dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Basi mbona hawamshukuru Jakaya Kikwete kwa kumpa Lowasa uwaziri mkuu ambao leo hii ndio uwaziri mkuu huo umemzika kwa heshima ya waziri mkuu mstaafu japo alijiuzulu kwa Kashfa?
Wanamtambua Lowasa kama Waziri Mkuu Mstaafu lakini hawamtambui aliyempa hicho cheo? Upuuzi mtupu.
Jakaya Kikwete hakutajwa kisa alimkata jina kwenye urais 2015. Hivi ili Kikwete awe mzuri ilikuwa lazima Lowasa awe Rais? Mbona alikatwa Bilal makamu wa rais, alikatwa pinda waziri mkuu kwanini nongwa iwe kwa Lowasa tu? Yaani kanakwamba hakutakiwa kufa bila kuwa Rais?
Hata hivyo si Kikwete peke yake alikuwa anakata majina.
Kashfa ya 2008 ndo ilimharibia Lowassa. Alitakiwa ajisafishe tuhuma za Ufisadi. Sio kumtaka Jakaya Kikwete ambebe.
Edward Lowassa cheo cha juu alichoandikiwa na Mwenyezi Mungu Muumba ni Uwaziri Mkuu. Uwaziri Mkuu wenyewe akaususa kwa kujiuzulu. Angeteuliwaje tena Uwaziri Mkuu alosusa?
Pamoja na kuwa bungeni kipindi kirefu, hivi ndo aina na vyeo Lowassa alikuwa anapewa.
Waziri wa maji na Mifugo (2000-2005), Waziri wa nchi Mazingira (1993-1998), Waziri katika ofisi ya waziri mkuu maafa na sera (1990-1993), Mkurugenzi mtendaji AICC (1989-1993) nk.
Amshukuru Kikwete kumpa Uwaziri Mkuu nadi kazikwa kitaifa.