Sitta akubali kuhusishwa na CCJ: "Mimi ni mtaji wa Urais"

Source: Habari leo au Uhuru, hayo magazeti yanatakiwa yatumike chooni na sio kusomwa na watu makini, Kiyabo = Njaa kali.

Bw. Kiyabo ambaye alibwaga manyanga CCJ baada ya kukosa usajili na kuhamia CHADEMA, na baadaye kurejea CCM na kushiriki katika kampeni dhidi ya Bw. Mpendazoe wakati wa kampeni kwenye Jimbo la Segerea, aliibuka jana na kumpinga Bw. Mpendazoe, akisema kuwa watu aliowataja kama waanzilishi hawakuwa wa kweli.

Ukiona mtu anatoka chooni (CCM) halafu anaingia bafuni (CCJ) halafu anaingia jikoni (CHADEMA) halafu anarudi chooni (CCM) basi ujue ana matatizo makubwa sana.

Muasisi aeleza 'siri' za CCJ

Na Gladness Mboma

ALIYEKUWA Mwenyekiti Mwanzilishi wa Chama cha Jamii (CCJ), Bw. Richard Kiyabo amejitokeza na kumpinga kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

(CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe juu ya waanzilishi wa Kilichokuwa Chama Cha Jamii (CCJ) huku akidai kuwa waliotajwa hawahusiki.

Bw. Kiyabo ambaye alibwaga manyanga CCJ baada ya kukosa usajili na kuhamia CHADEMA, na baadaye kurejea CCM na kushiriki katika kampeni dhidi ya Bw. Mpendazoe wakati wa kampeni kwenye Jimbo la Segerea, aliibuka jana na kumpinga Bw. Mpendazoe, akisema kuwa watu aliowataja kama waanzilishi hawakuwa wa kweli.

Bw. Mpendazoe amekaririwa juzi akiwataja Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Samueli Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nauye, Mbunge wa Lupa, Bw. Victor Mwambalaswa na Bw. Paul Makonda kuwa walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa CCJ.

Bw. Kiyabo alisema kuwa yeye na Bw. Renatus Muabhi ndio waliokuwa waanzilishi wa CCJ, na miongoni mwa watu waliojiunga nacho ni Bw. Mpendazoe ambaye alitaka kuwa Mwenyekiti wa Taifa, lakini hawakukubali ombi lake ambalo hakuliwasilisha kimaandishi.

"Chama kilimpitisha kuwa msemaji. Swali la kumuuliza Bw. Mpendazoe alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa ni hao aliowataja? Na je, hao walikuwa na nyadhifa zipi na kazi zipi za chama? Je, amesahau kwamba alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Bw. Sitta kwamba ajiunge na CCJ?," alihoji Bw. Kiyabo.

Bw. Kiyabo alisema kuwa vyama vya siasa hasa CHADEMA wanatakiwa kukumbuka kwamba siasa za udaku hazitawafikisha ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo wanajaribu kuonesha.

Alisema kuwa Watanzania wamekua kisiasa na ndio maana hawakuwaingiza CHADEMA ikulu kwa kura zao na kwamba kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kuchaguliwa kwenye chumba cha kupigia kura.

"Namshauri Bw. Mpendazoe na wenzake wa CHADEMA waache siasa za udaku. Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika na siyo udaku. Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha, mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera mpya ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi," alisema.

Alisema kuwa kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha, ambapo aliongeza kuwa CHADEMA wameonyesha kwamba nguvu ya umma siyo kura tena, 'bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani'.

Bw. Kyabo aliiponda CHADEMA, akisema kuwa wanajiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lakini ajabu wanayoyaonesha siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa 'chama chao ni cha maandamano na vurugu'.

"Je, wanaiheshimu kweli demokrasa? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watanzania kwa kura zao, sasa kwa nini hawawaheshimu, wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka CHADEMA ishinde uchaguzi. La hasha. Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao," alisisitiza bila kutoa mifano ya kauli hizo.

Alisema kuwa huu ni wakati wa kujenga Taifa, hivyo kinachotakiwa ni kushirikiana na serikali na siyo wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha na kuwataka Watanzania kuwa makini na wanasiasa wasioutakiwa mema utaifa wao na amani ya nchi.

