo kwani hata kama wangekwenda

ingekuwa kazi bure tu kwa sababu Maimartha alikuwa katika usingizi mara

baada ya kuchomwa sindano ile, alichowaambia ni kwamba wajiandae

kumwangalia siku inayofuatia.

“No problem” (Hakuna tatizo)” alisema Henry.

Siku hiyo ikaonekana kuwa siku yenye furaha kuliko siku zote katika maisha

yake, alifurahia kusikia kwamba hatimae Maimartha alikuwa amerudiwa na

fahamu zake huku akiwa na uwezo wa kuzungumza.

Ndani ya chumba cha hoteli, Henry alikuwa akimshukuru Mungu, hakuamini

kwamba mwisho wa siku alikuwa ametenda muujiza na kumrudishia fahamu

zake Maimartha. Mpaka analala saa tano usiku, bado Henry alikuwa mwenye

furaha tele.

Kwa sababu yeye ndiye alikuwa mwandishi pekee aliyejua hali ya Maimartha

ilivyokuwa ikiendelea nchini India, siku iliyofuata akaandika taarifa kuhusiana

na hali aliyokuwa nayo Maimartha hospitalini hapo.

Zilikuwa ni taarifa zilizowashtua Watanzania kwa furaha, hatimae maombi

waliyokuwa wakiyafanya kwa kipindi kirefu, wakati huo Mungu alikuwa

ametenda.

Magazeti yote na vyombo vingine vya habari vikaanza kuandika kuhusu taarifa

hiyo ila jambo la kusikitisha lililoandikwa ni kwamba Maimartha alikuwa

amepooza.

Wakristo hawakucha kuomba, kila siku Jumapili jioni walikuwa wakikutana

katika Kanisa la Praise And Worship na kuanza kumuombea Maimartha ili afya

yake itengemae na kuwa kama zamani.

Picha zake wakati yupo kitandani zilimsisimua kila mtu. Alionekana kama mfu

kitandani hapo, wengi waliokuwa na moyo mwepesi wakaanza kulia,

muonekano wake aliokuwa nao kitandani pale ulimuumiza kila mtu.

“R.I.P Maimartha,” alisema jamaa mmoja ambaye alishika Gazeti la Uwazi, kila

alipoiangalia picha ya Maimartha, hakuwa na matumaini kama msichana huyoa ngeweza kuamka tena.

Siku ambayo Henry na wazazi wake Maimartha walipofika hospitalini hapo kwaa jili ya kumwangalia Maimartha, hawakuamini kama siku hiyo wangewezak uongea na mgonjwa huyo kutokana na kipindi kirefu kuwa kimya kitandani.

Hawakuacha kumuomba Mungu, katika viti ambavyo walikuwa wamekaa huku
wakisubiri kuingia ndani, walikuwa wakiikutanisha mikono yao na kuanza
kusali.

Walimwamini Mungu, walijua kwamba hata kupata fahamu kwa Maimartha

ulikuwa ni muujiza mkubwa wa Mungu ambao alikuwa ameufanya katika
maisha yake.

Mpaka Dk. Amir anafika na kuwaambia kwamba mgonjwa alikuwaa mekwishaandaliwa na kuanza kuingia ndani, hawakuamini kama wangemkuta Maimartha akiwa macho huku akiwaangalia.

Walichoambiwa ndicho walichokutana nacho chumbani. Maimartha alikuwa
ameyafumbua macho yake, alikuwa akiangalia huku na kule, watu hao
walipoingia, machozi yakaanza kumbubujika.

Hakuwa na raha, moyo wake haukufurahi kabisa kila alipokuwa akikumbuka

kwamba kwa wakati huo mwili wake ulikuwa umepooza. Alitamani kutembea kama watu hao waliokuwa wameingia ndani ya chumba hicho, alitamani kuchezesha viungo vyake kama watu hao lakini kwa kipindi hicho
haikuwezekana kabisa.

Alikuwa kitandani hapo kama gogo, hakuwa na nguvu ya kugeuka kutoka
upande mmoja kwenda upande mwingine.

“Henry...” Maimartha alijikuta akiita kwa sauti ya chini, Henry akamsogelea.

“Maimartha, hatimae umerudiwa na fahamu,” alisema Henry huku machozi ya furaha yakianza kumtoka.

“Nimepooza Henry, siwezi hata kuugeuza mwili wangu kutoka sehemu moja kwenda nyingine,” alisema Maimartha, bado sauti yake ilikuwa ikisikika kwa chini kabisa.

Kana kwamba hakuwaona wazazi wake mahali pale. Maimartha alikuwa
akiongea na Henry tu kwani huyo ndiye mtu ambaye alikuwa naye karibu hata
kabla hajapatwa na majanga aliyokuwa ameyapata.

“Naomba unisamehe Maimartha, mimi ndiye niliyesababisha yote haya,”

alisema Henry kwa sauti ya chini, machozi ya furaha yaliyokuwa yakimbubujika yakabadilika na kuwa machozi yenye maumivu makali moyoni mwake.

“Si kosa lako Henry, ulifanya kile ulichotakiwa kufanya,” alisema Maimartha.

Bado sauti yake ilikuwa ni ya chini mno, kulikuwa na kazi ya ziada kumsikia

kile alichokuwa akikiongea mpaka ulisogeze sikio lako na kumsikiliza kwa
umakini.

Wazazi wake wakakisogelea kitanda kile, japokuwa binti yao alikuwaa merudiwa na fahamu lakini bado waliendelea kumuonea huruma kitandani pale. Ule, kwao ukaonekana kuwa mkubwa katika maisha ya Maimartha, hawakutarajia kama ingetokea siku ambayo Maimartha angekuwa katika hali hiyo.

“Maimartha...” aliita mama yake, bi Estelina.

“Mama...umekuja kuniona,” alisema Maimartha.

“Nimekuja mwanangu, nisingeweza kukuacha, hali yako inanisikitisha sana, kila siku nimekuwa nikimuomba Mungu urudi katika hali nzuri,” alisema bi Estelina huku naye akianza kububujikwa na machozi.

