Sitta akubali kuhusishwa na CCJ: "Mimi ni mtaji wa Urais"

Mimi nadhani huu niwakati wetu wakujua niyupi anayewezaa ku a mtaji wa uraisi wa tanzania na kua mtaji wa kurinda maslai ya watanzania,
Hapa alichokifanya mpendazoe ni wakati wa kuwamaliza wote watalajiwa wa chama cha magamba this is political game,nadhani hapa jamaa wa chadema wamefauru kwa hili?sijui ninani anafaa ku mtarajiwa wa baadae wa chama cha magamba...................:biggrin1:
 
Sita anaweza kujiona mtaji wa kisiasa papohapo sisi tukamuona mtaji wa kisiasa ktk hasara, binafsi sioni faida yake coz hayupo shupavu, baada ya uchaguzi alijaribu kujitutumua kuizungumzia serikali ktk vyombo vya habari lakini alipotishwa na UVCCM akatulia mpaka leo sijui walipomgusa. Mwanzo nilijua nina vichwa muhimu Sita na Mwakyembe wanaharakati kumbe ujasiri hakuna.
 
Tatizo ni kwamba watu hawajmuelewa Mpendazoe, yeye hajasema kuwa tatizo ni kuanzisha CCJ , yeye anasema kuwa hao watu sita walimsaliti. kwa maana nikwamba walifyata mkia baada ya kitu fulani!

Dk. Mwakyembe alisema kuwa tatizo la Mpendazoe ni kwamba ana papara wakati siasa hazitaki hivyo na wala siasa sio mdundiko ambao kila anayeusikia husindikiza kwa macho na kwa miguu.

"Sisi tumeamua kubaki ndani ya chama tawala kuendesha mapambano dhidi ya ufisadi. Tutaendelea na mapambano tukiwa humu ndani na tunafanikiwa sana," alisema Dk. Mwakyembe.
 
Aliyekuwa mtaji wa Urais nchi hii ni Augustine Lyatonga Mrema peke yake hadi sasa. Sitta anaangalia mianya ya kisiasa ilipo na mapungufu ya viongozi wenzake anayatumia vizuri tu. Nimefahamu sasa kwanini aling'olewa Uspika kirahisi namna ile na akakaa kimya, akaendelea kuwa mwanaCCM mtiifu ambaye amebaki kurusha viteke vya hapa na pale.
 
Kazi nzuri aliyoifanya Sita akiwa Spika haina ubishi kwa wapenda uwazi, ukweli na maendeleo. Ametuamsha na matunda yake yanaonekana na anayebisha siyo kwamba hajui bali ni mbinafsi tu, period. Kila binadamu ana mapungufu yake kwani hakuna binadamu mwenye sifa ya Malaika.
Kuzima kibabe hoja ya richmond ndo kazi nzuri!! au kumtishia dr wa kuweli atamwitia polisi ili asitwambie wizi wa epa ndo kazi nzuri ya six!! Au ni kuzuia hoja ya meremeta isijadiliwe bungeni ndo kazi nzuri unayotwambia!! Shwaini......!!
 
Watanzania kweli sisi wasahaulifu au ni tunasona na Kusahau???
Huyu ndugu Sitta alisha wahi kuwa Waziri wa Ujenzi aliiba pesa nyingi za Miradi ya Barabara alishitakiwa kwa rushwa na kuwekwa Jela na kuvuliwa Ubunge...

Well Serikali Moja ya CCM Madarakani ilimsafisha akashinda rufaa kiujanja ujanja karudi bungeni na sasa ana wafanyia Michezo Vyama Vya Siasa kupata Vyeo au Pesa, we should let this person go long time ago

Sisi kuendelea tuache kukumbatia Mizogo Wezi na tuwe na Wanasiasa bora sio Vigugumizi Matumbo Njaa!!!!
 
