Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!?

kipimo cha akili(Dimentia) Ulaya kipo sana ,mara nyingi wanafanyiwa watu wakiaanza tabia tofauti /kusahau/kuchanganyikiwa.etc.wataalam wanajua hili.
 
Mzee Mwkjj, umenifanya niache shughuli zangu muhimu za kujenga nchi na kuingia kutoa comment. Unajua mi naamini rais huyu na wasaidizi wake wana upeo mdogo sana, na ingetakiwa washauri wapime situation, wakiona mkuu ana tabia ya kuropoka wasimwachie microphone kwa muda mrefu kwani anaweza kutoboa siri. Sidhani kama ilikuwa sanctioned ye rais kusema hadharani eti alienda kupima akili. Aliropoka tu katika harakati za kutaka kufurahisha waandishi. Sasa baada ya kuropoka kaacha majibu mengi zaidi. Kila mtu ninayemjua nikimhoji ameonaje majibu ya rais, wanaibua ishu hii ya kupimwa akili!!! Kwa kweli ni aibu kubwa sana kwa rais kusema hivyo.
If we were in a decent democracy sasa hivi the oppositin would be demanding his resignation! Ila hapa tunaendelea kuongea tu online hiding behind pseudonyms, lakini muda umekaribia tutaanza kuongea kwa uwazi kabisa.
 
kupima ni swala la msingi sana kwake na hasa akili kwa sababu watu wote ni vichaa ila viwango vya kichaa husika vinatofautiana kwa kila mtu.

watu wote pamoja na hao madaktari. inakuwaje kama daktari anayekupima ana kichaa zaidi yako? halafu hivi akili inapimwaje?
 
Auntie Sophi,

Hebu tukutane AV booth ili tuongee vizuri. Utatangaza lini matokeo yako ya vipimo?
 
watu wote pamoja na hao madaktari. inakuwaje kama daktari anayekupima ana kichaa zaidi yako? halafu hivi akili inapimwaje?
Hilo la kupiwa akili nafikiri watu wengi wana tafsiri vibaya, nadhani yeye alikuwa anamanisha alipimwa Ubongo(akili?) kujua kama ana KIFAFA au la! Hii inatokana na yeye kuangukaanguka jukwaani mara kadhaa!
 
Mwanakijiji.
Serikali mara nyingi huwa hawapendi kutoa taarifa kama hizo especially kama Rais is involved. Lakini ukweli ni kwamba kama waliamua kumpima akili basi kutakuwa na dalili fulani ambazo watu wake wa karibu wameshaziona lakini hawapendi public wajue.
 
Nafikiri ni muda muafaka MIREMBE HOSPITAL ikawa UPGRADED kukawa na hadhi ya kuwahudumia viongozi serikalini na wengineo.
 
Mkwere, kwao kiswahili ni lugha rasmi, hata kama mtadai ni kikwere!

Hakukosea au kushindwa kutofautisha kati ya ubongo na akili!

Kaenda St. Anna, Nyamwicho wa kule kampa lile jani pana kama kiganja, akaingia Havana wakamsokotea tumbaku na mvuke wa miwa, kisha akaenda NYC kwa Joe Camel, akakaa kwenye kiti cha Sigmund akazoza na mpima akili akiangua kilio!

Jamani Mkwere kazidiwa, na ni lazima apime akili ajionee mwenyewe kama kuna utimamu wa yeye aendelee kuwa Rahisi au ajiondokee!

Lakini yeye kupimwa akili halinisumbui, bali ni hili la yeye kupimwa kila akisafiri na misafari yake ya kuja Marekani kutwa mara nne!

Je Rais wetu anaumwa nini hasa kwamba ni lazima aje nje ya nchi si kwa matibabu tuu, bali kupimwa mara kwa mara?

Je hali yake ya kiafya ya kimwili na sasa kiakili ni nzuri kwetu kama Taifa tuamini kuwa anauwezo wa kufanya kazi tuliyomkabidhi?

Au yeye ni Msukule, Mtaji kama Makamba alivyotamka?
 
Nadhani watu pia mmemiss kitu kimoja katika maelezo yake... majibu aliyopewa siyo kwamba ana "afya nzuri"! angalieni kaambiwa ana hali gani...
 
Mimi nadhaani ubongo wake unatatizo ndo maana anakumbwa na tatizo la kuanguka kweny jukwaa. Na ubongo wake ukiwa na taizo, basi akili yake (Uwezo wa kufanya maamuzi sahihi) pia itakuwa na tatizo.
Sijui Madaktari wake wa hapa nchini wanasemaje kuhusu hili jambo. Mmi naona kama anaona hali yake kiafya si nzuri, bora apumzike mapema na si kusubiri kupumzika baada ya mwaka mpya.
 