Bado mioyo yao haikupata faraja ile waliyotakiwa kuipata, japokuwa mtoto

wao, Maimartha alikuwa amerudiwa na fahamu na kuweza kuzungumza tena
lakini bado hawakufurahishwa kumuona akiwa katika hali ile, walitaka aweze kusimama na kutembea kama ilivyokuwa zamani.

“Mungu atatenda tu, nitasimama na kutembea kama zamani,” alisema

Maimartha kwa sauti ya chini.

Japokuwa alikuwa akipitia mateso makali kitandani pale bado moyo wake
ulikuwa na imani kubwa kwamba kuna siku angeweza kusimama tena na
kutembea kama ilivyokuwa zamani.

Hiyo ilikuwa ni imani yake ambayo kila siku ilikuwa ikitenda kazi moyoni
mwake. Mpaka kufikia kipindi hicho, bado aliendelea kujisaidia na kula kwa
kutumia mipira ile ambayo baada ya siku kadhaa ikatolewa na kuanza kutumia njia ya kawaida.

Hakika Maimartha aliendelea kuwa kwenye mateso makali kupita kawaida.

Alitamani kutembea kama alivyokuwa zamani lakini katika kipindi hicho, ajali
aliyokuwa ameipata ilibadilisha kila kitu.

“Kama Yesu aliwaponya watu waliopooza na kuwafanya vipofu kuona, kweli atashindwa kuniinua katika kitanda hiki?” aliuliza Maimartha.

“Anaweza. Bado haujamaliza kazi yake, itakupasa uendelee kuwa hai kwa ajili
ya kuifanya kazi yake,” alisema Henry huku kwa mbali akiachia tabasamu.

“Kama ataniponya, ni lini sasa?”

“Siku yoyote. Mungu huwa hawai na wala hakawii, anafanya mambo yake kwa wakati ulio sahihi.”

“Henry....”

“Naaam.”

“Unanipenda?”

“Umekuwa rafiki yangu kwa kipindi kirefu, ninakupenda Maimartha.”

“Simaanishi urafiki, macho yako yananionyeshea kila kitu, unanipenda?” aliuliza

Maimartha.

“Maimartha....” aliita Henry, akakaa kimya huku akijifikiria jibu la kutoa mahali hapo.

“Naomba unijibu Henry,” alisema Maimartha.

“Najisikia hivyo moyoni mwangu, sijui kwa nini, nilikuwa nakuchukulia kama

mtu wa kawaida, ila kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, nahisi kukupenda kwa mapenzi ya dhati,” alisema Henry kwa sauti ya chini, hakutaka wazazi wa

Maimartha wasikie.

“Nimepooza Henry, utanipenda vipi mtu kama mimi?” aliuliza Maimartha.

“Ninaamini utapona tu, na hata kama hautopona, bado hiyo si sababu ya

kunifanya nisikupende maishani mwangu. Najihisi kuwa na mapenzi mazito kwako, sijajua kwa nini, moyo wangu unaniambia kwamba wewe ndiye mke sahihi wa maisha yangu,” alisema Henry, yalikuwa maneno yenye kuumiza mno, yakamfanya Maimartha kububujikwa na machozi.

“Nimepooza Henry,” alisema Maimartha, alikuwa akijisikia uchungu kuwa katika hali ile.

“Maimartha, Mungu ameruhusu jambo hili kutokea, huwa hafanyi makosa

anaporuhusu jambo fulani litokee. Labda ameruhusu hili kwa kuwa anataka kuona ni kwa jinsi gani nitaweza kukuoneshea upendo wa dhati kutoka moyonim wangu. Maimartha, umepooza, ndiyo, lakini huu ni muda wangu wa kukuonyeshea mapenzi ya dhati. Ninakupenda Maimartha,” alisema Henry, naye
akajikuta akianza kububujikwa na machozi.

Alikuwa ameamua, kila siku alipokuwa hospitalini hapo,kila alipokuwaa kimwangalia Maimartha, aliuhisi moyo wake kuwa kwenye mapenzi ya dhati
kwa msichana huyo.

Moyo wake ulikuwa umekufa na kuoza, hakutaka tena kuwa na msichana
mwingine zaidi ya Maimartha ambaye alikuwa kitandani akisubiri kufa tu. Moyo wake ulizidiwa na mapenzi juu ya msichana huyo, hata kama alikuwa
amepooza kitandani, hilo hakujali, kitu alichokuwa akikisikiliza ni mapenzi
yaliyoanza kuchipuka moyoni mwake tu.

Henry alijikuta akiwa kwenye mapenzi ya msichana Maimartha kwa asilimia
mia moja. Kipindi cha kwanza aliona ni kitu kisichowezekana kwa mtu kama
yeye ambaye alikuwa amepanga kutokujiingiza katika mahusiano ya mapenzi kuanza kumpenda msichana yeyote yule.

Kwa Maimartha, ilimshangaza sana. Hakuwa na wazo la kuwa na msichana
huyo, si kwamba alikuwa amepooza tu bali hata kwenye kipindi alichokuwa
mzima wa afya, bado hakuwa akimpenda, kila siku alimchukulia kama mtu wa kawaida.

Leo hii, msichana huyo akiwa kitandani huku akiwa amepooza mwili mzima,
akajikuta akianza kuanguka katika mapenzi ya msichana huyo. Bado hakujua kitu hicho kilisababishwa na nini kwani kama ni ukaribu, aliwahi kuwa karibu na wasichana wengi lakini jambo hilo halikuwahi kutokea.

“Ninampenda Maimartha, nikisema simpendi nitakuwa najidanganya tu,”

alisema Henry katika kipindi ambacho alikuwa katika chumba cha hoteli.

“Lakini kwa nini imekuwa hivi? Mbona sikuwa nikimpenda toka kipindi cha
nyuma, kwa nini imekuwa leo?” alijiuliza Henry lakini hakupata jibu, suala
lilikuwa ni lilelile kwamba alikuwa kwenye mapenzi ya dhati na msichana huyo.

Siku iliyofuatia, aliamka kitandani na kujiandaa kwa ajili ya kwenda hospitalini kumuona Maimartha. Siku hiyo hakutaka kwenda mikono mitupu, alipitia katika duka la maua na kununua maua kadhaa na kadi ya kumtakia afya njema.

