Jakaya Kikwete: Lowassa alipopata changamoto na kukaa pembeni, tuliendelea kuwa Marafiki

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ametoa kauli hiyo baada ya kufika kutoa pole ya Msiba nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, 2024 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Moyo (JKCI).

Akizungumzia kiongozi huyo, Kikwete amesema Mwaka 2005 tulipoteuliwa kugombea Urais, mwenzangu akaja kuwa Waziri Mkuu tukapata changamoto katikati mwenzangu ikabidi akae pembeni, tukaendelea kuwa pamoja kuwa marafiki na kushirikiana kwa kila linalowezekana"

Kikwete ameongeza kuwa Lowassa ametoa mchango mkubwa katika taifa na yaliyotokea ni changamoto katika maisha lakini hayafuti mema na mazuri aliyofanya kwaajili ya nchi.

View attachment 2901750
ila mzee aisee ana moyo. ningekuwa mimi hata kuongea nisingeongea. tuwe wakweli. lowasa alipiga sana kampeni mzee awe rais, ila sikuile alipoachia ngazi imeweka picha kubwa sana. sitaki kuendelea kusema, ila nimalize kwa kusema pengine ulikuwa mpango wa Mungu manake tungetawaliwa na lowasa leo hii aisee tungekuwa tumeibiwa pesa hadi nchi ingekuwa masikini kuliko ilivyo. thanks JK.
 
Akizungumzia kiongozi huyo, Kikwete amesema Mwaka 2005 tulipoteuliwa kugombea Urais, mwenzangu akaja kuwa Waziri Mkuu tukapata changamoto katikati mwenzangu ikabidi akae pembeni, tukaendelea kuwa pamoja kuwa marafiki na kushirikiana kwa kila linalowezekana"
Yaleyale ya Chato 2021!!! Mnafiki sana huyu jamaa, na kama atawaachia watoto hiyo tabia basi ni hasara kubwa kwa kizazi chake, alimtosa mwenzake kwenye Richmond haikutosha akamtosa kwenye uchaguzi mkuu 2015 leo anasema alikuwa rafiki yake
 
Back
Top Bottom