Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
[h=2][/h] [h=3]Sitta: Katiba Inaniruhusu Kugombea Urais 2015[/h]
Waziri wa Africa Mashariki, Samuel Sitta, amesema yupo huru kugombea Urais licha ya kuwa katika umri wa uzee.
Waziri wa Africa Mashariki, Samuel Sitta, amesema yupo huru kugombea Urais licha ya kuwa katika umri wa uzee.
Amesema yeye ni raia mwenye umri unaokubalika kikatiba kugombea nafasi hiyo iliyo kubwa kuliko zote za uongozi wa nchi, hivyo anawashangaa wanaopata kiwewe kuhusu suala hilo. Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye bonanza la waandishi wa habari linaloandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) linalofanyika kwenye ufukwe wa Msasani jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Sitta anayeheshimika kwa kuwa kiongozi wa 'kasi na viwango' Hivi karibuni, kuliibuka hoja ya umri wa watu wanaostahili kuwania uraia nchini ambapo mbali na Rais Jakaya Kikwete, wabunge Zuberi Zitto (Chadema) na Januari Makamba (CCM), wamekaririwa wakisema ni wakati kwa vijana kupewa fursa ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Sitta ameongeza kuwa wanasiasa wanapokuwa wameandikwa tofauti kwenye magazeti na vyombo vingine wasikasirike bali wawe wawazi kuzungumza ukweli kuliko kukasrikia vyombo vya habari. Ameongeza kwamba kama una chunusi usoni na umejiangalia kwenye kioo ukaiona inakukera usikimbilie kuvunja kioo ila tafuta dawa ya kuitibu ile chunusi. Mbali na urais, Sitta ameibua hoja ya kuwepo mkusanyiko wa waandishi wa habari katika kanda hiyo, ili kubadilishana uzoefu na kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao kwa jamii. Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tisa la Tanzania amesema atawashawishi mawaziri wenzake katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuunga mkono wa la kuwakutanisha waandishi wa habari kwa kupeana uenyeji wa kutoka nchi moja hadi nyingine. "Kwa kuanzia mjumuiko huo utaanzia hapa Tanzania na ninatarajia kuwa utafanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu," alisema. Sitta alisema uwezo wa kufanyika kwa matamasha yatakayowajumuisha waandishi wa habari wa Africa Mashariki upo hasa kwa kushirikisha makampuni ya kibiashara yanayofanya shughuli zao kwenye nchi wanachama.