Alipofika hospitalini hapo, akamuwekea Maimartha maua yale pembeni na kisha kumbusu kwenye paji la uso. Japokuwa alikuwa amepooza kitandani, akahisi kabisa kwamba busu lile lilikuwa limemletea kitu cha tofauti mwilini mwake, akaachia tabasamu.

“Henry...” aliita Maimartha kwa sauti ya chini.

“Unasemaje kipenzi.”

“Mwili wangu umesisimka.”

“Mwili wako umesisimka?” aliuliza Henry kwa mshtuko.

“Ndiyo. Mwili wangu umesisimka,"alisema Maimartha huku akianza kububujikwa na machozi

“Hapana. Haiwezekani mwili wako kusisimka na wakati umepooza,” alisema Henry.

“Kweli Henry, mwili wangu umesisimka, busu lako lilitaka kunirudisha katika
hali ya kawaida,” alisema Maimartha huku akionekana kumaanisha kile
alichokuwa amekisema.

“Hebu jaribu kuunyanyua mkono wako,” alisema Henry na Maimartha kujaribu
kufanya hivyo.

“Siwezi. Nashindwa kufanya kitu chochote kile,” alisema Maimartha kwa sauti ya chini huku akionekana kuwa na majonzi.

Henry akanyong’onyea, kitendo cha kuona kwamba Maimartha hakuweza hata kuufanyisha kazi mwili wake kuliendelea kumpa uhakika kwamba bado msichana huyo hakuwa amepona na hata ile kauli ya kusema kwamba aliuhisi mwili wake ukisisimka haikuwa kweli.

“Kuna siku utasimama na kutembea tena,” Henry alimwambia Maimartha,

ilionekana kuwa kauli uliyojaa imani kubwa.

“Namtumaini Mungu, nitarudi kama nilivyokuwa,” alisema Maimartha.

Huku mapenzi baina ya watu hao wawili yakianza kuchipuka, hapo ndipo
ambapo Henry akamuomba Maimartha kumwadithia maisha yake ya nyuma kwa ajili ya kuandaa kitabu cha maisha yake.

Hilo halikuwa tatizo tena, alichokifanya Maimartha ni kumuahidi Henry kwamba kesho yake ingekuwa siku maalumu ya kuanza kumuhadithia kila kitu kilichokuwa kimetokea katika maisha yake ya nyuma.

Henry akaifurahi, hicho ndicho kitu alichokuwa akikitaka kwa kipindi kirefu kwa kuamini kwamba kingempa jina kubwa zaidi ya lile alilokuwa nalo katika kipindi hicho.

Siku iliyofuata, Henry alikuwa amejiandaa kwa kila kitu, mkono mwake alikuwa na vitendea kazi vyote kama kalamu na notebook yake tayari kwa kuanza kazi aliyotarajia kuifanya hospitalini.

Alipofika, mara baada ya maongezi ya hapa na pale likiwepo la kumjulia hali,

Henry akajiweka sawa tayari kwa kusikiliza kile alichokuwa akitaka kuhadithiwa na Maimartha huku yeye akiwa tayari kwa kuandika baadhi ya vitu.

“Henry, naomba usinichukie,” alisema Maimartha.

“Siwezi kukuchukia, kilichopita, kimepita, kamwe hakiwezi kunifanyan ikuchukie,” alisema Henry.

“Kweli?”

“Niamini.”

“Nashukuru kama unamaanisha.” alisema Maimartha.

Henry akajiweka vizuri, akaishika vizuri kalamu yake tayari kwa kuanza kazi
aliyokuwa akitamani kuifanya kwa kipindi kirefu. Maimartha akameza mate, kabla hajaanza kuongea kitu chochote kile, machozi yakaanza kumtoka, alionekana kuumizwa na matukio yake ya nyuma yaliyotokea katika maisha yake.

“Nitaanza mwanzo kabisa kipindi ambacho mama alikuwa amejifungua.

Sikuona ila alinihadithia kila kitu, nadhani natakiwa kuanzia hapo,” alisema Maimartha.

“Hakuna tatizo,” alisema Henry huku akijiweka sawa, notebook ilikuwa

mapajani mwake na kalamu mkononi mwake, alichokuwa akikitaka ni kuandika vitu muhimu ambavyo Maimartha angevitamka mahali hapo.

1987, Nungi, Singida.

Msichana mjamzito alikuwa akilia kwa maumivu makali alipokuwa katika
barabara ndogo iliyokuwa ikielekea katika Kijiji cha Muhalala mkoani Singida.

Wapita njia waliokuwa wakipita karibu na njia ile, wakaanza kumfuata msichana yule aliyekuwa akiendelea kulia kwa maumivu makali ya kutaka kujifungua huku akionekana kuhitaji msaada.

Tayari damu zikaanza kumtoka kitu kilichowafanya watu wale waliomfuata
kushikwa na wasiwasi kwamba kuona endapo wasingefanya kile kilichotakiwa
kufanywa basi hali ingeweza kuwa mbaya.

Kwa haraka sana msichana yule akalazwa chini na mwanaume mmoja
miongoni mwa watu wale waliomsogelea kukaa katikati ya miguu yake na kuanza kumtoa mtoto.

“Sukumaaaa...sukuma....” alisema mwanaume huyo huku akiwa ameiweka mikono yake tayari kwa kumvuta mtoto ambaye alionekana kuwa tayari kutoka.

Haikuwa kazi nyepesi, yalikuwa ni maumvivu makubwa mno aliyosikia
msichana huyo. Aliambiwa asukume, aliendelea kusukuma mpaka ukafika
wakati ambacho akaanzakukosa nguvu kabisa za kuendelea kusukuma.

“Nimechoka,” alisema msichana yule, sauti yake tu ilimaanisha kile alichokuwa akikiongea.

“Sukuma, sukuma,” alisema mwanaume yule huku mikono yake ikiwa tayari katikati ya mapaja ya msichana yule.