Kazi nzuri aliyoifanya Sita akiwa Spika haina ubishi kwa wapenda uwazi, ukweli na maendeleo. Ametuamsha na matunda yake yanaonekana na anayebisha siyo kwamba hajui bali ni mbinafsi tu, period. Kila binadamu ana mapungufu yake kwani hakuna binadamu mwenye sifa ya Malaika.
sitta atakumbukwa kwa kuwa spika bora kabisa tangu tupate uhuru na kama si kumaliza sakata la richmond sivyo angrstahili kuingia kwenye kundi la viongozi watatu bora kabisa nchi hii tangu tupate uhuru
 
Sitta amekuwa muungwana zaidi na mkweli kimsingi Mpendazoe anaonge hii hoja haisaidi chochote chama
 
Hivi na aliyekuwa mwenyekiti wa CCj baada ya kurudia kulivaa gamba kaishia wapi?

Yule ana njaa sana, walinipa uenyekiti wa Mkoa mmoja nikaona balaa ambalo sijawahi kuliona kabisa, kila siku alikuwa ananiomba vocha! Mara oh! Familia yangu haijala siku ya pili! Ninazo sms zake kibaoooo! Sijui walimtoa wapi Kiyabo.
Huyo hafai hata kuongoza familia yake. Mwacheni na njaa zake
 
Sitta amekuwa muungwana zaidi na mkweli kimsingi Mpendazoe anaonge hii hoja haisaidi chochote chama

mpendazoe amesaidia kutia mashaka ndani ya ccm,..sasa hivi hawajui wamuamini nani?kundi la lowassa haliaminiki na kundi la sitta haliaminiki,perfect timing chadema,..kwa ufupi nape alikuwa anakuja juu sana dhidi ya cdm,mascud ya epa,ubunge ubungo na msumari wa mwisho kwenye mdomo wa nape ni ccj,well done mpendazoe,..mnaombeza mpendazoe kwa move yake hamjui siasa..wanazuga tu lakini kimsingi hawaaminiani tena hao,bomu litalipuka soon,just wait and see
 

CDM mfikirie mara mbili kuhusu Mpendazoe, huyu ni mropokaji ipo siku atakuja kuwaumbua kwani siku yeyote atakimbia CDM na kujiunga na chama kingine. Nawashangaa mnampa kipaza sauti na kuropoka maneno mbovu mbofu jukwaani. Siasa za kusema watu binafsi mzikomeshe muanze kutuambia ni namna gani mtatuondoa watanzania katika lindi la umaskini.

wawape maiki ili tuone nani mwanasiasa aliye na vision na nani kakalia sherehe za akina mzee yusuf!
 

CDM mfikirie mara mbili kuhusu Mpendazoe, huyu ni mropokaji ipo siku atakuja kuwaumbua kwani siku yeyote atakimbia CDM na kujiunga na chama kingine. Nawashangaa mnampa kipaza sauti na kuropoka maneno mbovu mbofu jukwaani. Siasa za kusema watu binafsi mzikomeshe muanze kutuambia ni namna gani mtatuondoa watanzania katika lindi la umaskini.

hii ndiyo point kwa wanasiasa wote,
lakini wapi bwana
nchi hii hatutaweza kupata maendeleo kwa kulumbana majukwaani na kutajana majina tu.
Mtu anasimama jukwaani na kulaani wabunge wenzie bila kusema yeye amefanya nini na amefanikiwa na lipi
 
Huyo aliyekuwa mwenyekiti siwezi kuamini maneno yake kwa sasa kwa kuwa nahisi ana bias. Hata hivyo sioni mantiki yoyote ya mpendazoe kutaja waliokuwa waanzilishi wa chama hicho kwa kuwa hakuna faida yoyote.
 
Muasisi aeleza 'siri' za CCJ



Na Gladness Mboma

ALIYEKUWA Mwenyekiti Mwanzilishi wa Chama cha Jamii (CCJ), Bw. Richard Kiyabo amejitokeza na kumpinga kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe juu ya waanzilishi wa Kilichokuwa Chama Cha Jamii (CCJ) huku akidai kuwa waliotajwa hawahusiki.

Bw. Kiyabo ambaye alibwaga manyanga CCJ baada ya kukosa usajili na kuhamia CHADEMA, na baadaye kurejea CCM na kushiriki katika kampeni dhidi ya Bw. Mpendazoe wakati wa kampeni kwenye Jimbo la Segerea, aliibuka jana na kumpinga Bw. Mpendazoe, akisema kuwa watu aliowataja kama waanzilishi hawakuwa wa kweli.

