Sitta: Katiba Inaniruhusu Kugombea Urais 2015

Tatizo hapa media nazo zinatafuta habari za kuuza magezeti yao tu
Mfano issue ni waandishi ndio walimuuliza, sasa tulitaka akatae kujibu
Na ofkozi kajibu vyema kuwa katiba inamruhusu kugombe, tusubiri muda ukifika tutajua
 
Sitta yuko sahihi kwa sababu ana haki kikatiba.. Anaetoa comment kumbeza au kumtukana au kumponda kwa kutoa kauli hiyo.. atakuwa na tatizo la uchoyo na kujiona yeye (mtoa comment) ana haki kuliko wengine.. Tufike wakati tukubaliane kila mtu anayo haki kikatiba..
 
i luv mzee sitta.nchi hii ingekuwa na wazalendo wa kutosha kama huyu mzee na utajiri huu tulionao ardhini tungesonga mbele sana.

Huyu mzee ni mnafiki na opportunist, angekuwa mzalendo na sio mbinafsi asingeichinjia hoja ya Richmond baharini alivyokuwa Spika. Hivi sasa yeye kuutaka urais ni kuhofia kuwa kama Lowassa atashinda basi ndio utakuwa mwisho wa maisha yake ya kisiasa!! Hana lolote he is just protecting his personal interests. Hawezi kuwa Rais bora kwani anajifanya yeye ni bora kulikop binadamu wengine na hili unaweza kulidhihilisha ukienda ofisini kwake anavyoogopa kuonana na wanannchi; ni rahisi kumuona Mkweree kuliko Sitta!! Urais atauotea huko Urambo!
 
muulize baba yako kama amewahi kuwa na ujasiri kama wa sitta hata robo yake,angekuwa mnafiki tayari angakuwa amechafuka kama yalivyo mafisadi sasa,hebu taja basi watu unaohisi ni wazuri kuwa marais katika nchi hii bila kutumia fikra za mihemko kama mzee sitta hatakuwa bora,sitta ana utu,dira,mikakati na uwezo.

Nchii kwa sasa imekaa vibaya lakini mzee bado ananguvu za kueleza na kusimamia anachokiamini,kama ni personal interests ni kitu gani alichijinufaisha tangu atumikie serikali akiwa kijana mdogo,amejenga barabara ya dar to dodoma,daraja na barabara ya salenda bridge,uwaja wa ndege muulize ni kiongozi yupi mwingine TZ aliyesimama imara kama sitta au mwakyembe kwa waliopo kwa sasa au ndani ya baraza.

GAMBA KUBWA WEWE,ANGALIA HILO GAMBA LITAKUFANYA USHINDWE HATA KUTEMBEA,IPE TARAKA NDOA YAKO NA MAFISADI HAYABEBEKI TENA MAGAMBA NI MAZITO MNO KWA HALI YA SASA,mimi ni mzee nakuambia haya maneno ili ujue unachokiongea kwenye mtandao wa watu wenye fikra pevu
 
Back
Top Bottom