Walipoona kwamba kila walipoongea kipole msichana yule hakuwa akisukuma, wakaanza kumpiga vibao mfululizo mashavuni kitu kilichomfanya kuanza kazi ya kusukuma kwa mara nyingine.

Ingawa kulikuwa ni njiani kwenye vumbi lakini hakukuwa na mtu aliyejali hilo,
kitu walichokuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kuona mtoto huyo akizaliwa tu.
Damu hazikukoma, bado ziliendelea kutoka kama kawaida, njia ikajaa damu na majimaji ambayo yaliendelea kutoka kwa msichana yule, baada ya dakika kumi za maumivu, mwanaume yule akafanikiwa kumtoa mtoto huyo.

Mtoto alikuwa kimya, macho yake yalikuwa yamefumba, alichokifanya ni
kukikata kitovu na kisha kuanza kumtingishatingisha mtoto yule, akaanza kulia huku akikunjakunja ngumi hali iliyomfanya mwanaume yule kutoa tabasamu pana.

“Wa kike,” alisema mwanaume huyo.
Hapo ndipo walipoanza kushughulikia suala la kumpeleka katika zahanati
ndogo iliyokuwa katika Kijiji cha Muhalala.

Kijijini hapo, hakukuwa na maendeleo yoyote yale. Hakukuwa na usafiri wa
hospitalini, wanakijiji wenyewe hawakuwa wakimiliki hata baiskeli, ukiachana na hayo, hata vyakula vyenyewe vilikuwa ni vya shida mno.
Hali ilikuwa mbaya sana, japokuwa mwanamke yule alikuwa akitokwa na damu na hakukuwa na usafiri wowote ule, wakaanza kumbeba kumpeleka katika zahanati ya kijiji hicho ambacho kilikuwa na umbali wa zaidi ya kilomita tatu.

Mwendo ulikuwa mrefu wenye kuchosha lakini hawakutaka kuacha kuelekea katika zahanati hiyo.

Mwanamke yule wasiyemjua alikuwa akiendelea kupiga kelele za maumivu huku damu zikiendelea kumtoka hali iliyoonyesha kwamba angeweza kufariki muda wowote ule.

“Subirini kwanza,” alisema mzee mmoja.
“Kuna nini?”
“Damu zinamtoka sana. Hatuwezi kupata ngadungadu?” aliuliza mzee huyo.

“Ngoja tuangalie.”
Mzee mmoja akaingia porini. Ngadungadu yalikuwa ni aina ya majani ambayo yalikuwa yakiota sana porini huku kazi yake kubw awaliyokuwa wakitumia wanakijiji wa vijiji vya Singida ni kukaushia damu mwilini.

Hata kama mwili ulikuwa umepata jeraha la aina gani huku damu zikitoka,
ukipaka majani ya ngadungadu damu inakata kabisa.

Hayo ndiyo majani waliyokuwa wakiyataka mahali hapo. Haikuwa kazi ndogo kuyapata, baada ya dakika tano, mzee yule akawarudia mahali hapo huku akiwa na majani hayo ambapo kwa kutumia meno yao, wakayasaga na kisha kumpaka mwanamke yule sehemu za siri, damu ikakata.

“Tuondokeni,” alisema mzee yule ambaye alionekana kuwa kiongozi na safari kuendelea.
Kwa shida kubwa, kupata vilima na kushusha, kutembea katika sehemu
tambarare na mabondeni, mwisho wa siku wakajikuta wakiingia katika Kijiji cha Muhalala ambapo wakampeleka mwanamke yule katika zahanati ndogo huku akiwa amepoteza fahamu.

“Mleteni,” alisema nesi mmoja miongoni mwa manesi wanne waliokuwepo nje ya zahanati ile.

Msichana yule akachukuliwa na kupandishwa juu ya kitanda, hakuwa
akijitambua na alikuwa amepoteza damu nyingi sana njiani, Hapo ndipo
matibabu yalipoanza.

Kwanza akasafishwa na kulazwa huku dripu ikining’inizwa juu na maji yakiingia kidogokidogo kwenye mshipa wake. Baada ya dakika ishirini, nesi mmoja akawafuata wanaume wale.
“Mnamfahamu huyu msichana?” aliuliza nesi mmoja.

“Hapana. Tulikutana naye njiani, tukaamua kumsaidia,” alijibu mwanaume mmoja.

“Kwa hiyo hamumfahamu kabisa?”
“Ndiyo dada. Kuna nini? Amekufa?”
“Hapana. Dokta anataka kuongea na ndugu zake.”
“Labda tuseme sisi ndiyo ndugu zake, kwa hiyo kuna nini?”
“Nifuateni.”

Yule nesi akaanza kuingia ndani, wanaume wale watatu wakainuka na kuanza kumfuta. Nesi akaingia katika chumba kidogo kilichokuwa kikitumika kama ofisi ya daktari mkuu wa zahanati ile, nao wakaingia.
Macho yao yakatua usoni mwa mzee mmoja mwenye ndevu nyingi aliyekuwa amevaa miwani usoni. Uso wake haukuwa na tabasamu hata kidogo, alionekana kuwa ‘serious’ kila wakati.

Wanaume wale walipoingia, akaishusha miwani yake na kuanza kuwaangalia, aliporidhika, akachukua faili lililokuwa mezani na kuanza kulifungua.

Akaanza kuyapitisha macho yake ndani ya faili lile, aliporidhika, akayainua macho yake na kuanza kuwaangalia tena.
“Mgonjwa wenu amepoteza kiasi kikubwa cha damu, inabidi asafirishwe
kuelekea Singida Mjini,” alisema dokta yule.

“Na vipi kuhusu mtoto wake?”
“Mtoto wake tumemwangalia, anaendelea vizuri japokuwa naye tulimkuta na tatizo kidogo, ila anaendelea vizuri. Itampasa asafirishwe na mama yake
kuelekea Mjini,” alisema dokta yule.
“Hilo si tatizo. Gari si lipo?”
Gari lipo ila kwa sasa lipo Mwasa, kwenye saa nane mchana watakuwa
wamekwishafika hapa. Si unajua tuna gari moja tu la hospitali,” alisema dokta
yule.

“Basi hakuna tatizo. Tutasubiri.”
“Sawa. Ila inabidi mchangie mafuta,” alisema dokta yule.
“Hakuna tatizo.”

Ilipofika saa nane mchana, gari aina ya ‘defender’ likasimama nje ya hospitali
ile, kwa haraka manesi waliokuwepo ndani ya zahanati wakatoka huku wakiwa wamembeba msichana yule na mtoto wake, wakamuweka ndani ya gari lile.

“Na sisi si tunakwenda?” aliuliza mwanaume mmoja.

“Ndiyo. Ila hela ya mafuta iko wapi?” aliuliza dokta yule. Mwanaume mmoja
akamfuata na kumpa kiasi cha shilingi mia tano ambacho walikuwa
wamechanga na dokta kumpa dereva.
“Ongozana nao,” alisema dokta akimwambia nesi mmoja.

Safari haikuwa fupi, kutokana na ubovu mkubwa wa barabara iliyokuwa na
mashimo mengi, gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa taratibu sana hali iliyowapelekea kuchoka kupita kawaida.

Kila wakati, walikuwa wakimwangalia mwanamke yule waliyekuwa wakimsaidia, kwa muonekana wake alionekana kuwa binti mdogo ambaye kwa kukadiria tu alikuwa na miak isiyozidi ishirini.

Vichwa vyao vilikuwa na maswali mengi ya kuuliza lakini katika kipindi hicho, kila mmoja alikuwa kimya akiifuatilia safari hiyo ambayo kwa ujumla ilionekana kuwa kero kutokana na mashimo mengi barabarani.

Walichukua masaa matatu, wakafika Singida Mjini ambapo wakampeleka katika Hospitali ya Mkoa na matibabu kuanza rasmi huku wanaume hao wakibaki kwenye mabenchi.

“Hapa tutachelewa. Tukatoeni taarifa kwa manesi ili kama vipi tuondoke,”
alishauri mwanaume mmoja.

“Hakuna tatizo,” aliunga mkono mwanaume mwingine na wote kumfuata dokta na kumweleza kila kitu kuhusiana na safri yao mpaka walipomkuta mwanamke huyo.
“Hakuna tatizo. Nyie nendeni, nawaahidi atapona tu,” alisema dokta huyo na wanaume wale kuondoka zao.

Namtaka mtoto wangu, dokta, mtoto wangu yupo wapi?” aliuliza msichana yule kwa sauti ya juu iliyoonekana kuwa kelele hospitalini hapo.

“Nyamaza, mtoto wako yupo salama,” alisema nesi mmoja.
“Yupo wapi? Nionyesheeni mtoto wangu kwanza,” alisema msichana yule.

Kwa sababu alikuwa akipiga sana kelele, walichokifanya manesi waliokuwa ndani ya chumba kile ni kumletea mtoto wake ambaye alionekana kuwa katika hali ya usafi.

Msichana yule akaonyesha tabasamu pana usoni mwake, kumuona mtoto wake kukampa faraja kubwa, akamchukua na kuanza kummwagia mabusu mfululizo usoni
“Nakupenda mwanangu,” alisema msichana yule.

Kuanzia siku hiyo, msichana huyo akawa mtu wa kukaa hospitalini hapo. Uso wake ulionekana kuwa na majonzi makubwa, hakuamini kama aliweza
kujifungua mtoto yule salama.

Kila alipokuwa akimwangalia, alikuwa akilia tu. Moyo wake ulijawa na
maumivu, maisha yake ya nyuma yalimuumiza kupita kawaida, hakuamini kama mwisho wa siku alikuwa amemshika mtoto wake mikononi mwake.

Kila walipokuwa wakimwangalia, manesi walikuwa wakimshangaa. Kwa
muonekano wake tu, alionekana kuwa na kitu moyoni mwake, alionekana
kuumizwa na kitu fulani lakini hakuwa radhi kukizungumza mahali hapo.

Manesi hawakutaka kukaa kimya, walichokifanya ni kuanza kumdadisi ili kujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea kwa msichana yule, kwa nini alijifungulia njiani? Alikuwa akitoka wapi? Na ndugu zake walikuwa wapi?
“Nilifukuzwa na baba baada ya kumwambia kwamba nilikuwa na mimba,” alisema msichana yule kwa sauti ya chini.
“Umetoka wapi?”
“Kijijini kwetu.”
“Wapi?”

Hakutaka kulijibu swali hilo, akabaki kimya kwa muda. Kilio cha kwikwi kilianza kusikika kutoka kwake. Alilia kwa sekunde kadhaa, akajitahidi kunyamaza na kuyafuta machozi yake.
“Nimetokea Nungi,” alijibu msichana yule.

“Sawa. Ni nani aliyekupa ujauzito huu?”
“Sijui. Ninachokumbuka ni kwamba kuna siku nilibakwa na vijana wanne kijijini kwetu wakati natoka kwenye mkutano wa injili,” alisema msichana yule.

“Ulibakwa na vijana wanne?”
“Ndiyo.”
“Ikawaje sasa?”
“Nilipokwenda nyumbani, sikuwaambia wazazi, nilijifungia chumbani nikilia tu
kwani nilijisikia maumivu makubwa moyoni mwangu. Nilimuomba Mungu anipe amani na furaha kama niliyokuwa nayo lakini ilishindikana kabisa.

Baada ya miezi miwili, kwenda kupima, nikaambia nina ujauzito,” alisema msichana huyo.
“Pole sana. Wazazi wako wameokoka?”
“Hakuna aliyeokoka. Nilipoamua kuokoka, wakanitenga, wao ni wapagani, hawalijui kanisa wala msikiti, wapowapo tu. Kwa kipindi kirefu walikuwa wakinisisitizia kwamba sikutakiwa kwenda kanisani, niliwabishia sana na ndiyo
maana hata nilipowaambia kwamba nina mimba, wakanifukuza,” alisema
msichana huyo.

“Ukaenda kuishi wapi baada ya hapo?”
“Nilikuwa katika cha Mbwenini, huko, nikajiunga na kikundi kimoja cha ngoma kilichokuwa kikimilikiwa na mwanamke mmoja aliyekuwa akiitwa Ebeza.

“Nikaishi na mwanamke yule kwa miezi kadhaa, mimba yangu ilipoanza
kuonekana ndipo hapo alipoanza kuninyanyasa. Siku moja kabla ya kujifungua, nikaamua kutoroka kwani mambo yalikuwa magumu mno,” alisema msichana huyo.

“Pole sana. Unaitwa nani?”
“Naitwa Estelina.”
“Pole Estelina,” alisema nesi mwingine.
“Asante dada.”
Estelina aliendelea kukaa hospitalini pale kwa takribani siku mbili na ndipo
aliporuhusiwa kuondoka nyumbani. Siku hiyo ilikuwa ni ya majonzi kwake,
hakuwa na sehemu ya kwenda na wala hakutaka kurudi nyumbani kwao wala
kwa bi Ebeza.

Japokuwa hakutaka kwenda huko lakini hakuwa na sehemu yoyote ile ya kuishi
jambo lililomfanya kuwa na wakati mgumu mno.

Manesi walipoligundua hilo, wakaamua kuchanga fedha na kisha kumgawia,
kilikuwa ni zaidi ya shilingi elfu moja, hicho ndicho ambacho alitakiwa kuanza nacho maisha. Kwa mwaka huo 1988, kiasi hicho kilikuwa kikubwa sana.
“Nitabaki hapahapa mjini, mpaka nipate fedha zaidi,” alisema Estelina.
Huo ndiyo uamuzi aliokuwa ameufikia muda huo, alitaka kuendelea kubaki hapo mjini kwa ajili ya kukusanya fedha ili akizipata ajue ni kitu gani kilichokuwa
kikifuatia.

“Nitafanya kazi baa,” alijisemea Estelina.
Hakutaka kuchagua kazi, hakuwa na sehemu yoyote ya kulala na wala hakuwa na uwezo wowote wa kupanga chumba hivyo maisha yake kwa wakati huyo alitegemea kuishi mitaani tu.
Mtoto, kwake akaonekana kuwa usumbufu mkubwa, kuna wakati alitamani kumtupa sehemu ili aendelee na maisha yake lakini kuna wakati roho ya huruma ilikuwa ikimjia na kuona kwamba kile nacho kilikuwa ni kiumbe cha Mungu.

Akaamua kumvumilia, japokuwa alikuwa mtoto wa kulialia kila wakati lakini hayo yote akaona si kitu, hakuona kama hizo zilikuwa sababu zilizojitosheleza za kumtupa mtoto wake.

“Naomba kazi,” alisema Estelina, alikuwa katika chumba kimoja ambacho kilitumika kama ofisi ya meneja wa baa ya Mapesapesa iliyokuwa hapo Singida
Mjini.

“Nani kakwambia kuna kazi hapa?” aliuliza meneja huyo, alikuwa mzee mwenye mvi huku mdomo wake ukionyesha kwamba alikuwa mzuri wa kuvuta tumbaku.

“Nimeona tangazo hapo nje.”
“Si kwa mabinti waliozaa, tunataka wasichana wabichiwabichi, ili hata
wakiangaliwa na wateja, wavutiwe,” alisema meneja yule, mzee Mapunda.
“Naomba unipe nafasi,” aliomba Estelina huku akipiga magoti.
“Hakuna kazi kwa wakimama, tunataka mabinti.”

“Ila naweza kuwaburudisha wateja hata kwa kuimba,” alisema Estelina.
“Unajua kuimba?”
“Najua.”
“hebu imba kidogo nisikie,” alisema mzee Mapunda.
Hapo ndipo Estelina alipoanza kuimba. Sauti yake ilikuwa ni ya kipekee mno,
kila alipozidi kuimba zaidi na ndipo mzee Mapunda akaonekana kuvutiwa zaidi mpaka wakati mwingine kutikisa kichwa chake, juu kwenda chini, chini kwenda juu.

“Safi sana. Nilikuwa natafuta muimbaji, nahisi utatufaa,” alisema meneja
Mapunda.

Kwa sababu alikuwa na kipaji cha kuimba, hiyo ikaonekana kuwa nafasi yake ya kipekee ya kuwa muimbaji ndani ya baa hiyo. Akapewa chumba ambacho alikuwa akilala na wenzie wawili ambao kuishi na Estelina ilionekana kuwa mzigo mkubwa.

Kila wakati mtoto wake alikuwa akilia tu, haikujalisha kama ni usiku au
mchana. Mtoto akawa kero kwa wenzake, kuna wakati walikuwa wakimwambia ukweli kwamba mtoto wake alikera lakini kila siku walipoona hali hiyo inazidi, wakaamua kukaa kimya huku wakikereka mioyoni mwao.

Kila siku kazi yake kubwa katika baa hiyo ilikuwa ni kuimba tu. Japokuwa
alikuwa akipenda sana kufanya hivyo lakini kazi ile ikaonekana kuwa kero
kwake.

Kila wakati wanaume waliokuwa wakija hapo kunywa walikuwaw akimshikashika makalio yake na hata wengine wakidiriki kumwambia waende wakalale pamoja kitu ambacho kwake hakikuweza kukubalika.

Kutokana na mvuto wa nyimbo nzuri alizokuwa akiziimba, wateja wengi
wakaanza kumiminika ndani ya baa hiyo, sifa zikaanza kusambaa kila sehemu kwamba ndani ya baa hiyo kulikuwa na binti mdogo aliyekuwa akiimba nyimbo nzuri.

“Huwa ninakuja hapa kwa ajili ya huyu mwanamuziki tu,” alisema jamaa
mmoja ambaye alikuwa amekaa kwenye meza moja na wenzake watano.

“Ana sauti nzuri sana. Unajua sauti hii inaweza kumtoa nyoka pangoni!”
alisema jamaa mwingine na wote kuanza kucheka.

Mameneja waliokuwa wakimiliki baa nyingine walipoona hivyo, nao wakaanza kuwaweka waimbaji katika baa zao. Hiyo haikusaidia, sauti ya Estelina ilikuwa ni ya kipekee sana ambapo kila alipokuwa akiimba, hata kama ulikuwa wapi, pale unapoisikia tu ilikuwa ni lazima uende huko kushuhudia.

Baa ya Mapesapesa ikaanza kupata watu wengi, hata wale ambao hawakuwa wanywaji, kila walipokuwa wakipita na kumuona Estelina akiimba, walisimama na kuanza kumsikiliza.

Taarifa juu ya Estelina hazikuishia hapo, kila siku zilizidi kusambaa sehemu mbalimbali kwamba kulikuwa na msichana aliyekuwa akiimba kwa sauti nzuri kama malaika jambo lililoendelea kuwakusanya watu ndani ya baa hiyo. Wageni kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine, kila walipokuwa wakiingia ndani ya Singida, waliambiwa kuhusu Estelina kitu kilichowafanya kumiminika zaidi ndani ya baa hiyo.

“Aiseee, huyu dada anaimba balaa, sauti yake naifananisha na Diana Rose,” alisema mwanaume mmoja na kumtaja mwanamuziki huyo wa Marekani aliyekuwa akivuma sana kipindi hicho.

“Hebu isikilize sauti yake, hii ni sauti ya mrembo haswa,” aliingilia jamaa mwingine.

Mbali na kipaji cha uimbaji alichokuwa nacho, kwa uzuri, Estelina alikuwa ameumbika sana. Alikuwa mrefu wa saizi ya kati, mweupe, nyuma alikuwa amejaziajazia huku sura yake ikiwa ni ya kitoto ambayo kwa wazungu wangeiita ‘Babyface’.

Ukiachana na hayo, Estelina alikuwa na mguu iliyojaa, kiuno chake kilionekana wazi na kila alipokuwa akipiga hatua, huku nyuma milima miwili ilikuwa ikipishana, huu ukienda huku, ule unakwenda kule.
Mbali na umbo hilo, kuwa na mtoto, bado Estelina alikuwa na kifua kizuri.

Matiti yake hayakuwa yamelala kama ilivyokuwa kwa wanawake wengine waliozaa, chake, kilikuwa kimesimama kitu kilichoonyesha kama alikuwa ametoka kuvunja ungo juzi. Umbo lake liliwatoa udenda wanaume wengi kitu kilichowapelekea umtongoza mara kwa mara lakini msichana huyo hakutaka kuwaelewa kabisa.

Mameneja wa baa nyingine wakagundua kwamba mafanikio ya Baa ya Mapesapesa ilikuwa ni sauti nzuri ya Estelina. Japokuwa walikuwa na wasichana wao waliokuwa wakiimba lakini kwa Estelina alionekana kuwa tofauti kabisa.

Waliwaita wasichana kujaribu kuimba, wengi waliweza lakini kamwe hawakuufikia uwezo wa sauti nzuri iliyokuwa ikisikika kutoka kwa Estelina.

“Tunataka uje kufanya kazi kwetu,” alisema jamaa mmoja, alikuwa meneja wa Baa ya Polepole.

“Mtanilipa shilingi ngapi kwa siku?” aliuliza Estelina.
“Kwani hapa unalipwa kiasi gani?”
“Elfu moja.”
“Sisi tutakupa elfu moja na mia tano.”
“Sawa. Ngoja nijifikirie.”
“Tukupe muda gani?”
“Wiki moja.”

Dunia haikuwa na siri, japokuwa walikuwa wamekaa wawili tu wakiongea, baada ya siku mbili maneno hayo yakamfikia mzee Mapunda ambaye kwaharakaharaka akamuita Estelina ofisini na kuanza kuongea naye.

“Naomba usituache, nitakulia elfu mbili na mia tano kwa siku,” alisema mzee mapunda.

“Hiyo tu?” aliuliza Estelina?”
“Na chumba. Kitakuwa chumba cha peke yako, nitamuajiri mfanyakazi awe anakaa na mtoto wako,” alisema mzee Mapunda.

“Hakuna tatizo.” Sauti yake nzuri iliendelea kuwavutia watu wengi. Mzee mapunda alikwishagundua kwamba wateja wengi walimiminika katika baa yake kwa ajili ya Estelina tu na ndiyo maana hakutaka kumpoteza mtu huyo.
Alijiahidi kumfanyia kila kitu kuhakikisha kwamba anamshikilia, anakuwa wake na kuendelea kuwavutia wateja mahali hapo. Baa ya Mapesapesa iliendelea kukua zaidi, kila siku watu walikuwa wakimiminika katika baa hiyo, ghafla bin vuu, Estelina akajikuta akianza kuukwaa ustaa hapo Singida Mjini kutokana na umahiri wake katika kuimba.

Estelina aliendelea kuimba kama kawaida, akapata umaarufu mkubwa huku Baa ya Mapesapesa ikizidi kupata wateja wengi. Sauti yake bado iliendelea kuwa kivutio kwa watu wengi. Jina lake lilikua na kuheshimika kila kona.

Sifa zake, mbali na Singida, watu kutoka Dodoma wakaanza kusikia mengi kuhusu Estelina kitu kilichowafanya kusafiri kuelekea huko, nao walitaka kuisikia hiyo sauti ambayo ilijulikana kama ya kumtoa nyoka pangoni.
Walipofika huko, waliamini kile kilichokuwa kimeongelewa, sauti yake ilikuwa ni zaidi ya ile iliyozungumziwa kwamba ni ya kumtoa nyoka pangoni.

Kabla ya Estelina kufika katika baa hiyo, kwa siku zilikuwa zikiletwa kreti za pombe kumi na mbili lakini mara baada ya msichana huyo kufika katika baa hiyo, bosi, mzee Mapunda akaanza kuleta zaidi ya kreti mia mbili kwa siku na zote zilikuwa zikiisha.

Yalikuwa ni mafanikio makubwa na ndiyo maana kila siku alikuwa akipambana kuhakikisha kwamba anambakisha Estelina ndani ya baa yake, hakutaka aende sehemu yoyote ile.

Kwa Estelina, maisha yake yalikuwa yamebadilika, alianza taratibu kupokea kiasi kidogo cha fedha na mwisho wa siku dau lilipanda na kufikia kiasi cha shilingi elfu tano.