"Tukumbuke kwamba suala la amani ni sawa na nyanya ikitumbuliwa kuishona tena huwa ni kazi ngumu sana. Bila amani shughuli za kimaendeleo haziwezi kufanyika, hata shughuli zao wenyewe CHADEMA hawataweza kuzifanya," alisema.

Naye Katibu CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Kilumbe Nge'nda alisema kuwa wamesikitishwa na taarifa zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA kuhusu Bw. Nape kuwa aliomba kugombea kwenye chama hicho baada ya CCM kumteua mwanachama mwingine kugombea jimbo la Ubungo.

"Ukweli ni kwamba Bw. Nape alikuwa miongoni mwa wanachama 13 waliojitokeza kuomba wateuliwe na CCM kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo lakini kipindi chote cha mchakato wa kampeni za kutafuta mgombea ndani ya CCM, alikuwa akitoa kauli kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kwamba ataheshimu matokeo na atakuwa tayari kumsaidia mgombea yeyote atakayeteuliwa na CCM ili chama kipate ushindi," alisema.

Alisema kuwa Bw. Nape hajawahi kuomba kuteuliwa kugombea CHADEMA na ingekuwa hivyo asingepata hata nguvu ya kuanika ufisadi unaokiandama chama hicho 'cha wanaharakati kinachofanana na chama cha wanasiasa'.

Hivi karibuni, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CHADEMA, Bw. Mabere marando alisema Bw. Nape baada ya kushindwa kura za maoni ndani ya CCM aliomba kugombea kupitia CHADEMA lakini baada ya kumjadili ndani ya vikao walibaini hana sifa kumshinda Bw. John Mnyika ambaye kwa sasa ndiye mbunge wa jimbo

jamani source ya habari hizi ni UHURU NA HABARI LEO,sasa cjui mi mtu gani makini anayeweza yaamin magazeti haya??????????????????????????

Nauona Mkono wa Rostam, Lowassa, Chenge kuvuruga Kampeni dhidi ya Mafisadi
CCJ leo, wapi na wapi? Halafu viongozi ndani ya CCM wanaotumainiwa na wananchi wanatajwa kuhusika na chama kilichokufa (Nape, Sitta na Mwakyembe). Wanatajwa leo ili iweje? Hawakutajwa jana kwa nini? Kwa nini watajwe na majeruhi wa siasa kwa jina Mpendazoe na siyo Msajili wa Vyama au nyaraka za Ofisi yake? Halafu vyombo vya habari vya Rostam (MTANZANIA, RAI, CHANNEL TEN) vinashabikia kweli kweli udaku wa Mpendazoe, kuna jambo! Halafu Mpendazoe ambaye nakaa naye jirani Tabata, kwa ghafla maisha yake yamebadilika: haombiombi tena fedha (ni mwombaji mzuri), gari lake (SUZUKI) lililokuwa juu ya mawe sasa linatembea na limepakwa rangi; anakarabati uzio wa nyumba yake na sasa yuko ziarani na watoto wake hawalii tena njaa (ni makaangizo tu ya kuku mchana na jioni!), hawazungumzii tena mafisadi watatu ndani ya CCM ila mawe yote kwa Kikwete na akina Nape, Sitta, Mwakyembe ambao, tutake tusitake, ni mtaji muhimu wa CCM mwaka 2015! Hapana, hapa kuna kitu! Nauona Mkono wa RA, EL na Vijisenti na kwa muda wamefanikiwa sana kuahirisha suala lao!

Sitta kwa majibu haya... uan akili saaaana hakuna wa kukufuata tena. jibu toshaaaa.. loh kumbe shule ina umuhimu wakeaiseee, kimyaaaaaaa

Sasa nimeamini kweli SITTA alimtoa Lowasa kwa chuki binafsi za kukosa uwaziri mkuu.

Jamaa ni mbinafi huyu ingekuwa enzi ya Mwalimu angeondolewa kwenye chama arudi Tabora akarine asali

hee bado kuna watu wanamlilia lowassa humu?

Back
Top Bottom