Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!?

wamekuta ana akili ngapi sasa???
eee! tuambiwe tujjue dereva wetu yupoje!! usikute zimeisha zote!
 
Kwa tatizo hilo hata kama angekuwa nalo hapa nchini hatuwezi kumpima rais wetu mpaka akapimwe nje ya nchi? Kwa mpango huu tutajenga hospitali ya maana hapa nchini kweli? Maana imeshakuwa utamaduni sasa hata mafua ukishakuwa na madaraka lazima ukapimwe nje?

Wataalamu wa afya watusaidie kuhusu hili.
 
Hapana jamani sii kwamba blongata ya mheshimiwa ina mushkeli bali kilishomsukuma kupima akili ni kampeni ya kivitendo ya kuwashawishi mwawaziri wake kupima akili kutokana na kuropoka hovyo sawa na ushauri wa Malecela kwa SS.
 
Wengine walisema oooh anatibiwa kwa waganga wa kienyeji! Sasa tunaomba tuambiwe ni daktari wa hospitali au mlingotini aliyempima akili?
 
zanaki umepiga magogoni....!!! ...ime click..pia kwangu ..aliondoka na gulf stream akiwa na mama ...amerudi na emirates akiwa peke yake...!! ....au ndege walipotoka jamaica au trinad ilimpeleka mama kutembelea ma shost zake...??
na ni kweli aliondoka ijumaa cuba....amefika jana ...kweli atakuwa amechoka sana kwa sana kwa safari ya masaa72..toka cuba....badala ya masaa 18!!......si aseme tu alimrudisha mama nyumbani akaendelea na bi mdogo....its time sasa wananchi wajuwe status .....mbona we were okay with MWINYI polygamous status...si dhambi!!..ila ukificha ni dhambi!!!

amezidi kupiga miayo!!

Ama kweli Watanzania sio Mabwege tena...Dr. Harrison Mwakyembe
 
KUtoka mwananchi:

NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.

Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?

Haitakuwa vibaya akatumegea kidogo waliyoyaona katika akili yake maana lazima itakuwa na kasoro ya aina moja au nyingine mpaka kuwa kiongozi dhaifu kiasi hiki.

Ana vyombo vyote vya dola nyuma yake Jeshi, polisi, FFU, Mahakama na Watanzania milioni 40 lakini anashindwa kumchukulia hatua fisadi mkubwa ndani ya nchi yetu papa fisadi Rostam Aziz pamoja na kuwa na ushahidi wa kutosha kuhusika na wizi wa shilingi bilioni zaidi ya 200. Kikwete anaogopa hata kuamuru huyu fisadi ahojiwe tu, hii si dalili ya akili iliyo kamili hata kidogo.

Kama akili yake ni sawa na bado ni dhaifu kiasi hiki pamoja na nguvu kubwa alizokabidhiwa na Watanzania, basi tunahitaji Rais mwenye akili nusu ili afanye kweli dhidi ya mafisadi.
 
Rais wa JMT ni mtu kama walivyo watu wengine,ana matatizo ya afya kama ilivyo kwa watu wengineingawa tatizo lake ni kubwa hasa kwa nafasi ya Rais.Aina ya ugonjwa alionao Rais wetu mpendwa chaguo la Mungu ndiyo kikwazo kikubwa katika kutekeleza majukumu yake.

Unapokuwa na Rais mwenye matatizo ya akili anayeongoza watu milioni 40 na ushee na katiba inayompa madaraka makubwa yanakaribina na yale ya mwenyezi mungu bila shaka mwenye matatizo ya akili ni wananchi milioni 40 tuliokubali kumpeleka magogoni kwa kura za kishindo.

Wenye matatizo ya akili ni CC,NEC na mkutano mkuu wa CCM waliowakataa watu ambao kwa fikra zangu wasingetufikisha hapa tulipo sasa.Wenye matatizo ya akili ni vyombo vya habari vilivyowaaminisha watanzania kwamba Tanzania ni lazima iongozwe na Kikwete na genge lake la wasanii.

Wenye matatizo ya akili ni mimi na wewe tunayemjadili mtu ambaye kwa vigezo vyote hakustahili kuwa Rais wa Tanzania.

wakati mwingine ukweli unauma; lakini nadhani umegusa karibu zaidi na ukweli.
 
zanaki umepiga magogoni....!!! ...ime click..pia kwangu ..aliondoka na gulf stream akiwa na mama ...amerudi na emirates akiwa peke yake...!! ....au ndege walipotoka jamaica au trinad ilimpeleka mama kutembelea ma shost zake...??
na ni kweli aliondoka ijumaa cuba....amefika jana ...kweli atakuwa amechoka sana kwa sana kwa safari ya masaa72..toka cuba....badala ya masaa 18!!......si aseme tu alimrudisha mama nyumbani akaendelea na bi mdogo....its time sasa wananchi wajuwe status .....mbona we were okay with MWINYI polygamous status...si dhambi!!..ila ukificha ni dhambi!!!

amezidi kupiga miayo!!

na watu bwana kushindwa kuunganisha mambo.... hivi hamjawahi kuuliza kule UAE kuna nini?
 
mtu anaenda kupimwa kile alicho na wasiwasi nacho mwilini mwake, sasa mkulu ana mashaka na akili yake hivyo ni haki yake kuamua ipimwe. Nampongeza sana maana hiyo ni dalili nzuri kujishuku.


watu mna majibu utadhani mnaigilizia!
 
I can now understand why it takes ages for him to decide mambo muhimu ya nchi.Pia kutokuwa na msimamo thabiti kuhusu mustakabali mzima wa nchi yetu!Ningekuwa mimi ningesema tu nilichekiwa afya BUT anything kuhusu akili ningeweka kibindoni!It will spark controversy!!!


yaani nacheka hapa hadi machozi!
 
Ndugu wananchi mliomo hapa, mimi sina neno lolote zaidi ya kuomba mama yangu mpendwa sana, Sophia Simba ikiwezekana nae aende kupata huduma hii ya kipimo cha Ubongo! Hii itatufanya tumuelewe vizuri zaidi kwenye matamko yake ya huko mbeleni. Na pia anaweza kujiweka vizuri kwenye ulingo wa siasa kama ndio fani bado anayoipenda.

Mungu Ibariki Tanzania, asanteni kwa kunisoma
 
hivi ni yeye mwenyewe au ni washauri wake ndio waliomshauri akacheki akili?
na hasa sijuhi kilikuwa ni kipimo gani, IQ, utahahira au uchizi?

kweli watajulikana kwa matendo yao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom