Sitaki urais, ni mzigo - Pinda

Safi sana, wazo zuri. Sasa wakorofi kinachofuata ni kwamba mtapigwa tuu. Nami nasema Pinda awapige tuu. Maana tumechoka sasa.
 
Kwa hiyo ina maana saivi urais imekuwa ni kama usanii wa bongo flavour kila mtu anaimba ili mradi anatoa sauti? Au mnaongelea urais gani? Labda wa kilimo na ufugaji nyuki. Au kama vipi makamu wake atakuwa Zitto Kabwe.
 
Iwapo kweli CCM wanauenzi muungano kwa kuipigia debe hoja ya serikali mbili, basi safari hii ni zamu ya Zanzibar kutoa rais wa jamhuri ya muungano. Tofauti ya hapo ni unafiki tu!!
 
Tunawezaje kuwa na raisi ,ambaye wazee wamemuomba ?hii inamaanisha bado ni mtumwa wa fikra ,ambaye anaamuliwa (kuombwa) kufanya jambo pasipo maamuzi Yake mwenyewe,mtu wa hivi ni tatizo tena kubwa,maana hata katika uongozi wake watarudi tena hao wazee kumuomba afanye kile wanachokifikiria wao.Ifikie hatua hawa watu wanaotaka uongozi kwa kisingizio cha kuombwa tuwakatae,Kama ni suala la uongozi mhusika anatakiwa awe na nia Yake ya dhati ya kutaka kuongoza
 
Sasa wakimtaka PINDA… CCM si ndio inayojitakia matatizo? wanagawana madaraka hadi urais jamani?

Sasa itakuwa nchi imetawaliwa na WAKRISTO - Catholics; na WAISLAMU - Sunni

Hiyo Balance ya CCM iko wapi eh? Mmeona ubaya wa kutuchagulia viongozi badala ya uwezo wao wa kisiasa????
 
Kutokana na sifa alizo nazo anafaa kuwa Rais wa Tanzania mwakani. Moja ya sifa alizo nazo ni pamoja na kuwa kiongozi ambae Hana kashfa yoyote ndani ya serikali,ni kiongozi mchapa kazi, msikivu,Anae tanguliza maslahi ya Taifa Mbele na sio mbinafsi ni moja ya viongozi wachache wazalendo wa kweli waliobakia nchini. Mungu naomba umuoteshe kama alivyowahi kutamka mwenyewe ili awe mmoja wa wagombea ambae ataipeperusha bendera ya CCM mwakani
 
Kulialia siyo sifa ya kiongozi
 
Back
Top Bottom