Mheshimiwa raisi hajafanya makosa kupima akili yake bwana...General body check up ni muhimu hata kama dalili hazianza kujionyesha.
lakini hata kama ingejulikana anamatatizo hata asingethubutu hata kuwaambia wananchi kuwa alipima akili, na hata amekutwa na matatizo hawezi kuongea ukweli hadharani kwani heshima yake itashuka...
 
KUtoka mwananchi:

NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.

Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?


Watanzania tuacheni mzaha:
JK ni kweli mwenye matatizo ya akili

  • Hii ni baada ya kukubali mwenyewe kupimwa akili yake
  • Asifiwa kwa kukubali kupimwa akili kwenye hospitali ya wendawazimu huko Caribbean
  • Mhe Zitto nae bora akubali kupimwa ili turejeshe tamaa yetu kwake
Tandika, Dar Es Salaam
Bila ya kujali kuwa Bi Waridi wa JF atasema tena kuwa "hii sio ndio Wamarekani wanaita shit ya ng'ombe dume", Wagagagigikoko walionesha mshangao mkubwa kama walivyopigwa Watanzania wengi kuhusu maneno ya yule Mwenyekiti wa Kijiji cha Butiama kule Tarime ajulikanae kwa pseudonym lake la Mzee Mwanakijiji, pamoja na ma-nazi wake 35 waliompa "Thank You Baba" pale JF, baada ya Mzee Mwanakijiji kulia hadharani kuwa eti hataki kabisa na wala hapendi tena Rais wetu kupimwa akili, kwani hio inadhalilisha Taifa na kuwadhalilisha wananchi.

Wagagaggigikoko wameshangazwa sana na hii patriotism isiokuwa na mpango na wala muelekeo ya huyu Mzee Mwanakijiji ambae anaheshimika sana pale JF na ambae ametoa jumbe zaidi ya 16,000 kuisifu CCM pale ukumbini..
" La maana ambalo angeweza kulifanya Mzee Mwanakijiji sio mtu mzima kulia hadharani, bali kumuombea dua Rais wetu mpenzi ili huo muondoko wa akili uwe kidogo kidogo ili apate kumaliza na hio miaka 5 ijayo kwa salama na amani. Lakini, kukasirika na kusema kuwa tumedhalilishwa wakati kila mtu anajua kuwa Rais wetu kweli ni mwenye tatizo la akili ni kudharau ushauri mzuri wa kitaalamu unaotolewa na madaktari wa Rais wetu", waliendelea Wagagagigikoko.

" You don't need to be a neuro-surgeon kufahamu kwamba matatizo ya ugonjwa wa akili yanakuja kwa spells (attacks) – kama vile ilivyomtokea Mwanza. Pale mgonjwa anapopata attack ndio wakati mzuri wa mngonjwa kupimwa ili extent ya maradhi yake ijulikanwe. Hii attack inatokea wakati wowote ule na haingojei mpaka urudi safari au mpaka uwepo DSM," kafahamishwa Mzee Mwanakijiji kwenye barua pepe aliyopelekewa huko kijijini kwake kwa kupitia ma-nazi wake wawili ambao wote majina yao ya mwanzo ni PAKA!
"Kama sio mtu aliyepata hio attack ya akili huko Jamaica, inawezekanaje Rais wa nchi mwenye akili zake timamu akubali kupanda bembea kama mtoto wa shule, wakati theluthi mbili ya watu wake wanalala na njaa? Mzee Mwanakijiji ni lazima ufahamu kuwa kwa mtu mzima aliejukuu kupanda bembea (baada ya kuwaachia wajukuu zake kupanda) ni dalili ya kuonesha kutokuwa mzima akilini, na kwahivyo usistaajabu kwanini akili zake zikachunguzwa na wataalamu nje ya nchi," alimalizia muandishi wa Wagagagigikoko.

"Ugonjwa wa akili ni sawa na ugonjwa mwengine wowote ule. Ikiwa tunamruhusu Rais wetu kuenda nje kupima moyo wake na afya yake yote in general, sasa kwanini iwe tunadhalilishwa kama anakuenda nje kupima akili yake?" Wagagagigikoko walimuuliza Mzee Mwanakijiji kwa sauti kali sana kama vile alikuwepo mbele yao pale makao makuu yao nyuma ya Kariakoo.
"Kwa upande mwengine, ni vizuri Rais wetu kaenda kucheki akili zake huko nje, kwani sasa nchi za nje wanajua kuwa matatizo yetu ya umaskini nchini sababu yake ni nini, na labda wanaweza kutusaidia zaidi kwa misaada kuliko hapo mwanzo", alielezwa Mzee Mwanakijiji.
"Hii sio dementia na wala sio Alzheimer", alisema Daktari wa Wagagagigikoko na akaendelea, "Mtu akikwambia nipime homa, basi huyo either tayari homa anayo, au tayari anaona baridi baridi na homa inamtambalia karibu karibu. Ugonjwa wa akili upo hivyo hivyo. Mtu mwenye akili timamu hatotaka apimwe akili. Ukimsikia mtu anataka apimwe akili au anashauriwa apimwe akili yake, basi tayari huyo ana matatizo ya akili", kamalizia Daktari huyo.
Memba mmoja wa JF alinukuliwa na Daktari wa Wagagagigikoko kwenye msg yake ukumbini akisema, " mtu anaenda kupimwa kile alicho na wasiwasi nacho mwilini mwake, sasa mkulu ana mashaka na akili yake hivyo ni haki yake kuamua ipimwe. Nampongeza sana maana hiyo ni dalili nzuri kujishuku", alimaliza memba huyo, huku akimpiga vijembe JK kuwa tayari ni muendawazimu wa kuokota vikopo mitaani..

Kuonekana kwamba JK anayo matatizo ya akili iwe sasa ni fundisho na somo kubwa kwa Watanzania kuwapima ma-Rais wetu kabla ya kuapishwa. "Na huyu mjukuu wake Mzee Mwanakijiji aitwae Zitto nae pia apimwe, kwasababu haya mambo anayoyafanya hayafahamiki kabisa", alieleza mwana-kada mmoja ambae chama chake hakukitaja.
Alivyoshikiliwa aelezee zaidi kwanini anamtia Mhe Zitto ambae hana kosa kwenye balaa hili alisema, " Ninaamini kuwa yeye Mhe Zitto hajaharibikiwa akili kiasi hicho kama Rais wetu, kwani hata bembea bado hajapanda, lakini kule kumsifia Dr Rashid hadharani, pamoja na hii tisha tisha yake kwa Dr Slaa na Mbowe kuwa anatembea na barua ya kuhama Chadema mfukoni mwake huko Ujerumani, na ukijumlisha na yale maneneo yake ya juzi kuwa atachukuwa uamuzi ambao haujafikiriwa na yoyote – mambo kama haya yatamtia mashaka daktari yoyote yule wa akili akiyasikia, na kwahivyo bora nae Mhe Zitto (bila ya kumkusudia vibaya) afuate mfano mzuri wa Rais wetu na aende kwa hiari yake kupimwa akili yake, ili tupate kurejesha tamaa yetu kwake", walimalizia Wagagagigikoko.

Sources: Wagagagigikoko News Network (Wanene)
 
Mimi binafsi nimekosa muongozo maana humu mimi ni mgeni, Yani nimesoma haya maelezo humu mpaka nahisi kudata maana sielewi naona manyota-nyota,
Nipeni muongozo jamani hii hali ni mbaya sio nzuri kabisa.
 
Mimi binafsi nimekosa muongozo maana humu mimi ni mgeni, Yani nimesoma haya maelezo humu mpaka nahisi kudata maana sielewi naona manyota-nyota,
Nipeni muongozo jamani hii hali ni mbaya sio nzuri kabisa.

Join Date: Thu Feb 2008
Posts: 696
Thanks: 0
Thanked 15 Times in 11 Posts
Rep Power: 23

Ni mgeni kwenye thread au kujiunga JF?? naona unakaribia 2yrs.
Elezea vizuri kwani hueleweki.
 
Rais apimwe akili kwani anaonyesha dalili za ugonjwa wa akili? Labda kuna vitu anafanya kama vile kachanganyikiwa ndio maana wakaamua kumpima ugonjwa wa akili.

hivi huyu rais hata kwa kumtazama tu unamuona ana akili?? yaani walioamua kumpima akili walikuwa sahihi wala mi sishangai..we utu uzima wote ule anaacha kuangalia na ku deal na mambo ya msingi ya taifa na matatizo yake yeye anaenda kubembea
 
Jamani mimi nimesema ni mgeni kwenye Post kama hizi za masiasaaa!!!! hauelewi?