Bw. Mpendazoe amekaririwa juzi akiwataja Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Samueli Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nauye, Mbunge wa Lupa, Bw. Victor Mwambalaswa na Bw. Paul Makonda kuwa walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa CCJ.

Bw. Kiyabo alisema kuwa yeye na Bw. Renatus Muabhi ndio waliokuwa waanzilishi wa CCJ, na miongoni mwa watu waliojiunga nacho ni Bw. Mpendazoe ambaye alitaka kuwa Mwenyekiti wa Taifa, lakini hawakukubali ombi lake ambalo hakuliwasilisha kimaandishi.

"Chama kilimpitisha kuwa msemaji. Swali la kumuuliza Bw. Mpendazoe alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa ni hao aliowataja? Na je, hao walikuwa na nyadhifa zipi na kazi zipi za chama? Je, amesahau kwamba alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Bw. Sitta kwamba ajiunge na CCJ?," alihoji Bw. Kiyabo.

Bw. Kiyabo alisema kuwa vyama vya siasa hasa CHADEMA wanatakiwa kukumbuka kwamba siasa za udaku hazitawafikisha ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo wanajaribu kuonesha.

Alisema kuwa Watanzania wamekua kisiasa na ndio maana hawakuwaingiza CHADEMA ikulu kwa kura zao na kwamba kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kuchaguliwa kwenye chumba cha kupigia kura.

"Namshauri Bw. Mpendazoe na wenzake wa CHADEMA waache siasa za udaku. Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika na siyo udaku. Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha, mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera mpya ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi," alisema.

Alisema kuwa kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha, ambapo aliongeza kuwa CHADEMA wameonyesha kwamba nguvu ya umma siyo kura tena, 'bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani'.

Bw. Kyabo aliiponda CHADEMA, akisema kuwa wanajiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lakini ajabu wanayoyaonesha siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa 'chama chao ni cha maandamano na vurugu'.

"Je, wanaiheshimu kweli demokrasa? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watanzania kwa kura zao, sasa kwa nini hawawaheshimu, wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka CHADEMA ishinde uchaguzi. La hasha. Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao," alisisitiza bila kutoa mifano ya kauli hizo.

Alisema kuwa huu ni wakati wa kujenga Taifa, hivyo kinachotakiwa ni kushirikiana na serikali na siyo wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha na kuwataka Watanzania kuwa makini na wanasiasa wasioutakiwa mema utaifa wao na amani ya nchi.

"Tukumbuke kwamba suala la amani ni sawa na nyanya ikitumbuliwa kuishona tena huwa ni kazi ngumu sana. Bila amani shughuli za kimaendeleo haziwezi kufanyika, hata shughuli zao wenyewe CHADEMA hawataweza kuzifanya," alisema.

Naye Katibu CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Kilumbe Nge'nda alisema kuwa wamesikitishwa na taarifa zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA kuhusu Bw. Nape kuwa aliomba kugombea kwenye chama hicho baada ya CCM kumteua mwanachama mwingine kugombea jimbo la Ubungo.

"Ukweli ni kwamba Bw. Nape alikuwa miongoni mwa wanachama 13 waliojitokeza kuomba wateuliwe na CCM kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo lakini kipindi chote cha mchakato wa kampeni za kutafuta mgombea ndani ya CCM, alikuwa akitoa kauli kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kwamba ataheshimu matokeo na atakuwa tayari kumsaidia mgombea yeyote atakayeteuliwa na CCM ili chama kipate ushindi," alisema.

Alisema kuwa Bw. Nape hajawahi kuomba kuteuliwa kugombea CHADEMA na ingekuwa hivyo asingepata hata nguvu ya kuanika ufisadi unaokiandama chama hicho 'cha wanaharakati kinachofanana na chama cha wanasiasa'.

Hivi karibuni, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CHADEMA, Bw. Mabere marando alisema Bw. Nape baada ya kushindwa kura za maoni ndani ya CCM aliomba kugombea kupitia CHADEMA lakini baada ya kumjadili ndani ya vikao walibaini hana sifa kumshinda Bw. John Mnyika ambaye kwa sasa ndiye mbunge wa jimbo
 
NJAA HAIMPENDEZI MTU
Bw. Richard Kiyabo ana njaa kwa hiyo ni CCM inayoweza kumwondolea njaa
 
Back
Top Bottom