Hiyo ilikuwa mwaka 1991, kiasi hicho kilikuwa kikubwa ambacho kiliyabadilisha maisha yake kwa ujumla. Mtoto wake, Maimartha alikuwa amekua, kwa wakati huo alikuwa na miaka mitatu.
“Estelina, ninataka kukuoa, haki ya Mungu tena,” alisema Steven, jamaa aliyekuwa akiendesha magari ya mizigo kutoka Singida, kwenda Dar na sehemu nyingine nchini Tanzania.
“Unataka kunioa?” aliuliza Estelina.
“Ndiyo, nataka nikuweke ndani kabisa, halafu tunakwenda Mjini Dar es Salaam
kuishi pamoja,” alisema Steven.
“Hapana, sitaki kwenda Dar.”
“Kwa nini Estelina? Unajua Dar kuzuri, ukienda kule, kuna baa nyingi, utakuwa ukiimba na kulipwa kiasi kikubwa cha fedha,” alisema Steven.
“Sitaki kwenda Dar na sitaki kuolewa.”

Steven alikuwa mmoja miongoni mwa vijana wengi waliokuwa wakimtaka kimapenzi Estelina. Hakuwa msichana mwepesi wa kuwakubali wanaume, kila alipokuwa akiambiwa kwamba anataka kuolewa, Estelina alikuwa akikataa kabisa.

Aliyathamini sana maisha yake, aliwafahamu watu wengi ambao walikuwa wakiteseka ndani ya ndoa zao, walikuwa wamefuatwa vizuri na wanaume kwa ahadi ya kuolewa, baada ya kuingia kwenye ndoa, matatizo yalianza.

Yeye kama yeye alikuwa akijiweza kimaisha, alilala sehemu nzuri, alikuwa vizuri na alilipia matumizi ya kila kitu alichokuwa akikihitaji, hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuolewa.

Kila mwanaume aliyekuwa akimfuata, alimkatalia kwa kumwambia kwamba alijisikia vizuri kuishi peke yake kuliko kuishi na mtu.

Kuimba katika baa ya Mapesapesa hakukuisha, kila siku watu walikuwa wakikusanyika katika baa hiyo, viti havikutosha na hata eneo lilikuwa dogo lakini mzee Mapunda hakutaka kubadilisha eneo, alitaka kubaki hapohapo.

Mwaka wa tano ulipoingia, bado Estelina alionekana kuwa msichana mrembo sana ambaye alimvutia kila mtu aliyekuwa akimwangalia. Figa yake ilikuwa matata, nyuma alikuwa amejaa, sura ilikuwa nzuri. “Dada habari yako,” alimsalimia kijana mmoja, huyu alikuwa Paul. “Nzuri. Mambo vipi.” “Poa tu. Wewe ndiye muimbaji hapa?” aliuliza kijana huyo. “Ndiyo mimi. Kuna lolote?” “Yeah! Nilipita hapa jana, niliisikia sauti yako, hakika umebarikiwa,” alisema kijana yule.“Nashukuru.”

Estelina hakuwa na muda wa kuongea na wanaume, kila mwanaume aliyekuja mbele yake, aliongea naye kidogo na kuondoka zake. Aliwajua vilivyo wanaume, wengi walikuwa wakija katika sura ya upole lakini mioyo yao ilikuwa mikali zaidi ya simba.

Mwanaume huyo, Paul hakuacha kuja mahali hapo, kila siku alikuwa akija na kumsalimia Estelina, alipoanza kuimba tu, Paul alikuwa akiondoka zake.

Hali hiyo ikaendelea kwa mwezi mzima mpaka Estelina akaijua ratiba kamili ya Paul kuja hapo baa na kuongea naye. Kwake, kijana Paul alionekana kuwa tofauti na wanaume wengine.

Paul alikuwa kijana mpole kupita kawaida, kila alipokuwa akiongea naye, alikuwa akisikika kiupole sana. Japokuwa alikuwa amemzoea kwa kipindi kirefu, lakini kamwe kijana huyo hakuwahi kumtongoza, alikuwa akipiga naye stori kawaida tu na kuondoka zake.

Hakuwa mlevi, kila alipofika hapo baa, alikuwa akiagiza soda na chakula, anakula, Estelina alipokuwa akitaka kuimba, ananyanyuka na kuondoka zake.

Taratibu, Estelina akaanza kuumia moyoni, alitamani sana Paul aisikie sauti yake kila alipokuwa akiimba lakini mwanaume huyo alikuwa akiondoka kila Estelina alipotaka kuimba.

Tayari moyoni mwake kukaanza kujengeka kitu cha tofauti sana, kila alipokuwa akimuona Paul, alijisikia kabisa kuwa na furaha zaidi na kila mwanaume huyo alipokuwa akiondoka, moyoni alijisikia mnyonge.

Hali hiyo ilimuumiza mno, alivumilia zaidi lakini mwisho wa siku akashindwa kuvumilia, alichokifanya ni kumsubiria mwanaume huyo afike tena hapo baa na kumuuliza ni kitu gani kilichokuwa kikimsibu mpaka kuondoka kabla ya yeye kuanza kuimba.

Katika siku hiyo ambayo alikuwa akimsubiri Paul kwa hamu kubwa, hakuweza kutokea mahali hapo. Estelina akaanza kupatwa na wasiwasi, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimemsibu.

Siku hiyo akajipa moyo kwa kuona kwamba inawezekana alikuwa bize, akasubiri siku inayofuatia, nayo hakutokea, Estelina akanyong’onyea. Hatimae wiki nzima ikapita, bado Paul hakutokea.

Mwezi wa kwanza ukatimia, mwezi wa pili ukaingia na wa tatu kukatika, Paul hakurudi tena hapo baa kitu kilichomsononesha mno Estelina.
“Paul, upo wapi? Rudi mahali hapa japo hata siku moja tu, nimekukumbukamno,” alisema Estelina, maneno hayo hayakusaidia kitu chochote, mwezi wa sita ukakatika, Paul hakuonekana machoni mwake.
 
Back
Top Bottom