Nd. Mkenya,

Kama wewe ni mgeni, basi napenda kukufahamisha kuwa Wagagagigikoko kama wanavyotueleza kuwa wao ni News Network hapa Tanzania na ofisi zao wanasema zipo nyuma ya Kariokoo. Wao ni wasanii, na news zao wanazileta hapa ukumbini in a sarcastic way, ili ukizisoma pia ufurahi. Kama hufuatilii kile kinachoendelea hutofahamu kitu. Itakuchukuwa muda kidogo.
Juu ya yote hayo, wanayoyasema ni kuwa mengi yanakuwa ni kweli, kwani inaonesha wanafanya utaftishi sana. Moja lao la kweli ni kule walivyotutabiria kuwa Dr Mohamed Gharib Bilal ndio chaguo la Waznz kwa mwaka 2010. Wengi tumecheki kule Dodoma na tumeelezwa kuwa hio ni kweli na hata ukiwauliza uongozi wa CUF watakueleza kuwa hio ni sawa.
Wengi tumeshukuru kufahamu mapema nani ataiongoza ZNZ baada ya Karume, kwani hatuumizi kichwa chetu tena kwa upande wa ZNZ. Kwa hilo tunawashukuru Wagagagigikoko for keeping us abreast with ZNZ's news.

Kwa Bara naona hawajasema kitu, lakini kwavile mzee wetu JK anamatatizo kidogo ya akili sijui Wagagagigikoko kwa sasa watamtabiri nani. Tunangojea kuwasikiliza, kwani najua na wao wamo mbioni kujua hilo, japokuwa wenyewe CCM hapa JF wamehamaki kwa hio siri yao ya ugonjwa wa akili wa Mwenyekiti wao kutoka nje na unaweza kuona vipi Mzee Mwanakijiji alipokuja juu hapo juu. La kushangaza zaidi ni kuwa hii habari kaitoa yeye mwenyewe JK na haikutoka kutoka kwa Kulikoni au Wagagagigikoko. Sasa kama Mzee Mwanakijiji kahamaki, basi sio bora aende Ikulu akamueleze jamaa kuwa haya mambo mengine hayafai kutolewa nje!!!!
Hahahahahahahaha!!!!! Siasa za CCM zinachekesha kweli. Kiongozi anasema ukweli wanachama akina Mzee Mwanakijiji hawataki na wanahamaki. Sijui tutafika vipi!!!.
Natuami nimeweza kukusaidia, kama bado hujatosheka, basi nenda kwenye tovuti lao la habari:
www.wagagagigikoko.com
Ukilitembelea hilo tovuti fanya iwe usiku, kwani mara nyingi mchana linakuwa lipo chini kwaajili ya kutiwa news za kila siku!
Kwa leo bye ndugu. Nimesahau kidogo, vipi mambo huko Kenya? Hebu tuelezee kidogo. Nyinyi wenzetu ni mashujaa sio kama sisi!!!
 
Hahahahahahahaha!!!!! Siasa za CCM zinachekesha kweli. Kiongozi anasema ukweli wanachama akina Mzee Mwanakijiji hawataki na wanahamaki.

Bw/Bi Ngida1,

Naona wewe na Wagagagigikoko hamjamfahamu Mzee Mwanakijiji. Yeye japokuwa kweli ni CCM yeka, lakini hajahamaki kwasababu JK ni mwenye matatizo ya akili. Yeye kahamaki kwasababu: kwanini kenda kuchunguzwa nje juu ya suala hili na kuwa anaona aibu kuwa Rais wa nchi anakuenda kuchunguzwa akili zake. Sasa Nd. Ngida1 unadhania hawa watu wa nje watasema nini kuhusu nchi yetu? Sio watatuona sisi sote hapa Tanzania ni wandawazimu??????
 

zanaki umepiga magogoni....!!! ...ime click..pia kwangu ..aliondoka na gulf stream akiwa na mama ...amerudi na emirates akiwa peke yake...!! ....au ndege walipotoka jamaica au trinad ilimpeleka mama kutembelea ma shost zake...??
na ni kweli aliondoka ijumaa cuba....amefika jana ...kweli atakuwa amechoka sana kwa sana kwa safari ya masaa72..toka cuba....badala ya masaa 18!!......si aseme tu alimrudisha mama nyumbani akaendelea na bi mdogo....its time sasa wananchi wajuwe status .....mbona we were okay with MWINYI polygamous status...si dhambi!!..ila ukificha ni dhambi!!!

amezidi kupiga miayo!![/SIZE]


hii kupiga miayo anaonekana anakuwa ana njaa sana..ndo maana nikashauri wawe wanamuwekea visheti and karanga za kutafuna kwenye mfuko wa koti
 
Back
Top Bottom